text
stringlengths 1k
24.2k
| label
class label 6
classes |
---|---|
Pretoria, Afrika Kusini PICHA ya kutisha ya uhalifu wa mazingira, imetangazwa kuwa
mshindi katika tuzo za shindano la wapiga picha la mwaka huu. Picha hiyo, iliopigwa na mpiga picha wa Afrika Kusini,
Brent Stirton inaoyesha hali ya faru mweusi ndani ya Hifadhi Hluhluwe Imfolozi. Wawindaji haramu, walimuua mnyama huyo usiku kabla ya
kumtoa pembe zake. Stirton alipiga picha hiyo, ikiwa miongoni mwa uchunguzi
kuhusu biashara haramu ya bidhaa za faru. Mpiga picha huyo, alizuru zaidi ya maeneo 30 uliofanyika
uhalifu huo, wakati wa uchunguzi wake ambao aliutaja kuwa wa kuogofya. Stirton ambaye alipokea tuzo hiyo katika tamasha la chakula
cha jioni lililofanyika jumba la kumbukumbu mjini London , anaamini unyama huo aliofanyiwa faru ulitekelezwa na wakazi wa eneo hilo. Lengo kubwa la uwindaji huo,ni kuuza pembe mbili za faru
huyo kwa wafanyibiashara. Wafanyibiashara hao, baadaye huzipeleka pembe hizo hadi
Afrika Kusini kupitia Msumbiji hadi China ama Vietnam. Katika mataifa hayo,pembe za faru zina thamani ya juu
ikilinganishwa na dhahabu ama dawa ya kulevya ya Cocaine. Biashara hiyo, hupata msukumo wa imani sawa na kucha za
vidole vya mguuni, zinaweza kutibu ugonjwa wowote kutoka saratani hadi mawe ya
figo. Brent Stirton aliambia BBC : Kwa mimi kushinda tuzo hii,
kwa majaii kuweza kutambua kazi yangu ni wazi kwamba tunaishi katika muda
tofauti na kwamba hili ni suala nyeti. ”Suala la kuangamia kwa baadhi ya wanyama ni la kweli na
faru ni mojawapo ya aina ya wanyama wanaoendelea kuangamia kwa kiwango kikubwa
na ninashukuru kwamba majaji waliweza kutambua picha yangu kwa kuwa
inaliangazia swala hili kwa hatua nyengine”. Lewis Blackwell, mwenyekiti wa jopo la majaji hao wa WPY,
alisema picha ya faru ilikuwa na athari kubwa katika jopo lake. ”Watu wanaweza kusinywa ama kushtushwa, ukweli ni kwamba
picha hiyo inakuvutia na kukufanya kuhisi kana unataka kujifunza mengi.Unataka kujua habari
kuihusu. Na huwezi kuitoroka kwa sababu inakuangazia yale yanayoendelea duniani”. | 2kimataifa
|
Hoja hiyo ilitolewa juzi na wadau wa soka ambao wameendelea kujitokeza kununua bidhaa mbalimbali za michezo katika duka la vifaa vya michezo la Azam Fc lililofunguliwa mtaa wa Kariakoo na Mkunguni.Duka hilo lenye bidhaa mbalimbali za michezo vikiwamo viatu, fulana, bukta, mabegi, kofia, soksi na vinginevyo limekuwa kivutio kikubwa kwa mashabiki pamoja na wadau wa soka kwa ujumla.Mmoja kati ya mashabiki wa timu ya Azam Fc, Juma Saidi akizungumza na gazeti hili katika duka hilo alisema klabu hiyo imejisogeza zaidi na mashabiki wake kwa kuwafungulia duka, lakini aliwataka kufungua maduka mengine mikoani.Alisema kuwa ameguswa zaidi na uwepo wa jezi kwa ajili ya watoto na kusema kuwa hatua hiyo ni nzuri kwa kuwa inaanza kuwajenga watoto kuipenda timu tangu wakiwa wadogo.“Najua kinachowafanya watu wengi kuzipenda timu kubwa hizo mbili za Simba na Yanga ni kwa sababu tangu wakiwa wanakua wamekuwa wakizisikia zaidi na kwa sasa kama Azam ikitaka kuendelea kupata wateja ni vema wakaanza kuwekeza kama hivi kwa watoto tangu wakiwa wadogo,” alisema Saidi.Kwa upande wake Iren Mwikange alisema kuwa mikoani kuna mashabiki wengi wa timu hiyo na kuitaka klabu hiyo kuwa na mikakati ya kuwafikia kwa huduma bidhaa zenye nembo ya Azama Fc. | 5michezo
|
Na ZAINAB IDDY-DAR ES SALAAM
TIMU ya taifa ya vijana walio chini ya miaka 17, Serengeti Boys, leo inarusha karata yake muhimu dhidi ya Niger katika mchezo wa Kombe la Afrika kwa vijana nchini Gabon.
Mchezo huo utafanyika katika Uwanja wa Port Gentil mjini Port Gentil, ambapo kikosi hicho kikiwa kimevuna poibnti nne katika michezo yake miwili ya awali, ikianza kupata suluhu dhidi ya Mali Mei 15, mwaka huu kabla ya kuifunga Angola mabao 2-1.
Kocha Mkuu wa Serengeti Boys, Bakari Shime amesema kuwa mchezo huo ni muhimu kupata matokeo ili kujiweka katika nafasi ya kucheza hatua inayofuata.
“Tumejiandaa vema kuwania nafasi ya angalau kuingia nusu fainali,” alisema Shime.
Naye Nahodha wa timu hiyo, Dickson Job aliwatoa shaka Watanzania akisema vijana wote wako vema kwa ajili ya mchezo huo kwani mpira wa miguu kwao ni ajira kwa manufaa ya yao binafsi, familia na taifa ambalo limewatua Gabon kutafuta Kombe la Mataifa ya Afrika.
Serengeti Boys inahitaji sare ya aina yoyote ili iweze kuvuka huku Niger ambayo ina pointi moja ikiburuza mkia katika Kundi B. | 5michezo
|
Yanga inaanza kampeni hizo ikiaminika kuwa na kikosi bora chenye uwezo wa kutetea taji hilo.Yanga iliifunga Coastal Union mechi zote katika ligi ya msimu uliopita, ikiwemo ile ya pili iliyofanyika kwenye Uwanja wa Taifa ambapo ilifungwa mabao nane.Akizungumzia mechi hiyo jana kocha wa Yanga, Hans van Pluijm alisema ana matarajio makubwa na timu yake kuibuka na ushindi.“Nilikuwa na muda mrefu wa kuandaa kikosi changu, nadhani sasa ni wakati wa wachezaji wangu kufanyia kazi yale waliyofundishwa,” alisema.Kuhusu suala la wachezaji wake wa kigeni kuzuiwa na Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Katibu Mkuu wa Yanga Dk Jonas Tiboroha alisema jana kuwa wachezaji wao wote watacheza.Awali, kulikuwa na taarifa kwamba Yanga imeshindwa kulipa dola za Marekani 2,000 kwa kila mchezaji kati ya wachezaji wake saba wa kigeni hivyo TFF imewazuia.“Nawahakikishia wapenzi na mashabiki wa Yanga kwamba tumekamilisha taratibu zote za usajili kwa wachezaji wetu wa kigeni na hakuna atakayeshindwa kucheza labda kama kocha hatomtumia,” alisema.Wachezaji wa kigeni wa Yanga ni Haruna Niyonzima wa Rwanda, Mbuyu Twite kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, Vincent Bossou wa Togo, Andrey Coutinho wa Brazil, Thabani Kamusoko, Donald Ngoma wa Zimbabwe na Amisi Tambwe wa Burundi. | 5michezo
|
Na Mwandishi Wetu-DAR ES SALAAM
SHIRIKA la Umoja wa Mataifa la Mpango wa Chakula Dunini (WFP), limepokea mchango wa Euro milioni 9.5 kutoka Umoja wa Ulaya (EU) kwa lengo la kuunga mkono mradi wenye thamani ya Euro milioni 24.5 (takribani Sh bilioni 50) kusaidia na kukuza usalama wa chakula na lishe katika mikoa ya kanda ya kati.
Mradi huo umeandaliwa ili kuimarisha usalama wa chakula na lishe kwa watu wapatao 40,000 na wakati huohuo ukichangia katika kupunguza utapiamlo katika wilaya zinazolengwa za Bahi na Chamwino mkoani Dodoma, Ikungi na Singida Vijijini katika Mkoa wa Singida.
Mchango wa EU ulitangazwa jana Dar es Salaam katika hafla ya kusaini makubaliano katika Jengo la Umoja jijini Dar es Salaam uliofanywa na Katibu Mkuu Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dk. Mpoki Ulisubisya, Mwakilishi wa WFP Tanzania, Michael Dunford na Mkuu wa Ubalozi wa Umoja wa Ulaya nchini, Roeland Van De Geer.
“Licha ya kuimarika kwa viashiria vingi vya afya katika muongo uliopita, bado hakuna hatua kubwa katika kuimarisha hali ya lishe ya watoto na wanawake nchini Tanzania.
“Kuwapo viwango vya juu vya kudumaa, kukosa uzito wa kuridhisha na upungufu wa viinilishe nchini kunaashiria dharura ya kimyakimya. Utayari wa kisiasa katika safu ya viongozi wa juu katika kukabili lishe duni nchini Tanzania kwa mtazamo wa sekta nyingi kwa hakika ni mageuzi makubwa.
“Kupitia mradi huu, EU pamoja na WFP ziko katika nafasi nzuri ya kubaini na kuunga mkono uhusiano kati ya kilimo, afya, usalama wa chakula na lishe, ambao hapo kabla haukuwa umeelezwa kwa kina au kufuatiliwa kikamilifu,” alisema Van De Geer. | 3kitaifa
|
Na MWANDISHI WETU-DAR ES SALAAM WAZIRI Mkuu wa zamani, Edward Lowassa, amewakaribisha makada wote wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) waliokatwa katika uchaguzi kujiunga na Chadema. Wiki iliyopita Kamati Kuu ya CCM na baadaye Halmashauri Kuu, vilipitia majina 1,400 ya walioomba ridhaa ya kugombea nafasi ya Mwenyekiti wa Wilaya za CCM ambazo ni sawa na zile za kiserikali na kufanikiwa kuchuja hadi kufikia 161. Akitangaza maazimio ya Halmashauri Kuu ya chama hicho, Katibu wa Itikadi na Uenezi, Humphrey Polepole, alitaja wilaya tano, zikiwamo Siha, Moshi Mjini, Hai na Makete, kuwa hazikupata wagombea wenye sifa kutokana na kasoro nyingi za kimaadili na kikanuni zilizojitokeza. Kutokana na uamuzi huo, Polepole alisema wilaya hizo zitaanza upya mchakato wa uchaguzi katika ngazi hiyo. Katika taarifa yake kwa vyombo vya habari jana, Lowassa alisema: “Nimesoma na kusikia baadhi ya waliokuwa viongozi katika Chama Cha Mapinduzi wamekatwa ama kutetea nafasi zao au kugombea, kwa sababu mbalimbali. Na jina langu limekuwa likiendelea kutajwa tajwa humo. “Mimi nawaambia hawa Watanzania wenzetu waliokatwa huko CCM nawakaribisha huku Ukawa wafurahie demokrasia. “Huku niliko kuna maisha mazuri ya kisiasa, uhuru wa fikra na demokrasia halisi,” alisema Lowassa, ambaye pia ni mjumbe wa Kamati Kuu ya Chadema. Mbunge huyo wa zamani wa Monduli alisema Baba wa Taifa, Hayati Mwalimu Nyerere alisema ni wakati mwafaka kwa Tanzania kuwa na mfumo wa vyama vingi. | 3kitaifa
|
Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI), Profesa Mohammed Janabi amedai mfanyabiashara Yusuf Manji aliwahi kufanyiwa uchunguzi katika taasisi hiyo kuangalia kama vyuma vilivyopo katika moyo vimeziba ama la. Profesa Janabi medai hayo wakati akitoa ushahidi katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar es Salaam leo Agosti 30, mbele ya Hakimu Mkazi Mfawidhi, Cyprian Mkeha akiongozwa na mmoja wa mawakili wa Manji, Hajra Mungula ambapo anakuwa shahidi wa kwanza kumtetea Manji anayekabiliwa na mashtaka ya kutumia dawa za kulevya ikiwamo heroin. Profesa Janabi amedai Manji aliwahi kulazwa katika taasisi hiyo mara mbili tofauti, Februari na Julai mwaka huu ambapo alipofika Februari alitokea Polisi akiwa na matatizo ya moyo na alikuwa akisikia maumivu upande wa kushoto wa moyo hivyo alifanyiwa uchunguzi kuangalia kama vyuma vilivyopo katika moyo wake vimeziba ama la. “Alipofikishwa kwa matibabu alipewa dawa aina tatu tofauti za moyo na kabla ya hapo alikuwa na tatizo la mgongo na kukosa usingizi, kwa tatizo hilo alikuwa akipatiwa matibabu Hospitali ya Agha Khan,” amedai Profesa Janabi. Shahidi amedai mgonjwa wa moyo mwenye chuma katika moyo wake, kabla hajawekewa chuma hicho huelezwa vitu ambavyo hatakiwi kutumia ikiwemo kuvuta sigara na matumizi ya dawa za kulevya ikiwemo heroine kwani yana athari kubwa na hufanya mirija kuziba na kusababisha kufanyiwa upasuaji mkubwa. Wakili wa Serikali Mkuu, Timony Vitalis alipomuhoji shahidi huyo kama anajua athari za mgonjwa wa moyo kutumia dawa za kulevya, alijibu yeye ni daktari wa moyo na anazijua athari. Kesi hiyo itaendelea leo kwa mashahidi upande wa mshtakiwa kuendelea kutoa ushahidi. | 3kitaifa
|
LONDON, ENGLAND
LIGI Kuu nchini England iliendelea jana kwenye viwanja mbalimbali, huku mchezo ambao ulipigwa mapema ukiwa kati ya Middlesbrough, ambayo ilikubali kichapo cha mabao 3-1 dhidi ya Manchester United.
Mchezo huo, ambao ulipigwa Uwanja wa Riverside, wenyeji walijikuta wakiwa katika wakati mgumu wa kuzuia mashambulizi ya mara kwa mara kutoka kwa wapinzani wao.
Manchester United waliutawala mchezo katika dakika 45 za kipindi cha kwanza na waliweza kupata bao katika dakika ya 30, lililowekwa wavuni na Marouane Fellaini, baada ya krosi safi iliyopigwa na Ashley Young.
Wenyeji waliingia uwanjani wakitumia mfumo wa 4-3-3, wakati huo wapinzani wao, Manchester United wakitumia 3-4-3 ambapo walionekana kujaza viungo.
Hadi dakika 45 za kipindi cha kwanza zinamalizika United walikuwa wanaongoza bao moja, baada ya kipindi cha pili kuanza bado United walionekana kuutawala mchezo na kutafuta bao la pili.
Bao la pili lilipatikana dakika ya 62, ambalo liliwekwa wavuni na kiungo wao, Jesse Lingard, baada ya kupewa pasi ya mwisho kutoka kwa Juan Mata.
Baada ya Mata kutoa pasi ya mwisho katika bao la pili, kocha wa klabu hiyo, Jose Mourinho, alifanya mabadiliko ambapo alimtoa kiungo huyo na kumpa nafasi Marcos Rojo amalizie dakika 20, lakini kutoka kwake kulionekana kupunguza kasi ya Manchester United na kuwapa nafasi wapinzani wao kucheza eneo la katikati.
Zikiwa zimebakia dakika 13, Middlesbrough walifanikiwa kupata bao la kufutia machozi, lililowekwa wavuni na nyota wao, Rudy Gestede.
Mourinho aliendelea kufanya mabadiliko ambapo mfungaji wa bao la pili ambaye anacheza nafasi ya kiungo, Lingard alipumzishwa na nafasi yake ikachukuliwa na Anthony Martial kwa ajili ya kuongeza nguvu katika safu ya ushambuliaji, mchezaji huyo aliingia katika dakika ya 80.
Zikiwa zimebakia sekunde chache mchezo huo kumalizika, United waliongeza bao la tatu ambalo lilifungwa na Antonio Valencia na mara baada ya mchezo huo kuanza, hatimaye mwamuzi Jonathan Moss alimaliza mchezo. | 5michezo
|
NAIBU Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Atashasta Nditiye amesema serikali haitumii kigezo cha mvuto katika kuajiri watumishi wa Shirika la Ndege nchini (ATCL).Kauli hiyo imekuja siku moja baada ya Mbunge wa Kigoma Kusini (CCM), Husna Mwilima kutaka shirika hilo liajiri wahudumu wenye mvuto ili kufanya shirika hilo kuonekana.“Naomba nitoe ufafanuzi wa jambo ambalo lilisemwa bungeni jana (juzi) ni kuwa ajira za shirika la ndege haziangalii mvuto.”smesema Nditiye.Amesema serikali na shirika hilo vimeainisha sifa mbalimbali za kuajiri, ikiwa ni pamoja na kuwa Mtanzania mwenye umri kuanzia miaka 18 na kuendelea.“Pia awe anayefahamu lugha za Kingereza na Kiswahili kwa ufasaha na awe na cheti cha kuongoza ndege ama cha kufanya kazi ndani ya ndege. Sifa muhimu ni lazima awe na leseni ya kuruka ambayo inatolewa na Mamlaka ya Anga (TCAA),” alisema.Nditiye alitaja sifa nyingine za ziada ni kuwa na ufahamu wa mambo mbalimbali ya kitaifa, kidunia, utalii na kuongeza pia anatakiwa kuwa na hekima, heshima, maadili na kwamba watamchunguza kama anafaa kuajiriwa.“Sifa nyingine zote zinazozungumzwa si sifa zinazozingatiwa na ATCL wala serikali yetu ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania.”Katika swali la msingi, Mbunge wa Igalula, Mussa Ntimizi (CCM), alisema,“wananchi wa Kata ya Tura katika Vijiji vya Mwamlela, Mmunyu na Ikongwa hawana kabisa mawasiliano ya simu, licha ya umuhimu wa mawasiliano kiusalama na kiuchumi. Ntimizi alitaka kujua serikali inatoa ahadi gani ya kupatikana kwa mawasiliano katika vijiji hivyo.Akijibu swali hilo, Nditiye alisema serikali kupitia Mfuko wa Mawasiliano kwa Wote imeendelea kutekeleza miradi mbalimbali ya kufikisha huduma za mawasiliano kote nchini.Alisema kuwa Julai mwaka huu mfuko ulitangaza zabuni ya awamu ya nne kwa ajili ya kufikisha huduma za mawasiliano katika kata 521 zenye vijiji 1,222. Nditiye alisema kuwa kata ya Tura ilijumuishwa kwenye zabuni, ikiwa na vijiji vya Karangasi, Mmunyu na Mwamlela na kwamba ilifunguliwa na baada ya tathmini, kupata mzabuni katika maeneo haya. Utekelezaji utaanza baada ya mkataba kusainiwa mwezi Desemba mwaka huu. | 3kitaifa
|
Na LEONARD MANG’OHA-DAR ES SALAAM
MAMLAKAya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji Tanzania (EWURA) imetangaza kushuka kwa bei ya petroli huku dizeli na mafuta ya taa vikipanda kwa wastani wa Sh saba hadi 12 kwa lita moja.
Bei hiyo ni tofutti ikilinganishwa zilizotangazwa Machi Mosi mwaka huu.
Taarifa ya Mkurugenzi Mkuu wa Ewura, Felix Ngamlagosi Dar es Salaam jana ilieleza kuwa bei hiyo itaanza kutumika rasmi hii leo.
Taarifa hiyo ilieleza kuwa bei ya rejareja ya petroli imepungua kwa Sh tatu kwa lita moja sawa na asilimia 0.13, huku bei ya jumla ikishuka kwa Sh 5.65 kwa lita au asilimia 0.29.
Wakati petroli ikishuka, bei ya dizeli imepanda kwa Sh 12 kwa lita moja sawa na asilimia 0.63, bei ya jumla imeongezeka kwa Sh 9.11 kwa lita sawa na asilimia 0.50.
“Bei ya rejareja ya mafuta ya taa imepanda kwa Sh saba kwa lita sawa na asilimia 0.36 ambako bei ya jumla imepanda kwa Sh 3.68 kwa lita sawa na asilimia 0.21.
“Kwa kiasi kikubwa, mabadiliko haya ya bei yametokana na mabadiliko ya bei za mafuta katika soko la dunia, mfumuko wa bei na gharama za usafirishaji (BPS Premiums) ikilinganishwa na mwezi uliopita,” ilieleza sehemu ya taarifa hiyo.
Ilisema Machi mwaka huu hakuna mzigo wa mafuta uliyopokelewa nchini kupitia bandari ya Tanga.
“Ongezeko hilo la bei za mafuta linatokana na ongezeko la faida ya wauza mafuta wa jumla na rejareja kutokana marekebisho yaliyofanywa kukidhi matakwa ya mfumko wa bei kwa mujibu wa kanuni ya ukokotoaji wa bei za mafuta katika mwaka 2016,” iliongeza taarifa hiyo. | 3kitaifa
|
MANCHESTER, ENGLAND BAADA ya klabu ya Manchester United kutoka sare ya 3-3 dhidi ya Newcastle United, kocha Van Gaal amewatupia lawama wachezaji wake, Jesse Lingard na Marouane Fellaini. Mchezo huo wa Ligi Kuu nchini England ambao ulipigwa juzi kwenye Uwanja wa St. James Park, Manchester walishindwa kutamba mbele ya wenyeji wake japokuwa klabu hiyo ilikuwa inaongoza kwa mabao 2-0. Hata hivyo, Van Gaal aliwatupia lawama wachezaji wake kwa kupoteza nafasi ambazo walizipata katika mchezo huo. “Tunaweza kujilaumu wenyewe kwa kuwa tulikuwa na uwezo wa kuumaliza mchezo mapema kutokana na jinsi tulivyokuwa tunaumiliki, lakini wachezaji wangu kama vile Jesse Lingard na Marouane Fellaini walipata nafasi za kutupatia furaha lakini walishindwa. “Tumefanikiwa kupata mabao matatu na wao wamepata matatu lakini haina maana yoyote kwetu kwa kuwa tumeondoka na pointi moja wakati tulikuwa na nafasi ya kuondoka na pointi tatu. Katika mchezo huo mshambuliaji wa Manchester United, Wayne Rooney, alitoa mchango mkubwa wa kupachika mabao mawili katika sare hiyo ya mabao 3-3. | 5michezo
|
ELIYA MBONEA-KARAGWE KESHO Rais Dk. John Magufuli
anatarajiwa kufungua Hifadhi ya
Burigi-Chato yenye ukubwa wa kilometa za mraba 4,702. Akizungumza kwenye mahojiano na
wanahabari waliotembelea hifadhi za Burigi-Chato, Ibanda Kyerwa na Rumanyika
Karagwe, Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Costantine Kanyasu, alisema
watakaowekeza katika hifadhi hizo hawatajutia fursa hiyo. “Wawekezaji wa Kitanzania
katika sekta ya utalii changamkieni maeneo yaliyotengwa na kuyatumia kibiashara
kabla wageni hawajayachangamkia. “Uwekezaji unaotakiwa kwenye maeneo hayo si wa
maghorofa, ni huduma bora, ndiyo maana watalii hupendelea kulala kwenye mahema
na kuona vitu wanavyovitaka,” alisema Kanyasu. Alisema katika eneo ambalo
Tanzania haijafanikiwa kulitumia hata kwa asilimia 30, ni eneo la biashara ya
utalii, kwamba hadi sasa zinatumika asilimia 10 hadi 25 ya vivutio vilivyopo. “Tanzania ni ya kwanza Afrika kuwa na vivutio
vingi, tungeweza kupokea watalii milioni 10 kwa mwaka. Lakini watalii hao
wanatafutwa na nani? “Kazi ya Serikali ni kuuza
maeneo ya hifadhi, wafanyabiashara wa Kitanzania kwa ubia na wengine wana
wajibu wa kutafuta wateja na kuwekeza kwenye sekta ya utalii ili wapate
utajiri,” alisema. Katika mahojiano hayo, Kanyasu alizitaja
sababu za kupandisha hadhi yaliyokuwa mapori ya akiba na kuwa hifadhi za taifa
kwanza ilikuwa ni kuyaongezea thamani. “Tunaamini Tanapa wamekuwa na
uzoefu na utaalamu wa kufanya biashara ya utalii kwa muda mrefu na wana uwezo
wa kusimamia biashara ya utalii. “Hifadhi ya taifa ni hatua ya
juu kabisa ya uhifadhi ambapo tunaamini kutaongeza thamani na kuhamasisha
wawekezaji kwenda maeneo hayo na kuyatumia kibiashara. “Utalii wa Kaskazini umeimarika si kwa bahati
mbaya, kwa sababu mgeni akiteremkia Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Kilimanjaro
(KIA), anaweza kwenda Hifadhi ya Mkomazi, Kilimanjaro, Arusha, Manyara,
Tarangite na Ngorongoro na Serengeti. “Hivyo uwapo wa Hifadhi ya
Taifa Burigi-Chato, Ibanda Kyerwa na Rumanyika Karagwe, Rubondo, Gombe na
Katavi, kutafanya ukanda huo kuwa eneo kubwa, hivyo mtalii kuchagua aanzie
wapi,” alisema Kanyasu. Alisema kuanza kupokea watalii
kwenye hifadhi hizo kutavuta idadi kubwa ya wawekezaji waliohofia kwenda
kuwekeza kutokana na hofu ya kuwa na hifadhi moja ambayo ikipokea watalii 500
inakuwa imejaa. “Kujengwa Uwanja wa Ndege wa
Kimataifa wa Chato uliopo kilometa 180 kutoka Geita ni mkakati madhubuti wa kuunyanyua
na kutangaza utalii kwenye ukanda huo. “Uwanja ule una umuhimu,
utaongeza thamani ya hifadhi na pili watalii watakwenda kwenye hifadhi zilizopo
maeneo hayo kwa gharama nafuu,” alisema Kanyasu. | 3kitaifa
|
Kwa pointi hizo, Yanga imeiivua ubingwa Azam FC, kwani timu hiyo ya Chamazi inao uwezo wa kufikisha pointi 54 tu katika mechi zake tatu zilizobaki kukamilisha msimu huu.Yanga imetangaza ubingwa jana baada ya kuibugiza Polisi Morogoro kwa mabao 4-1 kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam, huku mshambuliaji wa zamani wa Simba, Amissi Tambwe akifunga mabao matatu ‘hat-trick.’Mabingwa hao wa kihistoria wa Bara ambao wamefikisha rekodi ya kutwaa taji mara 25 kama Bayern Munich ya Ujerumani juzi, ilitwaa taji hilo kwa mara ya mwisho mwaka 2013. Simba inayoifuatia imetwaa taji hilo mara 18.Kwa ubingwa huo, Yanga sasa watarejea katika nafasi ya kuiwakilisha nchi katika Ligi ya Mabingwa Afrika baada ya msimu huu kushiriki Kombe la Shirikisho kutokana na kumaliza nafasi ya pili msimu uliopita nyuma ya Azam FC. Yanga imetawazwa bingwabaada ya kufikisha pointi 55, ikishinda mechi 17, ikitoka sare mara nne, kufungwa mara tatu na kufunga mabao 51 huku ikifungwa 15.Imebakiza mechi mbili dhidi ya Azam FC utakaochezwa Mei 6 na kumaliza ligi kwa kuikabili Ndanda FC mjini Mtwara, Mei 9. Tangu ilipofungwa na Simba, Machi 8, mwaka huu kwa bao 1-0, Yanga haijapoteza mechi yoyote ikicheza mechi nane mfululizo ikiondoka na ushindi.Tambwe alifunga bao safi la kwanza katika dakika ya 41 akiunganisha krosi safi ya Simon Msuva na kuasha nderemo kwa mashabiki wa Yanga upande wa kusini unaokaliwa na mashabiki wa klabu hiyo ya Jangwani.Polisi walianza kipindi cha pili kwa nguvu na dakika nne walimtoa mshambuliaji wa Yanga anayecheza kwa mkopo, Said Bahanuzi na kumuingiza Nicholaus Kabipe, lakini mabadiliko hayo hayakuisaidia na badala yake Yanga walipata bao katika dakika ya 53 likifungwa tena na Tambwe akimalizia mpira uliotemwa na kipa wa Polisi, Abdul Ibad.Mpira wa bao hilo ulianzia kwa Msuva aliyepiga shuti kali lililotemwa na kipa huyo na mpira kumkuta mfungaji aliyeujaza wavuni na hapo, sherehe za ubingwa kwa mashabiki wa Yanga waliofurika uwanjani zikaanza.Tambwe alijihakikishia kuondoka na mpira baada ya kufunga bao la tatu kwa kichwa akikamilisha ‘hat-trick’ katika dakika ya 59 akiunganisha krosi ya Mrisho Ngassa.Ubingwa ulikamilishwa sare Yanga katika dakika ya 66 baada ya Msuva kufunga bao la nne kwa shuti kali baada ya akiwahi pasi murua ya kupenyezewa na Ngassa ambaye hakuwa mchoyo katika kutengeneza nafasi za kufunga jana. Kwa bao hilo, Msuva amezidi kujiweka pazuri kutwaa Kiatu cha Dhahabu akiongoza kwa kufunga mabao 17 wakati Tambwe anamfuatia akiwa na mabao 14. Moja alilifunga akiwa Simba.Bantu Admin aliifungia Polisi Moro bao la kufutia machozi katika dakika ya 83 baada ya kupiga shuti kali lililogonga ‘mtambaa panya’ kabla ya kutinga wavuni baada ya kumshinda kipa Deogratius Munishi ‘Dida.’Wakati Yanga ikiwa imeshajihakikishia ushindi huo, Mkuu wa Idara ya Habari wa Yanga, Jerry Muro alianzisha sherehe za ubingwa kwa kufungua mvinyo, huku mashabiki wakiwa na fulana zilizoandikwa ‘Yanga bingwa 2014/15…ubingwa wa mapema zaidi.’Mara baada ya pambano kumalizika, wachezaji wa Yanga wakiongozwa na kocha wao mkuu, Hans van der Pluijm walizunguka uwanja kuwapongeza mashabiki wao wakiwa na fulana zilizoandikwa ‘Yanga Bingwa 2014-2015.’Vita sasa imebaki katika kusaka nafasi ya pili, ambapo Azam FC na Simba ambazo zitacheza mwishoni mwa wiki, kila moja inawania nafasi hiyo, huku Azam ikiwa na pointi 45 wakati Wekundu wa Msimbazi wana pointi 41.Mbali na nafasi hiyo, pia vita kali nyingine iko katika kupigania kutoshuka daraja, ambapo Ndanda FC, Polisi Moro, Tanzania Prisons kila moja ina pointi 25 pamoja na timu nne zenye pointi 28, zikipigana vikumbo kuepuka kushuka.Yanga: Munishi, Juma Abdul, Oscar Joshua, Mbuyu Twite, Kelvin Yondani, Said Juma, Msuva/ Jeryson Tegete, Haruna Niyonzima/ Nizar Khalfan, Tambwe/ Hussein Javu, Ngassa na Kpah Sherman. Polisi Moro: Ibad, Ally Teru, Hassan Mganga, Meshack Abel/ Bakari Nahodha, Laban Kambole, Anafi Selemani, Bantu, Said Mkangu, Bahanuzi/Kabipe, Seleman Kassim na James Abrose/Mussa Mohamed. | 5michezo
|
RAIS John Magufuli ameitaka Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU), kuhakikisha inabana kila kona bila kujali chama, taasisi au mtu katika vita dhidi ya rushwa nchini.Alitoa agizo hilo Dar es Salaam jana wakati akipokea taarifa ya utendaji ya mwaka mmoja ya Takukuru pamoja na kumwapisha Kamishna wa Polisi, Valentino Mlowola kuwa Balozi wa kwanza wa Tanzania nchini Cuba. Baada ya kupokea taarifa hiyo ya hali ya rushwa nchini, Rais Magufuli alisema rushwa ni adui wa haki, amani na maendeleo, hivyo Takukuru lazima ibane kila kona, kila chama, kila taasisi na kila mtu bila woga.Alimtaka Mkurugenzi Mkuu wa Takukuru, Kamishna wa Polisi, Diwani Athumani, kwa kutumia mamlaka aliyonayo pamoja na cheo chake cha kipolisi, kwa kusaidiana na wasaidizi wake akiwemo Naibu Mkurugenzi Mkuu, Brigedia Jenerali John Mbungo na watendaji wengine, kumshughulikia mtu yeyote anayejihusisha na vitendo vya rushwa.“Nchi hii ina wajuaji wengi, maajabu mengi yanafanyika, Mkurugenzi Mkuu amezungumza hapa kuhusu kulipa kodi, hilo ni eneo mojawapo ambalo nchi hii inaibiwa sana, wapo baadhi ya wafanyabiashara wana mashine za kielektroniki za serikali na nyingine za kwao wenyewe, kwa hiyo mapato yanayoingia serikalini siyo yale yanayotakiwa, na hayo yanafanyika mpaka leo,” alisema Rais Magufuli.Aliongeza, “Mkurugenzi Mkuu pia ulinieleza kuwa kuna mtu aliingiza magari 194 bila kuyalipia kodi na kodi aliyokwepa ni zaidi ya shilingi bilioni nane, na mtu huyo anatetewa sana na watu, nimekuweka wewe kuwa Mkurugenzi Mkuu wa Takukuru, kwa kuwa wewe ni Kamishna wa Polisi, si kwa bahati mbaya. Ukishindwa kumkamata mtu kwa sheria za Takukuru, tumia za Polisi kumweka ndani mtu yeyote.” Aidha, pia alimtaka bosi huyo wa Takukuru, kuwafikisha mahakamani watumishi wake wanaotuhumiwa kwa vitendo vya rushwa, akiwemo mmoja wa wakurugenzi aliyewatapeli viwanja wafanyakazi wenzake.Rais Magufuli alisema mkurugenzi huyo ambaye yuko Makao Makuu ya Takukuru, aliwauzia viwanja hewa wafanyakazi wenzake Bagamoyo mkoani Pwani vyenye thamani ya zaidi ya Sh bilioni moja na hajafikishwa mahakamani wala kurudisha fedha hizo. Alisema jambo hilo limekuwepo kwa muda mrefu tangu Kamishna Mlowola akiwa Mkurugenzi Mkuu wa taasisi hiyo na alishindwa kumchukulia hatua mtuhumiwa huyo.Kuhusu kuitaka Takukuru ifanye kazi yake bila woga, Rais Magufuli pia alifichua mpango wa rushwa uliokuwa umesukwa na baadhi ya viongozi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Wilaya ya Ilala mkoani Dar es Salaam. Alisema alipigiwa simu na watu fulani, wakimweleza kuwa wanaombwa rushwa na viongozi wa CCM ili wapangishwe kwenye majengo yao yaliyopo Ilala. Alisema viongozi hao wa CCM, walitaka watu hao kulipia majengo, lakini pia waliwataka wawape rushwa kwa kuwa ndiyo kula yao.“Nikamtafuta mkurugenzi mmoja wa Takukuru na kumwagiza ahakikishe watu hao wanakamatwa tena wakiwa wamevaa nguo za kijani, baada ya masaa mawili mmoja akashikwa, halafu akawapigia simu wenzake na kuwaambia kwamba ameshapata mgawo wake, nao wakasema tunakuja, walipofika nao wakakamatwa,” alisema.Katika kuonesha namna mambo yasivyokwenda sawa katika baadhi ya taasisi za serikali, Rais Magufuli pia alisema baadhi ya maduka ya kubadilishia fedha, yalikuwa yakitumika vibaya kwa kutoroshea fedha nje ya nchi, lakini pia yalikuwa kama uchochoro wa kupitishia fedha za dawa za kulevya. Alisema baada ya kugundua madudu mengi yanafanyika kupitia maduka hayo, aliamua kumuagiza Gavana wa Benki Kuu (BoT), Profesa Florens Luoga kuyafuatilia. Rais Magufuli alisema watu wanakwenda kuchukua fedha BoT kwa ajili ya kuuza kwenye maduka yao ya kubadilishia fedha, lakini walikuwa hawasemi waliuza kiasi gani.Wakati mwingine wanafanya mipango na kupandisha kiwango cha kubadilishia dola kufikia Sh 2,400, hali inayolenga kuyumbisha uchumi wa nchi. Katika hayo yote, Rais Magufuli aliitaka Takukuru kuhakikisha inamfikia kila mtu au chama au taasisi katika vita dhidi ya rushwa kwa kuwa rushwa ikidhibitiwa, Tanzania itafanikiwa sana.Aliwapongeza Takukuru kwa kuokoa Sh bilioni 70.3 katika vita dhidi ya rushwa ambazo zitasaidia katika kutoa huduma za jamii ikiwemo kununua dawa, kutoa elimu na kulipa mishahara ya wafanyakazi. Kuhusu ombi la Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Utumishi na Utawala Bora, George Mkuchika, la kuwapeleka wafanyakazi wa Takukuru katika wilaya 21 ambazo hazina watendaji hao, Rais Magufuli aliziagiza mamlaka husika kulitekeleza hilo haraka. | 3kitaifa
|
Khamis Sharif – Zanzibar SERIKALI
ya Mapinduzi ya Zanzibar (SMZ) imezindua mkakati wa afya ya jamii wenye lengo
la kuhakikisha huduma za afya zinaimarika zaidi, kuanzia ngazi ya familia,
jamii na taifa kiujumla. Mpango
mkakati huo umezinduliwa na Waziri wa Biashara, Viwanda na Masoko Zanzibar, Balozi
Amina Salum Ali wakati wa mkutano wa 12 wa kutathmini shughuli za sekta ya afya
Zanzibar huko Mtoni mjini Unguja. Waziri Amina alisema Zanzibar imepiga hatua kubwa katika
kusambaza huduma za afya mijini na vijijini, lakini kuzinduliwa kwa mkakati huo
kutapunguza changamoto za maradhi kwa wananchi zinazoendelea kujitokeza na
kuongeza ufanisi katika sekta za afya. Alisema
Serikali itafanya kila juhudi ili kuhakikisha mkakati huo unakuwa endelevu,
kwani unagusa nyanja mbalimbali, ikiwamo kupunguza vifo vya wajawazito na
watoto wakati wa kujifungua. Aidha
Balozi Amina aliwataka wafanyakazi watakaoshughulikia mpango huo kuhakikisha
wanatumia nafasi hiyo kuona malengo yaliyowekwa yanafikiwa. “Nielekeze
shukurani kwa washirika wa maendeleo kuainisha michango yao mikubwa, hii ni
hatua njema na uimara wa uhusiano wetu kwao, kwani mbali ya kusaidia kuimarisha
sekta ya afya, pia michango yao huonekana katika sekta nyingine za elimu, maji,
miundombinu na umeme,” alisema Balozi Amina. Akizungumzia
kuhusu mafanikio yaliyofikiwa katika sekta ya afya, Katibu Mkuu Wizara Afya
Zanzibar, Asha Ali Abdalla alisema hatua kubwa imefikiwa katika kuimarisha
Hospitali ya Mnazi Mmoja kutoka kuwa hospitali ya kawaida na kufikia kuwa ya
rufaa na moja ya hospitali zinazotoa mafunzo katika ukanda wa Afrika Mashariki. Alisema
Serikali imefanya juhudi kuongeza madaktari bingwa na wafanyakazi wa kada nyingine
za afya na kuongeza vitendea kazi muhimu katika hospitali na vituo vya afya
ambavyo vinaongeza ufanisi wa kutoa huduma kwa sasa. Aliongeza
kuwa hatua zilizochukuliwa na Serikali pamoja na wananchi kwa kushirikiana na
washirika wa maendeleo Zanzibar imeweza kudhibiti maradhi ya malaria ambayo yalikuwa
yakiwasumbua wananchi wengi na kuathiri nguvu kazi ya kuimarisha uchumi. Alisema
pia juhudi nyingine iliyochukuliwa ni ile ya kudhibiti kuenea kwa virusi
vya Ukimwi na kupunguza maradhi ya malaria pamoja na mengine nyemelezi nchini. Mwakilishi
wa Shirikiala la Afya Duniani (WHO) Zanzibar, Dk. Ghirmay Andemichael aliisifu
SMZ kwa kufanikiwa kudhibiti malaria na kupunguza kusambaa kwa kipindupindu –
magonjwa ambayo kwa miaka kadhaa iliyopita yalikuwa tishio kwa wananchi. Alisema
uamuzi wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kuongeza bajeti ya Wizara ya Afya
kila mwaka, umeleta mafanikio makubwa katika kuwapatia huduma wananchi. Dk.
