text
stringlengths 1k
24.2k
| label
class label 6
classes |
---|---|
NAIROBI, KENYA RAIS Uhuru Kenyatta, ametangaza nyongeza ya asilimia tano kwa kiwango cha chini cha mshahara nchini Kenya wakati wa maadhimisho ya Siku ya Wafanyakazi. Tangazo hilo lilitolewa jana kwa niaba yake na Waziri wa Kazi, Balozi Ukur Yatani Kanacho aliyewaongoza viongozi wengine mashuhuri serikalini na upinzani kuadhimisha siku hiyo kwenye Viwanja vya Uhuru Park, jijini Nairobi. “Wafanyakazi wa umma watapata nyongeza ya asilimia tano,” alisema Rais Kenyatta kwenye hotuba yake iliyosomwa na Waziri Yatani. Hotuba ya Kenyatta iliegemea nguzo zake kuu nne katika awamu yake ya pili na ya mwisho ambazo ni; kuangazia usalama wa chakula, makazi bora na nafuu, ujenzi wa viwanda ili kukabiliana na ukosefu wa ajira hasa kwa vijana, na matibabu bora. Kenyatta mwaka 2017 alitangaza nyongeza ya asilimia 18 kwa wafanyakazi wa umma. Hata hivyo, Katibu Mkuu wa Muungano wa wafanyakazi (Cotu), Francis Atwoli amesema agizo hilo halijatekelezwa kwa baadhi ya kampuni na taasisi. “Kuna kampuni nyingi hazijatekeleza agizo hilo. Rais pia alipendekeza kodi kwa wanaopokea mshahara wa chini ya Sh100,000 upunguzwe lakini hayo yote hayajaheshimiwa,” alisema Atwoli. Cotu pia imekosoa pendekezo linaloongozwa na Kiongozi wa Wengi Bungeni Aden Duale la kutathmini sheria za kudhibiti miungano ya wafanyakazi kwa lengo la kupunguza majukumu yao. Miungano ya wafanyakazi Kenya imekuwa ikiandaa migomo ya kitaifa, ili kutetea haki zao na mbunge huyo wa Garissa mjini anapania kuwasilisha muswada bungeni wa kudhibiti miungano hiyo. “Waziri Ukur Yattani tunakushauri ujiondoe kwa mjadala huo wa kurekebisha sheria za miungano ya wafanyakazi,” Atwoli alionya. Kinara wa upinzani Raila Odinga aliyehudhuria maadhimisho hayo, alisema makubaliano yake na Rais Uhuru Kenyatta ya Machi 2018, yalilenga kuimarisha maisha ya Wakenya. “Mazungumzo yetu yaliegemea kuimarisha maisha ya wananchi wote, kwa msingi wa bidhaa na kodi nafuu ya nyumba,” alisema Odinga. Aliongeza kuwa Nasa imeungana na Serikali ya Jubilee ili kuangazia masaibu yanayokumba Wakenya ikiwamo kukabiliana na kero za ufisadi. Kadhalika, kiongozi huyo alizingumzia kuhusu marufuku ya Nasa kununua bidhaa za kampuni zilizounga utawala wa Jubilee, akisema kutokana na makubaliano yake na Kenyatta wamezisamehe na hivyo wafuasi wake waache kuzisusia. | 2kimataifa
|
IDADI ya vifo vya waendesha bodaboda nchini vitokanavyo na ajali imepungua katika kipindi cha robo ya kwanza ya mwaka huu kinachoanzia Januari hadi Machi, ikilinganishwa na idadi ya vifo vya bodaboda kwa kipindi kama hicho kwa mwaka jana. Mwanasheria wa Kikosi cha Usalama Barabarani, Afande Deusi Sokoni akizungumza na gazeti hili katika mahojiano maalumu alisema kuwa idadi ya waendeshaji bodaboda waliopoteza maisha kwa mwaka huu ni 73 huku majeruhi wakiwa 121.Alisema, kwa mwaka jana kwa kipindi kama hicho waliopoteza maisha walikuwa ni 108 huku waliojeruhiwa ni 214. Sokoni aliongeza kuwa robo ya kwanza ya mwaka huu kwa upande wa waendesha baiskeli waliopoteza maisha kwa ajali za barabarani walikuwa 23 idadi ambayo ni sawa na ya majeruhi lakini mwaka jana kuanzia Januari hadi Machi, idadi ya waliokufa ilikuwa ni 34 huku waliojeruhiwa wakiwa 30. Alisema pia waendesha mikokoteni tisa wamekufa na wanne wamejeruhiwa huku mwaka jana aliyekufa alikuwa mmoja na 12 walijeruhiwa. Kundi la watembea kwa miguu ambalo ni moja kati ya waathirika wakubwa wa ajali kwa mwaka huu wamekufa 90 na kujeruhiwa 106. Wakati kwa mwaka jana waliokufa walikuwa 163 na kujeruhiwa 179. Kwa upande wa abiria waliokufa kwa ajali kwa mwaka huu ni 108 na 393 wamekumbwa na majeraha mbalimbali wakati kwa mwaka jana waliokufa walikuwa 191 na majeruhi 575. | 3kitaifa
|
NA ABDUCADO EMMANUEL, DAR ES SALAAM HOMA ya pambano la watani wa jadi imezidi kupanda kwa timu zote kuingia mafichoni, lakini kitakachojiri kwenye mchezo huo ni ama Yanga kufuta uteja au Simba kuendeleza ubabe dhidi ya Wanajangwani hao katika Uwanja wa Taifa Jumamosi hii. Katika kujiandaa na mechi hiyo, timu zote zimekimbilia visiwani Zanzibar, Yanga ikiwa Pemba tokea Jumapili iliyopita na Simba ilirejea juzi Unguja kwenye kambi ya awali kabla ya kuanza kwa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara (VPL). Tofauti na msimu uliopita, msimu huu timu zote mbili zitaingia dimbani zikiwa na kasi ya ushindi kwenye mechi zote tatu walizocheza, hivyo kila timu itakuwa na morali nzuri ya kumtambia mwenzake. Msimu uliopita Simba ilipata sare mechi zote tatu za awali kabla ya kuivaa Yanga, huku hasimu wake akishinda mbili na kufungwa moja na mechi baina yao ikaisha kwa suluhu. Mzunguko wa pili kibao kikaigeukia Yanga, walishindwa kufurukuta kwa kufungwa bao 1-0 lililowekwa kimiani na mshambuliaji kutoka Uganda, Emmanuel Okwi, aliyeuzwa Ulaya kwenda timu ya Sonderjyske ya Denmark. Ukiwa ni mchezo wa 80 wa Ligi Kuu kwa watani wa jadi tokea ligi hiyo ianze, Yanga mpaka sasa ina ukame wa mechi nne wa kushindwa kuifunga Simba, sawa na dakika 360. Mara ya mwisho kuwafunga wekundu hao ilikuwa ni Mei 18, mwaka juzi, walipoichapa mabao 2-0 na kutwaa ubingwa wa ligi kwa mara ya 24, wafungaji wakiwa Didier Kavumbagu na Hamis Kiiza, ambaye hivi sasa yupo Simba. Kinachowauma zaidi Yanga kuelekea kila mchezo dhidi ya Simba ni ile kumbukumbu mbaya waliyokuwa nayo ya kukubali kichapo cha mbwa mwizi cha mabao 5-0, walichopewa Mei 7, 2012 na Simba kutwaa ubingwa wa ligi kwa mara ya mwisho, kwani hadi sasa wanahaha kulisaka kombe bila mafanikio. Wakati pambano hilo likikaribia, tumeona namna wachezaji wa kigeni walivyong’ara kwa timu zote mbili katika kupachika mabao na huenda ikaamuliwa na nyota hao. Kiiza, aliyekatwa Yanga msimu uliopita na Kocha Marcio Maximo, ameibukia Simba msimu huu na ndiye kinara wa ufungaji mabao Ligi Kuu, akiwa na mabao matano, ni wazi atakuwa na uchu wa kuwazodoa mabosi wake wa zamani. Kama ilivyo kwa Kiiza, nyota wa Yanga, Amissi Tambwe, ambaye alikatwa na Simba msimu uliopita, akiwa na mabao matatu mpaka sasa sawa na mshambuliaji mwenzake Donald Ngoma, naye atataka kudhihirisha ubora wake kwa kuiua Simba. Lakini historia inawabana wachezaji wazawa kwa misimu minne iliyopita kuanzia 2011-12, kwani katika mabao 19 yaliyofungwa kwenye mechi nane zilizopita, wageni wamefunga 12 na wazawa saba. Mechi yao ya mwisho kuisha kwa wazawa kufunga kwenye ligi ilikuwa ni sare ya 1-1 kwenye mzunguko wa pili 2013/14, Haruna Chanongo akifunga kwa Simba na Simon Msuva akaisawazishia Yanga. Nyota wapya wa kigeni wa Yanga wanaotarajia kucheza mchezo huo kwa mara ya kwanza ni Ngoma, Thabani Kamusoko na Vincent Bossou, huku wa Simba wakiwa ni Justice Madjavi, Emery Nimubona, Vincent Angban kama watachezeshwa. Kocha wa Yanga, Hans van Pluijm, ataingia kwenye mchezo wake wa tatu wa ligi dhidi ya Simba, miwili ya awali aliambulia pointi moja, wa kwanza akitoa sare na mwingine akipoteza msimu uliopita, Dylan Kerr wa Simba yeye utakuwa ni mchezo wake wa kwanza wa watani. | 5michezo
|
JAJI Mkuu wa Tanzania, Profesa Ibrahimu Juma amesema ufasaha katika kujieleza kwa lugha ya kiingereza kwa mawakili walio wengi bado ni changamoto licha ya sheria kutumia zaidi lugha hiyo.Alisema amegundua changamoto hiyo baada ya kupata nafasi ya kukutana ana kwa ana na waombaji wa uwakili wapatao 824 kwa mujibu wa kifungu 8 (3) cha Sheria ya Mawakili. Miongoni mwa mawakili 909 waliokubaliwa kupata uwakili, saba ni majaji akiwemo aliyekuwa Mkurugenzi wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru), Valentino Mlowola na Msajili wa Mahakama ya Rufani, John Kahyoza. Wengine ni balozi mstaafu na mwanadiplomasia wa Umoja wa Mataifa, Tuvako Manongi, Hakimu Mkazi Mkuu wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, Thomas Simba, maofisa wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ), polisi, mapadre, mashehe na watu wengine.Akizungumza wakati wa kuwakubali mawakili hao jana kwenye viwanja vya Shule ya Sheria kwa Vitendo, alisema lengo la kuwahoji ni kutaka kujiridhisha na ufahamu na matumizi ya lugha ya kiingereza kwa mambo yanayozunguka sheria kwa Tanzania na dunia. Profesa Juma alisema changamoto ya kujieleza inatakiwa kufanyiwa kazi na mfumo wa elimu pamoja na Baraza la Sheria Tanzania chini ya Jaji Kiongozi. “Mwalimu Nyerere aliwahi kutamka kwamba kiingereza ni ‘Kiswahili cha Dunia’. Hivyo, kwa wakili anayetaka kujifunza na kujiendeleza katika ushindani wa karne ya 21, hawezi kukwepa umuhimu wa kuwa na ufasaha katika lugha ya kiingereza,” alifafanua Profesa Juma.Aliongeza kuwa ingawa elimu kutoka shule ya msingi, sekondari, vyuo na elimu ya sheria kwa vitendo imejengwa katika misingina maudhui ya karne ya 20, huduma za uwakili watakazozitoa ni lazima zikidhi ushindani na matarajio ya huduma za karne ya 21. Alieleza mawakili hao wanaweza kutoa huduma zenye ubora na ushindani kama watajisomea maeneo mapya na kujiendeleza kitaaluna kwa kutumia mifumo ya Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (Tehama). Alisema katika kujiendeleza, mawakili hao wanapaswa kuelewa changamoto zinazoikabili nchi ya Tanzania na namna gani sheria unaweza kukabiliana na changamoto hizo.“Maboresho makubwa yanaendelea kwa sasa ndani ya Mahakama ya Tanzania kupitia Programu za Maboresho na Mpango Mkakati wa miaka mitano ambayo imesaidia majaji na mahakimu kujipima kwa kupunguza mrundikano wa mashauri,” alieleza. Kwa mujibu wa Jaji Mkuu, maboresho yamefanikisha ujenzi wa majengo mapya ya mahakama na kufanya ukarabati mkubwa, pia kujenga misingi ya kudumu ya kuwa mahakama itakayoendeshwa kwa uwazi na kuzingatia mifumo ya kisasa ya Tehama.Alisisitiza kuwa mawakili wanapaswa kujitayarisha na mabadiliko ya sheria na kanuni za uendeshaji wa mashauri ziboreshwe na zieleweke kwa urahisi na ziharakishe utoaji wa haki. Pia, Profesa Juma aliwataka mawakili hao kubaki ndani ya misingi ya maadili na uwakili bora kwa kuzingatia Kanuni za Kimaadili, Nidhamu na Tabia njema za mawakili namba 118 ya 2018.Alisema kanuni hizo zinawakumbusha mawakili mambo ya msingi katika kazi za uwakili na vile vile zinatoa tahadhari kuwa hatua za kinidhamu zitachukuliwa kwa yoyote atakayekiuka kanuni hizo. “Wakili ni ofisa wa mahakama mwenye tabia njema isiyo na dosari, ukweli na kufanya kazi kwa kuheshimu misingi ya haki. Wakili anatakiwa kuheshimu wateja wake, wananchi na mawakili wenzake pia kuheshimu wataalamu kutoka fani nyingine bila kusahau kuheshimu mahakama na mfumo wa sheria na utoaji haji,” alisisitiza.Jaji alisema kanuni zimeainisha mifano ya wakili ambaye atachukuliwa kuwa amekosa uadilifu na tabia njema endapo atakiuka sheria za nchi, kuficha ukweli kwa wateja, matusina kutoa taarifa za uongo au maneno ya kudhalilisha maofisa mwengine wa mahakama. Hata hivyo, alisema kanuni zimetoa mifano ya huduma mbovu zinazoweza kusababisha mawakili kuchukuliwa hatua za kinidhamu na kusimamishwa uwakili kama vile kushindwa kumpa mteja taarifa muhimu za maswala yanayomuhusu, kushindwa kutoa taarifa kwa mteja zinapohitajika na kushindwa kutoa huduma kwa sababu ya ulevi na matumizi ya dawa za kulevya.Pia alisema kutoa huduma mbovu kwa mfano ubovu wa hati za kimahakama kwa niaba ya mteja wake na kusababisha kuchelewa kwa shauri au kusababisha gharama zisizo za lazima dhidi ya mteja. Profesa Juma alieleza sababu nyingine za zitakazosababisha mawakili kusimamishwa ni kutoa huduma mbovu, kutayarisha hati za kimahakama zisizoeleweka na makosa ya kiufundi katika hati za kimahakama. “Kushindwa kuwa na ofisi ambazo wateja, mawakili wenzako na mahakama zinazoweza kukufikia na kuwasilisha taarifa.Hivi karibuni tutamtaka kila wakili ajisajili eneo ilipo ofisi yake, mtaa na postikodi ili aweze kufikiwa,” alisisitiza. Kwa upande wake, Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Profesa Adelardus Kilangi alisema mawakili wanatakiwa kuzingatia sheria kwa kutotenda makosa ya jinai, kuzingatia maslahi ya mteja dhisi ya maslahi hao binafsi na kuisaidia mahakama kupata haki. Pia alisema mawakili watakaochaguliwa kufanya kazi za utumishi wa umma wanapaswa kuchagua suala moja kwa sababu ni ukiukwaji wa maadili wakili kunufaika mara mbili. Naye, Rais wa Chama cha Mawakili Tanganyika (TLS), Fatma Karume alisema asilimia 99 ya mawakili wao wanafuata maadili ya taaluma hiyo na kwamba kesi 27 pekee ndio zinawataja mawakili wanaokiuka maadili. Fatma alisema kazi ya mawakili ji kusaidia mahakama kupata haki na kwamba hakuna haki bila hekima. | 3kitaifa
|
Akizungumza na gazeti hili, Bossou, anayefanya vizuri tangu achukue nafasi ya Nadir Haroub ‘Cannavaro’ aliye majeruhi, alisema wana kikosi bora chenye hadhi kubwa Afrika sawa na Al Ahly, hivyo haoni sababu ya kuwahofia zaidi ya kuongeza bidii na kuhakikisha wanawatoa.“Tuache kuweka hofu kabla ya mchezo, Al Ahly ni timu yenye ubora sawa na Yanga, hivyo tunachotakiwa ni kupambana na siyo kuwajadili wachezaji wao au kocha wao tukifanya hivyo tutashindwa kutimiza malengo tuliyojiwekea,” alisema Bossou.Alisema amewahi kucheza Etoile du Sahel, siku za nyuma hivyo anafahamu vyema mbinu chafu zinazotumiwa na timu kutoka Afrika Kaskazini na atahakikisha anaisaidia Yanga kuepuka mbinu hizo.Alisema kitu cha msingi wanachotakiwa ni kuhakikisha wanaitumia vizuri mechi ya nyumbani kupata ushindi, kwani kinyume na hapo itakua tabu kuwafunga watakapokuwa kwao kutokana na fitna walizokuwa nazo ndani na nje ya uwanja.Bossou amewataka wachezaji wenzake kutumia nafasi hiyo waliyoipata kuitangaza klabu na wao wenyewe kwa kucheza kwa juhudi na kuwatoa Al Ahly, ili waweze kucheza hatua ya makundi. | 5michezo
|
Kulwa Mzee, Dar es Salaam Mshtakiwa Hamisi Luwongo anayetuhumiwa kumuua mkewe Naomi Marijani kisha kumchoma na magunia mawili ya mkaa, ameomba apewe laini (sim card), zake mbili zenye zaidi ya Sh milioni tano ili awape ndugu zake wakamlipie mwanawe ada. Mshtakiwa huyo amedai hayo leo Jumanne Agosti 27, katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu mbele ya Hakimu Mkazi, Salum Ally, wakati kesi hiyo ilipotajwa. Wakili wa Serikali Mwandamizi, Wankyo Simon amedai upelelezi haujakamilika akaomba kesi iahirishwe. Kabla ya kuahirisha, mshtakiwa aliomba kuzungumza na mahakama ilimruhusu. “Mheshimiwa Kituo Kikuu cha Polisi (Central) kuna simu zangu nne lakini katika hizo simu kuna laini mbili ya Tigo na Airtel, zina zaidi ya Sh milioni tano, naomba simu ziletwe mahakamani nihamishie hizo fedha kwa ndugu yangu zikasaidie kumlipia mwanangu ada,” amedai. Wakili Wankyo alipinga akidai hicho kinachoombwa ni kielelezo hakiwezi kutolewa, lakini anaweza kuandika barua kwa Mkurugenzi wa Mashtaka (DPP) anaweza kumsaidia. Hakimu Ally alimuagiza mshtakiwa kufuata ushauri wa Jamhuri wa kuandika barua kwa DPP sababu anachoomba ni kielelezo na kesi hiyo haijaanza kusikilizwa. | 3kitaifa
|
SHIRIKA la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC) limetia saini mkataba wa mauziano ya gesi asilia na kampuni ya Shreeji Silicate Tz Ltd kwa miaka 10 inayoweza kuongezeka kulingana na makubaliano.Meneja wa Biashara za Gesi, Dora Ernest alisema amesema TPDC itauza gesi asilia futi za ujazo milioni 0.4408 kwa siku kwa miaka miwili kiasi kitakachoongezeka hadi futi za ujazo milioni 0.9 kwa siku. Alisema hayo jana Dar es Salaam baada ya kutia saini makubaliano na Shreeji Silicates waitumie.Dora alisema kampuni hiyo ni mteja wa 45 wa viwandani na kiwanda chake kiko Mkuranga na anachukua gesi asilia kutoka bomba linalosambaza gesi kwa kiwanda cha vigae kilichopo Mkuranga ambacho kimechukua gesi kutoka kituo cha valvu namba 12 (BVS 12) kilichopo Njopeka, Mkuranga.Mkurugenzi wa Shreeji Silicates Tz Ltd, Mukkasa Rao alisema kwa kutumia gesi asilia wana uhakika wa kuokoa asilimia 30 ya gharama za uzalishaji zinazotokana na nishati kitu hivyo kuongeza ufanisi. Rao anaeleza kuwa kampuni yake inajishughulisha na uzalishaji wa kemikali za sodium silicates ambazo hutumika kuzalisha bidhaa za sabuni za aina mbalimbali.Alisema matumizi ya gesi asilia ni nafuu ukilinganisha na vyanzo vingine vya nishati na TPDC kama kampuni ya Taifa ya Mafuta ndio yenye jukumu la kusambaza nishati hiyo kwa wateja kuzalisha umeme viwandani, majumbani na magari. Dora alisema TPDC inatumia kampuni tanzu ya GASCO kusambaza gesi hiyo ambayo ni rafiki wa mazingira hivyo wenye viwanda na wananchi wanahimizwa kutumia rasilimali hii ili kulinda mazingira. | 3kitaifa
|
WABUNGE wamechachamaa bungeni wakiomba sheria ya hakimiliki na hakishiriki ya 1999 ibadilishwe ili kuwasaidia wasanii kulinda kazi na haki zao kwani hadi sasa wanapata kipato duni kisicholingana na ubora wa kazi zao.Wabunge hao, Maulid Mtulia wa Kinondoni (CCM) na Joseph Mbilinyi wa Mikumi (Chadema), wamelalamika kitendo cha wasanii kuendelea kudhulumiwa kazi zao na wakaomba serikali ilete muswada wa mabadiliko ya sheria bungeni ili ipewe meno kulinda kazi zao. Mtulia alihoji serikali ina mkakati gani wa kuwasaidia wasanii ili kupata stahiki zao na akahoji sera na sheria zinasaidiaje wasanii hao kumiliki na kunufaika na kazi zao za sanaa.Mbunge wa Mikumi, Mbilinyi akiuliza swali la nyongeza bungeni, alihoji lini sheria namba 7 ya mwaka 1999 itapelekwa bungeni ili kubadilishwa ipewe meno ya kuwasaidia wasanii kupata stahili za kazi zao. Akijibu hoja hizo, Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Juliana Shonza (pichani) alisema katika hatua ya kwanza mkakati uliopo ni kuhakikisha Chama cha Hakishiriki Tanzania (COSOTA) kinakuwa chini ya wizara ya habari kutoka wizara ya viwanda ili kazi na haki za wasanii zidhibitiwe vizuri.Shonza alisema ni kweli sheria hiyo ina upungufu lakini kabla ya kufanyiwa marekebisho, inatakiwa kuhakikisha Cosota inarudishwa ili kuwa taasisi chini ya wizara ya habari kwani sasa ipo wizara ya viwanda na biashara. Alisema ni kweli wasanii wanasajili kazi za Cosota ambayo ipo chini ya wizara ya viwanda na biashara hata kama wizara ya habari ndiyo yenye dhamana ya kusimamia wasanii nchini.Shonza alisema wizara inatambua changamoto zinazowakumba wanasanii nchini, lakini akawaomba watengeneze kazi zenye ubora na ubunifu wa hali ya juu ili kushindana kwenye soko. Alisema ili kunusuru kazi zao zisiibiwe wanaweza kuachana na mtindo wa kutengeneza kazi katika CD, wakasonga mbele kisayansi na kiteknolojia kwa kutengeneza kazi zao kwa njia ya mtandao kama alivyofanya msanii Wema Sepetu ambaye amepata faida kubwa.Shonza aliwaonya wasanii kuepuka kuingia mikataba mibovu na wasambazaji wa kazi zao, badala ya kuuza kazi tu wanauza hata kazi-mama ambayo inawafanya waendelee kuumia wakati wote. Shonza alisema Sera ya Utamaduni ya mwaka 1997 ilielekeza kuanzishwa kwa chombo cha kusimamia hakimiliki ambayo ni sehemu muhimu ya dhana pana ya milikibunifu.Hivyo mwaka 1999 ikatungwa sheria ya hakimiliki na hakishiriki ambayo chini yake maslahi ya watunzi wa kazi za sanaa, wafasiri, watayarishaji wa vihifadhia sauti, wachapishaji yanalindwa kicheria na chombo cha kusimamia haki hizo Cosota kilianzishwa.Hivyo sera na sheria vipo kulinda maslahi ya wasanii, lakini tatizo ni uelewa mdogo wa wasanii wenyewe kuhusu haki zao na ulinzi wake kisheria. Ili kukabiliana na tatizo la wasanii hilo, Serikali kupitia Bodi ya Filamu Tanzania na Baraza la Sanaa la Taifa, imetoa elimu kwa wadau 5,200 kuhusu masuala ya hakimiliki, hakishiriki, mikataba na makubaliano kupitia mafunzo ya kuwajengea uwezo ili wawe walinzi wa kazi nahaki zaokwa kuingia mikataba yenye maslahi. | 5michezo
|
BAADA ya Shirikisho la Soka nchini (TFF) kutoa taarifa kuwa Tanzania itakuwa na timu nne kwenye michuano ya klabu Afrika, Simba imesema ilikuwa siku ya kihistoria kutinga robo fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika na kuongeza alama ambazo zimeiwezesha nchi kuingiza timu nne kwenye michuano ya kimataifa kwa msimu wa 2019/2020. Kwa mujibu wa TFF, Shirikisho la Soka Afrika (Caf) limethibitisha kuwa pointi 12 ambazo zimepatikana zimesaidia nchi kuongezewa timu mbili hivyo kwenye Ligi ya Mabingwa hivyo zitakwenda Simba na Yanga huku shirikisho zikienda Azam FC na KMC. Simba wameweka ujumbe kwenye mtandao wa Instagram, ikionesha kumbukumbu ya siku walipoitoa AS Vita na kutinga hatua ya robo fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika uliosomeka “Ilikuwa siku ya kihistoria kutinga robo fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika na kuongeza alama ambazo zimeiwezesha nchi yetu kuingiza timu nne kwenye michuano ya kimataifa kwa msimu wa 2019/2020”. Ujumbe huo ulimalizika kwa maneno yaliyoandikwa kwa herufi kubwa ambayo ni “SIMBA IKISHINDA, TANZANIA IMESHINDA”. Naye mwekezaji wa Simba ambaye pia ni mfanyabiashara mashuhuri Afrika, Mohamed Dewji ‘Mo’ ameandika kwenye ukurasa wake wa Instagram kuwa “Tunajivunia kuwa sehemu ya kufanikisha nchi yetu kuingiza timu nne kwenye michuano ya kimataifa, na tutaendelea kupambana kuhakikisha tunapata mafanikio makubwa kimataifa kwa maslahi ya klabu na nchi yetu. Hongera kwa Wanasimba kwa kazi kubwa tuliyoifanya, tunastahili pongezi”. Timu mbili zitashiriki katika Ligi ya Mabingwa na timu mbili nyingine zitashiriki Kombe la Shirikisho na nafasi hiyo kwa Tanzania imekuja baada ya kuwa katika nafasi 12 bora kwenye viwango vya ubora vya CAF.Kwa mujibu wa Kanuni za Ligi Kuu zilizofanyiwa marekebisho na Kamati ya Utendaji baada ya kupatikana nafasi nne (4), timu za Tanzania zitakazowakilisha kwenye mashindano hayo ni Simba na Yanga kwenye Ligi ya Mabingwa (CAF CL), Azam FC na KMC Kombe la Shirikisho (CAF CC). KMC itawakilisha Kombe la Shirikisho kwa mujibu wa kanuni hiyo, ambayo inatamka kama timu iliyomaliza nafasi ya tatu itakuwa ndio bingwa wa Kombe la FA, basi mshindi wa nne anapata nafasi ya kucheza Kombe la Shirikisho kwa sababu bingwa wa FA anaiwakilisha nchi kwenye mashindano hayo. Tayari CAF imefungua dirisha kwa mashirikisho kusajili timu kupitia mtandao wa CMS na mwisho wa usajili ni Juni 30 ambapo TFF inatakiwa iwe imesajili timu zitakazoshiriki kwenye mashindano ya Kimataifa msimu wa 2019/2020. | 5michezo
|
Na MWANDISHI WETU – ZANZIBAR
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk. Ali Mohamed Shein, ameipongeza Serikali ya Cuba kwa kuendelea kuiunga mkono Zanzibar katika kuimarisha sekta ya afya.
Dk. Shein alisema kuna haja ya kuendelea na hatua hiyo kwa sekta nyingine ili kuzidisha uhusiano na ushirikiano wa kihistoria uliopo kati ya nchi hizo mbili.
Akizungumza na Balozi mpya wa Cuba nchini, Lucas Domingo Hernandez Polledo, Ikulu mjini Unguja, Dk. Shein alieleza kuwa Cuba ni nchi ya mwanzo kuyatambua Mapinduzi matukufu ya Zanzibar ya mwaka 1964.
Katika mazungumzo hayo, Dk. Shein alimweleza balozi huyo kuwa Cuba ina historia kubwa katika juhudi za kuiunga mkono Zanzibar kwenye sekta za maendeleo, hasa sekta ya afya kwani tokea mwaka 1966 nchi hiyo imekuwa ikipeka madaktari wake kwa awamu kwenda kufanya kazi Zanzibar.
Aidha alieleza kuwa mbali ya madaktari hao kutoa huduma ya afya kwa jamii, Cuba imekuza uhusiano wake kwa SMZ kwa kuanzisha chuo cha udaktari ambacho tayari kimetoa madaktari wazalendo ambao hivi sasa wanatoa huduma za afya hapa nchini.
Dk. Shein alisema: “Madaktari hao kutoka Cuba wamekuwa wakifanya kazi ya kutoa huduma ya afya kwa wananchi wa Unguja na Pemba usiku na mchana kwa kushirikiana na madaktari wazalendo.
“Zanzibar ina mengi ya kujifunza katika sekta ya utalii kutoka Cuba, kutokana na nchi hiyo kujiimarisha kwenye sekta hiyo na kupata mafanikio makubwa sambamba na kuendeleza vyanzo vyake vya utalii, likiwamo eneo maarufu la ukanda wa kitalii la ‘Varadero’.”
Naye Balozi Polledo alimweleza Dk. Shein kuwa Cuba inathamini sana uhusiano na ushirikiano wa kihistoria kati yake na Zanzibar na kuahidi kuwa nchi yake itaendelea kuudumisha.
