text
stringlengths
1k
24.2k
label
class label
6 classes
MBUNGE wa Jimbo la Dodoma Mjini, Anthony Mavunde (CCM) ametoa vifaa vya kujifungulia 350 na mashuka 100 ili kusaidia wanawake kujifungua salama katika jimbo hilo.Akikabidhi vifaa hivyo katika Kituo cha Afya Makole Jijini Dodoma jana, Mavunde alisema ametoa vifaa hivyo kwa vituo vyote vya afya na zahanati vinavyotoa huduma ya kusaidia wanawake kujifungua.“Natambua baadhi ya wanawake wamekuwa wakikosa vifaa vya kujifungulia kutokana kukosa fedha, ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya Sikukuu ya Wapendanao (juzi) nimeona nitoe msaada huu ili kupunguza vifo vya akinamama na watoto vinavyotokana na uzazi,” alisema Mavunde ambaye ni Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Ajira na Vijana).Alisema mifuko hiyo ina aina 10 za vifaa hivyo. “Upendo wangu ni kuwajali watu wenye mahitaji maalumu. Nimewaletea mifuko 350 yenye vifaa vyote vya kujifungulia ambapo mfuko mmoja gharama yake ni shilingi 21,000 pia nimetoa mashuka 100 pamoja na maji kwa ajili ya wagonjwa mbali mbali,” alisema. Aidha, alisema hatua hiyo ni utekelezaji wa ahadi yake wakati wa kampeni kwamba atahakikisha anaboresha sekta ya afya na ni mwendelezo wa utoaji vifaa kwa sekta hiyo.
3kitaifa
Timu 16 zitashiriki katika ligi hiyo itakayotoa bingwa wa Tanzania Bara ambaye ataiwakilisha katika kuwania ufalme wa soka Afrika na michuano ya Kombe la Kagame kwa mabingwa wa Afrika Mashariki na Kati.Mabingwa watetezi, Yanga ya mitaa ya Twiga na Jangwani itaongoza timu nyingine 15 za Azam FC (Dar es Salaam), Simba, Mbeya City (Mbeya), Coastal Union (Tanga), Kagera Sugar (Kagera), Mtibwa Sugar (Morogoro), JKT Ruvu (Pwani), Ndanda FC (Mtwara), Stand United (Shinyanga), Tanzania Prisons (Mbeya) na Mgambo JKT (Tanga).Timu hizo zitaungana na timu nne zilizopanda Ligi Kuu msimu huu ambazo ni African Sports (Tanga), Majimaji FC (Songea), Toto Africans (Mwanza) na Mwadui FC ya Shinyanga. Siku chache kabla ya kuanza kwa ligi hiyo, Yanga na Coastal Union zimeanza kutambiana kuwa kila moja itashinda katika mchezo wao kwa ajili ya kuanza msimu vizuri.Yanga itawakaribisha Coastal Union kwenye Uwanja wa Taifa, Jumapili ijayo ikiwa ni mechi yao ya ufunguzi.Katika kuhakikisha wanashinda mchezo wao wa kwanza nyumbani, Yanga wamesema wanatarajiwa kuingia kambini kati ya leo au kesho wilayani Bagamoyo, Mkoa wa Pwani kujiandaa na mchezo huo.Akizungumzia mchezo huo, Mkuu wa Idara ya Habari na Mawasiliano wa Yanga, Jerry Muro alitamba kuwa lazima Yanga washinde kwani imefanya usajili wa wachezaji wengi wazuri.“Tuna kikosi imara ambacho kimejipanga kuwafunga Coastal Union, ukiangalia wachezaji wetu wengi wako kwenye timu za taifa na wameonekana kuwa tishio sisi tunawaambia Coastal kuwa tutawamaliza,” alisema Muro.Muro alisema Yanga itaendelea kujenga historia msimu huu kwa kuhakikisha wanashinda kwa kila mchezo. Kikosi hicho kilianza mazoezi ya kawaida jana huku wakiendelea kuwasubiri wachezaji waliokuwa wakizitumikia timu zao za taifa ili waunganike pamoja kwa ajili ya kambi.Kwa mujibu wa Muro, wachezaji wa kimataifa Haruna Niyonzima wa Rwanda na Amisi Tambwe wa Burundi walitarajiwa kuwasili jana kujiunga na wenzao.Kwa upande wa Coastal Union, Ofisa Habari, Oscar Assenga alisema timu hiyo inaendelea na mazoezi kwenye Uwanja wa Mkwakwani na wakati wowote wataelekea Dar es Salaam kwa ajili ya mchezo huo.Asseanga alisema kikosi kimejipanga na kinahitaji kuweka historia kwenye Uwanja wa Taifa ya kuibuka na ushindi.“Tumekuwa na historia mbaya ya kufungwa kwenye Uwanja wa Taifa, kikosi chetu msimu hakiko tayari kuendelea kuweka historia hiyo mbaya, tuna imani tutashinda na kuwashangaza Yanga,” alisema Assenga.
5michezo
*Pluijm asema hana taarifa ya kibarua chake kuwa shakani Na WINFRIDA NGONYANI-DAR ES SALAAM KLABU ya Free State Stars ya Afrika Kusini, imeungana na Yanga katika kutaka kunasa saini ya Mzambia, George Lwandamina, aliyetajwa kufanya mazungumzo na Yanga kwa ajili ya kujiunga na mabingwa hao watetezi wa Ligi Kuu Tanzania Bara. Free State Stars klabu ambayo aliwahi kuchezea winga wa zamani wa Yanga, Mrisho Ngassa, iliwahi kuwa chini ya Kocha Mmalawi, Kinnah Phiri ambaye anaifundisha Mbeya City, lakini kwa sasa mshambuliaji aliyewahi kuichezea klabu za Simba na Yanga Mganda, Hamis Kiiza, amejiunga nayo. Akizungumza na MTANZANIA jana, Lwandamina ambaye ameifundisha Klabu ya Zesco United kwa mafanikio ambayo msimu huu ilifanikiwa kuingia hatua ya nusu fainali ya michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika kabla ya kutolewa na Mamelody Sundown ya Afrika Kusini, kocha huyo alisema anazo ofa nyingi mezani ambazo zimemfikia hivyo ataangalia ipi itakuwa na manufaa kwake. “Timu ambazo nimezungumza nazo ni Yanga na Free State, ila zipo nyingine zimetuma ofa ambazo bado sijazijibu, naangalia timu yenye masilahi niweze kujiunga nayo, pia si masilahi tu naangalia na ubora wake hasa ushiriki wa michuano ya kimataifa inayohusisha klabu,” alisema. Kocha huyo aliyeifundisha Zesco kwa miaka mitatu ya mafanikio, alisema anatumai klabu zote zilizotuma ofa zimeona uwezo wake wa kunoa timu na kuzipa mafanikio, hivyo si kama zimebahatisha kutuma ofa zao. Hata hivyo, Kocha wa Yanga, Hans van der Pluijm, alisema hana taarifa ya kibarua chake kuwa shakani. “Sijapata taarifa yoyote bado, nasoma magazetini subirini labda uongozi utaeleza hatima ya haya yanayosemwa,” alisema Pluijm.
5michezo
WAZIRI wa Kilimo, Japhet Hasunga amesema timu ya wataalamu wa uhakiki wa wakulima wa zao la korosho imeongezeka katika mikoa ya Mtwara, Lindi na Ruvuma kutoka 11 hadi kufi kia 20 ili kuongeza uharaka wa uhakiki kwa ajili ya malipo ya wakulima hao.Aliyasema hayo wakati akizungumza na waandishi wa habari mkoani Mtwara kwa lengo la kutoa ufafanuzi zaidi juu ya hali ya ununuzi wa zao hilo kwa msimu huu wa 2018/2019.Alisema timu hiyo ya wataalamu tayari imewasili mkoani Pwani kwa ajili ya kuanza uhakiki wa wakulima wa korosho kuanzia hivi sasa ambapo mkoa wa Pwani utakuwa mkoa wa nne kuhakikiwa ukiungana na mikoa ya Lindi, Mtwara na Ruvuma.“Hadi kufikia Desemba 1, mwaka huu jumla ya vyama vya ushirika 212 vimeshahakikiwa kati ya vyama 504 vilivyopo katika mikoa hiyo mitatu ya Kusini kama vile Lindi, Mtwara na Ruvuma,” alisema Hasunga.Alisema vyama 157 tayari vimeshalipwa fedha zao kati ya vyama 617 ambavyo vinajihusisha na ushirika wa korosho nchini. Hasunga alisema kuwa, hadi hivi sasa jumla ya fedha zilizolipwa kwa wakulima wa korosho ni Sh bilioni 35.54 na kilo milioni 10,769 za korosho zimeshalipwa.Alisema kuwa, hadi kufikia Disemba 1, mwaka huu idadi ya wakulima ambao tayari wameshalipwa fedha zao ni wakulima 34,938 Alifafanua zaidi kuwa, “Katika Mkoa wa Lindi tayari shilingi bilioni 12.7 zimelipwa wakati katika Mkoa wa Ruvuma ni shilingi bilioni 4.9 na Mkoa wa Mtwara ni shilingi bilioni 17.9,” alisema.
3kitaifa
Daktari Bingwa wa Radiolojia kutoka Taasisi ya Mifupa katika Hospitali ya Taifa Muhimbili (MOI), Mechris Mango amesema, kuna baadhi ya watu wanahofu kupima kipimo hicho cha picha kwa madai kuwa kinasababisha mtu kupunguza umri wa kuishi jambo ambalo si kweli.Amesema kuna kiwango kikifikia ndio inaweza kusababisha mionzi lakini vipimo vya sasa vimewekwa katika mfumo ambao hauwezi kufikia katika kiwango cha madhara."Haiwezekani mtaalamu anayepima kipimo hicho kufikia kiwango chenye madhara kwa mpimwaji, mashine za sasa zimetengenezwa kwa namna ambayo hazitaruhusu na kabla ya kufikia huko zinatoa mlio wa tahadhari."Ni kama gari, unapoendesha ikiisha mafuta itakuwashia taa kukupa tahadhari halitazimika tu, na mashine zetu ni hivyo ukipitiliza utapata mlio kukuashiria unakoelekea huko sio salama na haitakuruhusu kuendelea ukibonyeza haiendi," amesema Dk Mango.Amesema hata hivyo kuna mionzi hatari kila mahali, kwenye jua, rangi za nyumba, kwenye dunia lakini mionzi ya kwenye kipimo imedhibitiwa katika mashine zake.Amesema, kuna bodi zinazosimamia mionzi hiyo iliyoko kwenye vipimo vya X-ray isiwe na madhara kwa binadamu kuhakikisha kwamba mionzi inayotolewa ni salama kwa na pia wanaotumia mashine hizo wanafundishwa.Alisema matangazo yaliyopo kwenye nyumba vya X-ray kuwataka watu wasikae eneo hilo ni kwa tahadhari tu kwa kuwa eneo hilo wakati wote mashine zinafanya kazi."Tunachoambiwa ni mionzi inaweza kuleta madhara sasa hayo madhara ndiyo yanayoweza kufupisha maisha, ukiwa na kansa lazima maisha yatapungua"amesema.Dk Mango amesema kipimo hicho hakipunguzi umri wa mtu kuishi bali ni kwa sababu vipimo hivyo vina mionzi ambayo inaweza kusababisha mgonjwa kama saratani"Sio kwamba mionzi hiyo inaua au inapunguza umri wa kuishi bali mionzi inaweza kukusababishia maradhi kama saratani kwa hiyo ukiwa na ugonjwa ambao hautibiki si unapunguza umri wa kuishi," amesema.
3kitaifa
RAIS John Magufuli ameagiza wananchi kuunganishiwa maji katika maeneo yaliyo karibu na vyanzo vya maji badala ya kurukwa huku wakibaki wanahangaika kuyatafuta.Rais Magufuli aliyasema hayo jana wakati alipozungumza na wananchi wa eneo la Kimnyaki, Kata ya Kimnyaki wilayani Arumeru mara baada ya kuweka jiwe la msingi la mradi wa maji wenye thamani ya Sh bilioni 520 zilizotolewa kwa mkopo kutoka Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB).Akizungumzia kuhusu maji, Rais Magufuli alisema mradi huo wa maji utawasaidia wananchi wa maeneo hayo kupata maji safi na salama na akaagiza Mamlaka za maji kuwaunganishia maji wananchi wanaoishi karibu na vyanzo vya maji .Alisema watanzania wanachotaka hivi sasa ni kuona fedha au miradi inayofanyika inawanufaisha.Alimuagiza Waziri wa Maji na Umwagiliaji, Profesa Makame Mbarawa kuhakikisha wakandarasi hao 10 waliopewa kazi za kukamilisha mradi huo mkubwa wa wa maji wanafanyakazi usiku na mchana kwa ajili ya kuhakikisha kero ya maji ina tatuliwa Mkoani Arusha na nchi nzima.“Nakuagiza Waziri wa Maji kuhakikisha wale wakandarasi wote ambao wanakuwa vikwazo katika miradi ya maji wanaondoka kwani wananchi wanahitaji maji na si maneno yanayopoteza muda, pia kule eneo la Olonyosambu ambapo wananchi wanakunywa maji yenye floride mradi huu uwafikie ili kupunguza tatizo lao,” aliagiza.Aidha, kutokana na wananchi wa eneo hilo kukabiliwa na changamoto ya barabara, Dk Magufuli aliagiza Wakala wa Barabara za Mijini na Vijijini (Tarura ) kujenga barabara hiyo yenye kilomita 18 kutoka Sanawari hadi Ngaramtoni kwa kiwango cha lami.Akizungumza katika uzinduzi huo, pia alimuagiza Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Isack Kamwelwe kuhakikisha anakaa na mkandarasi wa kampuni ya Nipo Goup Ltd iliyopewa kazi za kusambaza umeme vijijini kuitwa mara moja na kukaa na viongozi husika ili kujua ni kwanini yupo nyuma ya kiwango alichotakiwa kuwepo kwa sasa kwani wananchi wanahitaji umeme.Waziri wa Maji Profesa Mbarawa amesema wizara hiyo imetekeleza miradi 8,801 nchi nzima ikiwemo miradi 500 mikubwa iliyogharimu kiasi cha Sh bilioni 520.Alisema pia wamejenga mradi ya maji kutoka Same-Mwanga hadi Korogwe utakaogharimu kiasi cha Sh trilioni 1.2 utaenda hadi Zanzibar na mwakani zabuni zitafunguliwa kwa ajili ya kupata wakandarasi.Mwakilishi kutoka Benki ya Maendeleo ya Afrika (Afdb), Alex Mobiru alisema mradi huo wa maji unaonyesha ushirikiano kati ya Tanzania na Benki ya Maendeleo ya Afrika.Alisema mradi huo unaendana na malengo ya waanzilishi wa benki hiyo ili kuhakikisha nchi za Afrika zinakuwa na maendeleo ambapo utaboresha huduma mbalimbali za maji.“Tunaamini kuwa hakuna mtoto atakayekosa kwenda shule sababu ya maji ikiwemo wananchi kuwa walemavu sababu ya kukosa maji,” alieleza.Mhandisi wa Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Jiji la Arusha (Auwsa) Ruth Koya akitoa taarifa ya mradi alisema hali ya upatikanaji wa maji jijini Arusha ni asilimia 48 na lengo la serikali ni kufikia asilimia 100Alisema kazi zilizofanywa katika mradi huo wa maji ni kuhakikisha wanatafuta maeneo ya vyanzo vya maji na kupitia mradi huo wa maji wana wakandarasi 10 waliojumuisha uchimbaji wa visima 11 vikiwemo vikubwa na vidogo.Alisema mradi huo wa maji utanufaisha watu milioni moja wa kata saba za wilaya ya Arumeru na mara baada ya mradi huo kukamilika tatizo la maji litapungua na upungufu wa maji katika Jiji la Arusha utakuwa umekamilika.Alisema kazi zilizopongwa ni kuchimba visima, kuongeza mtandao wa bomba za kusafirisha maji, ujenzi wa mabwawa wa kutibu maji na ujenzi wa vyoo vya mfano kwenye shule mbalimbali.Alisema katika utekelezaji wa mradi huo, jumla ya visima 13 vimechimbwa ikiwemo ulazaji wa mabomba ya maji taka na ujenzi wa mabomba y maji taka pia mradi huo wa utakapokamilika utawezesha wananchi wengine kupata maji na kupunguza wastani wa maji yanayopotea kufika asilimia 25.Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Mrisho Gambo alieleza machache ambayo serikali imeyafanya ambayo ni utaratibu wa kuwa na elimu bure ambapo awali wazazi walezi wakishindwa kuwasomesha watoto wao kutokana na umaskini waliona.Naye Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Arusha, Lootha Sanare alisema mafuriko ya mwaka 2015 yamehamia CCM kwani Longido, ina mbunge wa CCM, Monduli CCM na Mkoa wa Arusha una madiwani 51 wa CCM.Alisema wabunge wa Meru, Godson Meseyeki na Arumeru, Joshua Nassari hawapo majimboni wananchi wanalalamika kwani hawatatui kero zao Mbunge wa viti maalum (CCM) Amina Mollel alisema Rais Magufuli ni zawadi kwa Watanzania sababu yeye ni zawadi kutoka kwa Mungu na kuishukuru Serikali kwa kutoa elimu bure iliyowasaidia watoto wengi wakiwemo walemavu kwenda shule.Wabunge wa mkoa huo wa Arusha walimshukuru Dk Magufuli na serikali yake ya awamu ya tano kwa kuwezesha kuwepo kwa miradi mingi ya maendeleo ikiwemo ya maji, hali inayosaidia kutatua tatizo la maji katika majimbo yao.Mbunge wa Simanjiro, James ole Milya alisema japokuwa kwa sasa Simanjiro kuna kiangazi, lakini anashukuru serikali kwani kupitia mradi uliopo wa maji, mwakani wana simanjiro wanatarajia kupata maji.Mbunge wa Longido, Dk, Stephen Kiruswa alisema wanamsubiri rais huyo aendele Longido kwa ajili ya kuzindua pia mradi wa maji ambao umekamilika.Mbunge wa Monduli, Julius Kalanga alisema Rais aachane na kelele za wachache wasiopenda maendeleo na kumuomba rais huyo aende Monduli angalau akawasalimie wananchi lakini pia kuangalia uwezekano wa kutatua tatizo la maji ambalo kwa sasa ndio changamoto kubwa iliyopo."Unapowadhuru wengine nasi wanamonduli usitupite, tunaomba maji, maji maji , wewe ni Rais wa Wanyonge tupo nyuma yako na sisi Monduli kuna maeneo ambayo haturuhusiwi kukanyaga na mifugo yetu tunashukuru umeyafuta baadhi ya mashamba " alisisitiza.
3kitaifa
ABDUCADO EMMANUEL NA MWALI IBRAHIM, DAR KOCHA Mkuu wa timu ya Taifa ya Tanzania, ‘Taifa Stars’, Mart Nooij raia wa Uholanzi, yupo shakani kuendelea kukinoa kikosi hicho kutokana na matokeo mabaya aliyopata kwenye michuano ya Kombe la Cosafa. Stars imeambulia vipigo kwenye mechi mbili za awali za Kundi B la michuano hiyo na timu ndogo Swaziland (1-0) na Madagascar (2-0), leo itamalizia ratiba kwa kuchuana na Lesotho iliyoko juu yake. Habari za ndani zilizoifikia MTANZANIA jana zimeeleza kuwa, baadhi ya wajumbe wa Kamati ya Utendaji ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), hawaridhishwi na mwenendo wa kikosi hicho tokea Mholanzi huyo alipokabidhiwa mikoba hiyo Aprili mwaka jana akimrithi Mdenish, Kim Poulsen. “Kila siku timu ya Taifa imekuwa ikipanda na kushuka na tumeshindwa kukaa kwenye mwelekeo mmoja, matokeo tuliyopata Cosafa ndiyo yameharibu kila kitu na kibarua chake kitajadiliwa mara baada ya timu kurejea Dar es Salaam mwishoni mwa wiki hii,” alisema. Habari hizo zilizidi kueleza kuwa suala la upangaji kikosi na uhitaji wa kikosi hicho, nalo limewachukiza baadhi ya wajumbe na wengi wanajiuliza ataweza mtihani wa kuiongoza Stars kufuzu michuano ya Mataifa ya Afrika (Afcon) 2017 na ile ya Wachezaji wa Ndani (CHAN) mwakani. Nooij amelalamikiwa na wadau wengi wa soka nchini kwa uamuzi wake wa mara kwa mara wa kuteua kikosi kinachojirudia, wakiwemo wachezaji wanaokaa benchi huku akiwafungia vioo baadhi waliong’ara kwenye klabu zao. Hata hivyo, taarifa iliyotumwa jana na TFF imeeleza kuwa, Kamati hiyo itakutana Jumapili hii kwenye kikao cha kawaida, huku moja ya ajenda ikiwa ni kupokea na kujadili mwenendo, maandalizi na maendeleo ya timu za Taifa za Tanzania ikiwemo Stars. Mara baada ya kipigo dhidi ya Madagascar, Nooij alinukuliwa na kituo cha televisheni cha Supersports 9 akieleza kuwa: “Tumefungwa kama tulivyofungwa na Swaziland, kwangu mimi sio jambo kubwa, nimekuja kwenye michuano hii kwa ajili ya maandalizi ya CHAN na Afcon, nimekuja huku bila baadhi ya wachezaji wangu muhimu ambao wamepata majeruhi.” Makocha wafunguka Kocha Msaidizi wa Yanga, Charles Mkwasa, amesema tatizo linaloiangusha timu hiyo linaanzia kwenye uteuzi wa kikosi, baadhi ya wachezaji walioitwa ni majeruhi hivyo kocha alipaswa kuwasiliana kwanza na makocha wa timu walizotoka ili kuweza kupata taarifa zao kabla ya kuwaita. “Wachezaji wamechezeshwa nafasi si zao hivyo kushindwa kuzimudu, wengine wamekuwa wakicheza kipindi cha pili kwenye klabu zao, lakini kwenye timu hiyo ya Taifa ndio wamechaguliwa kikosi cha kwanza na kucheza muda mrefu, hivyo lazima watafanya vibaya,” alisema. Aliongeza hata wachezaji nao hawakuwa makini uwanjani, kwani walikuwa wakicheza utadhani hawataki ushindi licha ya kupangwa na timu dhaifu, jambo ambalo liliifanya Stars kuonekana dhaifu zaidi ya vibonde hao. Naye Kocha Mkuu wa Mbeya City, Juma Mwambusi, amesema ufike wakati wa TFF kuthamini na kuheshimu mchango wa makocha wazawa na kuondoa fikra mgando kuwa wazawa hawawezi na kuthamini wageni pekee, huku akihoji mbona kwenye ligi wamekuwa wakizifunga timu zenye makocha wa kigeni. “Pia ni vigezo gani alivyotumia kuita timu kama mchezaji kwenye timu yake anakaa benchi, anawezaje kuitwa timu ya Taifa hujiulizi kwanini amekuwa hatumiki kwenye kikosi chake, ipo haja ya kufanya mabadiliko kwani hali hii ni aibu kwa nchi, huku akiwataka wadau wa soka kuweza kumpa mawazo Rais wa TFF (Jamal Malinzi) kama alivyoomba,” alisema. Kocha wa JKT Ruvu, Fred Minziro, alisema kocha huyo anapaswa kubadilisha timu hiyo aliyoikariri kila mara anapoiita, amedai bila kufanya hivyo itaendelea kupata matokeo mabaya.
5michezo
Kulwa Mzee -Dar es salaam MWANDISHI wa habari za uchunguzi, Erick Kabendera (39), anayekabiliwa na mashtaka matatu, likiwamo la kutakatisha zaidi ya Sh milioni 173, ataendelea kusota rumande hadi Agosti 30, kesi yake itakapotajwa. Kabendera ambaye aliingia Gereza la Segerea wiki mbili zilizopita, jana kesi yake ilitajwa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, Dar es Salaam mbele ya Hakimu Mkazi, Augustine Mmbando baada ya Hakimu Mkazi Mwandamizi Augustine Rwizile anayesikiliza kesi hiyo kuwa na udhuru. Wakili wa Serikali Mwandamizi, Wankyo Simon, alidai kesi ilikuwa inatajwa, upelelezi haujakamilika na wanaomba tarehe nyingine ya kutajwa. Hakimu Mmbando aliahirisha kesi hiyo hadi Agosti 30, kwa kutajwa na mshtakiwa ataendelea kuwa rumande. Kwa mujibu wa hati ya mashtaka, katika shtaka la kwanza, kati ya Januari mwaka 2015 na Julai 2019, maeneo mbalimbali ya Dar es Salaam, Kabendera na wengine ambao hawapo mahakamani, anadaiwa alitoa msaada kwenye genge la uhalifu kwa nia ya kujipatia fedha. Katika shtaka la pili la kukwepa kodi, inadaiwa kati ya Januari, 2015 na Julai 2019 maeneo mbalimbali ya Dar es Salaam bila sababu za msingi, mshtakiwa alikwepa kulipa kodi Sh 173,247,047.02 kwa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA). Katika shtaka la tatu la kutakatisha fedha, inadaiwa katika tarehe hizo mshtakiwa alitakatisha kiasi hicho cha fedha huku akijua zimetokana na zao la kusaidia genge la uhalifu na kukwepa kodi.
3kitaifa
Chelsea Kiungo mshambuliaji wa klabu ya Chelsea, Eden Hazard, ameweka wazi kuwa ataondoka ndani ya klabu hiyo mwakani endapo watashindwa kufuzu kushiriki Ligi ya Mabingwa Ulaya. Hata hivyo, mchezaji huyo amekuwa akihusishwa kutaka kujiunga na Real Madrid. AC Milan UONGOZI wa klabu ya AC Milan upo kwenye mipango ya kutaka kumsajili kiungo wa klabu ya Paris Saint-Germain, Adrien Rabiot, wakati wa uhamisho wa dirisha dogo Januari. Mchezaji huyo anatarajia kumaliza mkataba wake msimu wa 2018-19. Real Madrid MATAJIRI wa soka nchini Hispania, Real Madrid, wameanza kumuwinda kinda wa Manchester City, Brahim Diaz. Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 19 yupo katika mwaka wa mwisho wa mkataba wake na amedai hataki kuondoka kwa mkopo. Napoli UONGOZI wa klabu ya Napoli, umethibitisha kuwa unakaribia kumalizana na beki wao wa pembeni, Elseid Hysaj, kwa ajili ya kumpa mkataba mpya. Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 24, amekuwa akiwindwa na klabu ya Juventus. Man United MIPANGO ya Manchester United ni kuhakikisha inamwongezea mkataba mpya nyota wake, Ander Herrera, ili aweze kubaki kwenye viwanja vya Old Trafford. Mkataba wa mchezaji huyo unatarajia kumalizika majira ya joto mwakani. Juventus MATAJIRI wa soka nchini Italia, Juventus, wameingia kwenye vita dhidi ya Inter Milan kwa ajili ya kuwania saini ya mshambuliaji wa klabu ya Fiorentina, Federico Chiesa. Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 20, tayari ameitwa kwenye kikosi cha timu ya taifa ya Italia. Tottenham KINDA wa klabu ya Ajax, Frenkie De Jong, anaweza kuonekana akiwa na uzi wa klabu ya Tottenham katika kipindi cha Januari mwakani kutokana na klabu hiyo kuonesha nia ya kuitaka saini yake. Hata hivyo, Tottenham haijafanya usajili wakati huu wa kiangazi. Man United KOCHA wa klabu ya Wolves, Nuno Espirito Santo, ametajwa kwenye orodha ya makocha wanaowindwa na klabu ya Manchester United kwa ajili ya kuchukua nafasi ya Jose Mourinho endapo atafungashiwa virago vyake. Barcelona KIUNGO wa klabu ya Barcelona, Sergio Busquets, anatarajia kukutana na uongozi wa klabu hiyo kwa ajili ya kusaini mkataba mpya. Mazungumzo ya mkataba mpya yalianza kuzungumzwa tangu mapema mwaka huu na sasa wamefikia hatua za mwisho.
5michezo
BAADA ya vinara wa Ligi Kuu Yanga kutinga robo fainali michuano ya Kombe la Shirikisho la Azam (FA) jana ilipita Rufi ji kuhani msiba wa Kaimu Mwenyekiti wa Kamati ya Usajili na Mashindano, Mustapha Urungu.Ulungu aliyefariki dunia mwishoni mwa wiki iliyopita alipumzishwa Rufiji ambapo kikosi kizima cha Yanga kilichokuwa Ruangwa, Lindi kilipita kutoa salamu za mwisho kabla ya kurejea Dar es Salaam kujiandaa na mchezo ujao wa ligi dhidi ya Alliance.Akizungumza na gazeti hili jana Mratibu wa Yanga, Hafidh Saleh alisema wanatambua mchango mkubwa wa marehemu Urungu na kwa sababu walikosekana kwenye maziko, wakaona wapite alikopumzishwa kutoa heshima zao. “Hatukuwepo kwenye maziko yake kutokana na majukumu yaliyokuwa mbele yetu, tukaona tupite kutoa salamu zetu za mwisho kwake, kwa kutambua na mchango wake,”alisema.Yanga mwishoni mwa wiki iliyopita ilikuwa na mchezo dhidi ya timu ya Daraja la Kwanza Namungo FC wa michuano ya FA ambapo iliibuka na ushindi wa bao 1-0 na kutinga hatua ya robo fainali.Mbali ya Yanga, timu nyingine zilizofuzu hatua hiyo ni Kagera Sugar, Alliance, KMC, Singida, African Lyon na Lipuli. Akizungumzia mchezo uliopita dhidi ya Namungo, mchezaji Deus Kaseke aliyetoa krosi ya bao lililofungwa na mshambuliaji Heritier Makambo, alisema anashukuru kwani juhudi zimewasaidia kupata ushindi. “Tunashukuru kwa ushindi tumefuata maelekezo ya mwalimu, tumejituma na kupata goli. Namungo pia ni wazuri wamecheza mchezo mzuri na wakiendelea hivi wanaweza kupanda Ligi Kuu,” alisema.Kaseke alisema wapo tayari kwa yeyote watakayepangwa naye hatua inayofuata. Mpinzani wao anayefuata atajulikana baada ya kufanyika kwa droo itakayochezeshwa na wadhamini wa michuano hiyo Azam Media. Mchezaji wa Namungo, Reliants Lusajo alisema uzoefu umeibeba Yanga na kupata ushindi huo. Alisema kilichowagharimu walishindwa kutumia nafasi karibu mbili walizopata tofauti na wenzao wametumia makosa yao kuwaadhibu.
3kitaifa
Washindi hao ni Gabriel Fernandis (18) mwanafunzi na mkazi wa Musoma mkoani Mara ambaye amejishindia Shilingi milioni moja na Hamisi Rashid (52) wa Tabora aliyejinyakulia Shilingi milioni tatu.Pamoja na kukabidhiwa zawadi hizo, Airtel imeendesha droo ya wiki ya tatu ya “Jiongeze na Mshiko” katika ofisi ya makao makuu ya kampuni hiyo yaliyopo Morocco jijini Dar es Salaam ambayo ilihudhuriwa na waandishi wa habari na wasimamizi kutoka bodi ya Bahati Nasibu Tanzania.Akizungumza mara baada ya kukabidhiwa zawadi yake, Grabriel Fernandis alisema: “Nimefurahi sana kuibuka mshindi katika promosheni hii ambayo nimeshiriki bure, bila gharama yoyote kwa kujibu maswali na kujiongezea pointi zilizoniwezesha kushinda. Nafurahia ushindi huu kwa sababu pesa hizi zitanisaidia kujiendeleza kwenye masomo yangu.”Akizungumza na waandishi wa habari, Ofisa Uhusiano na Matukio wa Airtel, Dangio Kaniki, alisema wamefurahishwa kama kampuni kuwazawadia washindi wa wiki ya kwanza na ya pili ya promosheni ya “Jiongeze na Mshiko”.Alisema ni matumaini yake kuwa pesa hizo walizoshinda zitawawezesha kuendesha shughuli zao za kijamii na kiuchumi. Walioibuka washindi katika droo ya tatu jana ni Afrillious Kapinaa (21), mwanafunzi na mkazi wa Dar es Saalam aliyejishindia Shilingi milioni 1 pamoja na Shangai Rodger (53) mfanyakazi wa TRA na mkazi wa Tanga aliyejishindia Shilingi milioni tatu.
