text
stringlengths
1k
24.2k
label
class label
6 classes
NAIBU Waziri Ofi si ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Dk Mary Mwanjelwa amewataka watumishi wa Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma kufanya kazi kwa weledi itakayoisaidia Serikali kupata watumishi wenye sifa katika ajira.Akizungumza wakati alipotembelea ofisi za sekretarieti hiyo Dar es Salaam jana, mbali na kuipongeza kutokana na juhudi inazozifanya kufanikisha mchakato wa ajira za watumishi mbalimbali serikalini, alisema kimsingi weledi wa kazi kwa watumishi hao pia utaisaidia serikali kuepuka kupata waajiriwa wasio na sifa pale inapowahitaji.Dk Mwanjelwa alisema mwenendo mzuri wa kazi kwa watumishi na utasaidia kuleta tija kwa taifa kutokana na ugumu uliopo katika mchakato wa kuwapata watumishi wenye sifa suala ambalo endapo kama halitosimamiwa vizuri linaweza kuleta madhara makubwa katika taifa.“Mfanye kazi kwa kuzingatia uadilifu, lakini pia mpango mkakati mlionao unapaswa kuendana na utekelezaji wa malengo mbalimbali mliyojiwekea na mnayoitekeleza, jambo ninaloamini kuwa ndiyo msingi na uhai wa kazi kwa watumishi,” alisema Dk Mwanjelwa aliyeteuliwa hivi karibuni kushika wadhifa huo.Aidha, alisema uwepo wa chombo hicho kinachofanya kazi ya kuwatafuta watumishi wanaoenda kufanya kazi serikali, kimeleta manufaa makubwa ikiwemo kudhibiti wimbi la watumishi wasio na sifa za kuajirika wakiwemo wenye vyeti vya kughushi jambo liliiepushia serikali hasara.Alisema ili ifanye kazi zake kitaalamu zaidi, inapaswa kuongeza maboresho ya mfumo wake wa kielektroniki katika mchakato huo wa ajira ili kupunguza malalamiko ya wananchi wanaoomba nafasi za kazi kupitia mfumo huo.Katibu Mtendaji wa sekretarieti hiyo, Xavier Daudi mbali na kubainisha majukumu mbalimbali yanayofanywa na sekretarieti hiyo, alisema mchakato wa kuwapata watumishi wenye sifa za kufanya kazi serikalini una changamoto nyingi na kwamba uwepo wa taasisi hiyo umesaidia kutoa matokeo chanya.Daudi alisema katika mchakato wake wa kuhakikisha wanasimamia eneo hilo la ajira, wamebaini vyeti feki 2,103 vilivyokuwemo katika ajira, hatua aliyodai uwepo wao katika utumishi ulikuwa hasara kwa serikali.Aidha, alisema ili kufikia azma ya serikali, kuna kila sababu ya kumaliza changamoto ya uwepo wahitimu wasio kutoka vyuo mbalimbali ambao wengi wao hujitokeza kuomba ajira wakijua wazi hawana sifa zinazohitajika.