Balozi huyo alimuhakikishia Dk. Shein kuwa Cuba iko tayari kuendeleza uhusiano huo kwa kuimarisha sekta nyingine za maendeleo ikiwamo utalii, elimu na nyenginezo. | 3kitaifa
|
JESHI la Polisi mkoani Pwani linamsaka Alex Makaptura kwa tuhuma za wizi wa ng’ombe, mali ya mfugaji mkazi wa Pongwe Musungura wilaya ya Chalinze Wilaya ya Bagamoyo, Makundi Steti (49).Mfugaji huyo ameibiwa ng’ombe 21 wenye thamani ya Sh milioni 5.2 waliokuwa malishoni.Aidha, mtuhumiwa huyo alikutwa na ng’ombe wengine 40, ambao walikutwa wakiwa na alama mbalimbali ikiwa inaashiria kuwa ni wa wizi.Hayo yalisemwa mjini Kibaha na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Pwani, Wankyo Nyigesa. Kwamba mtuhumiwa huyo alitoroka baada ya kugundua anatafutwa na polisi.Nyigesa alisema tukio hilo ni la Aprili 27 na baada ya kufuatilia walikamata gari namba T576DEQ aina ya Toyota Hiace, ambapo walimkuta Emanuel Jonas (22) akiwa na nyama ya ngombe wawili waliochinjwa waliodhaniwa kuibiwa na alikiri kuuziwa na mtuhumiwa.“Tulipofika nyumbani kwa mtuhumiwa alitoroka na tuliwakuta ngombe hao majike yakiwa 18, madume mawili na ndama wa rika mbalimbali 20 na tulibaini kuwa ngombe hawa waliibiwa maeneo mbalimbali,” alisema Nyigesa.Alisema kuwa katika mahojiano, walifanikiwa kumkamata Shaban Kitanga, mkazi wa Manga wilaya ya Handeni mkoa wa Tanga kwa tuhuma ya kuhusika na tukio hilo la wizi wa ngombe hao 40.“Ngombe hao 40 ambao walikutwa na alama tofauti kuashiria kuwa si mali ya mtu mmoja na walipelekwa kwenye Ranchi ya Taifa ya Ruvu ili waweze kutambuliwa na wahusika,” alisema Nyigesa.Aliwataka watu waliowahi kuibiwa ngombe wao, kufika jeshi la polisi ili waonyeshwe ng’ombe hao na kuwatambua.Alitaka wananchi waendelee kutoa taarifa za uhalifu ili hatua za kisheria ziweze kuchukuliwa. | 3kitaifa
|
KIFO cha bilionea wa Kitanzania ambaye pia ni Mwenyekiti wa Kampuni za IPP, Dk Reginald Mengi kimegusa wengi katika nchi wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC).Mfanyabiashara huyo mzalendo na mwekezaji mkubwa katika sekta ya viwanda ambaye pia aligusa maisha ya kila siku ya watu wengi, aliaga dunia Alhamisi iliyopita Dubai katika Falme za Kiarabu baada ya kuugua ghafla. Ameondoka duniani akiwa na mipango mingi ya kutanua wigo wa uwekezaji katika nchi za EAC, kwani mbali ya Tanzania, Dk Mengi alishaanza mipango ya kupeleka nishati ya gesi nchini Rwanda kwa ajili ya matumizi ya magari ikiwa ni mbadala wa mafuta ya petroli na dizeli.Rwanda ingekuwa nchi ya kwanza Afrika Mashariki na Kati kunufaika na mradi wa gesi hiyo asilia kutoka mikoa ya Lindi na Mtwara. Kupitia kampuni ya IPP Energy, Dk Mengi aliyefariki dunia akiwa na umri wa miaka 75, alipanga pia kusambaza huduma hiyo katika nchi jirani za Kenya, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC), Burundi na hata Msumbiji ambako mradi huo haujafika.Kwa mujibu wa Godfrey Bitesigirwe, meneja wa mradi huo, tayari mazungumzo baina ya serikali ya Rwanda na uongozi wa IPP Energy Ltd ya Tanzania yalishakamilika na vibali kutolewa. Bitesigirwe alisema kama mradi huo ungeanza, Rwanda isingekuwa na haja ya kuagiza tena mafuta kutoka nchi za nje. Alisema Rwanda ilichaguliwa kuwa kitovu cha mradi huo, kabla ya kusambazwa katika nchi nyingine za ndani na nje ya Afrika Mashariki.Mkurugenzi wa Mamlaka ya Udhibiti wa Mazingira Rwanda, Mhandisi Coleta Ruhamya alikiri kuwa, serikali kupitia Wizara ya Miundombinu, Mamlaka ya Mapato na Mamlaka ya Mazingira, imeanza kutafuta suluhu ya tatizo la magari yanayotoa moshi na moja ya jawabu ni matumizi ya gesi asilia kwa magari. Na kwa mujibu wa ripoti ya Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF), matumizi ya mali asili kwenye maendeleo ya bara la Afrika yanaweza kuwa ni suluhisho la kudumu la umaskini barani humu.Mbali ya uwekezaji katika sekta ya nishati, Dk Mengi pia alikuwa mbioni kuanzisha kiwanda kikubwa cha vifaa vya kielektroniki, IPP Touchmate kilichokuwa kitengeneze simu za kisasa, kompyuta mpakato na vifaa vyake, kwa ajili ya soko la Tanzania, Afrika Mashariki na Afrika kwa ujumla. Mwili wa Dk Mengi ulitarajiwa kuletwa jana nchini kutoka Dubai, na utatarajiwa kuagwa leo jijini Dar es Salaam kabla ya kupelekwa Moshi mkoani Kilimanjaro kwa maziko keshokutwa. | 3kitaifa
|
LONDON, ENGLAND NYOTA wa zamani wa klabu ya Arsenal na timu ya taifa ya Ufaransa, Thierry Henry, amedai kuwa anatamani kuja kuwa kocha wa klabu hiyo ambayo inafundishwa na aliyekuwa kocha wake, Arsene Wenger. Wenger alimteua Henry kuwa kocha mkuu wa timu ya vijana chini ya umri wa miaka 18, lakini aliamua kuachana na timu hiyo ya vijana mara baada ya Wenger kumtaka achague jambo moja kuwa kocha wa timu hiyo au kuwa mchambuzi wa habari za michezo. Henry mbali na kuwa kocha wa vijana, pia alikuwa na mkataba katika kituo cha utangazaji cha Sky Sports kwa ajili ya masuala ya uchambuzi, hivyo alikuwa anafanya kazi sehemu zote mbili kwa wakati tofauti. Kauli ya Wenger ilionekana kumgusa sana Henry, hivyo aliamua kuachana na ukocha katika klabu hiyo ya vijana na kuendelea na majukumu yake ya uchambuzi. Hata hivyo, mchambuzi huyo ameweka wazi kuwa ana ndoto za kuja kuwa kocha wa klabu hiyo kutokana na kuwa na mapenzi ya dhati. “Nitakuwa muongo nikisema kuwa sitaki kuja kuwa kocha wa Arsenal, siku zote nimekuwa nikiipenda klabu hiyo kwa kuwa nimekuwa hapo kwa miaka mingi, hivyo Arsenal bado ni timu ninayoipenda. “Ninaamini ipo siku nitakuja kuwa kocha wa Arsenal, si mbali sana kutoka sasa kwa kuwa ni kazi yangu. “Kwa sasa naweza kuwa kocha wa klabu yoyote kutokana na leseni yangu, hivyo ninachokiangalia ni kuja kuwa kocha wa Arsenal, naendelea kujifunza mambo mbalimbali katika soka ili kuja kuwa bora zaidi. “Ninachokijua ni kwamba kabla ya kuja kuwa kocha mkuu, lazima uwe na uzoefu, ninachojaribu kukifanya ni kuyafanya yale yote ambayo kocha anatakiwa kuyafanya. “Ninaitakia kila la heri Arsenal kwa sasa na katika msimu mpya wa Ligi Kuu, ninaamini itafanya vizuri,” alisema Henry. | 5michezo
|
KWA siku saba kuanzia leo, Bunge litajadili mapendekezo ya bajeti ya serikali ya Sh Trilioni 33.11 ambayo kwa kiasi kikubwa imegusa hali ya maisha ya watanzania huku ikihitaji watanzania kufanya kazi kwa bidii na kulipa kodi kwa hiari ili kufanikisha azma ya kukusanya fedha hiyo, ambayo asilimia kubwa inatokana na mapato ya ndani.Bajeti hiyo ilizua gumzo kwa wananchi hasa kwa kuonesha dhamira ya kweli ya serikali ya awamu ya tano, moja kwa sababu ya kufuta tozo kero 54, zilizokuwa mwiba na vikwazo kwa wafanyabiashara, lakini pia kupunguza ushuru au kuufuta kwa baadhi ya vitu kama vile tozo ya uchimbaji visima binafsi.Waziri wa Fedha na Mipango, Dk Philip Mpango ambaye aliwasilisha hotuba hiyo mwishoni mwa wiki bungeni mjini hapa, alisema Sura ya Bajeti inaonesha kuwa jumla ya Sh trilioni 33.11 zinatarajiwa kukusanywa na kutumika katika kipindi cha 2019/2020.Katika fedha hizo mapato ya ndani yanaarajiwa kuwa Sh trilioni 23.05 sawa na asilimia 69.6 ya bajeti yote na kwamba serikali imelenga kukusanya mapato ya kodi ya jumla ya Sh.trilioni 19.10 sawa na asilimia 12.9 ya Pato la Taifa.Wakati serikali ikidhamiria kukusanya mapato hayo kwa njia ya kodi, pia yapo mapato ambayo sio ya kodi yanayotarajiwa kukusanywa kwa kipindi hicho ambayo jumla yake ni Sh trilioni 3.18 na mapato kutoka vyanzo vya Halmashauri ni Sh bilioni 765.5.Kwa makisio na matarajio haya ni wazi kwamba watanzania wanapaswa kujidhatiti na kulipa kodi kwa hiari na hiyo inawezekana kutokana na bajeti hii kuja na sura ya kuwainua wanyonge kwa kufuta kodi kero na kutoa mwanya zaidi wa wananchi kulipa kwa hiari.Katika mjadala wa leo na siku hizo saba matarajio ya wananchi ni kusikia wabunge wakigusia mambo ya msingi kama vile vipaumbele vya serikali kwa mwaka 2019/2020 ambavyo ni pamoja na azma ya kujenga uchumi wa viwanda.Katika hili wananchi wanategemea kusikia jinsi gani malighafi za ndani zitatumika kwenye viwanda vilivyopo na sio kutegemea malighafi kutoka nje lakini pia mjadala kuhusu viwanda vya samaki vilivyopo vinatoa ajira kiasi gani na jinsi gani kipato cha mwananchi kinaongezeka na kumnufaisha.Jambo la msingi pia katika mjadala unaoanza leo ni kusikia masuala ya pembejeo za kilimo na upatikanaji wake umemsaidiaje mkulima kuleta tija kwenye kilimo ambacho kimepewa kipaumbele kwenye bajeti hii kama eneo muhimu la kutiliwa mkazo.Pia mjadala kuhusu bajeti wananchi wanategemea jinsi gani wabunge watajadili masuala ya ukuaji uchumi na maendeleo ya watu, kwani hali ya uchumi inaonesha kuwa pato la mtanzania limekua kutoka Dola 1,044 mwaka 2017 hadi Dola 1,090 mwaka 2018.Lakini pia wakati bajeti ya mwaka 2019/2020 ikionesha ni bajeti ya kujitegemea zaidi kwa mapato ya ndani, huku misaada na mikopo kutoka nje ikiwa ni asilimia ndogo ya bajeti isiyozidi Sh trilioni nne.Suala la mradi wa kufua umeme kwenye mto Rufiji nao litakuwa moja ya hoja zitakazojadiliwa kutokana na bajeti hiyo kutenga Sh.trilioni 1.44 kama kianzio cha ujenzi wa mradi huo mkubwa nchini.Pia masuala ya ujenzi wa reli ya kisasa ya SGR ambayo umetengewa Sh trilioni 2.48 unategemewa kuwa mjadala mzito, kwani miradi hiyo ikifanikiwa kutekelezwa itaipaisha Tanzania na kuifanya nchi inayoelekea uchumi wa kati.Mjadala huo unatarajiwa kuhitimishwa kwa kupigwa kura ya wazi kwa wabunge wote hapo Juni 25, mwaka huu ili kuamua kama bajeti hiyo ipite au la.Baada ya hapo siku chache zilizobakia kabla ya bunge kusitishwa hapo Juni 28 mwaka huu miswada mbalimbali ukiwemo wa Sheria ya Fedha za Matumizi wa Mwaka 2019 (The Appropriation Bill, 2019) utasomwa. | 3kitaifa
|
MANCHESTER, ENGLAND KOCHA mpya wa klabu ya Crystal Palace, Roy Hodgson, amesema ubora wa klabu ya Manchester United ni sawa na bondia mwenye uwezo wa hali ya juu. Manchester United juzi ilishuka dimbani kwenye Uwanja wa nyumbani wa Old Trafford na kufanikiwa kuibuka na ushindi wa mabao 4-0 dhidi ya Crystal Palace, hivyo Hodgson amedai hawakuwa na uwezo wa kuwazuia wapinzani hao wasiibuke na ushindi. Mchezo huo ulikuwa wa saba katika michuano hiyo ya ligi kuu msimu huu, lakini Crystal Palace haikufanikiwa kupata ushindi kwa michezo yote na kuifanya ishike nafasi ya mwisho kwenye msimamo. Hodgson mwenye umri wa miaka 70, amekuwa kwenye kazi ya ukocha kwa miaka 40 huku akifundisha jumla ya timu 21 tofuti, alichukua nafasi ya kuifundisha klabu hiyo ya Crystal Palace baada ya aliyekuwa kocha wa timu hiyo, Franke de Boer, kufukuzwa kazi kutokana na kupoteza michezo mitano ya ligi, hivyo Hudgson amekiri kuwa Man United ni habari nyingine. “Nadhani lazima tukubaliane na matokeo, tulikutana na klabu ambayo ilikuwa kwenye uwezo wa hali ya juu kama bondia, hivyo tulikuwa na kila sababu ya kufungwa katika mchezo huo, siwezi kuwalalamikia wachezaji kwa kuwa hawakuwa na jinsi walizidiwa kila idara. “Kikubwa ni kujipanga kwa ajili ya michezo inayofuata, ninaamini nitapambana kuhakikisha tunaleta furaha kwa mashabiki na kuondoka kwenye nafasi tuliopo kwa sasa,” alisema Hodgson. Hata hivyo, kocha huyo anaamini kuwa kikosi chake kisingefungwa mabao mengi endapo wachezaji wake nane majeruhi wangekuwepo kama vile Christian Benteke, Wilfried Zaha, Ruben Loftus-Cheek na wengine. Mchezo unaofuata Crystal Palace watakuwa kwenye Uwanja wa nyumbani Oktoba 14 dhidi ya mabingwa watetezi, huo utakuwa mtihani mwingine kwa kocha Hodgson ambaye ana kazi ngumu kuhakikisha timu hiyo inabaki kwenye ligi msimu ujao.
| 5michezo
|
NA FARAJA MASINDE-DAR ES SALAAM MAHAKAMA ya Wilaya ya Ilala, Dar es Salaam imemhukumu kifungo cha miaka minne jela au kulipa faini Sh milioni moja sambamba na kulipa fidia ya Sh milioni 20, Vishal Pandia (33) raia wa India, baada ya kupatikana na hatia ya wizi wa Sh milioni 20. Akisoma hukumu hiyo jana, Hakimu Mkazi wa Mahakama ya Ilala, Flora Haule, alidai mahakama ilijiridhisha na ushahidi uliowasilishwa na upande wa mashtaka ambao ulikuwa na mashahidi wanne. “Mahakama imejiridhisha na ushahidi uliowasilishwa na upande wa mashtaka, hivyo inakutia hatiani kutumikia kifungo cha miaka minne jela au kulipa faini ya Sh milioni moja, pia unatakiwa kumlipa mlalamikaji fidia ya Sh milioni 20 ambazo unatakiwa kuzilipa kabla ya kulipa faini au kwenda jela, ili iwe onyo na fundisho kwa wote wenye tabia za wizi,” alisema Hakimu Haule. Mtuhumiwa ambaye ni mhasibu, hakupewa nafasi ya kujitetea kwa kuwa alikuwa ameruka dhamana, na hivyo kuilazimu mahakama hiyo kutoa hukumu Novemba mwaka huu kabla ya kukamatwa tena jana na kusomewa hukumu upya. Kwa mujibu wa hati ya mashtaka, ilidaiwa kuwa mtuhumiwa katika tarehe isiyofahamika kati ya mwezi Aprili na Mei 2013, maeneo ya Kiwalani Dar es Salaam, aliiba Sh milioni 17.7 mali ya Kampuni ya Guru Engineering Work Ltd akiwa ameaminiwa fedha hizo kwenda kulipa ushuru TRA na badala yake alitoweka nazo. Mshtakiwa anatumikia kifungo. | 3kitaifa
|
TAASISI inayojishughulisha na huduma za kuboresha afya pamoja na tohara kwa wanaume (Intra Health) imewafikia wanaume 305,715 mwaka huu na kuwafanyia tohara, jambo linalosaidia kupunguza maambukizi ya ugonjwa wa Ukimwi nchini. Aidha wanaume takriban 400,560 wanatarajiwa kufikiwa na kufanyiwa tohara hadi ifikapo mwaka 2019 katika mikoa saba na wilaya 33 nchini. Hayo yalisemwa jana Dar es Salaam na Mkurugenzi wa Programu kutoka Intra Health Dk Pastory Sekule wakati akieleza kuhusu utekelezwaji wa Mradi wa Tohara Plus ukiwa na lengo la kuimarisha huduma za tohara na kuhakikisha wanaume wa miaka 10 hadi 29 wanafanyiwa tohara na kufikia asilimia 90 katika mwaka 2020.Aidha alisema taasisi pia inaelekeza nguvu kwa kufanya tohara kwa watoto wachanga kuanzia mwezi mmoja hadi miezi miwili na huduma hiyo iweze kuwa endelevu ni lazima wakubwa wawe tayari wamefanyiwa kitendo hicho. Alisema mradi wa Tohara Plus unatekelezwa katika mikoa saba na wilaya 33 na taasisi hiyo kwa kushirikiana na wadau wengine wakiwemo Shirika la Tayoa na Afya Plus.Aliitaja mikoa inayoshiriki katika mradi huo pamoja na kiwango kiwango cha wanaume wasiofanyiwa to hara kwenye mabano kuwa ni pamoja na Simiyu asilimia (53), Shinyanga (52.5), Kagera (39), Kigoma (33.6), Geita (33), Mwanza (22.4) na Mara asilimia (9.5). Alisema mradi huo unafanyika katika mikoa ambayo kiwango cha maambukizi ya Ukimwi kiko juu huku wanaume wakiwa hawajafanyiwa tohara wakiwa na sababu mbalimbali.Hata hivyo, alisema kumekuwa na changamoto katika kuwafikia wanaume wenye umri mkubwa kuanzia miaka 20 na kuendelea huku wengine wakionesha kutokujua faida za tohara na wengine wakiona kama itakuwa kidonda kisichopona.“Ili kuwafikia watu wenye umri mkubwa wakati mwingine huduma inaweza kutolea usiku, wengine wakikataa kufanyiwa tohara na mhudumu wa kike lakini pia tunawahimiza wenzi wao waweze kuwaelimisha umuhimu wa tohara,” alisema Dk Sekule.Kuhusu watoto wachanga alisema wanalenga kuwafikia watoto 10,284, huku wakiongeza huduma iweze kutolewa kwa usahihi na kwa usalama zaidi ambapo wanahimiza tohara kufanyika pindi mtoto akianza huduma za chanjo nyingine. “Ikitokea tohara ikafanywa huondoa uwezekano wa maambukizi ya Ukimwi kwa asilimia 60, ingawaje sio kwamba ni tohara peke yake ndio inayopunguza maambukizi ya Ukimwi bali pia kuna uhitaji wa kutumia kondomu na hata kubadili tabia za mahusiano,” alisema. | 3kitaifa
|
Mwenyekiti wa Shiwata, Cassim Taalib alisema jana Dar es Salaam kuwa maandalizi ya sherehe hizo zitaambatana na ugawaji nyumba 31 kati ya hizo moja kubwa, tatu ndogo na misingi 27 ya nyumba hivyo kufikisha jumla ya nyumba 150.Alisema baba yake Mbwana, Ali Samatta amethibitisha kuwepo kwa mwanawe katika sherehe hizo ambazo naye ametunukiwa kuwa mwanachama wa heshima wa mtandao huo na kukubali kushirikiana kuhakikisha michezo inakua nchini.“Baba yake Samatta alisema wakati akiwa kijana alikuwa mfungaji mzuri kwa timu alizowahi kuchezea miaka ya 1960 kama vile timu ya Sekondari ya Mzumbe, timu ya mkoa wa Morogoro, timu ya Polisi na badaye aliwahi kuichezea Simba akiwa na akina Hamisi Kilomoni, “ alisema Taalib.Alisema sherehe hizo pia zitapambwa na wasanii kutoka vikundi mbalimbali vya ngoma na sarakasi kutoka, Dar es Salaam na mkoa wa Pwani.Alisema Shiwata ilimzawadia uanachama wa heshima mchezaji huyo baada ya kuchaguliwa kuwa mchezaji bora wa Afrika kwa wachezaji wa ligi za ndani na kutangaza kumpatia eneo la ekari tano kwa ajili ya kujenga kituo cha wanamichezo. Hivi sasa Samatta anachezea timu ya KRC Genk ya Ubelgiji na ameonesha uwezo wa hali ya juu katika timu hiyo iliyopo Ligi Kuu nchini humo. Samatta pia ni nahodha wa timu ya Taifa ya Tanzania ‘Taifa Stars’. | 5michezo
|
RAIS John Magufuli amesema mgogoro wa ardhi wa vijiji 33 katika Wilaya ya Mbarali mkoani Mbeya, kati ya wananchi na wawekezaji, utapatiwa ufumbuzi hivi karibuni, kwa kuwa ripoti ya Tume ya mawaziri wanane aliyoiunda, imeshakabidhiwa serikalini.Kauli hiyo ya Rais Magufuli ilikuja baada ya Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, William Lukuvi kumweleza kuwa kazi aliyowatuma wameshaimaliza na tayari ripoti wameikabidhi kwa Katibu Mkuu Kiongozi, ambaye pia na Katibu wa Baraza la Mawaziri. Kwa mujibu wa Lukuvi, wakazi wa vijiji hivyo 33 walipaswa kuondolewa kupitia Tangazo la Serikali Namba 28 kutokana na vijiji hivyo kuwa ndani ya hifadhi.Hata hivyo, uamuzi huo ulisitishwa na Rais Magufuli na kuamua kuunda Tume ya Mawaziri wanane ili kufuatilia suala hilo ili uamuzi wa haki, utolewe kwa upande wa wananchi na upande wa serikali.Lukuvi alimweleza jana Rais Magufuli kwenye mkutano wake wa hadhara na wananchi wilayani Mbarali mkoani Mbeya kuwa kazi ya kupitia upya maeneo, taarifa mbalimbali na sheria kuhusu mgogoro huo wameshaikamilisha. Kwa mujibu wa Waziri Lukuvi, Tume hiyo imeshakabidhi ripoti yake kwa Katibu Mkuu Kiongozi ambaye ni Katibu wa Baraza la Mawiziri ili iweze kujadili katika Baraza la Mawaziri chini ya uenyekiti wa Rais Magufuli na kisha kutolewa uamuzi wa ama kuwaondoa wananchi katika vijiji hivyo 33 au la.“Kazi tumeimaliza, tumepata taarifa ya mkoa, tumezungumza na viongozi na wananchi hawa, Baraza la Mawiziri litaketi chini yako na kukushauri na ikikupendeza uamuzi wa vijiji hivi 33 na vijiji vingine vilivyokuwa na matatizo kama hapa Mbarali uweze kutolewa, kwa hiyo Wanambarali suala ya GN 28 limekwisha, msubiri matokeo yakayotolewa na vikao halali,”alieleza Lukuvi.Kuhusu mgogoro wa mashamba ya Kapunga na Highland, Lukuvi alisema nao umeshafanyiwa kazi. Alisema mashamba hayo yalibinafsishwa na serikali kwa mujibu wa sheria na wanunuzi walipatikana. Alisema shamba la Kapunga lilinunuliwa na Kampuni ya Tanzania Export Trading Company ya Patel, wakati shamba la Highland lilinunuliwa na Mbunge wa Mbarali wa sasa, Haroon Mulla Pirmohamed.Baada ya hayo yote, Lukuvi alisema baada ya Serikali ya Awamu ya Tano kuingia madarakani, iliamua kufunga ekari 4,675 zilizokuwa zimeingizwa kwa mwenye shamba wakati zilitakiwa kuwa za wananchi na kuongeza kuwa kazi ya kuzirudisha ilikamilika mwaka 2016 wakati huo Mkuu wa Mkoa wa Mbeya akiwa Abbas Kandoro.“Baada ya mgogoro kati ya vijiji 11 na mmiliki wa shamba la Highland, tulifanya uhakiki ili kujiridhisha kama kweli shamba hili liliingia kwenye mipaka ya wananchi, baada ya uhakiki, ekari 1,352 zilikatwa kutoka shamba hili na kurudishiwa wananchi na mwaka 2018 Highland alipewa hati nyingine ambayo ina pungufu ya eneo la awali kwa ekari 1,352, na shamba namba 77 na 78 pia limerudishwa ambazo ni eakari 1,375,”alieleza Lukuvi.Bonde la Mto Ruaha Kuhusu uharibifu wa Bonde la Mto Ruaha, ambalo pia hujulikana kama Bonde la Usangu ni moja ya mabonde manne makubwa hapa nchini likiwemo Bonde la Mto Kilombero na Rufiji chini, alisema Bonde hilo lina ukubwa wa Kilomita za Mraba 85,554 sawa na asilimia 47 ya Bonde la Rufiji. Alisema vijiji 33 katika eneo hilo, viliathirika kutokana na Tangazo Namba 28 la Serikali ambapo kabla ya tangazo hilo, eneo hilo lilikuwa na ukubwa wa hekta 10,000, lakini baada ya tangazo likaongezwa na kuwa hekta 20,000.Kwa mujibu wa Rais Magufuli, katika hilo, kuna mambo ambayo serikali ilikosea na kuna mambo ambayo wananchi nao pia walikosea. Alisema kwa upande wa serikali wakati inatoa tangazo hilo la kufuta vijiji 33 vilivyokuwa na wakazi takribani 40,000, haikuelezwa wananchi hao wataenda wapi. Lakini, pia alihoji ni kweli kwamba serikali ilikuwa inalihitaji eneo lote hilo. Kwa kuwa Mto Ruaha Mkuu unaundwa na mito tisa, matumizi ya maji yaliyofanywa na wananchi wa eneo hilo kwa kilimo cha umwagiliaji, ulitishia uhai wa mto huo ambao ni muhimu kwa uzalishaji wa umeme kwa mabwawa ya Mtera na Kidatu na maporomoko ya Mto Rufiji ya Stiegler’s Gorge.Mbali na shughuli hizo za kilimo, wananchi pia walikuwa wakikata miti hovyo, kuingiza mifugo holela na shughuli holela za uchimbaji madini, ambavyo vyote viliathiri ustawi wa mto huo. Alisema kwenye miaka ya 1960, maji ya mto huo yalikuwa yakimiminika wakati wote. Lakini, kwa sasa maji hukatika hata kwa miezi sita na kusababisha vifo vya wanyama wakiwemo viboko na samaki.Kijiji cha Machimbo Kuhusu wananchi wa Kijiji cha Machimbo kutaka kulipwa fidia, Rais Magufuli alisema wananchi hao walishalipwa fidia ya Sh milioni 800 na waliobaki wanatakiwa kulipwa Sh milioni 31 tu. Alisema wananchi hao baada ya kuchukua fidia hiyo, hawakuhama na waliendelea na shughuli zao, hivyo hawatalipwa na wanatakiwa kuondoka.Alisema kama watabaki, watatakiwa kurudisha fedha hizo. “Kuna mradi mmoja uligharimu zaidi ya shilingi bilioni 20, baadaye mradi huo ukagawiwa kwa wananchi na kila mmoja alipata hekta 1 ili walime, lakini wananchi wale wakaanza kuuza maeneo yao kwa wafanyabiashara na waliowauzia wanajulikana, baada ya kuwauzia yakaenda kwenye mikono ya wajanja na wajanja hao wakaanza kuwakodishia wananchi kwa shilingi milioni 1,” alisema Rais Magufuli.Kuhusu ekari 4,675 na ekari 1,300 alizoagiza zirudi kwa wananchi, Rais Magufuli alitaka kujiridhisha kuhusu hilo na kuwaagiza Waziri wa Ardhi, Mkuu wa Mkoa, Mkuu wa Wilaya na Mkurugenzi, wampatie orodha ya watu waliopewa ekari hizo kwa sababu zinaweza kuwa ekari hewa. Rais Magufuli pia alisema Mwekezaji wa Shamba namba 77 na 78, alipewa kihalali na aliamua kukodisha mashamba hayo kwa wananchi kwa gharama ya Sh 2,295 kwa ekari, lakini madalali waliyauza maeneo hayo kwa kuyakodisha kwa Sh 600,000 hadi Sh 700,000, hivyo alimwagiza Mkuu wa Wilaya ahakikishe madalali hao wanatafutwa. | 3kitaifa
|
WAFANYABIASHARA wa madini ya rubi waliopo katika mji wa Mundarara na vitongoji vyake wilayani Longido mkoani Arusha, wamempongeza Rais John Magufuli (JPM) kwa agizo lake la kuhakikisha huduma ya soko la madini inakuwa katika kila mkoa.Mmoja wa wafanyabiashara wakubwa wa rubi na mmiliki wa kampuni ya Mundarara Minning, Rahimu Mollel alisema kwa niaba ya wenzake kuwa Rais Magufuli ameangalia vitu vingi muhimu katika sekta hiyo kibiashara na kuamua kila mkoa wenye machimbo, kufungua soko, jambo litakalonufaisha wafanyabiashara wa madini kote nchini. Mollel alisema jitihada hizo za Rais zinapaswa kuungwa mkono na wafanyabiashara wote wa madini na kuwa waaminifu katika kufanya biashara hiyo katika masoko yatakayofunguliwa.Alieleza kuwa mkoani Arusha soko hilo limefunguliwa katika Mji wa Namanga kilometa 50 kutoka katika migodi ya rubi iliyopo katika mji wa Mundarara. Alisema Mkoa wa Arusha kuamua kufungua soko la madini Namanga kutasaidia baadhi ya wafanyabiashara kutosafiri umbali mrefu na madini hadi Arusha mjini kwenda kufanya biashara na pia kutasadia kwa wale wasiokuwa waaminifu waliokuwa wakitorosha madini nchi jirani kufanya biashara Namanga na serikali kunufaika na kodi. | 3kitaifa
|
UCHAGUZI Mkuu wa Yanga unatarajiwa kufanyika Aprili 28, huku klabu hiyo ikiongozwa na kamati za muda baada ya viongozi wake wawili kujiuzulu jana.Mwenyekiti wa Baraza la Wadhamini wa Klabu ya Yanga, George Mkuchika alisema jana kuwa tarehe hiyo ya uchaguzi wataiwasilisha kwa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) ili kupata ridhaa. Alisema wameunda kamati mbili, moja itakuwa na watu saba, ambayo itakuwa na jukumu la kuisimamia timu katika mashindano mbalimbali, huku kamati nyingine ya watu 10 itakuwa na jukumu la kusimamia mchakato mzima wa uchaguzi wa klabu hiyo.Kamati ya usimamizi wa timu inaongozwa na Lucas Mashauri ambaye ni mwenyekiti wakati makamu wake ni Said Ntimizi wakati wajumbe ni Hussein Ndama, Samuel Lukumay na Hussein Nyika, ambao mapema jana walitangaza kujiuzulu, na Maulid Kitenge na Mosses Katabaro. Kamati ya kusimamia uchaguzi inaundwa na mwenyekiti Samuel Mapande wakati baadhi ya wajumbe ni Daniel Mlelwa, Mustafa Nagali, Geofrey Mapunda, Samuel Mangesho, Issa Gavu, Venance Mwamoto, Seif Gulamali na Dastun Kitandula.Alisema kuwa wanachama wasiwe na wasiwasi kwani uchaguzi huo utasimamiwa na wana Yanga wenyewe na TFF wameshakubali kuhusu hilo. Alisema kuwa dirisha la kuchukua fomu limefunguliwa rasmi na zitatolewa klabuni, ambapo wale waliochukua fomu watalazimika kuchukua bila malipo yoyote ya ziada. Mjumbe mwingine wa Bodi ya Wadhamini, Mama Fatuma Karume aliwataka vijana, wanawake na wanaume kujitokeza kwa wingi kuchukua fomu kwa ajili ya kuwania nafasi mbalimbali za uongozi.Awali kabla ya kutangaza kamati hiyo, Lukumay na Nyika waliungana na wenzao wawili, Siza Lyimo na Thobias Lingalangala waliojiuzulu tangu wiki iliyopita, huku wakiziacha mali za klabu pamoja na usimamizi wa timu chini ya Baraza la Udhamini. Wakizungumza na waandishi wa habari jana kwenye Ofisi za Makao Makuu ya Klabu hiyo Jangwani, walisema wameamua kuungana na wengine waliojiuzulu kwa vipindi tofauti kupisha uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika baadaye mwaka huu.MAPATO Katika hatua nyingine Mratibu wa Yanga, Hafidh Salehe alitangaza mapato waliyokusanya tangu kutangazwa kwa kampeni ya kuhamasisha uchangiaji ni zaidi ya Sh milioni 60, ambazo zimehifadhiwa katika Benki ya CRDB na nyingine zipo kwenye simu kupitia huduma ya Mpesa na Tigo Pesa na kuomba wanachama kuendelea kuchangia timu.Alisema zile fedha zinazochangishwa kwenye mechi mbalimbali haziingii katika akaunti hiyo bali hutumika kuwapa wachezaji kama bonasi. SAFARI YA MWANZA Kikosi cha wachezaji 20 cha Yanga kinatarajiwa kuondoka leo alfajiri kuifuata Alliance kwa ajili ya mchezo wa Kombe la FA utakaochezwa Jumamosi, huku wachezaji sita wakibaki kutokana na majeruhi na sababu nyingine.Kwa mujibu wa Ofisa Habari wa Yanga, Dismas Ten, wachezaji hao ni Abdallah Shaibu anayetumikia adhabu ya TFF, Juma Abdul, Mwinyi Haji, Juma Mahadhi, Mohamed Issa ‘Banka’ majeruhi na Ramadhan Kabwili anatumikia kikosi cha taifa cha vijana Ngorongoro Heroes. | 5michezo
|
MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Kisutu, Dar es Salaam imeshindwa kusikiliza kesi ya uchochezi inayomkabili Mwenyekiti wa Taifa wa Chadema, Freeman Mbowe na wenzake, kwa sababu mshitakiwa huyo ana miadi na daktari.Akiwasilisha hoja ya kuomba ahirisho la kesi hiyo likiambatana na nyaraka za daktari mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu Thomas Simba, Wakili wa Utetezi Peter Kibatala alidai afya ya Mbowe si nzuri na alitakiwa kuonana na daktari jana.“Mheshimiwa hali ya mshitakiwa bado si nzuri na alitakiwa kuonana na daktari lakini kwa kuheshimu amri ya Mahakama amelazimika kuomba daktari aahirishe miadi ili aweze kuhudhuria hivyo tunaomba ahirisho na kesi hii iendelee kuanzia Desemba 2 hadi 6, mwaka huu,” alidai Kibatala.Akijibu hoja hiyo, Mkurugenzi Msaidizi wa Mashitaka, Joseph Pande alidai Kibatala aliomba ahirisho Novemba 26 na kukubaliwa bila kuwepo maelezo ya miadi ya daktari hivyo inashangaza kuona taarifa hizo zikiwasilishwa jana. Alidai kama afya ya mshitakiwa ilikuwa haijakaa sawa na ana miadi na daktari ilitakiwa iwasilishwe Novemba 26, mwaka huu au wakati wowote mapema kabla ya shauri hilo.“Inashangaza taarifa hizi kuwasilishwa hapa leo nadhani taarifa hizi zilitakiwa kuwasilishwa mapema lakini kuzileta wakati huu ni kupoteza muda hivyo hatuoni sababu ya kuahirisha kesi,” alidai Pande.Mkurugenzi Msaidizi wa Mashtaka, Faraja Nchimbi alitoa hoja mbadala na kuomba mahakama iendelee na kesi hiyo kwa kufuata Kifungu cha 147 cha Sheria ya Ushahidi Sura ya Tano kinachoruhusu mshitakiwa mwingine kuendelea na ushahidi.“Mheshimiwa ikikupendeza niiombe mahakama ifuate Kifungu cha 147 cha Sheria ya Ushahidi Sura ya Tano kinachoruhusu mahakama imruhusu mshitakiwa aendelee na matibabu lakini iendelee kusikiliza ushahidi wa mshitakiwa mwingine,” alidai Nchimbi.Akitoa uamuzi baada ya kusikiliza hoja za pande zote mbili, Hakimu Simba alisema kesi hiyo ni ndefu na wasipokuwa makini haitaisha hivyo aliiahirisha jana tu kinyume cha maombi ya upande wa utetezi.Kesi hiyo itasikilizwa tena leo saa nne na nusu asubuhi. Novemba 26, mwaka huu, mahakama hiyo iliahirisha kesi hiyo hadi jana kwa madai kuwa hali ya afya ya Mbowe ambaye pia ni Mbunge wa Hai mkoani Kilimanjaro, haikuwa nzuri na alihitaji kupumzika. Ilielezwa mahakamani hapo kuwa anaumwa malaria, homa ya dengue na shinikizo la damu.Mbali na Mbowe, washitakiwa wengine katika kesi hiyo ni Naibu Katibu Mkuu Chadema Zanzibar, Salum Mwalimu, wabunge John Mnyika (Kibamba), John Heche (Tarime Vijijini), Halima Mdee (Kawe), Ester Bulaya (Bunda Mjini), Peter Msigwa (Iringa Mjini), Esther Matiko (Tarime Mjini) na Katibu Mkuu wa chama hicho, Dk Vincent Mashinji.Washitakiwa hao kwa pamoja wanakabiliwa na mashitaka 13 yakiwamo ya kula njama, kufanya mkusanyiko wenye ghasia, kuhamasisha hisia za chuki, kushawishi hali ya kutoridhika, uchochezi na kushawishi utendaji jinai kati ya Februari Mosi na 16, 2018, Dar es Salaam. | 3kitaifa
|
Kwa mujibu wa taarifa ya TFF, Kamati hiyo ilikutana Mei 5, mwaka huu na kufikia uamuzi huo. Ilisema kuwa akitoa utetezi wake mbele ya Kamati ya Nidhamu, Muro alikiri na kujutia kufanya kosa hilo na kudai ilitokana na ugeni wake katika uongozi wa michezo, kwa kuzingatia hilo kamatiilimwepusha na adhabu ya kufungiwa.“Kwa mujibu wa Ibara ya 53 (2)ya Kanuni za Nidhamu za TFF toleo la 2012, kwa kuidhalilisha TFF na Bodi yake ya Ligi mbele ya umma, Kamati imemtoza faini ya Sh 5,000,000 (milioni tano) Jerry Muro na kuwaonya viongozi wengine wa familia ya mpira wa miguu kutojihusisha na vitendo vya matamshi ya aina hiyo,” ilieleza TFF.Kuhusu shitaka linalomhusisha mshambuliaji wa Yanga, Amissi Tambwe kumshika kwa kumdhalilisha beki wa Simba, Juuko Mursheed, na kiongozi wa Friend Rangers, Hery Chibakasa kuhamasisha vurugu katika mchezo dhidi ya Majimaji ya Songea, mapema mwaka huu, kamati imeahirisha mashitaka hayo mpaka tarehe nyingine itakayopangwa.Aidha, Kamati iliahirisha malalamiko dhidi ya Mohamed Hussein, Muhibu Kanu, Manfred Luambano, Venance Joseph, Mussa Senyange, Saleh Ali, Shafii Maganga na Ismail Salim baada ya kupokea taarifa za udhuru zilizosababishwa na mgomo wa madereva wa mabasi ya abiria ya mikoani.Katika hatua nyingine, Katibu Mkuu wa TFF, Mwesigwa Selestine ameomba radhi kwa vyombo kutokana na madai ya waandishi wa habari kupata usumbufu wakati wa utoaji wa zawadi kwa mabingwa na washindi wa pili wa Ligi Kuu.Mwesigwa amesema kwa niaba ya TFF, anaomba radhi kwa usumbufu wowote uliowapata waandishi na wadau wote walioshindwa kushuhudia vyema tukio hilo.“TFF na FIFA vinatambua umuhimu na nafasi ya wanahabari na vyombo vya habari si tu katika kuutangaza mchezo, bali pia katika kutia chachu maendeleo ya mchezo wenyewe,” alisema Mwesigwa.Hali mbaya ya hewa ilivuruga utaratibu uliokuwa umepangwa awali kuanzia itifaki ya shughuli za kabla na wakati wa mchezo na zile za utoaji tuzo.Aidha, Mwesigwa alisema TFF itaendelea kushirikiana vema na jumuiya ya wanahabari, ikiwa ni pamoja na kuhakikisha kwamba wana mazingira mazuri wanapofanya kazi kwenye matukio ya mpira wa miguu. | 5michezo
|
NAIBU Katibu Mkuu (OR-TAMISEMI) anayeshughulikia Afya, Dk Doroth Gwajima amewataka wazazi na walezi kuwa makini na kuimarisha ulinzi na usalama wa mtoto wakati wa msimu sikukuu ya Idd.Dk Gwajima alisema hayo alipotembelea kituo cha kulelea watoto cha nyumba ya matumaini kilichopo kata ya Mihuji jijini Dodoma na kutoa misaada ya vitu mbalimbali kwa ajili ya sikukuu.“Ni wajibu wa kila mzazi kutekeleza jukumu lake la msingi la kuhakikisha mtoto yuko salama na anasherekea sikukuku katika mazingira rafiki na yenye kumjenga kimwili na kiakili zaidi bila kupata dhahama ya aina yoyote,” alisema Gwajima.Aidha, Dk Gwajima alimpongeza kituo hicho kwa jukumu kubwa walilo nalo la kuhakikisha watoto waliopo hapo wanapata malezi bora huku akiwaasa watoto kuzidisha upendo na mshikamano miongozi mwao. Kwa upande wake, Mkurugenzi Msaidizi anayeshughulikia masuala ya ustawi wa Jamii, OR-TAMISEMI, Rashed Maftah, alisema moja ya majukumu yao ya msingi na wajibu wao katika kuzihudumia Mamlaka zote 184 nchini katika kuhakikisha watoto waliokatika mazingira magumu wanapata vituo vya kuwalea katika misingi bora na usalama wao unaimarika.“Dini iliyosafi ni yenye kuwajali yatima na wenye uhitaji kwa kuunganika na kushiriki nao katika mahitaji yao ya Msingi, aidha Sheria ya mtoto namba 21 ya mwaka 2009 kanuni ya 12 inahimiza suala la kulelea watoto,” alisema Maftah. Akizungumza kwa niaba ya walezi wa kituo hicho, mmoja ya walezi, Sista Urea, alisema kituo hicho kina jumla ya watoto 63 na kimekuwa kikifanya kazi zake toka mwaka 1995 kwa kuhudumia watoto wanaopatikana katika mazingira magumu na ukatili wa kijinsia kutoka mikoa ya Dodoma na Singida. | 3kitaifa
|
Rais John Magufuli amemwagiza Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Albert Chalamila kuhakikisha serikali inagharamia matibabu ya mtoto aliyelawitiwa mkoani Mbeya.Mama wa mtoto huyo mwenye umri wa miaka 9, aliyejitambulisha kwa jina la Swaumu, alimwambia Rais Magufuli jana, Ijumaa kuwa mwanaye ana hali mbaya kiafya ikiwa ni pamoja na kutokwa na haja kubwa mfululizo, baada ya kulawitiwa na mwanaume wa miaka 53.Mama huyo alieleza kuwa hatahivyo amekuwa hapati ushirikiano wa kutosha kutoka kwenye vyombo vya dola. Akizungumza leo, Jumamosi katika viwanja vya Sabasaba, alipokuwa akifungua barabara ya Mbeya-Lwanjilo-Chunya na kuweka jiwe la msingi la ujenzi wa barabara ya Chunya- Makongolosi, Rais Magufuli amesema amefatilia kesi hiyo na mwanaume huyo amehukumiwa kifungo cha maisha.“Nilituma watu wangu waende gerezani kuangalia kama mtuhumiwa huyo yupo, na ni kweli walimkuta na wakampiga picha wakaniletea, na ninampongeza Hakimu Mkazi Michael Mteite, aliyetolea hukumu kesi hiyo,” alisema.Aliongeza kuwa jina la Hakimu huyo Mteite lipelekwe kwenye mapendekezo kwa Jaji Mkuu, kwa majina yatakayoteuliwa Ujaji, ili naye awe Jaji. | 3kitaifa
|
NA CHRISTOPHER MSEKENA IMEKUWA ni wiki ya matukio katika anga la burudani ndani na nje ya Bongo. Mashabiki wameyapa nafasi matukio makubwa ya mastaa kwa kuyajadili na kufanya yawe gumzo kwa namna moja ama nyingine. Swaggaz tunakusogezea matukio yote yaliyokuwa gumzo wiki hii kwa kuanzania hapa Bongo na tutamalizia kule Marekani ambako nako kumewaka moto kwa marapa Pusha T Drake kuvuana nguo. NGWEA AKUMBUKWA Hili ni gumzo la kumbukizi ya mitano ya kifo cha rapa na mkali wa mitindo huru wa muda wote Albert Mangwea, aliyefariki dunia Mei 28 mwaka 2013 huko, Johanesburg Afrika Kusini kisha mwili wake kurudishwa Bongo na kuzikwa Kihonda,Morogoro Juni 6 mwaka huo. Moja ya vitu vilivokuwa gumzo wiki hii ni mastaa mbalimbali kutumia nafasi zao kumkumbuka Ngwea kwa uwezo wake kimuziki, ucheshi, utani, kuwa mbele ya wakati, kuishi vizuri na watu pamoja na roho yake safi iliyomuwezesha kuishi na kila mtu katika mazingira yoyote. Miongoni mwa mastaa ambao hawawezi kumsahau Ngwea, ni Fid Q ambaye ataendelea kumkumbuka rapa huyo kwa kumfutisha mistari mbele ya P Funk Majani wakati wanarekodi wimbo CNN. Fid Q anasema alilazimika kufuta mistari baada ya kusikiliza mistari ya Ngwea na kugundua kuwa ilikuwa ni mizito kuliko yake. Ukiacha hilo gumzo la Fid Q, Jumbe nyingi ambazo aliziacha kupitia mtandao wa Twitter, siku moja kabla ya kufa kwake ndiyo zimefanya mashabiki waendelee kumkumbuka zaidi na kuona rapa huyo alikuwa anaaga bila kujua saa kadhaa mbele angefariki dunia. Miongoni mwa twiti hizo alizoandika Ngwea siku moja kabla ya kifo ni: “ Mambo 5 ya kumfanya mpenzi wako akupende kwa dhati (1) Mpe hela (2) Mpe hela (3) Wewe mpe hela (4) Nakwambia mpe hela (5) We mpe hela tu utaona”. “Sometimes mambo madogo madogo katika maisha yanaumiza sana kama unabisha kalia sindano”. Lakini pia siku hiyo mtangazaji Sam Misago alimuuliza Ngwea kama yupo salama maana amekuwa kimya sana naye akajibu : ‘Am perfect bro no worries’ (Nipo sawa kaka hakuna mashaka). Hizo ndiyo baadhi ya Twitter ambazo wiki hii zimetumiwa na mashabiki wengi kumkumbuka Ngwea ikiwa ni miaka mitano sasa imepita toka lipofariki dunia. GEORGE TYSON NAYE Ukiacha Ngwea, mwongozaji na mtayarishaji wa filamu mwenye asili ya Kenya George Otieno Ukumu Tyson, naye amefanyiwa kumbukizi ya kifo chake wiki hii, ikiwa ni miaka minne imepita toka afariki dunia kwa ajali ya gari mjini Morogoro, akiwa katika harakati za kuandaa kipindi cha The Mboni Show kilichokuwa kinaruka EATV. George aliyezaa na Monalisa mtoto mmoja anayeitwa Sonia, alijizolea heshima kubwa katika tasnia ya filamu kwa kutengeneza filamu kitofauti na waandaaji wengi akiwatumia watangazaji, wasanii wa muziki, wanamichezo na wanasiasa. Filamu kama Girl Friend na Dilema zinazoishi mpaka leo ni miongoni mwa kazi zake. AY ambaye aliwahi kushiriki katika filamu ya Girl Friend, aliposikia taarifa za msiba huo alikwenda hospitali ya Morogoro na kukuta jeneza aliloliona ni baya, ndipo alipokwenda kununua lingine nzuri kulingana na hadhi ya George (kwa mujibu wa Mboni). Mkali huyo alizikwa kijijini kwao Siaya, Kenya. PUSHA T & DRAKE Bifu katika muziki wa rap duniani kote ni kawaida. Mara nyingi hutumika kibiashara pale Mc au rapa anapotaka kuingiza sokoni singo au albamu yake hutumia bifu bandia kuongeza usikivu na msukumo wa mashabiki kuitafuta bidhaa hiyo. Wiki hii nchini Marekani rapa Pusha T na Drake wamepasha kipolo bifu lao lililoanza mwaka 2012, kwa wawili hao kukosoana katika muziki wao japo ilikuwa kimya kimya lakini hivi sasa wameamua kuliweka wazi kupitia mitandao ya kijamii. Kupitia wimbo Infrared Pusha T, alim ‘diss’ Drake kuwa hawezi muziki kwani anaunga unga mistari kama ushindi wa Trump huku akiwatumia ‘Gostwriters’ (Watunzi wa nyimbo) kumwandikia nyimbo kitu ambacho kilimuudhi Drake. Drake naye alijibu kwa kupitia ‘Duppy Freestyle’, aliyoitoa akiwachana Pusha T na Kanye West, kitu ambacho aliwahi kukifanya siku za nyuma alipokuwa kwenye bifu na Meek Mill. PUSHA T AJIBU, DRAKE ATULIA Jumatano wiki hii Pusha T alimjibu Drake kwa kuachia wimbo The Story of Adidon ambao alisampo ngoma The Story of OJ wa Jay Z huku kava ikitumika picha ya Drake akiwa amepaka rangi nyeusi. Pusha T alidondosha dongo kwa Drake kuwa ametelekeza mtoto wake wa kiume aliyezaa na Sophie, ambaye ni mcheza filamu za ngono. Mpaka sasa Drake hajajibu chochote kitu ambacho kimezua gumzo kwamba Pusha T, amegusa kwenye ukweli na sasa anatazamiwa Champagne Papi huwenda atajibu tuhuma hizo katika albamu Scorpion, inayotarajia kutoka mwezi huu. | 0burudani
|
Umasikini na kiwango kidogo cha elimu mara nyingi vina uhusiano na vinaweza kuwa chanzo cha msongo wa mawazo. Umasikini na kiwango kidogo cha elimu au pasipo na elimu kabisa vina uhusiano wa karibu sana na hali mbaya ya afya. Mara nyingi katika maeneo mengi, watu wenye elimu kubwa wamekuwa na afya bora pia. Umasikini husababishwa na mambo mengi ikiwemo uzee, kutosoma, kutengwa, kubaguliwa, kipato kidogo, mtazamo wa jamii juu ya jinsia fulani, mfano; katika jamii nyingi mwanamke hunufaika kidogo na hategemewi kumiliki mali. Hii inawafanya wanawake wazee ambao ni masikini kuwa wengi katika jamii nyingi kuliko wanaume wazee masikini. Mbali na kiwango cha elimu, yako maeneo mengine yanayoweza kuchangia katika umasikini na kuleta sana msongo wa mawazo kama vile; Hali hizi zote huleta msongo wa mawazo na maumivu makali moyoni, hali ambayo huweza kuathiri afya na hali nzima ya maisha ya mwathirika. Hii inajumuisha watu wasio na uhakika wa mahali pa kulala na hata mahali pa kupumzika wakati wa mchana. Watu wasio na makazi maalumu wako wa rika tofauti kuanzia watoto wa umri wa miaka 18 na kuendelea. Asilimia 45 ya watu hawa wasio na makazi maalumu inachangiwa na wanaume wasio na ndoa. Familia zisizo na makazi maalumu zimeongezeka kwa kasi kutoka miaka ya 1990. Kukosa makazi au mahali pa kulala na kuzurura mitaani kunasababishwa na sababu nyingi zikiwemo ugomvi na kutoelewana katika familia, kukosa kazi, kukosa kipato, kutengwa kwa sababu ya tabia mbovu n.k. Asilimia 22 ya wazazi wasio na makazi ni kwa sababu ya ugomvi wa nyumbani. Familia zenye nafuu kiuchumi huweza kujihudumia mahitaji ya siku, wazazi huyamudu majukumu yao kama wazazi, hawana sana matatizo ya kifedha, mavazi wala malazi, matatizo ya kiafya na ya talaka pia ni machache kwao. Tofauti na sababu hizi, familia zenye kipato cha chini huishi kinyume na hali zilizoelezwa hapo juu. Familia zilizo bora huwawezesha watoto kuishi na baba na mama zao wa damu kwa muda mrefu na hii huwajengea watoto uwezo mkubwa wa kukabiliana na mikikimikiki ya maisha na ufanisi shuleni. Watu wenye umri mkubwa (wazee) au wenye ulemavu, hukutana na vipindi vya msongo wa mawazo vya mara kwa mara katika maisha yao ya kila siku, hasa kwa sababu ya mtazamo fulani jamii iliyonayo kuhusu wao. Katika jamii nyingi, watu wanapokuwa na umri mkubwa hulazimika kuwapisha wenye umri mdogo waendelee na kazi na wao hutengwa, wengine huwekwa katika nyumba maalumu za watu wazee, wengine hurudishwa vijijini ili wasiwazuie wengine kiutendaji. Tofauti na nchi nyingi, Japan hutumia wazee kama chemichemi ya uzoefu na ujuzi. Katika hali kama zilizotajwa hapo juu, mtu aliyezeeka hujiona hafai na ni mzigo katika jamii na kwa waliomzunguka, hii huleta msongo wa mawazo sana kwao. Tatizo hili ni kubwa sana katika nchi za kwetu ambako umri wa kustaafu ni mdogo (kati ya miaka 60-70). Tukiwaangalia watu wenye ulemavu, wao huwa katika wakati mgumu zaidi, kwa sababu hudharauliwa na kutengwa na hata kutungiwa majina ya kuwadhihaki. Maumivu huwa makali zaidi pale wanapokumbuka kuwa ulemavu wao si wa leo na kesho tu, bali ni wa maisha yao yote. Watu wengi hasa katika familia wamekuwa wakiona walemavu kama mizigo, wasio na faida na ambao huwapotezea muda wao wa kufanya mambo mengine ya maana zaidi. Ni lazima jamii ibadilike kimtazamo, iwajali, kuwapenda na kuwaheshimu walemavu, wote tukijua ya kuwa hata kama watu hawa hawana baadhi ya viungo vinavyofanya kazi au kutumika, viko vingine vinavyoweza kutumika kwa ufanisi zaidi. | 4afya
|
ZAIDI ya tani tatu za ufuta uliochanganywa na uwele umekamatwa katika kijiji cha Miguruwe, wilayani Kilwa mkoani Lindi . Kukamatwa huko kumetokana na wapokeaji wa ufuta huo katika Chama cha Msingi cha Ushirika (amcos), Zinga, kushtukia magunia ya ufuta wakati wakifanya ukaguzi wa awali kwa kutumia fito maalumu (bamboo).Mwenyekiti wa Amcos hiyo, Mshamu Mpwate alisema ufuta huo ulifikishwa jioni ya Juni 24, mwaka huu na mfanyabiashara aliyejitambulisha kwa jina moja la Cheche, ulifanyiwa ukaguzi Juni 25, mwaka huu kwa kuwa wao jioni huwa hawafanyikazi na ulipokaguliwa gunia la kwanza ulionekana kuwa una uchafu lakini walipokagua magunia hadi kumi wakajiuliza aina ya uchafu unaonekana katika maguni hayo.Alisema wamekuwa wakisisitiza ukaguzi wa awali kutokana na agizo la Mkuu wilaya ya Kilwa, Christopher Ngubiagai aliyetaka uongozi na vyama vya msingi kuhakikisha ubora wa ufuta ili soko lisiharibiwe na kwamba ilibainika kuwa ufuta huo umechanganywa na uwele baada ya ukaguzi wa kina na wananchi wanaojua nafaka ya uwele kuthibitisha.Mwenyekiti huyo alisema kwamba huenda jambo hilo limefanyika kwa makusudi kwa kuwa kijiji hicho wala tarafa hiyo hailimi uwele na kwamba katika miaka yake miwili ya uongozi hajawahi kukumbana na tatizo la aina hiyo kwenye misimu ya mauzo ya ufuta. Mkuu wa wilaya Ngubiagai akizungumza na waandishi wa habari alisema kwamba serikali inamsaka mfanyabiashara huyo ambaye ametoroka baada ya ujanja wake kubainika na kuongeza kuwa ufuta huo kwa sasa upo chini ya uangalizi wa serikali ya kijiji, utachambuliwa na kisha kuuzwa na fedha zake kutumika kwa maendeleo ya kijiji.Alivitaka vyama vya msingi kuwa imara , kukagua na kujiridhisha kabla ya mnada na pia wakati wa kuusafirisha baada ya kuufungasha pamoja na kuwataka viongozi wa vijiji ,kata na maofisa tarafa kutembelea na kukagua mara kwa mara uendeshaji wa biashara ya ufuta ili kubaini changamoto kwa haraka na kuzichukulia hatua.Mkuu huyo wa wilaya aliendelea kusema kwamba kupatikana kwa ufuta huo uliochanganywa unatoa somo kwa vyama vyote vya msingi kuwa na uangalifu mkubwa ili ufuta wa Kilwa uendelee kuwa bora na kuwataka wafanyabiashara kufuata utaratibu uliowekwa na mkoa ili kuhakikisha kwamba shughuli za uuzaji ufuta unaneemesha wakulima na kuondoa manung’uniko ya kucheleweshewa malipo yao. | 3kitaifa
|
NA PENDO MANGALA -DODOMA WILAYA ya Dodoma inakabiliwa na uhaba wa mbegu za mazao yanayostahamili ukame kama mtama, hali inayosababisha baadhi ya wafanyabiashara kufanya udanganyifu kwa kuuza mbegu feki. Dodoma ni miongoni mwa mikoa yenye ukame ambayo wataalamu wa kilimo wamekuwa wakiwashauri wananchi kulima mazao yanayostahamili ukame kama vile mtama, uwele na mihogo, huku wananchi wakitahadharishwa kuwa makini wakati wa kununua mbegu. Mkuu wa Ghala la Hifadhi ya Chakula Kanda ya Kati (NFRA), Hopf Mwakaje alisema mbegu za mtama kwa wilaya hiyo hazipatikani. Wakizungumzia hali ya mvua hadi sasa, baadhi ya wakulima wamesema japokuwa wananchi wameandaa mashamba na wengi wao wameshapanda, bado mvua haiwapi matumaini ya kupata mavuno, kwani msimu wake umepita. Mkulima mwingine, Anna Mng’ong’o, alisema hali ni mbaya kutokana na mbegu za mtama kutopatikana. “Tunaomba Serikali itusaidie mbegu ya mtama na uwele kutokana na kuwapo uhaba mkubwa mbegu,” alisema. Katibu Tawala wa Wilaya Dodoma, Jastina Mboneko, alisema chakula kipo cha kutosha na hakutakuwa na tatizo la njaa. MTANZANIA ilitembelea soko kuu la Mazengo na kushuhudia uwapo wa vyakula vingi. Mwenyekiti wa soko hilo, Godson Rugazama, alisema kumekuwapo na ongezeko la bei kutokana na wakulima kushindwa kutoa vyakula kwa wingi kwa hofu ya hali ya mvua. | 3kitaifa
|
Lakini katika mkataba huo wa mauziano, Stamico italazimika kuilipa kampuni hiyo ya Afrika Kusini dola za Marekani milioni 4.0 sawa za zaidi ya Sh bilioni 6.4, kama fidia ya miundombinu ya mgodi uliopo.Malipo hayo kwa mujibu wa Mkurugenzi Mkuu wa Stamico, Gray Mwakalukwa, sio ya mara moja bali inatokana na sehemu ya faida ya Stamico ya mauzo ya tanzanite kadri uchimbaji utakavyoendelea.Mitambo ya uchimbaji na uzalishaji itabaki kuwa mali ya Tanzanite One na itaendelea kutumika na wabia wataifanyia matengenezo itakayoharibika. Kwa ubia huo sasa eneo hilo lenye leseni ya uchimbaji ya miaka 10 iliyotolewa na Wizara ya Nishati na Madini Juni 20, 2013 sasa litachimbwa kwa ubia wa wasilimia 50 kwa 50 kati ya Stamico na Tanzania One kwa kipindi chote hicho.Mwakalukwa alisema umiliki huo unatokana na Serikali kusimamia utekelezaji wa Sera ya Madini ya mwaka 2009 na Sheria ya Madini ya mwaka 2010.Chini ya sheria hiyo kampuni za kigeni haziruhusiwi kumiliki hisa zaidi ya asilimia 50 katika uchimbaji wa madini ya vito.Alisema mkataba huo umezingatia makubaliano ya awali ambayo tayari yametiwa saini na miongoni mwa makubaliano hayo ni kuwa Stamico na Tanzanite One watakuwa na gawiwo sawa la asilimia 50 kwa 50 litakalotokana na faida. | 1uchumi
|
MSANII wa Bongo Fleva Zuwena Mohammed ‘Shilole’amempongeza Waziri wa maliasili na utalii Hamis Kigwangala kwa kuanzisha kampeni ya Twenzetu Kileleni inayoshirikisha wasanii wa aina mbalimbali nchini kufanya utalii Mlima Kirimanjaro. Wiki kadhaa zilizopita wasanii wa muziki na maigizo waliungana pamoja kufanya utalii wa ndani ambapo walikwenda kupanda Mlima Kilimajaro katika kuhamasisha utalii wa ndani.Kupitia ukurasa wake wa mtandao wa kijamii wa Instagram Shilole alisema ki kubwa alichovutiwa na kampeni hiyo ni kuona Waziri Kigwangala naye akijumuika na wasanii katika kufanya utalii huo na kwamba wengi watahamasika kwenye hilo.“Mimi sikwenda, ila nimehamasika zaidi na nitak wenda lazima kama sio peke yangu nitakwenda mwakani ikija tena,”alisema Shilole.Alienda mbali zaidi na kumpongeza msanii Hamis Mwinjuma ‘MwanaFA’ aliyewakilisha vyema utalii huo kwa kufika kilele cha Mlima Kilimanjaro pamoja na wasanii wengine akiwemo Nurdin Bilal ‘Shetta’. Aliwapongeza wote walioshiriki utalii huo na kwamba watahamasisha na wengine hata wasiokuwa wasanii katika kufanya utalii | 5michezo
|
Hayo yalisemwa juzi na Mkurugenzi wa Mifumo ya Malipo ya Kitaifa wa Benki Kuu, Bernard Dadi wakati akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es salaam.Alisema benki zote zinazotoa huduma, zinatakiwa kutoa huduma za malipo hayo kuanzia saa 3 asubuhi hadi saa mbili na nusu usiku, tofauti na awali huduma hiyo ilikuwa ikitolewa muda wa kazi pekee.“Tumeona ni bora kuongeza muda ili kurahisisha huduma hizi hapo awali kulikuwa na usumbufu mkubwa katika malipo, watu walikuwa wakichelewa kulipia kutokana na muda wa benki kuwa mchache na tunatarajia hapo baadae tutasogeza muda zaidi hadi masaa 24,” alisema Dadi.Alitaka pia benki kuhakikisha fedha zinaingizwa kwenye akaunti ndani ya saa mbili baada ya kulipwa ili kuondoa usumbufu kwa wateja.Aidha Dadi amewataka wananchi wanaokwenda kulipia benki kuhakikisha wanatumia jina sahihi ili kuondoa usumbufu wa malipo unaoweza kutokea na kusababisha muamala wa fedha kurudishwa na kusababisha ucheleweshaji wa malipo.Mkurugenzi wa Huduma za Kifedha BOT, Masian Kobelo alikanusha uvumi kuwa kwa sasa sarafu za shilingi mia tano hazipo kutokana na sarafu hiyo kuwa na madini ya almasi Alisema kuna baadhi ya watu wamekuwa wakidai kuwa sasa Benki Kuu imesitisha kutoa sarafu hizo kutokana na sarafu hizo kuwa na madini.Lakini, alisema hakuna ukweli wowote kuhusu suala hilo. Alisema sarafu hizo zipo za kutosha na zitasambazwa kwa wingi. “ Sarafu zipo nyingi na hakuna madini yoyote katika sarafu hizo, hayo ni maneno tu ya watu,” alisema Kobelo. | 1uchumi
|
MICHEZO ya hatua ya nusu fainali michuano ya kikapu ya Sprite Bball Kings inatarajiwa kutimua vumbi kesho kwenye Uwanja wa ndani wa Taifa. Wiki iliyopita ilipigwa michezo minne ya robo fainali na kushuhudiwa mabingwa watetezi Mchenga Bball Stars wakitinga hatua hiyo kwa mara nyingine baada ya kuiondoa TMT kwa vikapu 91-61 na kufufua matumaini ya kutetea ubingwa huo. Matokeo mengine timu ya Tamaduni iliifunga Ukonga Hitmen vikapu 102-67, Flying Dribblers ikashinda vikapu 90-77 dhidi ya Dream Chaser, Kg Dallas ikaiondosha Water Insitute kwa vikapu 91-84. Michezo ya kwanza itakuwa ni kati ya Mchenga Bball Stars na Flying Dribblers, mchezo mwingine ni kati ya Kg Dallas dhidi ya Tamaduni na baada ya hapo zitarudi- ana tena katika viwanja vya Don Bosco Osterbay. Msemaji wa mashindano hayo Goza Chuma alisema mashindano yamekuwa na mvuto mkubwa huku baadhi ya timu zikionyesha ukakamavu mkubwa na ufundi wa hali juu. Alisema kutokana na ubora wa kila timu ngumu kutabiri ni timu gani itaondoka na sh milioni 10 na kuongeza kuwa michuano hiyo imekuwa ya kipekee kutokana na hamasa kubwa ya watu wanaojitokeza kushuhudia mashindano hayo.“Michuano imekuwa migumu mno na huwezi kutabiri nani atakuwa bingwa, ila tunashukuru hamasa imechukua nafasi yake nafikiri mashindano yanawagusa watu wengi,”alisema Chuma. | 5michezo
|
Wamesema hatua hiyo ya serikali imeonesha namna serikali ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) ilivyo sikivu kwa wananchi inaowaongoza na ndiyo sababu ikawasikia na kukijali kilio chao.Viongozi wa waendesha boda boda hao, walitoa pongezi hizo katika kikao chao na Mwenyekiti wa Jumuiya ya Vijana wa CCM (UVCCM) Aman Kajuna aliyekutana nao ili kujua mapendekezo yao juu ya kero zinazowakabili katika utekelezaji wa majukumu yao.Viongozi hao waliotokea katika wilaya mbalimbali za mkoani hapa, ikiwemo Mbeya Mjini na Mbeya Vijijini, Chunya na Rungwe waliwapongeza pia wanahabari nchini wakisema walikuwa kiunganishi kizuri kati yao na serikali wakati wakitoa kilio cha kubadili namba za usajiri. “Katika mafanikio ya jambo hili hatuwezi kuwaacha wenzetu wanahabari. Walikuwa kiunganishi baina yetu na viongozi wa serikali. Tunaamini wao wamewezesha kwa kiasi kikubwa kuwepo kwa maafikiano mazuri juu ya jambo hili,” alisema mmoja wa viongozi hao, Paul Christophe kutoka Mbeya.Kwa upande wake Noah Mwakajebele kutoka Tukuyu wilayani Rungwe, alishauri maofisa wa Mamlaka ya Mapato (TRA) kuutumia muda ulioongezwa kupita katika kanda za bodaboda na kutoa elimu juu ya ubadilishwaji wa namba za usajili za pikipiki sambamba na kushauriana juu ya kero zinazoleta mkanganyiko juu ya shughuli hiyo. | 1uchumi
|
Msanii Wakazi amesema kitendo kilichofanywa na msanii mwenzi Harmonize cha kuzindua album yake kwenye ukumbi wa Mlimani city siku kadhaa zilizopita si kitu kipya kufanyika nchini licha ya ukubwa wake wa tamasha hilo Wakazi ambaye alikuwa mmoja kati ya waalikwa 500 walihudhulia uzinduzi huo amesema kuwa kitu kama hicho kimefanywa na wasanii wengi nchini licha ya Harmo kukiongeza thamani tukio hilo kutoka na kuiga kutoka kwa wakongwe waliofanya hivyo siku za nyuma “Konde hajafanya kitu kipya… maana 2 years ago tulirudisha desturi ya albums na Launch events. (Vee, Me, Nandy, One Incredible, Barnaba, Fid Q) na Diamond sema alifanyia Kenya. Konde ame combine zetu zote, na ku raise the bar to the 10th Power with some next leve” aliandik wakazi kwenye ukurasa wake wa Twitter Harmonize amefanikuwa kuzindua album yake ya kwanza ya Afroeast siku ya March 14 mwaka huu huku ikiwa album ya kwanza kutoka Afrika Mashariki kufikisha jumla ya wasikilizaji milioni 2 kwenye mtandao wa Audiomark kwa siku nne baada ya kuweka kwenye mtandao huo Konde hajafanya kitu kipya… maana 2 years ago tulirudisha desturi ya albums na Launch events. (Vee, Me, Nandy, One Incredible, Barnaba, Fid Q) na Diamond sema alifanyia Kenya. Konde ame combine zetu zote, na ku raise the bar to the 10th Power with some next level shit. HONGERA pic.twitter.com/mvScaKh7Oj — The Leader #FreeTito #FreeTheo (@Wakazi) March 18, 2020 | 0burudani
|
NA AMINA OMARI, TANGA
ASKARI wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ), MT 69500 Sajini Taji John Komba na wenzake watatu, wamepandishwa kizimbani katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Mkoa wa Tanga kwa tuhuma za mauaji ya kondakta wa daladala.
Sajini Komba na wenzake, wanatuhumiwa kumuua kondakta wa daladala inayofanya safari zake kati ya Nguvumali na Raskazoni.
Wakisomewa shtaka la mauaji linalowakabili mbele ya Hakimu Mkazi Mfawidhi, Hilda Lyatuu, Wakili wa Serikali, Donata Kazungu alisema Januari 26, mwaka huu katika kambi ya jeshi iliyoko eneo la Nguvumali, mshtakiwa Komba akiwa na wenzake wanadaiwa kumuua Salum Kassim.
akili Kazungu, aliwataja washtakiwa wengine kuwa ni Yohana Warioba, Bernard Nicholaus ambao ni askari mgambo katika kambi hiyo Adamu Juma na Sofia John ambao ni wanafunzi.
Hata hivyo, watuhumiwa hao hawakutakiwa kujibu chochote kutokana na mahakama hiyo kutokuwa na mamlaka ya kusikiliza kesi za mauaji.