Andemichael alieleza kwamba washirika wa maendeleo wataendelea
kushirikiana na SMZ katika kuimarisha huduma mbalimbali za kijamii, ikiwamo
utoaji wa huduma katika sekta ya afya nchini. | 4afya
|
SIMBA leo inashuka katika dimba la Taifa, Dar es Salaam kuivaa JS Souara ya Algeria kwenye mchezo wa Ligi ya Mabingwa wa Afrika ikiwa na matumaini ya ushindi mbele ya mashabiki wake.Wakizungumza jana kwa nyakati tofauti kocha wa Simba Patrick Aussems na kocha wa JS Souara, Neghiz Nabil kila mmoja alijigamba kuibuka na ushindi na kusifu kikosi cha mpinzani wake. Aussems alisema katika kikosi chake atamkosa Erasto Nyoni, ambaye aliumia goti la kulia kwenye mchezo wa Kombe la Mapinduzi dhidi ya KMKM, lakini akasema nafasi yake itazibwa na wachezaji wengine kwani Simba ina wachezaji wa kutosha mashabiki wasiwe na hofu.“Tunaiheshimu sana JS Souara maana wanatoka kwenye nchi yenye ligi nzuri Afrika na wanashika nafasi ya tano katika ligi ya kwao, tutamkosa Erasto Nyoni ambaye amekuwa katika kiwango bora katika michezo aliyocheza lakini wapo watu wa kuziba nafasi yake,” alisema Aussems Tunawaomba Watanzania waje kuishangilia Simba ili ipate nafasi ya kuchukua ubingwa wa Afrika kama walivyofanya katika mchezo dhidi ya Nkana Rangers,” aliongeza Naye kocha wa JS Souara Nabil alishukuru kwa maandalizi mazuri waliyopata na kusema Simba ni timu bora zaidi yao ila wanatamani kushinda mchezo wa leo.“Nashukuru tulifika jana (juzi) na tulipata mapokezi mazuri, tunaiheshimu Simba lakini ninatamani kushinda mchezo wa kesho (leo) ili kujiweka katika nafasi nzuri katika kundi letu,” alisema Nabil Pia alisema Thomas Ulimwengu kulingana na rekodi zake ni mchezo mzuri lakini kwa sasa anahitaji mazoezi sana ili arudi katika kiwango chake na katika mchezo huo atamkosa kipa wake mmoja.Simba ambayo ipo kundi D pamoja na Al Ahly ya Misri, AS Vita ya Congo DRC na JS Saoura ya Algeria inashuka katika dimba la Taifa ikiwa na kumbukumbu ya kuitoa Nkana Rangers ya Zambia kwa mabao 3-1 na kufanikiwa kutinga hatua ya makundi. Hivyo ina kibarua cha kuhakikisha Al Ahly ambayo ilicheza fainali ya Klabu Bingwa Afrika dhidi ya Esperance Tunis ya Tunisia msimu uliopita inazifunga pamoja na AS Vita Club ambayo ilicheza fainali ya Kombe la Shirikisho dhidi ya Wydad Casablanca ya Morocco.Wakati huohuo, Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dk. Harrison Mwakyembe amewaomba Watanzania kuungana naye kuishangilia Simba ili ishinde mchezo huo kwasababu hao ndio wawakilishi wa nchi waliosalia. “Nawaomba Watanzania tuoneshe uzalendo kwa Simba, tuishangilie kwa nguvu kuanzia dakika ya kwanza hadi dakika 90 ili ishinde kwa sababu ndio wawakilishi pekee waliosalia,” alisema Dk Mwakyembe. Mgeni rasmi katika mchezo huo anatarajiwa kuwa Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri wa Muungano wa Tanzania Dk Tulia Akson, ambaye atawaongoza maelfu ya Watanzania kuishangilia Simba. Msemaji wa Simba, Haji Manara ameibuka na kauli mbiu inayosema, `Simba Yes We Can’, kuelekea mchezo huo wa leo. | 5michezo
|
WAZIRI Mkuu, Kassim Majaliwa amewataka viongozi wa vyama vya ushirika nchini kutumia vizuri rasilimali za vyama hivyo na kwamba serikali haitalipa deni lolote lililokopwa na vyama hivyo.Ametoa agizo hilo wakati akizungumza kwa nyakati tofauti na wafanyabiashara na wadau wa zao la kahawa baada ya kuwasili mjini Bukoba kwa ajili ya ziara ya kikazi mkoani Kagera.“Biashara ya kununua madeni yaliyokopwa na vyama vya ushirika haipo kwenye Serikali hii ya Awamu ya Tano, badala yake itawachukulia hatua wote waliohusika na ubadhirifu huo,” amesema.Waziri Mkuu amepiga marufuku wafanyabiashara kuwaibia wakulima kwa kununua kahawa mbichi ikiwa shambani maarufu kama butura.Amesema serikali itachukua hatua kali kwa viongozi wa vyama vya ushirika ambao si waaminifu na wabadhirifu wa mali za ushirika na kusema wanataka wakulima wapate fedha.Kwa mujibu wa Waziri Mkuu serikali itahakikisha wafanyabiashara wote, hususani wa mazao ya kilimo wanakuwa na mfumo sahihi wa ununuzi wa mazao utakaoongeza tija kwao na kwa wakulima.Alisema kwa sasa Serikali inataka kuondoa mfumo uliopo wa vyama vya ushirika kufanya biashara na badala yake jukumu hilo libakie kwa wafanyabiashara.Kadhalika, aliwataka wafanyabiashara hao waihakikishie serikali kwamba watanunua kahawa yote iliyopo kwa wakulima pamoja na kwenye vyama vya ushirika. Wafanyabiashara wameridhia kununua kahawa yote.Awali, Waziri wa Kilimo Dk Charles Tizeba alisema katika msimu wa mwaka huu jumla ya kilogramu 3,000,464 za kahawa isiyokobolewa na kilogramu 8,191,86 za kahawa safi hazijanunuliwa.Alisema vyama vya ushirika vinakabiliwa na kiwango kidogo cha kahawa kinachonunuliwa mnadani na wakati mwingine kutonunuliwa kutokana na kushuka kwa bei katika soko la dunia.Changamoto nyingine ni kuwapo taarifa za upotoshaji kwa wakulima kutoka kwa walanguzi za kuzuia wakulima kukusanya kahawa yao kupitia vyama vya Ushirika vya Msingi kuwa wao watanunua na kuwapatia bei nzuri. | 3kitaifa
|
KUTOKANA na tahadhari ya kimbunga Kenneth kupiga katika pwani ya mikoa ya Mtwara na Lindi, serikali na taasisi zake zimechukua hatua za tahadhari katika kukabiliana na kimbunga hicho ili kuepuka maafa makubwa kwa wananchi wa mikoa hiyo na maeneo jirani.Katika taarifa yake kwa umma, Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Kazi, Ajira, Vijana na Wenye Ulemavu), Jenista Mhagama alisema kimbunga hicho kinatarajiwa kusababisha athari mbalimbali ikiwemo mtawanyiko mkubwa wa mafuriko na upepo mkali wa kasi ya kilomita 130 kwa saa katika uelekeo wa mashariki umbali wa kilomita 175 kutoka pwani ya Mtwara.Kwa mujibu wa Waziri Mhagama, kimbunga hicho pia kinatarajiwa kusogea na kuelekea katika pwani kusini mwa Tanzania na kitaambatana na mafuriko ikizingatiwa kuwa pwani ya mikoa ya Mtwara na Lindi ipo chini ya usawa wa bahari. Athari zingine ambazo kimbunga hicho kinaweza kusababisha zimetajwa kuwa ni maisha ya watu, uharibifu wa makazi, mali, mazao mashambani, miundombinu na mazingira, shughuli za usafirishaji kwa njia ya maji, anga na nchi kavu.“Serikali inaelekeza shughuli mbalimbali zinazofanywa kandokando na ndani ya Bahari ya Hindi hususani uvuvi, biashara ndogondogo, usafirishaji majini na anga zisitishwe katika kipindi hiki kilichotabiriwa kuwa hatarishi ili kuepusha athari zinazoweza kujitokeza, kamati za maafa zifuatilie kwa kina jambo hili,” alieleza Mhagama. Mamlaka ya Hali ya Hewa nchini (TMA), ilitabiri uwezekano wa kutokea kimbunga hicho na mafuriko katika maeneo ya pwani ya mikoa ya Mtwara na Lindi kuanzia Aprili 24-26, mwaka huu.Taasisi zajiandaa Katika kuchukua tahadhari ya kuepuka maafa yanayoweza kusababishwa na kimbunga Kenneth, Mkuu wa Mkoa wa Lindi ambaye pia ni Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma, Godfrey Zambi, ameagiza shule zote kwenye mikoa hiyo kufungwa pamoja na taasisi za umma ikiwemo ofisi za mkoa, fedha na binafsi kwa siku mbili kuanzia jana na kuwataka watu wabaki majumbani mwao, wasitaharuki kwa kukimbia hovyo kwa sababu za kiusalama.Alisema maeneo ambayo yanatakiwa kuendelea na kazi katika siku hizo mbili ni vituo vya afya, hospitali, polisi na magereza. Zambi alisema mkoa wake umetenga maeneo ya dharura ya milimani ambako wananchi wanaoishi mabondeni wanapaswa kwenda kuishi kwa muda, huku huduma za dharura za afya na zimamoto zikiwa zimewekwa katika hali ya utayari. Kwa mujibu wa mkuu wa mkoa huyo, wananchi wanaoishi kando kando ya ukanda wa pwani wanatakiwa kuhamia katika Shule za Sekondari za Angaza, Mpilipili, Lindi Sekondari, Uwanja wa Jeshi la Wananchi (JWTZ) na Uwanja wa Mpira wa Mtanda.“Tumesimamisha kwa tahadhari vyombo vya baharini pamoja na kivuko visifanye kazi, lakini pia maadhimisho ya siku ya malaria duniani nzilizopangwa kufanyika mkoani hapa kitaifa nazo tumezisitisha baada ya kushauriana na Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu,”alisema Zambi. Naye Mkurugenzi wa Kinga wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Watoto na Wazee, Dk Leonard Subi, aliwataka wananchi kuchukua tahadhari kwa kutokaa kwenye madirisha, nyumba ziwe wazi, wakae ndani na chini ya meza.Dk Subi alisema kuwa vituo vyote vya afya katika mikoa ya Lindi, Mtwara na Ruvuma vitakuwa wazi wakati wote kwa ajili ya kutoa huduma endapo kutatokea maafa. Kwa upande wake, Msajili wa Meli kutoka Shirika la Wakala wa Meli Tanzania (TASAC), Japhet Loisimaye, alisema wamiliki wa vyombo vya majini katika mikoa ya Dar es Salaam, Lindi na Wilaya ya Mafia nao wanatakiwa kusitisha shughuli zao kwa muda mpaka itakapotolewa tena taarifa nyingine ya hali ya usalama baharini.Loisimaye alisema japo kimbunga hicho kimeelezwa kupiga katika pwani ya Mkoa wa Mtwara kwa sehemu kubwa, lakini katika mikoa ya Dar es Salaam, Lindi na Wilaya ya Mafia kunaweza kuwa na upepo mkali unaoweza kusababisha maafa makubwa, hivyo ni vyema vyombo hivyo vidogo na vikubwa, vya abiria na mizigo visiingie majini katika siku hizo tatu za tahadhari.Kauli ya Zimamoto Kwa kuzingatia madhara yanayoweza kusababishwa na kimbunga Kenneth, Jeshi la Zimamoto na Uokoaji nchini limetoa wito kwa wananchi waishio katika maeneo hatarishi, ikiwemo pembezoni mwa bahari na kandokando ya mito, kuyahama maeneo hayo haraka. Kamishna wa Operesheni wa Jeshi hilo, Billy Mwakatage, alisema wananchi wanapaswa kufuatilia taarifa za utabiri kutoka Mamlaka ya Hali ya Hewa pamoja na kusikiliza vyombo vya habari na kuzingatia tahadhari zinazotolewa.Kwa kuwa kimbunga hicho kinaambatana na mvua kubwa, Mwakatage amewataka wananchi kuepuka kusimama au kuegesha magari yao chini ya miti mikubwa kwa kuwa kuna uwezekano wa miti mikubwa kuanguka, lakini pia mawe makubwa na udogo kuporomoka na kuziba barabara. Hali ya Zanzibar Kwa upande wa Zanzibar, Mamlaka ya Usafiri baharini Zanzibar (ZMA), imesitisha shughuli za usafiri wa baharini kuanzia jana mchana kutokana na tahadhari ya Kimbunga Kenneth. Kaimu Mkurugenzi wa ZMA, Ramadhan Hussein, alisema kuwa wamelazimika kusitisha shughuli za safari kwa vyombo vyote baharini hadi hapo taarifa zaidi ya Mamlaka ya Hali ya Hewa zitakapotolewa.Bunge latoa tahadhari Akiwa bungeni jana Waziri Mhagama aliwataka wananchi wanaoishi kando ya Bahari ya Hindi kujiepusha kwa kuondoka maeneo hayo kabla ya hali hatarishi ya kimbunga na mafuriko kutokea.Pia ilisema shughuli mbalimbali zinazofanywa kando na ndani ya Bahari ya Hindi zikiwemo za uvuvi, biashara ndogo na usafirishaji wa majini na anga, zinatakiwa kusimamishwa katika kipindi hicho ili kuepusha athari zinazoweza kutokea kwa wananchi. Alitoa taarifa hiyo kwa niaba ya Waziri Mkuu (PM) na Idara ya Maafa. Alisema kimbunga hicho kitaendelea kusogea kuelekea hadi Pwani ya Kusini ya nchi na kitaandamana na mafuriko kwani Pwani ya mikoa ya Mtwara na Lindi kwani mikoa hiyo ipo chini ya Usawa wa Bahari (ASL).Alisema hali hiyo inatarajiwa kuleta athari mbalimbali zikiwemo za mtawanyiko mkubwa wa mafuriko na upepo mkali ambavyo vinavyoweza kusababisha athati kwa maisha uharibifu wa makazi, mali, mazao shambani, miundombinu na mazingira kutokana na kuongezeka kwa kina cha maji ya Bahari ya Hindi katika kipindi kifupi. Aidha alisema, shughuli za usafirishaji kwa njia wa anga na kwenye maji na nchi kavu zinaweza kuathirika katika mikoa hiyo kutokana na hali mbaya inayotabiriwa na TMA. “Tunaendelea kusisitiza kwamba Kamati za Maafa katika ngazi za vijiji hadi mikoa katika maeneo husika, kwa mujibu wa sheria tuliyonayo, kufuatilia kwa karibu na kwa kina jambo hilo ambalo limekwisha kutabiriwa,” alisema.Taharuki Mtwara Wakati huo huo, Mwandishi Sijawa Omary anaripoti kutoka Mtwara kuwa wakazi wa mkoani humo walilazimika kukimbia makazi yao na kwenda maeneo mengine kwa ajili ya kunusuru maisha yao baada ya kimbunga Kenneth kupita pembezoni mwa mkoa huu kuelekea nchi jirani ya Msumbiji. Gazeti hili lilishuhudia namna ambavyo wananchi wa mkoa huo walivyokuwa wakihangaika huku na kule kufuata sehemu za kunusuru maisha yao juu ya tukio hilo. Baadhi ya maeneo ambayo wakazi hao walikusanyika kufuatia maelekezo yaliyotolewa na serikali ya mkoa huu kuwa wananchi waishio kando kando ya bahari wahamie kwenye maeneo ambayo yatakuwa salama kwao na hata likitokea tukio hilo madhara hayatakuwa makubwa kwao. Maeneo hayo ya muda ambayo wakazi hao walikusanyika ilikuwa ni pamoja na shule za msingi na sekondari, Uwanja wa Ndege wa Mtwara, Naliendele, Mangamba, Shule ya Sekondari ya Mustafa Sabodo na maeneo mengine.Mkazi eneo la Shule ya Msingi Tandika, Majengo Manispaa ya Mtwara Mikindani, Amina Abdul alisema kuwa, tukio hilo ilikuwa wakiona tu katika nchi za wenzao na madhara yake huwa ni makubwa na mkoa huu ni mara ya kwanza kuripotiwa kutokea kwa tukio hili. Mustafa Joki, mkazi wa Chuno alisema, mara baada ya serikali kutangaza janga hilo, yeye na familia yake wakafanya maamuzi ya kuchukua tahadhari ya kuhama makazi yao na kuhamia katika vituo ambayo wameelekezwa ili kunusuru maisha yao na kuomba tukio hilo lisitokee.Mkuu wa Mkoa wa Mtwara, Gelasius Byakanwa wakati akizungumza na wananchi hao walioko katika maeneo hayo alisema waendelea kuwa na subira kwa kubaki katika maeneo hayo ambayo ni salama kwao huku serikali ikiendelea kufuatilia zaidi hatua na hali inayoendelea kadiri muda unavyoendelea juu ya tukio hilo na kisha kuwapatia taarifa. Hata hivyo, mkuu huyo alikanusha uvumi uliosambaa kwenye mitandao mbalimbali ya kijamii kuwa hali Mtwara siyo shwari kwani mpaka sasa hali ni shwari na hakuna madhara yoyote ambayo yameweza kutokea hadi sasa kutokana watu wameweza kuchukua tahadhari.Meneja wa wa Mamlaka ya Hali ya Hewa Kanda ya Kusini, Daudi Amasi alisema, kuanzia majira ya asubuhi jana hii hali ya upepo ilianza na kilometa 20 ikaja hadi 30 ikafikia 40 ambapo hadi kufikia majira ya mchana hali ya upepo ilifikia kilometa 60 kwa saa. “Tunaendelea kusisitiza kwa wananchi wa maeneo hayo na maeneo mengine hapa nchini kuendelea kuchukua tahadhari pale panapotokea matukio kama haya na tunapotoa taarifa kama hizi basi wananchi uchukuwe tahadhari ili kuepeusha madhara yanayoweza kujitokeza,” alisema Amasi.Katika hatua nyingine mkuu huyo wa mkoa huyo amevunja kambi zote sita ambazo wakazi hao walikimbilia kwa ajili ya kunusuru maisha makambi ambayo serikali ya Mtwara ilitangaza. Alisema, endapo kutatokea mabadiliko yoyote juu ya tukio hilo watapatiwa taarifa kupitia vyombo vya habari ambavyo viko rasmi ambapo hadi hivi sasa mkoani hapa hali imekuwa shwari na hakujatokea tatizo lolote. | 3kitaifa
|
MADRID, HISPANIA USIKU wa Ulaya unatarajia kuendelea leo katika viwanja viwili, cha Vicente Calderon, Atletico Madrid watawakaribisha Barcelona, huku Benfica wakiwa kwenye uwanja wao wa Estadio da Luz na kuwakaribisha Bayern Munich. Mchezo wa awali ambao ulipigwa Nou Camp, Atletico walipokea kichapo cha mabao 2-1, hivyo leo hii wana kazi ngumu ya kuweza kutamba katika mchezo huo. Barcelona watahakikisha wanashinda mchezo huo kwa kutoa sare ya aina yoyote ili kuweza kusonga hatua ya nusu fainali, wakati huo Atletico ikihitaji ushindi wa zaidi ya bao moja. Kwa ubora walionao Barcelona bado wana nafasi kubwa ya kushinda kwa kuwa wanautolea macho mchezo huo kwa ajili ya kutetea ubingwa huku wakiwa na uhakika wa kutetea na Ligi Kuu. Kocha wa Barcelona, Luis Enrique, amedai kwamba macho yao wanayaelekeza katika mchezo wa leo hivyo lazima waibuke na ushindi dhidi ya kukosi cha Diego Simeone. Wakati huo mchezo mwingine ni kati ya Benfica ambao watajaribu kuutumia uwanja wao wa nyumbani. Katika mchezo wa awali, Bayern ilifanikiwa kushinda bao 1-0 katika dakika ya pili ya mchezo huo ambapo lilidumu hadi dakika 90 zinamalizika. Mchezo huo ulionekana kuwa mgumu wa Bayern japokuwa walikuwa nyumbani, hivyo tunatarajia kuona ugumu zaidi huku Benfica wakiwa nyumbani leo hii. Hata hivyo, kocha wa Bayern, Pep Guardiola, amedai kwamba atahakikisha anaingia hatua ya nusu fainali ili kujihakikishia anatwaa ubingwa huo. | 5michezo
|
MKUU wa Wilaya ya Kongwa, mkoani Dodoma ambaye ni mwenyekiti wa kamati ya ulinzi na usalama wilayani humo, Deogratias Ndejembi, amesema suala la ulinzi na usalama wakati wa uchaguzi wa serikali za mitaa linahusu jamii nzima na si la kamati hiyo pekee.Akizungumza katika kikao cha baraza la madiwani wa halmashauri hiyo juzi, Ndejembi alisema uchaguzi huo utakaofanyika Novemba 24, mwaka huu, ulinzi utaimarishwa katika maeneo yote ili kuhakikisha unafanyika kwa amani na huru.“Madiwani kila kata mkaniorodheshee idadi ya askari mgambo ili nifahamu wapo wangapi tuweze kujipanga vizuri kuhakikisha uchaguzi unaenda vizuri na unafanyika kwa amani,” alisema.Aidha, aliwataka wataalamu wa halmashauri hiyo kuhakikisha katika uchaguzi huo wanafuta maadili kikamilifu kwa kufuata miongozo na kanuni zilizowekwa kisheria. Pia aliwaeleza madiwani wa halmashauri hiyo ambao wote wanatokana na CCM kuwa, kazi iliyopo mbele yao ni kuhakikisha wanapatikana wagombea wanaokubalika na pasipo kutumia rushwa, wasio na makundi wala wasio na kashfa yoyote katika jamii Aliwatahadharisha madiwani hao kuepuka kukumbatia wagombea wasiokubalika kwa wananchi kwa maslahi yao binafsi.Mkuu huyo wa wilaya pia aliwaagiza wenyeviti wote wa vijiji kuhakikisha kabla hawajaondoka madarakani wasome mapato na matumizi kwa wananchi kwa njia ya kuitisha mikutano ya wananchi na kuwasisitiza madiwani hao kuhakikisha wanasimamia jambo hilo kikamilifu.Naye, mkurugenzi wa halmashauri hiyo, Dk Omary Nkullo, alisema ameshazipokea nyaraka za kanuni mpya za uchaguzi huo na hivi karibuni watapokea miongozo ya uchaguzi huo. Baadhi ya wananchi waliohudhuria kikao hicho kinachojadili masuala ya maendeleo ya wilaya zikiwamo huduma za jamii, uchumi na mazingira, walisema mamlaka husika zinatakiwa kutenda haki wakati wa uchaguzi ili kuhakikisha unakuwa salama. | 3kitaifa
|
CHAMA cha Wafanyakazi wa Taasisi za Elimu ya Juu Tanzania (THTU), kimeshauri serikali kufanya mapitio ya viwango vya kodi ya mtu binafsi hasa inayohusu makato ya kodi ya mshahara (PAYE).Akizungumza na vyombo vya habari, Mwenyekiti wa THTU, Dk Paul Loisulie alisema chama hicho kupitia Kamati ya Uchambuzi na Ushauri kuhusu Bajeti Kuu ya Serikali ya mwaka wa fedha 2019/2020, kinashauri kodi hiyo ifanyiwe mapitio.Aliishauri ifanyike mapitio katika viwango vya kodi vya mtu binafsi inayohusiana na makato ya kodi ya mshahara ili kumpatia mfanyakazi unafuu wa kodi. Dk Loisulie alisema mapendekezo hayo yamezingatia mfumo wa kodi wa nchi nyingine za Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) na nchi nyingine za Kusini mwa Jangwa la Sahara.“Pendekezo mahususi linalotolewa ni kupandisha kima cha chini kisichokatwa kodi kutoka shilingi 170,000 hadi 360,000 na hivyo itapunguza maumivu ya kodi kwa mfanyakazi,” alisema. Dk Loisulie alisema ifahamike kwamba kwa sasa hawajalizungumzia suala la kupandisha kima cha chini cha mshahara kwani Shirikisho la Vyama vya Wafanyakazi (TUCTA) limeshafanya wajibu huo ambao wanaunga mkono.Alisema mapendekezo haya ni mahususi kwa ajili ya kuleta unafuu wa kodi kwa mfanyakazi bila kubadili viwango vya asilimia vilivyopo kwa sasa. Hata hivyo alisema suala la kuboresha maslahi ya watumishi halijafanyika na kupewa uzito unaostahili katika bajeti za serikali hivyo kuwafanya watumishi kufanya kazi katika mazingira magumu na kuishi maisha yasiyo na staha na kuathiri utendaji wao wa kazi.Alisema suala la upandishwaji wa madaraja, nyongeza ya mwaka ya mshahara na malipo ya posho kwa watumishi limekuwa gumu kutekelezwa kwa kipindi cha miaka mitatu iliyopita, hivyo kuchangia malalamiko kutokana na ulimbikizwaji wa madai ya wafanyakazi na kuwafanya wabakie katika kipato au madaraja yaleyale kwa muda mrefu. | 3kitaifa
|
NA JENNIFER ULLEMBO, DAR ES SALAAM KIKOSI cha timu ya Yanga kinatarajiwa kuelekea jijini Tanga leo, tayari kwa mchezo wa Ligi Kuu dhidi ya Mgambo Shooting uliopangwa kufanyika Jumamosi hii kwenye Uwanja wa Mkwakwani mkoani humo. Kwa mujibu wa kocha mkuu wa Yanga, Hans Van der Pluijm, ataondoka na wachezaji wote wa timu hiyo na anatarajia kupanga kikosi kitakachoshuka dimbani kesho jioni. Pluijm alisema kuwa awali walikuwa na mpango wakuweka kambi mjini Bagamoyo, lakini kutokana na sababu zilizo nje ya uwezo wao waliamua kuahirisha zoezi hilo. “Kambi ya Bagamoyo ilikuwa ni mkakati wetu wa kwanza kujiwinda na mchezo dhidi ya Mgambo, lakini zipo sababu muhimu zilizopelekea tuahirishe, sasa tutawafuata wapinzani wetu bila kuweka kambi yoyote,” alisema. Mholanzi huyo alieleza wanaelekea jijini Tanga, wakiwa na lengo la kuchukua pointi tatu muhimu na kukiwezesha kikosi hicho kuendeleza gurudumu la ushindani waliloanza nalo msimu huu. “Maandalizi tuliyofanya yanatosha kuwafunga Mgambo, ndiyo maana hata kama tumeshindwa kuweka kambi kama tulivyokuwa tumepanga mwanzo, bado tuna matumaini ya kushinda mchezo huo,” alisema Pluijm. Timu hiyo inashikilia nafasi ya pili katika msimamo wa Ligi Kuu, ikiwa na jumla ya pointi 23 kutokana na michezo tisa iliyocheza sawa na Azam FC inayoongoza ligi hiyo kwa pointi 25. | 5michezo
|
MKUU wa Mkoa wa Mbeya, Albert Chalamila amewataka vijana mkoani humo kuchangamkia fursa zinazotokana katika ufugaji wa ng’ombe wa maziwa ili kuinua maisha yao kwa kuwa kuna soko la uhakika la bidhaa hiyo.“Wakati umefika kwa vijana badala ya kulalamika kuhusu ajira, wangejikita kwenye ufugaji wa ng’ombe wa maziwa ambao ni mkombozi mkubwa na hasa katika kuinua kipato. Soko la uhakika la maziwa lipo lakini uzalishaji ni mdogo,” amesema Chalamila.Akizungumza na waandishi wa habari jijini hapa, Chalamila alisema sekta ya ufugaji wa ng’ombe imekuwa na uhitaji mkubwa wa maziwa kupitia viwanda vya uzalishaji wa bidhaa za maziwa kikiwemo kiwanda cha Asas Dairies Limited cha mkoani Iringa.Amesema kiwanda kinazalisha chini ya uwezo wake kutokana na uhaba wa maziwa. Na kwamba ni fursa kwa vijana kujikita katika ufugaji na kubadilisha maisha yao.“Kampuni ya Asas inanunua maziwa katika wilaya za Rungwe na Busokelo mkoani hapa. Vijana wengi wamefanikiwa katika maisha yao kupitia ufugaji wa ng’ombe wa maziwa lakini bado maziwa hayatoshi,” amesema.Amesema fursa kama hiyo ikichangamkiwa itasaidia kupunguza tatizo la ajira kwa vijana walio wengi mkoani hapa na mikoa ya jirani tayari wameshapata mafanikio makubwa kupitia ufugaji.“Kampuni ya maziwa ya Asas imesongeza huduma kwa wafugaji ikiwemo kutoa elimu ya namna bora ya kufuga ng’ombe wachache wa maziwa ambao watawaletea faida kubwa kutoka na uzalishaji wa maziwa kwa wingi,” amesema Chalamila.Amesema, kampuni hiyo imeweka vituo vya kukusanya maziwa kutoka kwa wafugaji katika wilaya ya Rungwe na halmashauri ya Busokelo ili kumsaidia mfugaji kutopoteza maziwa yake na pia kiwanda kipate maziwa yatakayokwenda kuzalisha bidhaa mbalimbali zinazotokana na maziwa.“Nina taarifa kuwa Asas imepeleka madume ya ng’ombe manne Rungwe kwa lengo la kuendeleza kizazi cha ng’ombe bora wa maziwa ili kuongezeka uzalishaji wa maziwa,” amesema Chalamila.Aliongezea kuwa hilo limefanyika kutokana na uhitaji mkubwa wa maziwa kiwanda cha Asas na hivyo kuhamasisha watu kujikita katika sekta ya ufugaji.Ajira nyingi zimeweza kutengenezwa kupitia ufugaji.“Jitihada hizi zinaonesha uzalendo wa dhati alionao mwekezaji huyo katika kumsaidia mfugaji kuongeza kipato kupitia maziwa. Serikali ya Awamu ya Tano chini ya Rais John Magufuli inahamasisha uwekezaji kwenye lengo la kumwinua Mtanzania wa kawaida,” alisisitiza.Mratibu wa Kitaifa wa Asas Dairies, Lipita Mtimila amesema, kiwanda bado kinahitaji maziwa kutoka kwa wafugaji, kwani uhitaji wa bidhaa zinazotokana na maziwa ni mkubwa hivyo ni muhimu kuhamasisha wakulima kufuga ng’ombe wachache watakaoweza kuwahudumia.“Sisi kama Asas Dairies tutaendelea kutoa huduma kwa wafugaji ili kuongeza uzalishaji maziwa kwa wingi na yenye ubora unaohitajika kiwandani,” alisema Mtimila na kuongeza kuwa jamii ya wafugaji katika mnyororo wa thamani ya maziwa wamekuwa wakitoa ushirikiano mkubwa. | 1uchumi
|
Rais John Magufuli ameiagiza Wizara ya Maliasili na Utalii kuanzisha mchakato wa kuligawa pori la akiba la Selous katika sehemu mbili.Sehemu mojawapo, kwa mujibu wa Rais, itabaki kuwa pori kwa ajili ya shughuli za uwindaji na nyingine ipandishwe hadhi na kuwa Hifadhi ya Taifa.Rais Magufuli ametoa agizo hilo leo Ijumaa (Julai 26, 2019) katika sherehe ya uwekaji wa jiwe la Msingi la mradi wa ujenzi wa mradi wa uzalishaji Umeme wa Rufiji mkoani Pwani.Amependekeza kuwa hifadhi itakayoanzishwa iitwe ‘Nyerere National Park’ kumuenzi mwasisi wa Taifa la Tanzania, Hayati Mwalimu Julius Nyerere huku akitaka Bwawa la Umeme aliloweka jiwe la Msingi liitwe Nyerere.“Nataka hii Game Reserve ikatwe tuibadilishe iwe National Park ili watalii wawe wanakuja kutalii hapa wanaoingia humo badala ya watu kuja kuwinda wanyama pekee,” Rais alisema.Lakini Mkuu huyo wa nchi amesisitiza kuwa si kana kwamba agizo lake halina madhumuni ya kufutilia mbali shughuli za uwindaji kwani zitaendelea kama kawaida katika uwanda wa chini na uwanda wa juu utakuwa hifadhi.Kutokana na uamuzi huo, Rais Magufuli ameiagiza Wizara ya Ujenzi kuanza mara moja ujenzi wa barabara yenye urefu wa kilomita 60 kuanzia Fuga hadi Hifadhi ya Selous kwa kiwango cha lami huku akisisitiza pesa na dhahabu zilizorudishwa baada ya kukamatiwa nchini Kenya kutumika kukamilisha mradi huo. | 3kitaifa
|