1uchumi
Na CLARA MATIMO-MWANZA WATU watano wamefariki dunia na wengine 13 wamejeruhiwa baada ya gari lenye namba za usajili T 107 BBK Toyota Coaster mali ya Kampuni ya Auki ya jijini Mwanza, kugongana uso kwa uso na gari aina ya Scania lenye namba T 504 BZB likiwa na tela lenye namba T 880 ASA. Akizungumza na waandishi wa habari kuhusu ajali hiyo, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza, Ahmed Msangi, alisema tukio hilo lilitokea Desemba 16 saa 1:30 usiku katika Barabara ya Mwanza-Shinyanga, Kata ya Buhongwa jijini hapa. Alisema Coaster iliyokuwa ikitokea Katoro mkoani Geita kuja jijini Mwanza, ilikuwa ikiendeshwa na Badru Habibu (33), mkazi wa Nyegezi na Scania hilo lililokuwa likitoka jijini Mwanza kwenda Dar es Salaam, lilikuwa likiendeshwa na Salim Omary (28), mkazi wa Dar es Salaam. Kamanda Msangi alisema chanzo cha ajali hiyo ni mwendo kasi wa Coaster iliyokuwa imebeba abiria. Alisema kuwa dereva wa basi hilo dogo, alikuwa akiyapita magari mengine bila kuchukua tahadhari, ndipo aligongana na Scania hilo. “Hadi sasa kati ya waliofariki ni mwili wa mtu mmoja tu ambao umetambuliwa, marehemu huyo alikuwa anaitwa Abdul Mustafa, anakadiriwa kuwa na umri kati ya miaka 42 na 45. Miili mingine bado haijatambuliwa na ndugu zao. “Nawaomba wananchi wafike katika Hospitali ya Kanda ya Bugando ili kuitambua miili ya marehemu, maana tumeihifadhi katika chumba cha kuhifadhia maiti hospitalini hapo. Pia majeruhi wote wapo hapo hapo hospitalini, wanaendelea kupatiwa matibabu na hali zao zinaendelea vizuri,” alisema. Kamanda Msangi alitoa wito kwa waendeshaji wa vyombo vya moto, hususani magari ya  abiria, kuwa makini wawapo barabarani na kuendesha huku wakifuata kanuni, taratibu na sheria za barabarani. Kutokana na hali hiyo, alisema Jeshi la Polisi linawashikilia madereva wote wawili kwa mahojiano na uchunguzi ukikamilika watafikishwa mahakamani kwa mujibu wa sheria. “Kama tutabaini mwenye kosa ni mmoja, tutamfikisha mahakamani, lakini endapo wote wawili watakutwa na hatia, basi wote watakwenda mahakamani. Hatuwezi kuendelea kupoteza nguvu kazi ya taifa kutokana na uzembe wa madereva wasiozingatia sheria ya usalama barabarani,” alisema.  
3kitaifa
Taifa Stars usiku wa kumakia leo imepoteza matumaini ya kufuzu hatua ya 16 bora ya fainali za Afcon 2019 nchini Misri baada ya kukubali kipigo cha mabao 3-2 dhidi ya majirani zao Kenya katika mchezo wa Kundi C uliofanyika kwenye Uwanja wa June 30 uliopo jijini Cairo unaomilikiwa na Jeshi la Anga la nchi hiyo. Mtu aliyeleta majonzi makubwa kwa Watanzania ni Michael Olunga ambaye amefunga magoli mawili kwenye mchezo huo. Katika patashika hiyo, Tanzania ndio walikuwa wa kwanza kupata goli kupitia kwa Saimon Msuva mnamo dakika ya sita ya mchezo baada ya kazi nzuri iliyofanywa na nahodha Mbwana Samatta na kuipa uongozi Stars. Hata hivyo Kenya walipambana na  kusawazisha goli hilo kupitia kwa Michael Olunga dakika ya 39 kwa kichwa baada ya Aishi Manula kuukosa mpira wa adhabu ndogo uliopigwa na Ayub Timbe. Almanusura Taifa Stars iandike bao la pili mnamo dakika ya 12 wakati Msuva alipokuwa akienda kumchungulia golikipa wa Kenya lakini bahati mbaya alifanyiwa madhambi nje ya boksi la penati. Kabla ya goli la kusawazisha, Harambee Stars almanusura wapate goli mnamo dakika ya 14 ya mchezo baada ya shuti la Erick Ouma anayecheza soka la kulipwa nchini Sweeden kudakwa na Aishi Manula. Magoli yote yapo hapa I bet this game left you entertained…😍😉 Don't miss the match highlights, they're epic😅🔥👇#TotalAFCON2019 #FootballTogether pic.twitter.com/JPgwxSJk1K — CAF (@CAF_Online) June 28, 2019 Ramadhan Kessy alikosa nafasi ya kuipa Tanzania goli la pili dakika 36 kupitia mpira wa adhabu ndogo baada ya kipa wa Kenya Matasi kufanikiwa kuugusa na kugongwa mwamba na hatimaye kuwa kona ambayo hata hivyo haikuzaa matunda. Samatta aliiandikia Stars bao la pili baada ya kazi nzuri ya juhudi binafsi aliyoifanya akitokea upande wa kushoto mwa uwanja akiwadahaa mabeki wa Harambee Stars na hatimaye kuipa uongozi. Kenya walifanya mabadiliko kwa kumuingiza Bernard Ochieng kuchukua nafasi ya Calabar, ambaye alionekana kutokuwa vizuri upande wa winga. Kocha Emmanuel Amunike naye alifanya mabadiliko kwa kumuingiza Himid Mao kuchukua nafasi ya Mudathir Yahya. Kenya walifanikiwa kusawazisha kupitia kwa Omollo kufuatia mbinu nzuri ya kona fupi aliyoanzisha Timbe na kufanya matokeo kuwa 2-2. Hatimaye Olunga alididimiza ndoto na matumaini Tanzania kupata walau alama moja baada ya kufunga bao la tatu kwa upande wa Kenya dakika ya 80 kufuatia kazi nzuri iliyofanywa na Eric Johanna aliyeingia kutoka benchi. Mchezo wa mwisho kwa Taifa Stars ambao kimsingi utakuwa ni wa kukamilisha ratiba utakuwa dhidi ya Mbweha wa Kaskazini Algeria huku Kenya wakimaliza na Senegal. Kikosi cha Tanzania kilichoanza: 18. Aishi Manula (GK), 2. Gadiel Michael, 6. David Mwantika, 5. Kelvin Yondani, 22. Ramadhan Kessy, 23. Mudathir Yahya, 12. Simon Msuva, 4. Erasto Nyoni, 17. Farid Mussa, 10. Mbwana Samatta, 11. Thomas Ulimwengu Kikosi cha Kenya kilichoanza: 18. Patrick Matasi, 15. David Owino, 3. Abud Omar, 2. Joseph Okumu, 5. Musa Mohamed, 12. Victor Wanyama, 8. Johanna Omollo, 11. Francis Kahata 7. Ayub Timbe, 13. Eric Ouma, 14. Michael Olunga  
5michezo
MANCHESTER, ENGLAND KUINGO wa mshambuliaji wa klabu ya Manchester United, Paul Pogba, baada ya juzi kufanikiwa kupachika bao lake la kwanza kwa kipindi cha miezi miwili, ametumia ukurasa wake wa Instagram kutoa zawadi ya bao hilo kwa watumwa nchini Libya. Pogba juzi alishuka dimbani kwa mara ya kwanza baada ya kukaa kwa miezi miwili akiwa majeruhi, hivyo aliweza kuifungia bao timu yake na kutoa pasi moja ya mwisho katika ushindi wa mabao 4-1 dhidi ya Newcastle kwenye Uwanja wa Old Trafford, katika michuano ya Ligi Kuu nchini England. Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 24 ambaye ameweka rekodi ya kusajiliwa kwa kiasi kikubwa nchini humo akitokea Juventus, amedai anaguswa sana na vitendo vya ukatili ambavyo wanafanyiwa watu wa Libya, hivyo bao hilo liwe sehemu ya faraja kwao. “Furaha yangu ni kuona narudi uwanjani tena kwa mara nyingine, lakini kwa kipindi hiki chote nimekuwa nikiwaombea wale wote ambao wanateseka na utumwa nchini Libya, nina imani kwamba Mungu atawafanyia wapesi na kuwa upande wao na hali hiyo kufikia mwisho. Katika mchezo huo, Pogba alitajwa kuwa mchezaji bora kutokana na kila alichokifanya, hivyo alitumia nafasi hiyo kuwashukuru mashabiki na wale wote ambao walimuombea aweze kurudi uwanjani mapema. “Nawashukuru wale wote ambao walikuwa na mimi kwa kipindi chote cha kuuguza tatizo langu la nyama za paja, nawashukuru kwa dua zenu na sasa nipo fiti kwa ajili ya kuitumikia klabu yangu kwenye michuano mbalimbali. “Kikosi hiki kitakuwa kwenye ubora wake kwa kuwa mimi nimerudi uwanjani, Zlatan Ibrahimovic amerudi na Marcos amerudi uwanjani, tuna furaha sana, nilikuwa naumia sana wakati nipo nje huku nikiwa na lengo la kutaka kuisaidia timu lakini nashindwa kutokana na hali yangu. “Bado tuna nafasi ya kufanya vizuri kwa kuwa ni mapema kusema lolote baya, kila mmoja anapigania ili kumaliza msimu vizuri, hivyo kwa upande wetu bado tuna nafasi hiyo ya kufanya vizuri,” aliongeza. Kocha wa klabu hiyo, Jose Mourinho, ameweka wazi kuwa anatarajia kumpumzisha kiungo huyo kwenye mchezo dhidi ya FC Basel, keshokutwa katika michuano ya Ligi ya Mabingwa Ulaya hatua ya makundi. Hadi sasa United imefanikiwa kushinda michezo minne katika hatua hiyo na sasa inahitaji pointi moja kuweza kufuzu kwenye hatua ya mtoano
5michezo
Na ASHA BANI -DAR ES SALAAM SAA chache baada ya kumaliza kutoa tamko la msimamo wa vyama nane vya siasa vya upinzani kuhusu wakurugenzi wa halmashauri kuendelea kusimamia uchaguzi mdogo, Mwenyekiti wa Chauma, Hashim Rungwe  ametakiwa kuripoti Kituo cha Polisi Oysterbay leo. Polisi waliingia eneo la mkutano na kumkuta Rungwe akiwa na Mwenyekiti wa UPDP, Fahm Dovutwa na wanachana wengine.  Ofisa mmoja wa polisi baada ya kujitambulisha, alimtaka Rungwe kuripoti polisi leo kwa maelekezo zaidi. Awali katika mkutano wao na waandishi wa habari, Rungwe alisema Tume ya Uchaguzi (NEC) ilitangaza kufanyika kwa uchaguzi mdogo katika kata 32 utakaofanyika Juni 15, lakini walishangazwa na tangazo la wakurugenzi mbalimbali wa hamashauri nchini kuandika barua kwa vyama vya siasa juu ya mchakato wa kuchukua na kurudisha fomu hizo licha ya kuzuiwa na amri ya mahakama. Akisoma tamko hilo, alisema wanatambua kuwa uchaguzi wa madiwani unasimamiwa na Sheria ya Uchaguzi ya Serikali za Mitaa, licha ya kufanyika sambamba na Uchaguzi wa Rais na Wabunge ambao umekuwa ukifanyika chini ya Sheria ya Uchaguzi ya mwaka 1985. “Na itakumbukwa mnamo Mei 10, mwaka huu, Mahakama Kuu ilitoa uamuzi wa kuvifuta vifungu vya sheria ya Tume ya Taifa ya Uchaguzi ambavyo vilikuwa vinawapatia mamlaka wakurugenzi wa halmashauri nchini kuwa wasimamizi wa uchaguzi katika maeneo yao. “Hivyo basi kutokana na hukumu hii ya Mahakama Kuu, sisi vyama vinane ambavyo tumetia saini katika tamko hili, tunaitaka NEC kutumia mamlaka yake iliyopewa na Katiba ya Jamhuri ya Muungano Ibara ya 74 (15) (e) na kuteua wasimamizi wa uchaguzi huu nje na si wakurugenzi wa halmashauri. “Kama NEC itaendelea na msimamo wake wa kuidharau mahakama na kudharau amri halali, sisi vyama nane tutachukua hatua mbalimbali ikiwemo kutoshiriki uchaguzi,’’ alisema Rungwe. Aliongeza kuwa pia wamekubaliana kufanyika kwa mashauriano ya kina na wanaharakati waliofungua kesi, wakiongozwa na Chacha Wangwe, kuwapa ushirikiano wa kina ili waweze kuwasilisha shauri hilo Mahakama Kuu kukazia hukumu ya mahakama na kuitaka kuichukulia hatua tume hiyo. Tamko hilo lilitiwa saini na vyama hivyo nane ambavyo ni ACT Wazalendo, CCK, Chadema, DP, NCCR-Mageuzi, NLD, UPDP na Chauma. NEC YANENA Kutokana na madai hayo, MTANZANIA ilimtafuta Mkurugenzi wa NEC, Dk. Athumani Kihamia, ambaye alisema kuwa hawajaingilia wala kudharau mahakama bali wametumia utaratibu mwengine ambao hautaathiri uchaguzi. “Sisi NEC tupo sahihi, hatujadharau mahakama na wala hatutadharau amri ya mahakama yoyote itakayotolewa kwa maana kwa mujibu wa kifungu cha 7(1) na 7 (3) vya sheria ya sura ya 343 hatujagusa wala hatujaathiri uchaguzi, utafanyika kwa utaratibu mwengine mpaka rufaa itakapoisha,’’ alisema Dk. Kihamia.
3kitaifa
WAKATI kocha wa Yanga SC, Charles Mkwasa, akiendelea kutupa vijembe vya kuwafunga wapinzani wao Simba SC kwenye mchezo wao wa mwishoni mwa wiki hii, kikosi hicho leo kimetamba kuendeleza makali yake dhidi ya Biashara United katika mchezo wa Ligi Kuu Bara utakaochezwa Uwanja wa Uhuru Dar es Salaam.Yanga wanaingia kwenye mchezo huo wakiwa na hasira ya kuendeleza dozi ya kichapo lengo likiwa ni kuongeza idadi ya pointi kutoka 21 na kufikisha 24 na kuishusha Kagera Sugar.Yanga wanaoshika nafasi ya tano wanaingia kwenye mchezo huo wa 11 wakiwa na ari ya ushindi baada ya kuifunga Tanzania Prisons kwa bao 1-0 na kuvunja rekodi iliyowekwa na timu hiyo kushindwa kupoteza mchezo toka walipoanza msimu, wanakutana na Biashara ambayo ina morali ya kuibuka na ushindi kwenye michezo miwili iliyopita licha ya kushika nafasi ya 15 kwenye msimamo wa ligi wakiwa na pointi 15.Mchezo huo unatarajiwa kuwa mgumu kwani toka Biashara imepanda ligi hiyo msimu uliopita ni miongoni mwa timu inayoleta ushindani mkali kila inapokutana na Yanga. Aidha rekodi zinaonesha kwa msimu uliopita timu hizo zilipokutana kwenye michezo ya ligi hiyo Yanga ilishinda mara moja kwa mabao 2-1 Uwanja wa Taifa na mchezo wa mzunguko wa pili Biashara ilishinda kwa bao 1-0 kwenye uwanja wa Karume Mara .Kocha Mkwasa alisema ushindi walioupata kwenye mchezo wa juzi umewapa nguvu na huo ni mwanzo wa kuvuna matokeo mapya kuchagiza mbio zao za ubingwa.
5michezo
WAKATI timu ya soka ya taifa ya Bara Kilimanjaro Stars ikifungwa na Kenya bao 1-0 wenzao Zanzibar, Zanzibar Heroes wakitoshana nguvu na Sudan kwa kufungana bao 1-1 mwelekeo wa awali unaonekana kuwa mgumu kwa timu hizo za Tanzania.Timu hizo jana zimetupa karata zao za mwanzo katika ufunguzi wa michuano ya Baraza la Vyama vya soka vya Afrika Mashariki na Kati (CECAFA) jijini Kampala.Mchezo wa Kilimanjaro Stars na Harambee Stars ambao ulichezwa saa 10:00 jioni ulitabiriwa kuwa mgumu kwa kila timu kwa sababu, kila mmoja amejipanga kupambana kupata pointi tatu katika mchezo huo wa kwanza.Utabiri huo ulionekana kuwa kweli kwani Kenya walifanya shambulizi la kwanza dakika ya nne na kupata bao lililofungwa na Hassan Abdallah na kudumu kwa muda wote wa mchezo Tanzania na Kenya zinapokutana mechi huwa ngumu kutokana na kujuana kwani zimeshakutana mara kadhaa katika michuano tofauti iliyopita na katika michuano miwili ya Cecafa mwaka 2013 na 2017 Kenya ilishinda zote bao 1-0 kila mmoja.Zanzibar Heroes ambayo ilicheza mchezo wake mchana walianza kupata bao dakika ya 55 lililofungwa na Makame Musa lakini dakika 90 Montasir Yahya wa Sudan aliisawazishia timu yake na hivyo mchezo kumalizika kwa sare.Zanzibar sio mara ya kwanza kukutana na Sudan kwenye michuano hiyo, mwaka 2007 ziliwahi kutoka sare ya mabao 2-2 kisha 2010 Zanzibar ilishinda mabao 2-0. Kwa matokeo hayo Kenya inaongoza Kundi B ikiwa na pointi tatu, Zanzibar na Sudan zikifuatia zikiwa na pointi moja kila moja na Tanzania Bara haina pointi.Tanzania Bara itarejea tena uwanjani Desemba 10 kumenyana na Zanzibar kabla ya kukamilisha mechi zake za kundi hilo kwa kuikabili Sudan Desemba 14.Mashindano hayo yanaendelea leo kwa Kundi A ambapo Eritrea itacheza na Uganda na Burundi itaivaa Djibouti.Wakati huo huo timu ya Tanzania Bara ya wasichana waliochini ya Umri wa miaka 17, leo inashuka kwenye dimba la FUFA Technical Centre, Njeru, Jinja, Uganda kucheza na Eritrea katika mchezo wa mashindano ya Baraza la Vyama vya soka vya Afrika Mashariki na Kati (CECAFA)Mchezo wa Tanzania Bara na Eritrea utakaochezwa saa 5:00 asubuhi utakuwa wa kufungua dimba ukifuatiwa na mchezo wa Djibouti na Kenya utakaonza 7:30 mchana na Uganda itaivaa Burundi saa 10:00 jioni.Mashindano hayo ambayo yanachezwa kwa mtindo wa ligi yatamalizika Desemba 18 leo yatakuwa mapumziko
3kitaifa
Mwandishi Wetu Waziri wa Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi), Suleiman Jafo mepigilia msumari sakata la watumishi wa Hospitali ya Mji wa Bariadi wasichangishwe fedha kufidia mashine ya Ultrasound iliyoibwa hospitalini hapo. Jafo ametoa kauli hiyo leo Alhamisi Agosti 15, kauli ambayo inamuunga mkono Katibu Tawala wa Mkoa wa Simiyu, Jumanne Sagini ya kutaka watumishi hao wasilipishwe fedha kama walioamriwa na Mkuu wa Wilaya ya Bariadi, Festo Kiswaga jana Jumatano Agosti 14. Pamoja na mambo mengine, Jafo amemtaka Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Anthony Mtaka kuunda tume ya uchunguzi ili kuwabaini waliohusika na wizi wa mashine hiyo. “Kulikuwa na maelekezo kuwa wale watumishi 137 walipie ile mashine kwa kukatwa kwenye mshahara yao, nielekeze kwamba watumishi wetu hawa wanafanya kazi katika mazingira magumu sana, na tukumbuke hata tulipopata janga pale Morogoro watumishi wetu wa idara ya afya muda mwingi ndiyo walikuwa kimbilio kuwasaidia wananchi. “Kitendo kama hiki ni kuwakatisha tamaa na kuwaweka katika ya sintofahamu lakini kumbe inawezekana kuna watu walihusika. Lengo hapa ni kuwatafuta waliohusika, wabainishwe ni kina nani wachukuliwe hatua lakini pia wahakikishe mashine hii inarudi. “Kwa hiyo nitoe maelekezo kuwa watumishi hawa wasichangishwe fedha ya aina yoyote kwa sababu siyo jukumu lao, ni jukumu la ulinzi kwa hiyo Mkuu wa Mkoa namuelekeza kwanza aunde tume ya uchunguzi kuwabaini wahusika na watumishi hao waachwebwafanye kazi kwa sababu tunawategemea sana haipaswi kuwabebesha mzigo usiowahusu,” amesema Jafo. Mashine hiyo iliibiwa hospitalini hapo Agosti 5, mwaka huu ambapo jama mkuu wa wilaya alitoa agizo kwa watumishi hao kuchangia kulingana na mishahara yao ili kufidia mashine hiyo jambo lililopingwa na Sagini ambaye leo mchana alitangaza kutengua agizo hilo.
3kitaifa
Hayo yalisemwa na Ntibenda wakati alipowahutubia wafanyakazi katika maadhimisho ya Siku ya Wafanyakazi Duniani kimkoa yaliyofanyika jana Viwanja vya Shehe Amri Abeid jijini Arusha. Aliwasihi wafanyakazi kutumia vyema vyama vya wafanyakazi mahali pa kazi ili walete maendeleo kati ya waajiri pamoja na wafanyakazi wenyewe.Alisema ni vyema wafanyakazi wakatumia vyama vyao vya wafanyakazi mahali pa kazi ili kuzungumza mambo yao mbalimbali na kusuluhisha, badala ya waajiri kuwazuia ili kuleta maendeleo.Alitoa rai kwa waajiri kuacha tabia ya kutowapa mikataba ya ajira wafanyakazi wao, badala yake washirikiane kwa pamoja katika kuleta maendeleo, kwani kampuni ikipata maendeleo wanaostahili pongezi ni wafanyakazi mnaoshirikiana nao kwa pamoja.“Fanyeni kazi na mtumieni vyama vya wafanyakazi katika kaleta maendeleo badala ya kuvitumia vyama vya wafanyakazi katika kuleta maendeleo nanyi waajiri acheni tabia ya kuwazuia wafanyakazi katika kuleta maendeleo badala ya kuwakandamiza,” alisema Ntibenda.Pia alisema serikali ipo mbioni kufufua viwanda pamoja na reli ili kuinua sekta ya viwanda pamoja kuinua uchumi kwa mkoa wa Arusha na kusisitiza vijana kufanya kazi badala ya kukimbilia kucheza ‘pool table’ pamoja na kupiga debe kwa kuwanyang’anya wananchi vitu vyao.Cosmas Chikoti ambaye ni Mwenyekiti wa Muungano wa Vyama vya Wafanyakazi mkoa wa Arusha, aliomba serikali iangalie maslahi bora kwa wafanyakazi ikiwemo mikataba ya ajira pamoja na kusisitiza kuwa na mahusiano mema kati ya waajiri na waajiriwa.Hafla hiyo ilienda sambamba na maandamano ya wafanyakazi pamoja na kutoa zawadi kwa wafanyakazi bora ambapo pia wananchi mbalimbali walihudhuria ikiwemo wakuu wa wilaya za Arusha, wakurugenzi watendaji wa halmashauri na makatibu tawala mkoa na wilaya.
1uchumi
Na Hadija Omary, Lindi Mamlaka ya Bandari Tanzania (TPA), Kanda ya Mtwara imezipatia vifaa tiba vyenye thamani ya Sh milioni 33.3 halmashauri mbili za mkoa wa Lindi kwa lengo la kuboresha huduma mbalimbali za afya kwa wananchi wake. Vifaa hivyo ni pamoja na vitanda vinane kwa ajili ya kujifungulia na darubini sita zikazofanya kazi za kiuchunguzi wa kimaabara katika vituo mbalimbali vya afya. Akizungumza wakati wa kukabidhi vifaa hivyo kwa uongozi wa halmashauri hizo, Meneja wa Bandari mkoani Mtwara Nelson Mlali amesema lengo la kutoa msaada huo ni kuboresha huduma za Afya kwa wananchi. “Sisi tunaanza tu, lakini wenzetu wengi wanatusikia, nina imani watajitokeza kutuunga mkono ili kutatua changamoto hizi za afya kwani ni wazi kwamba changamoto za sekta ya afya ni nyingi na hatutaweza kuzimaliza kwa siku moja au kumaliza kwa kujitolea kwa taasisi nyingine hivyo natoa wito kwa taasisi nyingine kuunga mkono jitihada hizi,” amesema Mlali. Meya wa Manispaa ya Lindi, Mohamed Lihumbo ameishukuru mamlaka hiyo kuwa msaada huo na kuongeza kuwa umefika kipindi muafaka wakati ujenzi wa vituo vipya vya afya ukiendelea kwenye kata mbalimbali. Kwa upande wake Mganga Mkuu wa Wilaya ya Lindi, Dk. Ally Zuberi na Mganga Kituo cha Afya cha Mjini cha Manispaa Lindi, Richard Juma wamesema upatikanaji wa vifaa hivyo utawasaidia kutekeleza majukumu ya utoaji bora wa huduma kwa wagonjwa wanaofika kupata tiba.
3kitaifa
  Na RAMADHAN HASSAN – Dodoma MBUNGE wa Singida Mashariki, Tundu Lissu (Chadema), jana aliibuka bungeni na kusema Rais mstaafu, Jakaya Kikwete, hawezi  kupona kwenye sakata la mchanga wa madini wakati yeye ndiye mtu wa kwanza kusaini mikataba mikubwa ya madini nchini ambayo inapigiwa kelele leo. Akichangia jana jioni kwenye bajeti Kuu ya Serikali, Lissu alisema kamati ya pili iliyomkabidhi Rais Dk. John Magufuli ripoti yake juzi, imewagusa baadhi ya mawaziri, wanasheria na makamishna wa madini huku ikimwacha Kikwete. “Mtu wa kwanza kusaini mikataba na leseni za madini  tarehe 5 mwezi Agosti mwaka 1994 ni Meja Jakaya Mrisho Kikwete, leseni ya Bulyanhulu  hii inayopigiwa kelele leo, ilisainiwa na Jakaya Kikwete akiwa Waziri wa Maji, Nishati na Madini. “Hakuwa na kinga ya urais wakati ule kama aliyonayo leo. Kuhusiana na masuala aliyoyafanya wakati hajawa Rais na alisaini leseni, sio ya Bulyanhulu peke yake, ya Nzega na Geita, hizo leseni zina saini ya Kikwete, anaponaje? “Kwa mapendekezo haya anaponaje? Kama mnataka kweli kushughulikia watu wanaoshiriki mambo haya, mbona mnachagua chagua? “Hizi leseni na hizi sheria tatizo kubwa ni sheria za Tanzania tangu mwaka 1999, wenye kujua tumesema tatizo kubwa ni sheria za Tanzania, sisi ni wanachama wa mkataba wa kimataifa wa kulinda wawekezaji, sisi tumesaini mikataba na nchi moja moja zenye wawekezaji Tanzania, nchi 26 mikataba ya kulinda wawekezaji hawa. “Mheshimiwa Spika kama kuna mchango ambao utakumbuka ni kupiga marufuku hii habari ya Certificate of Agency, kwenye utungaji sheria imetuletea matatizo makubwa na ‘mabomu’, sheria za gesi asilia na mafuta mlizotufukuza hapa na mkazipitisha ni ‘mabomu’ matupu. “Katika taarifa hii ya jana, wamependekeza watu fulani fulani washughulikiwe; mawaziri, makamishna, Mwanasheria Mkuu bwana Chenge, Ngeleja, naombeni niwaambie kitu ili muwe na maarifa,” alisema Lissu. Alisema yeye siyo  mtaalamu wa maandiko matakatifu, lakini kuna sehemu katika maandiko hayo inayosema kuwa watu wa Mungu wanaangamia kwa kukosa maarifa. “Asubuhi umesema kwamba haya masuala ya madini yanahitaji semina, hilo ni jambo muhimu sana Mheshimiwa Spika kwa sababu hoja hiyo inahitaji maarifa sana na haiwezi kujadiliwa kwa hizi dakika tano tano au kumi kumi. “Nataka nijikite katika masuala ya madini kwa sababu ambazo zipo wazi kabisa, Kamati ya Rais ya Profesa Osoro na Kamati ya Profesa Mruma iliyopita, si ripoti za kwanza kuzungumzia na kuchunguza matatizo katika sekta ya madini katika nchi hii na Rais Magufuli si wa kwanza. “Mwaka 2002 Rais Mkapa  aliunda kamati iliyoongozwa na Mboma ambayo inaitwa Kamati ya Mboma, iliundwa kuchunguza matatizo katika sekta ya madini, hasa hasa madini ya vito vya thamani. “Mwaka 2004 Waziri Mkuu Frederick Sumaye, Serikali ya Mkapa iliunda Kamati ya Dk. Jonas Kipokola kuchunguza matatizo ya sekta ya madini, taarifa yake ni ya Agosti 2004, mwaka uliofuata 2005 Rais Mkapa na Serikali yake waliunda Kamati ya Bukuku, alikuwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha, kuchunguza matatizo ya sekta ya madini. “Mwaka 2006 miezi michache baada ya Rais Kikwete kutawazwa kuwa rais, akaunda Kamati ya Law Masha, bahati nzuri nimekuja na taarifa yake  hii hapa. “Kamati ya Law Masha iliundwa kuchunguza sheria za madini, kodi na fedha na mikataba ya madini na kila kitu cha madini, taarifa hii hapa. “Mwaka 2008 baada ya mgogoro wa Buzwagi hapa bungeni, Rais Kikwete aliunda Kamati ya Jaji Mark Bomani hii hapa, Kamati ya Bomani taarifa yake ni ya Aprili 2008. “Kamati ya Osoro na Mruma ni kamati ya sita kuundwa kushughulikia masuala ya madini, sasa nimekuja na muhtasari wa Kamati ya Profesa Oroso. “Naweza nikawaambia waheshimiwa wabunge hadidu za rejea za Kamati ya Mruma na Osoro ni zile zile zilizokuwa hadibu za rejea za Kipokola, Bukuku za Law Masha na za Kamati ya Bomani, matokeo yake, ‘Finding na Recommendation’ zipo hapa kwa kiasi kikubwa na Finding na Recommentantion zilizokuwa kwa Bukuku Kipokola Masha na Bomani hazijawahi kutekelezwa. “Watu ambao wameuza madini ya nchi hii walipitisha sheria kwenye Bunge hili hili na ndio maana inashindikana,” alisema Lissu. Akihitimisha Bunge jana jioni, Spika Ndugai, alisema amepokea ushauri wa Lissu kuhusu kutokubali kupitisha sheria kwa hati ya dharura na kusema endapo Serikali italeta sheria kwa dharura juu ya sheria za madini ama gesi, Bunge halitazipitisha kwa kuwa nchi imeibiwa vya kutosha.
3kitaifa
MADRID, HISPANIA MSHAMBULIAJI wa timu ya Atletico Madrid, Fernando Torres, ameendelea kuikumbuka kadi nyekundu ambayo alioneshwa katika mchezo wa robo fainali ya kwanza ya Ligi ya Mabingwa dhidi ya Barcelona na kudai kwamba bila kadi hiyo Atletico ingeshinda. Katika mchezo huo ambao ulipigwa kwenye Uwanja wa Nou Camp, Atletico walikuwa wa kwanza kupata bao, lakini Barcelona walifanikiwa kupata bao la kusawazisha na kuongeza katika ushindi wa mabao 2-1. Bao la pili la Atletico lilifungwa huku Atletico wakiwa pungufu baada ya mshambuliaji huyo kuoneshwa kadi nyekundu kutokana na utovu wa nidhamu na kuoneshwa kadi mbili za njano. Hata hivyo, Torres amedai kwamba wangeshinda mchezo huo kama wangeendelea kuwa 11. “Bado ninaifikiria kadi ambayo nilioneshwa kwenye mchezo wa robo fainali kwenye Uwanja wa Nou Camp, ninaamini tulikuwa na kila sababu ya kushinda kama tungeendelea kuwa 11 uwanjani. “Kadi ya kwanza ya njano ilikuwa sahihi, lakini ya pili haikuwa sahihi, ila ndicho kilichotokea na ninaamini mchezo wa kesho (leo) tunaweza kushinda nyumbani,” alisema Torres. Timu hizo zinatarajia kushuka dimbani leo hii kwa ajili ya marudiano ambapo lazima mmoja ayaage mashindano baada ya mchezo huo kumalizika.
5michezo
  Na MASYENENE DAMIAN, MAHAKAMA Kuu ya Tanzania Kanda ya Mwanza  imetupilia mbali kesi ya katiba iliyofunguliwa na Umoja wa Klabu za Waandishi wa Habari Tanzania (UTPC) na kampuni ya Hali Halisi Publishers kupinga sheria ya huduma za vyombo vya habari. Shauri hilo namba 2/2017 lilifunguliwa Januari 18, mwaka huu katika mahakama hiyo. Lilikuwa likisikilizwa na Jaji Jacquline De-Mello ambaye amelitupilia mbali kwa vile  mahakama hiyo kutokuwa na uwezo wa kulisikiliza. Shauri hilo lilitajwa jana ili kutolewa uamuzi kwa mapingamizi matano yaliyowasilishwa na serikali Februari 10, mwaka huu kupinga kusikilizwa   shauri hilo. Serikali lidai Mahakama hiyo haina uwezo wa kulisikiliza shauri hilo hivyo kuomba ilifute kwa gharama. Akisoma uamuzi wa mahakama hiyo, Jaji De-Mello alisema shauri hilo linatupwa kwa sababu liko katika mahakama isiyo na mamlaka ya kulisikiliza.   Akizungumza na MTANZANIA   nje ya mahakama jana,  Wakili wa walalamikaji, Edwin Hans alisema wao hawalalamikii uamuzi wa Waziri wa Habari, Sanaa na Michezo, Nape Nnauye ya kutunga kanuni za habari. Alisema wanachopinga ni sheria ya huduma za vyombo vya habari iliyotungwa na Bunge.   “Hukumu hii haina logic (mantiki) kabisa, sisi tunaipinga sheria hatupingi uamuzi wa waziri sasa wanavyotutaka twende ‘Judicial review’ hatuelewi kabisa. “Judicial review unaenda ukiwa unataka kuomba kibali cha mahakama kutengua uamuzi wa mtu ama taasisi.