Mwendesha mashtaka huyo, alidai upelelezi wa kesi hiyo haujakamilika na inatarajiwa kutajwa tena Februari 26, mwaka huu. | 3kitaifa
|
ASILIMIA 33 ya wanaume 672 mkoani Dar es Salaam wamebainika kuwa na upungufu wa nguvu za kiume. Utafiti uliofanywa na Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI) kwa wanaume 672 ambapo kila wanaume watatu mmoja aligundulika kukosa nguvu za kiume ambapo pia idadi kubwa walibainika kuwa na magonjwa ya shinikizo la damu na kisukari. Daktari Bingwa wa Magonjwa ya moyo, Dk. Pedro Pallangyo alisema utafiti huo ni kati ya tafiti 16 zilizompa ushindi wa tuzo ya watafiti vijana wa Afrika kwa mwaka 2016/17 (Young African Researchers Awards 2017) ambapo alifanya katika kipindi cha mwaka mmoja. “Hali hii inaashiria kuwa magonjwa ya kisukari na shinikizo la damu yamekuwa yakiongezeka mara kwa mara jambo ambalo linasababisha athari ya nguvu za kiume kuwa kubwa,” alisema Dk. Pallangyo. Pamoja na mambo mengine alisema changamoto hiyo inaweza kutatuliwa iwapo jamii itakuwa na utaratibu wa kufanya uchunguzi wa afya mara kwa mara ili kugundua tatizo mapema na kupata matibabu. “Kama mgonjwa akiwahi matibabu mapema kabla mishipa ya damu haijaathirika zaidi anaweza kudhibiti sukari na shinikizo la damu na kurudi katika hali yake ya kawaida,” alisema Dk Pallangyo. | 4afya
|
UBORESHAJI wa daftari la kudumu la wapiga kura mkoani Mtwara, unatarajia kuanza rasmi Januari 12 hadi 18 mwaka huu. Hivyo, watendaji wa uchaguzi wametakiwa kutoa taarifa zilizokuwa sahihi, kwa wakati na kwa utaratibu uliowekwa.Hali hiyo itasaidia kila mwananchi mwenye sifa ya kuandikishwa kuwa mpiga kura, kujiandikisha ikiwemo wale wenye uhitaji wa kuboresha taarifa zao. Rai hiyo ilitolewa jana na Kamishna wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), Balozi Omary Mapuri wakati wa mafunzo ya uboreshaji wa uandikishaji wa daftari la kudumu la wapiga kura, mjini hapa.Alisema kazi hiyo ya uandikishaji daftari la kudumu la wapiga kura kuelekea uchaguzi mkuu mwezi Oktoba mwaka huu, inategemea utendaji wao pamoja na wadau wengine kama vyama vya siasa, asasi za kiraia na viongozi wa dini. Alisema tume hiyo inatambua umuhimu wa kutoa mafunzo hayo kwa watendaji ili elimu hiyo iweze kufika kikamilifu kwa wadau na wananchi na jamii.Alisema lengo ni kujenga imani kwa wananchi na kuweka uwazi katika utekelezaji wa majukumu hayo, kwani kila kundi la wadau lina nafasi na umuhimu wake. Mjumbe wa Tume hiyo, Asina Omari alisema uboreshaji wa safari hii, hautahusisha wapiga kura wote walioandikishwa kwenye daftari la kudumu la wapiga kura mwaka 2015.Bali utahusu wapiga kura wapya, ambao wametimiza umri wa miaka 18 na wale ambao watatimiza miaka 18 siku ya uchaguzi mkuu huo. Vituo vya kuandikisha wapiga kura hapa nchini vimeongezeka kutoka 36,549 hadi vituo 37,407.Kwa mkoa wa Mtwara vituo hivyo vimeongezeka kutoka 1,747 vikivyokuwepo mwaka 2015 hadi kufikia 1,779 mwaka huu. Hadi sasa tayari mikoa 18 imekamilisha uandikishaji nchini, tangu zoezi hilo lilipozinduliwa Julai 18, mwaka jana mkoani Kilimanjaro. | 3kitaifa
|
MANCHESTER, England MTANDAO wa Sun umefichua kuwa Manchester City wanaangalia uwezekano wa kumpa mkataba mpya winga, Raheem Sterling ambao utamfanya awe anavuna kitita cha pauni 300,000 (zaidi ya Sh milioni 650) kwa wiki. Hayo ni maelekezo ya Pep Guardiola ambaye anataka kuona mchezaji huyo akibaki kwenye kikosi hicho, hata kwa kiasi hicho cha fedha ambacho kitamfanya kuwa mchezaji anayelipwa mshahara mnono zaidi Ligi Kuu England. Kama mambo yatakwenda vizuri katika mazungumzo ya mkataba huo, basi Sterling mwenye umri wa miaka 22 atampiku hata staa wa Manchester United, Paul Pogba ambaye anakinga pauni 290,000 (Sh milioni 638) kwa wiki. Man City wanataka kumpa mkataba mpya licha ya kwamba nyota huyo wa kimataifa wa England amebakisha miaka miwili katika ule aliosaini wakati anatua klabuni hapo akitokea Liverpool. Inasemekana kuwa kutokana na mkataba wake wa kwanza wa miaka mitano aliosaini mwaka 2015, nyota huyo anapokea si zaidi ya pauni 180,000. Sterling amekuwa kwenye kiwango kizuri msimu huu kwani bao lake katika mchezo dhidi ya Southampton lilikuwa la 13. “Alicheza vizuri, ndiyo maana Man City walitoa fedha nyingi kumsajili. Sifa zote ziende kwake,” alisema Guardiola baada ya mchezo huo. Wakati wa dirisha la usajili la majira ya kiangazi, nyota huyo alikaribia kuondoka Etihad, hasa baada ya Man City kuipelekea Arsenal ofa ya pauni milioni 60 kwa ajili ya Alexis Sanchez. Kwa upande wake, Kocha wa Gunners, Arsene Wenger, aliitaka Man City kutoa kiasi hicho cha fedha pamoja na kumruhusu Sterling aelekee Emirates, kitu ambacho hakikumwingia akilini Guardiola. | 5michezo
|
WACHIMBAJI wadogo wa madini wamemweleza Rais John Magufuli namna wizi wa madini unavyofanyika katika migodi mbalimbali nchini.Wachimbaji hao kutoka mikoa takribani yote ya Tanzania Bara, wapo jijini Dar es Salaam kushiriki Mkutano Mkuu wa Kisekta wa siku mbili ulioandaliwa na Wizara ya Madini kwa lengo la kujadili changamoto zinazoikabili sekta hiyo. Rais Magufuli ambaye alikuwa Mgeni Rasmi kwenye mkutano huo akiongozana na Makamu wa Rais, Samia Suluhu Hassan, aliambiwa kuwa kundi linaloongoza kwa wizi wa madini hapa nchini ni wageni kutoka nje ya nchi wanaojishughulisha na biashara hiyo.Mmoja wa wachimbaji hao aliyejitambulisha kwa jina la Samuel Rugemalira alimweleza Rais Magufuli kuwa wageni ndiyo wanaoongoza kwa kutorosha madini nje ya nchi. Alisema wageni hao hata wakikamatwa na Polisi na kufikishwa mahakamani, cha kushangaza baada ya muda mfupi huonekana tena migodini wakiendelea na biashara yao ya kutorosha madini.Naye Solomon Mihayo alifichua kuwa Polisi hawana uwezo wa kudhibiti utoroshaji wa madini kutokana na mbinu nyingi za udanganyifu zinazotumiwa na watoroshaji hao. Mihayo alimweleza Rais kuwa katika nchi zingine, madini hayalindwi na polisi bali na wamiliki wenyewe. Baadhi ya mbinu zinazotumika kutorosha madini kwa mujibu wa Mihayo ni pamoja na kutumia matairi ya akiba ya magari ambapo madini hutumbukizwa na kisha tairi kufungwa tena vizuri mbinu ambayo siyo rahisi kwa polisi kuigundua. Mbali na njia hiyo, mchimbaji huyo mdogo wa madini alisema kuwa matunda kama vile matikiti maji pamoja na kabichi nayo ni nyenzo muhimu inayotumiwa katika kutorosha madini nje ya nchi.Alisema watoroshaji hutumbukiza madini kati kati ya tikiti maji au kabichi na kulirudishia vizuri, hivyo kuvifanya vyombo vya dola na mamlaka zingine kutositukia kirahisi aina hiyo ya wizi wa madini. Njia nyingine ambayo ilikuwa siyo rahisi kuigundua katika kutorosha madini ni matumizi ya vioo vya pembeni vya magari (Suit mirror). Alisema watoroshaji hutumia vioo hivyo kuficha madini na kuvuka nayo nje ya mipaka ya Tanzania. Mihayo alisema njia nyingine inayotumika kutorosha madini kupitia viwanja vya ndege nchini ni matumizi ya karatasi maalumu.Alisema karatasi hiyo ambayo huuzwa kwa Sh 3,000 hutumiwa na watoroshaji kufungashia madini kwa kuwa ina uwezo wa kuzifanya mashinie za ukaguzi (scanner) kushindwa kugundua. Alisema yeye na wadau wengine wa madini kwa kushirikiana na vyombo vya dola na mamlaka za viwanja vya ndege nchini, walifanya jaribio la kupitisha madini kwenye mitambo hiyo kwa kutumia karatasi hizo maalum katika Kiwanja cha ndege cha Mwanza. Alisema madini hayo yaliweza kupita kwenye mitambo yote kiwanjani hapo bila kugundulika isipokuwa mtambo mmoja tu ndiyo ulibaini kuwepo kwa madini kwenye karatasi hizo. “Mheshimiwa Rais, mipaka yetu kama vile pale Namanga au Sirali hutumika sana kwa kutoroshea madini kutokana na mwingiliano wa watu.Kitendo cha watu kuingia na kutoka upande mmoja wa nchi kwenda upande wa nchi nyingine, umetoa mwanya kwa watoroshaji kuvusha madini,”alileza Mihayo. Kutokana na kufichuliwa kwa mbinu hizo za wizi wa madini, Rais Magufuli naye aliongeza kuwa licha ya kujengwa kwa ukuta kuzunguka machimbo ya Tanzanite huko Mirerani mkoani Manyara, lakini bado wizi wa madini hayo unaendelea.Rais Magufuli alisema kuwa baadhi ya watu hufanya mpango na wafugaji wanaojifanya kuchunga mifugo yao karibu na ukuta huo lakini lengo lao likiwa ni kutorosha madini. Rais alisema watu hao hurusha Tanzanite nje ya ukuta huo na kisha kuchukuliwa na watu hao wanaojifanya kuwa ni wafugaji. Namna ya kudhibiti wizi Katika kuhakikisha madini mbalimbali nchini yanalinufaisha taifa na siyo wageni ambao wametajwa kuwa vinara wa utoroshaji wa madini hayo, wadau hao wa madini wamependekeza kuwepo kwa soko la madini nchini ili shughuli zote za uuzaji na ununuaji zifanyike hapa nchini.Rais wa Shirikisho la Vyama vya Wachimbaji Wadogo wa Madini nchini (FEMATA), John Bina, alisema kuwa mpaka sasa hakuna masoko rasmi ya kuuza na kununua madini. Bina alisema jambo hilo linawafanya baadhi ya wachimbaji kuyatorosha madini hayo nje ya nchi ambako kuna soko. Alisema anachohitaji mchimbaji baada ya kupata madini ni fedha, hivyo anapokosa sehemu ya kuuzia madini hayo hapa nchini, huamua kuyatoroshea nje ya nchi.Kwa mujibu wa Bina, kama masoko ya madini ya uhakika yataanzishwa nchini, yatasaidia kudhibiti utoroshaji wa madini kwa kuwa itakuwa rahisi kwa Serikali kufuatilia kupitia vyombo vyake. “Pia hakuna bei sahihi na elelezi ya madini hapa nchini, matokeo yake kuna ukwepaji mkubwa wa kodi ya Serikali. Kuna fedha nyingi ya kununulia madini inayoingizwa nchini kwa njia ambazo siyo rasmi, hayo yote yanachangia madini kutoroshwa nje ya nchi,” alieleza Bina. Katika kukabiliana na utoroshaji wa madini ya Tanzanite, Rais huyo wa FEMATA, alipendekeza madini hayo yawekewe hati ya utambulisho ya Tanzania. Alisema hati hiyo ni muhimu kwa kuwa dunia itambua kuwa ni Tanzania pekee ndiyo inayozalisha Tanzanite na siyo nchi nyingine.Kwa mujibu wa wadau hao wa madini, njia nyingine ya kudhibiti wizi wa madini ni kuanzishwa kwa viwanda vya kuchenjulia madini kama vile dhahabu. Walisema kuwepo kwa mitambo hiyo kutasaidia kudhibiti watoroshaji wa madini ambao hutumia ukosefu huo wa mitambo ya kuchenjulia kutorosha madini. Kwa kuwa biashara ya madini imejaa ujanja mwingi na watu wanaofanya biashara hiyo ufahamu wa kutosha kuhusu masoko ya madini duniani, Askofu wa Kanisa la Ufufuo na Uzima, Josephat Gwajima, aliishauri Serikali kuajiri watu wenye akili na uelewa wa biashara hiyo ili kukabiliana na siasa ya biashara ya madini. | 3kitaifa
|
TUNU
NASSOR -Dar
es Salaam VIFO
vitokanavyo na uzazi vinaweza kupungua kutoka vifo 556 kwa kila vizazi 100,000
hadi 292 iwapo kutakuwa na uwekezaji wa kutosha katika uzazi wa mpango. Hayo
yamesemwa na Meneja Utetezi kutoka mradi wa Advance Family Planning, James
Mlali, alipowasilisha mada katika mafunzo ya waandishi wa habari juzi. Alisema
changamoto iliyopo ni kutokupelekwa kwa wakati fedha za bajeti zinazopangwa kwa
sekta hiyo. “Tunaiomba
Serikali kuhakikisha inapeleka kwa wakati bajeti inayopangwa katika uzazi wa
mpango ili huduma zitolewe kwa kiwango kilicho bora,” alisema Mlali. Alisema kwa mujibu wa takwimu, Mkoa wa Geita
unaongoza kwa kutokutumia njia za uzazi wa mpango. Aliongeza
kuwa uwekezaji zaidi katika afya ya uzazi wa mpango utasaidia kupunguza mimba
za utotoni kutoka 1,006 hadi kufikia 72 kwa mwaka. “Hii
itasaidia kuwapo kwa chakula cha kutosha kwa kuwa hadi sasa zaidi ya asilimia
54 ya Watanzania hawapati chakula mara tatu kwa siku,” alisema Mlali. Naye
Ofisa Utetezi, Halima Sharriff alisema kuwekeza zaidi katika afya ya uzazi wa
mpango kutasaidia kupunguza idadi ya vijana tegemezi kwa kuwa jamii itaweza
kuwa na watoto ambao wataandaliwa kwa kuwapa elimu na malezi bora. “Kwa
sasa Watanzania tegemezi ni asilimia 66.9 ambao asilimia 43.9 ni watoto wenye
umri kati ya miaka 0 hadi 14, vijana wenye umri kati ya miaka 15 hadi 24 ni
asilimia 19.1 na umri kuanzia 65 na zaidi ni asilimia 3.9,” alisema
Halima. | 4afya
|
|Veronica Romwald, Dar es salaam Taasisi ya Saratani Ocean Road (ORCI) itaanza kuwafanyiwa upasuaji wa kupandikiza matiti kwa wanawake waliopoteza matiti kutokana na ugonjwa wa saratani. Upasuaji huo kwa kitaalamu ujulikanao kama ‘Breast reconstruction after mastectomy’ utafanyywa kwa kurudishia tena kiungo hicho. Mkurugenzi wa ORCI, Dk. Julius Mwaiselage amesema hospitali hiyo iko katika maandalizi ya kufikia hatua hiyo ya upasuaji wa kibingwa ikiwa ni moja kati ya makubaliano ya ushirikiano na Taasisi ya Saratani ya nchini China (Chinese Academy of Medical Science – Cancer Hospital). “Saratani ya matiti ni miongoni mwa saratani zinaozoongoza kuwa na idadi kubwa ya wagonjwa wanaowapokewa na kuhudumiwa hospitalini hapa. “Hivyo, tutashirikiana na wataalamu wenzetu kutoka katika Taasisi hiyo, upande wa upasuaji wa saratani hii, ikigundulika mapema si lazima kutoa titi lote, tunaweza kutoa ule uvimbe uliopo pale na kuacha titi lakini lazima uwe na mashine za kisasa za kutoa tiba mionzi (LINAC) ambazo tayari tunazo,” amesema. | 4afya
|
WAZIRI Mkuu Kassim Majaliwa amewaagiza watendaji katika ngazi zote, wahakikishe kuwa vijana wanawezeshwa kushiriki shughuli za maendeleo.Alitoa agizo hilo jana wakati akizindua maadhimisho ya wiki ya vijana kitaifa kwa mwaka huu kwenye viwanja vya Mpilipili, nje kidogo ya mji wa Lindi.“Vijana tushirikiane na serikali na kufanya kazi kwa bidii ili kuunga mkono jitihada za serikali inayoongozwa na Rais John Magufuli, katika kuwaletea wananchi maendeleo. Hatua hii itatuwezesha kama taifa tuvuke na tufikie uchumi wa kati ifikapo mwaka 2025,” alisema.Alisema kuwa wakati akitembelea mabanda ya maonesho, aliona ubunifu wa kijana aliyeunda mashine ya kumsaidia mtoto njiti, apate joto na pia aliona kijana mwingine aliyebuni mtambo wa kupukuchua magunia 100 ya mahindi kwa saa.Pia, alitembelea banda la kikundi cha vijana kutoka China, Korea Kusini, Argentina, Arzebhaijan na Tanzania, ambao waliishi kwenye mazingira magumu na wakabadilika na kuamua kushiriki maonesho hayo ili kuwabadili mtazamo vijana wenzao.“Nimefurahi kuwaona hawa vijana, ninaamini watashirikiana na wenzao wa hapa kuwabadilisha vijana wa Tanzania wawe na fikra endelevu.”Akizungumzia mikakati ya kuwawezesha vijana kiuchumi, Waziri Mkuu alisema Ofisi ya Waziri Mkuu kupitia Programu ya Kukuza Ujuzi Nchini, imeanza kutoa mafunzo ya kilimo cha kisasa kwa kutumia teknolojia ya kitalu nyumba katika mikoa yote na halmashauri zote nchini.Alisema teknolojia hiyo itawasadia wakulima kupata mazao mengi katika eneo dogo na kupata mazao bora, yanayokidhi viwango katika soko la ndani na nje ya nchi.“Kwa kutumia teknolojia hii, vijana wengi watapata ajira katika sekta ya kilimo,”alisema. | 3kitaifa
|
LONDON, ENGLAND MAKOCHA wawili wapya, Maurizio Sarri wa Chelsea na Unai Emery wa Arsenal, leo kwa mara ya kwanza wanatarajia kuvaana katika mchezo wa Ligi Kuu England utakaochezwa Uwanja wa Stamford Bridge. Klabu zote zimefanya mabadiliko katika dirisha la usajili lililopita, zikiwa na matumaini kwamba zinaweza kupata mafanikio. Mchezo wa kwanza wa Ligi Kuu England, Chelsea iliifunga Huddersfield mabao 3-0 wakati Arsenal ikianza kwa kichapo cha mabao 2-0 kutoka kwa mabingwa watetezi Manchester City. Mchezo huo unaonekana kutoa muda wa ziada kwa makocha hao kujenga vikosi vyao kabla ya kufurahia mafanikio. Sarri atahitaji kushinda mchezo wa kwanza akiwa nyumbani wakati Emery hataitaji kupoteza tena baada ya kichapo cha mchezo uliopita. Chelsea imeifunga Arsenal mara 62 lakini imepoteza mara 76. Timu hizo zimewahi kutoka sare mara 52, ikijumuisha mara mbili msimu uliopita. Katika mchezo uliopita dhidi ya Huddersfield, Eden Hazard, alitumika kama mchezaji wa akiba ila inawezekana Sarri akamwanzisha dhidi ya Arsenal. Hata hivyo, inawezekana Hazard kuanza kikosi cha kwanza akichukua nafasi ya Willian da Silva au Pedro Rodriguez au akacheza nafasi ya ushambuliaji ambayo hucheza Alvaro Morata ambaye kwa sasa hayupo katika kiwango bora. Arsenal wanahaha kufanya uchaguzi safu yao ya ulinzi, Unai Emery, anaumiza kichwa kupata chaguo sahihi kumtafuta beki wa kushoto. Kuumia kwa Ainsley Maitland-Niles katika mchezo dhidi ya Manchester City, aliungana na Nacho Monreal na Sead Kolasinac, ambao wote wapo majeruhi. Emery anaweza kumtumia Stephan Lichtsteiner ambaye aliziba pengo la Maitland-Niles, kocha huyo pia ataendelea kumtumia Petr Cech dhidi ya kipa mpya, Bernd Leno. | 5michezo
|
IKIWA imebaki wiki moja ya kuwasilisha fomu ya Tamko la Rasilimali na Madeni kwa viongozi wa umma ni asilimia 17 tu ya viongozi hao, ndio wamefanya hivyo.Kamishna wa Maadili, Jaji Mstaafu Harold Nsekela amesema hakutakuwa na muda wa nyongeza na asilimia 83 ya waliobaki, watatakiwa kufanya haraka kabla ya muda kwisha au watakabiliana na Tume ya Maadili kwa hatua zaidi.Akizungumza na waandishi wa habari jana, Jaji Nsekela alionesha kukerwa na mwitikio mdogo wa uwasilishaji wa fomu hizo za tamko la rasilimali na madeni.Aliongeza kuwa kati ya viongozi 13,699 ni viongozi 2,369 tu ndio wamewasilisha hadi kufikia Desemba 20, mwaka huu.Alisisitiza viongozi hao kuhakikisha wanajaza taarifa sahihi za rasilimali na madeni yao katika ukurasa 18 wa fomu hiyo, kama inavyotakiwa.“Kujaza fomu dakika za mwisho na kwa shinikizo sio vizuri na mara nyingi kuna hatari ya kuruka baadhi ya taarifa muhimu wakati wa kujaza. Tunapaswa kujitahidi kuwa wawazi na kufuata maadili tunapofanya kazi hii,” alisisitiza.Kamishna huyo wa Maadili alisema jitihada hizo ni kutekeleza Sheria ya Maadili ya Viongozi wa Umma Namba 13 ya Mwaka 1995 (Ukurasa 398), hasa kuangalia tabia na maadili ya viongozi wa umma.Jaji Nsekela alibainisha kuwa kujaza fomu ya tamko ilikuwa ni lazima, ambapo kila kiongozi wa umma aliyeainishwa kwenye Sheria ya Maadili ya Viongozi wa Umma, anapaswa azingatie, kwani ni hitaji la kisheria na kikatiba.Alifafanua kuwa maendeleo ya haraka ya kiuchumi, yanaweza kuchochewa kwa kuzingatia maadili, hivyo viongozi wa umma watakaposhindwa kuwasilisha fomu za tamko ni kurudisha nyuma juhudi hizo.“Viongozi lazima waongozwe na sheria bila nguvu au shinikizo, hivyo kuwasilisha fomu ya tamko lazima kufanyike kulingana na sheria. Wale ambao watashindwa kufikia tarehe ya mwisho hawapaswi kulaumu mtu yeyote, kwani tumekuwa tunawakumbusha kila wakati,” alionya.Kamishna huyo alibainisha kuwa amekuwa akihamasisha na kuhabarisha umuhimu wa kutekeleza kanuni na maadili, ambayo ni lazima yazingatiwe na viongozi wote wa umma wakati wakitekeleza majukumu yao rasmi kwa kufuata kanuni za uongozi wa umma.Kusudi la kuweka misingi ni kuongeza imani kwa umma juu ya uadilifu wa viongozi wa umma katika mchakato wa maamuzi ya serikali. | 3kitaifa
|
Mara kwa mara busu na kupigana pambaja ni jambo ambalo huchukuliwa kuwa la kawaida kati ya wapendanao, lakini je umewahi kufiria kuhusu faida zake za kiafya. Nam, si siri tena, kubusiana kuna faida chungu nzima, kando na kuwa ishara ya mapenzi. Hizi ni baadhi ya faidi za kubusiana: 1. Huamsha homoni za furaha Kubusu kunaamsha akili ili kutoa kemikali kadhaa ambazo huutekenya mwili na kuuacha ukiwa umechangamka kwa furaha. Kemikali hizi ni pamoja na Oxytocinm Dopamine na Serotonin, kemikali hizi ni muhimu katika kuichangamsha mwili na akili kwa jumla. 2.Kuimarisha uhusiano Kemikali ya Oxytocin inafanya kazi muhimu ya kuimarisha uhusiano kati ya wapenzi. kemikali hii hutolewa na akili wakati wa kubusiana. 3.Huondoa msongo wa moyo Imebainika kuwa busu ni njia muhimu katika kupunguza msongo wa moyo. Kando na kubusu, ni vyema kumkumbatia na kumwambia mpenzi maneno matamu wakati wa kumbusu ili kuondoa kabisa msongo wa moyo. 4.Kupunguza shinikizo la damu Kubusu kunaimarisha mpigo wa moyo na hivyo kusaidia katika kuongeza kasi ya damu mwilini. Kasi ya damu mwilini inapoimarika nalo shinikizo la damu linapunguka. 5.Kupunguza uchungu wa hedhi Imebainika kuwa mwanadada ambaye hubusu mara kwa mara hawi na uchungu wakati wa hedhi ama kwa wengine hupunguka kabisa. Hii ni kwa sababu damu hupata urahisi wa kuteremka katika mishipa. 6.Huimarisha kinga ya mwili Utafiti uliofanyika 2004 ulibaini kuwa wapenzi ambao hubusiana mara kwa mara huwa na homoni moja katika mate yao. Hii husadia katika kuimarisha kinga ya mwili maana mwili unakuwa tayari kwa kemikali zisizo zake. Kilicho muhimu ni kuwa kubusu kuna faida kubwa pasi kuzingatia anayebusiwa wala wa kubusu. Kubusu kunaleta msisimko wa aina yake ambao husaidia katika kuuchangamsha mwili. | 0burudani
|
Na MWANDISHI WETU-MWANZA MSANII wa muziki wa Kizazi kipya nchini, Ali Kiba anayetamba na wimbo wake wa ‘Seduce Me’, amewapagawisha wakazi wa Mwanza waliofurika katika Uwanja wa CCM Kirumba, kushuhudia tamasha la Tigo Fiesta lililofanyika juzi usiku. Kiba ambaye alipanda jukwaani na kuimba wimbo huo, ilimlazimu kurudi jukwaani mara tatu kuimba wimbo huo ambao mashabiki walikuwa wakifuatisha kuimba wimbo huo pamoja naye. Kiba alionyesha umahiri wake wa kuimba wimbo huo pamoja na kucheza na hivyo kuamsha shangwe kwa mashabiki waliofurika katika uwanja huo. Tamasha hilo la Tigo Fiesta lilifunguliwa na msanii Rosa Ree ambaye alionyesha umahiri wake kwa kuimba nyimbo zake zikiwemo ‘Mchaga mchaga’ na ‘Up in the air’ na kisha kupanda jukwaani msanii Lulu Diva. Wasanii Roma na Stamina wao walikuja kivingine walipopanda jukwaani, kila mmoja na baiskeli yake na kuweka kitu tofauti kwenye wimbo wao wa ‘Huku ama kule’ na kuwa kivutio kwa mashabiki waliofurika katika uwanja huo. Pia msanii Ben Pol alipanda jukwaani na kuimba wimbo wake wa Moyo Mashine, huku akisindikizwa na msanii Mau Sama aliyepanda jukwaani kucheza naye na kufanya mashabiki wapige kelele za shangwe. Wasanii wengine walionogesha tamasha hilo ni Ommy Dimpoz ambaye alizindua wimbo wake mpya wa ‘Cheche’ uliokuwa gumzo pamoja na Rayvanny ambao hawakushiriki matamasha yaliyopita. Meneja wa Tigo Kanda ya Ziwa, Edgar Mapande, alisema mwaka huu wameamua kudhamini Fiesta ili kusaidia vipaji vya wasanii na kuwaletea wateja wao burudani na kurudisha faida kwa jamii. Kaulimbiu ya Tigo Fiesta mwaka huu ni ‘Tumekusoma’ na kwamba baada ya wasanii hao kuuwasha moto Mwanza, Ijumaa watahamia Tabora katika Uwanja wa Ali Hassan Mwinyi na burudani hiyo kuendelea katika mikoa ya Mwanza, Tabora na Dodoma. Maeneo mengine ambayo Tigo Fiesta itafanyika ni Iringa, Songea, Njombe, Sumbawanga, Morogoro, Tanga, Kilimanjaro, Mtwara na kuhitimishwa jijini Dar es Salaam. Akizungumza kuhusiana na tamasha la mwaka huu, Mwenyekiti wa Kamati ya Maandalizi ya Fiesta, Sebastian Maganga, alisema Tigo Fiesta ni burudani ya kipekee ndani ya Ukanda wa Afrika Mashariki na kwamba mashabiki wamefurahia burudani Arusha na wataendelea kufurahia zaidi katika mikoa mingine. “Tutawaletea wasanii wenye hadhi kulingana na mapendekezo ya mashabiki husika wa mkoa huo, tena wale waliojizolea sifa ndani na nje ya nchi,” alisema. | 0burudani
|
Akizungumza na gazeti hili kwa njia ya simu jana, Rage alisema ameambiwa fedha hizo tayari zimeshatumwa kwa klabu hiyo, hivyo ni jukumu la uongozi kuhakikisha masuala ya kimaendeleo yanapatikana.Alisema dola za Marekani 300,000 (zaidi ya Sh milioni 600 za Tanzania) ambazo Simba imepewa kwa kumuuza Okwi ni nyingi kama zikitumika vizuri na kwamba kama zikitumiwa vibaya si fedha nyingi.Pia Rage amesema Simba imepewa dola za Marekani 19,000 (karibu Sh milioni 40) kama riba kutokana na kuchelewa kupewa fedha karibu miaka mitatu sasa na kushauri viongozi wahakikishe wanazitumia vizuri na si kuelekeza katika malipo ya madeni.“Klabu ina changamoto nyingi za kufanya, sitaki kusema wafanye kitu gani, lakini Simba ina mambo mengi ya maendeleo waelekeze huko, hata kujenga sehemu ambapo wachezaji watakuwa wanaweka kambi yao ” alisema Rage na kuongeza kuwa anashukuru kusikia fedha hizo zimepatikana kwani wapo baadhi ya watu walikuwa wakimshutumu kwamba amekula fedha hizo. “Nilipigania sana hizo fedha wengine wakawa wananishutumu. Naamini sasa kile nilichokuwa nakifanya kimepatikana na nataka kiinufaishe Simba na si kuambiwa zimelipia madeni ya klabu,” alisema.Akizungumzia suala hilo, Ofisa Habari wa Simba, Haji Manara, alisema atalizungumzia wakati wowote kuanzia leo.“Nitaitisha mkutano na waandishi katika siku mbili hizi, nitafafanua mambo mengi,” alisema Manara.Okwi aliuzwa kwa dola za Kimarekani 300,000 Etoile du Sahel ya Tunisia miaka mitatu iliyopita, ambapo Etoile haikulipa fedha hizo Simba na baadaye ikaingia kwenye mgogoro na Okwi, aliyedai hakulipwa mshahara wake kwa miezi mitatu.Okwi akawafungulia Etoile kesi Shirikisho la Soka la Kimataifa (Fifa) na akaomba wakati mgogoro wao unaendelea, aruhusiwe kuchezea timu yoyote kulinda kipaji chake. Hivi sasa Okwi anacheza soka nchini Denmark. | 5michezo
|
HALMASHAURI nchini zimeagizwa kuendelea kukagua mashamba yote yaliyotaifi shwa wakati wa Azimio la Arusha ili yaandaliwe mipango ya matumizi ya ardhi na kupimwa.Aidha, viongozi wa vijiji na kata wametakiwa kuacha tabia ya kuwagawia ardhi kwa mtindo wa kuwakodisha wananchi, kwani kufanya hivyo ni kinyumecha utaratibu na sheria za nchi.Hayo yalibainishwa na Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Angelina Mabula alipokuwa akijibu swali la Mbunge wa Moshi Vijijini (Chadema), Anthony Komu.Katika swali lake, Komu alihoji ni lini serikali itatekeleza ahadi yake ya mara kwa mara ya kuyapima upya mashamba yaliyotaifishwa wakati wa Azimio la Arusha ambayo hivi sasa yamebadilishwa matumizi na kujengwa shule, zahanati, hospitali, makazi. Akijibu swali hilo, Mabula alikiri kuwa kuna mashamba kadhaa nchjini yaliyotaifishwa wakati wa Azimio la Arusha.“Baadhi ya mashamba hayo yaligawiwa kwa mashirika na taasisi za umma kwa ajili ya kuendeleza hususan kwa kilimo cha kahawa na mkonge,”alisema. Hata hivyo, alisema baadhi ya mashamba hayo yamebadilishiwa matumizi na yamekuwa yakitumiwa na wananchi kwa matumizi mbalimbali ya kiuchumi na kijamii ikiwemo makazi, shule, zahanati, hospitali.“Wizara yangu kwa kushirikiana na halmashauri nchini imeendelea kukagua, kuyaandalia mipango ya matumizi ya ardhi na kupima upya baadhi ya mashamba hayo,”alisema.Aidha, Mabula alisema baadhi ya mashamba ambayo Wizara kwa kushirikiana na Halmashauri imeyaandalia mpango wa matumizi ya ardhi ni pamoja na kihuhwi Estate, Sagulas Estate, Lewa Estate, Bombwera Estate, Geiglitz Azimio Kipapula pamoja na Kibaranga yote ya mkoa Tanga.“Mashamba mengine ni New Msowero Farm, Mvumi Farms/Estate Kilosa na Luipa Estate yaliyopo mkoani Morogoro,Kimsingi jukumu la kuandaa mipango ya matumizi ya mashamba hayo ni la Halmashauri husika yalipo mashamba hayo,”alisema.Alitoa rai kwa halmashauri zote nchini kuhakikisha zinatenga bajeti kwa ajili ya kupanga na kupima mashamba husika ili yaweze kutumika kwa tija kulingana na mahitaji halisi ya sasa.Aidha, Mabula alitaka viongozi wa vijiji na kata kuacha tabia ya kuwagawia ardhi kwa mtindo wa kuwakodisha wananchi, kwa kufanya hivyo ni kinyumecha utaratibu na sheria za nchi.Pia alitoa rai kwa wananchi kutumia ardhi yao kwa tija kwani ardhi haiongezeki wakati idadi ya watu, mifugo na shughuli za uzalishaji zinazohitaji ardhi zinazoongezeka.Mabula alikuwa akijibu swali la msingi la Mbunge wa Viti Maalum, Sonia Magogo(CCM) aliyeuliza, Je, Serikali ina mpango gani kuwasaidia wananchi wa Wilaya ya handeni ambao wanakosa ardhi ya kuendesha shughuli zao za kilimo kwa sababu ya kumilikiwa na wachache? | 3kitaifa
|
ZILIKUWA ni mbio zilizotokana na taharuki, kuokoa maisha kwa wabunge, baada ya king'ora cha tahadhari kulia kwenye Ukumbi wa Bunge, kuashiria tukio la hatari na kulazimika kikao cha Bunge kusimama kwa saa moja.Taharuki ya jana ni ya pili kutokea tangu kuanza vikao vya Mkutano wa Bunge la mwezi huu. Siku ya kwanza ya vikao vya Bunge wiki iliyopita, bundi aliingia ndani ya Ukumbi wa Bunge asubuhi na kurejea tena nyakati za usiku, jambo ambalo lilifanya baadhi ya wabunge kuingia hofu.Ilikuwa ni saa 5:02 asubuhi wakati wa kipindi cha maswali na majibu kikiendelea, ambako Naibu Waziri wa Kilimo, Omary Mgumba alikuwa ameanza akijibu swali la Mbunge wa Viti Maalumu, Bernadeta Mushashu (CCM), ghafla king'ora kililia kuashiria hali ya hatari na kusababisha baadhi ya wabunge kupiga kelele na kukimbia kutoka nje.Baadhi ya wabunge walisikika wakipiga kelele wakisema hatari....! Hatari....! Hatari...! huku wakikimbia bila kufuata utaratibu, hali iliyomfanya Mwenyekiti wa Bunge, Najma Giga, kutangaza kuahirisha shughuli za Bunge, bila kusema muda wa Bunge kurejea.Hata hivyo, mbio za wabunge wengi ziliishia eneo la maegesho ya magari na nje ya lango kuu la kuingia ukumbini, badala ya kuelekea kwenye eneo maalumu la kukusanyika wakati wa dharura. Muda mfupi gari la Jeshi la Zimamoto na Uokoaji liliwasili, ambapo askari wakiwa na ngazi waliingia ndani ya jengo la Bunge kuchunguza chanzo cha tukio hilo.Hata hivyo, saa tano na dakika 36 asubuhi, maofisa wa Bunge waliwaomba wabunge kurejea ndani ya ukumbi kuendelea na vikao mara baada ya hali kutulia.Lakini dakika 16 baadaye wabunge wakiwa wamerejea kwenye viti vyao na kabla ya Spika wa Bunge, Job Ndugai kuingia ukumbini, king'ora kililia tena kwa dakika moja, lakini sauti za wabunge zilisikika, zikisisitiza kutotoka huku wengine wakipeana mizaha kuwa hiyo ni majibu ya bundi. Saa 6:04 mchana ikiwa ni saa moja tangu kutokea kwa tukio hilo, Spika Ndugai aliingia ukumbini, akiwataka wabunge kutulia kuendelea na shughuli zilizopangwa kufanyika.“Poleni kwa yaliyotokea, wataalamu wanaendelea kufanya kazi, lakini bado hatuna taarifa kamili ya kubaini hasa kilichotokea.Majibu yakipatikana tutawaletea. Pia maswali ambayo hayakumalizika wakati wa kipindi cha maswali yatapangiwa utaratibu,” amesema Spika Ndugai. | 3kitaifa
|
Kadhalika, serikali imetakiwa kudhibiti matumizi ya dola nchini, hatua ambayo itasaidia kuimarisha thamani ya Shilingi ambayo kushuka kwake kunasababisha bidhaa zinazoingia nchini kupanda bei.Akichangia Bajeti ya Serikali kwa mwaka wa fedha 2025/16, Mbunge wa Mwibara (CCM), Kangi Lugola, alisema kuachwa kwa nchi yetu kuwa kama dampo la bidhaa za nje ambazo zingeweza kuzalishwa hapa nchini ni sababu mojawapo ya thamani ya Shilingi ya Tanzania kuyumba.“Leo hii (jana), Dola moja ya Marekani imefikia Sh 2,075… Hii ni kwa sababu tunasaka sana dola ili kuleta nchini bidhaa ambazo tunaweza kuzizalisha hapa nchini,” alisema akielekeza lawama kwa Wizara ya Viwanda na biashara kwa kushindwa kuhakikisha viwanda vinachanua nchini kama ilivyokuwa miaka ya 1970.Katika kuthibitisha maneno yake, Lugola alikuja na fuko la bidhaa, nyingi zikiwa zimetoka Kenya na China ambazo alizimwaga juu ya meza yake na kuzionesha moja baada ya nyingine.“Hili ni dodoki kutoka China, lingeweza kuzalishwa Tanzania, hii ni pamba ya masikioni, hiki ni kiberiti toka Kenya,” alisema akiendelea kutaja na kuonesha bidhaa zingine kama njiti za kutolea nyama kwenye meno, pipi, rula, penseli na kadhalika.Naye Mbunge wa Igunga, Dk Dalally Kafumu, alisema kupungua kwa thamani ya Shilingi ya Tanzania dhidi ya Dola ya Marekani pia kunachangiwa na matumizi yasiyodhibitiwa vyema ya dola.“Ukienda kwa nchi za wenzetu hawakuruhusu kununua bidhaa kwa dola. Ukitoa dola wanakuambia kachenji pale kwa sababu wanajua kwa kutumia dola holela ni rahisi pia kuzitorosha nje ya nchi yao,” alisema.Dk Kafumu alisema tatizo lingine lililochangia kuanguka kwa thamani ya pesa yetu ni kufungwa kwa migodi miwili ya dhahabu huku kukiwa hakuna mpango wa kuifungua upya au kufungua mingine zaidi.“Migodi miwili imefungwa kwa sababu wakati mwingine tunawasema vibaya wawekezaji,” alisema na kuongeza kwamba kwa tabia hiyo wawekezaji wengi wa madini watatukimbia. | 1uchumi
|
KATIKA kusherehekea sikukuu ya Idd el Hajj, Taasisi ya Fikra ya Kidini ‘Markaz’ imetoa msaada wa ng’ombe 180 na mbuzi 100 kwa vituo mbalimbali vya kulea watoto yatima vya Dar es Salaam. Akikabidhi msaada huo jana, Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Dk Hussein Mwinyi aliwataka waumini wa dini ya Kiislamu nchini kote kusherehekea sikukuu hiyo kwa upendo na amani ili kuenzi matendo mema yaliyoamrishwa katika vitabu vya Mwenyezi Mungu.Alisema sikukuu ya Idd el Hajj, ina maana kubwa kwa Waislamu duniani kote hivyo na kwamba kitendo cha taasisi ya Markaz kutoa msaada huo kwa jamii zisizojiweza kinapaswa kuigwa na waumini wengine waliojaliwa kuwa na uwezo wa kifedha. “Hata Mtume aliwahi kufanya tukio kama hili kwa kuchinja kondoo wake na kuwasaidia majirani na jamaa wengine, nasi kwa upendo huo tunapaswa kumuenzi kwa kutoa msaada wa wanyama kwa wenzetu pale tunapojaaliwa,” alisema Mwinyi.Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Taasisi ya Markaz, Alif Abdulrahman alisema taasisi hiyo imetoa msaada huo ili kuziwezesha jamii hizo kushiriki katika ibada ya kuchinja na hivyo kusherehekea sikukuu hiyo furaha na upendo kama ilivyo kwa watu wengine waliojaliwa kuwa na uwezo. Alisema pia wamefanya hivyo ili kuenzi utamaduni wa vizazi vilivyopita ikiwemo kwa Mtume Muhammad, ambaye aliishi vyema na kusaidiana na jamii yake katika masuala mbalimbali ya kibinadamu. Kwa upande wake, Msaidizi wa Shehe Mkuu wa Tanzania, Mufti Shaaban Zuberi, Shehe Hamid Jongo, mbali na kuipongeza taasisi ya Markaz kwa msaada iliyotoa kwa vituo vya watoto yatima alisema kitendo hicho kinapaswa kuigwa na watu wengine ili kuzipa faraja zinazohitaji misaada | 3kitaifa
|
RAIS wa Rwanda ambaye pia ni Mwenyekiti wa Umoja wa Afrika (AU), Paul Kagame ameendelea kuzisisitiza nchi za Afrika kuangalia uwezekano wa kujikwamua kiuchumi ili ziachane na utegemezi wa nchi za magharibi.Amesema kwa miaka mingi, Afrika imekuwa ikipokea kile kinachoitwa misaada kutoka nchi zilizoendelea, lakini mpaka sasa haijaonekana kuwa na manufaa kwa Waafrika, zaidi ya `kunyonywa’. Kagame aliyasema hayo mwishoni mwa wiki wakati akizungumza na jumuiya ya wafanyabiashara wa Ivory Coast, jijini hapa katika siku ya mwisho ya ziara yake ya kikazi ya siku mbili nchini hapa.“Kwanini Waafrika tuishi kwa kutegemea hisani za wengine? Afrika tuna watu wenye sifa za kuwaongoza wengine kujisimamia. Kwa ujumla, kupitia watu wetu tunaweza kubadilika na kufanya mambo makubwa zaidi. “Kikubwa ni kujiamini na kufuta dhana ya kutegemea kila kitu kutoka nje ya Afrika. Tumejaaliwa kila aina ya rasilimali inayoweza kututoa hapa tulipo, kikubwa ni uthubutu,” alisema Rais Kagame.Aliongeza kuwa, wanawake wasiachwe nyuma katika kushirikishwa kujikomboa kiuchumi, kwani wana nguvu kubwa huku akitolea mfano wa nchi yake ambayo asilimia 52 ya raia wake ni wanawake. Alitumia nafasi hiyo kuwakaribisha wafanyabiashara wa Ivory Coast kuwekeza nchini Rwanda, akisema hawatajuta, kwani ina soko kubwa hasa ikizingatiwa Rwanda ni nchi ya Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) yenye soko la watu kati ya milioni 150 na 170.“Tuna nguvu kubwa ya soko. Hilo linatupa nguvu na inabidi tuunganishe zaidi na kushirikishana kwa mambo mengi kabla ya kukimbilia nje ya Afrika,” alisema Kagame na kusisitiza kuwa, wapo mstari wa mbele katika vita dhidi ya rushwa, hivyo wawe na amani ya kutokumbana na urasimu wakiamua kuwekeza Rwanda. Katika ziara hiyo, Rais Kagame aliongozana na mkewe, Jeannette Kagame na maofisa waandamizi serikalini na walipokelewa na mwenyeji wao, Rais Alassane Ouattara na mkewe, Dominique Ouattara. | 3kitaifa