WAHITIMU 7,122 wanatarajiwa kutunukiwa vyeti katika mahafali ya tisa ya Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM), hivyo kufanya idadi ya wahitimu katika chuo hicho tangu kuanza kwake kufikia zaidi ya 43,000.Aidha, mahafali hayo pia yatatumika kumuaga Mkuu wa Chuo hicho, Rais mstaafu wa Awamu ya Tatu, Benjamin Mkapa ambaye Machi mwakani atakuwa anamaliza kipindi chake cha kuongoza chuo hicho.Hayo yalielezwa jana jijini hapa na Kaimu Makamu Mkuu wa chuo hicho, Profesa Peter Msoffe ambaye alikuwa akizungumzia mahafali hayo yatakayofanyika kwa siku mbili kuanzia kesho katika ukumbi wa Chimwaga.Alisema kati ya wahitimu hao 69 ni wa cheti, 673 wa Stashahada, 6,125 ni Shahada ya kwanza, 16 wa Stashahada za juu, 220 ni Shahada za Uzamili na 19 wa Shahada za Uzamivu.“Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dodoma, Benjamin William Mkapa atahudhuria mahafali hayo ya siku mbili ambayo pia yatahudhuriwa na Mwenyekiti wa Baraza la Chuo, Gaudentia Kabaka,” alisema.Alisema katika siku ya kesho, yatakuwa ni mahafali ya ndaki tano za Elimu, Sayansi za Ardhi, Afya, Sayansi za Kompyuta, Habari na Mawasiliano na Sayansi Asilia na Hisabati.Profesa Msoffe alisema mahafali ya siku ya Ijumaa yatakuwa ya ndaki mbili za Sanaa, Lugha na Sayansi za Jamii na ile Taaluma za Biashara na Sheria. Aidha, Profesa Msoffe alisema mahafali hayo yatatanguliwa na Mkutano Mkuu wa Jumuiko la wahitimu unaofanyika leo, ambapo mtoa mada mkuu atakuwa Balozi wa India nchini, Sandeep Arya ambaye atawasilisha mada juu ya Maisha ya Mahatma Gandhi na mchango wake kwa jamii.Akizungumzia kumuaga, Kaimu Makamu Mkuu wa chuo hicho, Profesa Msoffe alisema kwa mujibu wa Hati Idhini ya chuo Mkuu wa Chuo, Rais mstaafu Mkapa anamaliza muda ikiwa ameshatumikia vipindi viwili.Akizungumzia mipango ya maendeleo, Profesa Msoffe alisema mpango wa kujenga ndaki zilizobaki, upo kwenye hatua za kutafuta gharama na michoro. Profesa Msoffe alisema kwa upande wa shule ya sekondari, ambayo inafadhiliwa na serikali kwa asilimia 100 iko kwenye ujenzi. Alisisitiza kuendelea na mpango wa upandaji miti katika kuifanya Dodoma kuwa ya kijani.Akizungumzia mafanikio, Profesa Msoffe alisema hospitali ya chuo imepanda hadhi kutoka Kituo cha Afya hadi Hospitali ya Wilaya, hivyo chuo kina mpango wa kujenga majengo mengine zaidi ili kuweza kupanua uwezo wa utoaji wa huduma. Aidha, alisema Chuo na Hospitali ya Benjamini Mkapa wakishirikiana na Madaktari bingwa kutoka Tokushukai Medical Corporation na Tokyo Women’s Medical University ya Japan, wamefanikiwa kupandikiza figo kwa wagonjwa watatu. | 3kitaifa
|
MADIWANI wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) katika Halmashauri ya Wilaya ya Moshi mkoani Kilimanjaro, wameiomba serikali kuingilia kati na kuzuia matumizi ya zaidi ya Sh milioni 104 zinazotarajiwa kununua Ipad za madiwani.Wameomba fedha hizo zisinunue Ipad kama ilivyopangwa na madiwani wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) na badala yake zitumike kukarabati miundombinu ya barabara kwenye vijiji na kata za halmashauri hiyo.Diwani wa Kata ya Okaoni, Moris Makoyi (CCM), alisema fedha hizo zilipangwa zitumike kukarabati barabara baada ya kipindi cha mvua za masika kumalizika, lakini madiwani wa Chadema na Mwenyekiti wa Halmashauri, Michael Kilawila, wameamua zitumike kununua Ipad za madiwani na baadhi ya wataalam.“Hii ni rushwa kwa sababu wanakaribia kumaliza muda wao, vyoo vya wanafunzi mashuleni vimeanguka, zahanati hazina umeme, wakinamama wanashindwa kwenda kujifungua na wagonjwa wanafariki njiani kwa sababu barabara ni mbovu halafu wanataka kununua Ipad,” alisema.Alisema kipaumbele ni wananchi kupata maendeleo badala ya viongozi kujinufaisha wenyewe kwa vitu ambavyo havina msingi na kudai kuwa, mwenyekiti wa halmashauri hiyo amekuwa akipeleka miradi mingi ya maendeleo kwenye kata za Chadema.Diwani wa Kata ya Kahe Mashariki, Kamili Mmbando (CCM), aliomba serikali izuie matumizi ya fedha hizo akisema ni ufisadi ndani ya halmashauri kwani zikinunuliwa Ipad zitatumika zaidi kwa matumizi binafsi.Diwani wa Kilema Kaskazini, Anna Lyimo (CCM), aliwataka madiwani wakumbuke kuwa wamechaguliwa kwa ajili ya kutetea maslahi ya wananchi hivyo hawatakiwi kutumia vibaya fedha za umma bali zitumike kuleta maendeleo kwenye kata.Akijibu hoja za madiwani hao wa CCM, Mwenyekiti wa Halmashauri ya Moshi, Kilawila alisema halmashauri hiyo inaendeshwa bila kuangalia itikadi za vyama na kwamba waliamua kununua Ipad kwa ajili ya kupunguza matumizi ya kutoa nakala kivuli na usafiri wa kusambaza nyaraka za madiwani kwenye kata 32.“Tuliamua kuingia kwenye mfumo wa dijitali kwa sababu madiwani na wataalam wakiwa na Ipad itapunguza gharama za kutumia makaratasi na kutoa nakala kivuli na hatuna sababu za kupinga kwa sababu halmashauri nyingine zimefanya hivyo,” alisema. | 3kitaifa
|
MOGADISHU, SOMALIA DURU za habari nchini Somalia zimeripoti kujiri mlipuko wa bomu Jumapili usiku katika mji wa Baidoa, Kusini mwa nchi hiyo. Kwa mujibu wa ripoti, bomu hilo lililipuka wakati wa sherehe za Idul-Fitr katika mji huo. Aidha duru za habari ziliarifu kwamba katika hujuma hiyo kwa akali watu watano wameuawa na wengine 20 wamejeruhiwa. Hadi sasa hakuna kundi lililotangaza kuhusika na shambulizi hilo, ingawa inadhaniwa kwamba kundi la kigaidi la al-Shabab ndilo lililotekeleza jinai hiyo. Kundi la al-Shabab lenye mfungamano na kundi la kigaidi la Al-Qaedah hadi sasa limehusika na utegaji mabomu na mashambulizi mengi ndani ya Somalia na katika nchi jirani. Aidha kundi hilo limekuwa likifanya juhudi za kuiondoa madarakani serikali ya Somalia kuanzia mwaka 2007. Hata hivyo mwaka 2011 kundi hilo lilitimuliwa kutoka mjini Mogadishu na jeshi la serikali kwa kushirikiana na askari wa Umoja wa Afrika (AMISOM). Pamoja na hayo, bado limeendelea kudhibiti maeneo mengi ya vijijini nchini Somalia. Nchi hiyo ni moja ya nchi masikini zaidi na isiyo na uthabiti duniani. AP | 2kimataifa
|
Na SAFINA SARWATT WAFUGAJI jamii ya Wamaasai mkoani Kilimanjaro, wameshauriwa kupunguza idadi ya mifugo waliyonayo ili kukabiliana na tatizo la uharibifu wa mazingira na migogoro ya ardhi baina yao na wakulima. Kauli hiyo imetolewa na Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro, Anna Mghwira, wakati akizungumza na wananchi wa jamii ya Wamaasai wa Kata ya Mabogini wilayani Moshi Vijijini, katika zoezi la kubadilishana rika kutoka vijana kwenda uzee. Alisema kuna haja ya jamii hiyo kuanza kufuga kisasa na kupunguza idadi ya makundi makubwa ya mifugo ambayo yamekuwa yakiharibu mashamba ya wakulima na kusababisha migogoro ya mara kwa mara. “Kuna haja ya viongozi wa vijiji hivyo kuandaa mpango mkakati wa kusaidia jamii hiyo ya wafugaji kuwa na shughuli mbadala za kuwaingiza kipato pamoja na idadi ndogo ya mifugo kwa kuwa ongezeko la watu limesababisha uhaba wa ardhi,” aliongeza. kwa upande wake Diwani wa kata hiyo, Emmanuel Mzava, alisema wameanza utaratibu wa kutenga maeneo ambayo hayajaendelezwa kwa ajili ya malisho pamoja na kuunda kamati za kudhibiti makundi ya mifugo yanayokaa mbali na kuingizwa kwenye mashamba ya wakulima. Baadhi ya wafugaji walieleza adha kubwa wanayoipata kipindi cha kiangazi kuhama na makundi ya mifugo kwa ajili ya kutafuta malisho katika mikoa jirani. | 3kitaifa
|
KUELEKEA mchezo wa Kombe la Shirikisho unaochezwa leo katika Uwanja wa CCM Kirumba jijini hapa, makocha wa timu za Yanga na Pyramids FC wametambiana.Kocha Mkuu wa timu ya Pyramids FC, Sebastian Desabre amesema anaijua vizuri klabu ya Yanga SC, hivyo timu yake itapambana kuhakikisha inapata ushindi katika mchezo wa leo. Alisema ushindi ni muhimu kwao katika mchezo huo licha ya kuchezea ugenini kwani utawaweka vizuri kwa ajili ya ule wa marudiano utakaofanyika Misri mapema mwezi ujao. Kocha huyo wa zamani wa timu za Asec Mimosas, Club Recretivo de Libolo, JS Saoura na Wydad Athletic Club na timu ya taifa ya Uganda anasema watapambana kutokana na umuhimu wa mchezo huo ili kucheza makundi.Alisema kwa sasa lengo lao ni kuhakikisha wanashinda michezo yao yote miwili dhidi ya Yanga, wa leo wa ugenini na ule wa marudiano utakaofanyika kwao Misri.Alisema anaujua vyema mpira wa Afrika Mashariki hivyo timu yake haitasumbuka bali vijana wake watahakikisha wanaibuka na ushindi tu. Kwa upande wake, Kocha Mkuu wa timu ya Yanga SC, Mwinyi Zahera alisema timu yake imejipanga kuhakikisha inashinda mchezo huo. “Tumerekebisha safu yetu ya ushambuliaji naahidi tutatumia kila nafasi yetu tutakayoipata ili kushinda,” alisema Zahera. Alisema maandalizi yao kiujumla yako vizuri. Katika rekodi ya mchezo nane dhidi ya timu za nchini Misri, klabu ya Yanga haijawahi kushinda katika mechi za marudiano. Yanga imepoteza mara tano dhidi ya Al Ahly, pia imepoteza mara mbili dhidi ya timu ya Zamalek na mara moja dhidi ya Ismailia. Yanga SC itacheza mchezo wake wa marudiano nchini Misri katika jiji la Cairo, Novemba | 5michezo
|
Mwandishi wetu-Dar es Salaam RAIS Dk. John Magufuli amewataka mabalozi wa Tanzania
wanaoiwakilisha nchi maeneo mbalimbali duniani, kuhakikisha wanafanya kazi
ikiwa ni pamoja na kuleta nchini wawekezaji na wakikwamishwa na mtendaji ama
wizara wamweleze. Alisema hayo alipokutana na mabalozi 43 wa Tanzania walio
nchini tangu Agosti 13 walipokuwa wakizungumza Ikulu, Dar es Salaam jana. Taarifa iliyotolewa na Ikulu jana, ilisema pamoja na Rais
kuwaeleza hali ya uchumi wa nchi na maendeleo yanayopelekwa kwa wananchi,
aliwataka kutafuta wawekezaji watakaowekeza katika miradi yenye manufaa hapa
nchini. “Nataka
mabalozi mtuletee miradi ya maendeleo, ifike mahali balozi ujiulize kwa kuwa
kwangu balozi nimepeleka nini nyumbani? Nimewezesha kujengwa kiwanda? Kujengwa
barabara? Kujenga daraja au jengo fulani?” alisema Rais Magufuli. Aliwataka kuhakikisha wanasimamia na kufuatilia kwa
karibu masuala wanayoamini yana manufaa kwa nchi, ikiwemo uwekezaji na
wasikubali kukwamishwa na viongozi ama wizara yoyote. “Nataka muwe ‘very aggressive’,
na ukiona mtu anakukwamisha mimi nipo, niandikieni uone kama hatakwama yeye,
mimi nataka kuona vitu sio maneno maneno,” alisema Rais Magufuli. Katika hatua nyingine, mabalozi hao walimpongeza Rais Magufuli kwa utekelezaji wa miradi ya kimkakati
nchini. Mabalozi hao wametembelea miradi ya ujenzi wa bwawa la
Nyerere litakalozalisha megawati 2,115 katika Mto Rufiji, mradi wa ujenzi wa
reli ya kati kwa kiwango cha kisasa (SGR)
unaoanzia Dar es Salaam hadi Dodoma, jengo la tatu la abiria katika Uwanja wa
Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere na mradi wa ujenzi wa barabara za juu
katika makutano ya barabara ya Morogoro na Sam Nujoma (Ubungo Interchange). Miradi mingine waliyoitembelea ni, mradi wa upanuzi wa Bandari
ya Dar es Salaam, mradi wa usambazaji wa gesi (Taifa Gas), mradi wa udhibiti wa mawasiliano Tanzania na mradi
wa ujenzi wa daraja la Tanzanite (New
Selander Bridge) katika Bahari ya Hindi. Kwa upande wa Zanzibar, wametembelea mradi wa ujenzi wa
jengo la biashara na makazi eneo la Michenzani, mradi wa ujenzi wa jengo la tatu
la abiria katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Sheikh Abeid Amani Karume,
mradi wa ujenzi wa nyumba za kisasa wa Fumba Wilaya ya Magharibi, mradi wa
ujenzi wa Barabara ya Kaskazini – Bububu – Mkokotoni na mradi wa ujenzi wa
bandari ya mafuta na gesi katika eneo la Manga Pwani. Mabalozi hao wameeleza kuwa utekelezaji wa miradi hiyo na
juhudi nyingine kubwa zinazofanywa na Serikali katika nyanja mbalimbali za
huduma za jamii, zimeleta heshima kwa nchi na machoni mwa jumuiya ya kimataifa,
na zimedhihirisha kufikiwa kwa malengo ya Tanzania kuingia katika uchumi wa
kati ifikapo mwaka 2025. | 3kitaifa
|
KIU ya Rais mstaafu Benjamin Mkapa aliyokuwa nayo wakati wa utawala wake ya kutaka utoaji wa elimu bila malipo kwa wanafunzi, kwa angalau ngazi ya elimu ya msingi, imekatwa na Rais John Magufuli ambaye ameanzisha mpango wa elimu ya msingi hadi sekondari bure.Kiu ya Rais Mkapa ya kutaka utolewaji wa elimu ya msingi bure wakati wa utawala wake, imejidhihirisha katika Kitabu chake cha “My Life, My Purpose”, ambako amesema kwake alikuwa akiona kuwa nchi yenye maendeleo ni angalau inayoweza kuwapatia wananchi wake elimu bure, maji na huduma ya afya.Alibainisha kuwa alitoa hoja hiyo akiwa kwenye Mkutano wa Nchi za Jumuiya ya Madola uliofanyika Edinburgh nchini Scotland, ambako aliwaambia kuwa kuna mambo muhimu, ambayo ni ndio ya msingi kusaidia, yakifanyika yanaongeza utu na ubora wa maisha ya watu na watu wanaweza kuonekana kama watu na kuzungumza kama watu.Alisema, “Watu kwenye mkutano huo waliangalia baada ya kusema hayo na nilikuwa ninaongea nikikumbuka kuwa Mwalimu Julius Nyerere alikuwa akisema mara kwa mara kuwa maendeleo ni ya watu, mimi ninapenda dhana ya maendeleo ya nchi kama Cuba ambayo wananchi wake wanapata huduma bora na bure ya elimu, maji na afya na hayo ndio maendeleo, lakini kuona watu wakilala nje tena karibia na Ikulu ya Marekani, sasa Marekani inawezaje kuonekana kuwa ni Taifa kubwa.“Kwa Tanzania nilitaka angalau kwa kuanzia kuona kuwepo kwa elimu bure ya msingi, maji na hata huduma za afya na tunatakiwa kuwekea msisitizo kwenye hayo ndio tuseme kuwa tumeendelea, naona kwa sasa kuna hili na elimu bure linatekelezwa,” alieleza Mkapa.Alipoingia madarakani, Rais Magufuli moja kati ya mambo muhimu aliyoanza nayo ni kuhakikisha elimu bila malipo kuanzia ngazi ya shule ya msingi na sekondari inapatikana.Hatua hiyo imesaidia kuongeza kiwango cha usajili wa wanafunzi wa elimu ya msingi kwa maana ya darasa la kwanza hadi ile ya sekondari, ambapo takribani Sh bilioni 23 hutumika kila mwezi. Kwenye sekta ya afya, nako pia kuna mkakati wa ujenzi wa zahanati kila kata huku huduma za maji nazo zikizidi kuimarishwa, kwa kuboresha bajeti ya maji na kuwabana wakandarasi ili kuhakikisha maji ya uhakika na bora yanapatikana kwa wakati.Pia Mkapa katika kitabu hicho, alisema alikataa mtazamo wa watu kusema Tanzania imeendelea, kwa kutoa mfano wa ongezeko la majengo makubwa mijini, huku akibainisha kuwa alikuwa akitaka kuona kwanza maisha ya watu wa vijijini yanaimarika hasa wananchi wakiwa na maji, huduma za afya na elimu bila malipo.Hata hivyo, Mkapa alipongeza harakati za sasa za uboreshaji wa maisha ya watu wa vijijini, kwa kusema kuwa kwa sasa kuna nyumba nyingi nzuri vijijini na tena zinazovutia.Aidha, tangu aingie madarakani, Rais John Magufuli amehakikisha Wakala wa Umeme Vijijini (REA) unafikisha umeme katika kila kijiji, huku Waziri mwenye dhamana ya umeme, Dk Medard Kalemani akishinda mikoani akikimbizana na wakandarasi wa umeme ili watimize azma hiyo ya rais. Lengo la hatua hiyo ni kuhakikisha unapatikana umeme wa uhakika hadi vijijini, ambao hadi sasa umesambazwa kwa asilimia zaidi ya 60. | 3kitaifa
|
["Arsenal inaongoza Everton na Leicester katika kinyang'anyiro cha usajili wa beki wa Manchester United Chris Smalling, 30, muda wake wa mkopo Roma utakapomalizika. (Mirror)", 'Aston Villa bado inataka kumsaini Pedro mwezi Januari, huku winga huyo wa Uhispania wa miaka, 32, akiwa tayari kuondoka Chelsea. (Telegraph)', 'Juventus imempatia Erling Braut Haaland ofa ya mshahara wa euro milioni tatu sawa na(£2.5m) kwa mwaka baada ya kubaini kuwa mshambuliaji wa miaka 19 wa Red Bull Salzburg ana kipengee cha kuweza kuondoka kwa euro milioni 30 (£25.3m). (Corriere dello Sport - in Italian)', 'Naibu mkufunzi wa Manchester City Mikel Arteta sasa yuko katika orodha ya Arsenal watu watakaomrith Unai Emery baada ya Brendan Rodgers na mchezaji wa zamani wa Patrick Vieira kuonesha ishara ya kujiunga na Leicester na Nice. (Express)', 'Lakini Vieira anasema hhiyo haimaanishi kuwa hajalishwi na hali ilivyo katika uwanja wa Emirates Stadium. (Canal+, via Mail)', 'Na tetesi zinaarifu kuwa Vieira amewaambia marafiki zake kuwa kuchukua kazi ya Arsenal. (Daily Star)', 'Mkufunzi wa zamani wa Bayern Munich Niko Kovac pia anapania nafasi ya kazi Arsenal na anajiandaa kuhudhuria mechi ya ligi ya premia ya Gunners watakapokipiga dhidi ya West Ham siku ya Jumatatu . (Goal)', 'Licha ya tetesi zinazomhusisha na AC Milan, Bologna na Napoli, Zlatan Ibrahimovic, 38, huenda asirejee katika ligi kuu ya Italia maarufu Serie A baada ya kuondoka LA Galaxy, anasema ajenti wake Mino Raiola. (La Gazzetta dello Sport - in Italian)', 'Mkurugenzi wa soka wa AC Milan Frederic Massara anasema klabu yake inamsubiri Ibrahimovic kufanya maamuzi kuhusu hatua yake ya baadae. (Mundo Deportivo - in Spanish)', 'Wamiliki wa Paris St-Germain wanakaribia kupata sehemu ya umiliki wa Leeds ya thamani ya £120m itakayowawezesha kuchukua klabu hiyo ikiwa itafika ligi ya Primia. (Daily Star)', 'West Ham imewasiliana na Middlesbrough kuhusu uwezekano wa kumrudisha kipa wa Jamhuri ya Ireland Darren Randolph, 32, katika klabu hiyo. (90min)', 'Inter Milan inataka kumsajili beki wa kulia kushoto wa Chelsea na Uhispania Marcos Alonso, 28, mwezi Januari. (Calciomercato - in Italian)', 'Real Madrid iko tayari kuwaachilia mshambuliaji wa Colombia James Rodriguez, 28, na winga wa Wales Gareth Bale, 30, kama sehemu ya makubaliano ya kumpata kiungo wa kati wa Manchester United na mchezaji wa kimataifa wa Ufaransa Paul Pogba, 26. (Eldesmarque via Sunday Express)', 'Naibu mkufunzi wa Manchester City Mikel Arteta atalazimika kupitia mchakato mrefu wa mahojiano ikiwa anataka kuwa meneja wa kudumu wa Arsenal. (Sunday Telegraph)', 'Manchester City hawawezi kumsaini Jadon Sancho kutokana na kipengele walichoafikiana kama sehemu ya mkataba uliowawezesha kumuuza kwa klabu hiyo ya Ujerumani. Lakini mabingwa hao wa ligi ya Primia hawatakubali mpango wa kulipa ofa yoyote ya kumpata tena winga huyo. (Sunday Mirror)', 'Mkurugenzi wa michezo wa Borussia Dortmund Michael Zorc anasema mshambuliaji wa England Jadon Sancho, 19, hataondoka klabu hiyo mwezi Januari, licha ya tetesi zinayomhusisha na Manchester United. (Manchester Evening News)', 'Mkufunzi wa Barcelona Ernesto Valverde amedokeza kuwa kiungo wa kati Arturo Vidal huenda akajiunga na Manchester United. (Sunday Mirror)', 'Real Madrid lazima ikusanye £84m katika mauzo ya mwezi Januari ili kufikia sheria ya usawa wa malipo kwa wachezaji. (Sunday Mirror)', 'Rais wa Barcelona Josep Maria Bartomeu anasema kuwa anamtaka mshambuliaji wa Argentina Lionel Messi, 32, asaini kandarasi ya kurefusha muda wake katika klabu hiyo. (Marca)', "Meneja Jose Mourinho anataka kumsaini beki wa Juventus na Uturuki Merih Demiral kujiunga na Tottenham, na tayari ameungana na Arsenal na Manchester United katika kinyang'anyiro cha usajili wa kiungo huyo wa miaka 21-. (Sun)"] | 5michezo
|
NA ADAM MKWEPU, DAR ES SALAAM KLABU ya soka ya Yanga imeanza mipango ya chini kwa chini ya kumwinda mshambuliaji kinda raia wa Ghana, Awudu Zakari, ambaye amemaliza mkataba wake wa kuichezea timu ya Nogoon El- Mstakbal, inayoshiriki Ligi Kuu nchini Misri. Straika huyo mwenye umri wa miaka 20, alijiunga na Nogoon El- Mstakbal Januari mwaka jana, kwa mkataba wa mwaka mmoja na nusu akitokea timu ya Union Doula ya Cameroon, aliyoanza kuichezea tangu mwaka 2013 kama mchezaji wa kulipwa kwa mara ya kwanza. Ili kuhakikisha inampata nyota wa kimataifa mwenye vigezo na sifa zinazokubalika, mabingwa hao watetezi wameanza kuchunguza baadhi ya video za mshambuliaji huyo ili kujiridhisha zaidi na uwezo wake. Akizungumza na MTANZANIA jana kwa njia ya mtandao, Zakari alithibitisha kuwepo kwa mawasiliano kati yake na baadhi ya viongozi wa Yanga na kudai yupo tayari kujiunga na mabingwa hao wa Ligi Kuu Bara msimu uliopita katika dirisha la usajili msimu ujao. “Namuomba Mungu mambo yaende vizuri ili niweze kutimiza ndoto za kuichezea Yanga, kwani sina mpango wa kuongeza mkataba na timu niliyokuwa nikiichezea kutokana na migogoro ya kisiasa ya mara kwa mara nchini Misri,” alisema Zakari. Akizungumzia ushindani wa namba uliopo katika kikosi cha Yanga, Zakari alisema kama dili lake litafanikiwa yupo tayari kupambana ili aweze kucheza kikosi cha kwanza na kuisaidia timu hiyo kwa kuwa ana uwezo na kipaji cha kufanya hivyo. “Siku zote mimi ni mpambanaji, ndiyo maana siogopi kupigana kuhakikisha napata namba ya kucheza, ingawa siwajui wachezaji wote wanaoichezea timu hiyo. “Mchezaji ambaye ninamfahamu vizuri kwenye Ligi Kuu ya Tanzania Bara ni mshambualiaji Hamis Kiiza, raia wa Uganda niliyewahi kupata bahati ya kucheza naye katika timu ya Nogoon El Mstakbal,” alisema. Straika huyo alieleza kuwa bado hajaanza rasmi mazungumzo na uongozi wa Yanga, licha ya kuwepo kwa mawasiliano ya karibu na baadhi viongozi. Ikiwa dili ya mchezaji huyo itafanikiwa kwa msimu ujao, atakuwa ameongeza ushindani katika safu ya ushambuliaji ya timu hiyo ambayo kwa sasa inaongozwa na Amissi Tambwe, Donald Ngoma na Simon Msuva. Tambwe anaongoza katika kinyang’anyiro cha kuwania kiatu cha dhahabu msimu huu ambapo tayari amepachika wavuni mabao 13, huku Ngoma akifunga tisa. | 5michezo
|
Na MWANDISHI WETU- MBEYA KOCHA msaidizi wa timu ya Yanga, Juma Mwambusi, huenda akajiunga na kikosi cha maafande wa Tanzania Prisons kufuatia mabadiliko yanayotarajiwa kufanyika ndani ya benchi la ufundi la Wanajangwani hao. Mwambusi alijiunga na kikosi cha Yanga msimu uliopita akitoka katika klabu ya Mbeya City kurithi mikoba ya Charles Mkwasa ambaye alikabidhiwa majukumu ya kuifundisha timu ya soka ya Taifa ya Tanzania ‘Taifa Stars’. Hata hivyo, jana Mwambusi alisimama katika benchi la ufundi la Yanga wakati ikichuana vikali na Mtibwa Sugar katika mchezo wa Ligi Kuu uliochezwa Uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam. Mabingwa hao watetezi wa Ligi Kuu Tanzania Bara, kwa sasa wapo katika mazungumzo na kocha Mzambia, George Lwandamina ambaye anainoa timu ya Zesco, ili aweze kurithi mikoba ya Hans van der Pluijm raia wa Uholanzi, ambaye inadaiwa atapewa majukumu ya Mkurugenzi wa Ufundi. Inadaiwa kuwa Mwambusi akiondolewa Yanga upo uwezekano mkubwa wa kurejeshwa kwa Mkwasa ambaye alikubalika sana kutokana na ushauri mzuri aliokuwa akiutoa kwa Pluijm. Kwa sasa Prisons inafundishwa na kocha Abdul Mingange baada ya Salum Mayanga, aliyeinoa timu hiyo msimu uliopita kutimkia Mtibwa Sugar. | 5michezo
|
TIMU ya Taifa ya Tanzania, Taifa Stars, leo inatupa karata yake muhimu katika mbio za kusaka nafasi ya kufuzu kucheza fainali za nne za Kombe la Mataifa ya Afrika kwa Wachezaji wa Nyumbani (Chan 2020) itakapocheza dhidi ya Kenya, Harambee Stars.Taifa Stars na Harambee Stars zilitoka sare ya kutofungana bao katika mchezo wa kwanza uliofanyika kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam Jumapili iliyopita na kuifanya Stars kuwa na kibarua kigumu katika mchezo huo wa ugenini ili kusonga mbele. Mchezo huo wa marudiano utafanyika kwenye Uwanja wa Moi Kasarani jijini Nairobi, Kenya na mshindi wa jumla, atapata nafasi ya kucheza raundi ya mwisho ya kufuzu dhidi ya Sudan.Timu yetu ya Taifa Stars inahitaji sare yoyote ya mabao au ushindi wa aina yoyote ili iweze kufuzu kucheza dhidi ya Sudan wakati wenyeji wao Kenya, wenyewe wanahitaji ushindi tu ili wasonge mbele.Pamoja na mlima mrefu uliopo mbele ya Taifa Stars katika mchezo huo wa kesho ugenini, lakini bado timu yetu ina nafasi ya kufanya vizuri na kucheza raundi ya mwisho ya kufuzu dhidi ya Sudan. Lakini hilo litawezekana endapo wachezaji watapambana kwa nguvu zote na kurekebisha makosa mengi ya ufungaji, yalijitokeza katika mchezo wa kwanza kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam. Ni matarajio yetu kuwa Kaimu Kocha Mkuu wa timu hiyo, Etienne Ndayiragije pamoja na benchi lake lote la ufundi, walishabaini makosa yaliyofanywa katika mchezo wa kwanza na watakuwa wameshayarekebisha. Sasa ni jukumu la wachezaji wa Stars kuwapa raha wapenzi wa soka nchini, ambao kwa mara ya mwisho timu yao ilicheza fainali hizo za Chan mwaka 2009 nchini Ivory Coast, ambazo zilikuwa fainali za kwanza tangu kuanzishwa kwake.Shirikisho la Soka Afrika (Caf) lilianzisha mashindano hayo ikiwa na lengo maalum la kutaka kuwatangaza au kuwatumia wachezaji ambao hawajapata timu nje ya nchi zao na wanaendelea kucheza ligi za nyumbani. Timu nyingi za mataifa mbalimbali zimekuwa zikiwatumia wachezaji wanaocheza soka nje ya nchi kwa ajili ya kuunda timu za taifa, ambazo hushiriki mechi mbalimbali za mashindano na hata za kimataifa za kirafiki, hivyo wale wa ndani hawapati fursa hiyo.Pamoja na yote, mchezo wa kesho ni muhimu sana kwa Taifa Stars, hivyo pambaneni ili mshinde licha ya kucheza ugenini. Kila la heri Taifa Stars katika mchezo wenu huo, tuko nyuma yenu tukiwaombea. | 5michezo
|
MUNICH, UJERUMANI KOCHA wa Bayern Munich, Carlo Ancelotti, amedai kuwa ameachiwa kazi nyepesi na aliyekuwa kocha wa timu hiyo, Pep Guardiola ambaye amejiunga na klabu ya Manchester City. Ancelotti amesema kuwa anaamini atafanikiwa katika klabu hiyo ya Bayern Munich kutokana na Guardiola kuweka njia ya mafanikio ya klabu hiyo. Guardiola akiwa katika klabu hiyo ya Bayern, alifanikiwa kutwaa mataji saba katika misimu mitatu ambayo aliitumikia ikiwa pamoja na kutwaa taji la Bundesliga. Ancelotti amedai kuwa anavutiwa na uwezo wa wachezaji hao ambao umeachwa na kocha Guardiola. “Ni kazi nyepesi sana kwa sasa katika klabu hii kwa kuwa nimewakuta wachezaji wakiwa katika ubora wa hali ya juu. “Ninaamini ubora wa timu hii umeachwa na Guardiola, nimeikuta timu hii ikiwa katika ubora wa hali ya juu, hivyo sina kazi kubwa ya kuifundisha timu hii. “Misingi ambayo imeachwa na Guardiola ninaamini siwezi kuiacha au kuibadilisha kwa sasa kwa kuwa ni mizuri na itanipa mafanikio japokuwa nina mipango yangu ambayo ninaweza kuiweka hapa,” alisema Ancelotti. Bayern kwa sasa inashika nafasi ya kwanza katika msimamo wa ligi ikiwa na pointi 16 huku nafasi ya pili ikishikwa na Hertha Berlin ambayo na pointi 13 baada ya timu hizo kucheza michezo sita. “Ninajua kwamba timu yangu inafanya vizuri, nimekuwa nikiiangalia timu hii kwa misimu mitatu iliopita, hivyo kikubwa ni kuendelea na kasi hii kwa ajili ya kuipa mataji,” aliongeza. Kocha huyo mwenye umri wa miaka 57, aliwahi kuzifundisha klabu kubwa duniani kama vile AC Milan, Paris Saint-Germain, Real Madrid pamoja na klabu ya Chelsea.