3kitaifa
WAZIRI Mkuu, Kassim Majaliwa amewaagiza wakuu wa mikoa nchini, wahakikishe wanasimamia ipasavyo ujenzi wa vyumba vya madarasa vikamilike kwa wakati ili wanafunzi wote waliochaguliwa kujiunga na kidato cha kwanza mwaka 2020 waanze masomo kwa pamoja.Amesema lengo la serikali ni kuhakikisha wanafunzi wote wanaanza kusoma kwa pamoja, kwa sababu wakipishana muda wa kuanza masomo, baadhi yao wanashindwa kufanya vizuri, jambo ambalo si sahihi.Kwa mujibu wa taarifa ya Ofisi ya Waziri Mkuu kwa vyombo vya habari, Waziri Mkuu alitoa agizo hilo jana wakati akitoa Taarifa ya Utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) ya 2015/2020 kwenye Mkutano wa Halmashauri Kuu ya CCM Wilaya ya Ruangwa.Jumla ya watahiniwa 933,369 sawa na asilimia 98.55 ya waliosajiliwa, walifanya mtihani wa kumaliza elimu ya msingi mwaka huu na kati yao watahiniwa 759,737 wamefaulu ambao ni sawa na asilimia 81.50.Kati yao wasichana ni 395,738 ambao ni sawa na asilimia 80.87 na wavulana ni 363,999 sawa na asilimia 82.20. Mwaka jana watahiniwa waliofaulu walikuwa asilimia 77.72, hivyo kuna ongezeko la ufaulu kwa asilimia 3.78. “Wakuu wa mikoa hakikisheni vyumba vya madarasa vinakamilika ili wanafunzi wote waliofaulu waanze masomo kwa pamoja.Kitendo cha wanafunzi kupishana kuanza masomo kinawafanya waliochelewa kutofanya vizuri katika mitihani yao,” alisema Waziri Mkuu. Kadhalika, aliwasisitiza viongozi hao, wahakikishe wanasimamia vizuri elimu kwa watoto wa kike na kuwachukulia hatua watu wote, watakaobainika kuwakatisha masomo iwe kwa kuwaoa, kuwaozoesha au kuwapa ujauzito.Alisema serikali imeweka sheria kali ya kumlinda mtoto wa kike, lengo ni kumuwezesha amalize masomo yake ili ajikwamue kiuchumi na aondokane na utegemezi, hivyo ni marufuku kuwakatisha masomo.“Watoto wa kike wanatakiwa kuheshimiwa katika jamii na serikali itatoa adhabu kali ya kifungo cha miaka 30 jela kwa mtu atakayekatisha elimu ya mtoto wa kike iwe kwa kumuoa au kumpa ujauzito,” alisema.Alisema serikali inataka kuona idadi kubwa ya watoto wa kike, wanatimiza malengo yao kielimu, hivyo ni lazima wakaondolewa vishawishi kwa kuboresha mazingira yao ya kujifunzia ikiwamo kuongeza idadi ya mabweni.Wakati huo huo, Waziri Mkuu ameishukuru Serikali ya Awamu ya Tano inayoongozwa na Rais Dk John Magufuli kwa kutoa fedha nyingi kwa ajili ya utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo nchini, ikiwamo wilaya ya Ruangwa ambayo imepewa Sh bilioni 38 kwa ajili ya utekelezaji wa miradi ya kimkakati.Alitumia fursa hiyo kuupongeza uongozi wa Halmashauri ya Wilaya ya Ruangwa, kwa kubuni mradi wa kimkakati wa ujenzi wa ghala la kuhifadhia mazao na pembejeo, linalojengwa katika Kijiji cha Lipande kwa gharama ya Sh bilioni 5.45.Ghala hilo ambalo limeanza kutumika lina uwezo wa kuhifadhi tani 20,000, litaiwezesha halmashauri kujiongezea mapato ya ndani na kusaidia kupunguza utegemezi kutoka Serikali Kuu na wafadhili. Pia litapunguza gharama za usafirishaji wa korosho, walizokuwa wanatozwa wakulima wakati wa kusafirisha mazao.Alisema katika kipindi cha miaka minne ya Serikali ya Awamu ya Tano, miradi mingi ya kimkakati imetekelezwa nchini ambayo ni pamoja na ujenzi wa reli ya kisasa (SGR), upanuzi wa bandari za Mtwara, Dar es Salaam na Tanga, uboreshwaji wa viwanja vya ndege, ununuzi wa rada na ununuzi wa ndege mpya.Alisema Serikali ya Awamu ya Tano tangu ilipoingia madarakani mwaka 2015, kipaumbele chake kilikuwa ni kukuza kiwango cha uchumi kutoka cha chini kwenda cha kati ifikapo mwaka 2025 kupitia sekta ya viwanda.
3kitaifa
AGIZO la Rais John Magufuli la kutaka kila kijiji kupata umeme, limeungwa mkono na Mtanzania anayeishi nchini Poland, Julius Zellah, ambaye amejitolea kuzalisha nishati ya umeme katika eneo la Ilungu, Mbeya Vijijini.Kampuni ya Mtanzania huyo, ya Texpol Development Company (TDC) Limited, kwa kushirikiana na Light for Africa ya Poland ambayo ni taasisi ya Diaspora wa Tanzania nchini humo, zimechukua hatua ya kusaidia wananchi waishio katika vijiji vya eneo hilo kuwa na umeme, unaotokana na maporomoko ya maji kwenye mito mikubwa na milima.Akizungumza kutoka Poland, Zellah ambaye ni mlezi wa mradi huo, anasema wamepania kumsaidia Rais Magufuli na Waziri wa Nishati, Dk Merdad Kalemani. Anampongeza Rais Magufuli, kwa hatua anazochukua za kuhakikisha wananchi wanyonge na wenye kipato cha chini, wanapata umeme ili uwasaidie kurahisisha huduma za jamii, ikiwemo zahanati na shule na kwa ajili ya uzalishaji mali, kama viwanda vidogo. Zellah anamuomba Dk Kalemani kutembelea Ilungu, kukagua mradi ulipoishia na kumalizia vijiji vilivyobaki ili wananchi wapate nishati hiyo waliyoisubiri tangu uhuru. Anasema ni faraja kubwa kwa Serikali kuona wananchi hao wanatoka kwenye giza na kupata mwanga.Zellah amewajengea bure chanzo cha umeme wananchi wa vijiji 10 vya Kata ya Ilungu katika Wilaya ya Mbeya Vijijini, bila kutumia fedha za serikali. Anasema huo ni mchango wake kwa serikali ambayo imepania kujenga viwanda. Vijiji vilivyopata umeme ni Ifupa, Shango, Itiwa, Mwela, Mashese, Ngole, Nzumba, Isyonje, Nyalwela A na Nyalwela B.Katika mradi huo, ameweza kupeleka umeme na maji katika Shule ya Sekondari ya Serikali ya Ilungu, shule sita za msingi na zahanati tano. Umeme huo umepelekwa pia kwenye nyumba zote za wafanyakazi wa taasisi za serikali katika kata hiyo. Kata ya Ilungu haifikiki kwa urahisi kwa sababu iko milimani, karibu meta 2,800 kutoka usawa wa bahari.Usafiri huwa ni mgumu maradufu wakati wa kipindi cha mvua. Kata hiyo ya Ilungu iko umbali wa kilometa 52 kutoka Mbeya mjini. Ipo katika barabara inayounganisha miji ya Mbeya na Njombe na inapakana na Kata za Kitulo, Makete, Igurusi, Igoma na Irambo. Kazi ya kujenga miundombinu hiyo ya umeme,ilianza mwaka 2013 baada ya wakazi wa Kijiji cha Ifupa kumsomea risala ndefu Zellah ya kukosa umeme, ulioahidiwa na Shirika la Umeme nchini (Tanesco) zaidi ya miaka 10.Mtanzania huyo aliwasihi wananchi wa kata yote ya Ilungu wasiilaumu serikali kutokana na kuwa na majuku mengi, bali wampe baraka zao aweze kuwajengea miundombinu ya kuzalisha umeme; na washirikiane naye katika kazi hiyo ngumu na yenye gharama kubwa. Hadi mwaka 2018, mradi huo ulikuwa umekamailika kwa asilimia karibu 90 na wananchi zaidi ya 16,000 wamenufaika na umeme huo.Gharama za ujenzi wa kazi hiyo hadi sasa ni takribani Sh bilioni 6.8 na utakapokamilika, itakuwa Sh bilioni 7.4. Zellah na kampuni yake ya Texpol, alikubaliana na Wakala wa Umeme Vijijini (Rea) kuwa mradi wa Ilungu utakapopatikana fedha ya serikali itaenda kuokoa maeneo mengine ya mkoani Mbeya. Baadaye ilipopatikana pesa ya serikali, Rea walitumia fursa hiyo kusambaza umeme katika Wilaya ya Chunya, kitu ambacho ni faida kubwa kwa Serikali ya Tanzania.Baada ya kumaliza usambazaji umeme, Zellah alianza jitahada za kujenga umeme wa maji kwa kutumia maporomoko ya Mto Ishinga, nje kidogo ya Kijiji cha Mwela. Ili kufanikisha kazi hiyo, kampuni hiyo ya Texpol ikishirikiana na taasisi ya Light for Africa Foundation kutoka Poland, inayounga mkono mradi huo, walianza kutafuta vyanzo vya fedha kutoka taasisi za fedha Poland.Walilenga kukamilisha umeme kwenye maeneo mengine ya vijiji vya Kata ya Ilungu na uliobaki kuunganisha kwenye mkongo wa taifa. Vijiji vilivyobaki kuunganishwa ni Nyalwela C, Nkumburu na Mabande, vyenye watu zaidi ya 6,000. Taasisi ya Light for Africa Foundation ikiongozwa na Alicja Bajowska (Mama Waka Waka) kutoka Poland, wamesaidia miradi kadhaa ya jamii katika Wilaya ya Mbeya Vijijini, ikiwemo kupeleka majiko ya kisasa, viti na meza 200.Vingine ni vitanda 123 vya chuma kwa mabweni ya wasichana wa Shule ya Sekondari ya Serikali ya Ilungu, ambako kwa muda mrefu wanafunzi walikuwa wanalala sakafuni na kusababisha waugue kila mara. Pia, taasisi hiyo imepeleka vifaa vya afya 500 (mama kit) vya kisasa vya kusaidia akina mama wakati wa kujifungua. Mwaka juzi Balozi wa Poland nchini Tanzania, Dk Ewelina Lubieniecka alimkabidhi vifaa hivyo Mganga Mkuu wa Wilaya ya Mbeya Vijijini. Miundombinu ya usambazaji wa umeme ni sehemu ya kuendeleza mradi wa umeme wa maji wa karibu megawati 6.5 katika Kata ya Ilungu, uliobuniwa na kampuni ya Texpol Development Company (TDC) Limited, ikisaidiwa na Light for Africa.Lengo la kuendeleza mradi wa nguvu ya maji ni kuwezesha wananchi wa Kata Ilungu, kupata umeme wa gharama nafuu ili waanzishe viwanda vidogo kama vile useremala, kusaga nafaka, kuchomelea milango na madirisha, kutunza vyakula na kuendesha kwa ufanisi shule na vituo vya afya. Umeme wa maji utasaidia pia kurudisha gharama kubwa, zilizotumika kujenga miundomninu ya umeme kwa kata nzima.Ikumbukwe kuwa, tangu mwaka 2003, wananchi wa Kijiji cha Ifupa Kata ya Ilungu, wamekuwa wakiomba umeme kutoka Tanesco na kuahidiwa kupata nishati hiyo huku wakitakiwa kufanya kutandaza nyaya (wiring) katika nyumba zao. Baadhi walitandaza nyaya hizo, lakini hadi 2013 TDC ilipokubali mchakato wa kujenga mradi wa umeme, wakawzi walikuwa hawajapata umeme kutoka Tanesco.Wakati utafiti wa uwezekano wa mradi wa umeme wa maji unaendelea, TDC iliona kuwa ni busara kujenga miundombinu ya usambazaji karibu na eneo la mradi ili umeme huo usaidie pia wananchi. hadi makala haya yanakwenda mitamboni, Texpol bado haijamaliza mradi wake kutokana na pesa yote kutumika kwenye miundombinu ya umeme huo. Kampuni ya Texpol ilihamasishwa na wananchi wa kata nzima na ikatoa fedha kwa ajili ya ujenzi wa miundombinu ya usambazaji umeme. Pesa hiyo ilitoka ndani na nje ya nchi, hasa Poland anakoishi Mtanzania huyo, Zellah, ambaye ni Makamu Mwenyekiti wa Diaspora Tanzania nchini Poland.Ujenzi wa miundombinu hiyo ulianza kwa kilovoti 33 kutoka mkongo wa Tanesco unaotoka Mbeya kwenda Makete na kupeleka umeme huo hadi Kijiji cha Ifupa na baadaye, kata nzima ya Ilungu. Umeme huo ulijengwa chini ya usimamizi wa Tanesco. Texpol walilipa ada zote zinazohitajika kwa Tanesco kwa kusimamia kazi hiyo ngumu.Kampuni ya Texpol ilipata nyaraka zote muhimu za kisheria kwa kazi hiyo, ikiwemo leseni ya uuzaji umeme kutoka Tanesco. Vibali vingine vya kisheria ni kutoka Wizara ya Nishati, REA, MFA, NEMC, TANESCO, TIC na Mamlaka ya Bonde la Maji Rufiji.Zellah na Mama Waka Waka wanawataka Watanzania duniani kote, wasisubiri serikali ifanye kazi hiyo peke yake, bali waige mfano huu na kuisaidia kuzalisha umeme mbadala na kuusambaza kwa wananchi katika maeneo ambayo serikali bado haijafanya hivyo. Hatua hiyo itawezesha vijiji vyote vya Tanzania, kupata umeme kwa muda mfupi na kwa gharama ndogo.
3kitaifa
Kwa mujibu wa Dk Kigoda, lengo la kufanya hivyo ni kuwapa maofisa wa viwango wa ZBS wigo mpana wa kujifunza masuala hayo, ili waende sambamba na wenzao wa TBS katika kudhibiti ubora wa bidhaa.Kigoda alilieleza gazeti hili Dar es Salam jana kuwa ushirikiano wa hivi karibuni kati ya mashirika hayo mawili unalenga kuhakikisha bidhaa zinazoingizwa sokoni ni boa, kulingana na viwango vya kitaifa vilivyowekwa.“Kwa sasa ni lazima TBS iibebe sana ZBS kwa sababu ndilo shirika lililotangulia na lina uzoefu wa kutosha katika masuala ya kudhibiti ubora. “...Ili kufanikisha lengo hilo, nafasi za mafunzo ya upimaji na udhibiti viwango zitakazotolewa kwa TBS zitahusisha ZBS pia. Ziara za TBS kwenda nje kutembelea mashirika ya viwango nazo zitawahusisha maofisa wa ZBS, ili wasibaki nyuma,”Dk Kigoda alisema.Aliongeza kuwa idadi ya maofisa wa ZBS watakao husika katika mialiko ya kimafunzo itakayoletwa au kutafutwa na TBS kuwa haitakuwa maalumu, ingawa shirika hilo linalotajwa kuwa mama litakuwa na nafasi kubwa zaidi.Wakati akizungumzia mafunzo ya udhibiti viwango hivi kaibuni, Waziri wa Biashara, Viwanda na Masoko wa Zanzibar, Nasor Ahmed Mazrui alisema, wanategemea kujifunza zaidi kutoka kwa maofisa wa TBS kwa sababu ni wazoefu zaidi yao.
1uchumi
RAIS wa Zanzibar, Dk Ali Mohamed Shein amesema ili kutekeleza sera ya elimu bila malipo, serikali inaendelea na juhudi za kuimarisha miundombinu ya kielimu ili kwenda sambamba na mahitaji yaliyopo.Alisema hayo jana katika uwekaji wa jiwe la msingi Shule ya Msingi Kwarara, Wilaya ya Magharibi ‘B’ Unguja. Alisema kutokana na ongezeko kubwa la wanafunzi hali inayotokana na kiwango kikubwa cha wakazi wa Zanzibar, serikali inalazimika kuongeza idadi ya madarasa shule za msingi na sekondari.Alisema ongezeko la watu kutoka 300,000 mwaka 1964 hadi milioni 1.5 imefanya kuwepo mahitaji makubwa ya madarasa huku baadhi ya shule zikiwa na wanafunzi wanaofikia 234 katika darasa moja. Alisema hivi karibuni serikali imeagiza madawati na madawati 44,000 kutoka nchini China na kubainisha kuwa nusu ya samani hizo zimewasili nchini na kugawiwa katika shule za msingi na sekondari zilizopo.Dk Shein alisema azma ya serikali ni kuwataka wazazi na walezi wa wanafunzi kutokuchangia huduma za kielimu shule za msingi na sekondari za vitabu na madaftari. Alisema lengo la serikali ni kuwaandaa vijana kielimu kuwa na wataalamu wa fani mbali mbali kuliwezesha Taifa kupata maendeleo ya haraka.Alisema uchumi wa Zanzibar unaimarika kadri miaka inavyosonga mbele kuokana na makusanyo mazuri ya mapato na kubainisha kuwa hivi sasa serikali inakusanya kati ya Sh bilioni 65 hadi 70 kwa mwezi, hivyo kumudu gharama za uendeshaji wa miradi mbali mbali ya maendeeo ikiwemo ya maji na barabara. Alisema hali hiyo imechangia kufanikisha azma ya serikali ya kusomesha wataalamu wa fani tofauti.Dk Shein aliipongeza Taasisi ya Good Neighbor ya Jamhuri ya Korea Kusini kwa kujenga shule hiyo. Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali, Riziki Pembe Juma alisema wizara hiyo kwa kushirikiana na Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, Idara Maalumu na Vikosi vya SMZ na Jamhuri ya Korea Kusini italiendeleza jengo hilo katika awamu inayofuata. Waziri Pembe alimhakikishia Rais Shein kuwa huduma za kielimu pamoja na vitabu na madaftari zitaendelea kutolewa bure nchini kote ili kwenda sambamba na Sera ya Elimu.
3kitaifa
WENLING, CHINA WATU takribani 13 wamekufa na zaidi ya milioni moja wamelazimishwa kuondoka katika nyumba zao wakati kimbunga Lekima kikiikumba China. Vyombo vya habari vya Serikali vimechapisha taarifa inayoeleza kuwa watu 16 hawajulikani walipo baada ya kimbunga hicho kuukumba mji wa Wenling . Mji wa Wenling, upo katikati ya Taiwan na Jiji la kibiashara la Shanghai. Awali kimbunga hicho kilielezwa kitakuwa kikubwa, lakini kilipungua baada ya kutokea kikielezwa kuwa na kasi ya kilomita 187 kwa saa (116mph). Kimbunga hicho kimekuja wakati bwawa likivunjika kingo zake huko Wenzhou, karibu na mahali ambako kilitua. Hadi kufikia jana mchana kilikuwa kimepungua kasi kikielekea jimbo la Zhejiang,  huku kikitarajia kuikumba Shanghai, jiji lenye watu zaidi ya milioni 20. Kabla ya kimbunga hicho kutua, mamlaka za China zilikuwa zimejipanga na hata kilipotokea timu ya wafanyakazi wa dharura walikuwa wakionekana kuokoa waendesha magari  waliokuwa wamekwama  kwenye mafuriko. Kimbunga hicho kimesababisha miti kuanguka na umeme kukatika katika maeneo mengi. Inakadiriwa nyumba milioni 2.7 zimekosa umeme, kutokana na kuwapo kwa upepo mkali. Katika jiji la Shanghai tayari mamlaka zilizuia zaidi ya maelfu ya safari za ndege  na huduma za treni ikiwa ni maandalizi ya kukabiliana na kimbunga hicho. Pamoja na kwamba kinatarajiwa kufika Shanghai kikiwa kimepungua kasi lakini bado kinaweza kusababisha athari kutokana na mafuriko makubwa. Wakazi takribani 250,000 wameokolewa, huku wengine  800,000 wa mji Zhejiang wakichukulia kutoka katika majumba yao. Hiki ni kimbunga cha tisa kutokea ndani ya mwaka huu. Shirika la habari la nchini China la Xinhua lilisema kuwa pamoja na kwamba kimbunga hiki ni cha tisa kwa mwaka huu lakini kilikuwa kikali. Jana mchana mamlaka ya hali ya hewa nchini China ilisema kuwa kimbunga hicho kilikuwa kikiondoka kuelekea Kaskazini kwa kasi ya kilomita 15 kwa saa (9mph). Awali wakati kilipopita Taiwani kilisabaisha madhara ikiwamo watu kujeruhiwa na mali nyingi kuharibika. Kimbunga hicho kimekuja siku moja baada ya wataalamu kuonya juu ya kutokea kwa tetemeko lenye mgandamizo sita, hali ambayo kukutana kwa vitu hivyo viwili kwa pamoja kungesababisha mvua kubwa na maporomoko ya ardhi. Wakati kimbunga Lekima kikiwa ni miongoni mwa vimbunga viwili vinavyotikisa sasa Magharibi mwa Pasifiki, upande wa Mashariki unatikiswa na kimbunga Krosa ambacho kimesababisha mvua kubwa katika visiwa vya Mariana na Guam. Utabiri wa hali ya hewa unaonyesha kuwa kimbunga hicho kinaelekea kaskazini magharibi na huenda kikaikumba Japan.
2kimataifa
WASHINGTON, Marekani RAIS mstaafu wa Marekani, Barrack Obama kwa mara nyingine tena amemkosoa mrithi wake, Donald Trump kwa jinsi anavyolishughulikia suala la virusi vya ugonjwa wa corona. Katika hotuba kwa hafla iliyorushwa  kupitia mtandao, alisema  mlipuko wa virusi vya corona umedhihirisha maofisa wengine hawafanyi kazi walioajiriwa kusimamia. Alisema ni ‘janga la machafuko’ jinsi Rais Trump anavyoangazia suala hilo katika mkutano uliovuja wiki iliopita. Obama aliwahutubia wanafunzi wa shule katika sherehe ilioandaliwa na LeBron James na ilikuwa mojawapo ya programu maalumu ambayo ilishirikisha watu maarufu kama vile ndugu wa Jonas, Megan Rapinoe, Pharrell Williams na mwanaharakati wa elimu, Malala Yousafzai. Katika hotuba yake kwa takriban zaidi ya taasisi 10 za wanafunzi weusi na vyuo vikuu, Obama alisema Covid-19 ilifichua mianya na makosa katika uongozi wa taifa hilo. ”Zaidi ya chochote kile janga hili linaonesha wazi  wengi wa maofisa walio uongozini hawajui wanachofanya”, alisema. Zaidi ya watu 1,200 wamefariki kutokana na virusi vya corona nchini Marekani katika kipindi cha saa 24, kulingana na takwimu mpya kutoka Chuo Kikuu cha John Hopkins. Idadi ya watu waliofariki ni 89,000, ambayo ndio ya juu zaidi duniani. Obama pia alizungumzia kwa urefu jinsi virusi hivyo vinavyozidi kuiathiri jamii ya watu weusi nchini humo. ”Ugonjwa kama huu unafichua ukosefu wa usawa uliopo na mzigo wa ziada ambao jamii ya watu weusi wamekuwa wakikabiliana nao katika historia ya taifa hili”, alisema. Idadi kubwa ya Wamarekani weusi, wamekufa na wengine kulazwa hospitalini. Rais huyo wa zamani pia alizungumzia kuhusu mauaji ya Ahmaud Arbery aliyekuwa akifanya mazoezi ya kukimbia  ambaye alipigwa risasi na maofisa wa polisi weupe Februari, mwaka huu – katika hotuba yake. Alisema  ubaguzi wa rangi ulibainika wazi nchini humo wakati mtu mweusi anapofanya mazoezi ya kukimbia na watu fulani wanahisi wanaweza kumsimamisha na kumuuliza maswali na kumpiga risasi, anapokataa kuwajibu. ”Iwapo dunia itaimarika , itategemea nyinyi”, aliwaambia mahafala hao. Obama amenyamaza kwa kipindi kirefu tangu alipoondoka madarakani mnamo Januari, 2017 na hajawahi kuzungumzia kuhusu vitendo vya mrithi wake. Lakini wawili hao, wamekabiliana vilivyo katika siku za hivi karibuni, hatua iliomfanya Rais Trump kumshutumu Obama na washauri wake kwa kuendeleza juhudi za kihalifu kuhujumu utawala wale. ”Ni uhalifu mkuu wa kisiasa katika historia ya Marekani , kwa kiwango kikubwa”, rais huyo aliandika katika mtandao wake wa twitter wiki iliopita.
2kimataifa
ELIZABETH HOMBO, Dar Na GUSTAPHU HAULE, Kibaha RAIS Dk. John Magufuli amesema ndani ya utawala wake hakuna mwanafunzi atakayepata mimba na kuruhusiwa kurudi shuleni. Amezitaka taasisi zinazotetea utaratibu wa wanafunzi waliopata mimba kurudi shuleni, kufungua shule zao za wazazi lakini si kuilazimisha Serikali kufanya hivyo. Rais Magufuli ametoa agizo hilo   siku chache baada ya Taasisi ya HakiElimu kuitaka Serikali kuharakisha kupitia na kupitisha  miongozo  watoto wa kike waliojifungua warejee shuleni na kuendelea na masomo. Mbali na HakiElimu, pia wadau mbalimbali na baadhi ya wabunge wamekuwa wakitetea utaratibu wa wanafunzi wanaopata mimba kurudi shuleni wakitoa sababu mbalimbali za watoto wa kike kubeba mimba. Akizungumza jana akiwa katika ziara yake mkoani Pwani ambako pia alizindua viwanda saba, Rais alisema katu katika utawala wake hataruhusu utaratibu huo huku akizitaka taasisi binafsi zinazotetea wanafunzi waliopata mimba kurudi shuleni wafungue shule zao za wazazi. “Yaani anapata mimba amezaa mtoto iwe kwa makusudi,  kwa bahati mbaya au kwa raha yake, yaani aende shuleni ameshazaa! Si atawafundisha hawa wengine ambao hawajazaa! “Halafu akipata mimba tena ya pili anaenda nyumbani akizaa anarudi shuleni anapata wa tatu tena hivyo hivyo, yaani tusomeshe wazazi? “Nataka niwaambie na hizi Ngo’s na wote mnaonisikia ndani ya utawala wangu kama rais, hakuna mwenye mimba atakayerudi shuleni. “Nataka niwaeleze tukienda kwa mzaha wa namna hiyo na tukisikiliza hizi Ngo’s wanakotupeleka wanalimaliza taifa letu,” alisema Rais Dk Magufuli. Alisema Serikali yake ilitenga Sh bilioni 18 kwa ajili ya elimu bure  kwa sababu wapo watoto wa masikini ambao wanapata shida, lakini wanapokuwapo wachache wanaotetea hayo taifa litafika pabaya. Alisema hivi sasa ukifanywa uchunguzi watu ambao wanatetea hayo ndiyo hao hao ambao nao walipata mimba wakiwa shuleni. “Sasa narudia tena, hakuna mwenye mtoto katika elimu ya darasa la kwanza hadi sekondari kurudi shuleni kwa sababu amechagua maisha hayo ya mtoto akalee vizuri mtoto wake. “Lakini hata kama amepata mimba kwa bahati mbaya, yako mambo mengi ya kufanya ambayo yanaruhusu mtu aliyejifungua kufanya anaweza kwenda VETA, akajifunza kushona cherehani, akakopa kulima kilimo cha kisasa. “Labda ukazalie chuo kikuu huko wanaruhusiwa uwe mwaka wa kwanza, wa pili wewe zaa tu. “Lakini sekondari uzae halafu urudi tunapoteza maadili yetu, watazaa mno, itafika baada ya miaka kadhaa mtakuta darasa la kwanza wote wana watoto, wanawahi kwenda kunyonyesha kwa sababu mchezo huo ni mzuri na kila mmoja angependa aufanye,” alisema. Hata hivyo alivitaka vyombo vya dola kuhakikisha wale ambao wanawapa mimba wanafunzi sheria ifuatwe. “Nitoe wito kwa vyombo vya dola kwa sababu watakuja watu watasema, je wanaowapatia mimba itakuwaje? Sasa, je mimi niwabadilishe maumbile yao?   Wanaowapa mimba sheria ipo atakwenda kutumikia miaka 30. “Watu wa ajabu sana, hatuwezi kupeleka taifa hili katika maadili hayo. Kama wanaowatetea ni wazazi hawazuiliwi na hizi Ngo’s si wakafungue shule za wazazi kwa sababu wanakula tu fedha za bure za wafadhili lakini siyo waiamrishe Serikali kutekeleza hayo. “Nakupongeza Mama Salma Kikwete (Mbunge wa Kuteuliwa), ulisimama bungeni ukipinga haya endelea hivyo hivyo. “Sisi wote tuna watoto hata kama nina mtoto wangu wa kile apate mimba halafu arudi shuleni, wafanye halafu waone kama nitawarudisha shuleni. “Wametuletea watu kubakana wanaume kwa wanaume, wanawake kwa wanawake, wakati hata mbuzi au ng’ombe hafanyi huo mchezo… umeshawahi kuona mbuzi anakosea au ng’ombe?” alisema. PEMBEJEO HEWA Rais Dk. Magufuli alizungumzia suala la pembejeo hewa za kilimo ambako watu waliofariki dunia miaka zaidi ya 30 iliyopita wameandikiwa pembejeo kwenye vitabu. “Kuna watumishi hewa, vyeti hewa, wanafunzi hewa,   hivi sasa pia kuna pembejeo hewa. Wamepewa pembejeo na wameandikishwa wakati wamekufa zaidi ya miaka 30 sasa walikuwa wanatoka makaburini kuja kulima? Hata yanatokea Tanzania tu,” alisema. Aliwataka wakurugenzi wote nchini kabla ya Juni 30 mwaka huu, wawe wamekwenda kwenye kiwanda cha dawa za kuua mbu  kuchukua dawa hizo kwa ajili ya kuzisambaza. Katika hatua nyingine Rais Magufuli, alimtaka Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Charles Mwijage, kurudisha serikalini viwanda vyote vinavyomilikiwa na wawekezaji walioshindwa kuviendeleza. Alisema kama wawekezaji hao watakuwa wabishi ni vema wakamatwe na ikiwezekana wapelekwe mahakamani ili iwe fundisho kwa wawekezaji wengine ambao watakuwa wanamiliki wa viwanda bila kuviendeleza.