3kitaifa
MWANDISHI WETU-DAR ES SALAAM MATUMIZI ya zebaki katika uchimbaji wa madini  umeelezwa kuwa hatarishi kwa afya ya binadamu  hasa kwa watumiaji ambao ni wachimbaji wadogo wa madini pamoja na mazingira yanayoizunguka eneo husika. Akizungumza wakati wa kufunga maadhimisho ya Siku tatu ya miaka 50 ya taaluma ya Jiolojia  mwishoni mwa wiki jijini Dar es Salaam, Waziri wa Madini, Doto Biteko, alisema wizara imeingia mkataba unaozuia matumizi ya zebaki duniani kwani  ni kemikali ambayo si rafiki kwa afya ya mwanadamu pamoja na Mazingira yanayozunguka. “Saidieni katika kuhakikisha umoja wenu unasaidia taifa hasa katika kutunza rasilimali zetu. Tuungane na serikali kuhakikisha madini yetu yanachimbwa kihalali huku tukizingatia usalama wa wachimbaji, watu wanaowazunguka na mazingira kwa ujumla ili kuleta tija kwa nchi yetu,” alisema. Alisema jiolojia ni moja ya taaluma inayogusa karibia nyanja zote za maisha na kuwaomba wanajiolojia kushirikiana na serikali katika kuhakikisha mbadala wa zebaki unasisitizwa kama njia moja wapo ya kupunguza athari ambazo zingepelekea uharibifu wa mazingira. Waziri Biteko alisema taaluma ya jiolojia ni muhimu sana hasa katika sekta ya madini kwani  sekta  hiyo  ni muhimu kwa ajili ya uchumi wa nchi  hivyo kuna kila sababu ya wanajiolojia kufanya kazi zao kikamilifu na kuunga mkono azma ya Serikali ya Awamu ya Tano ya kujenga Uchumi wa Kati na viwanda ifikapo 2025. “Nendeni mkawe chachu ya mabadiliko ya sekta hii kwa manufaa ya nchi yetu na sio kwa manufaa binafsi. Mkawe waaminifu katika kazi zenu bila hivyo mtakua mnakwamisha watanzania wenzenu hasa wale wanaojipinda kuhakikisha wanapata mitaji ya kuwawezesha kufanya uchimbaji wa madini kikamilifu,” alisema Biteko. Aidha alisema NEMC watatangaza kipindi cha mpito juu ya matumizi ya Zebaki na kuwataka wadau kutoa ushirikiano stahiki. Naye Mkurugenzi Mkuu wa Baraza la Taifa la Uhifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC), Dk. Samuel Gwamaka alisema matumizi ya zebaki katika uchimbaji wa madini ni hatari kiafya na serikali haiwezi kuacha watu wake wakapoteza maisha kwasababu yakupata faida. Alisema  serikali ya Awamu ya Tano chini ya uongozi wa Rais Dk. John Magufuli ina lengo la kuwafanya wachimbaji wadogo kukua na kuwa wachimbaji wakubwa.
3kitaifa
RAMADHAN HASSAN-DODOMA SERIKALI imesema kasi ya viongozi kutoa taarifa zao kupitia fomu ya matamko ya mali na madeni ni nzuri  huku Kiongozi wa Kambi Rasmi ya  upinzani bungeni, Freeman Mbowe akitajwa kuwa ni mfano wa kuigwa katika zoezi hilo. Imeelezwa kuwa katika kipindi cha 2018 jumla ya viongozi 15,303 walirejesha fomu za maadili ambao ni sawa na asilimia 98 ya viongozi 15,552 ya viongozi waliotakiwa kurejesha fomu hizo. Pia Serikali imewataka viongozi ambao wanarejesha fomu hizo kuhakikisha wanazipeleka wenyewe ili kulinda siri zao. Hayo yalielezwa jana Jijini hapa na Kamishina wa Tume ya Maadili ya viongozi wa umma, Harold Nsekela wakati akizungumza na Waandishi wa Habari kuelekea kilele cha maadhimisho ya siku ya Maadili na Haki za Binadamu. Aidha,alisema kila tarehe ya mwisho ya mwezi Desemba huwa ni lazima kwa viongozi wa umma kutoa taarifa za madeni na mali zao jambo ambalo wengi wamekuwa wakilitekeleza kwa kusukumwa. MBOWE ATAJWA Kamishna huyo alisema Mbowe ni mmoja  ya watu wanaotakiwa kuigwa  katika zoezi la  urejeshaji wa fomu za maadili ya umma. Alisema licha ya kiongozi huyo kuwa Gerezani lakini aliandika barua akiomba mara baada