| 5michezo
|
JUMLA ya Sh milioni tisa zimetolewa kwa Mabaraza ya Vijana matatu ya Mkoa wa kusini Unguja katika mwaka 2017/18 kwa ajili ya kutekeleza miradi ya maendeleo na kiuchumi.Hayo yamesemwa na Naibu Waziri wa Uwezeshaji, Vijana Wanawake na Watoto, Shadya Suleiman wakati akijibu swali la mwakilishi wa jimbo la Tunguu, Simai Mohamed Said.Mwakilishi huyo alitaka kufahamu mabaraza ya vijana yamewezeshwa kwa kiasi gani katika kutekeleza majukumu yake.Suleiman amesema fedha za kuyasaidia mabaraza hayo ya mikoa mbalimbali Unguja na Pemba zipo lakini hakuna mwamko kwa vijana kuomba fedha hizo.Alisema fedha zilizotolewa ni za kikundi cha Machuwi na Kitogani Mkoa wa kusini Unguja wanaojishughulisha na kilimo na ufugaji.Akifafanua zaidi, Suleiman aliwataka viongozi wa majimbo ikiwemo wajumbe wa Baraza la Wawakilishi kuwahamasisha vijana kuchangamkia fursa za fedha kwa ajili ya maendeleo.Nawaomba wabunge na wajumbe wa Baraza la Wawakilishi kuwahamasisha mabaraza ya vijana kuchukua mikopo ya fedha kwa ajili ya kujiendeleza kiuchumi na kujiajiri,'' alisema.Amesema kwamba lengo la Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar (SMZ) ni kuanzisha mabaraza ya vijana ambayo yataibua fursa za kiuchumi na maendeleo kwa ajili ya kuajiajiri.Amesema hakuna ubaguzi wala itikadi za kisiasa katika kuyaendesha na kuyasimamia mabaraza ya vijana kwa sababu yapo kwa ajili ya kuwawezesha vijana kiuchumi. | 1uchumi
|
SERIKALI imeshauriwa kuangalia upya suala la upatikanaji wa umeme wa uhakika vijijini ili kusaidia viwanda kuongeza thamani kwenye mazao ya kilimo na kuchochea uzalishaji zaidi.Ushauri huo umetolewa na Mshauri wa Utafiti, Alphonce Thomas wakati akiwasilisha matokeo ya tathmini ya athari za kiuchumi nchini kutokana na kutopatikana kwa umeme wa uhakika kwenye miradi ya uongezaji thamani ya mazao ya kilimo Mbeya, Iringa, Njombe na Songwe.Alisema miradi mingi ya biashara ya mazao ya kilimo inashindwa kujiendesha kutokana na umeme kwenye viwanda husika kuwa mdogo Alishauri suala umeme vijijini liangaliwe upya.Alisema umeme unaowekwa vijijini unalenga kukidhi matumizi ya nyumbani na si biashara hali inayofanya viwanda vingi vya uongezaji wa thamani ya mazao ya kilimo kutojiendesha.Alisema wafanyabiashara wengi wanaoongeza mnyororo wa thamani wa mazao ya kilimo waliofikiwa na utafiti huo maeneo ya Mpango wa Kuendeleza Kilimo Kusini mwa Tanzania ( SAGCOT), hawakulalamikia bei ya umeme, bali upatikanaji wa uhakika wa nishati hiyo.Alisema wafanyabiashara wadogo na wa kati wanaoongeza thamani mazao ya kilimo walipendekeza kupunguzwa kwa gharama za uunganishwaji umeme, kwani wengi hawakuwa na uwezo wa kulipia baadhi ya gharama hizo.Ofisa Kilimo mkoa wa Njombe, Wilson Joel alisema mwamko ni mkubwa kwa wenye viwanda vya mazao ya kilimo endapo kutakuwa na uhakika wa upatikanaji hali itakayochangia kuleta mageuzi katika sekta ya kilimo.Mshauri wa Kilimo mkoa wa Mbeya, Michael Sanga alisema miradi mingi inakwama kutokana na ukosefu wa nishati ya umeme wa uhakika. “Wengi wamekuwa wakipata hasara umeme unapokatika wakati wa uzalishaji hali inayowatia hasara kubwa hasa watengenezaji wa bidhaa kama tomato sauce,” alisema Sanga.Mtaalamu wa Sera SAGCOT, Prudence Lugendo alisema watakusanya mapendekezo ya wadau na kuyapeleka serikalini ili kutatua changamoto na kuboresha sekta ya kilimo na upatikanaji wa uhakika wa malighafi viwandani. | 3kitaifa
|
Kutokana na leseni hiyo, sasa benki hizo mbili zitakuwa zikijiendesha zenyewe huku wakikabiliwa na changamoto ya mtaji ambapo kwa utafiti wao, wanahitaji Sh bilioni 500 kwa miaka mitano, lakini Serikali imewapatia Sh bilioni 110 hivyo wanashirikiana na wadau mbalimbali kupata fedha hizo.Wakurugenzi watendaji wa benki hizo mbili, Mkurugenzi wa Benki ya Maendeleo, Peter Noni na Mkurugenzi wa Benki ya Biashara, Frank Mugeta, walitangaza rasmi jana katika Maonesho ya 39 ya Kimataifa ya Biashara ya Dar es Salaam yaliyoandaliwa na Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara (TANTRADE) kuwa na benki hizo zinazojitegemea tangu Juni 24, mwaka huu.Akizungumza jana, Noni alisema Serikali imetenga Sh bilioni 30 katika bajeti zake kila mwaka kwa lengo la kuongeza mtaji kwa ajili ya kutoa huduma za maendeleo, ikiwa ni pamoja na kuwekeza katika miundombinu ikiwepo reli na barabara.Alisema wanaishukuru Serikali ya awamu ya nne kwa kufanikisha mchakato huo, ulioanza baada ya kuingia madarakani na wamekamilisha wakiondoka kwa lengo la kuondoa umasikini na kusaidia pato la wananchi kukua toka asilimia saba hadi 15.Alisema benki hiyo inakuwa katika mikopo kwani mwaka jana walitoa Sh bilioni 100 na mwaka huu wanatarajia kutoa mikopo ya Sh bilioni 200.Noni alisema benki hiyo imefanikiwa kuanzisha Benki ya Kilimo ambayo inatarajiwa kuanza hivi karibuni kutoa huduma, ikiwemo mikopo kwa wakulima pamoja na kuwezesha Shirika la Reli Tanzania (TRL) Sh bilioni 12 kwa ajili ya kufufua treni na dola za Marekani milioni 18 kutengeneza vichwa vya treni vilivyochakaa na tayari kazi imeanza.Alisema pia wametoa mkopo wa dola za Marekani milioni 26 kwa ajili ya kuzalisha gesi mkoani Mtwara, kwa Kampuni ya Wentinorth na kutengeneza bomba la gesi kwa ajili ya kusafirisha gesi asilia na kupunguza gharama za umeme.Alisema pia katika kutoa msaada kwa jamii wanashirikiana na Kampuni ya Phils kutoka nchini Dubai, kwa ajili ya uwekezaji kwa kushirikiana na Manispaa za Jiji na wanawekeza Sh bilioni 10 kutengeneza miundombinu. | 1uchumi
|
Na Masyaga Matinyi – Arusha TANZANIA ipo katika hatari ya kupoteza soko la madini ya vito baada ya Kenya kufuta ushuru wote pindi yanapoingia nchini humo. Hatua hiyo ya Kenya imefikiwa katika mkutano maalumu kuhusu sekta ya madini (Kenya Mining Forum) uliofanyika jijini Nairobi, Desemba 4 hadi 5, mwaka huu na kuhudhuriwa na Rais Uhuru Kenyatta, Naibu wake William Ruto na Waziri wa Madini, Dan Kazungu. Katika mpango mkakati uliotangazwa katika mkutano huo ulioshirikisha wajumbe zaidi ya 200 kutoka mataifa mbalimbali, Serikali ya Kenya ilisema inafungua mipaka yake ili kuruhusu madini ya vito kuingia bila vikwazo vyovyote. “Kufungua mipaka ya Kenya kuruhusu madini ya vito kutoka ukanda wa Afrika kuingia Kenya kwa uhuru bila vikwazo,” ilisema sehemu ya mpango mkakati. Pia katika mkutano huo, Serikali ya Kenya ilisema inaunda Shirika la Madini la Taifa huku ikikusudia kulifanya kuwa shirika kubwa la madini barani Afrika. Mbali na kulifanya kuwa shirika kubwa Afrika, pia itahakikisha linasajiliwa katika masoko makubwa ya hisa duniani, ambayo ni New York Stock Exchange (NSE) na London Stock Exchange (LSE), lengo likiwa kupata mitaji ya uwekezaji katika sekta ya madini. Wakati Kenya ikipanga mikakati hiyo yenye lengo la kuifanya kitovu cha biashara ya madini ya vito katika ukanda wa Afrika Mashariki na Kati, Tanzania imekuwa ikitoza ushuru kwa madini kama hayo yanayoingizwa nchini wakati wa maonyesho yanayofanyika jijini Arusha. Madini ya vito yanayoingizwa nchini hutozwa asilimia 18 ya Kodi ya Ongezeko la Thamani (VAT) na asilimia 25 ya ushuru kwa bidhaa zinazoingia nchini (import duty) kutokana na ukubwa wa mzigo. Alipoulizwa kuhusu hatua ambazo Tanzania inachukua au itachukua kukabiliana na changamoto hiyo, Waziri wa Madini, Angela Kairuki, alisema wizara yake ilipeleka mwakilishi katika mkutano huo Nairobi na ripoti inafanyiwa kazi. “Siwezi kuwa na jibu la moja kwa moja sasa, tulituma mwakilishi, hivyo tunasubiri ripoti yake, kisha tutakaa na kuangalia nini cha kufanya kwa masilahi ya taifa,” alisema Kairuki. Kwa upande wake, Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Charles Kichere, alisema ameipokea taarifa hiyo na watakutana na wadau wengine serikalini ili kutafuta mwafaka wa kukabiliana na changamoto hiyo ya kibiashara na uchumi. Kwa habari kamili nunua nakala yako ya MTANZANIA | 3kitaifa
|
WAKATI serikali ikiendelea na ujenzi wa reli ya kisasa kati ya Dar es Salaam na Mwanza yenye urefu wa kilometa 1,219 na pia kukarabati ile ya zamani maarufu kama `Reli ya Kati’, Shirika la Reli Tanzania (TRL), limetangaza kugeukia ujenzi wa reli za mijini, ikianza na Dar es Salaam na Dodoma.Lengo la reli hizo, limetajwa kuwa ni kuondoa msongamano katika maeneo ya mijini, lakini pia kuziunga sehemu zenye shughuli kuu za kiuchumi kama viwanda, ili kuweza kusafirisha bidhaa kwa urahisi.Hayo yamesemwa na Mkurugenzi Mkuu wa TRC, Masanja Kadogosa alipokuwa anazungumzia mikakati mbalimbali ya kuimarisha usafiri wa reli nchini. Alisema kwa Dar es Salaam, mbali ya kuimarisha safari za sasa za ndani ya Dar es Salaam na maeneo jirani kama Pugu, zitajengwa pia reli mpya kati ya Mbezi na Bagamoyo, nyingine itakwenda Mbagala, lakini itakuwepo pia ya kwenda Uwanja wa Ndege.“Mpango huu wa kuwa na mtandao mpana wa reli za mijini unalenga kukabiliana na foleni, hasa ikizingatiwa katika miji na majiji kunakuwa na watu wengi, hivyo kukwamisha katika shughuli zao na foleni.“Ndiyo maana tunaangalia uwezekano wa kuwa na mtandao wa reli, tukianza na Dar es Salaam na Dodoma. Haya mambo yapo katika mipango kwa muda mrefu, ila kwa sasa tunakwenda kutenda. Ni suala la muda tu,” alisema Kadogosa ambaye ofisi yake inajiandaa kufyatua jingo la ghorofa saba eneo la Ihumwa, jirani na mji mkuu wa kiserikali wa Dodoma.Aliongeza kuwa reli hizo zitasaidia pia usafirishaji wa bidhaa kutoka viwandani, kwani zitakuwepo pia zitakazoungwa na viwanda ili kurahisisha usafirishaji wa bidhaa na malighafi. Tayari Dar es Salaam kuna safari za treni za ndani ya jiji, ya Tazara- Pugu-Mwakanga, ya Stesheni ya Dar es Salaam-Pugu na Stesheni ya Dar es Salaam-Ubungo, ambazo zimetajwa kusaidia wakazi wake kutumia muda mfupi wa safari tofauti na mabasi ya abiria.Aidha, kwa kutumia usafiri wa treni, abiria wengi wamekuwa wakisafirishwa kwa wakati mmoja. Mathalani, kwa safari moja, treni kati ya Stesheni-Pugu husafirisha zaidi ya abiria 2,000 kutokana na mabehewa yake kati ya 19 na 23. Behewa moja hubeba abiria kati ya 80 na 120 na safari huchukua kati ya nusu saa na saa moja, wakati kwa safari kama hiyo kwa basi, abiria huweza kutumia hata saa 3-4. | 3kitaifa
|
“Hii ni dalili njema kwa uchumi wa nchi yetu na nchi jirani,” alisema Mkurugenzi wa kampuni inayojishughulisha na huduma za mizigo bandarini, Reindeer Investment Limited, Mlimuka Luhanga.Akizungumza mwishoni mwa wiki, Luhanga alisema juhudi za kuiimarisha Bandari ya Dar es Salaam zinaiweka Tanzania katika nafasi nzuri ya ushindani katika eneo la Afrika na kama kazi hiyo ikifanywa vyema, itakuwa faida kubwa kwa wafanyabiashara wa ndani na nje pamoja na nchi kwa ujumla.Luhanga ameipa changamoto Serikali kuimarisha zaidi usafiri wa reli nchini, kwani utasaidia kwa kiasi kikubwa kusafirisha bidhaa zinazopakuliwa bandarini na kuzisafirisha sehemu husika.“Kwa kutumia barabara tu hatuwezi kufanikisha kusafirisha mizigo yote kwa wakati na vilevile barabara zetu hazitadumu kwa muda mrefu, tunahitaji miundombinu ya reli kwa kuwa itasaidia sana kusafirisha mizigo ndani na nje ya nchi jirani,” alisema Mkurugenzi huyo.Mdau mwingine, Safari Kazimoto ambaye anajishughulisha na shughuli ya uingizaji magari kutoka nje na kuyauza, amesifu maboresho ya huduma ya Bandari na kusema yamerudisha imani kubwa kwa watumiaji wa Bandari ya Dar es Salaam.“Kwa miezi ya karibuni biashara yangu imeimarika kutokana na ufanisi katika Bandari na vilevile msongamano umepungua na kuleta imani kwa watumiaji wa Bandari ya Dar es Salaam,” alisema Kazimoto.Mfanyabiashara kutoka Congo DRC, Pierre Nzwagiba, alisema Bandari ya Dar es Salaam ni kubwa na ina uwezo mkubwa wa kupitisha mizigo mingi na maboresho yaliyofanywa hivi karibuni yataimarisha biashara.“Naipongeza TPA kwa kuchukua hatua za makusudi kuhakikisha imani ya watumiaji wa bandari hii wanarudi na wanaendelea kutumia huduma kama kawaida,” alisema Nzwagiba.Raia huyo wa Congo DRC, ameitaka Serikali kuendelea kuwekeza zaidi katika miundombinu na uboreshaji wa huduma bandarini na kutoridhika na maboresho hayo tu.Katika miaka ya hivi karibuni pamekuwepo mikakati mbalimbali inayofanywa na Serikali kupitia Wizara ya Uchukuzi, TPA pamoja na wadau wengine, kuhakikisha bandari ya Dar es Salaam inatoa huduma bora kwa wateja wa hapa nchini pamoja na wale wa nchi jirani.Kutokana na mikakati hiyo, pamekuwepo na ongezeko la shehena na tija katika kuhudumia shehena na meli zinazotumia bandari hiyo na kupungua kwa msongamano wa meli.Pia kumekuwepo punguzo kubwa la mrundikano wa mizigo na kufanikiwa kukomesha vitendo vya upotevu wa mizigo na wizi kwa kiasi kikubwa.Kwa mfano, kwa upande wa mapato, mwaka 2012/13 wastani wa Sh bilioni 371.7 zilikusanywa, sawa na ongezeko la asilimia 14.3 ukilinganisha na Sh bilioni 325.3 mwaka 2011/12.Katika mapato hayo, bandari bila ya makusanyo ya TICTS, ilikusanya Sh bilioni 324.5 mwaka 2012/13, ikiwa ni ongezeko la asilimia 18.9, ikilinganishwa na mapato ya Sh bilioni 272.9 mwaka 2011/12. | 1uchumi
|
Simba imekuwa na wakati mgumu katika kipindi cha misimu mitatu iliyopita kitu ambacho kimezipa nafasi Yanga na Azam kutawala ligi hiyo na kupata nafasi ya kuiwakilisha Tanzania katika michuano ya kimataifa.Mayanja amesema anaumia kuiona Simba moja ya timu yenye historia kubwa Afrika, ikisotea mafanikio kwa kipindi kirefu na kuiacha Azam ikifanya vizuri na kuwaacha mashabiki wa timu hiyo wakiendelea kusononeka.“Tatizo letu kubwa msimu huu ilikuwa ni kukosa wachezaji wa kimataifa wenye kutambua kazi yao Hamisi Kiiza na Justice Majabvi wanatakiwa kuongezewa wenzao kama ilivyo Yanga na Azam.“Nadhani hapa sasa viongozi wangu wanapaswa kuacha ubahili ili tuingie sokoni kipindi hiki kusaka wachezaji watakaorudisha timu kwenye ubora wake,” alisema Mayanja. Kocha huyo raia wa Uganda, alisema kwa aina ya wachezaji waliokuwa nao msimu huu licha ya vipaji vya kuucheza mpira lakini ni ngumu kupambana na timu kama Yanga au Azam ambazo zina wachezaji wenye uzoefu mkubwa na wanaojua majukumu yao uwanjani.Alisema beki kama Vicent Bossou, amecheza mashindano mengi makubwa na amekutana na wachezaji wenye viwango vya dunia, hivyo siyo rahisi kwa timu hiyo kushindana nayo kutokana na mchanganyiko mzuri waliokuwa nao kati ya wachezaji wa kigeni na wazawa.“Nawapongeza vijana wangu hadi kufika hapa wameonesha juhudi kubwa, lakini ukweli kama tutapenda kuondosha ufalme wa Yanga na Azam, lazima na sisi tuache ubahili tuingie sokoni kusajili wachezaji wenye viwango vya kimataifa, ili tuweze kurudi kwenye mbio za ushindani msimu ujao,” alisema Mayanja.Simba kwa sasa inashika nafasi ya tatu kwenye msimamo wa ligi ikiwa na pointi 57 nyuma ya Azam yenye pointi 58 na Yanga inayoongoza ligi hiyo. Simba leo itacheza na Azam katika mchezo wa ligi hiyo Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam. T | 5michezo
|
SERIKALI imebainisha kuwa inaendelea kumuenzi Baba wa Taifa Mwalimu Julius Nyerere, kwa kuhakikisha fikra na mipango mizuri aliyoiweka inatekelezwa kwa manufaa ya Watanzania wote.Hayo yamebainishwa na viongozi wa serikali awamu ya tano, akiwemo Rais John Magufuli na Rais wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, Dk Ali Mohammed Shein wakizungumza katika maeneo tofauti.Dk Shein amebainisha kwenye Uwanja wa Mkwakwani jijini Tanga kuwa katika kujibidiisha kuleta maendeleo, serikali inatekeleza fikra na mipango ya Baba wa Taifa ndio maana serikali zinahimiza ufanyaji kazi kwa bidii kupitia kalimbiu za ‘Hapa Kazi tu’ na ‘Tusifanye kazi kwa mazoea’.Dk Magufuli akizungumza na mjane wa Baba wa Taifa, Mama Maria Nyerere nyumbani kwake Msasani Jijini Dar es Salaam, alikokwenda kumtembelea jana baada ya kushiriki Ibada ya Misa Takatifu ya Jumapili iliyofanyika Kanisa la Mtakatifu Petro, Oysterbay, amesema Mwalimu Nyerere alifanya kazi kubwa ya kujenga misingi imara ya nchi kuwa na amani, umoja na mshikamano na pia kujenga misingi ya uchumi wa kujitegemea kupitia Azimio la Arusha.Kutokana na mazingira hayo alitoa mwito kwa Watanzania wote hasa vijana kuungana na serikali katika kuyaenzi kwa vitendo yaliyofanywa na Baba wa Taifa, na pia kuliombea Taifa.Mama Maria Nyerere amemshukuru Rais Magufuli kwa kuendelea kumuenzi Baba wa Taifa na amemhakikishia kuwa yeye na wana maombi wenzake pamoja na Watanzania wote wanamuombea yeye, viongozi wote na Taifa kwa ujumla.Aidha, akiwa nyumbani hapo Rais Magufuli aliyeongozana na mkewe Mama Janeth alikutana na mtoto wa Baba wa Taifa, Makongoro Nyerere na wajukuu wa Baba wa Taifa.Misa kanisani Mapema jana asubuhi Rais Magufuli aliungana na Waumini wa Kanisa la Mtakatifu Petro, Oysterbay Jijini Dar es Salaam kusali Misa Takatifu ambapo waumini hao wamemuombea Baba wa Taifa, aliyefariki dunia tarehe 14 Oktoba, 1999.Katika mahubiri yake Paroko Msaidizi, Padre Barthlomeo Bachoo alisema katika uhai wake Baba wa Taifa aliongoza Taifa kwa hekima kubwa, alipenda amani, haki, alipiga vita ukoloni, udini, ukabila, rushwa, uonevu na alikuwa mcha Mungu aliyekuwa akisali katika kanisa hilo.“Tunapomkumbuka Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Kambarage Nyerere kila Mtanzania ana wajibu wa kuliombea Taifa, kuwa balozi wa amani, upendo, umoja na mshikamano na pia tuwaombee viongozi wetu waishi falsafa ya Mwalimu Nyerere, tusimtafute Nyerere makaburini bali tumtafute katika mambo aliyotufundisha,” amesema Padre Bachoo.Baba huyo wa taifa alifariki dunia mwaka huo 1999 katika Hospitali ya St Thomas mjini London baada ya kupambana na kansa ya damu. Na kuzikwa katika kijiji cha Mwitongo, Butiama.Katika historia ya uongozi wake, aliiongoza Tanganyika tangu mwaka 1961 hadi 1964 kama waziri mkuu, kama rais; baada ya muungano wake na Zanzibar, aliongoza Tanzania kuanzia mwaka 1964 hadi mwaka 1985 kama rais.Mwalimu Nyerere ni kati ya viongozi wachache wa Afrika ambao wameacha madaraka kwa hiari baada ya kutawala kwa muda mrefu, akiwa bado anapendwa na wananchi walio wengi.Maneno ya Dk Shein Akizungumza katika shughuli ya kilele cha mbio za mwenge wa Uhuru na Kumbukumbu ya Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere pamoja na wiki ya Vijana Kitaifa, jijini Tanga, Dk Shein alisema kuwa serikali zote mbili zimejizatiti katika kuzisimamia rasilimali ili ziwanufaishe watanzania wote kwa kuwaletea maendeleo.Alisema kumeanzishwa mikakati maalumu ya kuendeleza sekta ya viwanda ili kuongeza fursa za ajira na kuwa na matumizi bora ya rasilimali zilizopo ili kuifanya nchi kuwa na uchumi imara kwa kuleta mapinduzi ya viwanda.Aliongeza kuwa jitihada zinazochukuliwa na serikali zote mbili katika kukabiliana na vitendo vya rushwa na uhujumu wa uchumi ni miongoni mwa jitihada za kuendeleza fikra za Mwalimu.Alisema kuwa pale inaposemwa kwamba zinafuatwa falsafa za Mwalimu, inapaswa kuonesha kwa vitendo kwamba rushwa inachukiwa na watu hawajihusishi na vitendo vya utoaji na upokeaaji rushwa.Matendo makuu ya Nyerere Akieleza jinsi anavyokumbukwa Baba wa Taifa, Rais Dk Shein alisema kuwa atakumbukwa kwa alivyowaunganisha Watanzania kwa kuviongoza na kuvihamasisha vikosi vya ulinzi na usalama kumkabili adui, Idd Amin wakati alipovamia taifa la Tanzania , kumuondoa katika ardhi na kumng’oa madarakani mwaka 1978.“Kwa hivyo kila wakati tunapomkumbuka Mwalimu tuwe tunazingatia umuhimu wa kutoisaliti nchi yetu.... tuyapende na kuyathamini mambo yetu na wala tusiyabeze... Mzee Abeid Karume alituhimiza umuhimu wa kupenda vyetu kwa kusema “Kithamini kilicho chako mpaka usahau cha mwenzako,” alisema Dk Shein.Aidha, Rais Dk Shein alisema kuwa ana amini kwamba endapo kila Mtanzania ataamua kwa dhati wa moyo wake kuyaenzi mambo mazuri ya Mwalimu Nyerere, Tanzania itapata maendeleo makubwa tena kwa haraka sana.Azungumzia Mwenge wa Uhuru Dk Shein alisema kuwa dhamira kubwa ya kukimbiza Mwenge wa Uhuru ni kuendelea kukumbushana misingi na mambo muhimu kwa maendeleo ya nchi sambamba na kutoa fursa ya kukutana na kukumbushana nafasi ya Tanzania mbele ya diplomasia ya Kitaifa.Pamoja na hayo, Rais huyo aliwaonya wale wote wanaojaribu kuupinga Mwenge wa Uhuru na kudai uwekwe kwenye makumbusho, na kubainisha kuwa katu serikali ya awamu ya tano haitaufuta badala yake itaendelea kuutunza kwani ni tunu ya taifa.Aliongeza: " Mwenge ni tunu ya taifa hatuwezi kuufuta tutahakikisha kwa nguvu zetu tunaulinda kwani hii ni tunu ya taifa, tena nasisitiza kama kauli aliyoitoa Rais Magufuli mwaka jana kwenye uwanja wa Amani Zanzibar kuwa tutahakikisha Mwenge wa Uhuru utaendelea kuwepo na viongozi wajao pia tutawarithisha uendelee kuwepo," alisema.Akizungumzia ukombozi wa nchi za bara la Afrika alisema kuwa Tanzania ilishiriki katika ukombozi wa nchi mbalimbali za Afrika kutokana na Juhudi za Mwalimu Julius Nyerere na kujenga umoja wa kitaifa.Waziri mkuu ashusha rungu Naye, Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa ametoa muda wa siku 10 kuanzia jana Jumapili kwa wakuu wa wilaya na wakurugenzi wa halmashauri 14 ambao katika halmashauri zao kuna miradi ya maendeleo ambayo imepitiwa na mbio za Mwenge kugundulika kuwa na kasoro na haina thamani ya viwango vya fedha."Hii miradi ambayo imepitiwa na mwenge wa Uhuru na kubainika kuwa na kasoro nataka kuanzia leo hadi tarehe 25 Oktoba wakuu wa wilaya na wakurugenzi wawe wamefikisha taarifa ofisi ya Rais Tamisemi kwa Waziri ili kujua ni hatua gani walizochukua na kuendelea na miradi hiyo hilo ni agizo" alisema.Aliongeza " Na ile miradi ambayo kiongozi wa mbio za Mwenge ameagiza vyombo vya ulinzi na usalama vichukue hatua,hatua hizo zichukuliwe haraka na ifikapo tarehe 20 ya mwezi huu niipate taarifa ofisini kwangu kwa wale wote waliohusika na ubadhirifu wa miradi hiyo," alisema.Safari ya Mwenge wa Uhuru Awali, Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi,Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Jenista Mhagama alisema kuwa Mwenge wa Uhuru mwaka huu umekimbizwa kwa umbali wa kilometa 28,283.8 katika mikoa 31 na halmashauri 195 katika siku 195.Mwenge huo ulikagua miradi ya maendeleo, kuweka mawe ya msingi, kutembelea miradi iliyopitiwa na mwenge wa mwaka 2017 ambapo jumla ya miradi 1,432 yenye thamani ya fedha shilingi 664,604,079,123.80 imezinduliwa na mingine kuwekewa mawe ya msingi.Kwa upande wa kasoro katika miradi jumla ya miradi 80 yenye thamani ya shilingi 27,503,446,495.66 kwenye halmashauri 64 ilitiliwa shaka na wakimbiza mwenge na haikuzinduliwa wala kuwekewa mawe ya msingi na kumtaka Waziri mwenye dhamana ya serikali za mitaa kuzichukulia hatua halmashauri hizo. | 3kitaifa
|
Na JUDITH NYANGE ASILIMIA 58 ya wanawake wilayani Misungwi wanaamini ni halali kupigwa na waume zao endapo watashindwa kutekeleza masuala mbalimbali ikiwamo kuunguza mboga. Hayo yalielezwa juzi na Mkurugenzi wa Shirika la Kutetea Haki za Wanawake Kivulini, Yassin Ally wakati wa uzinduzi wa awamu ya pili ya programu ya kutokomeza ukatili wa jinsia dhidi ya wanawake na wasichana (GBVII). Alisema walipoanza programu ya GBVI katika kata tano, waligundua kiwango cha ukatili katika Wilaya ya Misungwi kilikuwa asilimia 56 lakini baada ya utekelezaji kilishuka na kufikia asilimia 36. “Kwa mujibu wa tathimini ya taifa ya mwaka 2015/16, asilimia 58 ya wanawake wilayani Misungwi wanasema ni halali kwa mwanaume kumpiga endapo ameunguza mboga, kuondoka bila kuaga na kutotunza watoto hata kama hajapatiwa matumizi,” alisema Ally. Alisema pia katika Wilaya ya Misungwi ilibainika wananchi wengi wananyamaza wanapofanyiwa ukatili. Hata hivyo alisema baada ya utekelezaji wa GBVI wameweza kufichua matukio mbalimbali likiwamo la polisi aliyebaka na kuhukumiwa kifungo cha miaka 30. Naye Waziri wa Mambo ya Nje wa Ireland, Ciaran Cannon, alisema ukatili wa jinsia uwe wa mwili, ubakaji, kujamiana, hisia au uchumi unatambulika uduniani kote na unajulikana kama moja ya ukiukwaji wa haki za wanawake na wasichana. “Nchini Ireland ukatili wa majumbani ni tatizo, mwanamke mmoja kati ya saba ameathirika na ukatili wa mwili, ihisia au uchumi kutoka kwa mwenza wake katika maisha yake. “Kwa Tanzania asilimia 40 ya wanawake wamekumbwa na ukatili wa mwili na mwanamke mmoja kati ya watano ameshapitia unyanyaswaji katika maisha yake,” alisema Cannon. Alisema tatizo la unyanyasaji linasababisha gharama kubwa kwa kwa jamii, familia na nchi kwa ujumla pamoja na upatikanaji wa kipato. Alisema ndiyo sababu serikali ya nchi yake kupitia Mfuko wa Maendeleo wa Ireland imetoa fedha kwa Shirika la Kivulini kwa ajili ya kupinga ukatili wa jinsia. Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, John Mongella, alisema unyanyasaji wa jinsia ni jambo lililopitwa na wakati katika zama hizi na wote wanaoshiriki kuliendeleza ni washamba . “Kwenye jamii zetu bado kuna unyayasaji lakini hili ni jambo lilitopitwa na wakati sana, kama kuna mtu bado anashiriki unyanyasaji wa watoto, wanawake na kama kuna mama anashiriki unyanyasaji wa kina baba ajijue yeye ni mshamba na amepitwa na wakati. “Hakutakiwi kuwe na mama anayemnyanyasa baba wala baba anayemnyanyasa mama wala mtu anayenyanyasa watoto, awe wa kiume au wa kike, hatutegemei mambo haya yaendelee,” alisema Mongella. | 3kitaifa
|
Makubaliano hayo yaliyofikiwa jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki, yametajwa yataiwezesha kampuni hiyo kuanza kufunga mfumo unaojulikana kama ‘Profits’ utakaotumika kwa shughuli mbalimbali za benki hiyo inayotarajiwa kuanza Mei mwakani.Akizungumza kwenye makubaliano hayo, Mwenyekiti wa Bodi ya benki hiyo, Herman Kessy alisema hatua hiyo ni muhimu katika azma ya benki hiyo kufungua milango yake kwa wateja wake. “Huu ni mfumo mzuri na mkubwa utakaoifanya benki yetu kuwa ya kisasa kabisa katika utendaji wake,” aliwaambia waandishi wa habari.Kampuni hiyo imepata kazi hiyo ya kuandaa na kutekeleza mfumo huo baada ya kuibuka mshindi katika zabuni iliyoshindaniwa na kampuni kadhaa za ndani na nje ya nchi.“Wananchi wawe na amani kuwa matayarisho ya benki yao yanakwenda vizuri kabisa,” alisema Mwenyekiti huyo wa benki. Kampuni hiyo inatarajia kuanza kufunga mfumo huo Februari mwakani na kumaliza Septemba.Hadi kufikia Mei, imeelezwa benki itakuwa na uwezo wa kuanza kutoa huduma kwa wateja.Mkurugenzi wa masuala ya Benki na Fedha, Intrasoft International, Andreas Diamanteas alisema makubaliano hayo ni ya muhimu kwa MCB na kampuni yao.Alisema ni muhimu kwa benki kwa kuwa inatakiwa kufungua milango yake kwa wateja hivi karibuni na kwa kampuni hiyo kwa sababu mradi huo unafungua milango kwao nchini kwa kuwa ni wa kwanza kutekelezwa. | 1uchumi
|
Ujumbe wa kampuni hiyo ambayo imewekeza katika kilimo cha kisasa katika mataifa mbalimbali duniani ikiwemo Amerika, Afrika, Ulaya na Asia wamekutana na kufanya mazungumzo na Makamu wa Rais, Samia Suluhu Hassan Ikulu, Dar es Salaam jana.Ujumbe wa wawekezaji hao kutoka Indonesia uliongozwa na Mchugaji Vernon Fernande wa World Agape Ministries, ulimweleza makamu wa Rais kuwa wana nia ya dhati ya kuwekeza Tanzania na wanataka kupata ardhi kubwa kwa ajili ya kilimo cha kisasa kitakachokwenda pamoja na usindikaji wa mazao ili kuondoa tatizo la kusafisha malighafi nje ya nchini.Mchungaji huyo alisema mpaka sasa wameshatembelea maeneo mbalimbali nchini ikiwemo mkoa wa Morogoro lakini wanakutana na changamoto kubwa ya kukosekana kwa eneo la kutosha kwa ajili ya uwekezaji huo.Makamu wa Rais Mama Samia alionesha kufurashishwa na nia ya wawekezaji hao kuja kuwekeza kwenye sekta ya kilimo cha kisasa nchini.Alisema uwekezaji huo ukianza nchini, utatoa fursa ya ajira kwa Watanzania wengi na kuongeza pato la taifa na wawekezaji wenyewe.Aliwaahidi wawekezaji hao kuwa atashughulikia haraka kupatikana kwa eneo la ardhi kwa ajili ya uwekezaji huo ili kazi ya kujenga miundombinu kwenye eneo la uwekezaji ianze mara moja.Alibainisha kuwa Tanzania ina eneo kubwa na zuri kwa ajili ya kilimo hasa kilimo cha umwagiliaji ambalo bado halijaendelezwa hivyo kama wawekezaji wengi watajitokeza kuwekeza kwenye eneo hilo taifa litajitosheleza kwa chakula na kuuza ziada nje ya nchini. | 1uchumi
|
Na MOHAMED KASSARA -DAR ES SALAAM KIKOSI cha timu ya Taifa ya Tanzania ‘Taifa Stars’, leo kitakuwa na kibarua kizito cha kusaka ushindi dhidi ya Benin katika mchezo wa kimataifa wa kalenda ya Shirikisho la Soka la Kimataifa (Fifa). Stars itaingia katika mchezo huo ikiwa na kumbukumbu ya kulazimishwa sare ya bao 1-1 na Malawi katika mchezo kama huo uliochezwa Oktoba 7 kwenye Uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam. Matokeo ya mchezo huo yaliifanya Stars kushuka kwa nafasi tano katika viwango vya ubora vilivyotolewa na Fifa Oktoba, ikitoka nafasi ya 120 hadi 125. Mchezo huo utakuwa wa kwanza wa kirafiki kwa Stars kucheza ugenini, tangu kocha Salum Mayanga alipokabidhiwa jukumu la kuinoa timu hiyo Januari 2, mwaka huu, akirithi mikoba ya mtangulizi wake, Boniface Mkwasa. Mayanga ameiongoza Stars kucheza michezo minne ya kirafiki nyumbani bila kupoteza, dhidi ya timu za Botswana (mara mbili), Burundi na Malawi, akishinda mitatu na kutoka sare moja. Kocha huyo pia ameweka rekodi ya kuiongoza Stars kucheza jumla ya michezo 13 tangu achukue jukumu hilo, akishinda mitano, sare sita, huku akipoteza mmoja dhidi ya Zambia. Stars ilisafiri usiku wa kuamkia Alhamisi kwenda Benin na kikosi cha wachezaji 21. Kuelekea mchezo huo, Mayanga alifanya mabadiliko madogo ndani ya kikosi chake, akiwaacha beki Erasto Nyoni na kiungo Mzamiru Yassin ambao walilimwa kadi nyekundu katika mchezo dhidi ya Malawi na kuwajumuisha na Jonas Mkude na Mudathir Yahya. Katika mchezo huo, Stars itamkosa nahodha wake, Mbwana Samatta ambaye ameshindwa kujiunga na kikosi hicho kutokana na kusumbuliwa na maumivu ya goti aliyoyapata wakati akitumikia klabu yake ya KRC Genk katika mchezo wa Ligi Kuu ya Ubelgiji. Kukosekana kwa Samatta ambaye ndiye kiongozi wa safu ya ushambuliaji, kuna maana jukumu hilo sasa litaongozwa na Simon Msuva anayecheza soka la kulipwa katika klabu ya Diffa El Jadid inayoshiriki Ligi Kuu nchini Morocco. Kwa upande wa Benin, itaingia katika mchezo huo ikiwa na kumbukumbu ya kulazimisha bao 1-1 dhidi ya Congo Brazzaville katika mchezo wao uliopita. Leo Benin itashuka dimbani ikihitaji ushindi ili kulipa kisasi cha kupokea kipigo cha mabao 4-1 kutoka kwa Stars katika mchezo wa kirafiki uliochezwa Oktoba 12, 2014 kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam. Mabao ya Stars siku hiyo yalifungwa na Nadir Haroub ‘Cannavaro’ aliyekuwa nahodha, huku mengine yakiwekwa kambani na Amri Kiemba, Thomas Ulimwengu na Juma Luizio, bao la kufutia machozi la Benin likifungwa na Suanon Fadel. Akizungumza na MTANZANIA jana, Mayanga alisema anaamini wachezaji waliopo kwenye kikosi hicho watajituma na kushinda mchezo huo bila ya uwepo wa Samatta. Mayanga alisema wamepanga kucheza kwa nguvu ili kupata ushindi ambao ndiyo kiu ya Watanzania, lakini pia kumfariji Samatta ambaye ripoti ya daktari wa Genk inadai atakuwa nje ya uwanja kwa wiki sita. “Lazima nikiri kuwa Samatta ni mchezaji muhimu kwenye kikosi changu na kukosekana kwake kuna vitu tutavikosa, lakini nina matumaini ya kupata ushindi kupitia wachezaji waliopo,” alisema Mayanga. | 5michezo
|