3kitaifa
RAMADHAN HASSAN-DODOMA JESHI La Polisi mkoani Dodoma, linawashikilia watu watano kwa tuhuma za mauaji ya Mwalimu Eradius Lucas Mgaya wa Kijiji cha Chilungulu, Tarafa ya Bahi . Hayo yalisemwa jana na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma, Gilles Muroto wakati akiongea na waandishi wa habari. Alisema tukio hilo  lilitokea Aprili 7, mwaka huu ambapo inadaiwa kuwa watuhumiwa hao watano (hakiwataja majina)walimpiga mwalimu huyo na kitu chenye ncha kali na kumtupa kwenye shamba la shule baada ya kumvizia njiani wakati akirejea nyumbani kwake . “Bado tunaendelea kufanya uchunguzi kuhusiana na tukio la kifo cha Mwalimu Godfrey na tunaendelea kuwashikilia watuhumiwa wa mauaji hadi hapo uchunguzi utakapo kamilika,” alisema Kamanda Muroto. Wakati huo huo Kamanda huyo wa Mkoa wa Dodoma aliwataka wenye magari kuchukua tahadhari kuhifadhi magari yao katika mazingira salama ikiwa ni pamoja na kuepuka kuegesha magari katika mazingira yanayowavutia wahalifu kuiba. Alisema uchunguzi wa Jeshi la Polisi mkoani hapa umebaini kuwa magari yanayowaniwa zaidi ni yale yanayotumia funguo za ‘Sensor’ ambazo hazihitaji kuchongwa . “Tunawashauri kuchukua tahadhari zote ikibidi wafunge Car truck system kwenye magari au CCTV kamera kuongeza utambuzi wa wahalifu baada ya matukio,”alisisitiza. Aliwataka wenye magari kuwa makini na waosha magari, mafundi wao, madereva wanaotumia kusafirisha au kusafiri nao safari za mbali . “Wapo wageni wanaofika Dodoma kuazima magari kutembelea kwa matumizi binafsi kisha kuondoka ni vema kujua mienendo ya watu hao kwa sababu wanaweza kuwa chanzo cha kuandaa mazingira ya wizi wa magari,” alisema Muroto. Pamoja na Mambo mengine Kamanda huyo wa Dodoma alisema jeshi hilo linamshikilia Grace Rauwo (31), mkazi wa Mtoni kwa Azizi Ali jijini Dar es Salaam kwa kosa la wizi kwa njia ya mtandao. Alieleza kuwa Rauwo akiwa na gari lenye namba za usajiri T 745 DSS aina ya Toyota Crown rangi nyeupe analolitumia katika uhalifu na linalodhaniwa kuwa ni la wizi ambapo anafanya uhalifu huo na timu ya wenzake wakiwa wanajihusisha na wizi wa fedha kwa njia ya mtandao wakiwa wamejisajili Kama mawakala. “Grace na wenzake wamechonga laine za simu wanaingilia mifumo ya neno Siri za wateja na kiwaibia fedha ambapo kabla ya kukamatwa waliiba fedha kwa njia ya mtandao Shilingi milioni 27 na kugawana huku yeye akiamua kununua gari hilo lenye namba za usajili Namba T.749 DSS ambalo pia wanalitumia kufanyia uhalifu,” alisema Pamoja na halo pia alisema kuwa katika hatua lingine Jeshi hilo limemkamata Godfrey Shirima (22)  ambaye ni mpiga picha mkazi wa Mtaa wa Image Dodoma, akiwa na silaha aina ya bastola yenye namba za usajili 016975 akiimiliki kinyume na sheria ambapo amekuwa aikitumia katika matukio ya uhalifu. Kwa mujibu wa Kamanda Muroto mtuhumiwa huyo anatarajiwa kufikishwa mahakamani upelelezi utakapo kamilika. Aidha Kamanda huyo akitoa salamu za Sikukuu ya Pasaka alisema Jeshi la Polisi linategemea hakutakuwa na mikusanyiko isiyo ya lazima itakayoleta msongamano hasa wakati huu ambao kila raia anapaswa kuchukua tahadhari dhidi ya maambukizi ya virusi vya COVID 19 . “Wazazi wawalinde watoto wao na wasiwaruhusu kwenda kwenye mikusanyiko kama ilivyozoeleka, pia nawaomba watu wajiepushe na ulevi wa kupindukia na kuchukua tahadhali ya usalama barabarani,” alisema
3kitaifa
KINSHASA, DRC KATIBU mkuu wa Umoja wa Mataifa, Antonio Guterres, ameitaka serikali ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo inahakikisha nchi hiyo inafanya uchaguzi huru na wa haki pamoja na wananchi wote kupatiwa fursa sawa za kushiriki zoezi hilo linalotarajiwa kufanyika leo nchini humo. Guterres amesema hayo juzi wakati akitoa ujumbe wake kwa DRC, huku wananchi waliotimiza masharti ya kupiga kura wakitazamiwa kuelekea katika masanduku ya kupigia kura kumchangua kiongozi atakayerithi mikoba ya Rais Joseph Kabila. Wito wa Katibu Mkuu wa Umoja huo usisitiza kuwa pande zote husika za kisiasa kuhakikisha kuwa zoezi hilo linafanyika kwa uhuru na amani. “Vyombo vya dola, viongozi wa kisiasa, maafisa wa uchaguzi na asasi za kiraia zinapaswa kuendelea kushirikiana ili kuhakikisha kuwa kunakuwa na mazingira ya kufanyika uchaguzi huru na wa haki, na kwa amani.” Guterres amewataka Wakongamani kutumia fursa hiyo ya uchaguzi aliyoitaja kuwa ya kihistoria, kuzipa nguvu taasisi za kidemokrasia nchini humo. Tayari taasisi muhimu za ndani na nje ya nchi zimeelezea wasiwasi wao kuhusu uwezekano wa kutokea machafuko wakati na baada ya zoezi hilo. Hata hivyo taarifa ya Umoja wa Mataifa imewataka wadau wote kutekeleza wajibu wao na kujiepusha na kauli au vitendo vinavyoweza kuchochea ghasia ili kuhakikisha kuwa zoezi hilo la kidemokrasia linafanyika kwa amani. Mbali na kuhitimisha uongozi wa Kabila ambaye yuko madarakani toka mwaka 2001, wapiga kura pia watawachagua wabunge na wawakilishi wa mabunge ya mikoa.
2kimataifa
Kwa mujibu wa Gallus Runyeta, Ofisa Miradi wa Kampuni ya Selcom inayosimamia mfumo huo wa tiketi za kielektroniki kwenye uwanja huo, mapato yaliyotokana katika mchezio huo uliomalizika kwa Simba kushinda 1-0, yameongezeka kulinganisha na michezo iliyopita ya klabu hizo pinzani.Amesema ongezeko hilo la mapato limetokana na sababu kadhaa, ikiwamo watazamaji wa mchezo huo kuongezeka ikilinganishwa na mara ya mwisho timu hizo zilipokutana.Kwa mujibu wa Runyeta, idadi ya watu walioingia uwanjani kutazama mechi ya wiki iliyopita ni 47,569 ambayo mapato yake ni sawa na Sh 376,138,000 ikilinganishwa na watu 10,353 walioingia mara ya mwisho timu hizo zilipopambana Uwanja wa Uhuru na kuingiza mapato ya Sh 113, 450,000.Alisema sababu nyingine za ongezeko hilo la mapato ni udhibiti wa mapato uliosimamiwa na Selcom; upatikanaji wa Selcom Card kuwa rahisi kwa watumiaji wapya na wale wa zamani ambao walipoteza kadi zao, kuimarishwa kwa ulinzi na usalama na kusimamiwa kwa ukaguzi wa tiketi kulikofanywa vizuri na SumaJKT.“Upatikanaji wa Selcom Card ulirahisisha kwa kiasi kikubwa, kwani mashabiki walikuwa na uwezo wa kununua tiketi kwa njia ya simu kwa kupiga *150*50# au kwa njia ya Selcom Card App kabla ya kufika uwanjani. Jambo hili lilisababisha kutokuwapo kwa foleni kwa mawakala waliokuwa wanakatisha tiketi," aliongeza Runyeta.Aidha, sababu nyingine ni kunaswa kwa watumiaji tiketi feki waliochukuliwa hatua kali; maboresho katika utaratibu wa kuingia magetini ulioleta nidhamu ya hali ya juu, na uuzaji wa tiketi ulioboreshwa sana sambamba na kuwapo mawakala wa kutosha.Kadhalika, kwa mujibu wa Runyeta, miundombinu ya kielektroniki ilikuwa katika hali ya ubora mkubwa kuanzia kwenye mtandao hadi kwenye milango ya umeme ya kuingilia uwanjani.
5michezo
Rais wa Zanzibar Dk Ali Mohamed Shein anatazamiwa kuwaongoza mamia ya Wazanzibari katika maadhimisho ya Miaka 56 ya Mapinduzi ya Zanzibar, yatakayofanyika Uwanja wa Amaan mjini Unguja leo.Sherehe za miaka 56 ya Mapinduzi ya Zanzibar ni za mwisho kwa Rais Shein, ambaye anatarajiwa kumaliza muda wa 10 akiwa madarakani ifikapo mwezi wa Oktoba mwaka huu, utakapofanyika uchaguzi mkuu.Shein aliingia madarakani mwaka 2010 na kuunda Serikali ya Umoja wa Kitaifa, huku Maalim Seif Sharif Hamad akichaguliwa kuwa Makamu wa Kwanza wa Rais na Balozi Seif Ali Iddi kuwa Makamu wa Pili wa Rais.Hata hivyo, Serikali ya Umoja wa Kitaifa ambayo inatokana na Kura ya Maoni iliyopigwa na Wazanzibari, haikutekelezwa vizuri katika awamu ya pili ya miaka mitano, baada ya chama kikuu kilichokuwa kikiunda serikali hiyo cha CUF, kususia uchaguzi wa marudio wa Machi 2011, baada ya kufutwa uchaguzi wa Oktoba 25.Sherehe za Miaka 56 ya Mapinduzi ya Zanzibar, zitahudhuriwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk John Magufuli ambaye ameshiriki katika uzinduzi wa miradi mbalimbali, ikiwemo hoteli ya kitalii ya Verde na Shule ya Sekondari ya Mwanakwerekwe Unguja. Kwa muda wa wiki mbili, wananchi wa Zanzibar wamekuwa katika harakati kubwa za kushiriki uzinduzi na kuweka mawe ya msingi miradi mbalimbali ya maendeleo, ikiwa ni shamra shamra za miaka 56 ya Mapinduzi.Miongoni mwa miradi mikubwa iliyozinduliwa ni shule za sekondari zilizojengwa kwa ghorofa zilizopo Mwembe Shauri Unguja na Pemba Wingwi. Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar katika utekelezaji wa Ilani yake 2015-2020 na Dira ya Maendeleo 2020 imeweka kipaumbele ujenzi wa shule za kisasa za ghorofa ili kuchukuwa nafasi kubwa kwa wanafunzi. Hatua hiyo inakwenda sambamba na kutekeleza kwa vitendo Mapinduzi Daima kwa kuendelea kutoa elimu bila ya malipo, ikiwa ni ahadi ya Rais wa kwanza wa Zanzibar, hayati Abeid Amani Karume.“Suala la kuimarisha sekta ya elimu bure ilikuwa ni moja ya ahadi ya chama cha ASP kilichopigania Mapinduzi ya Zanzibar kwa kuifanya elimu kuwa bure,” alisema Riziki Pembe Juma, ambaye ni Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali.Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharibi, Unguja Hassan Khatib aliwataka wananchi kujitokeza kwa wingi katika kilele cha maadhimisho ya sherehe hizo ambazo ni utambulisho wa wananchi wa Zanzibar katika taifa lao huru.Kwa mujibu wa ratiba ya sherehe hizo, viongozi wote wakuu, wakiwemo marais wastaafu wa Jamhuri ya Muungano wamealikwa kuhudhuria sherehe hizo. Sherehe hizo zitapambwa na maandamano ya wananchi wa mikoa mitano ya Zanzibar, ikiwemo miwili kutoka Pemba ambao watapita mbele ya mgeni rasmin na kutoa salamu zao. Sherehe hizo zitaongozwa na vikosi vya ulinzi vya Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ), ambao watapita mbele ya viongozi wakuu kwa gwaride rasmin.Wananchi wa Zanzibar watapata nafasi ya kumsikiliza Rais Dk Ali Mohamed Shein katika hotuba yake, ambayo ni ya mwisho katika kipindi cha miaka kumi ya uongozi wake wa kuiongoza Zanzibar akiwa Rais na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi.Wazanzibari walilazimika kufanya Mapinduzi Januari 12 mwaka 1964, baada ya kuchochwa na madhila ya utawala wa Kisultani kutoka Oman. Mapinduzi hayo yalifanywa na Rais wa kwanza wa Zanzibar Hayati Abeid Amani Karume kwa kushirikiana na viongozi wa ASP Januari 12 mwaka 1964.
3kitaifa
MBUNGE wa Chemba, Juma Nkamia (CCM), amesema anamsubiri Spika wa Bunge, Job Ndugai, ili aweze kumwambia aache hoja yake binafsi ya kutaka muda wa Rais kuwepo madarakani uongezwe kutoka miaka mitano ya sasa hadi saba. Akizungumza na MTANZANIA kwa simu juzi, Nkamia alisema anaheshimu kauli ya Rais, Dk. John Magufuli, ambaye pia ni mwenyekiti wake, lakini anangoja uamuzi wa Spika kwa kua alishaandika barua yenye nia ya kuwasilisha hoja hiyo. Nkamia alisema licha ya mwenyekiti wake (Rais Magufuli) kuingilia kati, lakini Spika ndiye atakayemwambia aache hoja hiyo au laa kama taratibu za Bunge zinavyotaka. “Nimemsikia Rais akizungumzia hilo lakini nafuata kanuni za Bunge, hivyo Spika atanipa maelekezo ya nini cha kufanya, ndio maana kuna mihimili mitatu ikiwa ni pamoja na Mahakama, Bunge na Serikali kila mmoja una fanya kazi yake,’’ alisema Nkamia. Januari 13,  mwaka huu Rais Magufuli alifunga mjadala wa hoja hiyo kupitia mazungumzo yake na Katibu wa Halmashauri Kuu ya CCM (Itikadi na Uenezi), Humphrey Polepole kwamba hana mpango huo. Polepole alisema, Rais Magufuli alimwelekeza kuwajulisha wanachama wa CCM na Watanzania wote kuwa anasikitishwa na hafurahishwi na mjadala unaoendelea juu kuongezwa kwa kipindi cha urais kutoka miaka 5 iliyowekwa kwa mujibu wa Katiba hadi 7. “Rais Dk. Magufuli amewataka wanachama wa CCM na umma wa Watanzania kwa ujumla kuupuuza mjadala huo kwa kuwa haujawahi kujadiliwa katika kikao chochote cha chama na pia ni kinyume na katiba ya CCM na Katiba ya nchi,” alisema Polepole.
3kitaifa
RAIS John Magufuli amewahakikishia mabalozi na wawakilishi wa mashirika ya kimataifa kuwa Serikali ya Tanzania itaendeleza na kukuza zaidi ushirikiano na uhusiano mzuri uliopo kati ya Tanzania na nchi hizo katika nyanja za maendeleo na ustawi wa jamii.Rais Magufuli amesema hayo juzi usiku katika sherehe ya Mabalozi na Wawakilishi Mashirika ya Kimataifa (Sherry Party) iliyofanyika Ikulu jijini Dar es Salaam.Pamoja na kauli hiyo, Rais Magufuli amewashukuru wanadiplomasia hao kwa kuendelea kushirikiana na Tanzania katika utekelezaji wa mipango mbalimbali na kubainisha kuwa utekelezaji wa mipango hiyo hususani miradi ya maendeleo unafanyika kwa mafanikio makubwa.Alitaja baadhi ya mafanikio makubwa yaliyopatikana katika mwaka 2018 kuwa ni kulinda na kudumisha amani na usalama, kusimamia vizuri uchumi ambao ulikua kwa wastani wa asilimia saba na hivyo kuifanya Tanzania kuwa miongoni mwa nchi tano zenye uchumi unaokua kwa kasi zaidi barani Afrika.Mafanikio mengine ni kudhibiti mfumuko wa bei ambao ulikuwa wastani wa asilimia 3.5 na Tanzania kuibuka kinara katika kuvutia uwekezaji miongoni mwa nchi za Afrika Mashariki kwa kuvutia uwekezaji wenye thamani ya dola za Marekani bilioni 1.18.Rais Magufuli amebainisha kuwa katika mwaka 2018, Tanzania iliendelea kutekeleza miradi yake mikubwa ya miundombinu ikiwemo ujenzi wa reli ya kisasa (SGR) kutoka Dar es Salaam hadi Dodoma na kuanza maandalizi ya ujenzi wa mradi mkubwa wa kuzalisha umeme megawati 2,100 katika bonde la mto Rufiji.Mingine ni kuendeleza miradi ya kusambaza umeme, upanuzi wa bandari za Dar es Salaam, Mtwara na Tanga, ujenzi wa meli katika Ziwa Victoria, ujenzi wa barabara, viwanja vya ndege, jengo jipya la abiria kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam na ujenzi wa rada nne.Aliongeza kuwa miradi mingine ni upanuzi wa huduma muhimu za kijamii hususani afya, elimu na maji ambako vituo vya afya 305 na hospitali za wilaya 67 zinajengwa, kuimarisha huduma za matibabu ya kibingwa ambako katika mwaka 2018 Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete ilifanya upasuaji kwa wagonjwa 1,361, kutoa elimu ya msingi na sekondari bila malipo na upatikanaji wa maji vijijini kufikia asilimia 65 na mijini asilimia 80.Rais Magufuli alifafanua maeneo mengine kuwa ni kushiriki kikamilifu katika masuala ya kimataifa, kushiriki majukumu ya kulinda amani ambapo askari 1,900 wapo katika maeneo mbalimbali ya ulinzi wa amani na kuhudumia wakimbizi ambapo kwa sasa idadi ya wakimbizi waliopo nchini imefikia 324,420.Aidha, alisema katika mwaka huu, Tanzania imejipanga kuendeleza malengo mbalimbali yakiwemo kukuza uchumi kwa kuzingatia Mpango wa Maendeleo wa Taifa wa Miaka Mitano (2016/17-2020/21) unaoelekeza Tanzania kufikia uchumi wa kati na kuweka mkazo katika sekta ya kilimo, utalii, usafiri wa anga na madini.Aliwasihi mabalozi kuendelea kutangaza fursa mbalimbali za uwekezaji na biashara zilizopo nchini na ameahidi kuwa serikali itakuwa tayari wakati wote kuhakikisha wawekezaji watakaokuwa tayari kuwekeza wanapata ushirikiano wa kutosha kufanikisha uwekezaji huo kwa manufaa ya pande zote mbili.Akizungumza kwa niaba ya mabalozi na wawakilishi wa mashirika ya kimataifa, kiongozi wa mabalozi ambaye ni Balozi wa Comoro nchini, Dk Ahamada El Badaoui Mohammed alimshukuru Rais Magufuli kwa ushirikiano mkubwa ambao mabalozi wamekuwa wakiupata kutoka serikalini na ameahidi kuendeleza ushirikiano huo.Balozi Mohammed ameahidi kuwa mabalozi watampa ushirikiano wa kutosha Waziri mpya wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Profesa Palamagamba Kabudi. Alibainisha kuwa mabalozi wapo tayari kuendelea kuunga mkono juhudi za serikali zikiwemo vita dhidi ya rushwa, kuboresha maisha ya watu, kujenga viwanda na kuhakikisha Watanzania wananufaika na rasilimali zao.
3kitaifa
  Na Mwandishi wetu, MWENYEKITI wa Kamati ya Bunge ya Nishati na Madini, Dotto Biteko, amempongeza Rais Dk. John Magufuli kutokana na uamuzi wake wa kuunda kamati maalum kwa ajili ya kuchunguza mchanga wa madini. Akizungumza na MTANZANIA Dar es Salaam jana baada ya Rais Magufuli kukabidhiwa ripoti ya pili, Biteko alisema ripoti zote mbili zimethibitisha kilio cha Watanzania kuhusu kuibiwa rasilimali za madini uliofanywa kwa miaka mingi. “Rais amejibu kilio hiki cha Watanzania, wananchi walikuwa wanaamini na hasa wale wanaozunguka migodi kwamba tulikuwa tunaibiwa. “Ripoti zote mbili zimethibitisha ukweli juu ya kilio hiki na katika hili nampongeza Rais kwa uamuzi wake wa kuunda kamati maalumu ambazo zimetuletea matokeo chanya,” alisema. Hata hivyo Biteko ambaye pia ni Mbunge wa Bukombe, alisema kamati yake inasubiri maelekezo ya Spika wa Bunge, Job Ndugai, atakapounda kamati ya kufuatilia uchimbaji wa madini ya almasi. “Spika ameahidi kuunda kamati ya kufuatilia suala la uchimbaji wa madini ya almasi kabla ya Bunge hili la Bajeti halijaisha. “Siku zote sisi wabunge na wajumbe wa kamati za Bunge tumekuwa tukifanya kazi chini ya maelekezo ya Spika, hivyo katika hili tunasibiri mwongozo na maelekezo yake,” alisema.
3kitaifa
UTOAJI wa pasipoti mpya za kielektroniki unaendelea vizuri, na tayari kati ya Januari Mosi na Machi 25, mwaka huu, zimetolewa pasipoti 20,912.Msemaji wa Idara ya Uhamiaji nchini, Ally Mtanda alisema Dar es Salaam kuwa pasipoti za kawaida zilizotolewa katika kipindi hicho ni 20,771, kidiplomasia 111 na za utumishi 30.“Kazi ya kutoa pasipoti hizi inaendelea vizuri, changamoto zilizopo ni ndogo na kawaida tu, watu wengi wanajitokeza kuomba pasipoti hizi,” alisema Mtanda.Akizindua pasipoti hizo mapema mwaka jana, Rais John Magufuli alisema zitasaidia kuimarisha ulinzi na usalama wa mipaka ya nchi na kudhibiti ukusanyaji wa maduhuli ya serikali na kuimarisha utoaji wa huduma za kiuhamiaji kwa Watanzania na wageni wanaoingia na kuishi nchini.Alisema matumizi ya pasipoti mpya za kielektroniki, yataondoa matumizi ya pasipoti za kawaida zinazotumika sasa na kwamba zinakidhi viwango vya kimataifa kwa kuwa zina alama nyingi za kiusalama, na siyo rahisi kuzighushi.Uhamiaji pia inatoa viza za kielektroniki (e-Visa), vibali vya ukaazi vya kielektroniki (e-Permit) na udhibiti wa mipaka wa kielektroniki (e-Border Management).Pasipoti hizo mpya zinagharimu Sh 150,000 kila moja na zitatumika kwa miaka 10 kabla ya kuhuishwa tena.Katika hatua nyingine, msemaji huyo wa Uhamiaji alisema wahamiaji haramu 3,070 walikamatwa Januari na Februari mwaka huu.Alisema Januari walikamatwa 1,255, wakati Februari walikamatwa 1,715.Mtanda alisema wahamiaji walioondoshwa kutoka nchini kwa miezi ya Januari na Februari ni 2,952, waliofikishwa mahakamani ni 420, waliofungwa ni 30 na kwamba kesi za wahamiaji zinazoendelea ni 142.Alisema wahamiaji waliolipa faini katika kipindi hicho ni wanne, upelelezi unaendelea kwa wahamiaji 470, Watanzania waliorejeshwa nchini kutoka mataifa mbalimbali 184, wahamiaji walioachiwa huru 183, waliohalalisha ukaazi 218 na waliopelekwa ukimbizi 199.
3kitaifa
Mwandishi Wetu, Dar es Salaam Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH), imefunga mashine tatu za kusafisha damu kwa wagonjwa wenye matatizo ya figo katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa Amana. Aidha, mbali na mashine hizo zenye thamani ya Sh milioni 210, pia inatarajia kufunga mashine moja ya kusaidia mgonjwa kupumua (ventilator) yenye thamani ya Sh milioni 56.  Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Hospitali ya Muhimbili leo Jumapili Aprili 26, tayari wagonjwa wanaohitaji huduma ya kusafishwa damu wameanza kuhudumiwa na wafanyakazi wa Muhimbili waliopo Hospitali ya Amana tangu Ijumaa Aprili 24 ambapo dawa na vitendanishi vya kutoa huduma ya kusafisha figo kwa sasa vinagharamiwa na Muhimbili.  “Sambamba na hilo, Hospitali imefunga mtambo wa kuchuja maji (Portable RO) wenye thamani ya Sh milioni 28 na mtandao wenye miundombinu ya kusafirisha maji ili kuwezesha mashine hizo kufanya kazi ya kusafisha damu uliogharimu Sh milioni 12. “Kutokana na hilo, Muhimbili itapokea madaktari na wauguzi kutoka Hospitali ya Rufaa ya Amana kuanzia Aprili 28, mwaka huu ili kujengewa uwezo kwenye Kitengo cha Kusafisha Damu pamoja na vyumba vya wagonjwa wanaohitaji uangalizi maalumu (ICUs) aina tano tofauti,” amesema Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano ya Umma wa hospitali hiyo,  Aminiel Aligaesha.
3kitaifa
Derick Milton, Simiyu Wakala wa usambazaji maji vijijini (Ruwasa) Mkoa wa Simiyu umetoa msaada wa vifaa vya kunawia mikono vitakavyotumika kwenye baadhi ya shule za sekondari na hospitali mkoani humo ili kujikinga na virusi vya corona. Akikabidhi vifaa hivyo kwa Katibu Tawala wa mkoa huo, Jumanne Sagini Mhandisi wa Maji,  Mahobe Singu kwa niaba ya meneja wa mkoa amesema kuwa msaada huo umegharimu kiasi cha Sh. milioni 1.7. Amesema kuwa Ruwasa wametoa vifaa hivyo kwenye sehemu ambazo zina mkusanyiko mkubwa wa watu ikiwemo shule na hospitali ikiwa na lengo la kuunga juhudi za serikali katika mapambano dhidi ya virushi vya corona. Amevitaja vifaa hivyo ni pamoja na kontena tano zikiwa na stendi zake za kunawa mikono kwa kutumia miguu kufungulia maji na sabuni zinazotumika bila ya kushika. “Vifaa hivi tumeona kuvitoa kama mchango wetu kwa jamii katika mapambano dhidi ya ugonjwa huu, vitapelekwa katika hospitali ya rufaa ya mkoa, hospitali ya Wilaya ya Maswa na Shule ya Sekondari Dutwa,” amesema Mhandisi Singu. Akipokea Vifaa hivyo Katibu tawala amehukuru wakala huyo kwa kuunga mkono juhudi za mkoa na serikali katika kupamba na ugonjwa wa corona ambao unatajwa kuwepo nchini.
4afya
PATRICIA KIMELEMETA NA HERIETH FAUSTINE – Dar es Salaam MWENYEKITI wa Kamati ya Kitaifa ya Maadili, Amani na Haki za Binadamu kwa Jamii ya Viongozi wa Dini, Askofu Wiliam Mwamalanga, amesema amesikitishwa na kitendo cha Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda, kumtaja Freeman Mbowe kuwa miongoni mwa watuhumiwa wa biashara ya dawa za kulevya. Akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam jana, Askofu Mwamalanga alisema kamati yao ilitilia shaka Bilicanas iliyokuwa inamilikiwa na Kampuni ya Mbowe Hotels, kwamba ni moja ya maeneo yanayotumiwa na wafanyabiashara wa dawa za kulevya kufanya biashara zao, lakini si mwanasiasa huyo. Alisema ukumbi huo wa starehe kuhusishwa na biashara hiyo, haikumaanisha kwamba mmiliki wake ambaye pia ni Mbunge wa Hai na Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) anahusika.  “Sisi tulisema klabu ya Bilinacas inajihusisha na uuzaji na usambazaji wa dawa za kulevya kwa sababu walikuwa wanaingia watu mbalimbali ambao walikuwa wakiendesha shughuli hizo, lakini hatukumtaja mmiliki wake Mbowe ndiye anayejihusisha na dawa hizo,” alisema Askofu Mwamalanga. Alisema kamati hiyo itashirikiana na Serikali ili kuhakikisha biashara ya dawa za kulevya inatokomezwa na wahusika wote wanafikishwa kwenye mikono ya sheria. Kamati hiyo pia imempongeza Rais Dk. John Magufuli kumteua Kamishna wa Tume ya Kudhibiti Dawa za Kulevya mwenye taaluma ya kusimamia suala hilo, jambo ambalo limesaidia kutotajwa watuhumiwa hadharani badala yake wahusika waweze kuchukuliwa hatua.
3kitaifa
NAIBU Rais wa Kenya, William Ruto amefi chua kuwa kamwe hakuwahi kufi kiria kushika wadhifa mkubwa serikalini, kwani ndoto kubwa maishani mwake ilikuwa kuwa dereva wa treni.Alisema hayo hivi karibuni alipokutana na wakufunzi wa Tamasha la Filamu Kenya ofisini kwake Karen, jijini hapa na kuzungumzia alivyopambana kimaisha, akianza na kuuza karanga na nyama za kuku barabarani katika kituo kikuu cha reli.Alisema kati ya mwaka 1978 na 1980, aliuza vichwa vya kuku kwa kati ya Sh 12 na 14 za Kenya, na maisha yaliendelea kwa sababu alikuwa na dhamira ya kukabiliana na maisha.“Ndiyo mjue Mungu ni wa ajabu... Siku hizo, hata sikuamini eti naweza kuwa mtu... yaani ile nilikuwa nafikiria kabisa ni kuwa dereva wa gari moshi.“Hapo ndiyo nilikuwa nimejipanga. Pale nilikuwa nauza kuku palikuwa ni karibu na reli. Nilikuwa naona hii gari moshi inatembea nikasema, ‘hii kitu nitakuja kuendesha siku moja,” alisema na kuwafanya watu kuangua kicheko.Alisema hayo akilenga kuwapa ujasiri vijana, waweze kujitambua, kujithamini na kujiwekea malengo ya mbali ili waweze kufanikiwa kimaisha, bila ya kujali wametoka katika familia duni kiasi gani. Leo hii, ukitaja matajiri wakubwa nchini Kenya, jina la Ruto halikosekani.Na anakiri alianzia maisha juani sasa analia kivulini, na amewahi kukaririwa akisema, kama hakupata utajiri huo kihalali, ana hakika angekuwa anaozea jela.“Watu wengi wanakosea kuamini kwamba ni lazima uwe masikini kwa sababu wazazi wako walikuwa masikini, baadhi wanasema kuna watu walizaliwa wawe masikini, na hilo ni neno kwa mujibu wa shetani,” alisema Ruto.Alisisitiza kwamba anaweza kusema alivyopata kila senti aliyonayo, kwani amezipata kwa juhudi na kununua hisa kwenye kampuni na kumbukumbu zipo.“Nilivyokuwa mdogo niliuza kuku kwenye makutano ya reli jirani na nyumbani, fedha za kujikimu chuo kikuu nilitumia kumjengea baba yangu nyumba, nililipa karo za wadogo zangu, Mungu amekuwa mwema kwangu, na kwa kufanya kazi kwa bidii na kudhamiria, nina kitu,” alisema mwanasiasa huyo katika moja ya fursa alizopata kuzungumzia utajiri wake.Ruto ni nani?Ni mwanasiasa na bilionea kijana aliyeandika historia katika maisha yake na ya familia kwa ujumla. Aprili 9, mwaka 2013, kijana huyo mwenye umri wa miaka 52 na ambaye jina lake kamili ni William Kipchirchir Samoei arap Ruto, kwa mara ya kwanza aliapishwa rasmi kuwa Naibu Rais wa Kenya.Aliendelea na wadhifa huo kuanzia mwaka 2017 na sasa analenga kuushika urais kamili katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2022.Hakika, kijana huyu aliyezaliwa katika familia masikini katika Kijiji cha Sambut kilichopo Kitongoji cha Kamagut, Uasin Gishu nchini Kenya Desemba 21, 1966 ameandika historia mpya si kwa familia yake tu, bali hata yeye mwenyewe kwani amefanya mapinduzi makubwa ya kimaisha.Mama yake mzazi, Sarah Cheruiyot (68) anasema mwanawe alikuwa anatembea pekupeku kwenda shuleni kama watoto wengine kijijini hapo, na aliporudi nyumbani alikwenda kuchunga mbuzi.Ukifuatilia historia yake, tangu anauza karanga katika barabara kuu ya Eldoret kuisaidia familia yake kupata fedha za kujikimu, hadi alipo leo, utabaini kwamba penye nia pana njia, na hakuna linaloshindikana ili mradi uwe na dhamira ya kufika unapokusudia.Msomi huyo wa Sayansi kutoka Chuo Kikuu cha Nairobi, alianza kushika madaraka kwa kuteuliwa na Rais Daniel arap Moi kuwa Waziri Msaidizi wa Masuala ya Utawala na baadaye akateuliwa kuwa Waziri wa Mambo ya Ndani.Pia amewahi kuwa Katibu Mkuu wa KANU, akajiuzulu nafasi hiyo Oktoba 6, 2007. Aprili 13, 2008, Ruto aliteuliwa kuwa Waziri wa Kilimo katika Serikali ya Pamoja ya Mwai Kibaki na Raila Odinga, na Oktoba 19, 2010 akateuliwa kuwa Waziri wa Elimu ya Juu.Kijana huyo aliyeokoka na kuongoza kwaya ya umoja wa Wakristo wakati anasoma Chuo Kikuu, tangu mwaka 1997 amekuwa Mbunge wa Eldoret Kaskazini.Alihitimu Chuo Kikuu cha Nairobi mwaka 1990 na kupata Shahada ya Sayansi, na Shahada ya Uzamili ya Muundo wa Mimea.
3kitaifa
Na Mwandishi Wetu -PEMBA UONGOZI wa Mkoa wa Kusini Pemba kwa kushirikiana na Wizara ya Kilimo, Maliasili, Mifugo na Uvuvi umepongezwa kwa kuyabainisha na kuyarejesha serikalini mashamba ya Serikali na kuagiza kwa wale wote ambao bado wanayaficha wayarejeshe wenyewe kabla hawajachukuliwa hatua za kisheria. Hayo yalisemwa jana Kisiwani Pemba na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein ambapo alisema aliagiza kuchukuliwa hatua za kisheria bila kujali wadhifa wa mtu, cheo alichonacho au umaarufu wake. Agizo hilo alilitoa katika majumuisho ya ziara yake aliyoifanya kuanzia Agosti 24, mwaka huu ambapo aliwaagiza viongozi wa mikoa na wilaya kusimamia vizuri ukusanyaji mapato na kushirikiana na wafanyabiashara katika kuwashajiisha ili walipe kodi na kuongeza mapato ya Serikali. Aliwataka viongozi hao kutojiingiza katika kuwasaidia kukwepa kodi wala kuwakingia kifua kwa makosa yao wanayoyafanya katika kukwepa kulipa kodi. Pamoja na hali hiyo aliagiza Wizara ya Habari, Utalii, Utamaduni na Michezo kufanya mkutano maalumu na wakuu wa mikoa na wilaya zote za Unguja na Pemba kwa ajili ya kupanga na kupeana majukumu ya utekelezaji wa mpango wa utalii kwa wote.