|
Aliyekuwa msemaji wa Klabu ya Yanga, Jerry Muro amesema yeye aliachia kijiti kwa kina Antonio Nugaz lakini mwenzake Haji Manara bado kakomalia sijui ndio msukule wa Simba. Amesema ni vizuri kupokezana vijiti ama awaaachie wengine kama vipi arudi akafundishe madrasa. “Mimi niliachia kijiti kwa kina Antoni Nugaz, lakini upande wa @SimbaSCTTanzania mwenzangu kakomalia hapo sijui yeye ndio msukule wa Simba alaaniwe amtegemeaye mwsnadamu yeye kila muda Moooo… Mooooo,” amesema Jerry Muro ambaye ni mkuu wa Wilaya ya Arumeru ameyasema hayo leo ambapo amesema amerudi tena Yanga washirikiane na kwamba kesho wanatarajia ushindi. “Nimekuja tena Yanga sikuitwa ila karaha na fedheha zimezidi nikaona nije tena tushirikiane,” amesema. Aliongezea kuwa:” Viongozi wote wa Yanga wenye hela rudini tuishi kama tulivyokuwa tunaishi zamani na mnajua, mwenye gari alete, aliyekuwa anamwaga upupu amwage na aliyekuwa anatoa hela atoe,” amesema Jerry. 'Mimi niliachia kijiti kwa kina Antonio Nugaz, lakini upande wa @SimbaSCTanzania mwenzangu kakomalia hapo hapo sijui yeye ndio msukule wa Simba' – Jerry Muro#YangaPress pic.twitter.com/PdUFxQYTBI — East Africa TV (@eastafricatv) February 25, 2020 'Nimekuja tena Yanga sikuitwa ila karaha na fedheha zimezidi nikaona nije tena tushirikiane' – Jerry Muro#YangaPress pic.twitter.com/tByv6YWl9F — East Africa TV (@eastafricatv) February 25, 2020 'Viongozi wote wa Yanga wenye hela rudini tuishi kama tulivyokuwa tunaishi zamani na mnajua, mwenye gari alete, aliyekuwa anamwaga upupu amwage, aliyekuwa anatoa hela atoe' Jerry Muro#YangaPress pic.twitter.com/zjwObnGBpH — East Africa TV (@eastafricatv) February 25, 2020 | 5michezo
|
WAKATI leo Mkurugenzi Mkuu mpya wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru), Diwani Athuman anatarajiwa kuzungumza na vyombo vya habari kuhusu mikakati yake ya uendeshaji wa taasisi hiyo nyeti, maaskofu na mashehe wameshauri Sheria ya Kudhibiti na Kupambana na Rushwa ifumuliwe. Ushauri huo wa maaskofu na mashehe ulitolewa Dar es Salaam jana kupitia kwa Mwenyekiti wa Kamati ya Kitaifa ya Maaskofu na Mashehe ya Maadili, Amani na Haki za Binadamu kwa Jamii ya Madhehebu ya Dini nchini, Askofu William Mwamalanga.Mwamalanga ambaye ni Askofu wa Kanisa la Kiinjili la Kipentekoste nchini alitoa ushauri huo, Dar es Salaam jana wakati akifungua Kongamano la Amani kwa Vijana 3,000 kutoka madhehebu mbalimbali ya dini nchini. Amemuomba Rais Joh Magufuli kuagiza kufanyiwa marekebisho kwa sheria hiyo aliyosema inamzuia Mwanasheria wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) kumfikisha mtuhumiwa wa rushwa mahakamani hadi jalada lake litakapofikishwa kwanza kwa Mwendesha Mashitaka (DPP).Askofu Mwamalanga ameuita mfumo huo kuwa ni wa kikoloni na kuwa kwa kiwango kikubwa umekwamisha harakati za mapambano dhidi ya vitendo vya rushwa nchini na pia umesaidia kuwalinda wala rushwa vigogo kutokana na uwezo wao kifedha na baadala yake kushughulika na wala rushwa wadogo. “Huu ni mfumo ambao mimi kama kiongozi wa dini ambaye nina wajibu wa kuisaidia serikali katika mapambano dhidi ya vitendo vya rushwa nashauri kwa Rais Magufuli kuwa ni vema kama utabadilishwa maana vinginevyo mabosi wa pale Takukuru wataendelea kushindwa kufanya mabadiliko ya kimfumo.“Katika sheria ya kupambana na rushwa, ni kosa moja tu kati ya makosa 24 ya rushwa ndilo ambalo Mwanasheria wa Takukuru anaweza kumpeleka mtuhumiwa moja kwa moja mahakamani, katika kifungu kidogo cha 15 cha sheria hiyo, lakini makosa mengine yote sheria inasema ni lazima yapelekwe kwa DPP,” alisema Askofu Mwamalanga. Alisema mfumo huo umekuwa unaleta ukakasi kwa mabosi wa Takukuru kushughulika na magwiji wa rushwa nchini kwani wakati mwingine DPP anaweza kukwamisha kasi ya ushughulikiaji wa kesi hizo zilizopelekwa kwake kutoka Takukuru.“Jitihada za kupambana na rushwa haziwezi kufanikiwa chini ya mfumo huu ni lazima jitihada za makusudi zifanywe ili kuipa meno yote Takukuru ili iwe na uwezo wa kuwafikisha moja kwa moja watuhumiwa wote wa rushwa na hasa vigogo mahakamani,” alisema Askofu Mwamalanga. Alisema kama hilo litafanyiwa kazi, Tanzania itaungana na nchi nyingine za Afrika ambazo ziliamua kufuta sheria zilizokuwepo za kikoloni katika kukabiliana na vitendo vya rushwa katika nchi zao na kupata mafanikio makubwa.“Rushwa ni adui mkubwa wa haki, amani na ustawi wa taifa letu, ndiyo maana katika nchi nyingi za Asia, Ulaya na Marekani, hawana mzaha kabisa na suala la rushwa na mtu yoyote bila kujali wadhifa wao wanaadhibiwa vikali. Diwani Athuman kuunguruma leo Katika hatua nyingine, Mkurugenzi Mkuu mpya wa Takukuru, Diwani Athuman leo atanguruma na kuelezea mikakati yake ya kuendesha taasisi hiyo baada ya kuapishwa juzi na Rais Magufuli kushika wadhifa huo. Msemaji wa Takukuru, Mussa Misalaba alilieleza gazeti hili jana juu ya kuwepo kwa mkutano baina ya bosi huyo mpya wa Takukuru na vyombo vya habari.Diwani amechukua nafasi ya Valentino Mlowola ambaye ameondolewa katika nafasi hiyo na kuteuliwa kuwa balozi. Rais Magufuli alieleza kuwa moja ya sababu za kumuondoa Mlowola kwenye nafasi hiyo ni kutokana na kutoridhishwa na namna alivyoshughulikia migogoro ya ufisadi katika mauzo ya Hoteli ya Musoma na Shamba la Mifugo la Utegi, vyote vikiwa mkoani Mara. Aliyasema hayo wakati akizungumza na wakazi wa mji wa Tarime mkoani Mara, Septemba 7, mwaka huu. Juzi wakati akimuapisha, Rais Magufuli alimtaka Mkurugenzi Mkuu huyo wa Takukuru kuisafisha taasisi hiyo ikiwa ni pamoja na kuwaondoa kazini watendaji wanaojihusisha na vitendo vya rushwa. | 3kitaifa
|
Akitoa maelezo hayo juzi jioni bungeni, mbunge huyo alisema ametumia Kanuni ya 28 (8) ya Kanuni za Bunge za Kudumu.Alisema mashine hizo zimekuwa kero kwa wafanyabiashara na bei ni kubwa, ikilinganishwa na gharama halisi na pia bado matumizi yao hayajaeleweka kwa watumiaji wengi.“Naomba Serikali isitishe uuzaji wa mashine hizo bei ni kubwa sana, itoe elimu ya kutosha kuhusu matumizi, lakini pia ipitie upya sheria zote za kodi ili kufanya marekebisho katika sheria zitakazoonekana zina upungufu,” alisema Zambi.Alisema maelezo yake hayo, msingi wake ni malalamiko ya bei kubwa za mashine hizo, ambapo awali ziliuzwa Sh milioni mbili kwa wafanyabiashara ambao mzunguko wa biashara zao unafika Sh milioni 14 kwa mwaka.Hata hivyo, wafanyabiashara walikuwa wakilalamika kuwa bei hiyo ni kubwa sana na Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), ikapunguza bei hadi Sh 800,000.Msingi wa malalamiko ni kuwa mashine hizo huko zitokako bei yao huanzia kati ya dola 60 hadi 150 sawa na Sh 75,000 hadi Sh 300,000.Alihoji uhalali wa mashine hizo kuuzwa kati ya Sh 800,000 na Sh milioni 1.5 kwani ni sawa na kuibia Watanzania.“Baada ya kupokea malalamiko ya wafanyabiashara wakiwamo wa Mbeya, nilisafiri hadi Dubai na China ambako nilikuta zinauzwa dola 60 hadi 150 kutegemeana na aina ya mashine,” alisema Zambi. | 1uchumi
|
ULIPOBADILI mwelekeo kutoka ‘Kemo’ ya kiugumu enzi zile ulipokuwa unaishi Mji Kasoro Bahari a.k.a Morogoro na kuamua kujikita kwenye Zouk la malavidavi, mashabiki walikupokea vyema na bado wako nawe uliposukuma damu zao kwa mikong’osio yako ya ‘Moyo Sukuma Damu’ badala ya mengine. Lakini kwa sasa katika ‘Front’ yako ambayo ni kama umeiwahisha kwa haraka kabla moyo haujamaliza kusukuma damu, unajipa matumaini na kuhanikiza mabadiliko kwamba ‘Atabadilika’ ingawa wewe mwenyewe unahitaji kubadikika kwanza kwenye mtiririko wa ‘Back’ uliyotoka. Siyo kwenye Kemo lakini hii ya sasa kwenye malavidavi maana ukisikiliza maudhui yako na mikong’osio yako ni kama unajaribu kudhihirisha uwezo kwa kupita njia mbadala ya kimo cha sauti na uimbaji wako. Lakini kwa mweledi anakutambua kwamba bado hujabadilika kuweza kushawishi mashabiki wako, ni kama badala ya kula chungwa umeamua kula chenza ambalo ni tunda jamii mkabala na la awali. Hiyo ni sawa na maharage yalivyo na undugu na kunde au mbaazi yaani ni mlemle. Hata ukiangalia maudhui yako kwenye kichupa chako kipya cha ‘Kubadilika’ wewe mwenyewe hujabadilika kutoka ‘Back’ yako ya kusukuma damu hadi sasa, kile kichupa cha kwanza kilizimikiwa kutokana na jinsi ulivyokiibua manake eneo moja mabadiliko tu ya engo ya kamera lakini mnyange mtamu alikinogesha pia yale mambo ya hospitali. Lakini Ditto hiyo haimaanishi kuwa kila kichupa chako unachokiandaa kiwe katika maudhui yaleyale kwa muktadha wa mandhari ingawa sipingani kabisa na uwezo wako ninaamini una uwezo mkubwa wa kukonga kuliko tunaouona sasa ila tu labda ni masuala ya usimamizi. Kwamba ni namna gani unaandaliwa kuwasilisha lakini pia usisukumwe na mahitaji ya mbinyo kwamba toa kitu kingine kabla ya muda ili mashabiki wakukubali manake hiyo huwagharimu wasanii wengi, kwani mara nyingi unapotafuta ‘kutoka’ ngoma ya awali unaiwekea nguvu kubwa lakini ukifanikiwa inakupa kujiamini kupitiliza, kisha utahisi ya pili utaigonga na kupagawisha kama ya kwanza lakini usipokuwa mwangalifu mambo huwa tofauti, wewe siyo wa kwanza kukutana na hali kama hiyo katika muziki. Cheki mwenyewe hata hapa Bongo msanii anaibuka poa katika ‘Back’ kisha anatokota katika ‘Front’ manake anakuwa amejipa makonfidensi kupitiliza, kumbe umakini ndiyo unatakiwa ingawa kwako bado ndiyo kwanza umeanza kutudhihirishia mauwezo yako kwenye kutiririsha mavoko yanayogusa mtima. Kwahiyo hadi sasa iko poa japo pia haijafikia levo ya uwezo uliojificha ndani yako, fungukia mistari tukosome poa kisha utajikita mahala ambapo hakuna atakayekugusa kwani hata mikong’osio unayokita wasanii wengi ni kama wameitosa kwenye Bongo Fleva labda pengine iliwashinda au ‘walihit’ kwenye ‘Back’ wakaishiwa maarifa kwenye ‘Front’ ikawa mgando kama maziwa mbadala ya mtindi. Kwa hiyo? Weka mambo tuone uwezo wako tukisubiri ‘Front’ nyingine manake inaelekea unawakonga Wabongo kwa voko yako iliyonyooka kwa kimo cha kupanda na kushuka, pengine itawavuta wengine nao wajikite kwenye Zouk za malavidavi ya malalamiko ya kuhanikizwa migubiko ya zero distance. | 0burudani
|
NA MWALI IBRAHIM, DAR ES SALAAM HALI ya aliyekuwa Mwenyekiti wa klabu ya Simba, Ismail Aden Rage, imezidi kuimarika ambapo kwa sasa amelazwa katika Hospitali ya Aga Khan, Dar es Salaam. Rage alipata ajali juzi mkoani Dodoma, akiwa pamoja na majeruhi wenzake wanne walilazwa katika hospitali ya mkoa huo kabla ya kuhamishiwa Aga Khan. Akizungumza Dar es Salaam jana akiwa hospitalini hapo, Rage alisema anaendelea vizuri ambapo kwa mujibu wa daktari alisema itamchukua wiki tatu kupona kabisa bega lake. “Nashukuru naendelea vizuri na naendelea kupata huduma, daktari ameniambia baada ya wiki tatu nitakuwa nimepona kabisa hivyo naendelea na matibabu,” alisema. Akizungumzia ajali hiyo, Rage alisema dereva wa gari lao alikuwa anataka kulipita lori lakini ghafla dereva wa lori hilo akaingia katikati ya barabara. “Hata hivyo, tunamshukuru sana dereva wetu kwa kuwa alipoona hivyo, badala ya kuligonga lori aliamua kwenda pembeni ndipo gari letu liliporuka na kuingia kwenye korongo likapinduka,” alisema. Rage aliteguka bega la kushoto huku Munde akipata majeraha kichwani, usoni na kuvunjika mkono, majeruhi wengine wanaendelea na vipimo. Hata hivyo, Mwenyekiti wa Bunge Maalumu la Katiba, Samuel Sitta, kabla ya kuanza kwa vikao cha Bunge hilo alitoa taarifa kuhusiana na wabunge hao kupata ajali. “Kutokana na wenzetu kupata ajali uongozi wa Bunge hili, umeamua kuwasafirisha wajumbe hao kwenda Dar es Salaam kwa ajili ya uchunguzi zaidi,” alisema. Rage na Munde walikuwa wamelazwa katika wodi namba 18 Grade one, chumba namba moja na mbili wakiwa na majeraha mbalimbali mwilini. Kwa upande wake Mganga Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Ezekiel Mpuya alisema vipimo vilionyesha Munde pamoja na kupata majeraha usoni na kichwani pia alivunjika mkono wakati Rage ameteguka bega la kushoto. Alisema hadi jana hali zao zilikuwa zinaendelea vizuri na wangeruhusiwa. | 5michezo
|
Na SHERMARX NGAHEMERA, SHERIA ya Madini ya mwaka 2010 imefanyiwa mabadiliko makubwa, hivyo kuanzia sasa mambo ya utoaji wa Leseni za Madini umesimamishwa hadi itakapoundwa Tume au Kamisheni ya Madini kama sheria inavyotaka. Sheria ya Madini imefanyiwa mabadiliko makubwa na mabadiliko ya Sheria 2017 (Sheria Iliyoandikishwa na Mengineyo ya Mwaka 2017 ( Written Law Miscellaneous Ammenfments 2017), iliyopitishwa na kikao cha Bajeti na imesheheni makatazo ya mambo mengi ili kubana utoroshaji wa mapato ya Serikali. Sheria hiyo imefuta Wakala wa Madini iliyojulikana kama Tanzania Minerals Audit Agency (TMAA) na ofisi nane za kushughulikia madini nchini. Kwa maelezo ya Profesa James Mdoe, Katibu Mkuu Wizara ya Nishati na Madini, amewaambia waandishi wa habari kuwa wale wanaotaka kupeleka madini nje wanatakiwa kulipa ‘Clearing Fee’ ya kiwango cha asilimia moja ya thamani ya madini hayo, ambayo yamefanyiwa ukaguzi na kuthaminishwa na Ofisi ya Kamishina wa Madini kwa muda huo wa mpito hadi Kamisheni ya Madini itakapoanza kazi rasmi baada ya kuundwa. Aliainisha kuwa, hayo ni pamoja na majukumu yote ya kazi iliyokuwa inafanywa na TMAA kwa muda itafanywa na ofisi hiyo, ikiwamo makusanyo ya mrabaha kwa madini ya ujenzi na ya viwanda, uthibitishaji wa vocha za malipo na usalama wa madini migodini. Majukumu mengine yaliyoathirika ni usimamizi wa migodi kwa kupitia mahitaji ya wazalishaji wote wa madini na miradi yao, ukaguzi katika sehemu za kutokea na kusafirisha mizigo, ikiwamo viwanja vya ndege na mipaka ya nchi pamoja na bandari kuzuia upoteaji madini kwenda nje. Profesa Mdoe alisema kuwa, mrabaha kuhusu madini mbalimbali umeongezeka, ambapo madini ya metali kama dhahabu, shaba na fedha yameongezeka kutoka kiwango cha awali cha asilimia 4 hadi asilimia 6. Wakati huohuo madini ya vito na ya thamani kama almasi, yakuti, ganeti na tanzanite yameongezeka mrabaha kuwa wa asilimia 6 kutoka za awali asilimia 5. Wachimbaji wadogo kulipa kodi Alisema sheria mpya inataka kila mtu au taasisi katika mnyororo wa thamani atailipa serikali kwa mapato na huduma mbalimbali ambapo tozo ya asilimia 5 kwa mara ya kwanza itakusanywa na madalali na wafanyabiashara wakubwa (dealers) kutoka kwa wachimbaji wadogo wadogo kama kodi ya makusanyo (withholding tax) na kuwasilishwa kwa Mamlaka ya Kodi Tanzania (TRA) Amewataka wadau wote kushirikiana na wafanyakazi waliopo, kwani wanafanya majukumu yao kama ilivyoainishwa na Wizara na katika misingi ya sheria kwa mafanikio makubwa kukusanya maduhuli yote ya serikali katika wakati huu wa mpito. Aliwahakikishia wafanyakazi ambao hawakuhusika na mtafaruku wa biashara ya madini kuwa wataendelea na kazi kama kawaida na kupata stahiki zao za malipo kwa mpangilio mpya hadi hapo mabadiliko yatakapofanyika kikamilifu kwa sheria mpya. Wafanyakazi hao wameambiwa wataendelea kutoa mwendelezo wa leseni za wachimbaji wadogo wadogo, kwa vile maofisa wote wa TMAA na wale wa ofisi za kanda wako chini ya kanda, wakati utambulisho na vifaa vya kazi vyote vitatolewa na Kamishina wa Madini, vikiwamo mihuri, lakiri na risiti, vikionesha ofisi hiyo ya Kamishina wa Madini. Mabadiliko haya ni matokeo ya ripoti mbili zilizoanzishwa na Rais John Magufuli kuchunguza kuhusu mwenendo wa biashara ya madini na makinikia, ambayo ilifichua uozo na wizi wa kutisha na udanganyifu uliokithiri wa rasilimali za taifa za madini zenye thamani ya mamia ya shilingi trilioni na hivyo Bunge kubadilisha sheria mbalimbali zilizoleta mabadiliko makubwa ambayo yamelenga uboreshaji huduma na ukusanyaji mapato ya taifa. Matokeo yake kwa undani ni kupata sheria tatu ambazo zina mtazamo wa kuboresha Uchumi wa nchi, zikiwamo (Written Laws Miscellaneous Act , 2017, Natural Wealth and Resources (Permanent Sovereignty) Act 2017 na Natural Wealth and Contracts Review and Renegotiation of Unconscionable Terms Act 2017. Sheria hizo wanadai wengi ni sawa na tangazo la vita kwa ubeberu, mtazamo ambao Rais Magufuli ameuona na Waziri wake wa Katiba na Sheria, Profesa Palamagamba Kabudi kuukubali. | 3kitaifa
|
TUME ya Vyuo Vikuu Tanzania (TCU) imevifutia hati za usajili vyuo vikuu vitatu, vyuo vikuu vishiriki vitatu sambamba na vituo vya vyuo vikuu vitatu, vikiwamo Chuo Kikuu cha Kimataifa cha Tiba na Teknolojia (IMTU) na Chuo Kikuu cha Bagamoyo (UoB).Aidha, TCU imevipiga marufuku vyuo hivyo kutumia majina hayo au yanayoelekea kufanana na majina ya awali, endapo vitasajiliwa katika mamlaka nyingine za elimu nchini, kwani kufanya hivyo ni kupotosha umma.Katibu Mtendaji wa TCU, Profesa Charles Kihampa alisema: “Vyuo hivyo vikiamua kujisajili katika mamlaka nyingine, visitumie majina yaleyale, yanayofanana na ya awali, au yanayokaribia kufanana kwani kufanya hivyo ni kupotosha umma na kukiuka sheria”.Profesa Kihampa alisema jana kuwa tume hiyo, inaendelea kusitisha udahili wa wanafunzi wapya kwa ngazi zote za masomo katika programu zote kwa Chuo Kikuu cha Kumbukumbu ya Sebastian Kolowa (SEKOMU) cha Lushoto, Tanga.Aidha, alisema TCU imerejesha udahili wa wanafunzi wapya kwa Chuo Kikuu Kishiriki cha Afya na Sayansi Shirikishi cha Mt. Fransisco (SFUICHAS), baada ya kuridhishwa na marekebisho katika upungufu wa ubora, uliokuwa umebainishwa awali na hivyo kukidhi vigezo vya ubora kwa mujibu wa miongozo iliyopo.Vyuo vikuu vilivyofutiwa usajiliProfesa Kihampa alisema licha ya awali, vyuo vikuu hivyo na chuo kikuu kishiriki vilivyofutiwa hati za usajili, kupewa ushauri na mafunzo ya namna mbalimbali za kuboresha mazingira ya kujifunzia na kufundishia, pamoja na kutoa muda wa kufanya maboresho katika maeneo mbalimbali yaliyobnainishwa kwa miaka mitatu, havikufanya kama vilivyotakiwa.“Kwa kuzingatia muda uliotolewa na hali ya vyuo husika ikiwa ni pamoja na changamoto ya uhaba wa rasilimali watu na fedha, tume imeridhika kuwa baadhi ya vyuo havina uwezo wa kujiendesha hata vikipewa muda zaidi,”amesema.Alisemna kwa msingi huo, tume katika vikao vyake vya 89, 91, 92 na 97 vilivyofanyika kati ya Agosti 2019 na Januari 2020, imefuta hati za usajili katika Chuo Kikuu Kishiriki cha Josiah Kibira (JOKUCo) cha Bukoba, Kagera, Chuo Kikuu cha Mlima Meru (MMU) Mkoani Arusha, Chuo Kikuu cha Kimataifa cha Tiba na Teknolojia (IMTU) na Chuo Kikuu cha Bagamoyo (UoB), vyote vya Dar es Salaam. Katibu Mtendaji huyo wa TCU alisema tume imeridhia maombi ya wamiliki wa vyuo vikuu vishiriki viwili na vituo vitatu vya vyuo vikuu, kuhusu kusitisha utoaji wa mafunzo.“Tume katika kikao chake cha 97 kilichofanyika tarehe 20, Januari, 2020, imeridhia maombi ya wamiliki hao ya kusitisha utoaji wa mafunzo, hivyo tume imefuta hati za usajili za vyuo vikuu vishiriki na kufuta vibali vilivyoanzisha vituo vitatu vya vyuo vikuu,” alisema.Alitaja kuwa ni Chuo Kikuu cha Askofu Mkuu Yakobo (AJUCo) cha Songea, Ruvuma, Chuo Kikuu Kishiriki cha Kumbukumbu ya Kardinali Rugambwa (CARUMUCo) cha Kagera na Chuo Kikuu cha Teofilo Kisanji Kituo cha Dar es Salaam (TEKU Dar es Salaam Center).Pia Chuo Kikuu cha Mt. Yohana cha Tanzania Kituo cha Mt. Marko (SJUT St. Mark’s Center) na Chuo Kikuu cha Jomo Kenyatta cha Kilimo na Teknolojia (JKUAT) Kituo cha Arusha Kwa mujibu wa Katibu Mtendaji huyo wa TCU, tume inaendelea kusitisha udahili wa wanafunzi wapya na kutoa muda zaidi wa kutekeleza maelekezo ya tume kwa Chuo Kikuu cha Kumbukumbu ya Sebastin Kolowa (SEKOMU).“Chuo hiki kimemepewa muda wa miezi sita kukamilisha utekelezaji wa maelekezo ya tume. Wakati huo chuo hiki hakiruhusiwi kudahili wanafunzi wapya kwenye programu zote’’ alisema. Profesa Kihampa alisema kwa Chuo Kikuu Kishiriki cha Afya na Sayansi Shirikishi cha Mt. Fransisko (SFUCHAS), tume imerejesha udahili wa wanafunzi wapya katika chuo hicho.“Tume katika kikao chake cha Januari 20, 2020 imeruhusu chuo hicho kuanza kudahili wanafunzi wapya kunzia mwaka wa masomo 2020/ 2021,” alisema.Kati ya Oktoba 2016 na Januari 2017, TCU ilifanya ukaguzi maalumu kwa taasisi 64 za vyuo vikuu, vyuo vikuu vishiriki na vituo vya vyuo vikuu.Matokeo ya ukaguzi huo, yalibainisha kuwapo kwa kasoro mbalimbali katika uendeshaji wa vyuo vikuu nchini. Vyuo 45 vilikutwa na kasoro ndogo na kupewa ushauri, kisha vikarekebisha katika kipindi kifupi na kuendelea kutoa elimu.Hata hivyo, vyuo 19 vilivyokutwa na kasoro kubwa, vilipewa ushauri na muda wa marekebisho.Hata hivyo, vilishindwa kurekebisha katika kipindi kifupi, hivyo kuzuiwa kudahili wanafunzi wapya kuanzia mwaka wa masomo 2017/ 2018.Hadi Oktoba 2019, vyuo vikuu vinane kati ya 19 vilivyositishwa udahili, vilifanya marekebisho makubwa na hivyo kuruhusiwa kudahili na kuendelea kutoa mafunzo kwa baadhi ya programu za masomo. | 3kitaifa
|
['Mshambuliaji wa PSG Neymar jnr hataichezea timu hiyo katika mechi ya ufunguzi dhidi ya Nimes katika ligi ya daraja la kwanza nchini Ufaransa, huku mabingwa hao wa Ufaransa wakidai kwamba mchezaji huyo huenda akaihama klabu hiyo. ', 'Mkurugenzi wa michezo wa klabu ya PSG Leonardo amesema kuwa mazungumzo ya uhamisho wa mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 27 yamepiga hatua kubwa zaidi ya ilivyokuwa hapo awali. ', 'Hatahivyo klabu hiyo haijatoa ruhusa yoyote ya uhamisho, alisema. ', 'Mchezaji huyo ambye ndiye ghali zaidi duniani amehusishwa na uhamisho katika timu yake ya zamani ya Barcelona mbali na uhamisho mwengine wa Real Madrid. ', 'Neymar alijiunga na PSG 2017 wakati klabu hiyo , iliokuwa ikimilikiwa na kampuni ya uwekezaji ya michezo nchini Qatar ilimlipa Neymar kitita cha £200m ili kumwezesha kujiondoa katika kifungu cha sheria cha kandarasi yake. ', 'Mshambuliaji huyo amefunga magoli 34 katika misimu miwili akiwachezea mabingwa hao wa Ufaransa, ijapokuwa majeraha yameathiri vibaya kampeni yake.', 'Mkufunzi wa PSG Thomas Tuchel alisema kwamba Neymar alishiriki katika mazoezi siku ya Jumamosi lakini bapo alikuwa hajapona vizuri'] | 5michezo
|
Tunu Nassor – Dar es Salaam SERIKALI imesema itaendelea kushirikiana na sekta binafsi kutatua
tatizo la ajira nchini ambalo linazidi kuongezeka. Akizungumza juzi katika shindano la wajasiriamali wanavyuo la Global
Student Entrepreneur Award (GSEA), Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu,
Sera, Bunge, Kazi, Ajira na Walemavu, Anthony Mavunde alisema wanafarijika
kuona kuna taasisi zimeanza kulifanyia kazi tatizo hilo. Alisema takwimu zinaonesha kuwa tatizo bado ni kubwa hivyo njia pekee
ya kupunguza tatizo hilo ni kushirikiana na sekta binafsi katika kuwajengea uwezo
vijana kuzalisha ajira. “Tumefarijika kuona taasisi zinajitokeza kuwasaidia kuwajengea uwezo
vijana kuweza kujiajiri na kutoa ajira kwa wengine hivyo kama serikali
tutashirikiana nao kuhakikisha wanatimiza lengo hilo,” alisema Mavunde. Alisema nchi inatakiwa kuwawezesha vijana wake kwa kuwajengea
miundombinu wezeshi waweze kujiajiri. “Tutaendelea kuwasaidia vijana kupata mitaji itakayowawezesha
kuanzisha biashara zao waweze kuwasaidia wengine wasio na ajira,” alisema
Mavunde. Aliongeza kuwa wanaendelea kushughulikia changamoto zinazowakabili
vijana zikiwamo kutokuaminiwa na taasisi za fedha na kukosa mitaji. Kwa upande wake, Msimamizi wa GSEA nchini, Baraka Mtunga alisema
mashindano hayo yameshirikisha wanafunzi 27 waliopo katika vyuo nane. Alisema moja ya kigezo cha kuwa mwanachuo mjasiriamali bora ni kuwa
na uwezo wa kuzalisha si chini ya Sh milioni moja kwa kipindi cha mwaka mmoja. “Mshindi wa shindano hili amepata sh milioni moja na kupata msaada wa
kibiashara chini ya taasisi ya Enterprenuers’ organization na kufanikiwa
kushiriki katika mashindano ya Dunia
nchini Marekani,” alisema Mtunga. Naye mshindi wa shindano hilo Mosses Katala alisema changamoto kubwa
zinazosababisha wanavyuo kushindwa
kuanzisha biashara zao ni kukosa mitaji. “Binafsi kwa kushirikiana na wenzangu ilibidi kuomba msaada wa kupata
mtaji kutoka nje ya nchi ndipo tulipoanzisha utengeneaji wa chakula cha mifugo
kupitia funza,” alisema Mosses. | 3kitaifa
|
SERIKALI imesema imejipanga kuongeza ushirikiano na sekta binafsi katika kuhakikisha kuwa kero na vikwazo vinaondolewa ili kuweka mazingira bora ya biashara na kuvutia uwekezaji wa ndani na nje ya nchi.Waziri wa Kilimo, Japhet Hasunga aliyasema hayo jana wakati akimwakilisha Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa kufungua Mkutano Mkuu wa Mwaka wa Dharura wa Chama cha Wafanyabiashara Wenye Viwanda na Kilimo Tanzania (TCCIA) mwaka huu.Aidha alisema serikali imefanya uamuzi mahususi mwaka huu wa kuondoa mwingiliano wa utoaji wa huduma za mashirika ya TBS na TFDA ili kupunguza usumbufu kwa wafanyabiashara.Alisema hizo ni hatua za awali na alitoa mwito kwa TCCIA kuhakikisha wafanyabiashara wanafuata sheria, kanuni na taratibu zote zilizowekwa ili kuondoa usumbufu wote unaoweza kujitokeza wakati wa kufanya biashara.Alisema Rais John Magufuli alizindua Mpango wa Pili wa Maendeleo ya Kilimo (ASDP II), Juni 4, mwaka jana, kwa kutambua umuhimu wa sekta binafsi, moja ya maboresho makubwa ya ASDP II ukilinganisha na ASDP I ni kuipa nafasi kubwa zaidi sekta binafsi.Aliongeza kuwa ni wakati muafaka wa kubaini maeneo maalumu ambayo TCCIA itaendelea kutoa mchango mkubwa katika kutekeleza programu hiyo ili iweze kufikia malengo yaliyowekwa.Hasunga alisema ili kuhakikisha uboreshaji wa mazingira ya biashara nchini, serikali kwa kushirikiana na sekta binafsi iliandaa andiko maalumu, Mpango wa Kuboresha Biashara na Mazingira ya Uwekezaji Tanzania (Blue Print) ambalo lilikwishazinduliwa, pia mpango wa utekelezaji wake umeandaliwa na umeanza kutekelezwa.“Ni wajibu sasa wa kila pande yaani sekta ya umma na binafsi kuhakikisha kuwa yale yote yaliyoainishwa katika andiko hilo yanatekelezwa ipasavyo,” alisema Hasunga.Vile vile, alisema serikali imeendelea na jitihada za kuimarisha mabaraza ya biashara ya mikoa na wilaya ambapo tayari imeshaweka mwongozo wa mabaraza hayo ambayo TCCIA ni Sekretarieti.Aliwataka washiriki hao kuchangamkia fursa zilizopo katika miradi mikubwa inayotekelezwa na serikali nchini hasa miundombinu ya reli ya kisasa, mradi wa umeme wa bwawa la Julius Nyerere, barabara za kisasa, bomba la mafuta, manunuzi ya ndege na mingineyo.Alisema fursa hizo kwa kupitia sera ya uwezeshaji wazawa nao wakiwa wana nafasi kubwa ya kunufaika nazo.Alisema miradi hiyo ni mingi na itachukua muda mrefu ikitekelezwa kwa awamu tofauti.“Endapo kwa sababu moja au nyingine haukuweza kupata fursa ya kushiriki kazi kwenye mradi mmoja kwa sababu fulani zikiwemo sifa kadhaa basi, nakushauri ujipange vizuri kwenye miradi inayokuja, msikate tama,” alisisitiza Hasunga.Alisema serikali inatambua ushirikiano mzuri wa TCCIA na taasisi mbali mbali za Umoja wa Mataifa (UN) zikiwemo UNDP, Unido, Fao, UNV, Unesco, ILO na ITC pamoja na wadau wengine wa maendeleo. | 1uchumi
|
NAIBU Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia, Dk Avemaria Semakafu ameupa siku moja uongozi wa Chuo cha Ualimu Dakawa kufanya uhakiki ili kupata gharama za ukarabati wa bwalo la chakula.Hatua hiyo imefikiwa baada ya miundombinu katika chuo hicho kuharibiwa na mvua pamoja na upepo, ambapo paa la jengo hilo liliezuliwa. Dk Semakafu alisema serikali inakijenga upya chuo hicho na kuagiza kuwa kazi ya kwanza katika ujenzi huo mpya itakuwa ni kujenga bwalo na jiko. Miundombinu mingine iliyoharibiwa ni eneo la kuegesha magari, mgahawa na mifumo ya umeme.Katika hatua nyingine, aliagiza uongozi na wanafunzi kusimamia utunzaji wa mazingira katika chuo hicho ikiwa ni sehemu ya mafunzo katika kuwandaaa walimu. Makamu Mkuu wa chuo, Naileji Jacob aliishukuru wizara kwa kuchukua hatua haraka baada ya tukio hilo lililosababisha uharibifu mkubwa juzi. Aliahidi kutekeleza maagizo hayo kwa wakati.Katika hatua nyingine, akikagua maeneo ya chuo, Dk Semakafu aliagiza uongozi wa chuo kusimamia kuondolewa jengo la mtu binafsi lililojengwa ndani ya mpaka wa chuo.“Nakuagiza Makamu Mkuu wa chuo waliojenga mahali hapa wafike ofisini kwako wakiwa na mikataba yao na uiwakilishe wizarani, lakini kwa sasa hata baada ya uharibifu wa jengo hili haturusu ukarabati wowote kufanyika,” alisema Naibu Katibu Mkuu Elimu. | 3kitaifa
|
Kukosa uthubutu kwa kutiana uoga, ndiyo jambo linaloendelea hivi sasa katika tasnia ya muziki nchini; mfano, wasanii wengi hivi sasa wamekuwa wakitengeneza maudhui ya kazi zao ili kuwafurahisha BASATA. Ndiyo maana utasikia wasanii katika kazi zao eti “hapendagi mpasuo, hataki shida BASATA.” Ukiangalia majukumu waliyonayo BASATA, utagundua kuwa ofisi hii ambayo imepewa jukumu la kusimamia sanaa nchini, imepewa majukumu ambayo ni makubwa kiasi ambacho kinapelekea kuwa kama miungu watu kwenye hii tasnia. Mfano, katika mahojiano na BBC Afisa Habari wa BASATA akizungumzia sakata la kumfungia Diamond Platnum alisema “Kwa mujibu wa sheria tunaweza kumzuia kwenda kufanya nje ya nchi kwa sababu tutakataa kutoa vibali vya kumruhusu kutoka.” Katika yote hayo, kuna jambo ambalo hivi sasa BASATA wamekuwa wakilifanya ambalo kwa kiasi kikubwa litapelekea kupungua kwa ubunifu pamoja na ufanisi wa kazi za sanaa: ukaguzi wa maudhui. Sote tunajua hili ni moja ya jukumu la taasisi hii lakini ukaguzi wa BASATA nautilia shaka kidogo kwasababu katika sanaa unaweza kutunga ushairi, ukachora picha au ukachonga kinyago lakini maana ya kazi hiyo ni dhamana kwa hadhira siyo kwa msanii tena. Je, hawa BASATA hivi sasa ndiyo hadhira? Mfano, miaka ya hivi karibuni wametoa makatazo ya kazi mbalimbali za sanaa wakidai wasanii hao kuwa wamevunja taratibu au maadili ya tamaduni zetu lakini hawajaelezea ni kwa vipi. Kuna wimbo “I’m sorry JK” ambao aliutoa msanii Nikki Mbishi walidai wimbo ule unalengo la kuleta “maudhi kwa wananchi” maajabu ni kwamba katika maelezo yao hawakuonyesha ni nani alilalamika kuwa amekwazika na wimbo huo, jambo ambalo linaonekana mlalamikaji alikuwa ni BASATA mwenyewe. Lakini si hivyo tu, wasanii kama Diamond Platnumz, Ray Vany, Roma Mkatoliki, Maua Sama, Ney Wamitego kwa kiasi kikubwa wamekuwa wahanga wa rungu la BASATA kutokana na maudhui ya kazi zao. BASATA wanadai kuwa wasanii hawa wamevunja maadili na miiko ya tamaduni za kitanzania lakini mara nyingi baraza hili limekuwa likitoa sababu ambazo hazijitoshelezi; mfano, ni wimbo wa Mwanza ulioimbwa na msanii Ray Vany na Diamond Platnumz ulikuwa una kosa gani? Msanii anaweza kutoa wimbo lakini msanii huyu hana tena nguvu ya kuzuia au kudhibiti hadhira jinsi walivyopokea tungo; sasa inakuwaje BASATA wavae viatu vya hadhira na kudai eti, wimbo flani eti umevunja kanuni za mwenendo wa tamaduni za kitanzania. Nikiwa kama mmoja ya watengeneza maudhui jambo ambalo linakwaza siyo kukosolewa bali ni pale mtu flani anapojifunga kimaana: yaani unalazimisha ulivyoelewa wewe ndiyo yawe mawazo yangu. Hii ni mifano ya Nyimbo ambazo BASATA walizifungia baada ya kufanya uchambuzi (maoni); “I’m Sorry JK” Na Nikki Mbishi
Katika kipindi cha mpito mara baada ya serikali ya awamu ya tano kuchaguliwa, rais wa awamu ya nne, Dkt. Jakaya Kikwete, alipokuwa akiwaaga wananchi wake aliwaambia “Mimi naondoka lakini mtanikumbuka” watu wengi ikiwa ni pamoja na viongozi wa upinzani walipinga kauri hile. lakini baada ya kuingia JPM, mambo yalibadilika kiasi kwamba mbunge wa Arusha mjini, Bernad Lema alisema “Namkumbuka sana JK.” akiwa Kama msanii, Nikki Mbishi alikuwa anakosa gani kutumia kipindi kama hicho kuandika track ya “I’m sorry JK”? “Kiba 100” Rostam ft Maua Sama
Wasanii wanapoandika nyimbo zao, hutumia tamathali za semi ili kunogesha tungo zao bila hivyo kazi nyigi za kisanaa zingekuwa zinaonekana kama taharifa ya habari. Nimekumbuka kuna wimbo aliimba Msafiri Solo Thang “Miss Tanzania” kuna watu wengi waliweka maana zao katika wimbo hule, nilimpongeza sana Msafiri kwa kuchangamsha hadhira. Hivi sasa kumekuwa na mijadala ya nini kinachonogesha mapenzi; je, ni fedha, tendo la ndoa, urembo au utanashati. Katika wimbo huu Maua alijibu maswali hayo akitumia “mlinganishio” watu wengi wana majibu mengi sana ya hayo maswali lakini wengi huishia kusema fedha ndiyo unogesha mapenzi hivyo mwanaume “mashine” ni yule mwenye fedha na “kiba 100” ni yule asiye na fedha hayo ni mawazo yangu, BASATA wanaweza kuwa na ya kwao lakini haikupaswa kuwafungia kazi hii bali walipaswa kupongezwa kutokana na tungo yao. “Mwanza” Ray Vany ft Diamond
Pia, wimbo huu ambao ulitolewa na wasanii hawa kutoka lebo ya “WCB” ulifungiwa bila ya kutolewa maelezo ya kitaalamu. BASATA kama chombo cha kisanaa na fikiri hawafikiri kisanii, kama wangekuwa wanafikiri kisanii kazi hii ingetolewa maelezo ya kitaalamu kabisa na chombo hiki kilichojawa na wanazuoni wabobezi. Wasanii wanapokuwa wanatoa kazi zao za kisanaa, pia wanakuwa na malengo ya kibiashara. Unaweza kuwa na bidhaa inayofanya vizuri hapa Tanzania lakini, bila yakuwa na mkakati mzuri ukiipeleka Kenya ikafanya vibaya. WCB ni lebo ya muziki kubwa; wanapofanya kazi zao wanaitaji kazi zao kusikika kwa wingi katika nchi yao. Kimuziki, jiji la Mwanza linatambulika kama “Hip Hop City” wasanii wengi waliotokea Mwanza wanaimba miondoko ya Hip Hop. WCB waliona kuna haja kubwa ya hadhira iliyopo Mwanza kusikiliza nyimbo zao, hivyo kibao cha Mwanza ni sehemu ya mkakati wa kibiashara, hakuna sehemu yeyote wameimba matusi au wamevunja miiko ya tamaduni; je, ni kwa nini BASATA walifungia wimbo huu. Kama msanii Ney Wamitego alivyowahi kujibu mapigo ya BASATA, nafikiri wakati umefika kwa baraza la sanaa nchini kuitisha mdahalo wa wazi kabisa kati yake na wasanii pamoja na watengeneza maudhui ili waweze kutatua mgogoro wao kama sivyo, maisha ya wasanii na wasimamizi wa kazi zao yatakuwa kama yale ya katuni maarufu za “Tom & Jerry”.