Hayo yalisemwa jana jijini hapa na Mkurugenzi Mtendaji wa jiji hili, Juma Idd wakati alipozungumza na waandishi wa habari na kusema kuwa, miundombinu ya soko hilo kwa sasa imechakaa na imefikia mwisho wa uhai wake.Idd alisema, soko hilo halifai kukarabatiwa hivyo hatua iliyopo ni kubomolewa na kujengwa soko jipya litakalokuwa na miundombinu bora kuliko ilivyo sasa.Alisema wanamalizia uboreshaji wa miundombinu ya Soko la Shuma lililopo kata ya Elerai ambalo kuanzia sasa litakuwa likitumika kushushia bidhaa zote zikiwemo matunda, samaki na vitunguu, na wafanyabiashara watakuwa wakitumia magari madogo kubeba bidhaa zao hadi soko la Kilombero.Mkurugenzi huyo alisema, magari yote ya mizigo ya biashara hayaruhusiwi kushusha wala kupakia mizigo ndani ya soko la Kilombero na hayo ni maandalizi ya kulibomoa soko hilo ili lijengwe upya.Akijibu swali la kuondoa harufu ya maji taka na uchafu inayotoka kwenye chemba za kusafirishia maji taka na kusambaa maeneo mbalimbali ya jiji, alisisitiza kuwa hilo ni jukumu la Mamlaka ya Maji Safi na Taka Arusha (AUWSA).Alisema AUWSA inapochelewa kushughulikia uondoaji wa maji taka Halmashauri ya Jiji imekuwa ikiwatoza faini ambayo ni adhabu kwa ajili ya kuwakumbusha wajibu wao.Aliongeza kuwa, AUWSA imekamilisha mchakato wa kupata mkopo wa fedha Sh bilioni 200 kwa ajili ya kukarabati miundombinu yake ikiwemo usafirishaji wa maji taka, kuhamisha mabwawa ya maji taka kutoka eneo la Lemara kuyapeleka Terat kwenye eneo lililotengwa. | 1uchumi
|
Na ELIUD NGONDO-SONGWE ZAIDI ya nyumba 158 za Kijiji cha Mbebe, mkoani hapa, zimeezuliwa na upepo ulioambatana na mvua ya mawe na kusababisha kifo cha mtoto mmoja (6) baada ya kuangukiwa na ukuta wa moja ya nyumba hizo. Tukio hilo lilitokea jana saa nane mchana. Mvua hiyo iliyonyesha kwa zaidi ya dakika 30, pia imesababisha nyumba nyingine kubomoka. Mkurugenzi Mtendaji wa Wilaya ya Ileje, Haji Mnasi, aliwatembelea waathirika hao na kusema kuwa mvua hiyo imeleta janga ambalo wananchi wa kijiji hicho hawakutegemea. Mnasi alisema kaya 53 hazina makazi kabisa ya kuishi na nyingine zinahitaji marekebisho kidogo huku suala la chakula likiwa si kubwa sana. “Serikali itahakikisha wananchi wake wanaendelea kuishi kwenye makazi yao pamoja na taasisi zilizoathirika ambazo ni Shule ya Msingi Mbebe ambayo vyumba viwili vya madarasa vimeezuliwa paa zake na saruji mifuko 15 imeharibika. “Nyingine ni nyumba ya mwalimu wa Shule ya Msingi Mapogolo, ghala la chakula, ofisi ya kata, kituo cha mifugo majengo mawili yameezuliwa mapaa yake, Kanisa la Last Church of God, Kanisa la Moravian na ofisi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM),” alisema. Mwenyekiti wa Kijiji cha Mbebe, Raison Kashililika, alisema pamoja na kifo cha mtoto huyo, kuna majeruhi 21 ambao wawili kati yao walikimbizwa katika Hospitali ya Wilaya ya Ileje na wengine 19, walitibiwa katika Kituo cha Afya Mbebe. Kashililika aliwataja waliopata majeraha makubwa ni Betres Mgode na Sabina Sichinga wakazi wa Mbebe, huku mwili wa mtoto Joshua umezikwa katika Kijiji cha Shinji. Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Ileje, Ubatizo Songa, alisema halmashauri itaendelea kufanya jitihada kuhakikisha wananchi wanarejea katika makazi yao. | 3kitaifa
|
MENEJA Msaidizi wa Mradi wa Reli ya Kisasa (SGR), Christopher Mangwella amewashauri viongozi wa mkoa wa Dodoma kuweka mkakati wa kupanga miji kwa kupima ardhi katika maeneo ambayo zitajengwa stesheni za reli Gulwe, Ihumwa na Kikuyu mkoani humo.Akitoa taarifa ya maendeleo ya ujenzi wa SRG kipande cha Morogoro- Makutupora kwa Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Dk Binilith Mahenge, Mangwella alisema, upangaji wa miji katika maeneo hayo ni muhimu kwani maeneo hayo yatakua kimakazi, kibiashara na kwa shughuli nyingine.Alisema maeneo kama Ihumwa ambapo itajengwa karakana za kukarabati mabehewa na treni, yanatakiwa kupangwa na kubuniwa kwa ajili ya kuanzisha ukanda wa viwanda. Mangwella alisema eneo la Ihumwa ambalo pia lipo mkabala na bandari kavu, inatakiwa kupendekezwa kuanzishwa ukanda wa viwanda ili kuvutia wawekezaji kuwekeza sehemu ambayo malighafi na bidhaa zao zitasafirishwa na kuingia kwenye viwanda vyao.Aliipongeza Serikali ya Awamu ya Tano kwa kuthubutu kuanzisha ujenzi wa reli hiyo ya kisasa nchini, jambo ambalo lilishindikana kufanyika katika awamu nyingine. Aidha, Mangwella alisema, SGR ikikamilika itachochea mipango mingi ya Serikali katika kutekeleza sera ya viwanda na kuifikisha nchi kwenye uchumi wa kati ifikapo 2025.“Reli hiyo itachochea mapinduzi ya kiuchumi kwa kanda nzima ya Afrika Mashariki na Kati hususani nchi ambazo hazina bandari ambazo zitaitumia kusafirisha abiria na bidhaa zao,” alisema.Mangwella alisema kipande cha Morogoro- Makurupora kina urefu wa kilomita 422, ambapo njia kuu ni kilomita 336 na njia ya kupishana ni kilomita 86, alisema mkandarasi yupo kazini na mradi unaendelea kwa kasi.Alisema kipande hicho ambacho mkataba wake ulisaniwa Septemba 29, mwaka juzi na ujenzi wake kuanza Februari 26, mwaka jana, kitakamilika Februari 25, 2021, hivyo ni matarajio yao kipande cha Dar es salaam hadi Makutupora (Singida) kitakamilika Febaruri 2021.Alisema kipande cha Morogoro-Makurupora kinachojengwa na kampuni ya Yapi Merkezi pekee, kitasaidia sana kuinua uchumi na kuboresha maisha ya wananchi wa mikoa ya Morogoro, Dodoma na Singida kutokana na kutoa ajira na fursa nyingine.“Gharama za mradi katika kipande hicho ni Shilingi trilioni 4.4, wakati kipande cha Dar es Salaam hadi Morogoro ni Shilingi trilioni 2.7 na hivyo kufanya gharama za kipande cha Dar es Salaam hadi Makutupora kuwa shilingi trilioni 7.1.” Mangwella alisema kwa sasa mkandarasi ameshakamilisha ujenzi wa makambi katika eneo la Kilosa na Ihumwa, kambi ndogo katika eneo la Mkata na anaendelea na ujenzi wa kambi nyingine katika eneo la Gulwe wilayani Mpwapwa.Alisema kambi kubwa zitakuwa na uwezo wa kutumiwa na watu kati ya 900 hadi 1,000 huku kambi ndogo zikiwa na uwezo wa kuhudumia watu kati ya watu 500 na 600. Akizungumza mara baada ya kupokea taarifa hiyo, Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Dk Mahenge alipongeza kwa juhudi wanazofanya lakini akawataka kuwapa kipaumbele cha ajira wakazi wa maeneo inakopita reli hiyo maadamu wana sifa zinazostahili.Naye Mkuu wa Wilaya ya Mpwapwa, Jabir Shekimweri aliwataka wenyeji wa maeneo hayo inakopita reli kutumia fursa hiyo kuandika barua kuomba kazi na kuanzisha shughuli za kusaidia wanaojenga reli kupata huduma mfano za chakula. | 3kitaifa
|
NYOTA wa klabu ya Montreal Impact, Didier Drogba, juzi aligombana na shabiki wa klabu ya New York Red Bulls, baada ya mchezo wao wa ligi kuu kumalizika. Mshambuliaji huyo raia wa nchini Ivory Coast, alirushiana maneno na shabiki ambaye alikuwa karibu na mlango wa kuingia kwenye vyumba vya kubadilishia nguo, lakini walinzi wa uwanja huo waliweza kuwazuia wawili hao ambao tayari walianza kushikana mikono. Drogba anadai kwamba baada ya kumalizika kwa mchezo huo, kulikuwa na mashabiki wawili ambao walikuwa karibu sana na mlango wa kuingia kwenye vyumba ya kubadilishia nguo, hivyo aliwataka wasogee pembeni ili wachezaji wapite na ndipo vurugu hizo zikaanza. “Kulikuwa na mashabiki wengi, lakini wawili kati ya hao walikuwa karibu sana na mlango na wala sikuwa na nia mbaya ila niliwaomba watupishe ndipo wakaanza kurusha maneno. “Ni mambo ya kawaida kwa mashabiki kufanya mambo kama hayo, hasa pale timu yao inaposhinda au kufungwa,” alisema Drogba. Katika mchezo huo, timu ya Drogba ilipoteza dhidi ya wapinzani wao, New York Red Bulls kwa bao 1-0, hivyo kuwafanya mashabiki wa New York kuwa na furaha kubwa uwanjani hapo. Baadaye Drogba alitumia akaunti yake ya Twitter kuomba radhi kwa mashabiki ambao walijitokeza uwanjani hapo pamoja na wale walioliona tukio hilo kupitia mitandao ya kijamii. Tukio hilo lilitokea muda mfupi baada ya klabu yake ya zamani, Chelsea, kupokea kichapo cha mabao 3-0 dhidi ya Arsenal, hivyo mchezaji huyo alimpongeza mshambuliaji wa Arsenal, Theo Walcott, ambaye alifunga bao moja katika ushindi huo. “Hongera sana kaka Theo Walcott kwa ushindi wenu dhidi ya Chelsea, lakini ninaamini ushindi huo ulikuwa mwepesi kwenu sawa na panya kucheza cheza kama paka hayupo katika eneo hilo,” alisema Drogba. Drogba tangu ajiunge na klabu hiyo mwaka 2015, amefanikiwa kucheza michezo 32 na kufunga mabao 21, huku akitoa pasi 6 za ushindi, akipiga mashuti 134, huku kati ya mashuti hayo, 55 yaliweza kulenga lango, ameoneshwa kadi ya njano mara 5 na kadi nyekundu mara 1. | 5michezo
|
Na Ras Inno, JUMA moja lililopita Shirika la Kutetea Haki za Binadamu Duniani ‘Amnesty International’ lilitoa taarifa iliyotonesha kidonda cha madhila yaliyotokea nchini Nigeria miongo mitatu na nusu na ushei iliyopita, ambayo inawezekana dunia imeshayasau kutokana na kuangazia zaidi migogoro mingine inayofukuta kwa sasa katika maeneo mbalimbali. Serikali ya Nigeria imekanusha vikali yaliyobainishwa katika taarifa hiyo ya Amnesty inayotaja matukio ya mwaka mmoja uliopita lakini ikikumbusha machungu ambayo bado hayajasahaulika kwa walioumizwa. Ripoti hiyo imebainisha kwamba vikosi vya usalama vya Serikali vimewaua watu takribani 150 katika maandamano ya kuunga mkono jimbo lililoko Kusini Mashariki la Biafra linalotaka kujitenga, kwa kuwatwanga risasi waandamanaji wanachama wa kundi la waasilia wa Biafra (IPOB) katika matukio mbalimbali kwa muda wa mwaka mmoja uliopita hadi Agosti mwaka huu. Ni vuguvugu jipya linalozidi kukanganya mustakabali wa utulivu wa Taifa hilo kubwa barani Afrika, kwa kuwa bado halijamaliza matatizo ya Boko Haram Kaskazini Mashariki na sekeseke linaloendelea katika jimbo la Kusini la Delta. Kilichoanzisha hamkani mpya Biafra ni mwendelezo wa manung’uniko ya watu wa kabila la Igbo wanaoishi huko kwa eneo lao kupuuzwa kwa ukosefu wa maendeleo, miundombinu duni ya huduma za kijamii zikiwamo hospitali na shule pia wanasiasa weledi kutoka eneo hilo kutoteuliwa kushika nyadhifa serikalini. Vuguvugu hilo jipya liliibuka baada ya kiongozi wa IPOB, Nnamndi Kanu kutiwa kizuizini aliporejea Nigeria kutoka Uingereza anakoishi na kufunguliwa mashtaka ya uhaini kutokana na kuendesha redio yake jijini London inayodaiwa kuchochea kushambuliwa kwa vikosi vya Serikali. Kinachobainishwa na Amnesty ni kikonyo tu cha kina halisi kilichotokea wakati wa vita ya Biafra iliyorindima kuanzia mwaka 1967 hadi 1970, wakati jimbo hilo lililipojitangazia madaraka kamili na kujipa jina kutokana na ghuba iliyoko Kusini mwake na kujumuisha makabila mengine ya Waefik, Waibibio, Waanang, Waejang, Waeket, Waibeno na Waijaw. Taifa hilo lililojitenga lilisababisha mgawanyiko wa msimamo kwa wanachama wa umoja wa nchi huru za Afrika kwa kutambuliwa rasmi na nchi za Gabon, Tanzania, Ivory Coast na Zambia na nje ya Afrika lilitambuliwa na visiwa vya Haiti na kupata msaada kutoka kwa baadhi ya nchi zikiwamo Israel, Ufaransa, Uhispania na jumuya mbalimbali za kidini. Lakini baada ya mapigano ya miaka miwili na nusu Biafra ilishindwa na kurudishwa upya kwa Nigeria, kutokana na mbinu iliyolaaniwa vikali duniani kote iliyotumiwa na majeshi ya Nigeria kwamba “adui yako msababishie njaa” kwa kulizingira jimbo hilo na kusababisha baa la njaa lililoua wakazi milioni tatu wa eneo hilo. Kimsingi Biafra ilidaiwa kuwapo kabla hata Nigeria haijapata uhuru kutoka kwa wakoloni, kwa jina la ‘Biafara’ ikiunganisha maneno ghuba ‘Bay’ iliyokaliwa na watu wanaotokana na kizazi cha ‘Ephraim’ kwa kujinasibisha na Mto Nun ulioko Kusini mwa Nigeria ambalo ni jina la baba wa Joshua wa kabila la Ephraim anayesimuliwa kwenye Biblia linalomaanisha: ‘Baraka ya Mungu’ kwenye nchi aliyopewa. Kwa kuamini hivyo ubishani uliozaa mkanganyiko huo unasababishwa na mgawanyiko wa kiimani unaoligubika Taifa la Nigeria, ingawa kinachoigusa dunia kutokana na ripoti ya Amnesty hakihusiani na mashiko hayo bali haki za binadamu zinazokandamizwa, hususani ikikumbukwa kuwa Rais wa sasa wa Nigeria Muhammadu Buhari aliyewahi kutawala kijeshi mnamo miaka ya 1980 alikuwa Brigedia Meja aliyeongoza vikosi vya Serikali dhidi ya majeshi ya Biafra katika mapambano hayo, ambapo majeshi hayo yalishutumiwa kwa ukatili mkubwa na ni Buhari huyo huyo aliyetamka mwaka jana kuwa kulikoni kuruhusu vuguvugu la harakati za Biafra kujitenga kuibuka upya na kuligawanya Taifa la Nigeria, ni heri Taifa zima lizame bahari na kuangamia. Ni msimamo unaodhihirisha kuwa mgogoro huo haujamalizika bado kwani mashiko yaliyogawa msimamo wa OAU bado yanazua hisia, hata wakati Mwalimu Nyerere alipotetea msimamo wa Taifa letu kuitambua Biafra alisisitiza kuwa: “Kutokana na imani kwamba kila binadamu duniani anastahili kuwa na mahala anapopaita kwake bila kubughudhiwa, lakini wanachofanyiwa sasa watu wa Biafra ni sawa na Wayahudi walivyofanyiwa na Hitler ingawa wamebahatika kupata nchi waliyokimbilia kujinusuru na kujitangazia uhuru. Kwa muktadha huo tunalazimika kukosoa mgawanyiko wa OAU na kuitambua Biafra kama Taifa kamili ili kutimiza dhima kuwa madhumuni ya jamii na mifumo ya kisiasa ni kuwastawisha wanadamu”. Biafra ni kama pembe la ng’ombe lisilofichika lililoibuliwa upya kwa taarifa ya Amesty International na kukumbusha vuguvugu la mgawanyiko uliojitokeza wakati wa vita ya kujitenga, ingawa nchi nyingi barani Afrika ziliiunga mkono Serikali ya Nigeria iliyoongozwa na Jenerali Yakubu Gowon dhidi ya vikosi vya Biafra vilivyoongozwa na Chukwuemeka Odumegwu Ojukwu lakini zilifanya hivyo kwa kuhofia kufanikiwa kujitenga kwa Biafra kungeamsha hamasa za jamii zilizotaka kujitenga ndani ya mataifa mengine barani hapa. Ingawaje Afrika haijawahi kufanikiwa kuwa na sauti moja dhidi ya migogoro mingi huku mingine ikisababisha mapigano yanayoishia kufanikiwa kujitenga na kuanzishwa taifa jipya, kama ilivyotokea kwa Eritrea iliyopigana na kujitenga kutoka Ethiopia. | 3kitaifa
|
Safina Sarwatt – Moshi HOSPITALI ya Rufaa Kanda ya Kaskazini (KCMC), imesema iko kwenye mchakato wa hatua za kuanzisha maabara ya virusi vya korona ili kukabiliana na vizusi hivyo endapo itabainika kuwepo kwa mgonjwa wa korona. Mkurugenzi wa Mtendaji wa KCMC na Katibu Mkuu wa Shirika la Msamaria Mwema la Tanzania, Professa Gilearrd Masenga aliyesema hayo jana, wakati wa ibada ya shukrani ya maadhimisho miaka 49 tangu kuanzishwa kwa hospitali hiyo kuelekea miaka 50 . Professa Masenga, alisema hospitali tayari imetenga eneo maalumu kwa ajili kujenga maabara ya virusi vya korona. Alisema hospitali imejipanga kwa vifaa tiba pamoja na watalaamu kwa ajili ya dharura, endapo itatokea mgonjwa mwenye virusi vya korona kwa kushirikiana timu ya mkoa. “Tumejipanga kwa vifaa na watalaamu wetu wako tayari muda wote,tunashirikiana na hospitali ya rufaa ya mkoa wa Kilimanjaro, Mawenzi na timu iliyondwa na ofisi ya mkuu wa mkoa, nawaondoa hofu wananchi kwamba tupo vizuri, “alisema professa Masenga. Alisemakutokana na mkoa huo kuwa miongoni mwa mikoa ambayo inapokea wageni wengi kutoka nje ya nchi kwa sababu za utalii wa hifadhi ya Mlima Kilimanjaro, umeimarisha huduma muda wote. Alisema hospitali hiyo, ina madaktari na wauguzi wa ngazi mbalimbali, madaktari bingwa 76 ,madaktari wa kawaida 74 na madaktari wasaidizi wanne na (Clinical officers) 6. Alisema kwa miaka 49, sasa kuelekea jubilee ya miaka 50 ,hospitali imefanikiwa kupiga hatua kubwa katika fani ya kitabibu kwa kanda nzima ya kaskazini pamoja na taifa. “Mafanikio haya yanatokana na jitihada za uongozi na watumishi vitengo mbalimbali ndani ya hospitali ambao wamekuwa uti wa mgongo katika hatua tunazopiga siku baada ya siku, “alisema. Mkuu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), Askofu Dk. Fredrick Shoo aliipongeza hospitali hiyo kwa hatua kubwa waliyopiga katika utoaji wa huduma bora kwa wananchi, ambapo aliwataka kuongeza juhudi zaidi ili kuhakikisha kwamba wanaondoa changamoto ndogo ndogo zinazojitokeza. | 3kitaifa
|
Na MWANDISHI WETU-DAR ES SALAAM MKURUGENZI wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), Ramadhan Kailima, amesema licha ya mgombea wa ubunge David Djumbe wa Singida Kaskazini kujitoa katika kinyang’anyiro hicho, bado wanamtambua ni mgombea halali. Amesema mgombea huyo aliwasilisha barua ya kujitoa juzi, lakini NEC ilimgomea kwa kuwa barua hiyo badala ya kusainiwa na hakimu imesainiwa na wakili. Akizungumza Dar es Salaam jana, Kailima alisema kuwa mgombea huyo amekidhi vigezo kwa mujibu wa sheria. “Ili kuthibitisha kuwa David Djumbe ni mgombea halali wa Chadema, Desemba 19, mwaka huu (juzi), aliwasilisha barua ya kutaka kujitoa katika kinyang’anyiro hicho, lakini tume ilimkatalia kwa kuwa barua aliyowasilisha ilisainiwa na wakili badala ya hakimu,” alisema Kailima. Pamoja na ufafanuzi huo wa Kailima, mgombea huyo pamoja na Chadema bado wamesisitiza kuwa hawatoshiriki uchaguzi huo na barua waliyowasilisha imefuata utaratibu wote unaotakiwa kwa mujibu wa sheria. Wagombea wengine walioteuliwa ni Omari Sombi (AFP), Dalphina Patrick Mlewa (CUF), Monko Justine Joseph (CCM), Aloyce Mohamedi Nduguta (ADA TADEA) na Mchungaji Yohana Samuel Labisu (CCK). “David Djumbe aliwasilisha barua ya utambulisho wa mgombea kutoka Chadema, iliyosainiwa na Katibu wa Chadema Wilaya ya Singida Vijijini, Ndugu Amani Mloya, alipewa fomu ya uteuzi namba 8B ambapo kipengele C kilijazwa na Katibu wa Chadema Wilaya kuonyesha kuwa amedhaminiwa na chama na pia amejaza fomu namba 10 kukiri kufuata na kutii maadili ya uchaguzi mbele ya msimamizi wa uchaguzi wa jimbo hilo,” alisema Kailima. Mbali na hilo, alisema kuwa Chadema waliwasilisha ratiba ya mapendekezo ya kampeni kwa msimamizi wa uchaguzi wa jimbo sambamba na kumteua Shaban Lyimo kuwa mjumbe wa Kamati ya Maadili ambapo juzi alishiriki katika kikao na kupitia ratiba za kampeni za vyama vya siasa vilivyosimamisha wagombea katika jimbo hilo. Kailima amewataka viongozi wa Chadema kusoma vizuri na kufuata sheria za uchaguzi kwani ni haki ya mgombea kujitoa na Sheria ya Taifa ya Uchaguzi sura ya 343 Kifungu cha 48 (1) na (2) kinaelekeza taratibu za kujitoa mgombea ni kuandika barua binafsi ya kujitoa na kuwasilisha hati ya kiapo cha kujitoa iliyosainiwa na hakimu. Kuhusu sababu zinazotajwa na Chadema kujiengua katika kinyang’anyiro hicho kuwa ni hofu juu ya usalama wao, Kailima alisema jukumu la kusimamia usalama lipo chini ya Jeshi la Polisi na si NEC na kuwa madai hayo yawasilishwe Jeshi la Polisi Alisema zipo sababu za kisheria zinazosababisha kuahirishwa uchaguzi, lakini si kwa sababu chama kimoja cha siasa kimeamua kujitoa…… Kwa habari zaidi jipatie nakala yako ya MTANZANIA | 3kitaifa
|
BAADA ya miaka 45 kuwa pamoja, Umoja wa Ulaya (EU) umeikubalia Uingereza isiwe tena mwanachama wa jumuiya hiyo. Wakuu wa nchi na serikali za Umoja huo (Jumapili) huko Brussels, Ubelgiji, waliukubali mkataba wa kujitoa Uingereza kutoka ushirika huo kuanzia Machi 2019. Baada ya mkutano huo wa kilele, Waziri Mkuu wa Uingereza, Theresa May, alisema: “mkataba huo uliokuwa mezani ni bora kabisa kuweza kufikiwa na ulio wa pekee,” Wakuu wa nchi na Serikali 27 zilizobakia ndani ya Umoja huo waliliunga mkono Azimio la Kisiasa kuhusu uhusiano wa baadaye baina ya Umoja wa Ulaya na Uingereza. Mkataba huo wa kujitoa Uingereza umefikiwa baada ya mashauriano magumu baina ya Brussels na London yaliyodumu miezi 17. Licha ya kufikiwa tamati, lakini hisia za pande mbili si changamfu. Kansela Angela Merkel wa Ujerumani alisema: “Hii ni siku ya kihistoria ambayo inatoa hisia tafauti,” Naye Rais wa Tume ya Umoja wa Ulaya, Jean-Claude Junker, alisema hivi kuhusu kujitoa Uingereza: “Huu ni wakati wa huzuni,” Hata hivyo, alisema kwamba licha ya wasiwasi wote uliokuwapo, mkataba huo ndio ulio bora kabisa kuweza kufikiwa. Aliendelea kusema: “Ni wajibu wetu kuhakikisha Uingereza inaweza kujitoa kutoka Umoja wa Ulaya kwa njia ya mpangilio. Hivi sasa tumeweka misingi ya uhusiano wetu wa siku za mbele,” Mshauri wa Umoja wa Ulaya katika mazungumzo ya kufikia mwafaka huu, Michel Barnier, alisisitiza kwa kusema: “Mashauriano kabisa hayajaelekezwa dhidi ya Uingereza. Tutabaki tukifungamana na Uingereza kama washirika na marafiki,” Waziri Mkuu wa Uholanzi, Mark Rutte, alisema: “Hamna yeyote aliyeshinda chochote, sote tumepata hasara,” Mkataba huo unaweka kipindi cha mpito hadi mwisho wa mwaka 2020 ambapo Uingereza itaendelea kubaki ndani ya Soko Moja la Ndani la Ulaya na pia ndani ya Umoja wa Forodha. Pia umeweka utaratibu wa haki za raia wa Ungereza wanaoishi ndani ya nchi za Umoja wa Ulaya na zile za raia wa nchi za Umoja wa Ulaya huko Uingereza. Licha ya hayo, Uingereza itabidi ilipe kiasi fulani cha fedha kutokana na kuipata talaka hiyo. Maafikiano hayo pia yanataja juu ya suala la mpaka wa siku za baadaye baina ya Ireland ya Kaskazini ( ambayo ni sehemu ya Ufalme wa Uingereza) na Jamhuri ya Ireland ( ambayo ni mwanachama wa Umoja wa Ulaya). Lakini hicho kilichokiukwa huko Brussels ni kizingiti kimoja tu. Kuna vingine. Hapo Desemba 10, mwaka huu Bunge la Uingereza litabidi liuidhinishe au liukatae mkataba huu. Hakuna tamaa kubwa kwamba wingi wa wabunge watamfuata Waziri Mkuu May, licha ya yeye mwenyewe kuupigia sana debe. Katika tamko lake kwa taifa ambalo lilichapishwa katika magazeti mengi ya nchi hiyo, alisema: “Ukurasa mpya wa maisha unaanza,” Huko Brussels Theresa May alitaja mafanikio na maslahi iliyoyapata Uingereza kutokana na mkataba huo. Kwanza: Hakutakuwepo uhuru, kama ilivyo ssasa, wa raia wa nchi za Umoja wa Ulaya kuishi na kufanya kazi Uingereza bila ya kupewa vibali. Uingereza itaamua yenyewe kama inataka wahamiaji, pili: Uingereza itakoma kulipa Euro milioni 441 kila wiki katika Mfuko wa Umoja wa Ulaya na badala yake fedha hizo sasa zitatumiwa kwa huduma za afya za nchi hiyo na tatu: Uingereza itakuwa na mamlaka ya juu kabisa kuhusu sheria zitakazotungwa na Bunge lake. Haya ni matakwa yaliyotolewa na Waingereza waliotaka nchi yao ijitoe kutoka Umoja wa Ulaya wakati wa kampeni za Kura ya Maoni ya raia mwaka 2016. Matokeo ya kura hiyo ni kwamba wingi chupuchupu wa wapiga kura walitaka Uingereza iipe mgongo Ulaya. Hivi sasa inakisiwa wabunge kati ya 40-60 wa Chama tawala cha Conservative cha Waziri Mkuu May wataupinga mkataba huo, licha ya kuwepo pia wengine 10 ambao wanahisi ni bora kwa Uingereza kubakia ndani ya Umoja wa Ulaya. Vyama vya Upinzani vya Labour, Liberal Democratic na vile vile vya kizalendo vya Scotland na Wales vimesema wabunge wao wataupinga mkataba huo. Hakijulikani nini kitatokea baina ya sasa na Desemba 10, lakini Umoja wa Ulaya umeweka wazi kwamba mpira sasa uko upande wa Uingereza na kwamba Waingereza wanahitaji watumie busara katika kuucheza mpira huo. Pia Umoja huo umesisitiza kwamba ikiwa Waingereza wanafikiri, pindi wakiukataa mkataba huu wa sasa,watapata ulio bora zaidi hapo baadaye, basi wajue ‘wataula na chuya’ | 2kimataifa
|
Na KULWA MZEE -DAR ES SALAAM
SHAHIDI wa pili katika kesi inayomkabili msanii, Agnes Gerald maarufu Masogange, amedai mahakamani alimpeleka mshtakiwa huyo kwa mkemia na mkojo wake ulikuwa na rangi ya njano iliyopauka. Shahidi huyo ambaye ni Ofisa Mpelelezi, Judith alidai hayo baada ya kuhojiwa na Wakili wa utetezi, Reuben Simwanza, mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Wilbard Mashauri. Alidai alimpeleka Agnes katika ofisi hizo, Februari 15, mwaka hui, kutokana na kutuhumiwa kutumia dawa za kulevya au kusafirisha. Akiongozwa na Wakili wa Serikali, Constatine Kakula, kutoa ushahidi, Judith alidai siku hiyo alikuwepo ofisini akifanya kazi za kawaida, ambapo naibu mkuu wa upelelezi wa kanda hiyo, Ramadhani Kingai, alimwelekeza kumchukua Agnes na kumpeleka kwa mkemia. “Nilimchukua Agnes nikiwa nimeambatana na ofisa wa polisi Sospether hadi kwa mkemia mkuu ambapo tulifika saa saba mchana. “Tulipofika Sospether alienda kujaza fomu huku mimi nikiwa na mtuhumiwa tulienda mapokezi kwa taratibu nyingine. “Nikiwa mapokezi nilikabidhiwa chupa ndogo ya plastiki iliyokuwa na namba 006/2017 na kuelekezwa nimpeleke kwenye choo maalumu kwa ajili ya kutoa sampuli ya mkojo,” alidai. Shahidi huyo alidai aliondoka na mtuhumiwa huyo hadi chooni ambapo aliingia huku yeye akiwa nje na baada ya hapo alitoka na sampuli ya mkojo ambayo alienda kumkabidhi Sospeter. Shahidi huyo alimtambua Agnes mahakamani hapo kwamba ndiye aliyempeleka kwa mkemia mkuu wa Serikali. Akihojiwa maswali na wakili wa utetezi, Reuben Simwanza, shahidi huyo alidai alikabidhiwa mtuhumiwa huyo kumpeleka kwa mkemia na kwamba alitoa mkojo ambao ulikuwa na rangi ya njano iliyopauka. Shauri hilo limepangwa kuendelea na usikilizwaji wa mashahidi wa upande wa Jamhuri Alhamisi. Kabla ya kuendelea na usikilizwaji, mahakama hiyo ilikubali kupokea ripoti ya mkemia mkuu wa Serikali baada ya kufanyiwa uchunguzi sampuli ya mkojo wa Agnes. Uamuzi huo ulitolewa kutokana na mawakili wa mshtakiwa huyo, Nehemia Nkoko na Simwanza, kupinga mahakama kupokea ripoti hiyo iliyokuwa inataka kutolewa na mkemia Elias Mulima ambaye alipima sampuli ya mkojo huo. Baada ya kupokelewa kwa ripoti hiyo, shahidi huyo alihojiwa na wakili Simwanza, ambapo katika ushahidi wake aliieleza mahakama kuwa ana uhakika sampuli ya mkojo aliyoifanyia uchunguzi ilikuwa na Agnes. | 0burudani
|
WANAWAKE wa Kitanzania waliozaa na waliokuwa wapigania Uhuru wa Chama cha African National Congress (ANC) cha Afrika Kusini kambi ya Mazimbu mkoani Morogoro wamewasilisha matatizo yao kwa Rais wa Afrika Kusini, Cyril Ramaphosa alipofanya ziara ya siku moja mkoani Morogoro.Rais Ramaphosa alifanya ziara hiyo Agosti 16, mwaka huu mjini Morogoro eneo la Mazimbu ilipokuwa kambi na kitovu cha Wapigania Uhuru wa ANC wakati wakipigania uhuru wao dhidi ya utawala wa kibaguzi wa makaburu.Kiongozi huyo alimsikiliza binti, Homuto Mathe akisema baba yake alikuwa ni mpigania Uhuru wa ANC na alirudi kwao baada ya kupatikana Uhuru na akamwahidi angerejea kumchukua baada ya kuweka mambo sawa.Rais huyo alimsikiliza kabla ya kuondoka eneo la makaburi ya Wapigania Uhuru wa ANC, walikokuwa wakiishi kambi ya Mazimbu.Kijana huyo kabla ya kuonana na Rais, kwa ujasiri mkubwa aliwasilisha kilio chake na cha wenzake kwa viongozi waandamizi waliokuwa katika msafara wa Rais Ramaphosa dakika chache kabla hajapanda gari kuondoka hapo.Baada ya Rais Ramaphosa kuona kilichokuwa kinaendelea baina ya wasaizidi wake na kijana huyo alielekeza aletwe mbele yake amsikilize.Baada ya kumsikiliza, alielekeza kwa uongozi wa Solomon Mahlangu Freedom College ( SOMAFCO) ushughulikie jambo hilo.Wakizungumza na waandishi wa habari baada ya binti kuwasilisha ujumbe kwa Rais Ramaphosa, wanawake walidai wanachohitaji kwa waume zao ni kuletewa matunzo ya watoto, kujengewa makazi na huduma za afya.Walisema baadhi ya watoto wameshindwa kuendelea na masomo ya juu kutokana na vipato vyao duni ikizingatiwa sasa ni wazee.Monica Mathe ambaye binti yake ndiye aliwasilisha shida zao kwa Rais Ramaphosa alieleza wapigania uhuru hao walizaa watoto na wanawake wengi ambao baada ya wao kurejea kwao watoto hao wameachwa na sasa wakubwa.Monica alisema baadhi yao wanaishi mitaa ya Lukobe na Dark City,Manispaa ya Morogoro wakijishughulisha na kazi ndogo ndogo za kujipatia riziki ingawa baadhi yao wamezeeka.Kijana wa kiume, Mswandile Oscar Mali, wa tatu kuzaliwa kwa baba mpigania uhuru wa ANC, Oscar Mali aliyefariki dunia Machi 4, 1986 na kuzikwa katika makaburi ya Mazimbu alisema familia yao pia inaomba msaada huo.“Sisi tumezaliwa watatu , mmoja tayari alienda Afrika Kusini baada ya kuchukuliwa na ndugu zetu tukabaki wawili ambaye ni mimi na dada yangu na yeye ameolewa. Tupo na mama yetu Mtanzania Magreth ambaye ni mzee,” alisema.Alisema wanaiomba Serikali ya Afrika Kusini kuwasaidia kuwaunganisha na baba zao wapate matunzo kwani hawajapata msaada wowote.Kambi ya Mazimbu ilianzishwa mwaka 1978 mjini Morogoro na yalikuwa ni makazi ya wakimbizi, wapigania uhuru wa ANC wa Afrika Kusini na baadaye ilibadilishwa jina na kuitwa Kampasi ya Solomon Mahlangu. | 3kitaifa
|
KIKOSI cha mabingwa wa soka Tanzania Bara, Simba jana kilifi ka salama mjini Rustenburg, Afrika Kusini kwa ajili ya kambi ya wiki mbili.Msafara wa wachezaji 22 na viongozi wa benchi la ufundi la timu hiyo uliondoka jana asubuhi na ndege ya Shirika la Ndege la Tanzania. Simba ipo kwenye maandalizi ya kuanza msimu mpya wa Ligi Kuu pamoja na michuano ya kimataifa.Ligi Kuu Bara imepangwa kuanza Agosti 23 ambapo Simba itaanza JKT Tanzania, kabla ya mechi hiyo itacheza mechi ya ngao ya hisani dhidi ya mabingwa wa FA, Azam Agosti 17. Akizungumza muda mfupi baada ya kuwasili Rustenburg, meneja wa Simba, Patrick Rweyemamu alisema wamefika salama na kilichobaki ni kuelekeza nguvu kwenye maandalizi ya michuano inayowakabili na wanaamini watakaporudi watakuwa moto wa kuotea mbali.Alisema waliondoka na wachezaji 22, wachezaji wengine wanne wataungana nao kuanzia leo. “Awali ya yote tunamshukuru Mungu leo (jana) tumeondoka na msafara wa wachezaji 22 kwenda Afrika Kusini kwa ndege ya Air Tanzania na wengine watafuata kuanzia kesho (leo) au keshokutwa (kesho) kutokana na walichelewa kuja nchini kwa matatizo ya viza, hivyo watashughulikiwa taratibu waje kuungana na kikosi Afrika Kusini,” alisema Rweyemamu.Alisema kwenye benchi la ufundi linaloongozwa na Kocha Mkuu wa mabingwa hao Patrick Aussems kuna watu sita ambao wapo na kikosi hicho kuhakikisha maandalizi hayo yanakuwa na tija kuelekea kwenye michezo ya ligi na ya kimataifa. Simba itarejea nchini siku moja kabla ya Agosti 8 kwa ajili ya tamasha la Simba Day linalofanyika Agosti 8 ya kila mwaka, ikiwa ni mahsusi kutambulisha wachezaji na jezi zao za msimu kwa wanachama wao. | 3kitaifa
|
Kipa huyo raia wa Ivory Coast ametua kwa klabu hiyo yenye makazi yake Chamazi nje kidogo ya Jiji la Dar es Salaam ili kufanyiwa majaribio kwa nia ya kusajiliwa.Jana, alifanya mazoezi mepesi pamoja na beki raia wa nchi hiyo, Serge Wawa wakati wenzake wakijinoa vilivyo chini ya Kocha Mkuu Stewart Hall.Angban amekuja Azam FC kwa ajili ya kusaini mkataba wa kujiunga na timu hiyo baada ya kuwepo kwa mazungumzo kabla ya kutua nchini.Kipa huyo ambaye ametokea Klabu ya Jeunesse ambayo inashiriki Ligi Kuu ya kwao, aliwasili juzi na wachezaji wengine wawili wa Azam FC raia wa Ivory Coast, beki Serge na mshambuliaji Kipre Tchetche.Akizungumza wakati wa mazoezi hayo, Hall alisema anashukuru ujio wa kipa huyo na kusema kabla ya kusaini itabidi awe amefanya majaribio ili kujiridhisha na kiwango chake.“Ni kweli amekuja Azam ila yupo kwa majaribio endapo atafuzu basi atasaini mkataba ili aanze kutumikia klabu,” alisema Hall aliyerejeshwa kwa mara ya pili kuinoa timu baada ya kufukuzwa kwa Joseph Omog wa Cameroon kabla ya kumalizika kwa msimu uliopita wa Ligi Kuu Bara.Katika mazoezi ya jana, Angban, Wawa na Kipre Tchetche walifan ya mazoezi yao pekee kwa vile walichelewa, ili kutafuta kasi ya kuendana na wenzao ambao walishaanza mazoezi mwezi mmoja uliopita.Azam FC inamchukua kipa huyo kwa lengo la kuimarisha kikosi chake kwa ajili ya michuano ya Afrika, kwani mwakani itacheza Kombe la Shirikisho.Endapo atasaini Azam FC, kipa huyo atakwenda kugombea namba na makipa wa timu ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars, Aishi Manula na Mwadini Ali.Usajili wake ukikamilika, Azam itakuwa na wachezaji wanne kutoka Ivory Coast, akitanguliwa na pacha Kipre Herman Tchetche na Kipre Michael Balou pamoja na Serge.Angban alizaliwa Februari 2, 1985 mjini Anyama, Ivory Coast, na amewahi kudakia timu ya Taifa ya vijana chini ya umri wa miaka 20 ya Ivory Coast katika fainali za Afrika zilizofanyika Benin mwaka 2005 na pia aliiwakilisha nchi yake katika Michezo ya Olimpiki mwaka 2008.Amewahi kudakia timu ya Taifa ya wakubwa ya Ivory Coast ‘Tembo’ katika michuano ya CHAN, ikiwemo ile ya mwaka 2009 ambayo Tanzania ilicheza nao na kushinda bao 1-0 lililofungwa na Mrisho Ngassa, langoni akiwa yeye.Angban aliibukia katika klabu ya vijana ya Rio Sport d’Anyama kabla ya kupandishwa kikosi cha kwanza mwaka 2005, na timu za Sewe Sports, ASEC Mimosas kabla ya kwenda kuchezea timu ya vijana ya Chelsea chini ya U-20. | 5michezo