3kitaifa
Na RAMADHAN LIBENANGA – MOROGORO NI majonzi. Ndivyo unavyoweza kusema baada ya lori la mafuta kupinduka mjini Morogoro na kusababisha watu zaidi ya 60 kufariki dunia na wengine 70 kujeruhiwa walipokuwa wakichota mafuta. Hadi tunakwenda mtamboni jana, mmoja wa Ofisa wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Morogoro alisema mpaka jioni vifo vilikuwa 64 na majeruhi 70. Kwa mujibu wa baadhi ya mashuhuda, ajali hiyo ilitokea jana asubuhi majira ya saa mbili baada ya dereva wa lori kumkwepa mwendesha pikipiki na baadaye kushindwa kulimudu gari lake na kupinduka. Walisema baada ya gari hilo kupinduka, dereva alijaribu kuonya wananchi kutosogea karibu kwa sababu lilikuwa limebeba petroli na lingeweza kuwaka moto wakati wowote. Kwa mujibu wa mashuhuda hao, baadhi ya vijana wengi wao wakiwa waendesha bodaboda na wapigadebe Kituo cha Mabasi Msamvu, hawakusikia onyo hilo na wakaendelea kuchota mafuta. Walisema vijana hao na baadhi ya mama lishe waliokuwa karibu na eneo hilo, walichota mafuta hayo kwa takribani nusu saa kabla ya wenzao kwenda eneo la betri ya gari hilo wakijaribu kuzitoa ndipo moto ukawaka. HOSPITALI Kaimu Mganga Mkuu wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Morogoro, Ritha Lyamuya, alisema kwa asubuhi alipokea miili ya watu 62 na majeruhi 70. “Mpaka sasa tayari tumeshapokea miili ya watu 62 katika ajali hiyo ya moto na majeruhi 70 wamelazwa katika hospitali yetu,” alisema Dk. Lyamuya. POLISI Kamanda wa Polisi Mkoa wa Morogoro, Wilbroad Mtafungwa, alithibitisha watu 62 kufariki dunia katika ajali hiyo na majeruhi wakiwa ni 70. Alisema lori hilo … Kwa habari zaidi jipatie nakala yako ya gazeti la MTANZANIA.
3kitaifa
MAMLAKA ya Usafi ri wa Anga Tanzania (TCAA) imewataka wazazi na walezi kuwahamasisha watoto wao kusomea fani za usafi ri wa anga kwani taifa halina wataalam wa kutosha katika sekta hiyo.Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa TCAA, Vallery Chamulungu alitoa wito huo jana jijini Dar es Salaam wakati wa maadhimisho ya 75 ya siku ya kimataifa ya usafiri wa anga duniani tangu Shirika la Kimataifa la Usafiri wa Anga Duniani (ICAO) lianzishwe ambapo Tanzania ni mwanachama wa shirika hilo.Katika maadhimisho ya mwaka huu yaliyobeba kaulimbiu “Miaka 75 ya Kuunganisha Ulimwengu”, Chamulungu alisema TCAA kwa kushirikiana na wadau wengine wa usafiri wa anga, iliaanzisha shindano la insha kwa ajili ya wanafunzi wa shule za msingi na sekondari wenye umri wa miaka kati ya 10 na 13. Shindano hilo lilikuwa linamtaka mshiriki aelezee mchango wa Kampuni ya Ndege Tanzania (ATCL) katika uchumi wa taifa.Alisema lengo la shindano hilo ni kuamsha ari na hamasa kwa vijana wadogo wa Kitanzania kujifunza na kufuatilia masuala ya usafiri wa anga, mchango wake katika uchumi wa nchi na kuwajengea maarifa na ufahamu ili kuwaandaa kimasomo baadaye wajiunge na taaluma mbalimbali za usafiri wa anga taifa lipate wataalam wa kutosha.“Sekta ya usafiri wa anga nchini ina uhaba wa wataalam, shindano la insha tuliloanzisha ni mkakati wa kuamsha ari ya watoto wa Kitanzania wajue usafiri wa anga ni kitu gani na kuwajengea hamu ili waje kuwa wataalam wa sekta ya usafiri wa anga, wito wangu kwa wazazi na walezi ni kwamba wawaelekeze watoto kusomea fani za usafiri wa anga,”alieleza Chamulungu.Watoto watano kati ya 100 walioshiriki walishinda na kupewa zawadi za kompyuta mpakato, mabegi ya shule na beji mshindi wa kwanza hadi wa tatu na wa nne na wa tano walizawadiwa mabegi ya shule.ATCL imezawadia tiketi za ndege Dar es Salaam -Kilimanjaro na kurudi. Safari inaratibiwa na TCAA. Waliozawadiwa ni Huzeifa Amirali (12) wa Shule ya Al-Madresa-tus-Seifea-Tul- Burhania aliyesema anataka kuwa rubani, Albert Dida (11) kutoka Shule ya Msingi Libermann anayetaka kuwa mhandisi wa ndege, Yvonne Lyaruu (12) wa Shule ya Alpha High School kidato cha kwanza anayetaka udaktari, Maureen Slayo (11) wa Shule ya Msingi Harvard anayetaka udaktari na Alpha Mbise (12) wa Shule ya Fray Luis Amigo anayetamani uhandisi wa ndege.Mbali na insha hiyo, Chamulungu alisema ICAO ilitaka TCAA kupandisha bendara ya ICAO kilele cha Mlima Kilimanjaro kama sehemu ya kuitangaza zaidi Tanzania kimataifa. Kazi hiyo ya kuipandisha bendera ya ICAO Mlima Kilimanjaro ilianza Agosti 19 na kukamilika Agosti 22 mwaka huu. Alisema kwa kufanya hivyo pia inaondoa upotoshaji wa baadhi ya watu kutoka nchi jirani kudai kuwa Mlima Kilimanjaro uko kwenye nchi yao.
3kitaifa
WAZIRI wa Nchi, Ofi si ya Rais, Menejimenti na Utumishi wa Umma na Utawala Bora, George Mkuchika, amesema moja kati ya vikwazo vikubwa vinavyochelewesha kufikia uchumi wa viwanda ni rushwa, hivyo viongozi wa serikali wakatae kutoa na kupokea rushwa.Mkuchika ameyasema hayo katika hafla ya kuhitimisha kozi fupi ya tano ya viongozi, iliyofanyika katika Chuo cha Taifa cha Ulinzi (NDC), jijini Dar es Salaam.Mkuchika amesema rushwa inaumiza watu masikini, inadhoofisha uwezo wa serikali katika kutoa misaada ya kimsingi na kwamba tatizo hilo linaendelea kudumaza Taifa la Tanzania kwa muda mrefu sasa.Alisema pamoja na changamoto hiyo, serikali imejipanga kuhakikisha inaondoa hali hiyo na ndio maana hivi sasa baadhi ya mashirika yanayofanya utafiti ndani na Afrika Mashariki, yameeleza kuwa tangu Rais John Magufuli aingie madarakani, rushwa imeanza kushuka, na kwa nchi za Afrika Mashariki, Tanzania ipo vizuri katika suala hilo.Aliwaeleza viongozi hao kuwa serikali inategemea mambo makubwa kutoka kwao na majawabu ya namna gani ya kufikia uchumi wa viwanda ifikapo mwaka 2025.Alisema pia uongozi ni dhana inayoishi kwa kuendelea kujifunza kila siku, kwani dunia ya sasa na mifumo inabadilika kwa kasi kubwa pasipo uelewa wa kutosha, kama viongozi watashindwa kuendana na kasi hiyo.Katika hafla hiyo, Mkuchika aliwatunuku vyeti washiriki 24 miongoni mwao wakiwemo makatibu wakuu, naibu makatibu wakuu, wakuu wa mikoa, makatibu tawala, wakurugenzi wa taasisi za serikali, wakuu kutoka Kikosi cha Kutuliza Ghasia (FFU), Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) pamoja na Uhamiaji.Mkuu wa chuo hicho, Paul Massawe amesema, kwa siku tano, washiriki walipata fursa ya kujifunza mambo muhimu ikiwemo usalama, nadharia na kwa vitendo, taswira ya usalama, msimamo na itikadi kali kwa vijana wa Tanzania, matishio mapya ya kiusalama na usalama wa taifa na changamoto za teknolojia ya habari na mawasiliano.Pia usalama wa ndani ya nchi, uzalendo na uongozi nchini, uzalendo na usalama wa taifa, athari za rushwa kwa usalama wa taifa, uongozi wenye maadili na usalama wa taifa, na pia wamepata nafasi ya kufanya mazoezi.Vile vile usalama wa taifa na mazingira ya kistratejia, vyombo vya kitaifa vya ulinzi na usalama, majadiliano ya kistratejia, vyombo vya kitaifa vya ulinzi na usalama, majadiliano ya pamoja na wakuu wa vyombo vya ulinzi na usalama na mwisho wamepata nafasi kutembelea Makao Makuu ya Jeshi la Nchi Kavu, ambapo wameshuhudia uwezo wa jeshi lao katika kulinda mipaka ya nchi na rasilimali zake.
1uchumi
Manchester, England KLABU ya Manchester United imemzuia mchezaji wao mpya Odion Ighalo kufanya mazoezi pamoja na wachezaji wenzake kwenye Uwanja wa AON Complex, kutokana na kumuhofia kuwa na virusi vya Corona. Mchezaji huyo alijiunga na Manchester United wakati wa dirisha dogo la usajili wakati wa Januari mwaka huu akitokea klabu ya Shanghai Shenua ya nchini China kwa mkopo. Ighalo mwenye umri wa miaka 30, raia wa nchini Nigeria, alikuwa kwenye kiwango cha hali ya juu kwenye michuano ya Mataifa ya Afrika mwaka jana. Virusi hivyo vya Corona vinapatikana nchini China, hivyo United wanahofia mchezaji huyo kuwa navyo kwa kuwa alikuwa anacheza soka nchini humo na aliondoka wakati tayari vimegundulika. Hata hivyo, inasemekana kuwa mji wa Shanghai ambao alikuwa mchezaji huyo hadi anaondoka hapakuwa na dalili yoyote ya mtu kupatwa na virusi hivyo, huku ikidaiwa vimeanza kugundulika katika mji wa Wuhan. Lakini mchezaji huyo anaendelea na mazoezi chini ya kocha Wayne Richardson kwenye Uwanja wa GB Taekwondo Centre na kuna uwezekano kuanzia leo akaungana na wenzake kwa mara ya kwanza. Inasemekana kuwa zaidi ya watu 1,100 nchini China wamegundulika kuwa na virusi hivyo, hivyo Ighalo hakuweza kujiunga na klabu ya Manchester United wakati wa maandalizi ya Ligi huko nchini Hispania ambapo walikwenda kuweka kambi. Hali hiyo ya virusi imesababisha watu washindwe kusafiri kutoka China kwenda nchi zingine au kuingia China, lakini kwa upande wa Ighalo anafanyiwa vipimo vya mwisho kwa ajili ya kujiridhisha. Mchezaji huyo alisajiliwa na Manchester United siku ya mwisho ya kufungwa kwa dirisha dogo la usajili ambapo hadi sasa ni siku 15 na hajapata nafasi ya kujiunga na timu katika michezo yao. Kocha Ole Gunnar Solskjaer anaamini mchezaji huyo ataungana na timu wiki hii.
5michezo
['Meneja wa Liverpool Jurgen Klopp amefutilia mbali uwezekano wa kumsajili kiungo wa kati wa Barcelona, Philippe Coutinho, 27, ambaye aliondoka Anfield kwa kima cha £142m mwaka 2018. (ESPN)', 'Paris St-Germain imekubali kulipa £28m kumsajili kiungo wa kimataifa wa Senegal Idrissa Gueye, 29, kutoka Everton. (Mail)', 'Toffees wanaendelea kushauriana na Crystal Palace kuhusu usajili wa nyota wa kimataifa wa Ivory Coast Wilfried Zaha, 26, kwa pauni £80m. (Sky Sports)', 'Tottenham imewasiliana na Juventus kuhusu usajili wa nyota wa kimataifa wa Argentina international mshambuliaji Paulo Dybala, 25, ambaye bei yake anayekadiriwa kuwa £80m. (Evening Standard)', 'Manchester United wameomba kufahamishwa kuhusu hatma ya mchezaji Christian Eriksen, 27, wa Tottenham. Kandarasi ya nyota huyo wa kimataifa wa Denmark amesalia na mwaka mmoja kukamilika na huenda akauzwa kwa pauni milioni 70. (Mail)', 'United pia inamlenga mshambuliaji wa Lille na nyota wa kimataifa wa Ivory Coast Nicolas Pepe, 24, ambaye thamani yake inakadiriwa kuwa £70m, kuchukua nafasi ya mshambuliaji wa Ubelgiji Romelu Lukaku endapo atajiunga na Inter Milan. (Times)', 'Kiungo wa kati wa Kimataifa wa Serbia na Lazio Sergej Milinkovic-Savic, 24, amewaambia wachezaji wenzake kuwa ataondoka klabu hiyo msimu huu licha ya tetesi huendaakajiunga na Manchester United. (Il Tempo via Express)', 'Chelsea na West Ham wanapania kumsajili kwa mkopo winga wa Portsmouth Leon Maloney, 18 ambaye ameifungia Pompey academy mabao 26 msimu uliopita. (Sun)', 'Wolfsburg na RB Leipzig wanataka kumsajili kwa mkopo winga wa Arsenal wa miaka 18 Muingereza Emile Smith Rowe. (Independent)', 'Crystal Palace na Aston Villa wanataka kumsajili kiungo wa kimataifa wa Jamhuri ya Ireland anayecheza safu ya mashambulizi Jonathan Afolabi ambaye aliondoka Southampton mwisho wa msimu uliopita. (Football.London)', 'Sheffield United ambao wamepandishwa daraja kushiriki ligi kuu ya Premia wanatafakari uwezekano wa kumnunua kipa wa zamani wa kimataifa wa England Joe Hart, 32, kutoka Burnley. (Mail)', 'Villa wanashauriana na kipa wa Juventus, Mtaliano Mattia Perin baada ya uhamisho wake £13m kwenda Benfica kugonga mwamba baada ya kukosa uchunguzi wa kiafya. (Football Italia)', 'Barcelona wameweka dau la £24m kumnunua mlinzi wa Real Betis na Uhispania Junior Firpo. (Sport - in Spanish)', 'Tetesi Bora Jumatano', "Paris St-Germain wameishinda Juventus katika kinyang'anyiro cha kumsaini mlinzi wa Tottenham Danny Rose, 29, na wanaamini watafikia mkataba wa pauni milioni 20 kumsajili kiungo huyo wa kimataifa wa England . (Sun)", 'Naibu mwenyekiti mkuu wa Manchester United, Ed Woodward yuko mbioni kushughulikia suala la usajili wa wachezaji wapya, zikiwa zimesalia wiki mbili kabla ya muda wa mwisho wa uhamisho wa wachezaji kukamilia. (ESPN)', 'Woodward ana matumaini ya kukamilisha mchakato wa usajili wa mlinzi wa timu ya taifa ya England na klabu ya Leicester City, Harry Maguire, 26, na mchezaji wa safu ya kati wa Newcastle Sean Longstaff, 21. (London Evening Standard)', 'Meneja wa Liverpool Jurgen Klopp bado anapania kumnunua mchezaji mwingine mmoja msimu huu. (Liverpool Echo)', 'Mchezaji wa safu ya kati wa Sporting Lisbon na Ureno Bruno Fernandes, 24, amesema kuwa ataendelea kucheza katika ligi kuu ya Ureno licha ya tetesi zinazomhusisha na uhamisho wa kwenda Manchester United. (Mirror)', 'Mkufunzi wa Arsenal Unai Emery ana wiki mbili kuamua ikiwa atamuachilia winga wa England wa chini ya miaka-21 Reiss Nelson, 19, kujiunga na Hertha Berlin kwa mkopo msimu ujao. (Sun', 'Tottenham wanakaribia kumsaini kiungo wa kati wa Real Betis Muargentina Giovani lo Celso, 23, kwa kima cha pauni milioni 45. (Sun)']
5michezo
NA MWANDISHI WETU BARAZA la Sanaa la Taifa (Basata), limempongeza na kumpa usajili wa bure msanii, Joseph Stanford, aliyetembea kwa miguu umbali wa zaidi ya kilomita 1,200 kwa ajili ya kumpongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. John Magufuli. Stanford alitembea kutoka Mwanza kwenda Dar es Salaam kwa lengo la kupongeza utendaji na uundaji wa Idara ya Sanaa iliyo chini ya Wizara ya Habari, Michezo, Sanaa na Utamaduni wa Rais Magufuli. Kutokana na kujitoa huko kwa nchi, Basata imemsajili bure msanii huyo ili atambuliwe rasmi katika tasnia ya sanaa na baadaye kufanya kazi zake kwa kuzingatia sheria, kanuni na taratibu za sekta hiyo. Katibu Mtendaji wa Basata, Godfrey Mngereza, alisema Stanford ameonesha uzalendo wa hali ya juu kwa nchi yake kwani haikuwa kazi rahisi kutembea umbali mrefu usiku na mchana hadi kufika na kumpongeza Rais Magufuli. “Sisi kama Baraza tunafarijika sana, tunafurahi kuona wasanii na vijana kwa ujumla mnakuwa wazalendo na kufurahishwa na kasi ya utendaji wa Serikali ya awamu ya tano. Tunafurahi zaidi unapopeleka ujumbe wa wasanii kwamba wamefurahia kuundwa kwa idara ya sanaa,” alisema. Naye Stanford alifurahishwa na mapokezi ya Basata lakini alisisitiza kwamba ndoto yake ni kumfikishia salamu za pongezi Rais Magufuli huku akiamini kwamba atapata mafanikio kupitia kazi za sanaa. Msanii Stanford anatokea eneo la Mabatini jijini Mwanza na ametembea kwa siku 25 kutoka Mwanza hadi Dar es Salaam na ametumia kiasi cha shilingi 45,000 pekee.
5michezo
SHIRIKA la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Wakimbizi (UNHCR) lipo tayari kuingia kwenye mjadala na serikali kuangalia njia mbadala za kuwasaidia wakimbizi wanaohudumiwa hapa nchiniPia limeahidi kufuatilia kila aina ya mavazi yanayoingizwa nchini kuwasaidia wakimbizi ili kuhakikisha hayaingii mavazi yanayofanana na sare za wanajeshi kama ilivyotokea karibuni na kuleta mtafaruku.Akizungumza na waandishi wa habari jana Jijini Dar es Salaam, Mkuu wa UNHCR, Fillippo Grandi alisema Tanzania imekuwa ikisaidia wakimbizi kwa miaka mingi na kuna changamoto ambazo UNHCR imebaini na kuwa zinahitajia mjadala wa pamoja na serikali ili kuwasaidia wakimbizi waliopo nchini.Alizibainisha changamoto hizo kuwa ni pamoja na njia bora za kuwahudumia wakimbizi ambapo alisema kuwa wakimbizi sio lazima wakae kambini tu kama ilivyo ila wanaweza kufanya shughuli za kiuchumi. Alitolea mfano kwenye kambi ya Nyarugusu ambapo awali kulikuwa na soko lililokuwa likitumiwa na wakimbizi hao pamoja na wananchi wa eneo jirani kuuzia na kununua mazao kama njia mojawapo ya wakimbizi kujipatia kipato na kuwa kutokana na kufungwa kwa soko hilo baadhi yao sasa wameathirika.Pia alisema kwenye mfumo wa kuwapokea wakimbizi kuna changamoto za baadhi kukataliwa kuingia nchini wakati wengine ni wagonjwa. Alisema kuna haja ya kuwapokea kwanza wote wanaoomba kuingia. Aliongeza kuwa licha ya Tanzania kufanya kazi kubwa ya kuwapokea wakimbizi hao nchini na kuwasaidia kwa kila hali, imeonekana bado kuna changamoto ambazo UNHCR na wadau wengine wanalo jukumu la kusaidiana na Tanzania kuzitatua hasa kwenye sekta ya elimu, afya na maji. “Tanzania inakabiliwa na changamoto kadhaa katika namna ya kuwapokea na kuwarejesha majumbani kwao wakimbizi.Sina maana ya kuwa haifanyi kazi nzuri ila ninachomaanisha kuwa kuwa kuna haja ya kuwa na mjadalana Serikali tena shirikishi kubainisha sababu za changamoto hizo na kuzitatua,” alisema. Pia alisema suala la wakimbizi kurejea makwao linatakiwa kuwa ni la hiari zaidi na sio lazima au mkimbizi kuwekewa mazingira yoyote ya kuwalazimisha wakimbizi kurejea kwenye nchi waliyotoka.Aliongeza kuwa nchi ambazo wakimbizi wanarejea makwao pia zinapaswa kuandaa mazingira rafiki ya kiuchumi kwa wakimbizi ambayo yatawawezesha kuendeleza shughuli za kiuchumi kwa muda mrefu. Kuhusiana na mavazi yanayofanana na sare za jeshi yaliyokamatwa kambi ya wakimbizi Kigoma, Grandi alibainisha, sio lengo la UNHCR kuziingiza nchini na kuwa zilitokana na misaada ya watu mbalimbali. Alisema kuna nchi ambazo mavazi ya aina hiyo ni kitu cha kawaida na ndio walisaidia kuyaingiza nchini.Hata hivyo, alikiri k hilo ni kosa kwa kuwa haitakiwi mavazi yenye kuendana na sare za kijeshi kupewa wakimbizi kwani haitakiwi kujihusisha na shughuli za kijeshi hivyo hata mavazi yanayofanana sio mazuri. Mkuu huyo wa UNHCR alipongeza juhudi za Rais Mstaafu wa awamu ya tatu, Benjamin Mkapa za kupigania amani nchini Burundi na kutoa mwito kwa nchi za Burundi na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC) kupigania amani kwenye nchi zao ili wakimbizi waliotoka huko warejee nchini mwao.“Nimekutana na Rais John Magufuli, Waziri wa Mambo ya Nje, Augustine Mahiga na mawaziri wengine wanaohusika moja kwa moja na kuhudumia wakimbizi na nimefanya majadiliano yenye tija kubwa kwa faida ya wakimbizi. Ninaishukuru Tanzania kwa msaada wao mkubwa kwa wakimbizi hawa, “alisema. Grandi aliwasili nchini Jumanne wiki hii na kufanya mazungumzo na Rais Magufuli, Ikulu, Dar es Salaam ambapo alimwomba radhi kwa kupatikana kwa sare za jeshi kwenye kambi ya wakimbizi ya Kigoma.
3kitaifa
Simba na Azam FC zinagombania nafasi ya pili katika LigiKuu msimu huu zikitofautiana kwa pointi nne, huku kila mmoja ikionesha shauku ya kutaka kushinda katika mchezo huo ili kushiriki michuano ya kimataifa mwakani.Mabingwa wa zamani, Azam FC wako nafasi ya pili wakiwa na pointi 45 baada ya 23 wakati Simba iko nafasi ya tatu ikiwa na pointi 41 baada ya mechi 24.Yanga juzi ilitwaa ubingwa kwa kufikisha pointi 55 ikiwa na mechi mbili mkononi, pointi ambazo haziwezi kufikiwa na timu nyingine 13 zinazoshiriki ligi hiyo msimu huu wa 2014/15.Akizungumza na gazeti hili, Kopunovic alisema wanaitaka nafasi ya pili na ili kupata nafasi hiyo, ni lazima waifunge Azam FC. “Ni wakati wetu sasa kushiriki michuano ya kimataifa, yote hayo yanawezekana kimahesabu… ambo la muhimu ni kujipanga kwa mapambano,” alisema Kopunovic na kuongeza kuwa ili kufanya vyema, huwa na kawaida ya kuzungumza na wachezaji wake na kuwapa mbinu za ushindi.Alisema katika mchezo ujao, anatarajia kuwatumia baadhi ya wachezaji ambao hawakupata nafasi ya kuonekana katika baadhi ya michezo iliyopita. Miongoni mwao ni Dan Sserunkuma, nyota wa Uganda anayesugua benchi.Kopunovic alisema mfungaji bora huyo wa Ligi Kuu ya Kenya msimu uliopita, walikuwa katika majadiliano naye, lakini sasa mambo yanakwenda vizuri.Alisema anakiamini kikosi chake kwani kina vijana wengi wenye nguvu ambao wanacheza vizuri na kwa kujituma. Wakati Simba ikionesha tumaini la kushinda mchezo huo, mabingwa wa msimu wa 2013/14, Azam FC imekubali yaishe baada ya kupokonywa ubingwa na Yanga.Meneja wa Azam FC, Jemedari Said alisema jana kuwa hawana jinsi kwa sasa kwani kilichowarudisha nyuma kuna sehemu walijichanganya hivyo wanajipanga kuchukua nafasi hiyo ya pili.Said alisema watahakikisha wanapambana kwa uwezo wao kuchukua nafasi ya pili ili kuendelea kushiriki michuano ya kimataifa mwakani kama ambavyo imekuwa katika misimu mitatu iliyopita.
5michezo
Na NORA DAMIAN-DAR ES SALAAM KAMPUNI ya Magazeti ya Mwananchi Communication Limited (MCL), imeiomba serikali na vyombo vya ulinzi na usalama kusaidia kumtafuta Mwandishi wa Habari wa Gazeti ma Mwananchi, Azory Gwanda (42), aliyetekwa na watu wasiojulikana hivi karibuni. Gwanda alitoweka katika mazingira ya kutatanisha Novemba 21, mwaka huu, akiwa katika kituo chake cha kazi wilayani Kibiti, Mkoa wa Pwani. Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana, Mkurugenzi Mtendaji wa MCL, Francis Nanai alisema hadi sasa hawajapata taarifa zozote kutoka Jeshi la Polisi kuhusu kupotea kwa mwandishi huyo. “Gwanda alianza kuliandikia Mwananchi Septemba, mwaka 2015 na hatukuwahi kupata taarifa zozote kutoka kwake juu ya kutishiwa maisha. “Kwa hali tuliyonayo, hatuwezi kusema kazi yake ya mwisho aliyoifanya ni ipi, lakini tunaomba kama ameshikiliwa kwa kosa lolote apelekwe kwenye vyombo vya sheria ili haki itendeke,” alisema Nanai. Kwa mujibu wa Nanai, MCL wanatarajia kuandika barua kwa taasisi mbalimbali kuonyesha jinsi gani wasivyoridhishwa na utekwaji wa mwandishi wao wa habari. Barua hizo zitakwenda kwa Mkuu wa Jeshi la Polisi, Waziri wa Habari, Sanaa, Utamaduni na Michezo, Spika wa Bunge, Jukwaa la Wahariri Tanzania (TEF), Chama cha Wamiliki wa Vyombo vya Habari Tanzania (MOAT), Baraza la Habari Tanzania (MCT), Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC), Taasisi ya Vyombo vya Habari Kusini mwa Afrika (Misa–Tan) na Mtandao wa Watetezi wa Haki za Binadamu (THRDC). ALIVYOTOWEKA Akizungumzia jinsi tukio lilivyotokea, Nanai alisema kwa mara ya mwisho mwandishi huyo aliwasiliana na ofisi za Mwananchi, Novemba 20 mwaka huu kwa majukumu ya kikazi. “Kwa mujibu wa mkewe, Anna Pinoni (35) asubuhi ya Novemba 21, mwaka huu watu wanaokadiriwa kuwa wanne wakiwa na gari aina ya Toyota Land Cruiser lenye rangi nyeupe, walifika katikati ya mji wa Kibiti sehemu ambayo Gwanda hupatikana mara kwa mara na kumchukua. “Baadaye gari hilo lilielekea shambani kwake saa nne asubuhi na kumkuta mkewe huyo akiwa huko. “Kwa hiyo, Gwanda aliyekuwa amekaa kiti cha nyuma kwenye gari hilo alimuita mkewe huyo na kumuuliza alikokuwa ameweka ufunguo wa nyumba yao. “Mkewe alilisogelea gari na kuzungumza naye kutokea dirishani na kumwelekeza alipoficha ufunguo. Baadaye, Gwanda alimwambia mkewe huyo kwamba amepata safari ya dharura na kama asingerudi siku hiyo angerudi siku inayofuata kwa maana ya Novemba 22. “Tangu siku hiyo, Gwanda hajaonekana tena na namba zake za simu za mkononi hazipatikani. JUKWAA LA WAHARIRI Mwenyekiti wa Jukwaa la Wahariri (TEF), Theophil Makunga, jana alilisema tukio la kutoweka kwa mwandishi huyo linatishia uhuru wa vyombo vya habari nchini. “Kuna nia ovu katika kukamatwa kwa Gwanda kwa sababu kama alifanya kosa la jinai, sheria ingechukua mkondo wake.” alisema Makunga. UTPC YALAANI Nao Umoja wa Vilabu vya Waandishi wa Habari Tanzania (UPTC), umeviomba vyombo vya ulinzi na usalama kufanya uchunguzi wa haraka ili kufanikisha kupatikana kwa mwandishi huyo. Rais wa UTPC, Deogratious Nsokolo, alisema jana, kuwa wamepokea taarifa hiyo kwa mshtuko na wanalaani kitendo hicho.
3kitaifa
MAMBO yameanza kuiva kuelekea Uchaguzi wa Serikali za Mitaa baadaye mwaka huu na kuanzia leo wadau wataanza kutoa maoni yao kuhusu kanuni za uchaguzi huo. Kwa mujibu wa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, Selemani Jafo, maandalizi ya uchaguzi wa serikali za mitaa yanaenda vizuri na kinachosubiriwa kwa sasa ni kukamilika kwa kanuni za uchaguzi huo.Vyama vya siasa vyenye usajili vinatarajia kutoa maoni yao kwenye kanuni zitakazoongoza uchaguzi huo kuanzia leo Aprili Mosi na kesho Aprili 2, mwaka huu jijini Dodoma.Jafo aliyasema hayo alipozungumza na gazeti hili jijini hapa kuhusu maandalizi ya Uchaguzi wa Serikali za Mitaa unaotarajia kufanyika baadaye mwaka huu. Alisema maandalizi yote ya msingi kwa ajili ya uchaguzi huo yamefanywa na kuwa kwa sasa wanasubiri kukamilika kwa kanuni zitakazosimamia uchaguzi huo.Jafo alisema ofisi yake imepanga kukutana na vyama vya siasa vyenye usajili kwa ajili ya kupata maoni yao kwa ajili ya kanuni hizo kwa siku mbili za Aprili Mosi na 2, mwaka huu jijini Dodoma. Alisema Aprili 3, mwaka huu, utakuwa ni fursa kwa asasi za kiraia kutoa maoni kwenye kanuni hizo na baada ya hapo kurekebishwa tayari kwa kuanza kutumika.“Maandalizi ya Uchaguzi wa Serikali za Mitaa yanakwenda vizuri, na kwa sasa tuko katika hatua za mwisho za kukusanya maoni ya wadau kuhusu kanuni za uchaguzi zilizoandaliwa,” alisema Jafo. Aliongeza, “baada ya kupokea maoni ya vyama vya siasa vyenye usajili na kutoka kwa asasi za kiraia, na baada ya kukamilika kwa kanuni tutatangaza tarehe ya uchaguzi. Kimsingi maandalizi yote ya awali yamekamilika.”Katika Uchaguzi wa Serikali za Mitaa unaotumika kuchagua viongozi wa mitaa, vitongoji na vijiji uliofanyika Desemba 14 na 21, mwaka 2014, ulishirikisha vyama 15.Katika uchaguzi huo, Chama Cha Mapinduzi (CCM) kilifanya vizuri kwa kupata asilimia 84 za kura na kikifuatiwa na Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) na Chama cha Wananchi (CUF) kikishika nafasi ya tatu.
3kitaifa
WANAFUNZI wote katika shule za bweni nchini, wametakiwa kupimwa kujiridhisha na afya zao, ikiwemo ugonjwa wa kifua kikuu (TB) na kuondokana na ujazaji wa fomu za afya bila kupimwa.Agizo hilo limetolewa na Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu ambaye ameagiza shule zote za bweni, kutekeleza kazi hiyo na wakati huo huo waganga wakuu wa kila mkoa, wametakiwa kufanya ukaguzi kama utekelezaji umefanyika.Ummy alisema hayo jana jijini Dar e s Salaam wakati akikabidhi magari 10 na pikipiki 35 kwa uongozi wa mikoa, kwa ajili ya kusimamia na kuhakikisha wananchi wanapatiwa huduma ya kifua kikuu na ukoma ipasavyo.“Waganga wakuu wote, pitieni mkague shule zilizoko katika mikoa yenu, hakikisheni wanafunzi wamepimwa na siyo kujaziwa fomu za afya kiholela huku afya zao zikiwa hazieleweki,” alisema Ummy.Alisema, “Wazazi wamekuwa wakishiriki kutoa fedha hata elfu kumi ili watoto wao wajaziwe fomu za afya mashuleni, bila kupimwa, jambo ambalo linaonesha kuwa hakuna umakini katika kuzingatia afya.” Aliwataka madaktari kuzingatia miiko ya kazi zao kwa weledi kama inavyostahili. Alisema ni muhimu kwa waganga wakuu wa mikoa na wilaya, kutembelea shule za bweni kujua kama wanafunzi wamepimwa.Aliwaelekeza kukagua fomu za afya, kwa kuwa wapo wanafunzi wanaokwenda shuleni wakiwa wanaumwa, jambo ambalo wanaweza kuambukiza wengine. Kuhusu magari na pikipiki, alisema yamenunuliwa na serikali kupitia wizara wakishirikiana na Shirika la Kijerumani la Mapambano dhidi ya Kifua Kikuu na Ukoma (GLRA).Yamegharimu Sh milioni 778 lengo likiwa ni kuhakikisha huduma zinawafikia wananchi kwa wakati. Alisema yatasaidia katika usimamizi wa shughuli za mpango, kuhakikisha wagonjwa wa kifua kikuu na ukoma wanapatiwa elimu, wanagunduliwa na kupatiwa matibabu.Alitaja mikoa iliyokabidhiwa magari hayo ni Lindi, Tabora, Songwe, Kilimanjaro, Ilala, Mtwara, Kagera, Rukwa, Ruvuma na Pwani. Pikipiki zimegawiwa katika halmashauri 35. Kwa mujibu wa waziri, kila mwaka Tanzania inakadiriwa kuwa na wagonjwa wapya wa kifua kikuu wapatao 154,000.Kati yao, asilimia 44 ndiyo waliogunduliwa. Mwakilishi Mkazi wa GLRA, Burchard Rwamtoga alisema kuanzia mwaka 2016 shirika limekuwa likisaidia wizara kununua magari kwa bei nafuu hususani fedha zinazotolewa na Global Fund.Alisema ununuzi wa magari kwa njia hiyo, una nafuu na wamenunua magari matatu zaidi na pikipiki 35 badala ya 28.