Imeandikwa na David Andy | 0burudani
|
KIJIJI cha Kabukome ni kati ya vijiji 74 vya Wilaya ya Biharamulo. Kipo katika Kata ya Nyarubungo mkoani Kagera. Kinakadiliwa kuwa na wakazi 5,000 katika kaya 650.Kijiji hicho kinasifika kwa uzalishaji mkubwa wa mazao ya chakula kama mpunga, alizeti, mahindi, maharagwe. Hata hivyo, kijiji hicho kinafanya uzalishaji mashambani kwa njia za kienyeji ikiwamo ya kuzalisha kwa mkono, kusomba gunia mojamoja la mazao kichwani na kufanya shughuli zao taratibu.Kijiji hiki kinashuhudia kata nyingi hata ambazo hazizalishi kwa wingi vyakula zikiwa katika nuru ya kutosha, hivyo kinahitaji nishati ya umeme ili kukabiliana na mabadiliko mbalimbali ya teknolojia na kuzalisha maradufu.Wakulima kijijini hapo wanatembea kilomita 15 kufika Biharamulo mjini ili kukoboa mazao yako na kilometa 15 kurudi kijijini kwao kutafuta soko la kuuza mazao yao. Mwenyekiti wa Kijiji cha Kabukome, Kisabo Dominick anasema, hali hiyo inawafukuza wawekezaji na wanataka ikome kwani wawekezaji wangependa kuweka mashine za kukoboa mpunga, lakini hawana pa kuanzia kwa kuwa hakuna nishati ya umeme.Anasema licha ya ugumu katika kupata huduma hizo za kusaga na kukoboa mazao kutokana kulazimika kutembea umbali huo, pia ili kupata mahitaji kama mafuta ya taa, betri za tochi na nyingine, lazima mtu ajiandae kwa umbali huo.Anasema kilio cha nishati kama mwangaza wa kuyaangaza upya maisha ya kijiji hicho si kwa wakulima tu, bali hata wazee wasiomudu kutembea umbali huo kutafuta mahitaji ya msingi.“Tumefikisha kilio chetu kwa viongozi mbalimbali tunaendelea kuvumilia maana maendeleo ni hatua, lakini mimi kama mwenyekiti napenda niuthibitishie umma kuwa kama tutapata umeme na tukapata mashine za kusaga mazao yetu hapahapa, hakika huu utakuwa mlango wa kupata chakula na mazao ya akiba ya kutosha,” anasema Dominick.Desemba 5, mwaka huu mamia ya wananchi wa kijiji hiki na vijiji jirani wanakusanyika ili kumsikiliza Waziri wa Nishati, Dk Medard Kalemani na kujua hatima ya kijiji hiki katika suala la kupata nishati ya umeme. Majira ya saa 12.30 jioni waziri wa Nishati na timu ya wataalamu kutoka makao makuu ya Tanesco, wakala wa Nishati Vijijini (Rea) na watendaji wa Tanesco kutoka Kanda ya Ziwa, mkoa na wilaya ili kubaini kinagaubaga kinachokwamisha upatikanaji wa umeme katika kijiji hicho.Mbele ya Waziri Kalemani, Diwani wa Kata ya Nyarubungo, Furugence Zamukobao, anakiri Wizara ya Nishati kufanya kazi kubwa katika kuhakikisha umeme unasambaa nchini.Anasema kata hiyo ina vijiji 6 kati ya hivyo, viwili ‘havijaguswa’ na umeme. Vijiji hivyo ni Bukome na Rusanbya, lakini hata vijiji vilivyoguswa umeme umepita barabarani huku akitolea mfano wa kijiji anachotoka kuwa kati ya kaya 407 ni kaya 22 tu zilizonufaika. Anakiri mbele ya waziri kuwa, kijiji hicho kina manufaa makubwa na wawekezaji hupenda kuja kuwekeza katika kijiji hicho, lakini kutokuwepo kwa umeme kunawakimbiza wawekezaji hao.Diwani Zamukobao anasema kama kijiji hicho kingekuwa na nishati ya umeme, kingekuwa na mabadiliko chanya na makubwa ya kiuchumi. Ndipo Waziri Kaleman anawaondoa hofu wananchi wote nchini kuwa hakuna kijiji kitakachobaki bila kupata umeme iliwananchi wapate huduma karibu hata za kuchaji simu zao.Kwa kutambua umuhimu wa kijiji hicho anawataka Tanesco kuhakikisha nguzo na vifaa vingine vya kuwasha umeme katika vijiji hivi viwili visivyo na umeme zinafika hapo ifikapo Desemba 20 ili kuwaondolea adha ya kujitwisha mpunga kichwani na kutembea umbali wa kilometa 30 kutafuta huduma za kukoboa na kusaga.Anasema hadi kufikia Januari 30, mwaka ujao vijiji vya Kabukome na Kasabyua viwe vimepata huduma za umeme ili kuondoa kilio cha muda mrefu na hata kufungua milango ya uwekezaji katika kata hiyo. Waziri akatoa bure vifaa vya kuwashia umeme nyumbani ‘Umeta’ (Umeme Tayari) vipatavyo 50 na kusisitiza vifaa hivyo vigawiwe katika familia duni zisizo na uwezo wa kufanya wayaringi nkatika nyumba zao.“Hakuna mwananchi atakayetoka kijijini kwenda kufanya malipo ya umeme kinachotakiwa kufanyika ni mfanyakazi wa shirika la umeme kuweka ofisi katika makazi ya kijiji ili wananchi walipie na waunganishiwe,” anasema.Mkazi wa Kijiji cha Kabukome Kinyozi, Avitus Julian Gaya anasema kutokuwepo kwa umeme kumetoa mwanya kwa ‘wapiga dili’ kuingiza vifaa vya umeme utokanao na mionzi ya jua visivyokidhi mahitaji wala ubora unaotakiwa. Grasion Leonald anasema amepata mafunzo ya ufundi seremala na kuchomelea (welding), lakini analazimika kuuza bidhaa ndogondogo kwani shughuli zake zinahitaji umeme kwa kiasi kikubwa hasa welding ingawa vifa hivyo anavyo.Anasema kundi la vijana limepata mafunzo ya uchomeleaji hivyo kama umeme utapatikana kijijini hapo, watajiunga katika vikundi na kuwajibika kufanya kazi walizosomea na kupata ujuzi kuliko kufanya kazi za ‘kubangaiza’ ambazo hawakuwahi kufikiria.Anatoa mfano akisema wapo baadhi ya wananchi wanaoonekana si nadhifu kutokana na kukosekana kwa umeme kwani hata gharama ya kunyoa nywele kwa vinyozi ni Sh 2000, badala ya Sh 500 katika maeneo yenye umeme.Leonald anasema: “Katika hali ya kawaida, ni vigumu mwananchi kuchukua 2,000 kunyoa nywele kuliko kununua sukari…. kama agizo la waziri litazingatiwa la kupata umeme ifikapo Januari mwakani, basi milango ya uchumi itafunguka.”Mwalimu wa Shule ya Msingi Kuyenza iliyopo kijijini hapo, Aloyce Samweli, anasema kilio cha kutokuwepo kwa nishati si kwa wananchi pekee, bali hata wanafunzi ambao mitihani yao haiwezi kuchapishwa.Anasema kuchapishwa kwa mitihani katika shuloe za vijijini husaidia kuwaondolewa wanafunzi hofu wanapokutana na mitihani ya taifa ambao huwea imechapishwa na hivyo, kuiona kuwa ni ya kawaida. Kwa mujibu wa Meneja wa Shirika la umeme Tanesco wa Wilaya ya Biharamulo Ernest Midyango, wilaya hiyo ina vijiji 74 kati ya hivyo vijiji 51 tayari vimepata umeme.Anasema katika vijiji 74 kuna vitongoji 333 na vitongoji vinaendelea kusambaza huduma hizo huku shirika hilo kwa kushirikiana na Rea watahikikisha hawavuki muda wa serikali wa kusambaza umeme kwa wananchi kwani wakandarasi wako maeneo ya vijijini wanaendelea na kazi. | 3kitaifa
|
MKUU wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda ametoa siku tano kwa wakandarasi wote wa mkoa huo wenye miradi inayosuasua kuhakikisha wanatekeleza kwa sababu inatia doa utendaji kazi wa viongozi wa mkoa.Amezitaka bodi zote za zabuni zifanye kazi kwa weledi na kuacha kupokea rushwa kwa kuwa inakwamisha miradi. Akizungumza na waandishi wa habari jana, Makonda alisema ametoa siku tano kuanzia jana kwa wakandarasi wote wanaotekeleza miradi ndani ya mkoa huo kuhakikisha wanakuwa kwenye maeneo ya kazi na kutekeleza zabuni zao, vinginevyo hatasita kuwachukulia hatua hata kama miradi hiyo zabuni zake zilitolewa na wizara.“Ninawapa siku tano wakandarasi wote wenye miradi inayosuasua mkoa wa Dar es Salaam kuhakikisha wako ‘site’ na wanaendelea na kazi, kwa sababu tumebaini baadhi yao walidanganya kwenye makaratasi waliandika wana uwezo na ni daraja la kwana ila ukweli hawana uwezo huo na fedha pia hawana, nitashughulika nao hata kama zabuni hazikutolewa na ofisi ya mkoa,” alisema Makonda.Kauli ya Makonda imekuja ikiwa ni mwendelezo wa hatua kadhaa alizoanza kuzichukua baada ya Rais John Magufuli kukerwa na kutoridhishwa kwa utekelezwaji wa baadhi ya miradi ya maendeleo ya mkoani humo Septemba mwaka huu, na kutoa maagizo kwa viongozi wa mkoa huo. Septemba 16, mwaka huu, Rais Magufuli alifungua kiwanda cha kutengeneza mabomba na pia kutembelea Mradi wa Upanuzi wa Kiwanja cha Kimataifa wa Ndege wa Julius Nyerere (JNIA) kisha alifanya ziara ya kushtukiza kwenye machinjio ya Vingunguti ambako alioneshwa kukerwa na kusuasua kwa utelekezaji wa miradi ya maendeleo.Aidha, Rais Magufuli alihoji utendaji kazi wa viongozi wa mkoa huo na katika kutekeleza maagizo ya kiongozi mkubwa wa nchi, Makonda alianza kuchukua hatua kwa kutangaza kufanya kazi kwenye maeneo ya miradi na sasa amehamia kwa wakandarasi wa miradi inayosuasua kwa kuagiza wawe kwenye maeneo yao kuanzia jana. Makonda alisema kusuasua pia kwa baadhi ya miradi hiyo ya maendeleo kumesababishwa na baadhi ya viongozi wa bodi za zabuni kutoa zabuni hizo kwa njia ya rushwa huku wakifahamu wazi kwamba wakandarasi wanaowapa kazi hawana uwezo wa kifedha na vifaa.“Tumebaini kuwa baadhi ya wakandarasi wamedanganya na hili limefanyika kwa ushirikiano na baadhi ya bodi za zabuni ambazo wamepokea rushwa na kutoa zabuni kwa wakandarasi wanaofahamu wazi kuwa hawana uwezo wa kutekeleza kazi husika, na mimi nasema nitawafukuza na sitasita kuvunja mikataba yao,” alisema Makonda.Akitoa mfano, alisema mradi kama wa Maboresho ya Mto Ng’ombe wilayani Kinondoni, unaogharimu Sh bilioni 32 ukiwa na urefu wa kilometa 7.5, ambao haujaanza kutekelezwa ilhali mkataba ulishasainiwa Juni 16, mwaka huu.“Mfano mradi huu viongozi wa wilaya wanadanganya kuwa mkandarasi yupo site anaendelea na kazi lakini ukweli hakuna mkandarasi eneo la kazi, na miradi mingine kama ule wa Hospitali ya Kivule,” alisema.Mbali na Rais Magufuli kukerwa na utekelezaji wa miradi ya maendeleo mkoani humo, pia Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Selemani Jafo amechukizwa na kasi ndogo ya utekelezaji wa miradi hiyo na kuwataka watendaji wa mkoa kubadili kazi ya utendaji kazi wao. Katika hatua nyingine, Makonda ametangaza kamati maalumu ya watu 14 ya kuratibu matibabu ya watoto 500 wa ugonjwa wa moyo wanaotibiwa katika Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete kupitia mpango wa mkuu wa mkoa.Kamati hiyo itaongozwa na Mtendaji Mkuu mstaafu wa Benki ya CRDB, Dk Charles Kimei akiwa na wajumbe wengine 13 ambao wataratibu upatikanaji wa Sh bilioni moja kwa ajili ya matibabu ya watoto hao 500. Makonda alisema katika kuelekea mwisho wa mwaka ameamua kuandaa kamati hiyo ili kusaidia watoto hao wenye mahitaji ya tiba ili nao wapone na kuendelea na maisha yao. | 3kitaifa
|
*Magdalena ang’ara kwa wanawake *Wakata tiketi kushiriki mbio za Dunia Na ADAM MKWEPU-DAR ES SALAAM MWANARIADHA Alphonce Simbu amefanikiwa kung’ara kwa mara nyingine na kuipeperusha vyema bendera ya Tanzania, baada ya kushinda mbio za Standard Chartered Mumbai Marathon zilizofanyika jana nchini India. Ushindi huo umemwezesha kukata tiketi ya kushiriki mashindano ya riadha ya Dunia yanayotarajiwa kufanyika Agosti mwaka huu jijini London nchini Uingereza. Simba alishinda mbio hizo kwa kutumia muda wa saa 2:09:32, huku mpinzani wake aliyeshika nafasi ya pili, Bahadur Singh Dhoni, kutoka India akimaliza kwa kutumia saa 2:19:51 na mshindi wa tatu Sanjith Luwang alikimbia kwa muda wa saa 2:21:19. Ushindi huo umemwezesha Simbu kufuzu kwa kiwango cha daraja A katika mbio za Dunia zitakazofanyika jijini London, Uingereza pamoja na Mtanzania mwingine, Magdalena Crispian aliyeshika nafasi ya nne kwa upande wa wanawake akimaliza mbio za kilometa 31 kwa kutumia muda saa 2:34:51. Kwa ushindi huo, Simbu amefanikiwa kupata kitita cha Dola za Marekani 67,000 (sawa na Sh milioni 149). Katika kiasi hicho, Dola 42,000 zimetokana na ushindi alioupata katika mbio hizo, huku Dola 15,000 amepewa kwa ajili ya heshima ya ushiriki wake na Dola 10,000 zilitolewa kama ziada. Akizungumzia mafanikio ya mwanariadha huyo, Katibu Mkuu wa Shirikisho la Riadha Tanzania (RT), Wilhelm Gidabuday, aliliambia MTANZANIA kuwa ushindi huo umewapa uhakika wa kuingiza wanariadha wawili katika mbio za Dunia mwaka huu. “Simbu ameshinda mashindano makubwa yaliyopo kwenye orodha ya Jumuiya za mbio fupi na ndefu (AIMS), kwani amefanikiwa kupunguza muda wa dakika mbili ikilinganishwa na muda aliotumia katika mbio za Olimpiki zilizofanyika mwaka jana. “Simbu na Magdalena wamefikia viwango vya daraja ‘A’ kwa ajili ya kushiriki mbio zinazosimamiwa na Shirikisho la Riadha la Dunia (IAAF) za ‘IAAF Track and Field’ ambazo mwaka huu zitafanyika London, Uingereza,” alisema Gidabuday. Aidha, Katibu huyo alisema Simbu anatarajia kutua jijini Dar es Salaam leo akitokea India. Katika taarifa aliyoitoa kwenye mtandao wa wadhamini wa mbio hizo, Benki ya Standard Chartered, Simbu alisema ushindi huo umetokana na kuzifanyia kazi mbinu alizofundishwa na kocha wake. “Nilijiandaa vizuri, sikuogopa wala sikujali chochote kama ningekimbia kwenye milima au tambarare, lakini ushindi ndio ulikuwa kwenye malengo yangu,” alisema Simbu. Safari ya mafanikio kwa mwanariadha huyo ilianzia katika michezo ya Olimpiki mwaka jana alipofanikiwa kumaliza nafasi ya tano kwa kutumia muda wa saa 2:11:15 katika mbio za marathon (km 42) zilizofanyika jijini Rio de Jeneiro, nchini Brazil. | 5michezo
|
RAIS John Magufuli amesema Jeshi la Polisi na vyombo vingine vya ulinzi na usalama vinafanya kazi nzuri kwa nidhamu na weledi katika kuhakikisha nchi ina amani na utulivu.Aliyasema hayo jana wakati akifunga mafunzo ya Uofisa na Ukaguzi Msaidizi wa Polisi yaliyofanyika kwenye Chuo cha Taaluma ya Polisi kilichopo Kurasini jijini Dar es Salaam.Awali, Mkuu wa chuo hicho, Anthony Rutashurubugukwa alimweleza Rais Magufuli kuwa jumla ya askari 513 wamehitimu mafunzo hayo na wengine watatu walifariki dunia wakati wakiendelea na mafunzo. Rutashurubugukwa alisema miongoni mwa askari hao 513, waliohitimu mafunzo ya Uofisa walikuwa 120 na miongoni mwao askari wa kike 14 na askari wa kiume 106, na kwa upande wa Ukaguzi Msaidizi waliohitimu ni askari 393 na miongoni mwao askari wa kike 60 na askari wa kiume 333.Rais Magufuli ambaye alikuwa mgeni rasmi kwenye mahafali hayo, aliwaeleza Polisi na askari wengine kuwa anatambua kazi nzuri wanayoifanya katika kulinda amani na usalama wa nchi na kuwataka wasivunjike moyo kwa kuwa yuko pamoja nao. Alisema dhamira ya serikali yake ni kuhakikisha Jeshi la Polisi na majeshi mengine yanatimiza kazi zake kwa kuzingatia weledi.Aliyapongeza majeshi yote kwa kufanya kazi kwa ushirikiano na kuheshimiana wakiongozwa na kiongozi wao Mkuu wa Majeshi, Jenerali Venance Mabeyo. “Changamoto iliyopo sasa ni kubadilika kwa aina ya uhalifu kutokana na maendeleo ya sayansi na teknolojia.Maendeleo haya yameleta aina mpya ya uhalifu kama vile wizi wa mtandao, utakatishaji fedha na madawa ya kulevya, hivyo Jeshi la Polisi na vyombo vingine hamna budi nanyi kutafuta mbinu mpya za kukabiliana nayo,” alieleza Rais Magufuli ambaye ni Amiri Jeshi Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama nchini. Aidha, alisema pamoja na kazi nzuri, lakini ndani ya Jeshi la Polisi bado kuna baadhi ya askari wameshindwa kufanya kazi zao kwa weledi na kujituma.Alisema askari hao wamekuwa wakiwabimbikia wananchi kesi pamoja na kujihusisha na vitendo vya rushwa. Kutokana na vitendo hivyo, aliiagiza Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi na Mkuu wa Jeshi la Polisi, Simon Sirro kuchukua hatua dhidi ya askari hao kwa kuwa vitendo vyao siyo tu kwamba vinalichafua jeshi, bali pia serikali.Rais Magufuli aliwapongeza wahitimu wote na kuwakumbusha kuwa elimu siyo cheti tu, bali ni pamoja na kutumia maarifa yao katika kuboresha utendaji kazi wao. “Wengine mkitoka hapa mtaenda kupangiwa majukumu makubwa, mkaoneshe utofauti na mlivyokuwa kabla na baada ya kuhitimu mafunzo haya; mkafanye kazi kwa weledi, mkawasimamie vizuri askari walio chini yenu pamoja na kuwahudumia wananchi vizuri,” alieleza Rais Magufuli.Aliongeza, “Nitasikitika sana nikisikia mnawanyanyasa askari wa chini yenu, kujihusisha na rushwa, kuwabambikia kesi wananchi; kumbukeni wimbo wa Polisi ulioimbwa hapa, niliufuatilia mwanzo hadi mwisho, una mafundisho ya kutosha kwa Jeshi la Polisi.”Aliwakumbusha kuwa Polisi na vyombo vingine vy ulinzi na usalama ni vyombo nyeti kwa ustawi wa taifa na ndiyo maana hata wanasiasa wanafanya kazi zao vizuri kwa kuwa wanajua wako salama. Katika kutambua kazi kubwa inayofanywa na majeshi nchini, Rais Magufuli aliwataka pia kushiriki katika shughuli za kiuchumi kama vile viwanda vya kuzalisha maji, viwanda vya nafaka na viwanda vya kutengeneza sare za askari zenye ubora unaotakiwa.“Panueni wigo na mshiriki katika shughuli za kiuchumi. Kwa mfano, Jeshi la Magereza mna kiwanda cha kutengeneza viatu Karanga, mnaweza kushirikiana majeshi yote na mkafanya uwekezaji mkubwa,” alisisitiza. Aliyewahi kuwa Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini, Omari Mahita alikuwa kivutio kwenye mahafali hayo, na alipopewa nafasi na Rais ya kusalimia, alisema Rais Magufuli ni Rais wa kwanza kukubali kufunga mafunzo ya Uofisa na Ukaguzi Msaidizi kwa kuwa miaka ya nyuma walikuwa wakiambiwa kazi ya Rais ni kukamisheni tu. | 3kitaifa
|
Makubaliano haya ni awamu ya kwanza ya uendelezaji wa hekta 110 za eneo hilo huru la bandari, ambalo limetengwa na Serikali kwa ajili ya uwekezaji mbalimbali.Hekta hizo 10 zitaendelezwa kwa kuwekewa miundombinu inayotakiwa na kisha kugawiwa kwa kampuni za kimataifa, zinazofanya kazi za kutoa huduma mbalimbali kwa kampuni zinazofanya kazi ya utafiti wa mafuta na gesi katika Mkoa wa Mtwara.Kitakapomalizika, kituo hiki cha huduma kwa kampuni zinazofanya utafiti wa gesi na mafuta mkoani Mtwara kitakuwa cha kipekee, si kwa Tanzania pekee bali katika ukanda mzima wa Mashariki na Kusini mwa Afrika.Utiaji saini makubaliano hayo ya kihistoria mwishoni mwa wiki jijini Dar es Salaam, ulifanywa na Mkurugenzi Mkuu wa EPZA, Dk Adelhelm Meru na Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa TPA, Madeni Kipande.Utiaji saini ulishuhudiwa na Waziri wa Uchukuzi, Dk Harrison Mwakyembe na Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara, Gregory Teu.Akizungumza kwenye hafla hiyo, Dk Mwakyembe alisema hatua hiyo inatoa fursa kwa kampuni za kimataifa, zinazotoa huduma kwa kampuni za utafiti na uzalishaji wa gesi na mafuta kuwekeza Mtwara na pia kutoa huduma zake katika Afrika.Waziri Mwakyembe alisema kampuni saba ziko tayari kuwekeza katika eneo hilo. Alitaka mamlaka husika kuhakikisha zinafanya haraka na kwa usahihi matayarisho yote yanayotakiwa ili kampuni hizo ziweze kuanza kufanya kazi mara moja.“Mamlaka husika hazina budi kumaliza haraka na kwa usahihi matayarisho yanayotakiwa ili uwekezaji huu uanze mara moja,” alisema.Alisema kabla ya hapo kampuni hizo zilikuwa zikitoa huduma zake kutokea Mombasa, Kenya na Afrika ya Kusini. Waziri Teu alisema hatua hiyo ni muhimu kwa uchumi wa Tanzania.“Mtwara na Tanzania sasa vinafunguka zaidi,” alisema, na kuongeza kuwa baada ya kuanza kazi, kampuni hizo zitazalisha ajira kwa Watanzania na kuongeza wigo wa kodi kwa Serikali.Kwa upande wake, Dk Meru alisema hatua hiyo ni muhimu kwa kuwa kampuni hizo zitatoa huduma kwa kampuni zinazofanya utafiti na uzalishaji wa gesi na mafuta katika nchi za Kusini na Mashariki ya Afrika Alisema ujio wa kampuni hizo pia utasaidia katika kuendeleza sekta nyingine kama hoteli na kilimo katika Mkoa wa Mtwara.Baadhi ya kampuni zilizoonesha nia ya kuwekeza katika eneo hilo la hekta 10 ni Schlumberger, Weatherford and Halliburton International Inc kutoka Marekani.Nyingine ni Lena, FFF (T), Alpha Group and Queensway kutoka Dubai na Uingereza; Altus Tanzania Ltd kutoka Singapore; Tans Ocean Industries & Services Ltd ya Dubai na Intershore Tanzania Ltd ya Afrika Kusini. | 1uchumi
|
Anna Potinus, Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda amemtaka muigizaji wa
vichekesho, Idris Sultan kufika katika kituo chochote cha polisi kilichopo karibu
naye baada ya kufanyia ‘photoshop’ picha zake na kuweka kichwa cha Rais John
Magufuli ikiwa ni sehemu ya vichekesho vyake. Idris aliweka picha mbili katika mtandao wake wa kijamii wa Instagram na
kuambatanisha na ujumbe mfupi wa maneno uliosema “kwa siku moja tukabadilishana
kazi ili aenjoy birthday yake kwa amani,” aliandika Idriss huku akilenga kumtakia
heri Rais Magufuli katika siku yake hiyo ya kuzaliwa kwa njia ya utani. Katika picha hizo, moja inamuonyesha Idris akiwa ameketi kwenye kiti cha
Rais, Ikulu huku nyingine ikimwonyesha picha ya Rais Magufuli akiwa katika
mwonekano wa msanii huyo. Baada ya Makonda kuona picha hizo alimtaka msanii huyo kufika katika
kituo cha polisi ambapo atakuta ujumbe ambao amemuachia akidai kuwa kitendo
alichokifanya kinaonesha kuwa haijui mipaka yake ya kazi. “Naona mipaka ya kazi yako hauijuwi, nenda sasa hivi kituo chochote cha
polisi uwaambie Makonda kaniambia nije utakuta ujumbe wako,” ameandika Makonda
katika ukurasa wake wa Instagram. Naye Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamisi Kigwangala ameonesha kushangazwa
na kitendo cha msanii huyo kuitwa polisi kwa kusema kuwa Rais Magufuli ni mtu
wa watu na kwamba Idriss anafahamika kuwa sanaa yake ni ya uchekeshaji. “Nimeambiwa
kuna msanii wa vichekesho anatafutwa na polisi, akikamatwa mniambie,
nitajitolea mwanasheria wa kwenda kumuwekea dhamana na kumtetea. Rais wetu ni
mtu wa watu na imejidhihirisha kwa jinsi wananchi walivyojitolea kumuombea dua
siku ya kuzaliwa kwake! Wameonesha upendo,” ameandika Kigwangala. | 0burudani
|
PYONGYANG, Korea Kaskazini KIONGOZI wa nchi hii, Kim Jong-un, juzi aliondoka
kwa kutumia usafiri wa treni kwenda katika mji wa Hanoi kwa ajili ya mazungumzo
na Rais wa Marekani, Donald Trump. Mkutano kati ya Marekani na Korea Kaskazini
unatarajiwa kufanyika siku ya Jumatano na Alhamisi katika mji huo mkuu wa
Vietnam. Mkutano huu unakuja baada ya wa kwanza wa kihistoria
uliofanyika mwaka jana nchini Singapore na macho yote yatakuwa yakitazama kama
kuna hatua yoyote iliyopigwa tangu wakati huo kuhusu kuteketeza silaha za nyuklia. Taarifa zilizopatikana mji hapa zinaeleza kuwa Rais Kim Jong-un
amesafiri na dada yake, Kim Yo Jong na mmoja kati ya washauri wake muhimu,
Jenerali wa zamani, Kim Yong Chol. ”Tulipendana,” Trump aliuambia mkutano Septemba
mwaka jana kuhusu Kim.” Aliniandikia barua nzuri,” aliongeza kiongozi huyo. Hata hivyo, pamoja na maneno hayo mazuri, miezi
kadhaa baada ya mkutano wa Juni mwaka jana, ilitawaliwa na kauli za msuguano na
mahusiano yasiyoridhisha. Mkutano huu
unatarajiwa kuendeleza misingi ya mkutano uliopita kuhusu masuala ya silaha za
nyuklia, ambapo wataalamu wanasema jitihada zilizofanyika ni kidogo na kwamba
zikiwa zimebaki siku chache kabla ya mkutano huo wa Hanoi, ajenda zake
hazijawekwa wazi. Wachungizi wa masuala ya kisiasa wanasema kwamba,
licha ya mkutano wa Juni mwaka jana nchini Singapore kati ya viongozi hao kuwa
ulikuwa ni wa kihistoria, lakini makubaliano waliyoyatia saini hayakuwa dhahiri
na hatua kidogo zimechukuliwa kuhusu lengo la kukomesha silaha za nyuklia. Wanasema katika mkutano huo, Rais Trump aliahidi
kukomesha vitendo vya majaribio ya silaha za nyuklia, akishirikiana na Korea
Kusini ambavyo vimeighadhabisha Korea Kaskazini, lakini miezi imepita sasa
wengi wakihoji yeye amefanya nini kwa upande wake. | 2kimataifa
|
Wajawazito zaidi ya milioni mbili walihudhuria na kuandikishwa kliniki katika kipindi cha mwaka jana, ikilinganishwa na wajawazito milioni mbili mwaka 2017.Akizungumza na vyombo vya habari, Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu alisema mwongozo wa utoaji huduma za afya ya uzazi na mtoto, unaelekeza wajawazito kufikia katika vituo vya kutolea huduma mapema. “Wajawazito wanatakiwa kuanza huduma mapema kabla ya wiki 12 ya ujauzito na kuhudhuria kliniki angalau mara nne katika kipindi cha ujauzito ili waweze kupata huduma zote muhimu,” alisema.Alisema wizara iliendelea kuwahamasisha wajawazito kuhudhuria kliniki mapema, ambapo katika kipindi cha mwaka 2018 asilimia 25 ya wajawazito nchini, waliweza kufanya hudhurio la kwanza kabla ya wiki 12, ikilinganishwa na asilimia 18 mwaka 2017. “Takwimu zinaonyesha kuwa idadi ya wajawazito waliohudhuria kliniki angalau mara nne imeongezeka katika kipindi cha mwaka 2018 na kufikia asilimia 57 ikilinganishwa na asilimia 46 mwaka 2017,” alisema.Alisema mikoa ambayo bado kiwango cha mahudhurio ya wajawazito kliniki yapo chini ni Mkoa wa Mara asilimia 40, Njombe (40), Simiyu (41), Iringa (45), Tanga (46), Dodoma (47) na Ruvuma (49). “Huduma ya kumkinga mjamzito dhidi ya malaria iliimarika ambapo asilimia 79 ya wajawazito walipatiwa kinga dhidi ya malaria katika kipindi cha mwaka 2018 ikilinganishwa na asilimia 66 mwaka 2017,” alisema.Ummy alisema kuongezeka kwa wajawazito kufika kwenye vituo vya kutolea huduma za afya, kumechangiwa na kuongezeka kwa vituo vya kutoa huduma za afya nchini. Alisema hadi kufikia Desemba 2018, vituo vya kutolea huduma za afya nchini vilikuwa 7,768 kutoka vituo 7,435 mwaka 2017, sawa na ongezeko la vituo 333 kwa mwaka. “Pia katika vituo hivyo, serikali ilikuwa inamiliki asilimia 71 ya vituo vya kutolea huduma, mashirika ya dini asilimia 12, taasisi za serikali asilimia 3 na vituo binafsi asilimia 15,” alisema. Ummy alisema wakati ambapo hospitali zilikuwa asilimia 3, vituo vya afya asilimia 11 na zahanati asilimia 86. | 3kitaifa
|
Na KULWA MZEE- DAR ES SALAAM MAOMBI ya Jamhuri ya kutaka Mfanyabiashara Yusufali Manji ahojiwe na Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) kuhusiana na masuala ya kodi yamegonga mwamba baada ya mahakama hiyo kukataa kutoa ruhusa hiyo. Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jana ilikataa maombi hayo ya Jamhuri na kutoa sababu kwamba kesi iliyopo mahakamani inahusu uhujumu uchumi na si masuala ya kodi. Mahakama ilifikia uamuzi huo baada ya upande wa mashtaka kutaka Manji akahojiwe na TRA kuhusiana na masuala ya kodi. Akiwasilisha ombi hilo mbele ya Hakimu Mfawidhi, Cyprian Mkeha, Wakili wa Serikali Mwandamizi, Kishenyi Mutalemwa alidai awali waliomba hati ya kumuita mshtakiwa mahakamani lakini kwa sababu za afya hakuweza kufika. “Leo (jana) yupo mahakamani ni ombi letu achukuliwe na TRA kwa ajili ya mahojiano na ndani ya muda wa kazi atakuwa amerudishwa,”alidai. Wakili Alex Mgongolwa anayemtetea Manji alidai maombi hayo kwa jana si sahihi kwa kuwa walikwisha kufanya mawasiliano ya maandishi na TRA. Mgongolwa alidai Manji anao mawakili wengine wanaoshughulika na masuala ya kodi hivyo anahitaji kuwasiliana nao ili mahojiano hayo yawe na manufaa. Alihoji kuhusu mahojiano hayo kwamba anatakiwa Manji ama makampuni yake. Kishenyi alidai anayehitajiwa katika mahojiana hayo ni Manji na siyo makampuni yake na kwamba akifika huko akaona kuna hana ya kuwa na wataalamu wake atasema. Hakimu Mkeha baada ya kusikiliza hoja hizo, alisema hawezi kukubaliana na ombi hilo kwa kumruhusu Manji kwenda TRA kwa sababu kesi iliyopo mbele yake ni ya uhujumu uchumi na haihusiani na masuala ya kodi. Hakimu Mkeha aliahirisha kesi hadi Agosti 18, 2017 kwa ajili ya kutajwa na aliwaambia kwa kuwa mshtakiwa yuko katika maeneo ya mahakama watumie utaratibu wanaoona unafaa kukamilisha wanachohitaji. Katika kesi hiyo, Manji na wenzake watatu wanakabiliwa na mashtaka saba yakiwamo ya kukutwa na vitambaa vinavyotengeneza sare za Jeshi la Wananchi wa Tanzania vyenye thamani ya zaidi ya Sh milioni 200 na mihuri. Washtakiwa wengine wanaokabiliwa na kesi hiyo ni Deogratius Kisinda, Abdallah Sangey na Thobias Fwere Kesi hivyo ipo mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Huruma Shaidi ambaye amefiwa na mama yake mzazi hivyo kesi ikatajwa kwa Hakimu Mkeha. Manji na wenzake wanadaiwa kuwa Juni 30,2017 katika eneo la Chang’ombe ‘A’wilaya ya Temeke Dar es Salaam washtakiwa hao kwa pamoja walikutwa na polisi wakiwa na mabunda 35 ya vitambaa vinavyotumika kutengenezea sare za Jeshi la Wananchi Tanzania (JWTZ), zenye thamani ya Sh milioni 192.5 na kwamba mali hiyo ilipatikana kinyume cha sheria. | 3kitaifa
|