|
Wafanyabiashara hao ambao awali waliondolewa kufanya biashara zao katika maeneo yasiyoruhusiwa na askari waliokuwa wakisafisha jiji, wameonekana kurudi katika maeneo hayo na kuendelea na shughuli zao.Wakizungumza na gazeti hili, baadhi yao wamedai kuwa maeneo yaliyotengwa kwa ajili ya wafanyabiashara ni machache hivyo yanachukua wafanyabiashara wachache, jambo linalowafanya wao waendelee kutafuta riziki katika maeneo hayo.Mfanyabiashara Said Kudra anayefanya shughuli zake katika eneo la Ilala alisema, kitendo cha wao kuondolewa katika maeneo ya shughuli zao bila kuoneshwa maeneo yanayoruhusiwa si sahihi."Unajua ndugu mwandishi nikuhakikishie tu, kwamba hakuna mtu anayependa usumbufu wa aina hii wa kufukuzwa na kurudi, lakini hii inatokea kwa sababu tunafukuzwa lakini hakuna maeneo tunayoelekezwa twende," alisema Kudra.Alisema hata inapotokea wanaelekezwa maeneo ya kwenda, tayari maeneo hayo yanakuwa yameshajaa na hayana nafasi jambo linalowalazimu wao kurudi walipoondolewa.Naye Ester Julius wa Buguruni alisema kwa kiasi kikubwa baadhi yao wamekuwa wakitegemea maeneo hayo kupata riziki, hivyo serikali ione umuhimu wa kuongeza maeneo zaidi ambayo wanaweza kufanya biashara zao.Aidha, mfanyabiashara mwingine aliyejitambulisha kwa jina la Mama Dora wa Kinondoni Mkwajuni alisema, kikubwa ni serikali iweze kuangalia namna ya kuwasaidia badala ya kuwatimua maeneo hayo na kusababisha mitaji yao kupotea.Alisema baadhi yao wako tayari kuondoka katika maeneo hayo endapo wataelekezwa maeneo sahihi ya kufanyia biashara zao. Ofisa habari wa Manispaa ya Temeke, Joyce Msumba alisema manispaa hiyo inatarajia kujenga soko jipya la kisasa na lenye hadhi ya wilaya ambalo litatumiwa na wafanyabiashara ndogo."Hii iko kwenye mpango wa DMDP (Dar es Salaam Metropolitan Development Project) na tayari utafiti wa awali umeshafanyika na kuangalia linaweza kuchukua watu wa ngapi na ubora wake kwa ujumla," alisema Joyce.Aidha kwa Manispaa ya Kinondoni, wafanyabiashara hao walishatangaziwa masoko wanayotakiwa kwenda kufanya biashara zao.Aidha Ofisa Uhusiano wa Manispaa ya Ilala tabu Shaibu, mapema mwaka huu alisema manispaa hiyo imebaini kuwa wafanyabiashara 21,500 hawana maeneo ya kufanyia biashara jambo linalosababisha wavamie hifadhi za barabara. Alisema manispaa hiyo imerenga Sh milioni 240 kwa ajili ya ujenzi wa mabanda ya masoko ili wafanyabiashara hao waweze kupata sehemu za kufanyia shughuli zao. | 1uchumi
|
TIMU ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars, leo inashuka uwanjani nchini Misri kucheza mechi ya kirafi ki na timu ya taifa ya Zimbabwe kujipima ubavu kabla ya kuanza michuano ya Mataifa ya Afrika (Afcon 2019).Mchezo huo ni wa pili kwa Stars iliyopo katika Kundi C pamoja na timu za Senegal, Algeria na Kenya baada ya Alhamisi iliyopita kucheza na wenyeji wa michuano hiyo Misri na kukubali kipigo cha bao 1-0.Zimbabwe iliyo Kundi A pamoja na timu za Misri, DR Congo pamoja na Uganda, itatupa karata yake ya kwanza katika mchezo wa ufunguzi Juni 21 dhidi ya Misri. Kocha wa Stars, Emmanuel Amunike amepan- ga kukipima kikosi chake kwa mechi mbili kabla ya kuanza kwa mikikimikiki ya Afcon ili kujua uimara na udhaifu wa kikosi chake.Akizungumza hivi karibuni alisema kuwa amechagua kucheza mechi za kirafiki dhidi ya timu hizo ngumu, kwani zinamfanya kujua mapungufu yaliyopo katika kikosi chake. “Tunaweza kujirekebi- sha makosa yetu yaliyopo kabla ya kuanza katika mechi yetu ya kwanza ya Afcon, kucheza na timu ngumu ni chachu kwetu kuweza kupambana na kuonesha kitu tulichonacho,” alisema Amunike. | 5michezo
|
MWANDISHI WETU – MBEYA Wataalamu wa dawa za usingizi katika Hospitali ya
Rufaa ya kanda ya Mbeya wamepewa mafunzo ya matumizi ya dawa hizo ili kupunguza
athari zinazoweza kujitokeza wakati wa utoaji huduma hiyo. Akizungumza wakati wa ufunguzi wa mafunzo hayo ya
siku tatu Mganga Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Dk. Salum Manyata amesema wataalamu hao
wanajukumu kubwa la kuboresha utoaji wa huduma za dawa za usingizi kwa kina
mama wajawazito wakati wa upasuaji. “Ni vema washiriki wakatumia fursa hii walioipata
ya mafunzo ya kujengewa uwezo ili
kutekeleza yale ambayo wameyapata kwa kutoa huduma salama na sahihi kwa
wajawazito. Dk. Manyata amewaasa wataalamu hao kupeleka
mrejesho wa masuala mbalimbali mapya waliyoyapata kwa wengine katika vituo vyao
watakaporejea ili kuhakikisha taratibu zote zinasimamiwa vizuri. Mafunzo hayo yanatolewa na wakufunzi kutoka ndani
na nje ya nchi na kushirikisha wataalam 35 wa dawa za usingizi kutoka Nyanda za
Juu Kusini na kufadhiliwa na Chama cha Madaktari Bingwa wa dawa za usingizi duniani (WFSA) kwa
kushirikiana na Chama cha Madaktari Bingwa
wa dawa za usingiizi Tanzania (SAFE) kwa malengo ya kuwajengea uwezo
watoa huduma ya dawa ya usingizi katika vituo vya afya na hospitali . | 4afya
|
NA MWANDISHI WETU- Pwani WAZIRI wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Dk. Hussein Mwinyi, ameweka jiwe la msingi kwenye mradi wa chuo cha kisasa cha mafunzo ya kijeshi cha Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ). Chuo hicho kitatoa mafunzo maalumu kwa vikundi mbalimbali vya kijeshi ili kuwawezesha kukabilina na ugaidi nchini. Akizungumza jana, Dk. Mwinyi alisema chuo hicho kinachojengwa eneo la Mapinga, Wilaya ya Bagamoyo mkoani Pwani kwa hisani na ufadhili wa Jeshi la Ukombozi la Watu wa China, kitakuwa ishara ya kuimarisha ulinzi na usalama nchini. “Uzinduzi wa eneo hili la mradi wa chuo cha kijeshi umekuja kwa muda mwafaka kwani chuo hiki kitatoa mafunzo ya kisasa ya namna ya kukabilina na ugaidi pamoja na wahalifu hapa nchini,” alisema Dk. Mwinyi. Aliongeza kuwa mafunzo hayo yatawapa uwezo wanajeshi kupambana na wahalifu na ugaidi kwani vita vya sasa vimebadilika, ni tofauti na zamani. Kwa upande wake, Mkuu wa Majeshi, Jenerali Davis Mwamunyange, alisema chuo hicho kitagharimu dola za Marekani milioni 29 na kitakamilika ndani ya mwaka mmoja. Alisema chuo hicho kitatoa mafunzo kwa vikundi mbalimbali vya kijeshi na kitatoa mbinu mbalimbali za kisasa, namna ya kukabilina na ugaidi. Mwamunyange alisema mafunzo hayo yatatolewa kwa utaratibu wa vikundi mbalimbali ili kufundishwa mbinu mpya za kijeshi kwa kushirikina na Jeshi la Ukombozi la Watu wa China. Naye Balozi wa China nchini, Lu Youging, alisema Tanzania na China wamekuwa na ushirikiano mzuri kibiashara na kwenye masuala mbalimbali ya kijamii. Alisema mradi huo wa chuo unajengwa na Kampuni ya China ya Avic International ambayo inajengwa kwa viwango vya hali ya juu hadi ukamilike. | 3kitaifa
|
VINARA wa Ligi Kuu Tanzania Bara, Yanga jana waliendeleza wimbi la ushindi baada ya kuwafunga Azam bao 1-0 katika mchezo uliochezwa Uwanja wa Uhuru Dar es Salaam na kuzidi kunogesha mbio za ubingwa msimu huu.Mchezo huo ni wa kiporo na ulitakiwa kuchezwa mwaka jana, lakini haukuchezwa baada ya ratiba yake kuingiliana na michuano ya Kombe la Mapinduzi.Katika mchezo huo uliokuwa na ushindani kwa muda wote, hasa ufundi sehemu ya kiungo, ulishuhudiwa Yanga wakipata bao hilo pekee katika dakika ya 13 lililofungwa na Mrisho Ngassa.Ushindi huo umewafanya Yanga kuendelea kutamalaki kileleni kwa kufikisha pointi 77 baada ya kucheza michezo 32, ikiwa ni sawa na Azam wanaoshika nafasi ya tatu kwa pointi 66.Huku Simba anayetarajiwa kucheza jioni ya leo katika uwanja huohuo, ina pointi 69 ikishika nafasi ya pili ikiwa nyuma kwa michezo ikilinganishwa na wawili hao wanaowania mbio hizo za ubingwa.Feisal Salum alizawadiwa kadi ya njano baada ya kumchezea vibaya Joseph Mahundi wakati wanawania mpira wa juu.Mchezo huo ulilazimika kusimama mara kwa mara kupisha mlinda mlango wa Yanga, Klaus Kindoki aliyeonekana kuumia mara kwa mara baada ya kupangua michomo mikali ya wapinzani wao kufuatia mikikimiki iliyoelekezwa langoni mwake.Yanga walilazimika kufanya mabadiliko mapema yasiyokuwa ya kiufundi baada ya kutolewa Michael Gadiel aliyeumia kwa kugongana na mlinzi wa Azam na nafasi yake kuchukuliwa na Jaffary Mohamed.Katika mchezo huo, Azam walionekana kutawala zaidi mchezo huo hasa sehemu ya kiungo na kufanya mashambulizi ya mara kwa mara kupitia winga wao wa pembeni, lakini walishindwa kupata bao.Licha ya kuwatumia pia wachezaji wake waliowahi kuichezea Yanga, Obrey Chirwa na Donald Ngoma, Azam walishindwa kabisa kupata bao na kujikuta wakipoteza pointi zote tatu. | 5michezo
|
WILAYA ya Kongwa mkoani Dodoma imeanza mkakati wa kuongeza uzalishaji wa zao la alizeti katika msimu wa kilimo wa mwaka 2018/19.Mwenyekiti wa Baraza la Biashara wilayani humo, ambaye ni Mkuu wa Wilaya, Deogratias Ndejembi amesema hayo katika kikao cha baraza hilo.Ameongeza kuwa mkakati huo, utahusisha mnyororo wote wa thamani wa zao hilo, wakiwemo wazalishaji wa mbegu, wakulima, wenye viwanda vya kukamua mafuta ya alizeti na wanunuzi wa mashudu."Kitaitishwa kikao cha pamoja cha wadau wote ili kutanua uwigo wa mawazo kuona ni namna gani tunaongeza na kuboresha uzalishaji wa alizeti, " alisema Ndejembi.Takwimu inaonesha kuwa viwanda vyote vya alizeti wilaya ya Kongwa ni 99, lakini bado kuna uhaba wa mafuta, hali hii inaonesha kuwa bado wadau hawajajua juu ya kiwango cha mahitaji ya wateja wao,” alisema.Sebastian Msola ambaye ni mmoja wa wajumbe wa Baraza hilo kupitia Sekta ya Kilimo alisema mahitaji ya alizeti bado ni makubwa kuliko uzalishaji. Alisema kwa mwaka alizeti inayopatikana kwa mahitaji ya viwandani ni asilimia 30 tu, yaani wasindikaji husindika kwa miezi mitano tu na miezi mingine saba hukaa bila kufanya shughuli yoyote.Ofisa Kilimo wilayani humo, Jackson Shija ambaye ni mjumbe kupitia Sekta ya Umma alisema bado mbegu bora ni changamoto kwa wakulima wa zao hilo.Changamoto nyingine ni kilimo kisichokuwa cha kitaalamu, uvunaji mbaya na uhifadhi.Shija alisema ipo haja ya baadhi ya viwanda, kupewa elimu juu ya kuvitunza kwani baadhi ni vichafu. Baraza hilo lilijadili mambo mbalimbali, ikiwemo utozaji wa tozo za mazao ya bustani kama miwa, vitunguu, nyanya na kabichi, tozo za karanga zilizobanguliwa.Shija alisisitiza kuwa gharama za tozo, ziendane na thamani ya mazao na si ujazo au uzito.Ndejembi ameunda kikosi kazi shirikishi, kikijumuisha wajumbe wa sekta ya umma, sekta binafsi na madiwani kwa kusaidiana na Mtendaji wa Baraza hilo, Luig Mbuya. Kikosi kazi hicho kitatafiti kitaalamu namna ya kutoza ushuru rafiki kwenye vyombo vya usafiri, ikiwemo mikokoteni ya wanyama, magari aina za pickup canter na fuso.Mwakilishi wa Mradi Unaosaidia Kuboresha Mazingira ya Biashara LIC (Local Investiment Climate), Donald Liya alilishauri baraza hilo kuwa lifanye utafiti za kitaalamu za uzalishaji, unaoendana na upatikanaji wa masoko. | 1uchumi
|
SEKRETARIETI ya Maadili ya Viongozi wa Umma imesema sio viongozi wote nchini ni waaminifu, kwani hata katika jedwali la wenza katika fomu ya matamko ya mali zao, hawalijazi.Aidha, imesema viongozi wengine hawataki taarifa zao za mali kupelekwa kwa wenza wao, jambo linaloonesha kuwa kuna tatizo kutoka ndani kwa viongozi hao. Kamishna wa Sekretarieti hiyo, Jaji mstaafu Harold Nsekela alisema hayo jijini Dar es Salaam jana na kuwahimiza viongozi hao, kupeleka haraka taarifa zao kwa kuwa Desemba 31 ndio mwisho.Kuhusu kama taarifa za matamko zinazopelekwa na viongozi hao ni za kweli, Jaji Nsekela alisema kuna tatizo katika eneo hilo, na viongozi sio wote waaminifu. “Kwa mfano lile tamko kuna sehemu ya wenza wengine hawajazi, kuna wengine na hili tumelikuta tulipoenda kuhakiki, mtu na mwenza wake lakini wanaelekeza kuwa tarifa hizi usimwambie mwenzangu,” alisema Jaji Nsekela na kufafanua kuwa maana yake toka ndani kuna tatizo.Alisema maeneo mengine hawezi kusema kwa kuwa mengine ni ya siri. Kuhusu muda wa kurejesha taarifa zao, alisema inatakiwa hadi kufikia Desemba 31 kuwa tayari wamewasilisha matamko yao kwenye Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma.Aliwahimiza viongozi hao kurejesha matamko yao kwa sasa kwa kuwa ni tamko la mwaka, na viongozi wengi wana tabia ya kungojea tarehe za 25 ama 26 ndio hurejesha. Jaji Nsekela alisema matamko ya viongozi hao huainisha katika fomu hiyo na baadae ukaguzi wa mali hizo, uliofanywa na sekretarieti hiyo kwa lengo la kuhakiki kilichojazwa katika fomu hizo. Alisema baada ya kurejesha matamko hayo, huwatembelea viongozi mbalimbali kwa lengo la kujiridhisha na kile walichokijaza katika fomu zao. | 3kitaifa
|
LIGI Kuu ya soka ya wanawake inatarajiwa kuendelea leo baada ya kusimama kwa mwezi mmoja kupisha michuano ya kombe la Chalenji iliyofanyika nchini mwezi uliopita. Ligi hiyo ambayo inaingia katika mzunguko wa tatu leo itachezwa michezo sita katika viwanja vya miji tofauti.Bingwa mtetezi JKT Queens itacheza na Simba Queens kwenye Uwanja wa Meja Jenerali Isamuhyo, Mbweni Dar es Salaam. Mchezo huo unatarajiwa kuwa na upinzani kwani Simba Queens itahitaji kufuta uteja kwa JKT Queens kwa sababu katika michezo minne waliyokutana tangu msimu wa mwaka 2017 hadi 2018 Simba Queens imefungwa mechi zote.JKT Queens inaongoza msimamo ikiwa na pointi sita walizopata katika mechi za ugenini wakati Simba Queens ina pointi nne ilizozipata katika uwanja wake wa nyumbani, Karume. Endapo Simba Queens itashinda mechi hiyo itakuwa timu ya pili kuifunga JKT kwani Mlandizi Queens iliwahi kufanya hivyo msimu wa mwaka 2016/2017 walipotwaa ubingwa ligi ilipoanza lakini kama JKT Queens haitafungwa itaendeleza rekodi ya kutofungwa kwa msimu wa tatu.Mchezo mwingine utazikutanisha Yanga Princess ambayo itaialika Mlandizi Queens katika Uwanja wa Karume, Dar es Salaam. Yanga Princess msimu huu imeanza vyema kwa kushinda mechi zote mbili ilizocheza na kujikusanyia pointi sita huku Mlandizi Queens ikiwa na pointi tatu baada ya kucheza michezo miwili ikiifunga Panama Queens na kufungwa na Ruvuma Queens katika uwanja wa nyumbani Mabatini, Pwani.Mji wa Songea utakuwa unaandika historia kwa mara ya kwanza tangu Ligi Kuu ya wanawake Tanzania Bara ianzishwe msimu wa mwaka 2016/2017 kwani hawakuwa na timu ya wanawake lakini safari hii Ruvuma Queens itamenyana na TSC Queens katika Uwanja wa Majimaji Ruvuma Queens yenye pointi nne, mechi za mwanzo mbili ilicheza ugenini hivyo haijawahi kutumia uwanja huo kwa mechi za Ligi Kuu zaidi ya zile za kirafiki.Mchezo huo unatarajiwa kuwa mgumu kwasababu timu zote zimepanda daraja msimu huu lakini Ruvuma Queens inaonekana kuwa vizuri zaidi kutokana na kuwa na wachezaji wazoefu zaidi kwenye ligi ukilinganisha na TSC Queens yenye pointi tatu.Panama Queens ya Iringa ambayo haina pointi itaialika Alliance Girls ya Mwanza yenye pointi sita katika Uwanja wa Samora Iringa, Sisterz ya Kigoma yenye pointi tatu itacheza na vibonde Tanzanite Queens ambayo inashika mkia katika msimamo kwenye Uwanja wa Lake Tanganyika, Kigoma.Marsh Queens ya Mwanza itacheza na Baobab Queens ya Dodoma katika Uwanja wa Nyamagana, Mwanza, mchezo ambao unatarajiwa kuwa na ushindani kwani hakuna timu iliyoshinda mchezo wake katika ligi ya msimu huu.Katika kuwania kiatu cha ufungaji bora Fatuma Mustafa wa JKT Queens ana mabao sita akifuatiwa mchezaji mwenzake wa JKT Asha Rashid mwenye mabao matano na Mwapewa Mtumwa wa Yanga Princess ana mabao manne.Mwanahamisi Omar wa Simba Queens ana mabao mawili sawa na Philomena Daniel na Jamila Hassan wa Mlandizi Queens na Janeth Matulanga wa Alliance Girls. | 5michezo
|
WAKAZI wa Kijiji cha Kitandi, Wilaya ya Ruangwa, mkoani Lindi wamemuomba Mkuu wa Wilaya hiyo kupiga marufuku utolewaji wa dawa za uzazi wa mpango kwa wanafunzi wa shule za msingi na sekondari wilayani humo.Wakitoa maoni yao kwenye mdahalo wa kijiji ulioendeshwa na Chama cha Waandishi wa Habari Wanawake Tanzania (Tamwa) katika Uwanja wa Shule ya Msingi Kitandi kuhusiana na mila na desturi zinazosababisha madhara katika jamii, wakazi hao walionesha kukerwa na utolewaji wa dawa hizo.Mkazi wa kijiji hicho, Rashidi Mang’omba alimuomba mkuu huyo wa wilaya kuwafuatilia wazazi ambao wamegeuka chanzo cha utolewaji wa dawa hizo kwa watoto na kuongeza kuwa wakati jamii inawalalamikia watoa huduma za afya, imebainika kuwa kuna wazazi ambao wanashirikiana na wauguzi kuwawawekea vipandikizi mwanafunzi hao. “Wapo wazazi ambao wao ndio huwapeleka watoto kuwekewa vipandikizi hivyo na hiyo sio sawa kwa kuwa wanachochea watoto hao kujiingiza kwenye ngono mapema kwa kuwa wanakuwa hawana hofu ya kupata mimba,” alisema.Khalidi Silikali ameiomba serikali ya kijiji kuwachukulia hatua kali wazazi wanaokubali kumaliza kesi za mimba na unyanyasaji wa kijinsia kwa watoto na wanawake baina ya familia ya mtenda kosa na ile ya aliyetendewa kosa. “Huku kwetu hili jambo limekithiri sana kesi nyingi zimekuwa zinaishia majumbani jambo ambalo linapelekea kuongezeka kwa vitendo vya watoto kuacha shule na kuongezeka kwa mimba za utotoni,” alisema. | 3kitaifa
|
['Wachezaji wa Barcelona wako tayari kuchelewa kulipwa mshahara ikiwa hatua hiyo itasaidia klabu klabu hiyo kumsajili tena mshambuliaji wa kimataifa wa Brazil Neymar msimu wa joto, anasema beki, Gerard Pique.', "Barcelona ilifanya kila ''liwezekanalo katika uwezo wake'' kumsajili nyota huyo wa kimataifa lakini juhudi hizo ziligonga mwamba.", 'Neymar aliondoka Barcelona na kujiunga na Paris St-Germain kwa ada ya kuvunja rekodi duniani ya euro milioni 222 sawa na (£200m) mwaka 2017.', 'Pique alisema wachezaji wenzake waliiambia klabu hiyo kuwa wako tayari kuchelewa kulipwa mshahara ili kuisadia kufikia kanuni ya klabu ya malipo sawa ya wachezaji.', '"Tuko tayari kandarasi zetu zifanyiwe marekebisho," Pique alikimbia kituo cha radio cha Cadena Ser cha Uhispania.', '"Hutuna mpango wa kuchanga pesa, lakini tutarahisisha mambo kwa kuruhusu baadhi ya malipo kutekelezwa katika mwaka wa pili au watatu badala ya mwaka wa kwanza."', 'Barcelona ilitumia zaidi ya £200m msimu wa joto, katika usajili wa wachezaji kama Frenkie de Jong, kiungo wa kati kutoka Ajax na Antoine Griezmann kutoka Atletico Madrid.', 'Kanuni ya malipo sawa ya wachezaji, ambayo inazuia vilabu kutumia fedha kuliko uwezo wao, inasadikiwa kuwa moja ya suala ambalo Barcelona inatakiwa kushughulikia kabla ya kumsaini Neymar.'] | 5michezo
|
Mchezo huo unatarajia kuonyesha taswira ya bingwa wa msimu huu lakini pia, kuna uwezekano mkubwa wa Toto Africans kushuka daraja kama watakubali kipigo. Licha ya timu hizo kuhusishwa kuwa na mahusiano ya karibu, huenda ukawa ni mchezo mgumu kwa kila mmoja. Yanga inataka ushindi ili kujihakikishia nafasi ya kuwa bingwa na Toto inataka ushindi kujinusuru katika hatari ya kushuka daraja. Yanga iwapo itashinda mchezo huo itafikisha pointi 68, pointi ambazo kama Simba itashinda mechi yake ya mwisho dhidi ya Mwadui itazikisha, lakini Yanga ikiwa na silaha ya mechi yake ya mwisho dhidi ya Mbao.Hivyo Simba inatakiwa kuomba mambo mawili kwa wakati mmoja, Yanga ifungwe na Mbao na yenyewe iifunge Mwadui mabao mengi ili kuipiku Yanga kama ikibidi bingwa aamuliwe kwa wingi wa mabao. Kupoteza mechi ya leo kwa Toto iliyo nafasi ya pili kutoka mkiani, kunaashiria kuungana kwake na JKT Ruvu kushuka daraja. Mchezo wa mwisho wa Yanga dhidi ya Mbao FC unatabiriwa kuwa mgumu kutokana na timu hiyo ngeni msimu huu kuwaondosha wakongwe hao kwenye kombe la FA. Kocha Msaidizi wa Yanga Juma Mwambusi amesema hawawezi kuidharau Toto Africans, wataingia kwa tahadhari kusaka pointi tatu.Alisema mchezo huo utakuwa mgumu kwani Toto wanaweza kucheza vizuri ili kutafuta matokeo ya kujinusuru kwenye hatari ya kushuka daraja na wao wanahitaji kutetea taji lao hivyo, ni muhimu kwao kupambana. “Kikubwa tumejiandaa vizuri kuhakikisha kesho (leo), Mungu anatusaidia na kuondoka na pointi tatu. Toto ni timu nzuri inaweza kucheza mchezo mzuri kwasababu inataka matokeo,” alisema | 5michezo
|
MAKAMU wa Rais, Samia Suluhu Hassan amekusanya Sh milioni 370 katika harambee ya kuichangia timu ya taifa ya soka ya Tanzania ‘Taifa Stars ‘ iliyofanyika jana, huku akihimiza fedha hizo zitumike kama zilivyokusudiwa.Katika harambee hiyo iliyofanyika kwenye Hoteli ya Serena, ilihudhuriwa na wadau mbalimbali zikiwamo kampuni, benki na taasisi, ambapo Samia kwa upande wake alichangia Sh milioni 5 na kutoa Sh laki moja kwa ajili ya jezi ya msanii mtoto anayeitwa Mai. Taifa Stars iko Misri kushiriki fainali za 32 za Mataifa ya Afrika (Afcon 2019) zitakazoanza Juni 21 hadi Julai 19.Akizungumza kwenye harambee hiyo, Samia alisema bado kuna nafasi ya kuchangia na kuwahimiza watu kuendelea kupitia namba za akaunti zilizotangazwa ili kufikia lengo la Sh bilioni 1. “Zoezi letu la kuchangia limetusogeza mbele, niwashukuru wote walioshiriki na kuwaomba Watanzania waendelee kwa sababu zoezi ni endelevu, naamini wakichangia wote tutafika nusu ya lengo,” alisema.Mama Samia alisema sababu ya kuomba watu kuchangia ni kwa vile walikuwa hawajaiweka kwenye bajeti ya serikali na kwa kuwa ni timu ya wananchi ndio maana wamerudisha suala hilo kwao. Aliwataka Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) kutumia fedha hizo kwa umakini na kutopeleka watu wasio na kazi kwenye fainali hizo, akitoa mfano wa kamati ya ufundi ya watu 20 ambao sio wahusika.Kwa upande wake, Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dk Harrison Mwakyembe alisema wanachopigania ni motisha kwa wachezaji kuhakikisha wanafanya vizuri katika fainali za Afrika zinazotarajiwa kuanza leo. Alitaja namba za kuchangia kupitia CRDB 01J1019956700 ya TFF, M-Pesa namba 5595298 na NBC 0111010009781.Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda ambaye ni Mwenyekiti wa Kamati ya Hamasa ya Taifa Stars alisema morali ndio kitu pekee wanachohitaji timu ya taifa, wakiamini Watanzania wako nyuma yao na kuwashukuru wale wote walioshiriki kuchangia.Makonda pia, ameahidi kuwapa kiwanja cha ekari 15 TFF kwa ajili ya ujenzi wa viwanja na madarasa ya kufundishia soka na kituo kikubwa cha soka ili ifike mahali timu kutoka nje zivutiwe kuja kuweka kambi nchini na kuongeza mapato.Mmoja wa wadau wakubwa wa soka nchini, Benki ya KCB imesema imeamua kuunga mkono jitihada hizo za uchangiaji ili kuhakikisha Taifa Stars inafanya vizuri katika fainali hizo za Afrika, huku ikiahidi kuendelea kuonesha ushirikiano iwapo timu itafanikiwa kufika fainali.kizungumza kwenye harambee hiyo Mkuu wa Masoko, Mawasiliano na Uhusiano wa KCB, Christina Manyenye alisema huu ni mwaka wa tatu wamekuwa wakiunga mkono soka la Tanzania kuanzia kwenye ligi na sasa timu ya taifa ili kusaidia kuibua vipaji.“Sisi tumechangia jumla Sh milioni 11.5 ikiwa ni mchango wa Sh milioni 10 na jezi ya Mama Samia Sh milioni 1.5, kila inapotokea kusaidia michezo tutafanya hivyo, tunawaombea Taifa Stars wafanye vizuri,” alisema. Baadhi ya wadau wengine akiwemo Azim Dewji aliahidi kuchangia fedha kila hatua timu itakayofika. | 5michezo
|
UBALOZI wa Thailand nchini umeanza mikakati ya kutenga maeneo mbalimbali kwa ajili ya kilimo cha mpunga na kujenga viwanda kwa ajili ya kuchakata zao hilo.Huu ni uzalishaji wa kisasa ambao utashuhudia Uganda ikizalisha mpunga maradufu kutokana na uwepo wa ardhi yenye kufaa kwa kilimo hicho. Akizungumza katika siku ya kitaifa ya Thailand wiki iliyopita, Balozi huyo, Cherdkiat Atthakor ambaye anawakilisha katika eneo lote la Afrika Mashariki, alisema ofisi yake imewasiliana na wawekezaji wa Thailand kwa ajili ya kuja kuwekeza katika Kanda ya Afrika Mashariki.“Mbali na kiwanda cha mpunga, pia tutatengeneza kiwanda cha dawa ili kuwa rahisi kwa wakulima kupata dawa na kuvutia watalii wengi kwa maslahi ya Thailand na Uganda,” alisema balozi. “Mwaka jana tuliwaalika wafanyabiashara wakubwa kutoka nchini Thailand ili kujipatia soko kubwa la bidhaa zao lililopo hapa Uganda, wamefurahishwa na kufanya biashara barani Afrika,” aliongeza balozi huyo.Aliongeza kuwa watalii takribani milioni 25 wanaitembelea Thailand kila mwaka, hivyo kuna mipango ya kufanya utalii wa Uganda kuwa mashuhuri duniani kwa sababu Uganda imebarikiwa kuwa na vivutio vizuri. Balozi mdogo wa Thailand, Barbra Mulwana alisema Uganda inaendelea kufaidi matunda ya uhusiano mzuri kati yake na Thailand. Alisema upande wa elimu, kuna nafasi za wanafunzi 35 za ufadhili wa masomo nchini humo. | 3kitaifa
|
NA GAUDENCE MSUYA, Mwanza WAKALA wa Misitu Tanzania (TFS), Kanda ya Ziwa umetumia zaidi ya Sh milioni 600 kuwezesha jamii katika masuala ya elimu ya uhifadhi wa misitu, ufugaji nyuki na matumizi bora ya ardhi. Meneja wa wakala huo Kanda ya Ziwa, Ebrantino Mgiye, jana alisema kuwa wakala huo uliwezesha wananchi na jamii kupanda miti ili kuboresha ardhi iliyoharibiwa, kulinda ikolojia na kusaidia kupambana na mabadiliko ya tabia nchi katika mikoa ya Geita, Mwanza, Kagera, Mara na Simiyu. “TFS ina wajibu wa kuratibu na kusimamia shughuli za uhifadhi wa misitu kwa niaba ya Serikali, inalenga kupanda miti ya kutoa mazao ya misitu, kulinda vyanzo vya maji na viumbe hai walio kwenye hatari ya kutoweka ambapo mwaka 2019/20 ilitenga fedha zilizotumika kuiwezesha jamii kupanda miche milioni mbili baada ya wakala kuotesha miche hiyo na kuigawa kwa jamii bure,”alisema Mgiye. Alisema ili kurejesha miti iliyopotea kutokana na changamoto mbalimbali na shughuli za kibinadamu mwaka wa fedha 2020/21, TFS imetenga Sh. milioni 200 zitazowezesha shule kuotesha na kupanda miche milioni 3.7, pia Wataanzisha bustani za mikoa ambazo zitagharimu Sh milioni 182 ili kufikia lengo la kupanda miti milioni sita kwa kanda yote. Kuhusu uwezeshaji wa kiuchumi kwa vikundi vya kijamii vya ufugaji nyuki, alisema wametumia Sh milioni 40 kutoa elimu kwa vikundi 124 na mizinga 200 kwa vikundi 20 kikiwemo cha Umoja wa Kusaidiana wa Waandishi wa Habari Mkoa wa Mwanza (UKWAMA). Pia alisema mwaka 2019/2020 TFS ilitoa mafunzo ya ufungaji nyuki na kupanda miti kwa walemavu wasio sikia 60 ili kuwawezesha kuona namna bora ya kufuga nyuki na kuanzisha mashamba ya miti. “Tumefanya hivyo ili kuongeza uelewa na watambue ushiriki wao katika ufugaji na uanzishaji wa mashamba ya miti. Tumetoa madawati zaidi ya 200 kwa shule mbalimbali kusaidia kutatua changamoto hiyo, tunajenga mabweni ya wanafunzi huko Buhindi huko Buchosa tukishirikiana na halmashauri,”alisema Mgiye. Meneja huyo wa TFS Kanda ya Ziwa alieleza kama taasisi katika kupunguza migogoro ya ardhi kwa jamii, zaidi ya Sh milioni 200 zimetumika kutekeleza mpango wa matumizi bora ya ardhi kwa vijiji 13 katika wilaya za Geita na Biharamulo. | 3kitaifa
|
Katibu Mkuu wa Wizara ya Viwanda na Biashara, Mussa Uledi alisema hayo wakati akifunga maonesho ya 39 ya biashara na kusema kuunganishwa huko kumefanyika katika mikutano ya kibiashara kwa washiriki wa maonesho hayo.Alisema mazungumzo hayo ya kibiashara yafuatiliwe kwa kushirikiana na sekta binafsi ili yazae matunda.Uledi alisema maonesho ya mwaka huu yamefana kutokana na maandalizi mazuri, bidhaa zenye ubora wa hali ya juu zilizotokana na ubunifu mkubwa kwa wazalishaji, utangazaji wa bidhaa na wataalamu wa masoko wenye kutoa maelezo fasaha kuhusu bidhaa na huduma zao.Alisema amepata faraja kuwa na mabanda maalumu ya bidhaa za aTanzania kwa ajili ya kutangaza bidhaa za nchini, banda la asalina lile la elimu na kutoa ushauri wa kubainisha bidhaa zingine ili nazo zitafutiwe mabanda maalum ili zionekane na kutangazwa kwa lengo la kutafuta masoko.Alisema serikali itaendelea kutoa ushirikiano ili maonesho hayo yaendelee kuwa na kiwango cha kimataifa kwani mafanikio ya maonesho hayo yanahitaji ushirikiano wa serikali na wazalishaji wa bidhaa na watumiaji.Mkurugenzi wa TANTRADE, Jacqueline Maleko aliwashukuru washiriki wote na kuwakaribisha katika maonesho ya mwakani aliyoahidi kuwa bora zaidi. | 1uchumi
|
ZAINAB IDDY-DAR ES SALAAM WAKATI Wanayanga
wakimtwisha zigo la lawama kocha wao, Mwinyi Zahera, baada ya kupokea kipigo, nahodha
wa timu hiyo, Ibrahim Ajib, amesema sababu kubwa ni uwanja walioutumia na si
kocha. Yanga juzi ilijikuta
ikipoteza alama tatu mbele ya Lipuli FC, baada ya kufungwa bao 1-0, mechi
iliyochezwa Uwanja wa Samora Iringa huku Zahera akiwa jijini Dar es Salaam na timu
ikiwa chini ya Noel Mwandila. Matokeo hayo
yaliifanya Yanga kusalia kwenye nafasi ya kwanza ikiwa na alama zake 67, huku
Lipuli wakifikisha alama 44 kwenye nafasi ya nne. Akizungumza na
MTANZANIA, Ajib alisema wachezaji walitumia nguvu na akili nyingi ili wapate ushindi
lakini walijikuta wanatoka patupu. “Mechi za mikono zina
changamoto nyingi hususani katika suala la viwanja, lakini pia mpira una matokeo
matatu na tulioyapata ni sehemu mojawapo. “Sijaona sababu ya
kumlaumu kocha kwa ajili ya haya matokeo tulioyapata, kwani si mara ya kwanzo
yeye hayupo kwenye timu na sisi tunapata ushindi. Ajibu aliongeza:
“Hili limeshatokea tuangalie mechi inayokuja vipi tutajipanga kuhakikisha
haturudii makosa hata kama uwanja utakuwa si rafiki tena kwetu.” | 5michezo
|
Janeth Mushi, Arusha Katika kukabiliana na kupambana na maambukizi ya virusi vya corona nchini, Kanisa la Anglikana Tanzania, limejipanga kupunguza msongamano wa waumini kwa kuongeza idadi ya ibada zake. Hayo yamesemwa leo Alhamisi Machi 19, jijini Arusha na Askofu Mkuu wa Kanisa la Anglikan Tanzania, Dk. Maimbo Mndolwa ambaye pia ni Askofu wa Dayosisi ya Tanga, baada ya kumalizika kwa kikao kilichoshirikisha maaskofu wake 28 kutoka Dayosisi zote zilizopo Tanzania Bara na Visiwani. “Moja ya tahadhari tunazochukua ni pamoja na kupunguza idadi ya watu katika ibada kwa kuongeza ibada kama vile; mahali penye ibada moja sasa kutakuwa na ibada mbili,” amesema. Kikao hicho mbali na ajenda hiyo kimejadili kuhusu maadhimisho ya miaka 50 ya kanisa hilo nchini tangu mwaka 1970 yanayotarajiwa kufanyika makao makuu ya kanisa hilo yaliyopo mkoani Dodoma Septemba mwaka huu. “Kutokana na hali hiyo, tumeelekeza kila Dayosisi itenge siku maalumu ya maombi kuanzia leo Machi 19 na Ibada ya Ijumaa Kuu, itakuwa siku ya ibada ya pamoja ya Kanisa Anglikana Tanzania kuombea Taifa letu dhidi ya virusi hivyo vya corona,” amesema. | 3kitaifa
|
Na MOHAMED KASSARA-DAR ES SALAAM BINGWA wa mchezo wa gofu katika michuano ya wazi ya ‘Rwanda Open’, Victor Mbunda, amepania kunyakua ubingwa wa mashindano ya ‘Nyali Open’ yatakayofanyika Desemba mwaka huu jijini Mombasa, Kenya. Kinara huyo aliyeiwakilisha vyema Tanzania kwenye mashindano hayo yaliyomalizika Jumamosi iliyopita nchini Rwanda, amesema tayari ameanza kuifungia kazi michuano ya Nyali Open. Akizungumza na MTANZANIA jana, Victor alisema amepanga kuanza rasmi mazoezi leo kwa ajili ya maandalizi ya michuano hiyo ambayo itazikutanisha timu mbalimbali. “Namshukuru Mungu kwa mara ya kwanza nimeweza kuibuka kinara wa mashindano ya Rwanda Open, lakini kesho ‘leo’ nitaanza mazoezi ili kujiwekea mazingira mazuri ya ubingwa kwa mara nyingine,” alisema Mbunda. Kwa upande wake, meneja wa mchezaji huyo wa kituo cha Gymkhana, jijini Dar es Salaam, Juma Mlela, aliipongeza Kampuni ya New Habari (2006) Ltd kwa kutoa mwaliko kwa Mbunda na kueleza kuwa wamejipanga kuhakikisha wanaendeleza ubingwa kwenye mashindano mengine yaliyopo mbele yao. “Hadi sasa sina wasiwasi na wachezaji wangu kwa mashindano yoyote ya ndani, lakini pia nawatoa shaka Watanzania kwa upande wa mashindano ya kimataifa kutokana na ubingwa tuliopata juzi, tutazidi kupambana ili tufikie malengo,” alisema Mlela. Mbunda ambaye ni mchezaji wa ridhaa, ataungana na mshindi namba mbili wa mashindano ya Rwanda Open, Amani Said pia kutoka Tanzania ili kudhihirisha ubora wao katika michuano ya Nyali Open. | 5michezo
|