3kitaifa
MRADI wa Maji wa Itumba Isongole wenye thamani ya zaidi ya Sh milioni 800 wilayani Ileje mkoani Songwe, umekataliwa kuwekewa jiwe la msingi na Kiongozi wa Mbio za Mwenge kutokana na nyaraka ya taarifa na ile ya ujenzi kutofautiana hivyo gharama kuongezeka bila kuonyesha nyaraka inayoonesha mabadiliko hayo ya gharama. Kiongozi wa Mbio za Mwenge 2019, Mkongea Ali alisema wamegundua baadhi ya upungufu kwenye mradi huo ambayo yamewafanya kushindwa kuweka jiwe la msingi ambao ukikamilika utahudumia zaidi ya watu 3,000 katika kata za Itumba na Isongole.Alitaja upungufu kuwa ni nyaraka za kwenye mkataba kuongezeka bila kuandaa nyaraka za mabadiliko na mtalaamu mshauri kutokuwepo kwenye mradi wakati mbio za Mwenge zikiukagua mradi huo muhimu.“Mshauri wa mradi ni mtu muhimu sana sasa kwa nini hayupo hapa wakati yeye ndiye mwakilishi wa serikali , nani atatupa maelezo yanayoeleweka kama yeye hajajua umuhimu wake na umuhimu wa mbio za Mwenge kwenye miradi ya serikali,” aliuliza Ali. Alisema kwa kawaida kama kuna mabadiliko ya nyaraka katika mradi kwa sababu hizi ni fedha za serikali lazima iandaliwe nyaraka muhimu inayoashiria au kuonesha namna gharama zilivyoongezeka kwenye mradi huo. “Pia kwa nini msimamizi aliruhusu gharama kuongezeka kwenye mradi huu bila maelekezo au nyaraka yoyote inayoonesha gharama kuongezeka,” alihoji.Alimwagiza Mkuu wa Wilaya ya Ileje, Joseph Mkude kufanya uchunguzi akishirikiana na vyombo husika ili hatua zichukuliwe kama kutabainika ubadhirifu fedha za serikali.Naye mhandisi wa mradi huo, Abdallah Digelo alisema kuna gharama zilizoongezeka katika mradi kutokana na mabadiliko ya uboreshaji wa tangi na pia miundombinu ya eneo hilo kuwafanya kusafisha vifaa vingi vya ujenzi kwa kubebwa kwa kichwa hali iliyosababisha gharama kuongezeka na kuchelewa kwa mradi huo.
3kitaifa
Matokeo hayo yanaifanya Yanga kujiwekea mazingira mazuri ya kutwaa ubingwa kwani sasa imefikisha pointi 43 huku bingwa mtetezi Azam ikiwa na pointi 37 baada ya jana kulazimishwa sare ya bao 1-1 na Mbeya City kwenye uwanja wake wa nyumbani, Azam Complex Chamazi.Aidha ushindi huo ni kama salamu kwa Etoile du Sahel ya Tunisia ambayo Yanga itacheza nayo raundi ya 16 kwenye michuano ya Kombe la Shirikisho Afrika kati ya Aprili 17, 18 au 19 mwaka huu.Mshambuliaji Mrundi Amissi Tambwe ndiye aliyekuwa shujaa wa Yanga katika mchezo huo baada ya kufunga mabao manne na kufikisha idadi ya mabao tisa kwenye mechi za Ligi Kuu Tanzania bara.Tambwe alianza kuifungia Yanga bao la kwanza dakika ya tisa akimalizia kwa kichwa mpira wa Sherman aliyeurudisha ndani baada ya mpira wa adhabu ndogo uliopigwa kutoka kaskazini mwa Uwanja wa Taifa Dar es Saalam. Simon Msuva aliifungia Yanga bao la pili katika dakika ya 23 baada ya kuunganisha pasi safi ya Haruna Niyonzima.Tambwe aliifungia Yanga bao la tatu katika dakika ya 34 akiunganisha mpira wa shuti uliopigwa na Juma Abdul. Kabla ya bao hilo, Tambwe alikosa bao katika dakika ya 31 baada ya mpira aliopiga kugonga mwamba wa juu na kurudi uwanjani.Mchezaji huyo wa zamani wa Simba alikuwa nyota wa mchezo jana baada ya kufunga bao la nne katika dakika ya 48, na dakika mbili baadae Sherman alifunga bao la tano na la kwanza tangu ajiunge na Yanga kwenye dirisha dogo la usajili Desemba mwaka jana.Yanga iliendelea kuutawala mchezo huo uliochezeshwa na mwamuzi Simon Mbelwa wa Pwani na dakika ya 86 Msuva alifunga bao la sita akitumia vizuri pasi ya Tambwe, wakati mashabiki wakiwa bado wamesimama kushangilia bao hilo kiungo Salum Telela alifunga bao la saba kwa mpira alioupiga kiufundi akiwa nje ya eneo la hatari na mpira kumshinda kipa wa Coastal Union, Bakari Fikirini dakika ya 88.Wakati mashabiki wakiamini matokeo yatabaki hivyo Tambwe alihitimisha karamu ya mabao kwa upande wa Yanga dakika ya 90 baada ya kufunga bao la nane akipokea pasi nzuri kutoka kwa Niyonzima na kabla ya kufunga alimlamba chenga kipa wa Coastal, Bakari Fikirini na kuujaza mpira wavuni.Coastal Union inayofundishwa na kocha Jamhuri Kihwelo ‘Julio’ ilishindwa kuonesha ushindani katika mchezo huo licha ya dakika za awali mshambuliaji wake Mnigeria Iker Bright na kiungo Abdulhalim Humud kuonesha juhudi za kukabiliana na wachezaji wa Yanga.Baada ya kuona mambo magumu kipindi cha pili Julio, aliwatoa Mohamed Ally, Bright na Rajabu Mohamed na nafasi zao kuchukuliwa na Abbasi Athuman, Mohamed Mtindi na Shekuwe Mohamed lakini mabadiliko hayo hayakumsaidia.Kwa upande wa kocha wa Yanga, Hans van der Pluijm, aliwapumzisha Mbuyu Twite, Sherman na Oscar Joshua na nafasi zao kuchukuliwa na Hassan Dilunga, Nizar Khalfan na Andrew Charles na mabadiliko hayo yalimsaidia kuongeza idadi ya mabao.Kwenye uwanja wa Azam Complex Chamazi, wapinzani wa Yanga kwenye mbio za ubingwa wa Tanzania bara Azam FC walilazimishwa sare ya 1-1 na timu ya Mbeya City matokeo ambayo yameifanya Yanga kuiacha Azam kwa pointi sita, lakini yenyewe ikiwa pungufu kwa mchezo mmoja.Yanga: Ally Mustapha, Juma Abduli, Oscar Joshua/ Andrew Charles,Klevan Yondan, Nadir Haroub, Mbuyu Twite/Hassan Dilunga, Salum Telela, Simon Msuva, Haruna Niyonzima, Kpah Sherman/Nizar Khalfan, Amissi Tambwe.Coastal: Bakar Fikirini, Juma Hamadi, Mfuko Abdallah, Chuma Yusufu, Mtama Bakari, Abdulihalim Humud, Mohamed lly/Athuman Abassi, Yahya Ayoub, Rajabu Mohamed/Mohamed Mtindi,Iker bright/Shekuwe Mohamed na Rama Salim.
5michezo
Amina Omari,Muheza RUSHWA ya ngono imeelezwa ni miongoni mwa vitendo vya ukatili ambavyo vinaongoza kurudisha nyuma juhudi za maendeleo ya mwanamke nchini. Hayo yalisemwa na Ofisa Programu Harakati na Ujenzi wa Pamoja kutoka Mtandao wa Kijinsia Tanzania (TGNP), Anna Sangai wakati wa semina ya kuwajengea uwezo waandishi wa habari kuripotia habari za jinsia. Alisema kwa mujibu wa takwimu za ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS) za mwaka 2016/18, zinaonyesha  asilimia 45 ya wanawake kati ya umri wa miaka 15 -49, wamekuwa waathirika wa ukatili wa kijinsia,huku asilimia 25, ikiwa ukatilia wa kuumizwa mwili. Alisema vitendo vya unyanyasaji wa kingono,vimekuwapo pale ambapo mwanamke anashida ya kutafuta ajira,fursa za kimasomo na hasa nyakati za uchaguzi “Vitendo hivi vimekuwa vikichangia kuwaumiza wanawake kisaikolojia na ukandamizwaji wao,”alisema Sangai. Alisema mtandao huo,umekuwa na kazi ya kusaidia kujengea uwezo wanawake ili kutambua haki zake. Ofisa Habari wa TGNP, Monica John alisema vyombo vya habari vinajukumu la kuhakikisha wasaidia kundi hilo kupata haki zao . Alisema  kusaidia kundi hilo kutambua haki zao, ikiwamo huduma bora za afya ,ushiriki wa wanawake katika uongozi na chaguzi mbalimbali. Baadhi wa wanawake wa Kata ya Zirai, walisema mfumo dume wa wanaume kumiliki mali na ardhi, imekuwa ni kikwanzo cha maendeleo ya mwanamke. “Mwanamke wa vijijini hauna haki ya kushiriki  ngazi ya uamuzi,tukiwa sehemu ya wazalishaji tunabaki tunaangalia tu,”alisema Joice Stanley. Alisema kuwa licha ya kata hiyo  kuongoza kilimo cha viungo,ubovu wa barabara umekuwa  changamoto ya mazao yao kufika sokoni mapema,” alisema.
3kitaifa
NA VERONICA ROMWALD – DAR ES SALAAM KIWANGO cha maambukizi ya ugonjwa wa matende na mabusha katika mikoa ya Dar es Salaam na Lindi, imeelezwa bado kipo juu kwa kati ya asilimia 10 hadi 12. Kauli hiyo ilitolewa Dar es Salaam jana na Mratibu wa Taifa wa Mpango wa Taifa wa Udhibiti wa Magonjwa Yasiyopewa Kipaumbele, Dk. Upendo Mwingira, alipowasilisha mada katika semina ya kuwajengea waandishi wa habari uelewa wa shughuli wanazozitekeleza na kutoa taarifa ya ugawaji wa dawa kinga kwa wakazi wa Dar es Salaam unaotarajiwa kufanyika Desemba 15 hadi 20, mwaka huu. Alisema ili kuukabili ugonjwa huo, Serikali ilianzisha mpango huo mwaka 2009 na ziliteuliwa halmashauri 121 zilizoonekana kuwa na kiwango cha juu cha maambukizi na wananchi kuanza kupewa dawa kinga. “Tunajua hivi sasa kuna jumla ya halmashauri 185, wakati ule tunaanza mpango tuliteua halmashauri 212 kati ya hizo, 93 sawa na asilimia 77 tumeweza kukabili maambukizi na huko hatugawi tena dawa kinga. “Zimebaki halmashauri 28 ambazo zina kiwango cha juu, kwa upande wa mikoa ya Dar es Salaam na Lindi ndizo zenye kiwango cha juu zaidi, tunaona Dar es Salaam mwamko wa wananchi kujitokeza kumeza dawa kinga bado ni mdogo. “Ndiyo maana tunawahamasisha wananchi kujitokeza kumeza dawa kinga hizi, matende na mabusha tunaweza kuyakinga mtu asipate kwa njia hii,” alisema. Hata hivyo, alisema mtu anapopata busha njia pekee ya kutibu ni upasuaji. Alisema hadi sasa tayari wanaume 1,000 wamefanyiwa upasuaji wa kutibu mabusha na wapo wengine 3,000 wanasubiri upasuaji huo. Awali, Ofisa Mpango huo ulio chini ya Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Oscar Kaitaba, alisema ugonjwa huo husababishwa na minyoo. Alisema vimelea vya minyoo hiyo hubebwa na mbu na pindi anapomuuma binadamu huingia ndani ya mwili wake na kwenda kuziba njia ya majimaji. “Miaka ya zamani ilifahamika kwamba mbu pekee anayeeneza ugonjwa huu ni aina ya culex, lakini tafiti mbalimbali zinazoendelea kufanyika duniani zinaonyesha mbu wa aina zote hata yule anayeeneza ugonjwa wa malaria anaweza kueneza ugonjwa huu,” alisema.
4afya
Na Renatha Kipaka BAADHI ya mama tilie katika Manispaa ya Bukoba  Kagera wanalia na ukata kutokana na vyakula vyao  kukosa wateja. Kauli hiyo  ilitolewa kwa nyakati tofauti na kina mama hao   katika soko kuu la Bukoba Hao ni  Fatima Abduri, Mariam Jabili na Koku Mgisha. Akizungumzia hali hiyo, Fatima   alisema tangu ameanza kufanya biashara hiyo sasa ni miaka 10 lakini hivi sasa mambo yamekuwa tofauti  kufikia   kupika kilo moja ya mchele wakati alikuwa akipika kilo 10 kwa siku. “Siku zilizopita nilikuwa napika kilo 10 na wakati mwingine zaidi ya hapo lakini sasa ninapika kilo moja nayo haiishi. “Hivi sasa wakati mwingine   ninatoka nyumbani nawaacha watoto   hawana uhakika wa kula, yaani inasikitisha,”alisema mama huyo. Naye Mariam  alisema    ushuru nao ni tatizo kwa sababu mkusanyaji  ushuru hajui siku hiyo wameuza au hawajauza. Alisema   ushuru huwa wanalipa Sh 13,000 kwa mwezi, inafika wakati fedha hiyo inakosa kutokana na ugumu uliopo. “Mimi kipindi kilichopita nilikuwa na uwezo wa kupika ndizi mikungu miwili, mchele kilo 15 na vina kwisha. “Nikifika nyumbani familia yangu inaishi kwa furaha lakini sasa imekuwa tofauti kama ninauza Sh 2,000   wakati nina watoto sita si hatari hiyo,”alisema. Koku Mgisha alisema baada ya kuona anapika chakula anakimwaga kwa kukosa wateja,  kukigawa au wakati mwingine kukikopesha, aliona ni bora afunge biashara  na kukaa  nyumbani kwake Rwamisenye. “Wakati mwingine nasema kuwa wakati wa mwezi mtukufu hali huwa inakuwa hivi ingawa wakati huu imekuwa tishio. “Mimi kwa upande wangu nitumie nafasi hii kuiomba serikali kuwapunguzia mama ntilie ushuru … kipato ni kidogo  na asilimia kubwa   tunategemewa na familia kwa maana ya watoto,” alisema Mgisha. Alisema miaka iliyopita alikuwa akipata hadi Sh 20,000  kwa siku  kama faida na mtaji pembeni.
3kitaifa
Na NORA DAMIAN-DAR ES SALAAM JUKWAA la Wahariri Tanzania (TEF) limesema Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dk. Harrison Mwakyembe, amekiuka Sheria ya Huduma za Habari ya mwaka 2016 kwa kujivika mamlaka ya kimahakama ambayo kimsingi hana. Kifungu cha 59 cha Sheria ya Huduma za Habari ya 2016 kinatoa mamlaka kwa waziri kuzuia maudhui katika habari na si kufungia chombo cha habari kama Waziri Mwakyembe alivyofanya kwa kulifungia gazeti la Mawio. Akizungumza na waandishi wa habari jana, Mwenyekiti wa TEF, Theophil Makunga, alisema mchakato mzima wa kulifungia gazeti la Mawio umekiuka sheria hiyo ambayo Serikali imekuwa ikisisitiza kuwa inalenga kusimamia weledi katika sekta ya habari. “Jambo la kushangaza ni kwamba waziri mwenye dhamana ameamua kukiuka sheria hiyo kwa kutoa adhabu ambayo kimsingi ina sura ya uonevu. Maudhui yanayopaswa kuzuiwa na waziri ni yale yanayohatarisha usalama wa nchi au usalama wa umma. “Tuhuma kwamba Mawio lilikiuka vifungu namba 50 (a), (b), (c), (d) na (e) vya sheria hiyo si za kweli kwani sehemu ya sheria inataja makosa ambayo mwandishi wa habari anaweza kutiwa nayo hatiani ikiwa atafikishwa mbele ya mahakama,” alisema Makunga. Alifafanua kwamba vifungu hivyo vinahitimishwa kwa adhabu inayotolewa na sheria kwa makosa husika ambazo ni faini kati ya Sh milioni tano hadi Sh milioni 20, kifungo kati ya miaka mitatu hadi mitano au vyote kwa pamoja. “Kwa kuwa waziri si mahakama, hana mamlaka ya kisheria ya kuwatia hatiani Mawio na hawezi kuwa rejea ya makosa yaliyotajwa katika sheria hii. “Tunahuzunishwa na utamaduni uliojengeka wa kuona kwamba adhabu pekee ya kukimbilia ni kufungia vyombo vya habari, wizara hii imeacha dhana nzima ya malezi na mashauriano, mwenendo huu hauna afya kwa sekta ya habari na nchi yetu,” alisema. Jukwaa hilo limeushauri uongozi wa gazeti la Mawio kwenda mahakamani kutafuta haki yake kama walivyowahi kufanya wakati gazeti hilo lilipofutwa Januari mwaka jana. Naye Katibu wa TEF, Neville Meena, alisema mazingira ya ufanyaji kazi kwa waandishi wa habari nchini bado ni magumu, lakini wamejipanga kutumia njia ya mazungumzo ambayo wanaamini yanaweza kuleta majibu ya matatizo mbalimbali yanayoikabili sekta hiyo. Mjumbe wa TEF, Jesse Kwayu, alisema vyombo vya habari si adui wa Serikali, bali vipo kwa mujibu wa sheria na kuitaka Serikali kuacha kuvunja sheria inayosimamia sekta hiyo. “Waziri Mwakyembe ajiulize mara mbilimbili ni mtu sahihi kusimamia uhuru wa habari? Yeye si bwana jela, amekwenda pale (wizarani) kusaidia sekta ya habari ikue,” alisema Kwayu.
3kitaifa
VINARA wa Ligi Kuu Tanzania Bara (TPL), Yanga, leo jioni watakuwa na kibarua kigumu kuikabili Biashara United ya Musoma kwenye Uwanja wa Taifa katika mchezo wa Kombe la Azam (FA).Yanga wanaoongoza ligi kwa pointi 53, wanaingia kwenye mchezo huo wakiwa na kumbukumbu ya kufanya vibaya kwenye michuano ya SportPesa baada ya kuondoshwa kwenye hatua ya awali na timu ya Kariobangi Sharks kwa kichapo cha mabao 3-1. Mchezo huo unatazamiwa kuwa mgumu kwa pande zote kutokana na Biashara kuonesha kiwango bora kwenye michezo yao ya hivi karibuni baada ya kupata kocha mpya Amri Said.Kuelekea kwenye mchezo huo Ofisa Habari wa timu hiyo, Dismas Ten alisema kikosi hicho kimejiandaa vyema kwa kufanya mazoezi ambayo yatawawezesha kuibuka na ushindi kwenye mchezo huo ili kuhakikisha wanatwaa kikombe cha michuano hiyo msimu huu. “Kikosi chetu kipo fiti kwa mchezo wa leo dhidi ya Biashara tunafahamu ni moja ya timu inayoleta upinzani mkubwa sana kwa michezo yao waliyocheza hivi karibuni, ukiwemo ule dhidi ya Azam FC, tumejipanga kwa ushindi,” alisema Ten.Alisema kwenye mchezo huo watawakosa nyota wao Baruani Abdallah na Jaffari Mohamed wanaosumbuliwa na maumivu waliyoyapata katika mchezo uliopita. Aidha, alisema jambo la furaha kwenye kikosi hicho ni kuona wachezaji wao Raphael Daud na Juma Mahazi kurejea kikosini kwa kufanya mazoezi madogo madogo baada ya kupona majeraha yao lakini leo hawatakuwepo.Kikosi hicho cha Mkongomani Mwinyi Zahera kama kitafanikiwa kuibuka na ushindi watacheza dhidi ya Namungo FC inayoshiriki Ligi Daraja la Kwanza, ambao wameshatinga kwenye 16 bora. MKATABA KAKOLANYA Kwa upande mwingine, Kaimu Mwenyekiti wa timu hiyo, Simon Lukumay alisema jana kuwa wamepokea barua kutoka kwa Mwanasheria wa mchezaji wao, Beno Kakolanya anataka kuvunja mkataba na klabu hiyo. Barua hiyo imekuja siku chache kutokana na kauli ya kocha Zahera kusema hamhitaji mchezaji huyo kwenye kikosi hicho kwa kuwa alionesha utovu wa nidhamu ndani ya timu hiyo. Sakata hilo lilianza muda mrefu baada ya mchezaji huyo kugoma.
5michezo
PARIS, Ufaransa VIONGOZI mbalimbali duniani wanatarajia kuwasili nchini hapa kushiriki  wiki nzima  ya  kumbukumbuku za Vita Kuu ya Kwanza ya Dunia kuanzia   jana. Kwa mujibu wa taarifa iliyololewa    na Serikali,  Rais Emmanuel Macron anajiandaa kuwapokea viongozi zaidi ya 80 ambao  watashiriki wiki  hii  ambako atakuwa mwenyeji wa viongozi akiwamo Rais wa Marekani, Donald Trump na mwenzake wa Urusi, Vladmir Putin. Mbali na kuwapokea viongozi hao, pia Rais Macron atafanya ziara kaskazini mwa nchi  akitembelea maeneo yaliyohushudia mapambano  yaliyosababisha vifo vya maelfu  ya wanajeshi m  kwenye mitaro. Tarifa hiyo ilieleza kiongozi huyo atatumia fursa hiyo ya kimataifa kutoa onyo dhidi ya kuongezeka kwa siasa kali za umaarufu  mbele ya Trump anayendeleza sera ya “Marekani Kwanza” na viongozi wengine wa siasa za uzalendo. Maadhimisho hayo yatafikia kilele chake katika sherehe itakayofanyika katika lango la Arc de Triomphe mjini hapa, Novemba 11 mwaka huu  na kuhudhuriwa na viongozi kadhaa akiwamo Trump, Putin na Kansela wa Ujerumani, Angela Merkel, miaka 100 tangu kusainiwa makubaliano ya kuacha mapigano. Hafla katika eneo la mnara wa Kaburi la Mwanajeshi Asiyejulikana kwenye mtaa wa Champs-Elysees itafanyika huku kukiwa na  ulinzi mkali kutokana na mfululizo  wa mashambulio makali ya wanamgambo wa itikadi kali nchini hapa katika kipindi cha miaka mitatu iliyopita. Maadhimisho yalianza jana kwa tamasha la muziki linaloadhimisha urafiki kati ya maadui wawili wa zamani wakati wa vita, Ufaransa na Ujerumani, katika mji wa mpakani wa Strasbourg, ambalo lilihidhuriwa na Rais  Macron na Rais wa Ujerumani,  Frank-Walter Steinmeier. Pia kwa mujibu wa ratiba ya hafla hiyo, Rais Macron atatumia wiki nzima kuyatembelea maeneo yaliyoshuhudia mapambano katika upande wa magharibi, kutoka Verdun hadi Somme.
2kimataifa
Na KULWA MZEE-DAR ES SALAAM MRATIBU Msaidizi wa Jeshi la Polisi, ASP Kimweli, amedai alimsikia Mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Lissu, akisema dikteta uchwara ni lazima apingwe kwa nguvu zote kama amefanya utawala wa kijinga, hawawezi kuvumilia utawala mbovu wa kidikteta uchwara, hata kama alichaguliwa kuwa Rais. ASP Kimweli alidai hayo katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Godfrey Mwambapa, alipokuwa akitoa ushahidi wa upande wa mashtaka akiongozwa na Wakili wa Serikali Mwandamizi, Mohammed Salum. Shahidi huyo alidai maneno ya Lissu aliyotoa Juni 28, mwaka huu,  aliyaona ni ya uchochezi kwa sababu ni mbunge aliyechaguliwa na watu, mwanasheria na kiongozi wa chama, hivyo kuzungumza kwake mbele ya vyombo vya habari, maneno yangesambazwa na kuwa tatizo katika nchi. Alidai kuwa Lissu alipotoka ndani ya mahakama, alikuwa na kundi kubwa la watu, alifika nalo nje na kuanza kuzungumza. Kwamba alimsikia Lissu alisema nchi ipo ndani ya giza nene mamlaka ya Serikali mbovu ya kidikteta uchwara yanapaswa kupingwa kwa nguvu zote. “Dikteta uchwara huyu ni lazima apingwe kwa nguvu zote kama amefanya utawala wa kijinga, hatuwezi kuendelea kuvumilia utawala mbovu wa kidikteta uchwara, hata kama ulichaguliwa kuwa rais ni lazima kila mahali upingwe, hata kama tutapelekwa mahakamani kwa ajili ya kufungwa mdomo tutapambana tutashinda,” Kimweli alidai hayo maneno yalitamkwa na mshtakiwa. Alidai hakuchukua hatua yoyote wakati Lissu akitamka maneno hayo, kwa sababu alijua ni mtu anatambulika na anaweza kuitwa polisi wakati wowote. Akihojiwa na Wakili Peter Kibatala kwamba alibaini nini kuhusu dikkteta uchwara lazima apingwe, Kimweli alidai hakumtaja ni nani na wala yeye hakujua ni nani, na kwamba hakuna nchi iliyotajwa na wala hakueleza ni kwa namna gani ipingwe. Shahidi huyo alidai ni kweli mbunge wa upinzani anaruhusiwa kupinga Serikali iliyopo madarakani kwa nguvu zote, kwa demokrasia na kwa mujibu wa sheria. Kesi hiyo iliahirishwa hadi Januari 18, 2017 mashahidi wa upande wa mashtaka watakapoendelea kutoa ushahidi. Lissu anadaiwa kutoa kauli za uchochezi dhidi ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano.
3kitaifa
ZIKIWA zimesalia siku chache kwa Wizara ya Nishati kuwasilisha bungeni bajeti ya mwaka wa fedha 2019/20, Waziri wa Wizara hiyo, Dk Medard Kalemani amebainisha mafanikio yaliyopatikana kwenye sekta ya nishati.Waziri alibainisha mafanikio hayo katika kipindi cha miaka mitatu na kuiwezesha Tanzania kuingia kwenye rekodi ya dunia kuwa miongoni mwa mataifa machache yanayotekeleza miradi mikubwa ya nishati.Akizungumza mwishoni mwa wiki iliyopita wakati akifungua kikao cha Baraza la Wafanyakazi wa Wizara ya Nishati kilichofanyika jijini hapa, Kalemani alieleza kuwa Tanzania imeingia kwenye rekodi ya utekelezaji wa miradi mikubwa ya kimkakati ya uzalishaji nishati ya umeme.Alisema tangu kupatikana Uhuru, kwa Tanzania Bara vijiji 2,018 pekee ndio vilikuwa vimeunganishiwa umeme lakini katika kipindi cha miaka mitatu cha Rais John Magufuli akiwa madarakani, vijiji 7,012 vimeunganishwa kwenye nishati hiyo.“Hii inamaanisha kuwa katika kipindi cha miaka mitatu vijiji 5,000 vimeunganishiwa umeme. Sasa Watanzania wanafahamu kuwa umeme ni haki yao ya msingi ndio maana ukienda maeneo ambayo hakuna nishati hii basi wananchi watakusimamisha na mabango kuonesha uhitaji wao,” alisema.Alisema serikali bado inaendelea kupeleka umeme vijijini ambapo mwaka 2015 kulikuwa na vijiji takribani 2,000 lakini mwaka 2018 kulikuwa na vijiji 4,000 na sasa vijiji vilivyofikishiwa nishati hiyo vimefikia 7,012 ikiwa zaidi ya asilimia 240 ya vijiji vilivyokuwa na umeme kabla ya mwaka 2016.“Mafanikio hayo ni matokeo ya hatua ngumu za mabadiliko zilizochukuliwa ndani ya wizara hiyo nyeti kwa lengo la kuleta mageuzi na ufanisi katika kuwahudumia wananchi.”Aidha, Dk Kalemani alisema tayari mradi wa kuunganisha nishati ya gesi asilia umekwishaanza kutekelezwa ambapo jijini Dar es Salaam baadhi ya viwanda vimeunganishiwa ili kuongeza tija ya uzalishaji.“Kazi yetu ni kuwapelekea wananchi umeme. Tumejikita sana kwenye sekta hiyo kwa sababu kama mnavyokumbuka miaka mitatu iliyopita hali ya umeme nchini ilikuwa mbaya lakini sasa imeendelea kuimarika,” aliwaeleza wajumbe wa baraza hilo.Alisema serikali inatekeleza mradi mkubwa wa kuzalisha umeme kwa kutumia nguvu ya maji kwenye Mto Rufiji ambao taifa linajivunia.“Ni mradi wa 60 kati ya mabwawa 70 makubwa duniani. Kwa mara ya kwanza Tanzania tumeingia kwenye chati ya dunia kwa mabwawa ya kuzalisha umeme. Lakini pia kwa Afrika, tumeingia kwenye historia ya kuwa na mradi mkubwa wa nne na wa kwanza kwenye ukanda wa nchi za Afrika Mashariki,” alisema.
3kitaifa
Lisbon, Ureno MFANYAKAZI wa benki aliyekuwa akisimamia akaunti za kampuni ya mafuta Sonangol, ambayo mwenyekiti wake alikuwa Isabel Dos Santos katika benki ya EuroBic nchini Ureno, amekutwa amekufa mjini Lisbon Mfanyakazi huyo, Nuno Ribeiro da Cunha mwenye umri wa miaka 45 anahusishwa na kesi ya ufujaji na ulanguzi wa fedha za Isabel ambaye ni mwanamke tajiri barani Afrika, Isabel dos Santos. Akaunti alizokuwa akizisimamia zilikuwa katika benki ya EuroBic nchini Ureno ambayo Isabel ana hisa. Kifo chake hicho kilichotokea Jumatano kiliripotiwa Alhamisi muda mfupi tu baada ya waendesha mashtaka nchini Angola kuwataja wote wawili kama washukiwa. Da Cunha alipatikana amefariki katika mojawapo ya mali zake mjini Lisbon. Chanzo kimoja cha polisi kilikidokeza chombo cha habari cha Portugal kwamba huenda mshukiwa huyo alijiua. Vyombo vya habari nchini humo vilinukuu polisi wakisema Da Cunha alikuwa tayari amejaribu kujiua mwezi huu na kwamba alikuwa akiugua shinikizo la akili. Isabel Dos Santos ambaye anakabiliwa na kesi ya ufisadi nchini Angola, mara zote amekuwa akikana mashtaka hayo. Jumatano wiki hii Eurobic ilisema kwamba itasitisha uhusiano wake wa kibiashara na Isabel Dos Santos ambaye ameripotiwa kuwa mwanahisa mkuu wa benki hiyo kupitia kampuni mbili anazomiliki
2kimataifa
Juzi Katibu Mtendaji wa BASATA, Godfrey Mngereza alitoa tamko la kuufungia wimbo huo kutokana na kubeba ujumbe ambao unakejeli na kudhalilisha baadhi ya wasanii.Pia katika hoja zake za kuufungia wimbo huo Mngereza alisema kuwa msanii huyo amejidhalilisha mwenyewe pia kwa kuwa ameshindwa kufuata misingi na maadili ya kazi yake.Akizungumza kuhusiana na kufungiwa kwa wimbo huo msanii huyo ambaye katika wimbo wake huo pia amekejeli utendaji wa baraza hilo, alisema kuwa baraza hilo limechelewa kuufungia wimbo wake kwani tayari kila mtu anao.Alisema kuwa wapo wasanii ambao amegusia maisha yao na kuonekana kuwa ni kama vile ameingilia maisha ya watu binafsi ila kwa upande wake amefanya kazi yake kama msanii.“Najua nikisema kuwa Ray mtu mzima na amekuwa anafanya sanaa ya filamu muda mrefu lakini anaishi kwao, hapo nimekosea nini mimi naona ni kama vile nimefundisha kwanza,” alisema msanii huyo.Alisema: “Wasanii wamekuwa wakipenda kuwasema watu wengine na wao hawasemwi na hapo tunakuwa hatujajifunza kabisa na mimi nimewakumbusha kitu”.Wasanii waliotajwa kwenye wimbo huo ni Wema Sepetu, Ray na wengine wengi huku akilisema Basata kuwa ni baraza lisiloweza kung’ata.Nay wa Mitego amekuwa kwa muda mrefu akilaumiwa kwa nyimbo zake ambazo zimeonekana kuwakejeli watu wa aina mbalimbali na kwa miaka mingi amekuwa akifanya hivyo.Aliwahi kuimba wimbo uitwao Nasema Nao ambao nao ulikuwa ukigusia maisha binafsi ya wasanii wa aina mbalimbali wa muziki wa Bongo Fleva na Filamu.