Na BEATRICE MOSSES-MANYARA WAZIRI wa Tamisemi, George Simbachawene, amezitaka wilaya nyingine nchini kuiga Wilaya ya Simanjiro mkoani Manyara, kwa kuwa wilaya hiyo imejenga majengo mazuri ya madarasa, maabara na nyumba za walimu. Simbachawene aliyasema hayo jana kwenye ziara yake ya siku moja wilayani Simanjiro, baada ya kufika katika Shule ya Sekondari Loiborsiret iliyoko wilayani humo. “Majengo ya Simanjiro yamejengwa vizuri kwa sababu yamesimamiwa vizuri na kujengwa kwa ubora unaotakiwa. “Kwa hiyo, viongozi wa wilaya nyingine nchini wanapaswa kupata somo kupitia ujenzi huo ambao thamani ya fedha inaendana na thamani ya ujenzi wa miundombinu iliyofanyika. “Nasema hivyo kwa sababu baadhi ya maeneo, viongozi wanashindwa kusimamia ili yajengwe majengo bora yanayodumu. “Pamoja na hayo, nawapongeza pia wanafunzi wa shule hii ambao wengi wao ni jamii ya kifugaji wa kimasai, kwani baadhi yao nimekagua madaftari yao na kubaini kiwango cha taaluma ni kizuri tofauti na matarajio yangu. “Kwa hiyo, walimu wa shule hii wanastahili pongezi nyingi kwa kufanya kazi yao kwa uadilifu na pia wanafunzi nao kwa upande wao wanatakiwa kupongezwa kwa sababu wanatimiza wajibu wao ipasavyo,” alisema Simbachawene. Naye Mhandisi wa Ujenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Simanjiro, Martin Mwashambwa, alisema ujenzi huo umegharimu Sh milioni 219.9. “Ujenzi huo umehusisha nyumba kubwa yenye uwezo wa kuishi familia sita iliyogharimu shilingi milioni 149.9 na vyumba viwili vya madarasa vya thamani ya shilingi milioni 49.6. “Ujenzi mwingine ni wa vyoo vya wanafunzi wa shule hiyo uliohusisha matundu manane yenye thamani ya shilingi milioni 20. 3,” alisema. | 3kitaifa
|
Mkurugenzi wa Takwimu za Jamii na Sensa ya Watu na Makazi wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS), Ephraim Kwesigabo, alisema hayo juzi na kuongeza kuwa kasi ya upandaji wa bei za bidhaa na huduma kwa mwaka ulioishia Agosti mwaka huu, imeongezeka ikilinganishwa na kasi iliyokuwepo kwa mwaka ulioishia Julai.Aidha alisema fahirisi za bei imeongezeka hadi 149.31 Agosti kutoka 149.16 Julai mwaka huu ambapo pia alitaja baadhi ya bidhaa zisizo za vyakula zilizochangia kuongezeka kwa fahirisi, kuwa ni bia kwa asilimia 2.5, sare za shule kwa asilimia 1.5, mkaa kwa asilimia 1.1 na samani kwa asilimia 2.4.Nyingine ni bidhaa za jamii ya kitambaa kwa matumizi ya nyumbani kwa asilimia 1.5, huduma za meno asilimia 1.0, huduma ya chakula kwenye migahawa asilimia 0.4 na huduma ya kulala hotelini asilimia 1.4.“Kwa ujumla mfumuko wa bei una mwelekeo unaofanana na nchi nyingine za Afrika Mashariki mfano mfumuko wa bei nchini Kenya umeongezeka hadi asilimia 8.36 Agosti mwaka huu ikilinganishwa na asilimia 7.67 Julai mwaka huu,” alisema.Alisema kwa upande mwingine mfumuko wa bei nchini Uganda umeendelea kupungua hadi asilimia 2.8 Agosti 2014 kutoka asilimia 4.3 Julai, mwaka huu.Alitoa mwito wa wanahabari kuwaelimisha watunga sera na wananchi wote kwa ujumla kuhusu umuhimu wa matumizi ya takwimu hizo za bei pamoja na nyinginezo zinazotolewa na NBS.Pia aliwaomba wananchi kutoa ushirikiano wa dhati kwa ofisi za Takwimu za Mikoa wakati wa ukusanyaji wa takwimu mbalimbali kwa lengo la kutoa taarifa zilizo sahihi kwa ajili ya maendeleo ya nchi. | 1uchumi
|
KATIBU Mkuu, Wizara ya Mifugo na Uvuvi, Profesa Elisante ole Gabriel amewashauri wakuu wa mikoa, wilaya pamoja na wakurugenzi wa halmashauri nchini kushirikiana na kuwafikishia wafugaji mbegu za mifugo kwa bei rahisi ili kuboresha sekta ya mifugo pamoja na nyama.Gabriel ametoa ushauri huo hivi karibuni wakati alipotembelea Kituo cha Taifa cha Uzalishaji Mifugo kwa njia ya Chupa (NAIC) kilichopo Usa River Mkoani Arusha, kwa ajili ya kujionea ng'ombe bora 26 wanaotoa dozi 120,000 kila mwaka kwa ng'ombe mmoja.Amesema mbegu hizo ambazo huuzwa kwa dozi moja Sh 3,000 zinapaswa kumfikia mfugaji ili aweze kupandisha ng'ombe wa kawaida na kupata matokeo mazuri ya kuwa na mifugo bora, lakini mbegu hiyo hiyo bei yake inaweza kupanda kutokana na gharama za usafiri kutoka eneo moja hadi jingine.Aliwaondoa hofu wafugaji kuwa mbegu hizo bora haziondoi uhalisia wa ng'ombe wa asili au hata wa kisasa bali huleta tija zaidi katika kupata uhakika wa mifugo bora inayoleta thamani kwenye mazao hayo.“Mbegu hizi ni bora na zinapaswa kuwafikia wafugaji ili kila mtu apate mifugo bora kwa manufaa ya mfugaji, pia naagiza wafugaji kutotupa mazao yote ya mifugo kwani kila kitu cha ng'ombe kina faida hususan meno yake ambayo yanaweza kutengeneza mkufu na hereni,” alisema.Akizungumzia mitambo kuharibika na kutokuwa na wataalamu wa kuzalisha mbegu kwa hewa baridi, alisisitiza kuwa ni vyema sasa kituo hicho kuhakikisha kinakuwa na wataalamu wa ndani, badala ya sasa ambapo wanatumia wataalamu wa kutengeneza mtambo huo kutoka nje.Mkurugenzi wa NAIC , Paul Mollel alisisitiza kuwa wanataka kutengeneza mbegu bora kutoka kwenye madume bora na kuwafikia wafugaji.Alisema wapo kwenye mchakato wa kutengeneza mashine hizo za Liquid Nitrogen ambazo zinakuwa zinaharibika mara kwa mara na hivi sasa wanazalisha mbegu bora dozi 12,000 kwa siku. Kwa mwaka dume moja hatoa mbegu zaidi ya 120,000.Kaimu Mkurugenzi wa Uzalishaji, Mifugo na Masoko, Dk Asimwe Rwiguza alisema Wizara ya Mifugo na Uvuvi imejipanga kuhakikisha inapunguza gharama za kupunguza bei za uhamilishaji kwa gharama ndogo kwa lengo la kuwafikia wafugaji kwa gharama ndogo kupitia mikoa, wilaya na zifike kwenye halmashauri kwa gharama nafuu.Alisema vituo vingine vipo katika mikoa mbalimbali ikiwemo Pwani, Mwanza, Dodoma, Mbeya, Lindi pamoja na Iringa kwa ajili ya kutengeneza hewa baridi ya kutunzia mbegu katika mikoa hiyo. | 3kitaifa
|
MAJONZI jana yalitawala kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam baada ya Simba kutolewa katika michuano ya Ligi ya Mabingwa wa Afrika, licha ya kutoka sare ya bao 1-1 na UD do Songo ya Msumbiji.Simba imetolewa kwa kanuni baada ya kutoka suluhu na Ud Songo katika mchezo wa mwanzo uliofanyika Beira, Msumbiji na jana kutoka sare ya 1-1, hivyo Simba imeondolewa kwa faida ya bao la ugenini.Bao lililowatoa Simba lilipatikana katika dakika ya 13 lilifungwa na Luis Miquissone kwa mpira wa adhabu ndogo, baada ya mchezaji wa Simba kumkwatua mchezaji wa Songo.Pamoja na Simba kupata bao la kusawazisha kwa penalti iliyopigwa na Erasto Nyoni na kurudisha matumaini kwa wapenzi wao kuwa huenda timu yao ingepata bao la ushindi dakika za mwisho kama walivyokuwa wakifanya katika mechi za msimu uliopita.Kocha wa Simba, Patrick Aussems alisema baada ya mchezo huo kuwa, timu yake ilijitahidi kucheza vizuri na kutengeneza nafasi nyingi za kufunga, lakini hawakuwa na bahati ya kufunga.Alisema baada ya kutolewa katika mashindano ya kimataifa, sasa Simba wanaelekeza nguvu zao katika Ligi Kuu na Kombe la Azam Federation (FA Cup) ili kufanya vizuri na kupata tena nafasi ya kucheza mashindano ya kimataifa msimu ujao.Alisema walijitahidi kufanya mabadiliko lakini bahati haikuwa yao na wametolewa katika mashindano ya kimataifa na sasa wanaangalia mbele katika mashindano ya nyumbani.Kocha UD Songo alisema baada ya mchezo huo kuwa walijipanga kuishambulia Simba kwa nguvu na kuijengea presha ili watoe mwanya wa kufunga, “na hilo ndilo lililotokea kwani presha ilipozidi tulipata bao.”Simba ilikuwa ikipewa nafasi kubwa ya kusonga mbele baada yua msimu uliopita kucheza hadi robo fainali ya Ligi ya Mabingwa wa Afrika na sasa imeisia katika hatua ya awali na kushindwa hata kucheza raundi ya kwanza.Wekundu hao wa Msimbazi imekuwa timu ya pili ya Tanzania kutolewa, baada ya KMC katika michuano ya Kombe la Shirikisho wakati Yanga wakitinga raundi ya kwanza baada ya kuitoa Township Rollers ya Botswana kwa kuifunga 1-0 na Azam kusonga mbele baada ya kuifunga Fasil ya Ethiopia kwa mabao 3-1.Kikosi cha Simba: Aishi Manula, Gadiel Michael, Erasto Nyoni, Pascal Wawa, Salum Kapombe, Deo Kanda, Sharaf Shiboub, Jonas Mkude, Francis Kahata/Hassan Dilunga, Meddie Kagere na Clatous Chama. | 5michezo
|
SHIRIKA la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF), limepanga kutumia vitambulisho vya wajasiriamali, vilivyotolewa na Rais John Magufuli kwa ajili ya kuwasajili wanachama wapya wa mfuko huo kwa upande wa sekta isiyo rasmi.Aidha, shirika hilo limeweka mfumo wa Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (TEHAMA), utakaotumika kutunza kumbukumbu za fedha hivyo kuongeza udhibiti wa ndani na usahihi wa taarifa.Hayo yamebainishwa na Mkurugenzi Mkuu wa NSSF, William Erio alipokuwa akielezea utekelezaji wa maagizo ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC) iliyoyatoa kwa shirika hilo katika kikao cha Oktoba 31, mwaka jana kwa hesabu zilizoishia Juni 2017.Kuhusu utekelezaji wa agizo la kuongeza wanachama kutoka kwenye sekta isiyo rasmi, Erio alisema tayari mfuko umeshasajili mfumo mpya wa sekta isiyo rasmi kwa Mamlaka ya Usimamizi wa Mifuko ya Hifadhi ya Jamii (SSRA).Alisema matarajio ya mfuko ni kuandikisha waendesha bodaboda na bajaji wapatao 22,000 na kuwa kati ya Januari na Aprili wameandikisha wanachama 4,300.“Tumepanga kuyafikia makundi mengine kwa kutumia vitambulisho vya wajasiriamali vilivyotolewa na serikali kwa kuwasiliana na mamlaka za Serikali za Mitaa na mikoa. Pia moja ya mafao tutakayotoa ni bima ya afya na tayari tumeanza mazungumzi na NHIF ili fao hilo litolewe na mfuko huo,” alisema.Alisema mfuko umetekeleza agizo la kutunza kumbukumbu za fedha kwa kutumia mfumo wa Tehama ili kuongeza udhibiti wa ndani na usahihi wa taarifa zinazotolewa, na kuwa mfuko umeweka upya mfumo wake wa fedha na kuusimika rasmi Aprili 8, mwaka huu.Kwa sasa kumbukumbu zake zote za fedha, zitatunzwa kielektroniki na hesabu za mwaka wa fedha unaoishia Juni mwaka huu zitatolewa ndani ya mfumo huu.Kuhusu utekelezaji wa agizo la masuala ya usuluhishi wa hesabu ambayo hayajapata majibu kutoka benki, Erio alisema kuanzia Mei 2, mwaka huu, NSSF imeanza rasmi kufanya usuluhishi wa kibenki kwa kutumia mfumo mpya wa kieletroniki.“Masuala ya usuluhishi wa kibenki yalikuwa na changamoto kutokana na zoezi la usuluhishi kufanyika pasipo kutumia mfumo wa kieletroniki na usuluhishi ulikuwa ukifanyika katika ofisi za mikoa na hivyo kufanya utaratibu wa ufuatiliaji kuchukua muda mredu katika kutatatua. | 1uchumi
|
KOCHA wa Simba, Patrick Aussems amesema ameridhishwa na kiwango kilichooneshwa na wachezaji wake licha ya kutoka suluhu kwenye mchezo wa juzi dhidi ya TP Mazembe ya Congo kwenye Uwanja wa Taifa Dar es Salaam.Mchezo huo wa kwanza wa robo fainali ya Ligi ya Mabingwa wa Afrika, na hivyo Simba kuwa na kibarua kigumu cha kufanya katika mchezo wa marudiano utakaofanyika Lubumbashi wikiendi hii.Huo ni mchezo wa kwanza kwa mabingwa hao watetezi wa Ligi Kuu Tanzania Bara kushindwa kupata ushindi wa pointi tatu kwenye uwanja huo, baada ya kushinda mechi zake zote za awali na zile za makundi za michuano hiyo, walizocheza kwenye uwanja huo.Matokeo hayo ni furaha kwa Mazembe ambao wanarekodi nzuri ya kutumia vyema uwanja wao wa nyumbani hali inayowaweka Simba kuwa mguu mmoja ndani na mwingine nje na hatma yao ya kuendelea au kutoendelea kubaki Lubumbashi, Congo katika mchezo wa marudiano.Akizungumza baada ya kukamilika kwa mchezo huo Aussems alisema wachezaji wa timu hiyo walicheza vizuri na kuridhishwa na kiwango kilichooneshwa, huku akijipa matumaini kuwa timu yake bado ina nafasi ya kufanya vizuri.“Licha ya kutoka suluhu nimeridhishwa na kiwango kilichooneshwa na wachezaji wangu, walitengeneza nafasi nyingi lakini walishindwa kutumia, kufanya makosa kwa mchezaji ni kawaida kwenye mchezo hata sisi makocha wakati mwingine tunafanya makosa nitaongea nao na kulifanyia kazi kabla ya mechi ya marudiano,” alisema Aussems.Kwa upande wake kocha wa TP Mazembe ambaye ni mchezaji wa zamani wa timu hiyo, Mihayo Kazembe alisema wamepata ushindani mkubwa kutoka Simba hali ambayo hawakutegemae kulingana na rekodi zao za michezo ya nyuma waliyocheza na Simba.Simba ilifungwa mara mbili, nyumbani na ugenini katika michuano hiyo ya Ligi ya Mabingwa wa Afrika mwaka 2011.Alisema ushindani ulikuwa mkubwa kila timu ilicheza vizuri walitengeneza nafasi za kupata mabao, lakini walikosa umakini wa kuzitumia vizuri nafasi hizo. | 5michezo
|
ALIYEKUWA Meneja wa Benki ya Wanawake Tanzania (TWB) tawi la Mkwepu, Dar es Salaam Priscus Shirima (37), amefi kishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, akikabiliwa na mashitaka ya matatu, ikiwemo utakatishaji fedha Sh milioni 120.Shirima alifikishwa mahakamani hapo jana na kusomewa mashitaka mbele ya Hakimu Mfawidhi, Kelvin Mhina na kusomewa mashitaka ya uhujumu uchumi. Wakili wa Serikali, Wankyo Simon, alidai Juni 20, 2016, katika Benki ya TWB tawi la Mkwepu, wilaya ya Ilala, akiwa kama Meneja wa tawi hilo, aliyeajiriwa na benki hiyo, akiwa na nia ya uovu, alifanya muamala wa uongo kwa kuhamisha Sh milioni 120 kutoka akaunti namba 0310137001 ambayo ni ya Florah Lyatuu kwenda akaunti namba 0380073121, ambayo ni ya kwake.Katika mashitaka ya pili, siku na eneo hilo hilo, mshitakiwa akiwa kama meneja wa tawi hilo, aliyeajiriwa na benki hiyo, aliiba Sh milioni 120. Wankyo alidai katika mashitaka ya tatu ambayo ni utakatishaji fedha, mshitakiwa huyo anadaiwa kutenda kosa hilo, kati ya Juni 2016, katika benki hiyo.Ilidaiwa kuwa mtuhumiwa alijihusisha na muamala wa Sh milioni 120 kwa kuruhusu na kufanya malipo kutoka akaunti namba 0380073121 inayomilikiwa na taasisi hiyo, akilipa Kampuni ya Sekorizi Ltd kupitia hundi tatu zenye namba 000127, 648806 na 1648791, huku akifahamu kuwa fedha hizo ni zao la uhalifu.Mshitakiwa hakutakiwa kusema chochote kwa sababu mahakama haina mamlaka wa kusikiliza kesi hiyo. Hakimu Mhina aliahirisha kesi hiyo hadi Desemba 27, mwaka huu itakapotajwa na mshitakiwa amerudishwa rumande kutokana mashitaka ya utakatishaji fedha kutokuwa na dhamana | 3kitaifa
|
KENYA jana ilizidi kujiimarisha katika mashindano ya Kombe la Chalenji ya Afrika Mashariki kwa Wanawake baada ya kuikandamiza Djibout kwa mabao 12-0 katika mchezo uliofanyika kwenye Uwanja wa Azam Complex Chamazi jijini Dar es Salaam.Wakati Kenya ikitoa kisago hicho, Waganda wamejihakikishia kucheza nusu fainali baada ya kuifunga Ethiopia kwa bao 1-0 katika mchezo uliofanyika baadaye jana kwenye uwanja huo huo.Jentrix Shikangwa ndiye alikuwa nyota wa mchezo huo baada ya pekee yake kufunga mabao manne katika dakika ya 14, 16, 55 na 84 huku mengine matatu yakifungwa na Mwanalima Jeliko katika dakika ya 35, 86 na 89 na Mecy Auro akifunga mawili katika dakika ya 52 na 65.Kenya hawakutosheka na mabao hayo na waliendelea kulisakama lango la Djibout na kufanikiwa kupata bao la 12 kupitia kwa Vivian Makokha katika dakika ya 12 na Janet Bundi katika dakika ya 45.Wakati huohuo, Uganda iliondoka na pointi tatu muhimu jana baada ya kuifunga Ethiopia katika mchezo mkali na wakusisimua uliofanyika baadaye jana kwenye Uwanja huo huo wa Chamazi Complex. Bao hilo pekee lilifungwa na Najjemba Fauzia katika dakika ya 73. | 5michezo
|
Na VERONICA ROMWALD – DAR ES SALAAM SERIKALI inakusudia kupanua huduma za matibabu ya dharura katika Hospitali ya Kanda Mbeya na Hospitali ya Mount Meru, ili kuboresha huduma za matibabu kwa wagonjwa wanaohitaji msaada wa dharura. Kwa sasa hospitali pekee yenye idara maalumu inayotoa huduma ya matibabu ya dharura nchini ni Hospitali ya Taifa Muhimbili. Hayo yalielezwa jana na Katibu Mkuu – Afya wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dk. Mpoki Ulisubsya, alipokuwa akizindua Kongamano Kuu la pili la Watoa Huduma za Tiba ya Dharura na Kuokoa Maisha. “Kihistoria nchini mwetu, Hospitali ya Taifa Muhimbili ndiyo pekee ambayo ina idara maalumu kwa ajili ya kutoa huduma za dharura kwa watu wanaohitaji huduma hiyo kuokoa maisha yao,” alisema. Alisema kutokana na hali hiyo, Serikali imepanga kupanua wigo wa huduma hiyo katika maeneo mengine kwa kuanzia na Hospitali ya Kanda Mbeya na Mount Meru. “Tunakusudia pia huduma hizi zianze kutolewa hadi katika hospitali binafsi kisha tutaendelea hadi katika hospitali za rufaa za mikoa na wilaya,” alisema na kuongeza: “Kinachoendelea sasa ni kuwapa mafunzo wataalamu ili kuongeza idadi yao, tunao 27 na hivi karibuni kuna ambao watahitimu mafunzo na hivyo idadi hiyo itaongezeka hadi kufikia wataalamu 36. Alisema barani Afrika tafiti zinaonesha asilimia 40 ya watu hufariki dunia kutokana na kucheleweshwa kufikishwa hospitalini pale inapohitajika huduma za dharura. Mwenyekiti wa Kamati ya Maandalizi ya Kongamano hilo, Dk. Upendo George, alisema jumla ya wataalamu 250 wamepatiwa mafunzo kuongeza ujuzi wao. “Mafunzo hayo yalifanyika kabla ya kuja kwenye kongamano hili na tumewapa mbinu ambazo wanaweza kuzitumia hata kwa kutumia vifaa vichache walivyonavyo kuweza kuokoa maisha,” alisema. | 4afya
|
Amon Mtega, Songea KAMANDA wa polisi wa Mkoa wa Ruvuma, Simon Maigwa, amesema jeshi hilo linafanya uchunguzi wa vifo viwili vya kutatanisha vilivyotokea wilayani Mbinga, ambapo katika tukio la kwanza walikuta mifupa ya mtu anayedhaniwa kuwa ni mwanafunzi na tukio la pili msichana alikutwa kwenye nyumba ya wageni akiwa amefariki dunia. Akizungumza ofisi kwake jana, alisema tukio la kwanza ni kuokotwa kwa mifupa inayodhaniwa kuwa ni ya mwanafunzi wa kidato cha pili katika Shule ya Sekondari ya Mkwaya wilaya ya Mbinga, Luth Ndunguru. Alisema tukio la kuokotwa mifupa hiyo lilitokea Mei 17 mwaka huu saa saba mchana katika kitongoji cha Tungutu Kata ya Kilimani Wilaya ya Mbinga. Kamanda huyo alisema pembeni mwa mifupa hiyo kulikuwa na nguo pamoja na daftari zilizoandikwa jina la Luth Ndunguru. Alisema taarifa za awali zilionyesha marehemu huyo aliondoka nyumbani kwao Aprili 24 mwaka huu kuelekea Kijiji cha Mkwaya kuchukua madaftari yake aliyoyaacha katika chumba alichokuwa amepanga kabla ya shule kufungwa kutokana na tatizo la ugonjwa wa Covid 19 unaosababishwa na virusi vya corona. Alisema marehemu huyo ambaye alikuwa ni mwanafunzi wa kidato cha pili katika shule ya Sekondari ya Mkwaya tangu alipotoka nyumbani kwao, hakuonekana hadi mifupa na daftari zenye jina lake zilipopatika. Kamanda Maigwa alilitaja tukio la pili kuwa ni la Saada Athuman aliyekadiriwa kuwa na miaka 25 hadi 30 kukutwa kwenye moja ya nyumba ya wageni iliyopo Mbinga mkoani Ruvuma akiwa amefariki dunia . Alitaja tukio hilo kuwa lilitokea Mei 30 mwaka huu saa saba mchana katika moja ya nyumba za wageni na kuwa marehemu alikuwa ni muhudumu wa bar iitwayo waungwana Pub. Alisema marehemu alienda kwenye nyumba hiyo akiwa na mwanaume aliyejiandikisha kwenye kitabu cha wageni kuwa ni Jakson Duma anayedaiwa kuwa ni dereva kutoka Tanga. Alisema wakalala na ilipofika saa 12: 00 asubuhi, mwanaume huyo alirudisha funguo kwa muhudumu huku mlango ukiwa umefunga kwa nje. Kamanda huyo alisema mwanaume huyo alidai anaenda kituo cha mabasi cha wilayani kuchukua gari lakini hakurudi tena. Alisema baada ya mtuhumiwa kutokomea, muhudumu wa nyumba wa nyumba hiyo aliingiwa na hofu baada ya kuona msichana hatoki chumbani hadi ilipofika saa saba mchana ndipo akaamua kutoa taarifa katika kituo cha polisi. Alisema polisi walipovunja mlango walimkuta msichana akiwa amefariki dunia huku mwili wake ukiwa kitandani na mdomoni kunatokwa na mapovu. Kamanda alisema kufuatia matukio hayo jeshi la Polisi mkoani humo linaendelea na uchunguzi ili kubaini vyanzo halisi vya vifo hivyo pamoja na kuwasaka wahusika . | 3kitaifa
|
['Mshambuliaji wa zamani wa Liverpool Daniel Sturridge ametoa ofa ya mpaka pauni 30,000 kama zawadi akirejeshewa mbwa wake.', 'Sturridge,29, ambaye ameondoka Liverpool mwezi uliopita baada ya mkataba wake kuisha amesema mbwa wake huyo aliibiwa baada ya wezi kuvunja nyumban yake jijini Los Angeles Marekani akiwa matembezini. ', 'Mchezaji huyo amepakia video kwenye mtandao wake wa Instagram akionesha jinsi nyumaba yake iliyopo eneo la West Hollywood iivyoharibiwa. ', '"Tutalipa kiasi chochote kile ili kumpata mbwa wetu," amesema Sturridge. ', '"Yoyote atakayemrudisha mbwa wangu (atapata) elfu 20, elfu 30 (pauni), kiasi chochote kile." ', 'Sturridge pia ametuma picha nne za mbwa huyo na pia video zinazoonesha wanaaume watatu waliojifunika uso wakiingia kwenye nyumba hiyo. ', 'Amesema tukio hilo limetokea alipokuwa kwenye matembezi Jumatatu usiku. ', 'Sturridge amewaambia wafuasi wake: "Yeyote anayewajua waliovunja nyumba yangu, nitakulipa utakacho. Ninamaanisha nisemacho. ', '"Nitatoa pesa yeyote ile - haijalishi thamani."', 'Sturridge, kwa saasa anahusishwa na uhamisho kuelekea klabu ya Aston Villa ambayo inarejea EPL msimu ujao utaoanza Agosti. '] | 5michezo
|
Veronica Simba – Chato WAZIRI wa Nishati, Dk. Medard Kalemani, amewasha umeme vijiji vya Rwantaba na Nyarutefye vilivyopo Chato mkoani Geita na kufanya vijiji vilivyofikiwa na nishati hiyo kufikia 114 kati ya 115 vilivyopo kwenye wilaya hiyo. Akizungumza na wananchi wa Kijiji cha Nyarutefye juzi, muda mfupi kabla ya kuwasha umeme, Dk. Kalemani alisema ifikapo mwisho wa mwezi huu, vijiji vyote vya wilaya hiyo vitakuwa na umeme. Alisema Chato haitakuwa wilaya ya kwanza kuwashiwa umeme katika vijiji vyake vyote kwani tayari kuna wilaya 34 nchini ambazo hadi sasa vijiji vyake vyote vimefikiwa na huduma ya umeme. Dk. Kalemani alisema Serikali inaendelea kuunganisha umeme vijijini nchini kote na hadi kufikia Oktoba, vijiji 10,446 kati ya 12,268 vya nchi nzima vitakuwa vimeunganishwa. “Tutabaki na vijiji 1,822 ambavyo kufikia Juni 2021 vitakuwa vimeunganishwa na kufanya vijiji vyote nchini kuwa vimefikiwa na umeme,” alisema Dk. Kalemani. Katika hatua nyingine, Dk. Kalemani aliwaasa wananchi ambao umeme umefika katika maeneo yao, kuchangamkia fursa ya kulipia na kutandaza mfumo wa nyaya katika nyumba zao ili waunganishiwe. Alisema umeme utumike kwa matumizi yenye tija zaidi, hususan kiuchumi badala ya kuutumia kuwasha taa peke yake. Akijibu hoja za baadhi ya wananchi ambao wamedai kutounganishiwa umeme licha ya kulipia huduma hiyo, Dk. Kalemani aliagiza uongozi wa Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco), kuhakikisha wanawaunganishia wote wenye changamoto ya aina hiyo katika kipindi kisichozidi siku 14. Vilevile, aliwataka watendaji hao wa Tanesco nchi nzima kuharakisha ukarabati wa miundombinu ya umeme iliyoharibika kutokana na mvua zilizokuwa zikinyesha ili kuwaondolea wananchi adha ya ukosefu wa umeme. Kwa upande wake, Mkuu wa Wilaya ya Chato, Charles Kabeho, ambaye aliambatana na waziri katika ziara hiyo, alipongeza utendaji kazi wa Serikali kwani ahadi zake zinatekelezwa na wananchi wanashuhudia. Katika ziara hiyo, Dk. Kalemani pia aliambatana na Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Tanesco, Raymond Seya, Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Wakala wa Nishati Vijijini (REA), Amos Maganga na maofisa wengine waandamizi kutoka wizarani na katika taasisi hizo. | 3kitaifa
|
Mchezo huo utachezwa Geita utavuta hisia za mashabiki wengi, kwani timu ambayo itapoteza mchezo huo itajiweka kwenye wakati mgumu wa kucheza Ligi Kuu.Geita ina pointi 24 sawa na Polisi Tabora wakitofautiana kwa idadi ya mabao ya kufunga na kufungwa, ambapo inacheza na JKT Oljoro yenye pointi 22.Endapo JKT Oljoro itashinda mchezo huo itaipita Geita kwa pointi moja, kitendo ambacho kitasababisha michezo ya mwisho kuwa migumu zaidi.Vita ya kupanda kwenye kundi C inajumuisha Polisi Tabora ambao wana pointi 24 ambao leo watakuwa wageni wa JKT Kanembwa yenye pointi tatu mchezo ambao utachezwa kwenye Uwanja wa Lake Tanganyika.Pia Polisi Mara itaikaribisha Panone FC kwenye Uwanja wa Karume, Mara, mchezo ambao hauna msisimko kwani timu Panone wana pointi 15 na Polisi pointi 12, jambo linalowatoa kwenye mbio za kuwania kupanda daraja.Kwenye kundi A, Ashanti United ambayo ina pointi 22 itacheza na KMC FC yenye pointi 2, mchezo utakaochezwa Uwanja wa Karume, Dar es Salaam na African Lyon yenye pointi 23 wanaikaribisha Polisi Dar yenye pointi 14 mchezo unaochezwa Uwanja wa Mabatini, Pwani.Timu yoyote kati ya Ashanti United, KMC FC, African Lyon endapo itapoteza mchezo leo itajiweka pabaya kwenye mbio za kupanda Ligi Kuu msimu ujao.Michezo mingine kundi A itachezwa kesho ambapo Friends Rangers itaialika Mji Mkuu kwenye Uwanja wa Karume, Dar es Salaam na Kiluvya United dhidi ya Polisi Dodoma kwenye Uwanja wa Mabatini Pwani Michezo mingine ambayo ni ya kukamilisha ratiba itakayochezwa leo ni ya kundi B, kwani Ruvu Shooting walishapanda ni kati ya Polisi Morogoro itakayoikaribisha Njombe Mji kwenye Uwanja wa Jamhuri Morogoro.Kurugenzi FC wataikaribisha JKT Mlale, Burkinafaso FC wataialika Lipuli FC na Kimondo FC wataikaribisha Ruvu Shooting huko Vwawa Mbozi. | 5michezo
|
MWANDISHI WETU -DAR ES SALAAM MKUU wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda, amemuomba Rais
Dk. John Magufuli kuwapatia JWTZ mradi wa ujenzi wa Nyumba za NSSF zilizopo Kata
ya Toangoma ambazo ujenzi wake umesuasua zaidi ya miaka 15, jambo
linaloisababishia serikali hasara. Makonda amesema anaamini kwa utendaji kazi wa vijana wa
JWTZ, utawezesha majengo hayo kukamilika ndani ya muda mfupi na kuanza
kutumiwa. Hatua hiyo imekuja baada ya Makonda kuendelea na ziara ya
ukaguzi wa miradi ya maendeleo, ambapo jana ilikuwa zamu ya ukaguzi wa
maendeleo ya ujenzi wa majengo 12 ya magereza Ukonga, ambayo hivi karibuni Rais
Magufuli aliwanyang’anya Wakala wa Majengo nchini (TBA) baada ya kusuasua na
kuwakabidhi JWTZ, ambapo sasa ujenzi unakwenda vizuri. Kutokana na hayo, Makonda pia amewapongeza JWTZ kwa kasi
kubwa wanayoonyesha katika mradi huo na kueleza kuwa anaamini watakamilisha
ujenzi ndani ya muda uliokusudiwa. Kwa upande wa msimamizi wa ujenzi huo, Brigedia Charles
Mbuge, amesema ujenzi wa majengo hayo utakamilika na kukabidhiwa ndani ya miezi
miwili na nusu. Wakati huo huo, Makonda ameshangazwa na malipo makubwa
yanayofanywa katika miradi ya DMDP, akiwataka
Takukuru kuanza uchunguzi mara moja. Amemwagiza Mkurugenzi wa
Takukuru Mkoa wa Dar es Salaam kufanya uchunguzi wa utaratibu wa
upatikanaji wa tenda kwenye miradi ya DMDP. “Haiwezekani kilomita moja ya barabara ya DMDP Wilaya
ya Kinondoni inajengwa kwa shilingi bilioni 2.7, wakati kwa Wilaya ya Temeke
barabara kama hiyo inajengwa kwa shilingi milioni 900,” alisema. Makonda amebaini madudu hayo wakati wa mwendelezo wa ziara
yake ya ukaguzi wa miradi ya maendeleo kupitia fedha zinazotoka Serikali Kuu,
Halmashauri na fedha za wahisani, ambapo amekwazwa na matumizi mabaya ya fedha
za mkopo kutoka Benki ya Dunia. “Barabara za DMDP zimekuwa zikijengwa kwa kiasi
kikubwa cha pesa kuliko zile za Tanroads ambazo kwanza zina ubora mkubwa, uwezo
wa kubeba mzigo mkubwa na pia ni pana, katika miradi ya ujenzi wa barabara,
hospitali na shule nawapongeza Manispaa ya Temeke kwa kazi nzuri na kusimamia
vizuri miradi ya maendeleo, niwaombe muongeze bidii na kasi,” alisema
Makonda. | 3kitaifa
|
NA PATRICIA KIMELEMETA – PWANI
MBUNGE wa Chalinze, mkoani Pwani, Ridhiwani Kikwete, ameahidi kushughulikia tatizo la maji linalowakabili wananchi wa jimbo hilo.
Ridhiwani alisema mkakati uliopo ni kuhakikisha anasimamia upatikanaji wa maji kutoka Mto Wami na kuongeza idadi ya visima ili wananchi wa jimbo hilo waweze kupata huduma hiyo.
Alisema mbali na uhaba mkubwa katika baadhi ya maeneo, kukatika kwa maji mara kwa mara, ni tatizo jingine linalokera wananchi wa Chalinze.
Ridhiwani alisema mkakati aliokuwa nao awali umewezesha kuchimba visima katika vijiji mbalimbali jimboni humo ili kupunguza ukubwa wa tatizo.
“Tangu niingie madarakani, nimeweza kuchimba visima katika vijiji mbalimbali ili kupunguza ukubwa wa tatizo, jambo ambalo limechangia wananchi walio pembezoni na makao makuu ya halmashauri kutokuwa na shida kubwa ya maji kama ilivyokuwa awali,” alisema Ridhiwani.
Baadhi ya wakazi wa Halmashauri ya Chalinze wameitaka Serikali kushughulikia kero ya maji ili waepukane na adha ya kutembea umbali mrefu kutafuta maji.
“Chalinze tuna tatizo sugu la upatikanaji wa huduma ya maji safi na salama kwa miaka mingi, hali iliyosababisha kwenda umbali mrefu kutafuta maji katika marambo au mabwawa ili tuweze kutumia,” alisema Amina Semindu.
Alisema licha ya kuwapo Idara ya Maji ya Mto Wami, lakini mashine ya kusukuma maji imekuwa ikiharibika mara kwa mara, jambo ambalo limechangia wananchi kuendelea kutaabika na huduma hiyo muhimu.
Mkazi mwingine wa eneo hilo, Abdallah Omary, alisema kuwa Serikali inapaswa kuangalia sababu ya kuharibika mara kwa mara kwa mitambo ya kusukuma maji.