DAVAO, PHILIPPINES KATIKA mlolongo wa kauli zake tata kuhusu mashambulizi ya kingono, Rais Rodrigo Duterte ameripotiwa akisema atawapongeza wabakaji wakitenda jinai itakayowahukumu kifo. Akizungumza na wanadiplomasia wa Ufilipino Ijumaa iliyopita katika mji wa nyumbani wa Davao, ambako alihudumu kama meya kwa zaidi ya miongo miwili, Duterte alizungumzia masuala ya uhalifu unaotokana na mihadarati, ikiwamo ubakaji. “Kile nisichopenda ni watoto kubakwa. Mnaweza kubaka pengine mrembo wa Miss Universe. Hapo naweza kukupongeza kwa ujasiri wa kumbaka mtu ukifahamu kuwa utaishia kunyongwa,” Duterte anadaiwa kusema. Duterte (72), aliukwaa urais mwishoni mwa Juni 2016, na kipindi kisichozidi mwaka mmoja baadaye, alilaaniwa duniani kwa vita dhidi ya unga, ambayo imesababisha maelfu ya mauaji na ukiukaji wa haki za binadamu. Wakati akiendesha kampeni za urais Aprili 2016, Duterte alitoa kauli za kutisha kuhusu mmisionari wa Australia, ambaye alibakwa na kundi la watu na kuuawa wakati wa uasi gerezani mwaka 1989 mjini Davao, wakati akiwa meya. “Niliona uso wake na kujiwa na wazo: Wapumbavu, wamembaka kwa zamu, walipanga foleni. Nilikasirika kuwa alibakwa, lakini alikuwa mrembo. Nilidhani kama meya nilipaswa kuwa wa kwanza,” alisema. Baadaye aliwaambia wakosoaji wake maneno hayo hayakuwa utani na aligoma kuomba radhi. Mei mwaka huu, Rais Duterte aliwaambia askari wake angewaruhusu kubaka wanawake watatu kila mmoja. “Fanyeni kazi yenu. Mengine niachieni. Nitaenda jela kwa ajili yenu. Iwapo mtabaka watatu, nitaikubali,” alisema. Na wakati binti yake mwenyewe alipotangaza kuwa mwathirika wa ubakaji, Rais Duterte anaripotiwa kupuuza madai yake akimwita ‘malkia wa maigizo.’ Tangu aukwae urais, ametoa kila aina ya kauli tata kuanzia kumtusi Rais Barack Obama hadi kudai ameua wahalifu kwa mkono wake na kuwala nyama. | 2kimataifa
|
NA KULWA MZEE DAR ES SALAAM MAHAKAMA Kuu Kanda ya Dar es Salaam, imeombwa kutupilia mbali maombi yaliyofunguliwa na wabunge wanane na madiwani wawili wa Chama cha Wananchi (CUF), wakitaka wabunge wateule wa chama hicho wasiapishwe kwa sababu haina mamlaka ya kutoa uamuzi kwa amri wanazoziomba. Hoja hizo ziliwasilishwa jana na Wakili wa Serikali Mkuu, Gabrieli Malata mbele ya Jaji Lugano Mandambo, baada ya wadai kuwasilisha maombi. Wadai katika maombi hayo, ni Mbunge Severina Silvanus Mwijage, Saumu Heri Sakala, Salma Mohamed Mwassa, Riziki Shahali Ngwali, Raisa Abdallah Mussa, Miza Bakari Haji, Hadija Salum Ally Al-Qassmy na Halima Ali Mohamed na madiwani ni Elizabeth Sakala na Layla Madiba. Wadaiwa ni Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), Katibu wa Bunge, Bodi ya Wadhamini CUFna wabunge wateule wote. Akipinga maombi yao, Malata alidai njia waliyotumia kufikisha mahakamani maombi hayo si sahihi, kwani kifungu hicho cha Sheria ya Jala kinatoa ridhaa ya kutumia sheria za Uingereza na ukishapata ridhaa hiyo unapaswa kueleza unatumia sheria ipi. Alidai kufikisha maombi hayo mahakamani ni kuisumbua mahakama, wanatafuta nafuu ya jambo moja katika mamlaka mbili tofauti kwani wakati wanaomba zuio na wamewasilisha rufaa katika mkutano mkuu wa chama hicho. “Mheshimiwa Jaji, mahakama hii haina mamlaka ya kutoa amri wanazoomba kwa sababu mhimili wa Bunge unatekeleza majukumu yake kikatiba, kuna mazingira ambayo mahakama inaweza kutoa amri kwa muhimili mwingine lakini si mazingira kama haya,”alidai Malata. Wakili anayewakilisha Bodi ya Wadhamini CUF na wabunge wateule, Mashaka Ngole alidai maombi hayo ni batili kwa sababu yamewajumuisha wabunge wateule kuwa ni wadaiwa, wakati katika kesi ya msingi hawapo hivyo aliomba yatupwe. Akijibu,Wakili Peter Kibatala alidai kifungu cha sheria alichotumia ni sahihi pingamizi lililowasilishwa halikidhi vigezo vya kuwa pingamizi. Alidai amri ya zuio inaweza kutolewa na mahakama hata bila kuwapo kesi ya msingi, hivyo hoja ya wabunge wateule kutokuwepo katika kesi ya msingi haina mashiko. Kibatala aliomba mahakama hiyo, itoe amri ya kwamba hali iliyopo iendelee kuwa hivyo mpaka kesi zilizopo mahakamani zitakapotolewa uamuzi. Jaji Mwandambo, alisema hawezi kutoa amri yoyote kwa sasa, aliahirisha kesi hiyo hadi Agosti 4, mwaka huu kwa ajili ya kutoa uamuzi wa pingamizi na aliruhusu Wakili Kibatala kufanya marekebisho ya hati ya madai katika kesi ya msingi ambayo itatajwa Agosti 21 mwaka huu. Katika maombi hayo, wabunge waliovuliwa uanachama na ubunge wanaomba mahakama itoe amri ya kuzuia wabunge wateule kuapishwa hadi kesi ya msingi itakapomalizika na amri ya kuzuia utekelezaji wa uamuzi wa CUF. | 3kitaifa
|
LONDON, UINGEREZA UCHAGUZI
uliofanyika juzi nchini Uingereza na ambao ulionekana ni vigumu kutabiri
matokeo yake, hatimaye chama cha Conservative kimeshinda kwa kupata viti zaidi
ya 364 kati ya 650 kuliko ilivyotarajiwa na hivyo kuwaacha wengi katika hali ya
mshangao. Chama hicho
ambacho kilitikiswa ndani ya bunge kutokana na hoja ya Brexit kabla ya
kuitishwa kwa uchaguzi huo pia
kimenyakua ngome muhimu zilizokuwa zikishikiliwa na chama pinzani cha Labour. Wakati
Labour kikionekana kupoteza viti 59 chama cha Conservative kimeongeza viti
vipya 47 na Scottish National Party (SNP) kikijinyakulia viti 48 kati ya hivyo 13
vikiwa vipya. Kiongozi wa
chama cha Conservative, Boris Johnson amewashukuru wapiga kura wa Uingereza kwa
kushiriki kwa wingi katika uchaguzi huo. Akizungumza
na vyombo vya habari muda mfupi baada ya chama chake kushinda Jonhson amesema
hatua hiyo inaipatia serikali mpya fursa ya kuheshimu maamuzi ya kidemokrasia
ya raia wa Uingereza ili kuliimarisha taifa hilo. Chama cha
Johsnon kilihitaji kujipatia viti 326 ili kutangazwa kuwa mshindi lakini
kimepitisha idadi hiyo na kufikia viti 364. Waziri huyo
mkuu amesema uamuzi huo unampatia jukumu la kufanikisha Brexit na kuiondoa Uingereza
katika muungano wa Ulaya. ”Zaidi ya
yote nataka kuwashukuru watu wa taifa hili kwa kujitokeza kupiga kura ya
Disemba ambayo imebadilika na kuwa ya kihistoria, ambayo inatupatia sisi kama
serikali mpya fursa ya kuheshimu uamuzi wa kidemokarsia wa raia wa
kulibadilisha taifa hili na kuonyesha uwezo wa raia wa taifa hili”. Johnson
amesema atafanya kazi ‘usiku na mchana’ ili kuwalipa wapiga kura waliomuonyesha
uaminifu baada ya kukisadia chama chake cha Conservative kupata ushindi wa
kihistoria. Huku ikiwa imesalia maeneo mawili ya bunge kutangazwa
, chama cha Coservative kina wingi wa viti 76. Akiungumza
mjini London , waziri mkuu Johnson alisema kwamba ni jukumu lake kuindoa
Uingereza katika muungano wa EU . “Raia
wanataka mabadiliko” , alisema, ”hatuwezi kuwavunja moyo na hatutawavunja ” Hatua hiyo
inajiri muda mchache baada ya mpinzani mkuu wa Jonson, Jeremy Corbyn kusalimu
amri na kusema kwamba hatokiongoza tena chama hicho katika uchaguzi mkuu ujao. Uamuzi huo
wa Corbyn unajiri huku chama hicho kikikabiliwa na matokeo mabaya zaidi ya
uchaguzi katika miongo kadhaa. Fay Jones ,
Virginia Crosbie na Sarah Atherton atawakilisha chama cha Conservative katika
eneo la West Minister Chama cha Labour
kimepoteza viti kaskazini mwa England , Midlands na Wales yakiwa ni maeneo yaliyopiga
kura ya Brexit katika kura ya maoni ya 2016. Labour inatarajiwa kushinda viti 61 ikiwa ni chini
ya viti ilivyoshinda 2017 imedaiwa. Baadhi ya
maeneo bunge kama vile Darlington ama Workington , kaskazini mwa England
yataongozwa na mbunge wa Chama cha Conservative kwa mara ya kwanza katika
miongo kadhaa- ama katika matukio ya Bishop Auckland na Blyth Vally kwa mara ya
kwanza tangu viti hivyo kubuniwa. Lakini Labour
kimeshinda kiti cha eneo bunge la Putney, kusini magharibi mwa London kutoka
kwa Conservative. Chama cha
Uskochi cha kitaifa kimepata ushindi wake wa kwanza, kikishinda eneo bunge la
Rutherglen na Hamilton magharibi kutoka kwa chama cha Labour na Angus kutoka
kwa Conservative. Imebainika
kwamba Conservative watapata wabunge 357 ikiwa ni wabunge 39 zaidi ya uchaguzi
wa 2017 kura zote zitakapohesabiwa. Chama cha Labour
kitajipatia wabunge 201, SNP wabunge 55 , Liberal Democrats 13, Plaid Cymru 4
The Greens 1 brexit Party 0. Ongezeko la
wastani katika kura ya chama cha Conservative ni asilimia 2 ikiwa ni pointi
moja ya kilichotarajiwa katika kura hiyo. Kura ya
chama cha Labour ilipungua kwa asilimia 9 kulingana na utabiri wa matokeo ya
kura hiyo yasio rasmi. Nchini
Uskochi, kumekuwa na ongezeko la asilimia 9 katika chama cha kitaifa cha
Uskochi – ikiwa ni kiwango cha chini ya ilivyotabiriwa kwa asilimia 13 lakini
SNP kinaelekea kushinda viti 55. Waziri wa
masuala ya ndani wa chama cha Conservative, Priti Patel alisema kwamba serikali
itahakikisha Brexit inafanyika kwa haraka kabla ya Krisimasi kupitia
kuwasilisha miswada iwapo serikali yake itarudi mamlakani. Mbunge wa
zamani wa Conservative, Sir Alan Duncan ambaye amekuwa mkosoaji mkubwa wa Boris
Johnson amesema kwamba waziri mkuu huyo sasa ndiye mwanasiasa mwenye umaarufu
mkubwa Uingereza na kwamba uchaguzi huo umethibitisha hilo. Mgogoro
ulikuwa tayari umezuka katika chama cha Labour kuhusu ni nani anayefaa
kulaumiwa kutokana na matokeo mabaya kuwahi kutokea katika miongo kadhaa. Ilikuwa ni
siku mbaya kwa chama cha Labour huko Wales na hususan eneoa la Kaskazni Mashariki. Mwenyekiti
wa Labour, Ian Lavery ambaye alihifadhi kiti chake kwa uchache wa kura
alizopata awali amesema kwamba amesikitishwa na wapiga kura katika ngome za
chama cha Labour wanaomboleza kuhusu msimamao wa Brexit wa chama hicho. Kansela kivuli John McDonald aliambia BBC kwamba
matokeo ya kura yasio rasmi yalikuwa yanasikitisha kwa Labour. ”Nilidhania
ushindani utakuwa wa karibu mno” , alisema na kulaumu kile alichokitaja kuwa
uchaguzi wa Brexit. Baadhi ya
wagombea wa Labour wamekosoa uongozi wa Corbyn . Gareth Snell
alisema alitarajia kupoteza kura ya Stoke Central kwa chama cha Conservative na
alimtaka Corbyn na McDonald kuondoka
lakini pia akawalaumu wanachama wa chama hicho wanaopinga Brexit kwa kukisukuma
sana chama hicho. Ofisi ya
waziri mkuu katika taarifa yake imesema kwamba iwapo matokeo hayo yasio rasmi
yatathibitishwa na Johnson kurudi uongozini kutakuwa na mabadiliko machache ya
baraza la mawaziri siku ya Jumatatu. Muswada wa
makubaliano ya kujiondoa utakaorahisisha kuondoka kwa Uingereza Januari 31
utasomwa kwa mara ya pili katika bunge Disemba 20. Mabadiliko
makubwa ya baraza la mawaziri yatafanyika mwezi Februari, baada ya Uingereza
kuondoka EU huku taarifa ya bajeti ikitolewa mwezi Machi. Huu ni
uchaguzi wa Uingereza wa tatu chini ya miaka mitano na wa kwanza kufanyika mwezi
Disemba katika kipindi cha miaka 100 na umetawaliwa na kura ya maoni ya 2016 ya
kuondoka katika muungano wa Ulaya. Wakati wa
kampeni Johnson aliahidi kuiondoa Uingereza EU kufikia Januri 31, 2020 iwapo
angepata wingi wa kura. Chama cha Labour
kilifanya kampeni ya kuongeza matumizi
katika huduma za umma mbali na katika vituo vya afya. Chama cha
Liberal Democrats kiliahidi kufutilia mbali Brexit iwapo kiongozi wake Jo
Swinson angechaguliwa kuwa waziri mkuu, lakini kura ya maoni ilitabiri kwamba
ufuasi wao utapungua wakati wa kampeni. Chama cha
kitaifa cha Uskochi kilisema kwamba uungwaji mkono wao utaashiria kura ya maoni
ya pili kufanyika. Kiongozi wa
SNP Nicola Sturgeon alituma ujumbe wa twitter akisema kuwa kile kinachoonekana
kuwa ‘kikubwa ni kidogo’. Caroline
Lucas ambaye matokeo hayo yanaonyesha kwamba anatarajiwa kuwa mbunge wa pekee
wa chama hicho cha Green Party , alituma ujumbe katika twitter akisema: “Iwapo
matokeo haya ni ya kweli basi ni pigo kubwa kwa hali yetu ya hewa kwa kizazi
kijacho na demokrasi yetu”. Kiongozi wa
chama cha Liberal Democrat, J Swinson
amesema kwamba atajiuzulu baada ya kupoteza kiti chake kwa chama cha SNY kwa
kura 149. Swinson
ambaye alianza kampeni akisema huenda akawa waziri mkuu mpya wa Uingereza
alijipatia kura 19,523 ikilinganishwa na kura 19,672 za mgombea wa chama cha
SNP Amy Callaghan katika eneo la Dunbartonshire mashariki. Sir Ed Davey
na Barones Sal Brinton watakuwa kaimu viongozi wa chama hicho , wakati huu
ambapo sio mbunge tena. Swinson
alisema matokeo ya uchaguzi huo yataleta aibu kwa wengi. Chini ya
sheria za chama chama cha Liberal Democrat ni sharti kiwe na kiti kimoja
bungeni. | 2kimataifa
|
NA MWANDISHI WETU, DAR ES SALAAM SAKATA la upangaji wa matokeo katika michuano ya Ligi Daraja la Kwanza (FDL) iliyomalizika mwishoni mwa wiki iliyopita, limepelekwa kwenye Kamati ya Nidhamu ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) kwa uchunguzi zaidi. Juzi Kamati ya Uendeshaji na Usimamizi wa Ligi iliyokutana kupitia taarifa za mechi mbili za Kundi C za ligi hiyo, ilishindwa kutoa uamuzi juu ya suala hilo la kinidhamu na kumtaka Katibu Mkuu wa TFF, Selstine Mwesigwa, alipeleke Kamati ya Nidhamu. Timu za Kundi C zinazohusishwa na upangaji wa matokeo katika mechi za mwisho FDL ni JKT Kanembwa dhidi ya Geita Gold SC na Polisi Tabora dhidi ya JKT Oljoro. Awali kabla ya sakata hilo kufikishwa kwenye Kamati ya Uendeshaji na Usimamizi wa Ligi, TFF ilisimamisha matokeo na kugoma kutangaza timu itakayopanda daraja hadi taarifa zitakapopitiwa. Hata hivyo, baada ya kamati hiyo ya saa 72 kupitia taarifa za mechi hizo na vielelezo vingine, ilionyesha mashaka kutokana na kuwepo viashiria vya upangaji wa matokeo. Taarifa ya kamati hiyo ilieleza kwamba, kwa kuwa suala hilo ni la kinidhamu kwa mujibu wa ibara ya 50(1) na (11) ya katiba ya TFF na ibara ya 69 ya kanuni za nidhamu za shirikisho hilo, litaweza kufanyiwa uchunguzi na Kamati ya Nidhamu na kutolewa uamuzi. Tayari TFF imetangza timu mbili zilizofanikiwa kupanda daraja na kucheza Ligi Kuu Bara msimu ujao ambapo Ruvu Shooting imefanikiwa kutoka kundi B na African Lyon kutoka kundi A. | 5michezo
|
FREDY AZZAH na ELIZABETH HOMBO – Dodoma
RAIS Dk. John Magufuli ameonya kuwa mtu yeyote atakayejaribu kuuvunja Muungano wa Tanganyika na Zanzibar atavunjika yeye.
Aliyasema hayo jana mjini hapa, alipokuwa akihutubia maelfu ya wananchi waliojitokeza katika Uwanja wa Jamhuri kuadhimisha miaka 53 ya Muungano huo.
Maadhimisho hayo ni ya kwanza kufanyika mkoani Dodoma tangu kuundwa kwa Muungano huo wa Tanganyika na Zanzibar.
“Katika kutunza Muungano wetu, taifa la Tanzania litasonga mbele, kama nilivyoahidi mimi na Dk. Shein (Rais wa Zanzibar, Dk Ali Mohamed Shein). Leo tunasherehekea miaka 53 wakati tunatambua kabisa wenzetu waliotutangulia waliutunza Muungano huu kwa nguvu zote, wakina mzee Mwinyi (Ali Hassan), akina mzee Mkapa (Benjamin) akina mzee Jumbe (Aboud Jumbe), mzee Mkapa usilalamike wewe ni mzee sasa hivi, akina mzee Kikwete (Jakaya) pamoja na kwamba yeye anaonekana ni kijana kuliko mimi, ni kwa sababu ya shida tu.
“Unajua kuongoza nazo ni shida sana, siku hizi amekuwa kijana zaidi (Kikwete) anapendeza, napenda kurudi kuwaahidi ndugu zangu Watanzania, Muungano ndiyo silaha yetu, Muungano ndiyo jembe letu, Muungano ndiyo umoja wetu, Muungano ndiyo ushindi wetu, nataka niwahakikishie, mimi pamoja na Dk. Shein, tutaulinda Muungano kwa nguvu zote na kamwe asijitokeze mtu yeyote atakayejitahidi au kujaribu kuuvunja Muungano, atavunjika yeye,” alisema Rais Magufuli.
Pia alizungumzia umuhimu wa amani kuwa ni jambo la msingi na la kulinda kwa nguvu, kwa sababu ndiyo iliyofanya leo Muungano wa Tanzania na Zanzibar ukafikisha miaka 53.
“Waimbaji wameimba, tunaweza kufikisha miaka 53 ya Muungano kwa sababu ya amani na tunaweza kupata mafanikio yote tuliyonayo kwa sababu ya uwepo wa amani, hapa nchini bila ya amani mambo yote haya yasingewezekana,” alisema Rais Magufuli.
KUHAMIA DODOMA
Kuhusu ahadi yake ya Serikali yote kuhamia Dodoma ifikapo 2020, alisema hadi sasa zaidi ya watumishi 3,000 wameshahamia Dodoma.
Alisema pia katika bajeti inayoendelea kujadiliwa na Bunge sasa hivi, takribani Sh bilioni 200 zimetengwa kwa ujenzi wa ofisi za Serikali na nyumba za viongozi.
Dk. Magufuli alisema katika kuhakikisha Dodoma inapata hadhi ya kuwa Makao Makuu ya nchi, uwanja wa ndege wa Dodoma umetanuliwa, jiwe la msingi la reli ya kisasa ambayo pia itapita Dodoma limewekwa na ujenzi wa barabara na miundombinu mingine unaendelea.
Alitaja maandalizi mengine yanayoendelea kuwa ni pamoja na kuhakikisha umeme wa uhakika na maji vinapatikana na pia kuhakikisha kuna huduma za afya na elimu.
MAKOMANDOO
Maonyesho ya makomandoo wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) na yale ya kikundi cha chipukizi kinachoundwa na wanafunzi wa shule za sekondari za Dodoma, ambao Dk. Magufuli aliwaita ‘makomandoo watarajiwa’, yamefanya maadhimisho ya miaka 53 ya Muungano kuwa ya aina yake.
Baada ya gwaride la kawaida linaloundwa na vyombo mbalimbali vya ulinzi na usalama kumalizika, lilifuata onyesho la ukakamavu lililofanywa na makomando wa JWTZ, lililowaduwaza viongozi waliohudhuria maadhimisho hayo.
Baadhi ya maonyesho hayo ni pamoja namna ya kucheza karate, kumshambulia adui, kuvunjiwa tofali kichwani, kubeba wenzao kwa meno, kukunja nondo na kupigwa na mbao sehemu mbalimbali za mwili bila kudhurika.
Rais Mstaafu, mzee Ali Hassan Mwinyi, alionekana kutingisha kichwa wakati mmoja wa makomando alivyompiga kichwani mwenzake wakati wakifanya onyesho hilo.
Makamu wa Rais, Samia Suluhu Hassan, naye alionekana kuduwaa muda mwingi wakati kikosi hicho kilipokuwa kikifanya matukio, huku akionekana akizungumza jambo na Mkuu wa Jeshi hilo, Jenerali Venance Mabeyo.
Wakati wakifanya hivyo kwa kupokezana, mshereheshaji alisema makomandoo hao ni wale walioshiriki katika mapigano ya M23 katika nchi ya Jamhuri ya Demokrasia ya Kongo (DRC).
GWARIDE LA WANAFUNZI
Gwaride la wanafunzi wa sekondari za mjini Dodoma lilijumuisha wasichana na wavulana likiwa na vikosi vinne, huku vitatu vikiwa ni vya askari wa kawaida na kimoja cha makomandoo.
Vikosi hivyo, vilikuwa na viongozi wake kama vilivyo vile vya majeshi ya ulinzi na usalama na vilingia uwanjani na kutoa heshima kwa Rais kabla ya kusimama katikati ya uwanja na kuimba wimbo wa ‘Tazama Ramani’.
GWARIDE LA MBWA
Kulikuwa na gwaride la mbwa ambao walikuwa wakifanya kila wanachoelekezwa na askari wao.
Mbali na hilo, pia kulikuwa na mbwa wa kufichua bangi. Mmoja wa askari alificha bangi na baadaye mbwa akaitafuta kwa kunusa hadi alipoipata.
Mbwa mwingine aliyeonyesha umahiri ni wa kufichua wahalifu. Watu wawili waliigiza kama wahalifu na baadaye kushambuliwa kwa kung’atwa na mbwa hao.
JK KIVUTIO
Rais Mstaafu, Jakaya Kikwete, aliwasili saa 2:20 asubuhi Uwanja wa Jamhuri na baada ya kutambulishwa na mshereheshaji, uwanja mzima ulilipuka kwa shangwe. | 3kitaifa
|
NA RHOBI CHACHA AKIWA na wapambe 15 msanii wa Bongo Fleva, Nurdin Bilali ‘Shetta’, alilazimika kutumia nguvu za ziada ili kuingia na wapambe wake hao katika shoo ya kuadhimisha miaka 16 ya muziki kwa msanii Juma Nature, iliyofanyika katika Ukumbi wa Dar Live uliopo Mbagala jijini Dar es Salaam. Shetta ilimlazimu kufanya uamuzi huo baada ya njia yake ya kutishia kususia kufanya onyesho lake katika onyesho hilo kupuuzwa huku akikataliwa kuingia na idadi hiyo kubwa ya wapambe wake badala yake alitakiwa aingie na wapambe nane tu. Kabla ya Shetta kutumia nguvu, wapambe wake nane waliokubaliwa kuingia ukumbini walimtaka msanii wao huyo waondoke kama wenzao hawatakubaliwa kuingia huku wakilalamika kwamba mbona msani Nassib Abdul ‘Diamond’ huwa na wapambe wengi lakini hawawazuii. “Hapa kwa vile Shetta mnamzuia lakini angekuwa Diamond angeingia na wapambe wake hata ishirini na msingemzuia kwanini Shetta bora tusepe,” alipaza sauti mmoja wa wapambe hao. Hata hivyo, Shetta alipohojiwa alishangazwa na kukataliwa wakati huwa anaongozana na wapambe 15 katika kila onyesho lake, lakini hata hivyo onyesho lilifanyika kwa mafanikio na Nature akafurahia miaka yake 16 huku kituo cha EFM kikisherehekea mwaka mmoja tangu kuanzishwa kwake. | 0burudani
|
WANAFUNZI 4,294 walioomba nafasi vyuo vikuu tofauti na kudahiliwa chuo zaidi ya kimoja wanadaiwa hawajathibitisha udahili wao katika moja kati ya vyuo walivyochaguliwa.Tume Vyuo Vikuu Tanzania (TCU) imesema jana kuwa mwisho wa kuthibitisha ulikuwa juzi.Tangazo lililotolewa Oktoba 3, mwaka huu na Katibu Mkuu wa TCU, Profesa Charles Kihampa liliwataka waombaji wote wa udahili waliochaguliwa chuo zaidi ya kimoja awamu ya kwanza na ya pili kuthibitisha udahili wao kwenye chuo kimoja wanachopenda kwenda.Alisema waombaji hao walitumiwa namba maalumu kupitia simu zao ambazo zilitumika wakati wa kufanya maombi ya udahihi vyuoni.“Waombaji ambao majina yao yamechaguliwa na chuo zaidi ya kimoja walipaswa kuthibitisha udahili wao kwa kutumia namba maalumu iliyotumwa kupitia namba ya simu iliyotumika wakati wa kufanya maombi ya udahili chuoni. Tunasisitiza mwisho wa kuthibitisha ni Oktoba 5,mwaka huu,” amesema Profesa Kihampa jana.Amesema idadi hiyo ya waombaji 4,294 iko kwenye makundi mawili; la kwanza ni wale wa chaguo la kwanza ambapo waombaji 1,853 wamechaguliwa chuo zaidi ya kimoja na hadi Oktoba 3, walikuwa hawajathibitisha kokote.Kundi la pili ni la waombaji 2,441 ambao walichaguliwa chuo zaidi ya kimoja awamu ya pili ambao pia hawajathibitisha katika chuo kimojawapo kati ya vyuo walivyochaguliwa.Wakati TCU ikisema hayo, baadhi ya vyuo vikuu vimewataka wanafunzi waliochaguliwa kwa ajili ya masomo kwa mwaka 2018/19 kufika katika chuo husika kuchukua barua za udahili kwa ajili ya hatua nyingine za usajili.Mkurugenzi wa Mafunzo ya Shahada ya Kwanza katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM), Dk Egbert Mujuni katika taarifa yake ya Oktoba 3,mwaka huu inawataka wale wote waliochaguliwa kujiunga na chuo hicho kwenda kuchukua barua za udahili kuanzia kesho.Amesema wanafunzi waliochaguliwa kujiunga chuoni hapo Kampasi ya J.K Nyerere Mlimani, wanapaswa kuchukua barua za udahili kwa ajili ya taratibu nyingine za chuo kuanzia Oktoba.Aidha amesema, wale wanaoishi au kutoka nje ya mkoa wa Dar es Salaam wanaweza kuchukua barua zao wiki ya kwanza ya utambulisho chuoni Oktoba 27 hadi Novemba 3,mwaka huu.Dk Mujuni amesema waliochaguliwa kujiunga na masomo Chuo Kikuu Kishiriki cha Elimu(Duce) na Mkwawa (Muce) barua zao watazifuata huko kuanzia kesho hadi Novemba 3, mwaka huu. | 3kitaifa
|
Timu hiyo ya Ligi Kuu iliongoza baada ya bao la Willian katika dakika ya 62 na ilionekana kuibuka na ushindi. Kross ya Christensen ndani ya eneo la hatari liliiadhibu Chelsea baada ya Lionel Messi kuunasa mpira na kuifungia Barca bao la kusawazisha ugenini.Alipoulizwa kuhusu bao hilo, bosi huyo wa Chelsea, Conte alisema: "Nadhani kiwango cha Christensen kilikuwa kizuri, tunazungumzia mchezaji ambaye ndio kwanza ana umri wa miaka 21 hapa”."Inafurahisha kwamba alikuwa tayari kucheza mechi hii akiwa amepevuka kiakili, nina furaha sana, alikuwa miongoni mwa wachezaji bora usiku huu (juzi)."Ni ngumu kuchagua mchezaji mmoja au mwingine lakini nadhani Christensen alicheza mechi hii kwa kiwango kikubwa, nimefurahishwa na kiwango chake”.Wakati Barcelona ikitawala mchezo, Chelsea ndio iliyotengeneza nafasi nzuri, ambapo mashuti ya Willian yaligonga mwamba mara mbili katika kipindi cha kwanza na Eden Hazard alishindwa kufunga baada ya kushindwa kujiweka pazuri."Nadhani tulikuwa karibu kwenye kucheza mchezo sahihi,” alisema Conte."Nadhani tumeadhibiwa na kosa moja, lakini kama mnavyojua kucheza dhidi ya aina hii ya wachezaji Messi, kama [Andres] Iniesta, [Luis] Suarez, kama utafanya kocha litakugharimu”."Unapocheza dhidi ya Barcelona, tunajua kwamba kama unataka kucheza dhidi yao hatua kwa hatua, mnachanganyikiwa, unapoteza mechi sio kwa 1-0 au 2-0 lakini kama kilichotekea Hispania 4-0, 5-0 au 6-0. | 5michezo
|
NA VALERY KIYUNGU JUMAMOSI tulivu tunakutana hapa kwenye safu hii ya Old Skuli. Hapa ndiyo mahala ambapo mashabiki na wadau wa burudani tunapata wasaa wa kufahamu mambo kadha wa kadha yanayohusu muziki wa zamani na wasanii wake. Safu hii imekuwa ikikukutanisha na wanamuziki mbalimbali na kukupa nafasi ya kuwafahamu, leo pia Old Skuli inakukutanisha na Maurus Mzeru ambaye aliwahi kuwika kwenye tasnia hiyo ya muziki miaka mingi iliyopita. HISTORIA YAKE YA MUZIKI Ndani ya muziki alianza kufanya kazi zake mwaka 1969 pale alipojiunga na bendi ya Afro 70 iliyokuwa inaongozwa na mwanamuziki mahiri ambaye hivi sasa ni marehemu, Patrick Balisidya. Mkongwe huyo ambaye hivi sasa amejiwekea makazi yake Tandika jijini Dar es salaam akiendelea na kazi zake za muziki. Hakudumu sana kwenye bendi ya Afro 70 akaamua kuhamia kwenye bendi ya Kurugenzi Jazz iliyokuwa na makazi yake mkoani Arusha. Mwaka 1994 Mzeru alisafiri kutoka Dar es Salaam hadi mkoani Tanga, ambako alikwenda kuanzisha na kuwa mwasisi wa bendi ya Bandari –Tanga ambako hakukaa sana alirejea tena Dar es salaam. AKUTANA NA MBARAKA MWINSHEHE Mzeru alikutana na Mbaraka mwaka 1976 kwenye ukumbi wa DDC Kariakoo Jijini Dar es Salaam, wakati mkongwe huyo alipokuwa na bendi yake ya Super Volcano. Katika mazungumzo yao ukumbini hapo wawili hao, Mzeru ambaye ni mtunzi, muimbaji pia mpiga solo, alimweleza Mbaraka kuwa kwa wakati huo alikuwa amejiweka pembeni na muziki wa dansi. Wakati huo Mzeru alikuwa mfanyakazi kwenye kiwanda cha kutengeneza redio na betri za National Panasonic. Baada ya Mbaraka kupata maelezo hayo alimpa ushauri wa kurejea kwenye muziki kwani muziki ni taaluma na akamsisitiza popote alipo aanzishe bendi ili kuendeleza kipaji alichonacho. AUNDA NATIONAL PANASONIC SOUND Kufuatia ushauri huo wa bure kutoka kwa Mbaraka, Mzeru ndipo alipoamua kuunda bendi yake ya National Panasonic hiyo ilikuwa mwaka 1980 baada ya mwajiri wake kumuunga mkono. Baadhi ya wanamuziki walioshirikiana naye kuunda na kuasisi bendi hiyo ya National Panasonic ni pamoja na Shaka Msuwamwili na Manyama Ladislaus ambao chini ya uongozi wa Mzeru waliweza kufanya kazi nzuri. Waliweza kutunga, kurekodi na kuimba nyimbo zenye maadili kwa jamii pia zilizoweza kuwagusa wengi, baadhi ya nyimbo hizo ni pamoja na Matatizo ya Ndoa, Kuona ni fahari ya macho ambazo zilikuwa gumzo kwa mashabiki wa muziki wa dansi. ELIMU YAKE Alisema shule ya Kati ya Mtakatifu Xavier, ambayo kwa sasa inajullikana kama Kibasila hadi darasa la Nane, akiwa anaendelea kupiga muziki akiwa kwenye bendi ya Gold All Stars, ikiwa inatumiwa na mtindo wa Kalumbende. | 0burudani
|
NA FESTO POLEA KAMATI ya maandalizi ya Tamasha la Kimataifa la Filamu Zanzibar (ZIFF), imetangaza kuanza kupokea filamu za wasanii mbalimbali kote duniani ili zishindanishwe na kupitishwa kwa ajili ya kuonyeshwa katika tamasha hilo kwa mwakani. Mkurugenzi wa Tamasha hilo, Prof Martin Mhando, alisema licha ya uwepo wa hofu ya kutokuwepo kwa matamasha makubwa yanayofanyika visiwani Zanzibar, tamasha hilo la 18 lenye kauli mbiu ya ‘Ndiyo hii Safari Yetu’ litafanyika kama kawaida kuanzia Julai 9 hadi 17 mwaka 2016 katika viwanja vya Ngome Kongwe visiwani humo. “Naamini kukosekana kwa tamasha la Sauti za Busara lililotakiwa kufanyika Februari mwakani wengi wanaweza kuingiwa na hofu kwamba tamasha la Ziff nalo linaweza kutofanyika, hivyo waondoe hofu lakini pia tunaiomba Serikali ya Zanzibar na Tanzania kwa ujumla kusaidia matamasha haya yafanyike kama yanavyopangwa kwa kuwa yanaiingizia pato kubwa Serikali na kutangaza utalii wake kutokana na kuwa na wageni wengi kutoka sehemu mbalimbali duniani,’’ alisema Prof. Mhando. Aliongeza kwamba, kila mwaka tamasha la ZIFF hupokea zaidi ya filamu 60 kutoka Afrika Mashariki ya Kati, Ulaya, Latin America, Marekani na Asia. Filamu zinazopokelewa ni makala, filamu ndefu, filamu fupi, filamu za katuni, nchi za Jahazi, Filamu za Afrika Mashariki na video za muziki kutoka kwa wasanii wa Afrika Mashariki. | 0burudani
|
Wakati Yanga ikiwa mgeni kwenye Uwanja wa Sokoine Mbeya dhidi ya Tanzania Prisons, Simba itakuwa mwenyeji wa Mgambo JKT Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.Yanga itashuka dimbani ikitoka kupoteza mchezo uliopita dhidi ya Coastal Union ya Tanga, ambapo ilikula kichapo cha mabao 2-0 katika mchezo uliochezwa mwishoni mwa wiki iliyopita kwenye Uwanja wa Mkwakwani, Tanga.Aidha, Yanga itashuka dimbani ikiwa na kumbukumbu ya kuifunga Tanzania Prisons mabao 3-0 kwenye uwanja huo Septemba mwaka jana.Kocha Mkuu wa Yanga Hans Pluijm alisema watafanya kila linalowezekana kuhakikisha wanaondoka na pointi tatu na wana kila sababu ya kushinda ili kujiweka katika nafasi nzuri ya kulitetea taji lao la ubingwa.Lakini wakati Yanga ikijipa matumaini hayo, Tanzania Prisons inaonekana kuwa vizuri hasa inapotumia uwanja huo wa kwao.Timu hizo zinatofautiana kwa pointi 12, Yanga ikiwa na pointi 39 ikiwa imecheza michezo 16 na Prisons ikiwa na pointi 27 na ikiwa imecheza michezo 15 kwa kuwa na kiporo na Azam FC.Yanga inahitaji ushindi kujihakikishia nafasi yake ya kutetea taji lakini kama itakubali kichapo huenda ikashuka na Azam FC kama itafanya vizuri katika michezo yake ijayo ikapanda.Kwa upande wa Simba mara ya mwisho kucheza na Mgambo mwaka jana iliibuka na ushindi wa mabao 2-0. Iwapo Simba itashinda mchezo huo itakuwa imezisogelea Azam na Yanga.Kocha wa Simba, Jakson Mayanja alisema lengo lao ni kuhakikisha wanashinda ili kulikaribia taji la ubingwa.Licha ya kuwa Simba na Mgambo JKT hutofautiana kwa pointi nyingi, sio timu ya kudharau kwani lolote linaweza kutokea. Mgambo inashika nafasi ya nane ikiwa na pointi 17 huku Simba ikishika nafasi ya tatu ikiwa na pointi 36.Timu nyingine zinazocheza leo ni Kagera Sugar dhidi ya Majimaji. Pia, JKT Ruvu yenye pointi 13 dhidi ya Mbeya City yenye pointi 14, huku African Sports ikiumana na Mwadui na Mtibwa Sugar itavaana na Toto Africans. | 5michezo
|
YAOUNDE, CAMEROON TAIFA la Cameroon limepata pigo lingine baada ya kipa wa timu ya Taifa ya wanawake, Jeanine Djomnang, kupoteza maisha juzi wakati akifanya mazoezi katika timu yake ya Femina Stars Ebolowa. Mchezaji huyo alipoteza maisha akiwa njiani wakati anakimbizwa hospitali, ambapo inadaiwa kwamba alipatwa na mshtuko wa moyo mazoezini, huku Shirikisho la Soka la Cameroon likieleza kuwa bado halijapata taarifa kutoka kwa madaktari. Wiki moja kabla ya kifo chake, kipa huyo aliwahi kulalamika anasumbuliwa na matatizo ya kifua na kwenda hospitali, ambako alipatiwa matibabu na baadaye kujiunga na timu yake. Tukio hilo ni mshtuko mkubwa kwa Taifa la Cameroon, kwani ni siku moja imepita tangu nyota mwingine wa timu ya taifa ya wanaume, Patrick Ekeng, kupoteza maisha nchini Romania wakati akiitumikia klabu yake ya Dinamo Bucharest katika mchezo wa ligi. Ekeng ambaye alikuwa na umri wa miaka 26, alianguka peke yake uwanjani bila kugongana na mchezaji yeyote katika mchezo huo zikiwa zimepita dakika saba tangu aingie akitokea benchi. Shirikisho la Soka la Cameroon, lilielezea kusikitishwa kwake na msiba huo na kudai kuwa litaungana na familia ya marehemu ambapo pia limeandaa daftari la rambirambi kwa wachezaji hao, ambalo lipo katika ofisi za makao makuu jijini Yaounde. Kabla ya msiba huo kumalizika, shirikisho hilo limetangaza tena kifo cha Jeanine ambaye amepoteza maisha akiwa na umri wa miaka 26, ambapo limeelezea kuguswa kwa kiasi kikubwa kwa kuwapoteza wachezaji hao waliokuwa wakiipeperusha vyema bendera ya taifa. Jeanine alikuwa akitarajiwa kulisaidia Taifa lake katika michuano ya Kombe la Mataifa ya Afrika kwa Wanawake, iliyopangwa kuanza kutimua vumbi Novemba 19 hadi Desemba 3, mwaka huu ambapo Cameroon ni wenyeji wa michuano hiyo. Vifo vya Jeanine na Ekeng vimewagusa wadau wengi na kuacha maswali mengi kuwa ni kwanini wachezaji wengi wanapoteza maisha kwa kuanguka bila ya kugongana na mchezaji mwenzake. Nyota wa zamani wa timu ya Taifa ya Cameroon, Marc Vivien Foe, pia alipoteza maisha uwanjani wakati akiichezea timu hiyo katika mchezo dhidi ya Colombia mwaka 2003 na kuanguka dakika ya 72 akiwa peke yake katikati ya uwanja. Ekeng ambaye alifariki dunia wiki iliyopita, naye alianguka katikati ya uwanja dakika ya 70 hali inayowafanya watu wajiulize ni kwanini matukio hayo yanatokea kwa wachezaji wa Cameroon tu. | 5michezo