5michezo
NA SAADA SALIM- ZANZIBAR YANGA imeanza kufungua jicho lake katika usajili mkubwa, ambapo tayari jina la beki wa kushoto wa Singida United, Shafiq Batambuze, limetua mikononi mwa kocha mkuu wa timu hiyo, George Lwandamina. Batambuze amekuwa chachu ya mafanikio ya Singida United katika Ligi Kuu Tanzania Bara msimu huu tangu alipotua katika kikosi cha timu hiyo wakati wa dirisha kubwa la usajili. Taarifa za uhakika zilizoifikia MTANZANIA jana kutoka kwa kigogo mmoja wa Yanga, zinasema kiwango cha maana kinachoonyeshwa na beki huyo katika michuano ya Mapinduzi na Ligi Kuu Tanzania Bara, kimewashawishi kuliwasilisha jina lake katika benchi la ufundi ili kuangalia uwezekano wa kumsajili. Alisema wanaamini beki huyo ataziba vema pengo la Haji Mwinyi ambaye anatakiwa na AFC Leopards ya Kenya. “Ni beki mzuri, nimefanikiwa kumwona katika mechi nyingi anazocheza, yupo vizuri, pia ni muhimu kwetu kuja kuchukua nafasi ya Haji aliyepata ofa Kenya,” alisema. Kigogo huyo alisema AFC Leopards bado wanamuwinda beki wao huyo, hatua inayowashawishi kutafuta mbadala wake mapema ambaye ni Mutambuze. Beki huyo alipoulizwa kuhusiana na uwezekano wa kuhamia Yanga, alisema haoni tatizo kama wataafikiana kwa kuwa soka ni kazi yake. “Kwa kuwa mkataba wangu unaniruhusu kuzungumza na timu nyingine waje tuzungumze, lakini kwa sasa sitaongea chochote,” alisema Mutambuze. Kuhusu dau analohitaji alisema hawezi kuliweka wazi hadi Yanga watakapozungumza na kukubaliana. MTANZANIA halikuishia hapo, lilimtafuta Mwenyekiti wa Leopards, Daniel Mule, ambaye alisema mpango wa kumsajili Haji upo pale pale. “Tunasubiri dirisha kubwa Juni tuanze mchakato wa kuingia mkataba na beki huyo wa Yanga,” alisema Mule.
3kitaifa
Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu (HESLB) leo, Jumanne (Juni 4, 2019), imetoa mwongozo wa utoaji wa mikopo kwa mwaka wa masomo 2019/2020.Mbali na mambo mengine, mwongozo huo unamtaka mwombaji kuandaa nyaraka muhimu kama vyeti vya kuzaliwa ambavyo vimethibitishwa na Wakala wa Usajili, Ufilisi na Udhamini (RITA), Wakala wa Usajili wa Matukio ya Kijamii Zanzibar (ZCSRA).Aidha, kwa waombaji mikopo ambao wazazi wao wamefariki dunia watatakiwa kuwa na nakala za vyeti vya vifo ambavyo vimethibitishwa na RITA au ZCSRA.Haya yamesemwa na Mkurugenzi Mtendaji wa Bodi hiyo, Abdul-Razaq Badru katika mkutano na waandishi wa habari huku akisisitiza kuwa mwongozo huo utawasaidia waombaji kuepuka makosa wakati wa kuomba mkopo.“Waombaji wengi hukimbilia kwenye mtandao na kujaza fomu za maombi wakati mwingine bila kusoma mwongozo, kwa mwaka wa masomo 2018/19 waombaji zaidi ya 9,000 kati ya 57,539 waliokuwa na sifa za msingi walikosea kujaza fomu za maombi,” aliongeza.Mwongozo huo unapatikana kwenye tofuti ya bodi hiyo.
3kitaifa
Wapambe wa wagombea wa wagombea wa nafasi ya uenyekiti wa Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM), leo wametwangana hadharani wakituhumiana kuwa matapeli wa kisiasa. Vurugu hizo zilijitokeza leo Ijumaa, Septemba 22 kabla ya uchaguzi wa nafasi hizo uliofanyika katika ukumbi wa Hoteli ya Golden Rose, ambapo kwa mujibu wa mashuhuda wa tukio hilo, vurugu hizo zinadaiwa kudumu kwa dakika zisizozidi 20, zilitokana na wapambe wa wagombea Jimmy Pamba na Godliving Kisila kutofautiana kauli. Mmoja wa wapambe wa Kisila, Hussein Abdallah anadaiwa kumtuhumu Lameck Dudu ambaye anadaiwa kuwa kambi ya Pamba kuwa si mjumbe wa mkutano huo na ni tapeli wa kisiasa hivyo hakupaswa kuwepo katika uchaguzi huo. Baada ya kauli hiyo Dudu anadaiwa kumrushia ngumi na kijana mmoja aliyefahamika kwa jina la Sylvester Meda na kuanguka chini, hali iliyosababisha wapambe wengine wa pande zote mbili kutokukubaliana na hali hiyo na kuanza kupigana. “Wamenipiga na kunichania nguo zangu lakini sijui kosa langu ni lipi, UVCCM Arusha imezungukwa na wahuni, chama kinapaswa kuwachukulia hatua wote walioiabisha Jumuiya kwa maslahi yao,” amesema Meda.
3kitaifa
Nchemba aliyasema hayo mwishoni mwa wiki bungeni mjini hapa wakati akijibu hoja mbalimbali za wabunge zilizotolewa katika mjadala wa hotuba ya bajeti ya Ofisi ya Waziri Mkuu na Tamisemi kwa mwaka wa fedha 2015/16.Akijibu hoja hizo, ambazo nyingi zilitolewa na wabunge wa vyama vya upinzani wakisema serikali haijafanya chochote katika miradi ya maendeleo bali kilichoongezeka ni deni ya taifa, Nchemba alisema hata kama TRA na Halmashauri zote nchini zingekusanya mapato kwa asilimia 100, zingefikia asilimia 62 ya bajeti.“Kwanza watu wanaotazama bunge hili huko nje wakiwasikia hawa wanaosema serikali haijafanya chochote watawashangaa, wengi wanalalamika deni la taifa limeongezeka, ila miradi ya maendeleo iliyofanywa hawaioni…”,alisema Nchemba.Alifafanua, ikiwa TRA pekee ingekusanya mapato kwa asilimia 100 fedha hizo zingekuwa ni asilimia 57 ya bajeti na kwamba kama rais angeamua asikope taifa lingekuwa wapi hivi leo, hakuna nchi iliyotulazimisha kukopa,ila hiyo asilimia inayobaki ya bajeti ni lazima ipatikane kwa wahisani,” alisema Nchemba.Na kuwashangaa wabunge wa upinzani ambao wamekuwa wakibeza miradi mbalimbali na kusema kama wanapenda miradi iliyofanywa ni lazima wapende na deni lililopo.“Hivi unalipendaji jengo la bunge tunalokaa humu ndani ambalo tumelijenga kwa mkopo halafu usiupende mkopo wenyewe, utakipendaje Chuo Kikuu cha UDOM, kilichojengwa kwa mkopo alafu usipende deni lake”, hivyo hivyo kwa miradi ya barabara, umapita kwenye barabara nzuri halafu hampendi madeni yake,” alihoji Nchemba.Na kusema miradi ipatayo 360 iliyotekelezwa nchini imekamilika na mingine iko kwenye hatua za mwisho kutokana na fedha za mikopo kutoka kwa wahisani wa maendeleo, na kwamba hata reli ambayo inagharimu Sh trilioni 15 ni fedha za mkopo.“Ni vyema tukatimiza wajibu wetu, na ni heri aliyechoka kwa kufanya kazi kuliko yule mvivu aliyechoka kwa kutotambua kazi zilizofanywa,” alisisitiza Nchemba.Na kusema deni la nchi lililofikia takribani Trilioni 30, Nchemba alisema bado linalipika kwani kuna viashiria vyote vinavyoonesha ulipikaji wake na kwamba nchi haiwezi kuendelea bila kuwa na mikopo.“Tumekopa nchi mbalimbali, India, China, Japan na nchi nyingine na fedha zimetumika kwenye miradi ya maendeleo na leo mmeona mafanikio yake , kuna mtandao wa barabara za lami ambao umerahisisha usafiri kwa wananchi na kuokoa muda.
1uchumi
MKUU wa Wilaya ya Ilala, Dar es Salaam, Sophia Mjema amesema atapitia upya mkataba wa mkandarasi wa kuzoa taka kwa kuwa hafanyi kazi inavyotakiwa.Mkandarasi huyo ni Kampuni ya Josen Co. Ltd ambayo kwa mujibu wa mkuu wa wilaya, licha ya kushindwa kufanya kazi ipasavyo, amekuwa akitumia nguvu katika ukusanyaji wa ada.Pia Mjema amemuagiza Ofisa Usafi na Mazingira kuhakikisha wanakaa na wakandarasi wanaofanya kazi ya ukusanyaji taka kukagua vifaa wanavyotumia kufanya kazi hiyo kwa sababu imekuwa ikifanyika chini ya kiwango.Akizungumza katika mkutano na wananchi wa Kata ya Tabata jana jijini Dar es Salaam, Mjema amesema haiwezekani kampuni hiyo iwe inakusanya taka mara moja kwa mwezi kwani hali hiyo inasababisha uchafu wa mazingira."Nitahakikisha tunawakagua wakandarasi wote wanaolalamikiwa na endapo tutabaini kuwa hawana vifaa vya kutosha kukusanya taka, tutawaondoa kwa sababu hawafai kuchukua zabuni hiyo," amesema Mjema.Amesema wakandarasi wengi wamekuwa wakifanya kazi kwa mazoea hivyo ni lazima wawafuatilie kuhakikisha shughuli za uzoaji taka zinafanyika ipasavyo. Aidha, alisema kampuni ya Joshen inalalamikiwa kutumia mabavu katika ukusanyaji wa ada za taka na kupandikiza chuki baina ya wananchi na serikali yao."Vijana wa Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) na mgambo kazi yao ni kuhakikisha hali ya usafi na kuwaandikia faini wasiotekeleza maagizo lakini hawapaswi kuingia kwenye vyoo wala nyumba za watu kukagua," amesisitiza.Wananchi wa eneo hilo wamemlalamikia mmoja wa wafanyakazi wa mkandarasi hiyo, aliyetambulika kwa jina la Hamad kwamba pamoja na vijana wenzake hawakusanyi taka badala yake wanafanya shughuli za mazingira, mapato na ukaguzi.Hassan Ally Mkazi wa Mtambani, alisema mkandarasi huyo amekuwa akifanya kazi tofauti na aliyopewa kwa ajili ya kukusanya ada na kuzoa taka."Tunalipia shilingi 3,000 kwa kila kaya lakini taka zinachukuliwa kwa mwezi mara moja. Lakini pia, hawafanyi kazi waliyopewa lakini hao hao ndio wanaowakamata wanawake na watoto wao kupeleka mahabusu kwa eneo watakalokuta chafu, ndiyo wanaokagua nyumba zetu kama safi au chafu hivyo hatujui ni kazi gani wanaotakiwa kufanya," amesema Ally.Mkazi wa Tabata Msimbazi, Valentina Aveline amesema suala la kuchangishwa Sh 3,000 kisha gari kufuata taka mara moja kwa mwezi halitakiwi kwa sababu mvua zitakapoanza kunyesha hali ya usafi itakuwa mbaya na kusababisha magonjwa.Amesema awali walikuwa wanalipa Sh 1,000 lakini taka zilikuwa zinakusanywa kila wiki na mkandarasi wa mwanzo, lakini mkandarasi aliyepo anasababisha hali mbaya ya mazingira.Grace Kalua alisema wanaomba manispaa hiyo kumuondoa mkandarasi aliopo kwa sababu hana uwezo wa kusomba takataka eneo hilo.Alisema takataka zimekuwa nyingi na mkandarasi badala ya kufanya kazi yake anaingilia kazi za watu wengine.Mpaka sasa Mjema amepokea malalamiko 135 yanayohusu huduma za afya, barabara, elimu, maji na mazingira katika kata 26 za manispaa hiyo akiwa na lengo la kutembelea kata zote 36 kwa lengo la kusikiliza kero za wananchi na kuzitatua.
3kitaifa
Kwa mujibu wa ratiba za shoo alizoweka kwenye mtandao wake Diamond, baada ya kufanya shoo kubwa Kigali, Rwanda inayofuata ni hiyo ya tuzo za Glow-CAF.“Nawashukuru mashabiki wa Rwanda kwa kuniunga mkono katika shoo kubwa katika sherehe za kuukaribisha mwaka, nawapenda wote, sasa najipanga kuelekea Nigeria,” alisema Diamond kwenye mtandao.Diamond, ambaye alipata mafanikio makubwa mwaka jana kwa kutwaa tuzo nyingi za kimataifa, atafanya shoo hiyo kubwa kisha atarudi Dar es Salaam kufanya nyingine kabla ya kwenda Zanzibar na Mwanza aliko alikuwa kwa ajili ya burudani.Kwa mujibu wa mtandao wa glowworld, wasanii wengine wa Afrika walioalikwa kutumbuiza ni Hugh Masekela kutoka Afrika Kusini, Flavor wa Nigeria, Fally Ipupa wa Congo DRC, Hakim kutoa Misri, Kikundi cha kwaya cha Pan African kutoka Soweto Afrika Kusini na kundi la P-Square.Katika tuzo hizo ambazo huandaliwa kila mwaka zaidi ya wachezaji 40 wa Afrika wanaocheza soka la kulipwa nje ya nchi zao, na wale wanaocheza ndani ya Afrika wanawania.Tuzo zinazowaniwa ni mchezaji bora wa Afrika wa mwaka anayecheza nje, pia anayecheza ndani ya Afrika, timu bora ya taifa ya mwaka, klabu bora ya mwaka na kocha bora wa mwaka.Nyingine ni timu bora ya taifa ya wanawake, mwanasoka bora wa kike wa mwaka, chipukizi bora, mwamuzi bora, gwiji bora na mchezaji wa jumla.Wachezaji mbalimbali ambao waliwahi kushinda tuzo hizo ni Samuel Eto’o wa Cameroon mwaka 2005 na 2010, Didier Drogba wa Ivory Coast mwaka 2006 na 2009, Frederic Kanoute wa Mali mwaka 2007, Emmanuel Adebayor wa Togo 2008, Yaya Toure wa Ivory Coast mwaka 2011, 2012 na 2013, anapewa nafasi kubwa pia mwaka huu.
5michezo
MSHAMBULIAJI wa Azam FC, Obrey Chirwa amekuwa mchezaji wa tatu msimu huu kufunga mabao matatu katika mchezo mmoja, hat-trick, baada ya kufanya hivyo katika ushindi wa mabao 5-0 dhidi ya Alliance mchezo uliopigwa jana Uwanja wa Nyamagana, Mwanza.Chirwa alifunga mabao hayo dakika ya tano, 24 na 68 baada ya kazi nzuri iliyofanywa na mshambuliaji Shaban Chilunda, ambaye alifunga mabao mengine mawili katika dakika ya 32 na 52 kufuatiwa kazi nzuri ya Chirwa na beki Nicolas Wadada.Wengine ambao tayari wameshafunga hat-trick msimu huu ni Ditram Nchimbi wa Polisi Tanzania dhidi ya Yanga na Daluwesh Saliboko wa Lipuli walipocheza dhidi ya Singida United. Baada ya ushindi huo, Azam imesogea mpaka nafasi ya nne ikiwa na pointi 19 sawa na Namungo, ambao wote walishinda mechi zao za mwisho.Katika mchezo huo wa jana, Azam ilitawala kwa kiasi kikubwa na kufanikiwa kutengeneza nafasi nyingi, ambazo hazikuzaa matunda kutokana na kukosa umakini kwa washambuliaji wa timu hiyo.Licha ya kutawala mchezo huo, Azam iliendelea kuwa na uchu wa mabao, baada ya kufanya mabadiliko ya kutoka Obrey Chirwa na kuingia Shaban Hamis na kutoka Mudathir Yahya na kuingia Donald Ngoma.Mabadiliko hayo yaliendelea kuifanya timu hiyo kuendelea kumiliki mpira na kukosa umakini wa eneo la mwisho baada ya kazi nzuri iliyokuwa ikifanywa na viungo wa timu hiyo akiwemo Salum Abubakar. Matokeo mengine ya michezo ya jana ni Mbao ilishinda 2-0 dhidi ya KMC, Mtibwa ikaifunga Kagera mabao 3-1, Biashara ikaifunga Lipuli 1-0, Mbeya City ikiwa Sokoine ikalala 2-1 dhidi ya Mwadui na JKT Tanzania ilishinda 2-1.Wakati huohuo, Yanga wanaondola leo inaifuata Alliance ya Mwanza ambayo itacheza nayo keshokutwa Ijumaa kwenye Uwanja wa CCM Kirumba.
5michezo
Na Mwandishi Wetu, Zanzibar UMOJA wa Vijana wa CCM (UVCCM), umesema wakati huu Chama Cha Mapinduzi (CCM), kikifikisha miaka 41 tangu  kuundwa kwake Februari 5, mwaka 1977, vijana wa chama hicho  wanapaswa kuheshimu,  kutambua na kuthamini mchango wa waasisi  waliopitisha wazo la kuunganisha vyama vya TANU na ASP. Umoja huo umeeleza uamuzi wa viongozi wakuu wa vyama hivyo, Hayati Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Nyerere na  Hayati Sheikh Aboud Jumbe Mwinyi na halmashauri kuu za vyama hivyo unahitaji kuenziwa, kutunzwa na kutambuliwa. Kaimu Katibu Mkuu  wa UVCCM, Shaka Hamdu Shaka aliyasema hayo jana, baada ya kumalizika kikao cha kamati maalumu ya Halmashauri Kuu ya Taifa  kilichofanyika Ofisi Kuu ya CCM, Kiswandui mjini Zanzibar. Alisema kitendo cha kuungana TANU na ASP, kimeleta mafaniko makubwa kisiasa kwa kukifanya chama kipya cha CCM kiwe na nguvu kubwa kisiasa, sera bora, oganaizehsheni ya uhakika, mikakati na kuimarika kwa nidhamu  ndani ya chama . Alisema kimsingi viongozi hao waliona mbali kisiasa kwa kutumia ‘darubini’ kali ya kisiasa na kubaini ikiwa vyama hivyo vitaungana maadui wa ndani na nje watapata pigo. “Tumefika hapa tulipo, chama chetu kikifikisha miaka 41 kwa kweli ni jambo la kujivunia. Wazee wetu walichemsha bongo na kuona mbali zaidi. CCM imepata uimara licha  ya kupigajia maslahi ya wakulima na wafanyakazi,” alisema Shaka. Alisema chama hicho kimepata mafanikio makubwa kwa kusimamia sera za msingi katika malengo ya kuendeleza amani, kudumisha umoja wa kitaifa, kuleta usawa, kutetea haki za wanyonge na kupigania maslahi ya watu. “Wananchi wamelitumia soko la uwapo wa Muungano wa Tanganyika na Zanzibar chini ya Jamhuri ya muungano wa Tanzania kujijenga kiuchumi. Ustawi wa jamii umekuwa  kutokana na utulivu, usalama wa nchi, ulinzi wa maisha  ya watu  na mali zao. Hakuna ukorofi na utapitapi kwakuwa kinatawala chama makini chenye misingi,” alisisitiza .
3kitaifa
Baada ya kuachiwa huru, Mbasha alitoka nje ya chumba cha mahakama hiyo iliyoko Mtaa wa Lumumba, Kariakoo, Dar es Salaam, na kupiga magoti na kulia huku amenyanyua mikono juu ishara ya kumshukuru Mungu.Katika kesi hiyo, Mbasha alikabiliwa na mashitaka mawili ya ubakaji ambapo ilidaiwa alitenda makosa hayo maeneo ya Tabata Kimanga, jijini Dar es Salaam. Katika mashitaka ya kwanza ilidaiwa Mei 23, mwaka jana maeneo hayo, Wilaya ya Ilala, kinyume cha sheria za nchi, alimbaka msichana huyo.Pia ilidaiwa kuwa Mei 25, mwaka jana, Tabata Kimanga nyumbani kwa mshitakiwa, alimbaka tena mlalamikaji. Mbasha alikana mashitaka hayo na alikuwa nje kwa dhamana baada ya kulala siku moja mahabusu ya Keko.Akisoma hukumu hiyo jana kuanzia saa 4:45 hadi saa 5:15 asubuhi, Hakimu Mkazi Flora Mujaya alisema kwamba mahakama hiyo ilisikiliza mashahidi sita wa upande wa mashitaka, akiwemo mwathirika wa tukio hilo ambaye ni shemeji wa Mbasha mwenye umri wa miaka 17, pamoja na mke wa mwimbaji huyo, Flora.Hukumu hiyo ambayo ilisikilizwa katika chumba cha faragha, Hakimu Mujaya alisema shahidi wa kwanza katika kesi hiyo ambaye ni shemeji wa Mbasha aliiambia mahakama kuwa Mei 23, mwaka jana alibakwa na Mbasha nyumbani kwake, Tabata Kimanga baada ya Flora kwenda kuchukua CD za nyimbo zake.Pia alisema shahidi huyo alidai alibakwa kwa mara ya pili katika gari aina ya Ipsum walipokuwa wanatoka kumtafuta Flora ambaye alikuwa haonekani nyumbani. Akipitia ushahidi wa Daktari wa Hospitali ya Amana, Migole Mtuka, hakimu huyo alisema, daktari huyo alidai ndiye alimfanyia vipimo msichana huyo na kuwa hakuona dalili zozote za kuingiliwa kimwili na Mbasha.Alisema daktari huyo alidai kuwa binti huyo alifika hospitalini hapo Mei 26, mwaka jana, kwa ajili ya kufanyiwa vipimo na baada ya kumtaka kwenda maabara, hakwenda bali alitoroka na kurejea Juni 3, mwaka jana, baada siku nane kupita.Hata hivyo, Hakimu Mjaya alisema kupitia mashahidi wote mahakama iliona upungufu katika ushahidi huo ambapo ilimuona mshitakiwa hana hatia. “Kupitia ushahidi huu, mahakama imebaki na maswali kama kweli umebaka au la.Kwa hivyo, upande wa mashitaka umeshindwa kuthibitisha mashitaka haya bila ya kuacha shaka na mahakama inakuachia huru,’’ alisema Hakimu Mujaya. Mbasha alifika mahakamani akiongozana na mdogo wake wa kiume pamoja na Wakili wake, Mathew Kakamba.Akizungumza na waandishi wa habari nje ya mahakama hiyo, Mbasha alisema Mungu ni mwema huku akifuta machozi na kuwaambia waandishi kuwa atawasiliana nao. Awali, Mbasha alifikishwa kwa mara ya kwanza mahakamani hapo Juni 17, mwaka jana akitokea Kituo cha Polisi Tabata, Dar es Salaam na kusomewa mashitaka mbele ya Hakimu Wilberforce Luhwago. Jalada la kesi hiyo lilihamishwa kwa Hakimu Mkazi Mujaya baada ya Hakimu Luhwago kuwa na majukumu mengine ya kazi.
5michezo
Licha ya kupoteza mchezo wa kirafiki usiku wa kuamkia leo kwa kufungwa 1-0 dhidi ya Mafarao wa Misri, nahodha wa timu ya soka ya Taifa, Taifa Stars, Mbwana Samatta amesema kuwa wamepata kipimo sahihi. Katika mechi hiyo iliyochezwa katika Dimba la Borg El Arab, ambayo muda mwingi Misri walionekana kutawala walifunga bao la ushindi dakika ya 65 kupitia kwa beki wa kushoto Ahmed Elmohamady. Elmohamady, ambaye anachezea timu iliyopanda Ligi Kuu ya England Aston Villa, alifunga kwa kichwa mbele ya kiungo wa Tanzania, Farid Mussa anayechezea timu ya DC Tenerife ya Hispania. Samatta alisema kuwa wameona makosa yao na anaamini benchi la ufundi chini ya kocha, Emmanuel Amunike watayarekebisha kabla ya mchezo wao wa pili wa kirafiki dhidi ya Zimbabwe utaochezwa Jumapili usiku kabla ya mashindano ya AFCON yaliyopangwa kuanza Juni 21. Pamoja kupoteza mchezo huo, ambao nyota wa Misri, Mohammed Salah hakucheza, Taifa Stars ilicheza vizuri na kutengeneza nafasi kadhaa za kufunga na kushindwa kuzitimua. “Hiki ni kipimo sahihi kwetu, mechi hii imeonyesha jinsi gani mashindano haya ni magumu, naamini kocha na wenzake watafanya marekebisho kabla ya mashindano,” alisema Samatta.
5michezo
WANAUME wametakiwa kutoa ushirikiano na kuhakikisha kwamba akinamama wanafuata uzazi wa mpango kwa ajili ya kulinda afya zao na za watoto na kupata muda wa kufanya shughuli za maendeleo.Hayo yalisemwa na Waziri wa Afya, Hamad Rashid Mohamed wakati akizungumza na wanawake wa mkoa wa kaskazini Kivunge ambapo wanawake wengi walisema wanaume ndiyo kikwazo katika kutekeleza uzazi wa mpango.Rashid alisema kwa mujibu wa takwimu zilizopo za uzazi wa mpango katika Bara la Afrika, Zanzibar ipo nyuma katika kutekeleza uzazi wa mpango wenye kutoa unafuu mkubwa kwa wanawake katika kuimarisha afya zao na kufanya shughuli za maendeleo.Alisema utafiti unaonesha kwamba wanawake waliojiunga na uzazi wa mpango, afya zao ni nzuri pamoja na watoto wao huku wakipata muda mrefu wa kushughulikia familia zao pamoja na baba watoto.Alibainisha kuwa njia zote zinazotumika na wanawake hao kwa ajili ya uzazi wa mpango upo salama zikiwa zimethibitishwa na taasisi za kimataifa kwa ajili ya usalama wa wanawake.“Njia zote zinazotumika za uzazi wa mpango zipo salama zikiwa zimethibitishwa na taasisi za afya ikiwemo za kimataifa kuona kwamba mwanamke anakuwa salama kiafya wakati anazitumia,” alisema.Katibu Mkuu, Wizara ya Afya Asha Abdalla Ali alisema njia zote zinazotumiwa za uzazi wa mpango zipo salama kwa afya za wanawake na kwamba zimethibitishwa na taasisi za kimataifa za afya likiwemo Shirika la Afya la Umoja wa Mataifa(WHO).Aliwataka akinamama kufuata masharti ya uzazi wa mpango ambao husaidia kulinda afya za watoto na kupambana na matatizo ya utapiamlo ambayo huleta madhara makubwa kwa ukuaji wa watoto.“Tunalo tatizo la utapiamlo kwa watoto wetu ambalo kwa kiasi kikubwa linachangiwa na kushindwa kufuata masharti ya uzazi wa mpango na kuzaa mtoto mwengine bila ya kufikisha muda wa kumuachisha ziwa,” alisema.Zanzibar inatajwa kuwa na kiwango cha asilimia 32 cha akinamama kutumia uzazi wa mpango ambacho ni kidogo huku juhudi za makusudi zinahitajika katika kutoa elimu zaidi vijijni. Mkazi wa Mkwajuni Mkoa wa Kaskazini Unguja, Asia Iddi alisema wapo tayari kufuata uzazi wa mpango lakini tatizo kubwa lipo kwa waume zao ambao ndio wenye ruhusa kwa mujibu wa Sheria za Ndoa.
3kitaifa
Na Malima Lubasha-Musoma MAHAKAMA Kuu Kanda ya Musoma, imewahukumu kunyongwa hadi kufa watu watatu kwa kosa la kumuua Tabu Makanya (58) kwa kumchinja na kutenganisha kichwa na kiwiliwili. Waliohukumiwa kunyongwa hadi kufa ni Musiba Maregeba, Abeid Casimil na Ndaro Sumuni wote wakazi Kijiji cha Kwibara Kata ya Mugango Wilaya ya Musoma vijijini mkoani Mara, huku Wandwi Mugulu diwani wa Kata ya Mugango, akiachiwa huru. Hukumu hiyo imetolewa na Jaji Girson Mdeme wa hiyo baada ya kuridhika na ushahidi uliotolewa mahakamani na upande wa Jamuhuri.  Jaji Mdeme, alisema ametoa adhabu hiyo ya kunyongwa hadi kufa kwa washtakiwa baada ya kuridhika na ushahidi uliotolewa na mashahidi saba pamoja na vielelezo vilivyotolewa mahakamani na upande wa mashtaka.  Awali washtakiwa hao walihukumiwa kunyongwa hadi kufa na Mahakama Kuu Kanda ya Mwanza katika kesi namba 189/2013 ambayo hukumu yake ilitolewa Julai 14,2015. Jaji Mdeme alisema, wakati washtakiwa wakisubiri kunyongwa baada ya hukumu iliyotolewa na Mahakama Kuu Kanda ya Mwanza, walikata rufaa ambayo ilisikilizwa na na Mahakama Kuu Kanda ya Musoma  Agosti 16. Washtakiwa hao walikuwa wakituhumiwa kumuua Tabu Makanya (58) mkazi wa Kijiji cha Kwibara Kata Mugango, ambapo Februali 21 mwaka 2013 majira ya saa 5.00 usiku walivamia nyumba ya mwanamke huyo kwa kubomoa mlango kwa jiwe kubwa marufu fatuma. Ilidaiwa wakiwa na mapanga na tochi, baada ya kuingia ndani walitoa onyo kwa watoto wa Tabu na kuwata kukaa kimya bila kupiga kelele. Baada ya kuwatisha watoto, walimvamia mwanamke huyo kisha kumchinja na kutenganisha kichwa na kiwiliwili na kukiweka ndani ya mfuko wa sandarusi na kuondoka nacho.  Ilidaiwa wakati watuhumiwa hao wakiwa katika harakati za kutoka eneo la tukio, wananchi walifanikiwa kumkamata mtuhuniwa mmoja akiwa na kichwa hicho. Kuhusu diwani aliyekuwa amejumuishwa kwenye kesi hiyo, inadaiwa alikamata baada ya uchunguzi wa awali kuonesha kwamba yeye ndiye aliwatuma watu hao kumtafutia kichwa cha binadamu kwa makubaliano ya kuwapatia fedha.  Ilidaiwa kuwa, diwani huyo alitaka kichwa hicho ili kukitumia kishirikina kwenye masuala ya uvuvi wa samaki lakini baada ya jalada lake kupelekwa kwa Mwanasheria wa Serikali, aliondolewa kwenye kesi hiyo.