“Pale Idara ya Maji kuna tatizo… kwa sababu kila siku mashine zinaharibika jambo ambalo limesababisha wananchi kuendelea kutaabika na huduma hiyo… Tunaiomba Serikali kutumia jicho lake ili waweze kujua chanzo cha tatizo,” alisema Omary. | 3kitaifa
|
Msaani wa Bongo Fleva Harmonize amefunguka kuhusu uamzi wake wa kuandika ujumbe mrefu na mizto kumkingia kifua msanii mwenzake Rich Mavoko baada ya kupotea katika game kwa siku kadhaa. Hata hivyo Hramozi amesema yeye nia Mavoko licha ya kuw apmoja WCB siku za nyuma, hawakuwahi kuwa washikaji lakini alivutia na msanii huyo kuingia katika tasnia. “Nilikuwa tu najaribu kuelezea feelings zangu kuhusu Rich, nitakuwa muongo nikisema sioni kinachoendelea kuzungumzwa kuhusu yeye! Sijabahatika kuwa mmoja kati ya watu wa karibu wa Mavoko lakini yeye nimmoja kati ya watu ambao wamenifanya mimi niingie kwenye muziki” Alisema anaumizwa sana anapoona kuna baadhi ya watu wanafurahishwa na kuandika mitandaoni kwamba eti amepotea kimziki na mambo mengine. Familia Ngapi Zipo Nyuma Ya @richmavoko ..?? Na zinamtegemea Yeye KwaKila Jambo Hasa Hili La Kupata Mkate Wa Kilasiku VP Kuhusu Ndoto Za Familia Hizo Na Zinaishije Katikwa Wakati Huu…??? . Ndoto Ngapi Za Wasani Ambao Wanategemea Kuzifikia Hizo Ndoto Kupitia Mavoco ..?? Na Nyuma Ya Hao Wasanii Kuna Familia NyenginePia ..?? . Jeee Maumivu Malala Miko Ya Wazazi Wake Hasa Mama Mzazi Ambae Ndio Kama Roho Yake …!!! Ushajiuliza Ni Kauli Ngapi Za Uchungu Anazitoa Ambazo Zinaweza Kumpata Kila Anaefurahishwa Na Hili Kwa Makusudi ..??? . Mana Mzazi wa Mwenzio Ni wako Pia Laana Yake Haishindwi Kukupata …!! La Mwisho Kabisa Mgeukie Mwenzio Anaefurahia Na Kuifanya Hii Kuwa Ni Habari Njema Kwake Ya Kumfanya Atembee Kifua Mbele Na Hata Kuandika Mtandaoni Kwa Furaha MAVOCO KAPOTEA muulize Anafaidika Nanini …??? . Mungu Anasababu Na Maana Yake Bro @richimavoco Kama Mdogoako Nakuombea Najua Ukimya Wako Unamaana Kubwa Sanaa Ndani Yako Ninachojua Ni Kujiweka Sawa Na Kutuletea Kazi Zingine Tunakupenda Na Tunakuombea Mungu Akufanyie Wepesi…!!! Let's Go Bro Mdogoako Rafiki Yako Nipo Hapa Muda Wowote…!!!! RAMADAN KAREEM A post shared by KONDEBOY (@harmonize_tz) on May 5, 2020 at 10:20pm PDT | 0burudani
|
Na RAMADHAN HASSAN-DODOMA
WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amewataka wakuu wa wilaya wakurugenzi wa halmashauri nchini kuzingatia mipaka ya madaraka yao na kuhakikisha hatua wanazochukua katika utendaji wao zinafuata sheria, kanuni na taratibu katika utumishi wa umma.
Kauli hiyo aliitoa jana mjini hapa wakati akifungua mafunzo kwa wakuu wa wilaya na wakurugenzi wa halmashauri za wilaya.
Alisema viongozi hao wanatakiwa kusimamia kwa ukamilifu nidhamu katika utumishi wa umma kwa sababu wenyewe ni kioo katika kuishi kwa kuzingatia miiko ya utumishi.
Alisema mafunzo hayo yanalenga kuwajengea uwezo na kuendelea kuwaimarisha zaidi katika kusimamia shughuli za Serikali na maendeleo kwenye maeneo yao.
Waziri Mkuu pia amewataka viongozi hao kutoa kipaumbelea katika kufuatilia na kusimamia kwa makini sekta za afya, kilimo, elimu na maji kwa kuwa ndizo zinazogusa zaidi maisha ya wananchi .
“Simamieni na kuziba mianya yote ya upotevu wa dawa katika vituo vya kutolea huduma za afya na kudhibiti migogoro ya wakulima na wafugaji na kusimamia usafi na utunzaji wa mazingira katika maeneo yenu,” alisema.
Naye Naibu Waziri Nchi, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa-TAMISEMI, Suleiman Jafo alisema lengo la mafunzo hayo ni kuhakikisha viongozi hao wanapata mafanikio makubwa katika utendaji wao wa kazi Serikali iweze kupata tija.
Awali, Ofisa Mtendaji Mkuu wa Taasisi ya Uongozi, Profesa Joseph Semboja, alisema mafunzo hayo yametolewa kwa viongozi hao kuwajengea uwezo wa kuongoza kwa kuwa mazingira ya kufanyia kazi na mbinu za kungoza zinabadilika.
Alisema mafunzo hayo yatatolewa kwa awamu nne kupitia kanda nne tofauti ambako awamu ya kwanza imeanza na kanda ya kati na imehusisha mikoa sita ya Dodoma, Kigoma, Katavi, Tabora, Morogoro na Singida | 3kitaifa
|
WAKATI kikosi cha timu ya soka ya Tanzania, Taifa Stars, kikiendelea kujifua vilivyo nchini Misri baada ya kupata mechi mbili za majaribio dhidi ya wenyeji Misri na Zimbabwe kabla ya kuingia rasmi kwenye fainali hizo ambazo wanatarajia kushiriki kwa mara ya pili tangu walipofanya hivyo miaka 39 iliyopita.Taifa Stars iliposhiriki mara ya mwisho mwaka 1980 iliishia katika hatua ya makundi, hivyo mwaka huu ina kibarua cha kuhakikisha inavunja rekodi yake kwa kufuzu kwa hatua ya pili, ambayo ni 16 bora.Michuano hiyo ilianza kutimua vumbi jana, huku Taifa Stars ikitarajia kuanza kutupa karata zake kesho kwa mchezo dhidi ya vigogo vya Afrika, Senegal. Misri imekuwa mwenyeji wa mashindano hayo baada ya kupokwa kwa Cameroon kutokana na kushindwa kukamilisha maandalizi kwa wakati. Cameroon pia ndio mabingwa watetezi wa taji hilo.MIAKA 39 SASABaada ya kushiriki kwa mara ya mwisho fainali za Afcon mwaka 1980, imechukua takribani miaka 39 kwa Tanzania kurejea katika fainali za mashindano hayo, ambayo sasa hufanyika kila baada ya miaka miwili.Taifa Stars ilibuku nafasi ya kwenda Misri kwa staili ya aina yake baada ya kuwafunga majirani zao Uganda, The Cranes kwa mabao 3-0 siku ya mwisho ya mechi za makundi, katika mchezo uliopigwa kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.Katika fainali hizo za mwaka 1980 nchini Nigeria, Tanzania haikushinda mchezo hata mmoja katika hatua hiyo ya makundi, na ilimaliza katika nafasi ya mwisho ikiambulia pointi moja baada ya kutoka sare mechi moja na kufungwa mbili.Tanzania ilikuwa moja ya timu za mwisho kufuzu kwa fainali hizi za Afcon 2019 katika mchezo ulipigwa Machi 24 mwaka huu. Sasa Taifa Stars inaangalia kuvunja rekodi yake ya mwaka 1980 ya kucheza hatua ya makundi na ikivuka tu na kucheza hatua ya 16 bora, ndoto ya kocha Amunike itakuwa imetimia.Kikosi cha Stars kiliondoka nchini kikiwa na msafara wa wachezaji 32, ambapo kupitia mechi hizo za kirafiki wachezaji hao walichujwa na kubaki 23, idadi ambayo itahudumiwa na Shirikisho la Soka Afrika, Caf. KUPAMBANA STARS Wachezaji hao ni wazi wana kila sababu ya kupambana kwa jasho na damu kuhakikisha wanaipeperusha bendera vyema na kuwatoa kimasomaso Watanzania zaidi ya milini 50.Watanzania wana imani kubwa na kikosi hicho, lakini naweza kusema hicho nikipimo tosha kwa kocha wa kikosi hicho, Emmanuel Amunike kuwaonesha na kuwaaminisha watu waliokuwa na mtizamo hasi juu huku wakihoji uwezo na kazi hiyo.Kikosi hicho kimekita kambi nchini Misri baada ya kuridhishwa na miundombinu ya matayarisho ya wachezaji yatakayochangia wachezaji kupata morali na ari ya kufanya vizuri katika michezo ya kundi lao kisha kutinga hatua inayofuata.Taifa Stars wamepangwa Kundi C pamoja na majirani zao Kenya na timu vigogo Senegal na Algeria ambazo zimefanya uwekezaji mkubwa kwenye soka la vijana na wamepata uzoefu wa kushiriki mara nyingi michuano hiyo.Kombe la Mataifa ya Afrika (Afcon) kwa ufupi ni shindano kubwa lililoanzishwa mwaka 1957 lakini tangu mwaka 1968, fainali hizo zilikuwa zinafanyika kila baada ya miaka miwili makala haya yanakuletea uchambuzi mdogo kwa mataifa yaliyotwaa taji hilo mara nyingi na wachezaji waliofunga mabao mengi.MISRIMisri ndiyo taifa pekee lenye rekodi na historia kubwa ya kutwaa taji la michuano hiyo mara saba na kuyazidi mataifa mengine yaliyopata kushiriki kwa nyakati tofauti. Mafarao hao kwa mara ya kwanza walitwaa mwaka 1957, 1959, 1986, 1998, 2006, 2008 na 2010.GHANA NA CAMEROONMataifa hayo yanafuatia kwa kushika nafasi ya pili kwa kutwaa taji hilo mara nyingi baada ya Ghana walitwaa miaka ya 1969, 1965, 1978, huku Cameroon wakianza mwaka 1984, 1988, 2000 na 2002 na 1982.WABABE NIGERIAKitabu cha kumbukumbu kinaonesha Nigeria wanashika nafasi ya tatu, wamelitwaa taji hilo mara tatu, ikiwa ni mwaka 1980, 1994 na 2013.DR CONGO, IVORY COASTWanashika nafasi ya nne huku kila mmoja wao akiwa amechukua mara mbili, ambapo Congo wamechukua miaka ya 1968 na 1974 wakati Ivory Coast 1992 na 2015.WALIOFUNGA MABAO MENGIWachezaji 10 waliopata kutikisa kwenye michuano hiyo kwa kufunga mabao mengi na wanazidi kubaki kwenye kumbukumbu ya kitabu cha michuano hiyo mikubwa barani Afrika, Caf.Samuel Eto’o mshambuliaji na raia timu ya taifa ya Cameroon anashikilia uongozi kwa kufunga mabao 18, Laurent Pokou raia wa Ivory Coast ametumbukia nyavuni mara 14 akifuatiwa na Rashid Yekini raia wa Nigeria amefunga mabao 13. Wengine ni Hassan Shazly (Misri) 12, Hossam Hassan (Misri) 11, Ndaye Mulamba (Dr Congo) 10, Didier Drogba (Ivory Coast) 10, Joel Tieh (Ivory Coast) 10, Kalusha Bwalya (Zambia) 10. | 5michezo
|
Yanga inatarajiwa kuondoka kesho kuifuata USM Alger ya Algeria kwa ajili ya mchezo wa makundi wa michuano ya Kombe la Shirikisho Afrika utakaochezwa mjini Algiers mwishoni mwa wiki hii.Akizungumza na gazeti hili, Nsajigwa alisema wanajua wanakwenda kukutana na timu kubwa na ngumu, wanajipanga kuhakikisha wanaanza vizuri.“USM Alger ni miongoni mwa timu kubwa Afrika, tunawaheshimu na tunakwenda tukijua wazi hautakuwa mchezo rahisi, kikubwa kwetu ni kujipanga kufanya vizuri,” alisema.Timu hiyo ya Jangwani inakwenda kwenye mechi hiyo ikiwa imetoka kupoteza mechi ya ligi dhidi ya mtani wake wa jadi Simba kwa bao 1-0.Mwishoni mwa wiki iliyopita na Nsajigwa alisema hayo yameshapita wanachoangalia ni michuano hiyo ya kimataifa.Kitendo cha kupoteza mchezo huo ni kama wamejiondoa kwenye mbio za ubingwa dhidi ya vinara Simba iliyowaacha mbali kwa tofauti ya pointi 14.Kikosi cha Yanga tayari kilianza mazoezi tangu juzi kujiandaa na mchezo ambapo kesho kitaanza safari kwa shirika la ndege la Emirates kupitia Dubai.USM Alger iliwahi kufika fainali mwaka 2015 katika mchezo wa Ligi ya Mabingwa Afrika ambapo ilifungwa kwao na TP Mazembe hivyo, ni mchezo unaotazamwa kuwa wenye upinzani mkali.Baada ya mchezo huo, Yanga itarudi Dar es Salaam kuwasubiri Rayon Sport ya Rwanda Mei 16, mwaka huu kisha itakwenda ugenini Julai 18, mwaka huu, kuvaana na Gor Mahia ya Kenya. | 5michezo
|
Tunu Nassoro-Dar es Salaam RAIS Mstaafu Jakaya Kikwete, amesema cheo alichokuwanacho Mkurugenzi Mkuu mstaafu wa Usalama wa Taifa, marehemu
Apson Mwang’onda, hakikumpa jeuri na kiburi. Akitoa salamu za rambirambi katika ibada ya kuuaga mwili wa Mwang’onda
iliyofanyika katika kanisa la Mtakatifu Petro jijini Dar es Salaam, Kikwete
alisema mzee Apson alikuwa ni mkweli mwenye nidhamu na weledi wa hali ya juu. Alisema Mwang’onda aliipenda kazi yake na kuifanya kwa ujasiri na moyo
na kwa bidii zote. “Alitimiza wajibu wake ikiwa ni pamoja na kushari mambo kadhaa ya
namna bora ya kuendesha nchi na hivyo kuwa kiungo muhimu katika uongozi,”
alisema Kikwete. Alisema alikuwa akiikosoa Serikali
katika mambo mbayo imeteleza kwa kueleza kwa uwazi kilichokosewa. “Alikuwa akinikosoa kila
tulipokosea na kuniambia kuwa Serikali yako imefanya makosa haya, wala hakuwa
na uoga,” alisema Kikwete. Aliongeza alipoingia madarakani, Mwang’onda alimwambia yeye na wenzake
watakuwa wakimshauri katika kutekeleza majukumu yake hivyo awe tayari kupokea ushauri
hata kama utakuwa mbaya najiandae kuupokea. “Nashukuru aliniandaa kisaikolojia kwani hata aliponiletea taarifa
mbaya niliisoma na bahati nzuri alikuwa muungwana na ikiwa kubwa sana tulikaa wote
na kujadiliana,” alisema Kikwete. Alisema alimwomba amvumilie wakati wa kutekeleza majukumu yake ya kila
siku katika idara hiyo. Kikwete alisema hata Mwang’onda alipotaka kustaafu, alimwomba
kumwongeza muda ili aweze kuendelea kufanya naye kazi. “Alikubali na nilipotaka kumwongeza tena, alikataa na kusema anahitaji
kustaafu na kuwaachia wengine. Alisema mwisho wake walio nyuma yake ambao
wangeshika nafasi yake watastaafu yeye akiwa madarakani na hivyo kulazimika
tuchukue wadogo zaidi wasio na uzoefu wa kuongoza,” alisema Kikwete. Alisema marekemu ameacha alama katika taifa hasa mipango yake ya
kuboresha na kuiendeleza idara ya usalama nchini. Naye Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi na usalama mstaafu (CDF), George
Waitara, alisema Mwang’onda alikuwa na ushirikiano mkubwa katika utendaji kazi
wake. Alisema walitengeneza ushirikiano wa watu watatu ambao walikuwa ni
wakuu wa vyombo vya ulinzi na usalama. “Katika ushirikiano wetu hatukuwa wanafiki wala wajeuri, tulifanya
kazi kwa pamoja na hata tulipokutana tulijadili kuhusu amani ya nchi,” alisema
Waitara. Alisema Mwang’onda alikuwa ni msema ukweli hakusita kukosoa pale
alipoona mambo hayaendi sawa. “Hata alipostaafu alikuwa akiona jambo halijakaa vizuri aliniita na
kunieleza huku akitoa ushauri katika masuala muhimu,” alisema Waitara. Kwa upande wake Mkuu wa Jeshi la Polisi Mstaafu, Omary Mahita alisema
walifanya kazi na Mwang’onga kwa zaidi ya miaka 23 ambapo miaka 10 wakiwa ni
viongozi wa vyombo vya ulinzi na usalama. Alisema walitekeleza mambo
mbalimbali ya ulinzi na usalama wakiwa na ushirikiano wa watu watatu, Waitara,
mwang’onda na yeye. “Mwang’onda alitekeleza majukumu yake kwa mawazo na vitendo hivyo
kuturahisishia na sisi kazi zetu,” alisema Mahita. Alisema alikuwa akitoa ushauri kwa viongozi wa nchi bila kuwa na woga na kutoa mwongozo na mawazo
yake kiungwana. “Binafsi nitamkumbuka kwa kuwa tulikuwa tukisaidiana katika mambo
mbalimbali ya kijamii hasa pale nilipofiwa na baba yangu alinisaidia
kusafirisha maiti kwenda Morogoro kwa maziko. Katika msiba huo Katibu Mkuu mstaafu wa Chama cha Mapinduzi(CCM),
Abdurahman Kinana, alikuwa kivutio kwa wanahabari baada ya kutokuonekana kwa
muda mrefu baada ya kutoa waraka uliokuwa ukiikosoa Serikali. Waandishi wa habari walitaka kujua alikokuwa baada ya kutoa waraka huo
huku wakimsonga ingawa hakuwa tayari kuzungumza. Mwili wa Mwang’onda ulisafirishwa jana kwa ndege maalumu kuelekea
Kijiji cha Old Vwawa ambako utafanyiwa maziko leo. Marehemu ameacha mjane na
watoto watano. | 3kitaifa
|
WANAFUNZI wa shule za msingi na sekondari wapatao 304 wamekatisha masomo yao kutokana na mimba ndani ya kipindi cha miezi 12 mkoani Dodoma.Hayo yamebainishwa na Ofisa Elimu Mkoa wa Dodoma, Maria Lyimo wakati wa kuwasilisha taarifa ya maendeleo mkoa na hatua za kuinua ufaulu na nafasi ya mkoa kwenye Kikao cha Kamati ya Ushauri ya Mkoa (RCC).Lyimo alisema mimba kwa wanafunzi ni moja ya changamoto zinazokabili maendeleo ya elimu mkoani Dodoma na kuwa kuanzia Januari hadi Desemba mwaka huu, wanafuzi 67 wa shule za msingi na 237 wa sekondari wameachishwa masomo kutokana na kupata mimba.Alisema changamoto nyingine ni utoro wa wanafunzi.Akitolea mfano, Lyimo alisema asilimia saba ya wanafunzi wa shule za msingi kuanzia darasa la kwanza hadi la saba na asilimia sita ya wanafunzi wa sekondari kuanzia kidato cha kwanza hadi cha nne wamekosa masomo kuanzia Januari hadi Desemba kwa mwaka huu kutokana na utoro.Katika kukabiliana na tatizo la mimba na utoro, alisema wameweka mkakati wa kudhibiti hali hiyo kwenye ngazi ya halmashauri kwa kuwashirikisha wakurugenzi wa halmashauri, wakuu wa wilaya na vyombo vya usalama katika kuchukua hatua kwa wakati na kuzingatia sheria.Akitolea mfano walivyojifunza kwa mikoa ya Arusha na Kilimanjaro, amesema mikoa hiyo utoro unadhibitiwa na ofisi ya mkuu wa wilaya kwa kuwahusisha na kuwatumia maofisa tarafa na watendaji wa kata na walimu wakuu.“Kwa upande wa Dodoma kushughulikia changamoto hiyo sio wa kuridhisha, kwa mfano mwaka huu katika shule za sekondari mimba 237 zimeripotiwa, 155 zipo ngazi ya kata, 68 zipo polisi na 11 zipo mahakamani na ni kesi tatu tu za mimba zilizotolewa hukumu, hii inaashiria kuna ulegevu katika ushughulikiaji wa kesi za mimba hivyo kusababisha wanafunzi wengi wa kike kuachishwa shule,” amesema.Alisema mpango wa Mkoa wa Dodoma kwa mwaka 2020 ni kufaulisha wanafunzi kwa asilimia 90 kutoka asilimia 74.69 ya mwaka 2019 kwa mitihani ya shule za msingi, kidato cha nne kwa zaidi ya asilimia 50 kwa daraja la I-III na kidato cha sita ufaulu wa asilimia 100 kwa wanafunzi kupata daraja la I-III.Aidha, Kamati ya RCC kwa kauli moja ilipitisha azimio la kuundwa kamati ya mkoa ya kufuatilia maendeleo ya elimu kwa mkoa mzima. | 3kitaifa
|
WATU sita wamefariki dunia na wengine wawili kati ya 12 kujeruhiwa wakiwa katika Chumba cha Uangalizi Maalumu (ICU) kwa ajili ya uangalizi wa karibu baada ya lori lililokuwa likikwepa shimo kuhama na kuigonga Toyota Coaster usiku wa kuamkia jana jijini hapa.Akizungumza jana jijini hapa, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma, Gilles Muroto aliwataja waliofariki kuwa ni Omary Mdilo, Prisca Mbaigwa, Gihali Chilangazi, Simon Mtagwa na Shukuru Ruvuwesh.Maiti moja haijatambuliwa. Akielezea ajali hiyo iliyotokea eneo la Martin Luther katika Manispaa ya Jiji la Dodoma, Kamanda Muroto alisema ilitokea baada ya dereva wa lori lenye namba za usajili T 364 AZZ kuhama, akikwepa shimo na kwenda kukutana na Toyota Coaster yenye namba za usajili T 846 AYU iliyokuwa kwenye njia yake.“Huyu dereva wa lori alikuwa anakwepa shimo na gari yake ikahama na kwenda kulivaa Coaster iliyokuwa site yake na kufumua rufu ya nyuma ya Coaster na kupeleka kutokea ajali hiyo iliyopoteza uhai wa watu sita,” alisema.Alisema majeruhi 12 waliofikishwa na kulazwa katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa na kati ya hao wanawake ni watatu na wanaume tisa, huku majeruhi wawili hali wako ICU. Aidha, Kamanda Muroto alisema baada ya ajali hiyo dereva wa lori aina ya Fuso, Joseph Zacharia (26) aliyekuwa ametoweka baada ya ajali, anashikiliwa na Polisi baada ya kumpata.“Ukiangalia utokeaji wa ajali, dereva wa Coaster hana makosa kwa sababu alikuwa katika site yake na lori likamfuata na kufumua rufu ya nyuma ya Coaster hiyo. Hivyo madereva wanapaswa kuwa makini na sheria za barabarani na sio kujidanganya kuwa msimu wa sikukuu kuna ajali nyingi, kitu ambacho sio kweli huku madereva wakiwa sehemuya kusababisha ajali hizo,” alisema Kamanda Muroto.Naye Muuguzi Mfawidhi wa Hospital ya Rufaa ya Mkoa wa Dodoma, Stanlay Mahundo alisema wamepokea majeruhi 12 na maiti sita wakiwamo wanaume watano na mwanamke mmoja.Mahundo alisema kati ya hao tayari maiti watano zimeshatambuliwa na ndugu zao ikibakia maiti moja.“Majeruhi hao wanaendelea vizuri tofauti na hali walizokuja nazo jana na hali kama inatendekea vizuri basi wengine tunatarajia waruhusiwe kesho (leo) kutokana na hali zao kuendelea kuimarika,” alisema.Aidha, alisema majeruhi wawili wengine ambao wapo ICU, nao hali zao sio mbaya sana na wanaendelea vizuri kutokana na huduma ambazo wamepatiwa. Muuguzi Khadija Ikaji alisema majeruhi ambao wamefanyiwa upasuaji mdogo, wanaendelea vizuri na kuruhusiwa kwao kutategemea na hali zao zitakavyozidi kuimarika. Mmoja wa majeruhi, Godfrey Kilimo ambaye ni mkazi wa Nzuguni alisema hakuona kilichotokea ila alisikia watu wakisema “wasaidieni hao bado wako hai.”“Sikujua nini kinaendelea, nilichosikia ni sauti za watu wakisema ‘wasaidieni hao bado wazima.’ Baada ya muda nilipoteza fahamu na nilipozinduka nilijikuta niko hospitali nimefungwa bandeji kichwani.“Nawashukuru sana madaktari wa hospitali hii wamefanya kazi kubwa ya kutupa huduma ili kuhakikisha tunarudi katika hali zetu,” alisema Kilimo.Shukuru Stephen pia mkazi wa Nzuguni, ambaye ni dereva wa bajaji alisema “kwa kweli sijui chochote katika ajali hii kwa sababu nilikuwa nimepitiwa na usingizi.” Kwa upande wa Diwani wa Nzuguni, Aloyce Luhega alisema ajali hiyo imeleta msiba mkubwa katika eneo hilo na kuwataka wananchi kuwa watulivu katika kipindi hiki kigumu. | 3kitaifa
|
NA ABDUCADO EMMANUEL, DAR ES SALAAM UONGOZI wa timu ya Yanga ulikuwa na kikao kizito na wenyeviti wa matawi ya klabu hiyo, moja ya hoja iliyojadiliwa ni baadhi ya wachezaji wao kudaiwa kuwa ni mamluki wa watani zao Simba. Kikao hicho kimefanyika siku chache mara baada ya Yanga kufungwa bao 1-0 dhidi ya mtani wake, Simba kwenye mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom, huku baadhi ya wachezaji wakihusishwa kuihujumu timu yao na kupelekea kila mara kushindwa kuwafunga wekundu hao. Baadhi ya wachezaji wanaotuhumiwa ni mabeki Kelvin Yondani na Mbuyu Twite, viungo Haruna Niyonzima na Simon Msuva na kipa Ally Mustafa ‘Barthez’, ambao wanadaiwa kuwa na mapenzi na Simba. Akizungumza jijini Dar es Salaam jana mara baada ya kikao hicho kilichofanyika Makao Makuu ya timu hiyo Mtaa wa Jangwani, Makamu Mwenyekiti wa Yanga, Clement Sanga, alisema wameshauriwa na viongozi wa matawi kubadilisha mfumo wao wa usajili ili kuweza kuwafunga Simba kwenye mechi zijazo. “Siwezi nikasema kuna mchezaji alihujumu timu, tulifungwa mabao rahisi tulipocheza na BDF XI kule Botswana, lakini mabao kama yale tukifungwa kwenye mechi ya Simba au Azam inakuwa tatizo, bao lile tulilofungwa lilikuwa la kimchezo na hakuna sababu ya hujuma. Ila kwenye kikao tulichokaa leo, viongozi wametushauri tubadilishe mfumo wetu wa usajili ili kuwa na njia sahihi ya kusajili wachezaji,” alisema. Sanga alisema katika kikao hicho viongozi wa matawi wameomba wanachama wa timu hiyo na uongozi kwa ujumla kusahau yaliyopita ya kufungwa na Simba na kuunganisha nguvu kuelekea mchezo wao wa Jumapili hii dhidi ya Platinum, ikwemo kutwaa ubingwa wa Ligi Kuu. | 5michezo
|
MAMLAKA ya Mapato Tanzania (TRA) imewataka wafanyabiashara na walipakodi nchini kutumia vizuri siku mbili zilizobaki kuwasilisha maombi yao ili wapate msamaha wa riba na adhabu.Mkurugenzi wa Huduma na Elimu kwa Mlipa Kodi wa Mamlaka hiyo, Richard Kayombo alisema jana kuwa licha ya mwitikio wa wafanyabiashara hao kuwa mzuri, lakini akatoa wito kwa wale ambao hawajawasilisha maombi yao, wafanye hivyo ikiwa wanataka kupata msamaha huo. Kayombo alisema kuwa wafanyabiashara ambao waliwasilisha maombi yao mapema tangu walipotakiwa kufanya hivyo mwezi Julai mwaka huu, tayari wameshapokea majibu ya maombi yao ya kusamehewa riba na adhabu.“Hakuna adhabu kwa wafanyabiashara na walipakodi watakaoshindwa kuwasilisha maombi yao TRA katika muda waliopewa, ila wajue kwamba kwa kushindwa kufanya hivyo, riba na adhabu ambazo walipaswa kusamehewa, ziko palepale,”alieleza Kayombo. Kwa mujibu wa Kayombo, wafanyabiashara na walipakodi watakaowasilisha maombi yao mpaka ifikapo Novemba 30 mwaka huu, watapata majibu ya maombi yao ndani ya mwezi mmoja.Hatua hiyo ya wafanyabiashara na walipa kodi kujitokeza kwa wingi inatokana na maamuzi ya Serikali kupitia TRA, kutangaza mwezi Julai mwaka huu msamaha wa riba na adhabu kwa wafanyabiashara na walipa kodi wote nchini.Msamaha huo unatokana na mabadiliko ya Sheria ya Kodi ya Mwaka 2015 yaliyofanywa na Bunge kwa kuingiza kipengele kinachompa mamlaka Kamishna Mkuu wa TRA kuweza kusamehe riba na adhabu zinazohusu kodi.Mkurugenzi huyo wa Huduma na Elimu kwa Mlipa Kodi wa TRA, aliwahi kueleza HabariLeo kuwa wafanyabiashara na walipakodi hao wanapaswa kuwa na nyaraka muhimu wakati wa kuwasilisha maombi yao zitakazowawezesha kupata msamaha huo. Agosti 14 mwaka huu, TRA ilikutana na wafanyabiashara na walipakodi jijini Dar es Salaam kwa ajili ya kutoa elimu ya kodi kwa umma wa wafanyabiashara na walipakodi nchini.Kamishna Mkuu wa TRA, Charles Kichere, ambaye aliwakilishwa kwenye semina hiyo na Kaimu Kamishna wa Idara ya Walipakodi Wakubwa, Alfred Mregi alisema kuwa msamaha huo wa riba na adhabu unahusu malimbikizo ya kodi zilizokuwepo huko nyuma.Kutokana na msamaha huo, wafanyabiashara na walipakodi watatakiwa kulipa tu kodi walizokuwa wakidaiwa pasipo riba na adhabu walizopaswa kuzilipa pamoja na kodi hizo. TRA ilisema kuwa nia ya msamaha huo maalumu ni kuwasaidia walipakodi na wafanyabiashara kuweza kuinua kiwango chao cha ulipaji kodi kwa hiari, na mara baada ya utaratibu huo maalumu kuisha, utaratibu wa zamani utaendelea kutumika. Kwa mujibu wa TRA, kupitia msamaha huo, mamlaka hiyo inatarajia kukusanya Sh bilioni 500. | 3kitaifa
|
RIPOTI ya Shirika la Kimataifa la Kupambana na Ufisadi, Transparency International, limesema mataifa yaliyopo chini ya Jangwa la Sahara barani Afrika yanaongoza kwa ufisadi ulimwenguni. Hali hiyo inaelezwa kutokea baada ya mataifa mengi kukokota juhudi zao zinapolikabili suala la ufisadi. Kwenye ripoti yake ya mwaka 2017, shirika hilo limesema limegundua maelezo yenye wasiwasi. Kaulimbiu ya Umoja wa Afrika ya mwaka huu ni; ‘Kushinda vita dhidi ya ufisadi, njia endelevu ya kubadilisha Afrika’. Ripoti hiyo inaonesha mabadiliko na kutoa matumaini kwa mataifa ya Afrika. Mabadiliko katika mataifa ya Rwanda na Cape Verde yanaonesha kuwa ufisadi unaweza kudhibitiwa pakiwa na juhudi na nia njema. Matunda ya vita ya muda mrefu katika mataifa kama vile Cote d’ Ivore na Senegal yanaonekana. Kwa upande mwingine vita dhidi ya ufisadi katika mataifa yaliyo chini ya orodha ya Shirika la Transparency International, kunaonyesha kuwa kibarua kigumu kwa mfano katika mataifa ya Sudan Kusini na Somalia. Licha ya kuwa Afrika ina mataifa mengi ambayo yanakabiliwa na ufisadi, kuna baadhi ya mataifa yanayopiga hatua kama vile Botswana, Shelisheli, Cape Verde, Rwanda na Namibia yakilinganishwa na mataifa kama vile Italia, Ugiriki na Hungary. Botswana na Shelisheli yaliyo na alama 61 na 60 yamefanya vyema zaidi ya taifa kama vile Uhispania ambayo ina alama 57. Katika Kanda ya Afrika Mashariki, Rwanda inaongoza huku ikiwa katika nafasi ya 48, Tanzania ni ya pili lakini ulimwenguni ni ya 103, Kenya ni ya tatu lakini ya 143 ulimwenguni. Uganda ni ya nne ikiwa ya 151 ulimwenguni na Burundi inashika nafasi ya 157 ulimwenguni. Sudan Kusini na Somalia ndio nchi zenye ufisadi zaidi ulimwenguni kati ya mataifa 179 na 180 ulimwenguni. Shirika hilo lenye makao yake jijini Berlin, linasema licha ya kuwa pana juhudi za kukabiliana na donda hilo ulimwenguni, kasi ya mataifa mengi ni mdogo. Vile vile limesema kuwa; “kuikabili vita dhidi ya ufisadi huchukua muda mrefu, miaka sita baadaye mataifa mengi hayajapiga hatua.” Ripoti hiyo imetolewa kutoka vyanzo 13, ikiwemo Benki ya Dunia, Benki ya Ustawi ya Afrika na Kongamano la Uchumi Ulimwenguni na kufanya uamuzi kutokana na viwango vya rushwa, ugavi wa fedha za umma, matumizi ya ofisi za umma kwa masilahi ya kibinafsi na masuala mengine ya ufisadi. Mataifa 180 yaliratibiwa kwenye utafiti huo. Maeneo bora yalikuwa Ulaya Magharibi na wastani wa alama 66, huku eneo lililofanya vibaya zaidi likiwa ukanda wa mataifa ya Afrika yaliyo Kusini mwa Jangwa la Sahara likiwa na wastani wa alama 32, likifuatwa kwa karibu na Asia ya Kati iliyokuwa na wastani wa alama 34. Kiwango cha wastani ulimwenguni ni alama 43. Kwa nchi za Ulaya, New Zealand na Denmark ziliongoza kwenye orodha hiyo zikiwa na alama 89 na 88, huku Somalia ikivuta mkia kwa alama tisa, kisha Sudan Kusini ikiwa na alama 12, Syria ikiwa na alama 14 na Afghanistan ikiwa na alama 15. Uingereza ilitajwa kuwa moja ya mataifa yaliyoimarika kwa kipindi cha miaka sita na kuongeza alama zake kuwa nane tangu mwaka 2012 na kufikia alama 82 na kuiweka juu ya Ujerumani kwa alama moja na kukabana koo na Uholanzi, Luxembourg na Canada. Marekani imeshika nafasi sawa na Austria na Ubelgiji katika nafasi ya 16 kwa alama 75. Shirika hilo limesema limekusanya takwimu kutoka kwa kamati ya kuwalinda wanahabari na kugundua kuwa wanahabari wamo hatarini kwenye mataifa fisadi. Kwa miaka sita iliyopita, zaidi ya wanahabari 10 wameuawa katika mataifa yaliyo chini ya alama 45 na mmoja wa wanahabari kati ya watano alikuwa anafanya stori kuhusu ufisadi. Mkurugenzi wa Shirika la Kimaitaifa la Transparency International, Patricia Moreira, amesema kampeni zenye kuchafua jina, dhuluma, ufisadi ni vyombo vinavyotumika na Serikali katika mbinu za kunyamazisha juhudi za kukabiliana na ufisadi. | 2kimataifa
|
WAGOMBEA wawili kati ya sita waliochukua fomu kuwania nafasi ya Urais wa Shirikisho la Soka Zanzibar (ZFF) wameenguliwa. Uchaguzi huo mkuu wa kwanza tangu kuundwa kwa Shirikisho hilo umepangwa kufanyika Juni 2 mwaka huu.Wagombea hao wameenguliwa na Kamati inayosimamia Uchaguzi huo kwa sababu tofauti baada ya kukamilika kwa usaili uliofanyika Mei 21 na 22 mwaka huu. Mwenyekiti wa Kamati ya Uchaguzi ya ZFF Fadhil Ramadhan Mberwa aliwataja wagombea hao waliokatwa ni Abrahman Mohammed Hussein na Haji Ali Salum.Alisema kuwa wagombea hao kila mmoja amekatwa kwa sababu tofauti ambapo Abrahman hakuhudhuria kwenye usaili na hivyo Kamati ilishindwa kumtathmini uadilifu wake kutokana na kuwa hawakufanya nae mahojiano.Kwa Haji alienguliwa baada ya kukosa uzoefu katika masuala ya mpira wa miguu. “Mmoja tulishindwa kumpitisha kwa sababu hakuja kwenye usaili na kwa kuwa hakuja hatukupata kuonana nae na kuona vyeti vyake na kushindwa kumtathmini uadilifu wake,” alisema. Kwa mgombea wa nafasi ya Makamu wa rais aliyeenguliwa ni Nassor Ali ambae alichelewa kwenye usaili.Mberwa alisema kuwa katika usaili wao kikubwa walichoangalia ni uzoefu wa mgombea katika uongozi wa soka, kiwango cha elimu na maadili katika masuala mbali mbali. “Kwa kuwa hili ni Shirikisho jipya kwa hivyo ni lazima tupate watu wasafi kwa kila eneo”, alisema.Wagombea waliopitishwa kuwania urais ni Khamis Abdalla Said, Ame Abdalla Dunia, Seif Kombo Pandu na Suleiman Mahmoud Jabir,na kwa upande wa Makamu ni Khamis Shaali, Salum Ubwa na Hussein Ahamada. Aidha alisema kuwa katika wagombea walioomba kwenye ngazi za mikoa wote wamepita. | 3kitaifa
|
Subsets and Splits
No community queries yet
The top public SQL queries from the community will appear here once available.