|
NA BEATRICE KAIZA, DAR ES SALAAM WASANII kutoka mataifa mbalimbali wamejishindia tuzo za African Muziki Magazine Awards (Afrimma) kwa mwaka huu, ambapo kwa Tanzania wasanii watatu wamenyakua tuzo hizo. Wasanii Watanzania walioshinda tuzo hizo zilizotolewa Dallas Texas, nchini Marekani ni Dj D Ommy kutoka Clouds FM aliyeshinda tuzo ya Dj bora Afrika, tuzo ya msanii bora chipukizi Afrika 2016 imekwenda kwa Harmonize, huku msanii bora wa kiume Afrika Mashariki akitangazwa kuwa ni Diamond Platnumz. Tuzo nyingine imekwenda kwa Wakenya, Sautisol wakinyakua tuzo ya kundi bora la muziki Afrika, Akothee akishinda msanii bora wa kike Afrika Mashariki na mkali wa muziki wa Injili, Willy Paul akishinda tuzo ya ‘Best Gospel Act’. Tuzo nyingine ni ya wimbo bora wa mwaka wa msanii Tecno ‘Duro’ kutoka Nigeria, Flavour wa Nigeria akaibuka msanii bora wa mwaka, Msanii bora Afrika Magharibi ikienda kwa Olamide, huku Patrick Elis akiibuka kuwa muongozaji bora wa video za wasanii. Washindani wa mshindi katika kipengele cha msanii bora wa kiume Afrika Mashariki ni Eddy Kenzo kutoka Uganda, Jacky Gosee kutoka Ethiopia, Ali Kiba kutoka Tanzania, Jose Chameleon kutoka Uganda, Bebe Cool kutoka Uganda, Sauti Sol kutoka Kenya, Dynamq kutoka South Sudan na Diamond Platnumz kutoka Tanzania. Waliokuwa washindani wa mshindi kipengele cha msanii bora chipukizi ni Adekunle Gold kutoka Nigeria, Falz kutoka Nigeria, Locko kutoka Cameroon, Nathi kutoka South Africa, Kofi Kinaata kutoka Ghana, Humblesmith kutoka Nigeria na Harmonize kutoka Tanzania. Pia waliokuwa washindani wa kipengele cha DJ bora Afrika ni Dj Spinall kutoka Nigea, Dj Joe Mfalme kutoka Kenya, Cndo kutoka Africa Kusini, Dj Neptune kutoka Nigeria, Dj Malvado Jnr kutoka Angola, Dj Labastille kutoka Cameroon na DJ D-Ommy kutoka Tanzania. | 0burudani
|
MWANDISHI WETU-DAR ES SALAAM WAZIRI wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto,
Ummy Mwalimu amesema viongozi
wa madhehebu ya dini na waganga wa tiba asili ni nguzo muhimu katika
kutokomeza Kifua Kikuu(TB) nchini. Ameyasema hayo mwishoni mwa wiki katika ufunguzi wa mkutano
wa kwanza wa wadau wenye lengo la ushirikiano katika kutokomeza Kifua
Kikuu (TB) nchini, uliofanyika Dar es Salaam. Waziri Ummy alisema waganga wa jadi na viongozi wa dini ni wadau
muhimu katika mapambano dhidi ya TB. Alisema utafiti uliofanywa 2018 na Mpango wa Taifa wa
kudhibiti kifua kikuu na ukoma unaonyesha waganga
wa jadi wamekuwa waathirika wakubwa wa ugonjwa wa kifua kikuu. Alisema viongozi wa
dini ni kundi jingine muhimu katika
mapambano dhidi ya kifua kikuu nchini kutokana na idadi kubwa ya waumini
wanaowaamini katika kufikisha ujumbe. “Waganga wa jadi ni wadau muhimu katika mapambano ya kifua kikuu, utafiti wa
2018 uliofanywa na mpango wa taifa wa kudhibiti Kifua Kikuu na Ukoma unaonyesha
waganga wa jadi na wenyewe wamekuwa waathirika
wa kifua kikuu. “… na viongozi wa dini tunawahitaji wanaposimama katika
makanisa na katika misikiti yetu ili wawe wanawakumbusha waumini juu ya Kifua
Kikuu,” alisema Waziri Ummy. Alisema mwaka 2017 Tanzania iligundua na kuwapatia matibabu
takribani wagonjwa 75,000 ikiwa ni asilimia 44 tu ya wagonjwa wanaokadiriwa
kuugua TB. Alisema hiyo ina
maana ya kuwa wagojwa 85,000 zaidi ya
asimilia 50 hawagunduliwi na hivyo kukosa matibabu kila mwaka nchini. Pia Waziri Ummy alisema TB huathiri takriban watu milioni 10.4 duniani
kila mwaka na asilimia 25 ya wagonjwa wanatoka barani Afrika. Tanzania ni
miongoni mwa nchi 13 barani Afrika zenye kiwango kikubwa cha wagonjwa wa TB na
inakadiriwa kuwa na wagonjwa wapya wa TB
154,000 kila mwaka. Alisema wizara kwa kushirikiana na wadau wa maendeleo,
imeendelea kutoa huduma za uchunguzi na matibabu bila malipo katika vituo vya
kutolea huduma vya serikali na binafsi, hali iliyoleta mafanikio ikiwamo kuvuka
malengo ya mwaka 2018 ambako walifikiwa wagonjwa 75,845 ikiwa ni ongezeko la asilimia 22 kutoka mwaka 2015. Mganga Mkuu wa Serikali, Profesa Mohammad Kambi,
alisema Tanzania ina wastani wa wagonjwa 154,000 ambao wanatakiwa kuibuliwa na kuanzishiwa matibabu. | 3kitaifa
|
Mafanikio hayo yamechangiwa na ongezeko la makusanyo ya riba kwa asilimia 14.22 kutokana na mikopo ambayo ilikuwa kwa asilimia 10.31 hivyo kuongeza kwa kiasi kikubwa faida itokanayo na riba.Katika kipindi cha mwaka 2013, mikopo iliyotolewa kwa wateja iliongezeka na kufikia Sh trilioni 1.99 ikilinganishwa na Sh trilioni 1.80 mwaka uliotangulia.Akitangaza mafanikio ya Benki ya CRDB katika kipindi cha mwaka jana, Mkurugenzi Mkuu wa benki hiyo, Dk Charles Kimei alisema mwaka jana ulikuwa wa mafanikio makubwa na kufanya benki hiyo kuendelea kuongoza nchini kwa kuwa na rasilimali nyingi.Katika mkutano huo uliohudhuriwa na wawekezaji katika benki hiyo kutoka Uingereza, Afrika Kusini, Marekani, Kenya pamoja na wawekezaji wazawa.Akizungumza, Dk Kimei alisema rasilimali za benki ya CRDB zimeongezeka kwa asilimia 17 na kufikia Sh trilioni 3.6 katika kipindi cha mwaka jana ilinganishwa na Sh trilioni 3.07 mwaka uliotangulia.“Pamoja na ufanisi kuongezeka na kuchangia kwa kiasi kikubwa katika mafanikio ya CRDB, lakini pia mazingira mazuri ya uchumi yaliyopo hapa nchini yamekuwa na nafasi ya pekee katika ustawi wa benki hi,” alisema Dk Kimei.Alisema katika kipindi cha mwaka jana, benki iliwekeza kwa kiwango kikubwa katika kupanua mtandao wake kwa kuanzisha matawi mapya sita, vituo vinne vya huduma na mashine 66 za kutolea pesa.Pia benki ilizindua Fahari Huduma ambayo imeweza kuwavuta karibu wateja na kupunguza gharama za kutoa Huduma kwa watu wasiofikiwa na Huduma za kibenki.Akifungua mkutano huo, Naibu Waziri wa Fedha, Adam Malima alisema benki ya CRDB imeendelea kupata mafanikio makubwa katika utoaji huduma za kibenki kutokana na uongozi thabiti, lakini kwa kiasi kikubwa uchumi wa nchi ulioimarika katika kipindi hiki.“Uchumi imara umekuwa chachu ya mafanikio ya Benki ya CRDB na kwa kuwakutanisha wawekezaji wa benki hii kutoka sehemu mbalimbali duniani itatoa ushuhuda mkubwa na kuendelea kuvutia uwekezaji zaidi katika sekta ya kibenki,” alisema. | 1uchumi
|
BRUSSELS, Ubelgiji RAIS wa Kamisheni ya Nishati wa Jumuiya ya nchi za Ulaya,EU, Maros Sefcovic, amesema kwamba tayari ameshafanya mazungumzo ya awali na nchi za Urusi na Ukraine ya kuongeza mkataba wa gesi kuendelea kupitia Ukraine pindi mkataba wa sasa utakapomalizika ifikapo mwakani. Sefcovic alitoa kauli hiyo juzi katika mahojiano na Shirika la Habari la Uingereza, Reuters na akasema kuwa mazungumzo ya kina yanatarajiwa kufanyika hivi karibuni. “Tumeshafikia makubaliano ya wali na washirika wetu hao wawili, Ukraine na Urusi na tumewaarika kufanya mazungumzo ya kina,”alisema Rais huyo wa Kamisheni ya Nishati Ulaya. “Mazungumzo ya kina yatafanyika hivi karibuni na jambo na muhimu litakuwa ni kuhusu kuendelea kuagiza gesi na tunataka iendelee kupitia Ukraine mara baada ya mkataba huu kumalizika mwakani,”aliongeza, Sefcovic Alisema kuwa Rais wa Urusi, Vladimir Putin naye alishamuhakikishia kuwa Serikali ya Moscow, tayari imeshafanya mazungumzo na Ukraine ili gesi hiyo iendelee kupitia nchini humo, baada ya wiki iliyopita kukutana na Kansela wa Ujerumani, Angela Merkel. | 2kimataifa
|
MENEJA wa Mamlaka ya Usimamizi wa Bima (TIRA) Kanda ya Kati, Stella Rutaguza ameonya kampuni zinazofanya biashara ya bima na kuzitaka kuacha tabia ya kutoza ada za bima chini ya kiwango kilichowekwa na Serikali.Rutaguza ametoa onyo hilo katika kikao kilichokutanisha TIRA na mameneja na wawakilishi wa kampuni, zinazofanya biashara ya bima katika mikoa ya Kanda ya Kati ambayo ni Morogoro, Singida, Tabora na Dodoma.Amesema hatua ya baadhi ya kampuni kutoza ada za bima chini ya kiwango kilichowekwa na serikali, kinaathari za kijamii na kiuchumi na kuwa kwa kufanya hivyo ni kwenda kinyume na maadili ya fani hiyo na pia kinyume na sheria na taratibu za bima.Rutaguza amesema mamlaka yake, imebaini baadhi ya kampuni za bima kutoza ada za bima chini ya kiwango kilichowekwa na serikali, ikiwa ni kuvutia wateja na kufikia malengo waliyowekewa na kusisitiza kuwa Mamlaka itachukua hatua kali kwa kampuni ambazo zitabainika kufanya hivyo kwani huo ni uhalifu.“Huwezi ku-bargain kwenye ada za bima kama vile unauza shati dukani au kwenye mitumba, kwa kufanya hivyo ni kwenda kinyume na maadili ya fani ya bima.“Suala la kutoa ada za bima chini ya kiwango, ni hatarishi kwa sababu linaathiri kampuni za bima kwani zitafika mahali ambapo zitashindwa kumudu majukumu yake ya msingi ya kulipa madai ya bima na kulipa fidia maana itakuwa na mtaji chini ya kiwango kinachotakiwa.“Mbaya zaidi ni kuwa watu walionunua bima kwenye kampuni hizi watashindwa kulipwa madai yao pindi panapotokea matatizo na hapo tatizo la kuanza kuzungushana linaibuka, suala hili linaathari za athari za kijamii na kiuchumi na ndio maana sisi kama mamlaka tunakemea tabia ya kulipa ada za bima chini ya kiwango.”amesema.Rutaguza alisema wafanyabiashara wa bima, wanapaswa kukumbuka kuwa viwango hivyo vimewekwa baada ya kufanyiwa tathimini ya tahadhari ya majanga nchini.Aidha, Rutaguza alisema katika kaguzi wanazofanya, pia wamebaini baadhi ya kampuni za bima, mawakala na madalali wa bima ambao wamekuwa wakiuza bima ambazo hazilingani na aina ya gari.“Kuna utakaowakuta wameweka stika ya binafsi kwenye gari ya biashara, kwa mfano gari ambalo linabeba abiria linatakiwa linunuliwe bima ambayo inawalinda mpaka abiria kulingana na idadi ya abiria ambapo kila abiriwa anakatiwa bima ya shilingi 30,000 kwa mwaka na si ya gari pekee.Akichangia, Charles Balisidya ambaye ni dalali wa bima katika Kampuni ya Bima ya Phonex, aliiomba TIRA kufanya ukaguzi wa kina katika ofisi za kampuni, mawakala na madalali wa bima ili kuwabaini wale wanaolipa ada za bima chini ya kiwango.“Kuna baadhi ya kampuni kwa kutaka kuvutia wateja wamekuwa wakipunguza ada za bima hata mpaka nusu ya bei halisi lakini wamekuwa wakiingiza taarifa sahihi kwenye mfumo wa TIRAMISS. Tuwaombe TIRA wafanye ukaguzi wa kina katika suala hili” alisema. | 3kitaifa
|
Wakato joto la mechi ya watani wa jadi likiendelea kupamba moto huku mashabiki wa timu zote wakitambiana kufungana Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda amesema ulinzi utauwa wa uhakika katika mechi hiyo. Mabingwa wa kihistoria wa Ligi kuu ya Soka Tanzania bara Yanga Sc Jumapili watakuwa dimbani kukichapa na Bingwa mtetezi wa ligi hiyo Simba Sc Makonda ambaye ni miongoni mwa washauri wa bodi ya wakurugenzi ya Simba amewaambiwa mashabiki wa timu zote kuwa wasiwe na wasi wasi katika suala la usalama. Amesema yeye kama Mwenyekiti wa Kamati ya ulinzi na usalama ya mkoa wamejipanga vyema kudhibiti hali ya usalama ndani na nje ya uwanja. MAKONDA AIBARIKI KARIAKOO DERBY: Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda @baba_keagan ametaja kuwa mechi ya watani wa jadi kati ya Yanga SC dhidi ya Simba SC itafanyika saa 11 jioni huku akiwatoa mashabiki wasiwasi kuhusu ulinzi na usalama kwa maelezo kuwa wamejipanga kudhibiti hali ya usalama ndani na nje ya uwanja. Mechi hiyo itaonyeshwa LIVE Azam Sports HD. Lipia kisimbuzi chako cha Azam TV mapema upate kuona mechi bila usumbufu wa kulipia dakika za mwisho. @yangasc @simbasctanzania @hajismanara @antonionugaz #WataniWaJadi #KariakooDerby #DarDerby A post shared by Azam Sports (@azamsports2) on Mar 6, 2020 at 1:51am PST | 5michezo
|
.Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amewaagiza Wakuu wa mikoa na wilaya nchini kuhakikisha Wananchi waliokuwa wakiishi mabondeni ambao waliokolewa na kuhamishiwa kwenye maeneo salama hawarejei tena. Waziri Mkuu Majaliwa ametoa agizo hilo wakati akizungumza na Wananchi katika mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye kijiji cha Kipindimbi wilaya ya Kilwa mkoani Lindi. “Haikubaliki watu waliokuwa wakiishi mabondeni ambao kwa sasa wamehamishiwa kwenye maeneo salama kuona wamerejea tena mabondeni, Wakuu wa mikoa na wilaya hakikisheni Wananchi hao hawarudi mabondeni”, amesisitiza Waziri Mkuu. Amesema Serikali inawataka Wananchi hao kutorudi tena mabondeni lengo likiwa ni kuwanusuru na maafa ya mafuriko yanayoweza kujirudia kufuatia mvua kubwa zinazoendelea kunyesha nchini. Kwa mujibu wa Waziri Mkuu Majaliwa, Serikali inawajibika kuhakikisha Wananchi wote wanakuwa salama, hivyo ni vyema kuchukua hatua za kuwaondoa wote waishio mabondeni ili kuwaepusha na maafa yanayoweza kuwapata.Mbali na kuzungumza na Wananchi katika kijiji hicho cha Kipindimbi, pia Waziri Mkuu ametembelea vijiji vingine vilivyokumbwa na maafa hayo ambavyo ni Nambilanje wilayani Ruangwa, Nakiu na Njinjo wilayani Kilwa na Kitomanga kilichopo wilayani Lindi ili kujionea athari za mafuriko na kuwapa pole Wananchi. “Naomba mpokee salamu za pole ninazozileta kwenu kutoka kwa Rais wetu mpendwa Dkt John Pombe Magufuli alizozitoa kwa Wananchi wote waliokumbwa na mafuriko hayo kwa kupoteza ndugu zetu wapendwa pamoja na mali”, amesema Waziri Mkuu. Awali, mkuu wa mkoa wa Lindi, – Godfrey Zambi alisema kuwa mvua hizo zilizonyesha mfululizo zilisababisha maafa makubwa ambapo watu 21 walifariki dunia huku wengine 26,481 katika kaya 4,344 wakikosa makazi. Amesema mbali na kusababisha vifo, pia maeneo mbalimbali ya kutolea huduma nayo yameathirika ikiwa ni pamoja na shule, zahanati, miundombinu ya barabara, maji na mashamba ambayo yamefunikwa na maji. “Mvua hizi zilisambaa katika wilaya zote za mkoa wa Lindi, hata hivyo athari kubwa zilitokea kwenye wilaya za Kilwa kata zilizoathirika ni saba, Ruangwa kata 18, Liwale kata Tatu na Lindi kata Nne”, amefafanua Zambi. | 3kitaifa
|
NA KULWA MZEE-DODOMA NI miswada yenye ncha kali kwa nchi. Ndivyo unavyoweza kusema baada ya Serikali kuwasilisha bungeni miswada mitatu kwa hati ya dharura ambayo inalinda rasilimali za nchi. Kuwasilishwa kwa miswada hiyo kunatokana na kauli ya Rais Dk. John Magufuli aliyoitoa Juni 12, wakati akipokea ripoti ya pili ya uchunguzi wa mchanga wa dhahabu (Makinikia) iliyokuwa ikiongozwa na Profesa Nehemiah Osoro. Katika hafla hiyo, Rais Magufuli alisema suala la mikataba ya madini litapelekwa bungeni hata kama ni kwa Bunge kuongeza wiki moja ili wabunge waweze kujadili na kupitia kifungu kwa kifungu sheria za madini na gesi. Kutokana na ahadi hiyo jana Spika wa Bunge, Job Ndugai, alitangaza mabadiliko ya ratiba ya vikao vya Bunge ikiwemo kuongezwa hadi Julai 5, ili kuruhusu miswada mipya mitatu ukiwemo wa madini kujadiliwa katika Kamati za Bunge. Miswada hiyo ilisomwa kwa mara kwanza jana bungeni na Bunge lilibadilisha ratiba ya awali ya kuahirisha Bunge kwa kuongeza siku tano ambapo sasa Bunge litaahirishwa Julai 5 mwaka huu. Spika Ndugai aliitaja miswada hiyo kuwa ni Muswada wa Sheria ya Marekebisho ya Sheria mbalimbali zenye upungufu uliojitokeza wa mwaka 2017 ambao utafanyiwa kazi na Kamati ya Bunge ya Katiba na Sheria Muswada wa mapitio, masharti hasi Moja kati ya miswada ambayo iliwasilishwa jana ni ule wa Sheria ya Mapitio na Majadiliano kuhusu Masharti Hasi katika mikataba inayohusu maliasili za nchi. Muswada huo wa sheria inayopendekezwa inakusudia kuweka utaratibu ambapo wananchi kupitia chombo chao cha uwakilishi yaani Bunge kupitia na kujadili makubaliano na mikataba yote inayohusu rasilimali za nchi ambayo imefungana na Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa lengo la kujiridhisha endapo masharti, makubaliano na mikataba hiyo haikinzani na maslahi ya wananchi na taifa kwa ujumla. Muswada huo unakusudia kutekeleza masharti ya Ibara za 8, 9 na 27 za Katiba ya Jamhuri ya Muungano ambazo pamoja na mambo mengine zinampa wajibu kila Mtanzania kuhakikisha kwamba anashiriki kikamilifu kulinda mali na rasimali za nchi kwa masilahi ya Watanzania na Jamhuri ya Muungano kwa ujumla. “Kwa kuzingatia wajibu wa kila Mtanzania na kwa kutambua wajibu wa Bunge kama chombo cha uwakilishi, Sheria inayopendekezwa imelipa nguvu Bunge kupitia mikataba yote inayohusiana na maliasili za nchi ambayo imeingiwa na Jamhuri ya Muungano ilikujiridhisha kwa masharti yaliyomo katika mikataba hayo yamezingatia maslahi ya Watanzania na Taifa kwa ujumla. “Muswada huu umegawanyika katika sehemu kuu tatu. Sehemu ya I inahusu masharti ya jumla kama vile jina la sheria na kuanza kutumika kwa sheria inayopendekezwa. Sehemu ya II inalipa Bunge la Jamhuri ya Muungano nguvu za kisheria ili kutekeleza wajibu wake wa kuisimamia Serikali iweze kupitia makubaliano na mikataba yote inayohusu maliasili za nchi ambayo imeingiwa na Jamhuri ya Muungano kwa lengo la kujiridhisha na masharti yaliyomo katika mikataba hiyo. “Kwa mujibu wa masharti yanayopendekezwa katika sehemu hii, baada ya kubaini masharti hasi katika mikataba hiyo Bunge linaweza kuitaka Serikali kufanya majadiliano upya na upande wa pili wa mkataba ili kuondoa masharti hayo. “Sehemu ya III inaweka utaratibu wa namna ya kuanzisha majadiliano na upande wa pili wa mikataba ili kuondoa masharti hasi kama yalivyobainishwa na Bunge kwa mujibu wa ibara ya 6(2) ya Muswada,” inasema sehemu ya maudhui ya muswada huo. Sheria inayopendekezwa imeainisha masharti ambayo kwa taswira yake ni masharti hasi na hayapaswi kuwemo katika mikataba inayohusu maliasili za nchi. Muswada Sheria Mbalimbali wa 2017 Muswada huu unakusudia kupendekeza kutungwa kwa Sheria ya Marekebisho ya Sheria Mbalimbali ambazo ni Sheria ya Madini, Sura ya 123, Sheria ya Petroli, Sura ya 392, Sheria ya Kodi ya Mapato, Sura ya 332, Sheria ya Kodi ya Ongezeko la Thamani Sura ya 148 na Sheria ya Bima, Sura ya 394. Marekebisho yanayopendekezwa yanalenga kuimarisha mifumo ya udhibiti na uwajibikaji katika sekta ya madini na petroli. Pia marekebisho katika Sheria za Kodi na Bima yanalenga kupanua wigo wa ukusanyaji wa mapato yanayohusiana na sekta ya madini na Petroli. Muswada huu umegawanyika katika Sehemu Kuu Saba. Sehemu ya I inahusu masharti ya jumla kama vile jina na kuanza kutumika kwa Sheria inayopendekezwa, matumizi na tafsiri ya misamiati mbalimbali. Sehemu ya II na ya III ya Muswada huu unapendekeza kufanyia marekebisho Sheria za Madini ya mwaka 2010 na Sheria ya Petroli ya mwaka 2015. Malengo ya marekebisho ni kuweka masharti yatakayowezesha wananchi na Taifa kuweza kunufaika na maliasili ya madini, petroli na gesi asilia. Ili kuwezesha kuwepo kwa manufaa haya, maudhui ya mapendekezo yameweka masharti yatakayowezesha, kutambua na kuweka Umiliki wa Madini, Petroli na Gesi Asilia kwa wananchi chini ya Usimamizi wa Rais kwa niaba ya wananchi. Kutambua haki na dhamana ya Serikali juu ya bidhaa zote na masalia yanayotokana na uchimbaji, uchakataji na uchenjuaji wa madini, kuweka ulinzi mahsusi wa maeneo yote ya uchimbaji wa madini. Kutambua ushiriki wa Serikali katika shughuli zote za uchimbaji, uchakataji na uchenjuaji wa madini na ununuzi wa hisa katika kampuni za uchimbaji madini, kuweka utaratibu wa Bunge kufanya mapitio na maridhio yamikataba ya uchimbaji na uendelezaji wa madini, kufanyia mapitio madaraka ya Waziri na Kamishina wa Madini. Sehemu ya IV ya Muswada inapendekeza marekebisho ya Sheria ya Kodi ya Mapato Sura ya 332 inapendekezwa kufanya marekebisho katika kifungu cha 8 na Jedwali la Kwanza la Sheria ya Kodi ya Mapato ili kujumuisha kama sehemu ya mapato ya biashara ya faida yoyote inayopatikana kutokana na haueni ya kodi kupitia mikataba mbalimbali ya kibiashara. Ambapo katika sehemu hiyo inapendekeza kurekebisha vifungu vya 65M na 65N kwa lengo la kuondoa mgongano baina ya Sheria za Kodi na Sheria za sekta ya madini na mafuta. Mgangano huo umekuwa ukisababisha Serikali kupoteza mapato. Sehemu ya V ya Muswada inapendekeza kufanya marekebisho katika Sheria ya Bima Sura ya 394. Marekebisho yanayopendekezwa katika Sheria hiyo yanalenga kumpa nguvu za kisheria Kamishina wa Mamlaka ya Udhibiti wa Sekta ya Bima (TIRA) kuainisha viwango vya chini vya ada ya Bima (Premium) kwa aina mbalimbali za Bima zitolewazo na kampuni za Bima. Marekebisho haya yanakusudiwa kuondoa utaratibu wa sasa ambapo kila wakala wa bima hujipangia kiwango cha ada anachotaka. Sambamba na marekebisho katika kifungu cha 72 inapendekezwa kufutwa kwa kifungu cha 134 na 137 na kuboresha masharti ya kifungu cha 133 ili kuondoa kasoro zilizopo sasa katika mfumo wa ukusanyaji wa ada ya bima (Premium) kupitia kwa mawakala wa bima. Kwa mujibu wa marekebisho yanayopendekezwa, bidhaa zotezinazoigizwa nchini zitakatiwa bima na kampuni za bima za Tanzania. Katika Sehemu ya VI, ya Muswada inapendekeza kufanya marekebisho katika kifungu cha 3(3) cha Sheria ya Usimamizi wa Kodi sura ya 438 ili kurekebisha tafsiri ya kodi kwa lengo la kutambua kodi inayotokana na ongezeko la faida. Inapendekezwa kurekebisha kifungu cha 54(1) ili kuongeza aya ndogo ya (i) kwa lengo la kubainisha tarehe ya kulipa kodi inayotokana na ongezeko la faida. Sehemu ya VII inapendekeza kurekebisha Sheria ya Kodi ya Ongezeko la Thamani Sura ya 148. Kurekebisha kifungu cha 68 cha Sheria hiyo ili kuweka masharti ya kuthaminisha madini kila baada ya muda fulani kwa lengo la kupatia thamani yake halisi kwa wakati husika. Hiyo itasaidia kujua na kutambua stahili ya nchi kwa kuzingatia thamani halisi ya madini kwa wakati husika. Muswada wa Sheria ya Mamlaka ya Nchi kuhusiana na Umiliki wa Maliasili wa mwaka 2017: Muswada huu unapendekeza kutungwa Sheria ya Mamlaka ya Nchi kuhusiana na Umiliki wa Maliasili, 2017 kwa kuweka masharti yanayohusianisha misingi iliyomo katika mikataba na itifaki mbalimbali ambazo Jamhuri ya Muungano imetia saini na kuridhia. Baadhi ya masharti yanayopendekezwa katika Muswada huu yanatokana na Azimio la Umoja wa Mataifa Namba 523(VI) la Januari 12 , 1952 na Azimio Namba 626(VII) la Desemba 21, 1952, Azimio Namba 1314(XIII) la Desemba 12, 1958, Azimio namba 1515(XV) la Desemba 15, 1960 Azimio Namba 1803 (XVII) la Desemba 14, 1962, Azimio Namba 2158(XXI) la Desemba 6, 1966, Azimio Namba XXV la Desemba 11, 1970 na Azimio namba 32 la Desemba 12, 1974. Kwa kuzingatia masharti yaliyomo katika mikataba hiyo, Muswada huu unakusudia kuweka masharti yatakayohakikisha kwamba hatua yoyote inayochukuliwa kuhusu uwekezaji wa rasilimali za Taifa inatambua na kuzingatia haki ya Jamhuri ya Muungano kama Taifa huru na lenye mamlaka kusimamia na kutumia rasilimali zake kwa masilahi ya Taifa. Muswada huu unakusudia kutekeleza masharti ya Ibara ya 27 ya Katiba ambayo, pamoja na mambo mengine, inamtaka kila Mtanzania kulinda na kusimamia kikamilifu rasilimali za nchi kwa masilahi ya wananchi na Taifa kwa ujumla. Hatua zinazopendekezwa katika Muswada huu zinalenga kulinda mali na rasilimali za Taifa na kuondoa aina yoyote ya upotevu au ubadhirifu wa rasilimali za nchi. Muswada huu umegawanyika katika sehemu tatu. Sehemu ya I inahusu masharti ya jumla kama vile jina, tarehe ya kuanza kutumika kwa sheria, matumizi ya sheria na ufafanuzi wa misamiati. Sehemu ya II inaainisha mahitaji ya msingi katika kuhakikisha kwamba mamlaka ya nchi juu ya rasilimali za Taifa yanatambuliwa na kulindwa. Sehemu ya III inatambua na kulinda mamlaka ya Jamhuri ya Muungano juu ya rasilimali na inampatia mamlaka Waziri ya kutengeneza kanuni. Spika Ndugai agawa kazi Kutokana na miswada hiyo Spika wa Bunge, Job Ndugai, alisema Muswada wa Sheria ya Marekebisho ya Sheria mbalimbali zenye upungufu uliojitokeza wa mwaka 2017 utafanyiwa kazi na Kamati ya Bunge ya Katiba na Sheria inayoongozwa na Mohammed Mchengerwa. Alisema mingine miwili ambayo itafanyiwa kazi na kamati ya pamoja itakayoongozwa na Dotto Bitteko ambayo ndani yake kuna kamati nne ni Muswada wa Sheria ya Mapitio na Majadiliano kuhusu Masharti Hasi katika Mikataba ya Maliasili za Nchi wa mwaka 2017. Muswada mwingine ni Muswada wa Sheria ya Mamlaka ya Nchi kuhusiana na Umiliki wa Maliasili wa Mwaka 2017. “Kamati ya pamoja itakuwa na kamati nne ndani yake, kamati hizo ni Kamati ya Nishati na Madini, Kamati ya Ardhi, Kamati ya Sheria Ndogo na Kamati ya Sheria na Katiba. “Kwa niaba yenu nimepokea hati ya dharura kutoka kwa mheshimiwa Rais, Kamati ya Uongozi ilikaa jana (juzi) kubadilisha ratiba, Bunge litaahirishwa Julai 5 badala ya Juni 30 kama ilivyokuwa. “Miswada mitatu mipya ya sheria imeshasomwa kwa mara ya kwanza, itapelekwa katika kamati za Bunge, kamati zitafanya kazi kuanzia leo(jana) itapanga jinsi ya kukutana na wadau mbalimbali, kisha taarifa itawasilishwa bungeni. “Kanuni inaeleza kwamba hati ya dharura itakayoletwa na Rais itakuja hati yenyewe yenye saini yake. Hati ya dharura imekuja kuna haja ya kulifanyia jambo hili kazi, tulijadiliana na kamati ya uongozi tukakubaliana suala hili lisonge mbele. “Wakati Rais Magufuli akipokea ripoti ya pili ya makinikia, kwa niaba yenu nilikubali kama kuna mambo yenye maslahi mapana kwa nchi tutayafanyia kazi,”alisema. Ndugai alisema kuna haja kwa Bunge kuwa na nafasi fulani katika masuala ya maadini na gesi ili kuzuia nchi kutumbikia katika mikataba mibovu. Hata hivyo Mbunge wa Kibamba, John Mnyika (Chadema) alipoomba mwongozo alipinga miswada hiyo mitatu mipya kuwasilishwa kwa hati nya dharura badaa yake alipendekeza hati hiyo iondolewe. Alisema kazi ya Bunge ni kutunga sheria na kwamba wabunge wawakilishi wa wananchi hivyo aliomba ijadiliwe katika Bunge lijalo ili wapate muda wa kukusanya maoni kwa wanaowawakilisha. “Hii miswada mitatu kwa umuhimu wake na maslahi yake kwa wananchi, sisi wawakilishi tulitakiwa kukutana na wananchi, ni bora ikasomwa leo kwa mara ya kwanza hati ya dharura ikaondolewa, miswada ikaletwa katika Bunge lijalo. “Kwa maelezo uliyotoa mheshimiwa Spika, wadau wataitwa kwa dharura wafike Dodoma kujadili, sisi wabunge vile vile, miswada mitatu inaletwa tuichaambue, mheshimiwa spika huu ni mtego wa kutufanya tushindwa kuishauri Serikali kwa kazi yetu ya kibunge,” alisema Mnyika. Akitoa maelezo ya Serikali Waziri wa Sera, Bunge, Kazi, Vijana na Walemavu, Jenista Mhagama alisema masharti ya kutunga sheria na masharti ya jumla yamewekwa katika fasihi ya nane ya kanuni za Bunge, masharti yameongezwa na kanuni ya 80 na kanuni nyinginezo. “Miswada ambayo imeletwa imekuja kwa hati ya dharura, ili Bunge liridhie kama miswada hii inastahili kujadiliwa na Bunge ama la, kanuni ya 80(4) inasema muswada wowote wa dharura hautaingizwa katika shughuli za Bunge bila kuwa na hati iliyowekwa sahihi na Rais kuthibitisha kwamba muswada huo wa dharura. “Kanuni zinaendelea kusema iwapo kamati inaona muswada wa sheria wa Serikali uliowasilishwa kwa hati ya dharura haustahili kamati hiyo ya uongozi itaishauri Serikali. “Kanuni zinaendelea kusema, muswada wowote uliokabidhiwa kwako spika utaonekana unastahili ama laa, utatoa picha baada ya kujadiliwa na kamati. “Sisi kama Serikali tumeshatimiza masharti yote ndani ya Bunge lako tukufu, tumeshakamilisha hatua zote za kufikisha miswada hiyo kwa hati ya dharura,”alisema Mhagama. Alisema wanaoweza kulishauri Bunge baada ya kuona uzito wa kazi iliyoletwa na Serikali ni kamati husika itakayopewa kazi ya kujadili miswada hiyo. | 3kitaifa
|
ESTHER MBUSSI-KYELA UJENZI wa Meli ya abiria ya MV Mbeya II, itakayofanya safari zake katika Ziwa Nyasa, unatarajiwa kukamilika Septemba. Meli hiyo iliyogharimu Sh bilioni 9.1, yenye uwezo wa kupakia mizigo tani 200 na abiria 200 kwa wakati mmoja, pia inatarajiwa kuwaondolea changamoto ya usafiri abiria wanaoishi katika Wilaya ya Kyela mkoani Mbeya na Ziwa Nyasa kwa ujumla. Akizungumza na waandishi wa habari katika Bandari ya Itungi, wilayani Kyela jana, Meneja wa Bandari za Ziwa Nyasa, Abeid Galus, alisema kukamilika kwa meli hiyo ya abiria itaenda kuondoa adha ya usafiri ziwani kwa sababu kwa sasa hakuna chombo chochote cha kuaminika kinachofanya kazi ziwani. “Watu wengi wamekuwa wakitumia maboti au mashua, lakini hakuna chombo madhubuti kinachofanya kazi ziwani, kwa hiyo ujio wa meli ya MV Mbeya II unaenda kuondoa changamoto hiyo ambayo imekuwepo kwa muda mrefu. “Ziwa hili ni hatari kidogo kwani lina mawimbi makubwa, kwa hiyo inaenda kumarisha usalama wa mizigo na abiria wanaokwenda sehemu mbalimbali,” alisema. Galus alisema ujenzi wa meli hiyo ulianza Julai mwaka juzi chini ya Kampuni ya Songoro Marine na umefikia zaidi ya asilimia 82 kwa hatua ya kufunga mitambo, kuweka vyumba, kufunga viti na umaliziaji. Akizungumzia meli zilizopo katika ziwa hilo kwa ujumla, alisema hivi sasa lina meli tatu zikiwamo mbili za mizigo na moja ya abiria. Alizitaja meli hizo za mizigo kuwa ni MV Njombe na MV Ruvuma ambazo kila moja ina uwezo wa kubeba tani 1,000 na tayari zimeshakamilika na zimeanza kufanya kazi tangu Julai mwaka juzi kwa ukanda wa Ziwa Nyasa na MV Mbeya II ya abiria. “Hadi sasa meli hizo zimeshafanya safari saba zikiwamo nne za majaribio na tatu za kibiashara ambazo inaendelea nazo,” alisema Galus. Pamoja na mambo mengine, Galus alisema uwepo wa meli hizo mbili za mizigo na matarajio ya kuanza kazi kwa meli ya abiria ya MV Mbeya II, utarahisisha shughuli za usafirishaji katika mwambao wa Ziwa Nyasa na kuboresha uchumi kwa jamii zinazoishi katika miji ya pembezoni mwa ziwa kwa kuongeza wigo na mwingiliano wa kibiashara na kutoa ajira kwa wakazi wa maeneo hayo. Aidha, alisema mradi mzima wa meli hiyo na miundombinu mingine inayoendelea katika bandari mbalimbali za Ziwa Nyasa, hususani Itungi na Kiwira, itazifanya Ziwa Nyasa kuanza kujitegemea kiuchumi tofauti na sasa ambapo inategemea ruzuku kutoka serikalini. | 3kitaifa
|
MWENYEKITI wa Kamati ya Tanzania Safari Channel, Profesa Faustin Kamuzora amesema kwamba wadau wa utalii nchini wamekubaliana kutoa bajeti ya Sh Bilioni tano ili kufanikisha uendeshaji wa televisheni hiyo ya serikali mahususi kwa kutangaza utalii na vivutio vyake hapa nchini.Akizungumza jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki, Profesa Kamuzora ambaye pia ni Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera na Uratibu) alisema fedha hizo zitatumika ndani ya miezi sita katika kununua vifaa, kuweka wataalamu na kununua vipindi. Aliongeza kwamba ripoti ya kamati hiyo juu ya utekelezaji wa maagizo ya serikali itakabidhiwa kwa Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa Januari 2 mwakani.“Kwa sasa mpaka miezi sita ijayo ili kuweza kufanikisha mipango ya uendeshaji wa kituo hicho cha televisheni tunahitaji kama bilioni tano ambapo kwenye kikao chetu wadau wamekubali kutoa kiasi hicho, TBC tayari ilikuwa na bajeti yake na mchango wao pia ni zaidi ya bajeti kwa kuwa wao wanaendesha televisheni hiyo,” alisema.Mwenyekiti huyo aliweka wazi kwamba kwa sasa runinga hiyo haina maudhui ya kutosha lakini wadau wamejipanga ili kuhakikisha kwamba ndani ya miezi sita suala hilo linapatiwa ufumbuzi ambapo kutakuwa na maudhui ya kutosha.Kuhusu ajira, Profesa Kamuzora alisema kwamba kuna watu wataajiriwa na watafanya kazi kwa kushirikiana na wafanyakazi wa TBC, pia aliongeza kwamba baadhi ya vipindi vitanunuliwa kutoka kwa makampuni ya nje.Profesa Kamuzora aliongeza kwamba pamoja na wataalamu hao watakoajiriwa, TBC itaendelea kuwatumia watumishi wake kutafuta maudhui ya televisheni hiyo wakati wanapokuwa katika utekelezaji wa majukumu mengine ya kikazi. | 3kitaifa
|
Subsets and Splits
No community queries yet
The top public SQL queries from the community will appear here once available.