3kitaifa
NA ZAINAB IDDY, WAWAKILISHI wa Tanzania katika michuano ya kimataifa, Yanga, kesho watakuwa Tokoradi nchini Ghana kucheza dhidi ya Medeama. Mchezo huo wa hatua ya makundi wa Kombe la Shirikisho Afrika ni  wamarudiano baina ya timu hizo, ambapo awali zilitoka sare ya bao 1-1 katika Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam wiki mbili zilizopita. Timu hizo za Kundi A, kila mmoja inahitaji matokeo ili aweze kujiweka kwenye nafasi nzuri ya kutinga hatua inayofuata, licha ya kupitwa na zaidi ya pointi tatu na wapinzani wao waliopo juu yao. Yanga wao katika michezo mitatu waliocheza wamejinyakulia pointi moja huku wakishika mkia kwenye msimamo wa kundi lao wakati Medeama wakiwa na pointi mbili mbele ya Wanajangwani. Kundi hilo linaongozwa na TP Mazembe ya Congo wenye pointi saba wakifuatiwa na Mo Bejaia ya Algeria wenye pointi tano kibindoni. Wanajangwani walianza kutupa karata yao katika hatua ya makundi kwa mechi dhidi ya Mo Bejaia ugenini na kufungwa 1-0, kisha wakapokea kipigo hicho tena kutoka kwa Mazembe wakiwa nyumbani kabla ya kupata sare mbele ya wageni wao Medeama. Kwa hesabu za haraka haraka unaweza kujifariji kuwa  Yanga itatinga  hatua ya nusu fainali, kwani mpira unadunda ndani ya uwanja dakika 90 na soka lina maajabu yake. Kulingana na nafasi waliyopo Yanga katika hatua hiyo ya makundi, zinahitajika rehema za Mungu ili waweze kusonga mbele, kwani ili watinge hatua ya nusu fainali wanahitaji kushinda michezo yake yote iliyobaki. Kama uliuangalia mchezo wao dhidi ya Mazembe na ule wa Medeama, ni wazi utakubali kuwa Wanajangwani hao wana wakati mgumu katika michezo yao ya marudiano hususani mbele ya timu hizo wakiwa ugenini. Katika mchezo wa Medeama, iwapo kama Waghana hao wangetulia ni wazi wangeondoka katika uwanja wa taifa si chini ya mabao matatu, kwani kipindi cha pili walikosa mabao mengi ya wazi lakini papara za wachezaji wake walipokuwa eneo la hatari ndio ilikuwa tatizo kwa Wanajangwani. Hali kama hiyo ilijitokeza pia kwa Mazembe, Yanga waliolala mbele kwa bao 1-0, hivyo ugumu unaonekana kwa Wanajangwani kutinga hatua ya nusu fainali. Inakumbukwa kuwa kila timu imebakiwa na mechi tatu mkononi kama Yanga watafanikiwa kushinda yote watakuwa wameweza kutinga nusu fainali. Yanga wanahitajika kuanza kuzisaka pointi 9 kwa Medeama kisha TP Mazembe na kumaliza nyumbani mbele ya Mo Bejaia  ili kutimiza jumla ya pointi 10. Iwapo ikishinda michezo hiyo itakuwa nyuma ya Mazembe watakaokuwa na pointi 13 kama watashinda mechi mbili, huku Bejaia ikiwa na pointi sita na Medeama tatu. Matokeo ambayo yatawawezesha kutinga hatua ya nusu fainali na hatimaye kutwaa ubingwa kwa mara ya kwanza na kuwashangaza wengi kama ilivyokuwa kwa Ureno ilivyofanya Euro. Licha ya hesabu Yanga inajifariji lakini benchi la ufundi linakazi kubwa kuhakikisha wanarekebisha makosa yaliyojitokeza kwenye michezo iliyopita. Yanga inahitajika kufanya marekebisho katika safu ya ushambuliaji iliyoonekana kupoteza nafasi ya kupata mabao ya wazi, mabeki  na safu ya ulinzi ambayo mechi ya Medeama Wanajangwani watamkosa Vicent Bossou anayetumikia adhabu ya kadi mbili za njano lakini kukiwa na nafasi kubwa nahodha Nadir Haroub ‘Cannavaro’ akaingia kuziba nafasi hiyo baada ya kuwa nje kwa muda mrefu kutokana na kukosa namba katika kikosi cha kocha Hans van de Pliujm. Mbali na hao, Bossou, Wanajangwani pia itawakosa Godfrey Mwashiuya na Deusi Kaseke ambao ni majeruhi na wanahitajika kuwa nje kwa kipindi kirefu. Ili kufikia malengo, wachezaji wanahitajika kujua na umuhimu wa kushinda mchezo huo na kutoruhusu wachezaji kutawaliwa na presha katika mioyo yao. Inawapasa kufahamu kuwa Medeama si timu ya kubeza ikiwa nyumbani, ukizingatia tayari wanawafahamu wachezaji gani hatari kwa Yanga  jambo ambalo wasipokuwa makini wanaweza kujikuta wakitawaliwa katika dakika zote za mchezo. Yote kwa yote dua na kumwachia Mungu ndiko kunahitajika kulingana na timu anazokwenda kucheza nazo ambazo mechi za kwanza zimewanyima pointi, lakini pia kazi inahitajika ili kufika mahali pazuri timu ya Yanga. Endapo Yanga itashindwa kupenya katika mashindano hayo ya pili kwa ukubwa Barani Afrika, itakuwa ni mara ya pili kwani mwaka 1998 iliishia hatua hiyo katika mashindano ya Ligi ya Mabingwa Afrika.
5michezo
Uchukuzi SC ambayo ipo chini ya benchi la ufundi mahiri linaloongozwa na Kenneth Mwaisabula `Mzazi’, waliwapeleka puta wapinzani wao na kuandika bao la kwanza lililofungwa kwa kichwa na Kado Nyoni, baada ya kuwahi mpira wa kona ya Omar Said ‘Chidi’ dakika ya 34.Hata hivyo, Ukaguzi walisawazisha dakika ya 50 mfungaji akiwa Ben Chezue aliyepiga mpira wa adhabu ndogo ulioenda moja kwa moja golini.Chezue aliingia dakika 49 kuchukua nafasi ya Deo Masanja aliyeumia. Uchukuzi SC iliongeza bao dakika ya 72 lililofungwa Issac Ibrahim aliyeachia shuti kali lililomshinda kipa wa Ukaguzi, Shomari Dumba.Nahodha wa Uchukuzi SC, Francis Charles alipigilia msumari wa mwisho kwa kufunga bao la tatu dakika ya 90 kwa njia ya penalti baada ya Bilal Mleli kushika mpira katika eneo la hatari.Akizungumza baada ya mechi, kocha Mwaisabula alisema Ukaguzi ni moja ya timu ngumu, lakini aliwapongeza wachezaji wake kwa kucheza vizuri na kutoka na ushindi mnono, ambao umesaidia kusafisha njia.Naye Mwenyekiti wa Uchukuzi SC, Mohamed Ally alisema wamekuja Dodoma kuchukua ubingwa na ana uhakika wa timu yake kufanya vyema kutokana na nidhamu ya mazoezi wanayofanya kila siku.Katika mchezo wa netiboli, timu ya Tamisemi iliifunga Tanesco kwa mabao 34-16, mabao ya Tamisemi yakifungwa na Imelda Hango na Flora Odilo huku yale ya Tanesco yakifungwa na Cartas Manamba na Asha Kitandala.
5michezo
UNAWEZA kutamani kila kitu utakachokiona katika mwili wa Ronaldo de Assis Moreira na ana majina mengi huyu binadamu, lakini maarufu anajulikana kwa jina la Ronaldinho Gaucho. Huyo ni fundi wa mpira ambaye hajadumu sana kwenye ulimwengu wa soka, ila jina lake litaendelea kudumu hadi mwisho wa maisha yake. Unaweza kuwa mpinzani wake na kumshutumu. Lakini mwisho wa siku utabaki kuwa shabiki wake. Na utaguswa na kutamani kumbukumbu zake. Ronaldinho, ambaye amemaliza soka lake akiwa Atletico Mineiro, aliumia kuona anamaliza soka lake huku akishindwa kutwaa taji la Kombe la Dunia la klabu, baada ya kufungwa na Raja Casablanca. Nguli huyo mwenye umri wa miaka 37, alishindwa kuisaidia timu yake kabla ya kuamua kustaafu kucheza soka la kulipwa. Alistaafu akiwa na maumivu mengi, licha ya tabasamu lake mororo mbele ya kadamnasi. Unaweza kumuona Zinedine Zidane akiwa kwenye ubora wake, Thierry Henry, Didier Drogba, Raúl González Blanco,  Daniel Rodríguez ‘Toti’, Miroslav Klose na wengine, lakini bado utakoshwa zaidi na Gaucho. Zama hizi zinatawaliwa na mshambuliaji wa Real Madrid, Cristiano Ronaldo ‘CR7’ pamoja na Lionel Messi wa Barcelona, wanafanya madoido mengi sana hawa watu, lakini bado hawajafanikiwa kuifuta picha ya Gaucho kwenye ubongo wa wapenda burudani ya mpira duniani. Gaucho acha aitwe Gaucho, anakupiga tobo huku anacheka, anakuvisha kanzu huku anacheka.Timu ikipata ubingwa wa Dunia yeye anacheka, ikitolewa robo fainali bado anacheka. Haya mabao tunayobishana siku hizi, yeye alishayafunga kitambo, chenga ndo usiseme, mipira ya adhabu ndo baba lao. Messi, CR7, Franky Ribery wa Bayern Munich hata kama wakichukua tuzo ya mchezaji bora, Ballon d’Or mara 10 kila mtu, bado Gaucho atawafunika wote kwenye ubongo wa wapenda burudani. Ana mambo mengi huyu mtu ndani na nje ya uwanja, kwani kabla wakina Theo Walcott hawajaja na sura zao za mahaba, Gaucho alishawateka wanawake kitambo. Huyu jamaa katimia kila kona. Huyo ndio nyota wa zamani wa timu ya taifa ya Brazil na klabu za PSG, Barcelona na AC Milan. Licha ya kutocheza soka la kiushindani tangu mwaka 2015, amekuwa akicheza michezo ya mabonanza. Kaka na wakala wa mchezaji huyo, Roberto Assis, amethibitisha kuwa umefika mwisho kwa fundi huyo wa Brazil kucheza soka. Ronaldinho alianzia soka yake katika klabu ya Gremio ya nchini kwao, kabla ya kujiunga na Paris St-Germain mwaka 2001 na baadaye kujiunga na Barcelona alikong’ara sana. Katika msimu wa 2010 -2011 alijiunga na AC Milan ya Italia, kabla ya kurudi kwao na kujiunga na Flamengo mwaka 2011. Kisha alichezea klabu ya Atletico Mineiro, na Queretaro ya nchini Mexico, na kurudi tena kwao Brazil katika klabu ya Fluminense. Kocha wa Manchester City, Pep Guardiola, ambaye alimuuza nyota huyo AC Milan, anasema kwamba Gaucho akiwa Barcelona hakukuwa na mchezaji yeyote wa kumfananisha naye kabla ya kutokea Messi. Ronaldinho aliisaidia Barcelona kuwa katika msingi wake ambao unaonekana sasa kama ambavyo anasema Guardiola, ambaye alimuuza nyota huyo ili kuandaa utawala mpya wa Messi ndani ya klabu hiyo. Gaucho ameshinda taji la La Liga mfululizo, Ligi ya Mabingwa Ulaya na Ballon d’Or wakati wa utukufu wake kutoka mwaka 2003 hadi 2008. Hata alipoondoka Barcelona ilimchukua muda Guardiola kutengeneza upya hitilafu iliyotokana na misingi aliyoacha Gaucho. “Wakati Joan Laporta alipokuwa rais wa Barcelona alisababisha athari kubwa na alipomsaini Ronaldinho ulikuwa mvuto mkubwa kwa Barcelona. “Ilisaidia kurejesha mustakabali wa klabu baada ya kipindi kirefu kupotea. Laporta akiwa rais na Ronaldinho ndani ya uwanja kwa pamoja walisaidia kurudisha heshima ya klabu kwa kipindi hicho. Gaucho alikuwa na mwaka mzuri alipoanza kucheza Barcelona, alishinda taji la ligi na Ligi ya Mabingwa Ulaya,” anasema Guardiola. Guardiola anasema: “Alikuwa ni mchezaji wa daraja la juu hadi Messi alivyofika, lakini sikuwahi kumwona mchezaji wa aina yake kabla. “Namtakia safari njema katika maisha yake, ana sifa nyingi si tu Barcelona, bali katika ulimwengu wa soka.” Ronaldinho ametokea kwenye familia ya watoto watatu, wa kike akiwa mmoja, lakini Ronaldinho alikuwa wa mwisho kuzaliwa katika familia ya mzee Joao de Assis Moreira, ambaye alikuwa anafanya kazi kwenye meli. Alizaliwa Machi 21, 1980. Maisha ya familia hiyo kwenye mji wa Porto Alegre huko nchini Brazil yalikuwa ya kawaida sana, kwa kuwa baba yao alikuwa anasumbuliwa na tatizo la moyo, lakini maisha yao yalianza kubadilika baada ya kaka wa mchezaji huyo, Roberto de Assis, kusajiliwa na klabu ya Gremia. Ronaldinho alianza kupenda mpira huku akiwa na umri wa miaka nane, alipata nafasi ya kucheza timu za mtaani na alionesha kiwango cha hali ya juu, alipata sifa nyingi kwa kuwa alionekana mchezaji mfupi na mdogo kwenye michuano ya mtaani, lakini alikuwa na uwezo wa pekee. Alianza kutambulika akiwa na umri wa miaka 13, baada ya vyombo vya habari kumuandika na kumuita jina la Ronaldinho, kutokana na kupachika mabao 23 peke yake kwenye mchezo mmoja wa ligi za mtaani, huku timu yake ikishinda mabao 23-0. Kutokana na kiwango hicho, Ronaldinho akachukuliwa na timu ya vijana ya Gremio, ambayo kaka yake alikuwa anacheza ya wakubwa, hivyo mwaka 1998 alipandishwa timu kubwa na kuonesha uwezo wake hadi 2001 alipojiunga na PSG. Dunia ilianza kumtambua vizuri mchezaji huyo mwaka 2003, alipojiunga na klabu ya Barcelona, hadi pale alipoondoka mwaka 2008 na kujiunga na klabu ya AC Milan. Dunia ilitamani kumuona mchezaji huyo zaidi ya miaka 10 akiwa na kiwango ambacho alikionesha katika klabu ya Barcelona, lakini kitu kinachopendwa zaidi na watu wengi hakiwezi kudumu sana, ndicho kilichotokea kwa Ronaldinho. Mchezaji huyo aliwahi kushangaza dunia baada ya kupigiwa makofi na mashabiki wa Real Madrid kwenye Uwanja wa Santiago Bernabeu, huku akiwa na klabu yake ya Barcelona, hiyo ni kutokana na na kukubalika na mashabiki duniani.
5michezo
Mwandishi Wetu-Dar es salaam RIPOTI mpya iliyotolewa na Jarida maarufu linalofuatilia watu wenye ukwasi mkubwa duniani la Forbes, imeonyesha kuwa ukwasi wa mfanyabiashara maarufu nchini, Mohammed Dewji maarufu kama Mo umeporomoka kwa Dola za Marekani milioni 300 katika kipindi cha mwaka mmoja. Kwa mujibu wa ripoti hiyo ya mwaka 2020, Mo ambaye mwaka 2019 utajiri wake ulikuwa unakadiriwa kufikia Dola za Marekani bilioni 1.9 hivi sasa anamiliki dola bilioni 1.6. Licha ya ukwasi wake kuporomoka, kijana huyo anayetambulika kama bilionea mdogo barani Afrika, hata hivyo amepanda kutoka nafasi ya 17 aliyokuwa akiishikilia mwaka 2019 hadi kufikia nafasi ya 16 mwaka huu. Wakati Mo akiporomoka kwa Dola milioni 300, tajiri namba moja barani Afrika, Aliko Dangote yeye utajiri wake umeonekana kupanda mara dufu.  Wakati ripoti ya Forbes ya mwaka 2019 ikimtaja Dangote kuwa na ukwasi wa Dola bilioni 4.3 ripoti ya mwaka huu imeonyesha amepanda hadi kufikia Dola bilioni10.1 akiendelea kushika nafasi hiyo hiyo ya kwanza. Utajiri wa Dangote ambaye ni raia wa Nigeria na aliyewekeza pia hapa nchini kupitia kwanda cha simenti mbali  na kutokana na bidhaa hiyo pia unatokana na uwekezaji katika sukari na unga. Nafasi ya pili katika orodha hiyo ya matajiri wa Afrika imeshikiliwa na bilionea Nassef Sawiris wa Misri ambaye ameonekana kupanda kutoka Dola bilioni 7.5 mwaka jana hadi kufikia dola bilioni 8 mwaka huu. Nafasi ya tatu imeshikwa na watu wawili Mike Adenuga na Nicky Oppenheimer ambao wote wana miliki dola bilioni 7.7. Bilionea Johann Rupert ameshika nafasi ya tano ($ bilioni 6.5), Issad Rebrab nafasi ya sita ($ bilioni 4.4), Mohamed Mansour nafasi ya saba ($ bilioni3.3), Abdulsamad Rabiu nafasi ya nane ($ bilioni 3.1), Naguib Sawiris nafasi ya tisa ($ bilioni 3).  Kwa upande wa wanawake walioingia katika orodha ya matajiri 20 barani Afrika, ni pamoja na binti wa Rais wa zamani wa Angola, Jose Dos Santos, Isabel ambaye ameshika nafasi ya 13 akiwa na ukwasi wa dola bilioni 2.2 na Folorunsho Alakija kutoka Nigeria ambaye ameshika nafasi ya 20 akiwa na dola bilioni moja.  NDOTO ZA MO Pamoja na ripoti ya jarida hilo kuonyesha ukwasi wa Mo umeporomoka na wakati huo huo akipanda daraja, mfanyabiashara huyo mwaka jana mwezi Oktoba alipita katika wakati mgumu baada ya kutekwa na watu wasiojulikana  na kushikiliwa kwa takribani siku tisa na hata kutishia maisha na biashara zake kabla ya kuachiwa. Pamoja na kupita katika hali hiyo bado amekuwa akitekeleza mipango ya kutanua biashara zake. Mipango hiyo ni pamoja na kuongeza viwanda katika nchi mbalimbali hususani barani Afrika.  Pia amekuwa na mazungumzo ya kina kuhusu kutanua biashara na viongozi kutoka nchi za Jamuhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC), Afrika Kusini, Zambia, Uganda, Madagascar, Comoro.   Katika mahojiano yake ya hivi karibuni Mo aliahidi kuwekeza Shilingi za Tanzania bilioni 500 hapa nchini na kutengeneza ajira za watu mbalimbali 100,000.  Mo ambaye ni mpenzi wa mpira wa miguu akiwa amewekeza katika klabu ya kubwa ya Simba Sports Club, ameahidi pia kuwekeza mamilioni ya shilingi kwenye maendeleo ya mchezo huo akishirikiana na ubalozi wa Sweden nchini.
3kitaifa
NA ADAM MKWEPU, DAR ES SALAAM KLABU ya soka ya Yanga imesema haiwezi kulipa kwa Shirikisho la Soka Afrika (CAF) asilimia tano ya mapato yaliyotokana na mchezo wa juzi wa Kombe la Shirikisho Afrika dhidi ya TP Mazembe ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC), kwa madai kuwa hawakuingiza mapato yoyote. Yanga iliondoa kiingilio katika mchezo huo wa pili wa Kundi A katika michuano hiyo uliochezwa katika Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam ili kutoa fursa kwa mashabiki wengi wajitokeze kuishangilia timu hiyo. Katika mchezo huo ambao Yanga ilipata kipigo cha bao 1-0 dhidi ya TP Mazembe, mashabiki walianza kuingia uwanjani mapema tangu saa 8:40 asubuhi ambapo mageti yalifungwa saa 11:50 baada ya uwanja kujaa. Akizungumza Dar es Salaam jana, Mkuu wa Idara ya Habari na Mawasiliano wa Yanga, Jerry Muro, alisema klabu hiyo ipo tayari kulipa asilimia 15 ya gharama za uwanja lakini si kulipa asilimia tano ya CAF kwa sababu hawakupata mapato yoyote. “Mashabiki walioingia uwanjani hawakulipa kiingilio hivyo hatutaweza kuilipa CAF kwa sababu hakuna fedha tulizopata kutokana na mchezo wa jana (juzi), katika makubaliano ya awali hatukukubaliana kuilipa CAF bali tulisema tutalipa gharama za mchezo ‘direct cost’ ikiwamo uwanja,” alisema Muro. Kwa upande wake, Katibu Mkuu wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Selestine Mwesigwa, alisema kikao cha awali kilichofanyika jijini Cairo, Misri kabla ya mchezo huo, Yanga ilikubali kulipa gharama za mashabiki wake pamoja na gharama za uwanja asilimia 15, mchezo 10%, CAF 5%, TFF 5% na Kodi ya Ongezeko la Thamani (VAT) 18%. “Kama Yanga iliamua kuingiza mashabiki wake bure uwanjani kikao hakitambui suala hilo kwa kuwa halikujadiliwa bali walikubali kuwalipia mashabiki wao bila kuathiri gharama watakazodaiwa kwenye mchezo,” alisema. CAF iliagiza kwamba mashabiki wanaotakiwa kuingia uwanjani wasizidi 40,000 ili kuepusha msongamano unaoweza kusababisha vurugu zisizo za msingi, hivyo inahesabika kuwa Yanga ililipia idadi ya mashabiki waliotajwa na shirikisho hilo linalosimamia michuano wanayoshiriki. Aidha, Mwesigwa alisema klabu ya Yanga pia itahusika kulipa gharama za uharibifu uliofanyika  uwanjani ambazo zipo nje ya asilimia 15 wanayotakiwa kulipa kwa ajili ya uwanja.
5michezo
TAASISI ya Utafiti wa Kilimo Tanzania (TARI), imechavusha mikungu 1290 ya michikichi ambayo inatarajiwa kutoa mbegu takribani milioni mbili lengo likiwa ni kupunguza uagizaji wa mafuta nje ya nchi na hatimaye kuisha kabisa.Kaimu Mkurugenzi wa Kituo cha Utafiti wa Michikichi Kihinga (TARI Kihinga), kilichopo mkoani Kigoma, Dk Filson Kagimbo alisema hayo alipokuwa akizungumza na Habari Leo katika maadhimisho ya sikukuu ya wakulima nane nane yanayofanyika mkoani Simiyu.Dk. Kagimbo alisema mbegu hiyo iliyochavushwa itatosha kupanda eneo la eka 38,000 ambapo kwa sasa mbegu 63,000 zimeshavunwa zenye uwezo wa kupanda eka 1260.Alisema zao hilo la michikichi ambalo ni maarufu kwa mafuta ya kula nay ale yanayotumika viwandani, ndio zao pekee linalotoa mafuta mengi kwa eneo la ardhi ambalo limelimwa.“Mfano ukiwa na mazao yote yanayotoa mafuta kila zao likawekwa kwenye eneo la eka moja, ni zao la mchikichi litatoa mafuta mengi kuliko mazao yote,” alisema.Alisema nchini Tanzania mafuta yanayotumika ya kula asilimia 60 hadi 64 ni ya mawese na katika hayo mafuta ya mchikichi yanayoliwa asilimia 99.3 yote yanaagizwa kutoka nchi za nje.“Maana yake ni kwamba mafuta ya mawese yanayozalishwa na kuliwa nchini ni asilimia 0.7,” alisema.Alisema nchini Tanzania uzalishaji wa zao la mchikichi upo chini ambao ni wastani wa tani 1.6 kwa hekta wakati nchi kama Malasia wanapata tani nane kwa hekta.Alitaja sababu kubwa ya uzalishaji mdogo kuwa ulimaji wa mbegu za kienyeji ambazo zinatoa mafuta kidogo kwani asilimia 90 ya michikichi yote inayolimwa nchini ni ya kienyeji, asilimia 10 ni ya kisasa aina ya Tenera.
3kitaifa
KOCHA Mkuu wa KMC, Jackson Mayanja (pichani) amesema kazi iliyoko mbele yao ya kuwakilisha nchi katika michuano ya Kombe la Shirikisho Afrika sio ndogo hivyo, wanajipanga kuhakikisha wanafanya vizuri.KMC itaanza kucheza mchezo wake wa kwanza ugenini Agosti 8, mwaka huu dhidi ya AS Kigali ya Rwanda na baadaye kurudiana Agosti 23, mwaka huu Dar es Salaam. Akizungumza na gazeti hili Mayanja alisema “tunahitaji maandalizi mazuri, uzuri ni kwamba tulikuwepo katika michuano ya Kagame, baadhi ya wachezaji wasiokuwa na uzoefu wa kimataifa, tunajipanga ili kuwa vizuri zaidi”.Alisema baadhi ya wachezaji wana uzoefu wa kimataifa na wengine hawana na kwamba wametumia michuano ya Kagame kujijenga na kujiweka vizuri zaidi. KMC imesajili wachezaji wengi msimu huu wa ndani na nje ya nchi kwa lengo la kuhakikisha inawakilisha kwa mara ya kwanza vizuri kwenye michuano hiyo baada ya kuonesha ushindani mzuri katika msimu wake wa kwanza wa ligi iliyopita. Mmoja wa nyota wake, Jean Mugiraneza aliyewahi kuichezea Azam FC, alisema kwa kile alichokiona katika timu yake mpya ya KMC anaamini watafanya vizuri.“Tutatumia mbinu zaidi tutakapokwenda ugenini. AS Kigali ni timu nzuri imebadilika sana, imebadilika kwasababu imefukuza wachezaji 17 na kusajili wengine,”alisema.Kiungo mchezaji wa zamani wa Yanga na Simba, Haruna Niyonzima kwa sasa anaitumikia timu hiyo ya Rwanda aliyojiunga nayo msimu huu baada ya kumaliza mkataba wake kwa wekundu wa Msimbazi.
3kitaifa
Mwandishi Wetu RAIS Dk. John Magufuli amemteua Gerald Kusaya kuwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Kilimo, kuchukua nafasi ya Mathew Mtigumwe, ambaye amepangiwa kazi nyingine katika Ofisi ya Waziri Mkuu. Ikumbukwe kuwa kabla ya kuteuliwa, Kusaya alikuwa mwenyekiti wa timu maalumu iliyoundwa na Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, kwa uchunguzi wa masuala mbalimbali katika tasnia ya zao la mkonge mkoani Tanga. Machi 1 mwaka huu, Kusaya aliwasilisha ripoti ya awali ya timu hiyo wakati Majaliwa alipoanza ziara mkoani Tanga, ambapo alisema wamebaini upotevu wa mabilioni ya shilingi uliosababishwa na uongozi wa Kampuni ya Katani Ltd. Kusaya alisema timu yake ilibaini ubadhirifu wa mabilioni ya fedha katika Kampuni ya Katani Ltd iliyopewa jukumu la kusimamia mashamba matano ya mkonge, ambayo iliingia katika madeni ambayo haiwezi kuyalipa. Alisema kutokana na ubadhirifu huo, uwezo wa Katani Ltd kulipa madeni ni mdogo kwa kuwa hadi Desemba 31 mwaka jana yalifikia zaidi ya Sh bilioni 70 wakati mali alizonazo zina thamani ya Sh bilioni 43. Kusaya alisema madeni hayo yanahusisha mikopo kutoka NSSF ambayo ni Sh bilioni 33.7 na makato ya kawaida ya NSSF yanayofikia Sh bilioni 1.5, kodi za TRA Sh bilioni 8.2 na madai ya wakulima Sh bilioni 31 na kwamba anaiomba Serikali muda zaidi ili wakamilishe ripoti hiyo na kuwashughulikia wahusika. Alisema hatua hizo ni pamoja na kutaifisha mali zilizochukuliwa na waliokuwa viongozi wa Katani Ltd kinyume cha utaratibu ikiwemo nyumba na mashamba na uuzaji wa hisa ambao haukufuata utaratibu. Mapendekezo mengine ni ya kurejeshwa serikalini kwa nyumba namba 176 eneo la Bombo ambayo ilimilikishwa kwa Mkurugenzi Mkuu wa Katani Ltd, Salum Shamte na nyumba 10 zilizoko ndani ya Jiji la Tanga katika maeneo ya Raskazone, Bombo, Nguvumali na Market Street ambazo zilidaiwa kununuliwa na watumishi hao kwa udanganyifu. Timu hiyo maalumu ya uchunguzi iliyokuwa na wajumbe 13, iliyohusisha maofisa kutoka ofisi mbalimbali za Serikali, iliundwa na Waziri Mkuu na ilifanya uchunguzi mkoani Tanga kuanzia Novemba 29, mwaka jana hadi Februari 7, mwaka huu.  Uchunguzi huo maalumu ulihusu masuala mbalimbali katika tasnia ya zao la mkonge mkoani Tanga ambayo ni pamoja na uzalishaji wa mkonge, bei ya zao la mkonge katika soko la ndani na nje ya nchi.
3kitaifa
Akizungumza kwenye mafunzo ya waandishi wa habari za michezo yaliyoandaliwa na Chama cha Waandishi wa Habari za Michezo Tanzania (TASWA) hivi karibuni, Nyambui alisema wanariadha wakongwe kama Filbert Bayi na baadhi ya wengine walikuwa wakihudumiwa kama wafalme na kufuatiliwa maendeleo yao.“Kwa mfano Bayi, alikuwa akifanya kazi Jeshini, walikuwa wakimjali kwani walimpa nyumba na alikuwa akipewa gari la kupelekwa mazoezini na kurudishwa, mimi mwenyewe mkuu wa mkoa kipindi hicho alikuwa akifuatilia mienendo yangu sasa na kuuliza naendeleaje, kwanini usifanye vizuri,” alisema.Alisema ukilinganisha na sasa ni tofauti kwani wanariadha wengi wanashindwa kufanya vizuri kutokana na wengi kutoka katika mazingira magumu tena yakiwa hayana msaada kwa viongozi wa eneo husika.Nyambui alitolea mfano kuwa kuna wengine huonekana kufanya vizuri katika mashindano ngazi ya mkoa lakini hawana vifaa vya michezo.“Nakumbuka kuna mwanariadha mmoja aliwahi kuja kwenye mashindano ya kitaifa alikuwa hana viatu, hivyo alikimbia akiwa hajavaa viatu na akafanya vizuri. Lakini alipokuja kupewa viatu alitoka malengelenge na kufanya vibaya, kwa sababu wanatoka kijijini hawakuandaliwa namna na kutumia viatu,” alisema.Alizungumzia pia, wanariadha hufanya vibaya kutokana na mazingira magumu anayoishi, kwani wanahitaji chakula kizuri na chenye nguvu, lakini wengi wana hali ngumu.
5michezo
MSHAMBULIAJI wa Yanga, Mkongo Heritier Makambo amesema ameamini timu hiyo ni kubwa kuliko wachezaji kutokana na kile alichokishuhudia juzi kwenye uwanja wa Jamhuri Morogoro.Makambo aliyejiunga na timu hiyo msimu huu akitokea Lupopo ya DR Congo alisema tukio alilolishuhudia uwepo wa mashabiki wengi wakijitokeza kumuaga nahodha wao Nadir Haroub ‘Canavaro’ hajawahi kuona. “Timu hii ya Yanga ni kubwa kuliko sisi wachezaji, nimeshuhudia kitu ambacho sijawahi kukiona, mashabiki wa klabu hii wamenishangaza kwani ni watulivu,” aliandika ujumbe huo kwenye ukurasa wake wa mtandao wa kijamii Instagram.Alisema anawashukuru wote waliojitokeza kwani walichangia kuwapa nguvu na moyo wa kupambana huku akimtakia kila la heri Canavaro katika majukumu mapya. “Nenda nahodha umefanya kile kilichostahili kufanywa na mchezaji mkubwa, najua ni msimu wangu wa kwanza lakini nilichokiona natarajia nitakipata,” alisema. Mchezaji huyo ndio mara yake ya kwanza kucheza kwenye mkusanyiko wa mashabiki wa klabu hiyo tena akiifungia bao 1- 0 katika mchezo wa kirafiki dhidi ya timu inayocheza Daraja la Kwanza ya Mawenzi.Mbali ya mchezo huo, pia aliifungia timu yake katika ushindi wa mabao 5-1 dhidi ya timu ya kituo cha Tanzanite cha Morogoro katika mchezo wa kirafiki ikiwa ni sehemu ya maandalizi yao kwa ajili ya msimu ujao wa ligi. Ujio wa mchezaji huyo aliyechukua nafasi ya Donald Ngoma huenda kukarejesha matumaini katika mbio za kuwania ubingwa wa Ligi Kuu msimu ujao. Katika hatua nyingine, Mkuu wa Idara ya Habari na Mawasiliano wa Yanga, Dismas Ten alisema sherehe za kumuaga Canavaro zitafanyika tena kwenye Uwanja wa Taifa mwishoni mwa wiki hii ambapo Yanga itacheza mchezo wa kimataifa dhidi ya USM Alger ya Algeria.
5michezo
Na ESTHER MBUSSI-DODOMA SPIKA wa Bunge, Job Ndugai ameitaka serikali kutoa tamko kuhusu wanafunzi waliokosa mikopo kutoka Bodi ya Mikopo kwa Elimu ya Juu (HELSB), kwa sababu ya kukosa fedha za kulipia ada ya usajili chuoni. Ndugai aliyasema hayo baada ya Mbunge wa Viti Maalumu, Martha Mlata (CCM) kuomba mwongozo wa Spika kuhusu wanafunzi hao akisema wanapofika vyuoni wanalipishwa ada ya usajili ili kupata mkopo huo. “Inashangaza wanafunzi waliodahiliwa wamekosa nafasi ilihali wana sifa lakini pia wengi waliopata nafasi hawajapata mkopo na wakati Rais alisema walio na sifa za kupata mkopo wasisumbuliwe lakini wanasumbuliwa ada ya usajili. “Ingawa idadi ya wanafunzi wanaopata mkopo imeongezeka lakini wanafunzi wanaopata mkopo ni wachache halafu bado wanapata taabu kuupata, naomba mwongozo wako kuhusu suala hili,” amesema Mlata. Akijibu, Spika Ndugai alisema jambo hilo ni muhimu likatolewa ufafanuzi kwa sababu si wanafunzi wa mwaka wa kwanza pekee wanaopata madhila hayo. “Naiomba serikali itoe tamko kesho (leo), haiwezekani mtoto afike chuoni alipie fedha ili apate haki yake ya mkopo. “Ndiyo maana wamezagaa tu mitaani maskini. Hawa ni watoto wa maskini, naomba kesho saa nne serikali itoe tamko au maelezo ya nini kinaendelea kuhusu watoto hawa,” alisema.
3kitaifa