ya kutoka ndio apeleke taarifa zake. “Nitawapa mfano hai mnajua kwamba Mbowe kuna wakati alikuwa ndani wakati matamko haya yanarudishwa lakini alipokuwa ndani kule rumande alituandikia barua kwamba jamani siwezi kurejesha hiyo fomu kwa sababu sehemu niliyopo siwezi kuandika tuliipokea. “Alipotoka alijaza tamko akatuletea,nadhani mmenielewa alituandikia barua tukaipokea alipotoka,”alisema Alisema kwa mujibu wa sheria, ni kosa kwa kiongozi kutojaza fomu za maadili kwani jambo hilo lipo kwa mujibu wa sheria hivyo wanaoshindwa kurejesha, wanakuwa wamekiuka maadili. ATAKA WAREJESHE KWA MKONO Vilevile Kamishana huyo aliwataka viongozi mbalimbali ambao wamekuwa wakirejesha fomu hizo wazirejeshe wenyewe kwa mkono ili kutunza siri. “Kwa hiyo unatakiwa wewe mwenyewe kiongozi ndio ulete hilo tamko na ninashauri ulete kwa usalama wa siri zako lile tamko ni la kwako kiongozi unachoandika mule ‘information’ ni za kwako kama kutakuwa na ukiukwaji wewe ndio utawajibika. “Wewe kama kiongozi unampa mtu mwingine kwa usalama wako lete mwenyewe siri zikivuja utamlalamikia nani utakuja kwetu kusema zimevuja? Viongozi wenzangu naomba pokeeni ushauri leteni wenyewe ili kutunza siri,”alisema. MKUCHIKA NA VIONGOZI KUWEKA WATEULE WA RAIS NDANI Kwa upande wake,Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Utumishi na Utawala bora, George Mkuchika alisema maadili kwa viongozi ni jambo lisilohitaji mjadala kwani Serikali imeendelea kuwa macho na kuwamulika wote ambao wanakiuka maadili. Mkuchika pia alisema kuna baadhi ya watu wanashindwa kutumia nafasi zao na badala yake wamekuwa ni watu wa kuwaweka ndani viongozi wa ngazi za chini jambo ambalo amekuwa akilipigia kelele. “Kwa sasa tunaanza kuwashughulikia hata polisi ambao wanakubali kuweka watu ndani, hivi unawezaje kukubali kiongozi amuweke ndani mtu bila kukupa maadishi, nawaambia tutawashughulikia watoa amri na wale polisi ambao wanakurupuka na kuwaweka watu hao,” alisema Mkuchika. MPANJU NA UFUKUZAJI WATU Naye, Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Katiba na Sheria, Amos Mpanju, alisema suala la watu kufukuzwa kazi bila kufuata utaratibu siyo jambo jema lakini akatetea maamuzi ambayo hutolewa na Rais kwa kuwatumbua watu kwamba yupo sahihi. Mpanju alisema ili mtu afukuzwe ni lazima kuwepo na sababu na nafasi ya kusikilizwa kwanza, lakini kwa kiongozi mkuu wa nchi hilo ni jambo la kawaida maana ndiyo mwenye uamuzi wa mwisho.
3kitaifa
Kwa mujibu wa taarifa ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) iliyotumwa kwa vyombo vya habari jana, Kamati ya idara hiyo iliyokutana Aprili 20, mwaka huu huko Zurich, Uswisi, ilitumia Franc 500 (sawa na Sh 1,145,500) hivyo Simba pia imeagizwa kuzilipa, ikiwa ni gharama za kikao cha kufuatilia utekelezaji sakata la mchezaji huyo, raia wa Kenya.Simba imeelezwa kupuuza kumlipa mchezaji Donald Musoti Omanua kwa wakati tangu mkataba wake uvunjwe. Musoti aliyesajiliwa na Simba msimu wa 2014/15 na kuachwa alilalamikia FIFA ambayo iliona ana hoja na hivyo Simba kutakiwa kumlipa dola 29,250 (sawa na Sh milioni 62.8) na kiasi kingine anachodai ni Dola 600 (Sh 1,290,000) zilizobaki katika usajili ambapo jumla yake ni Sh milioni 64.2.Pia Musoti anamlipa Mwanasheria wake dola 2,000 (Sh milioni 4.3 ) kwa ajili ya kusimamia kesi hiyo. Kwa mujibu wa taarifa hiyo, Felix Majani ambaye ni Mwanasheria wa Musoti, ambaye pia ni mmoja wa wanasheria wa Fifa, alifungua kesi katika shirikisho hilo kuwashitaki Simba kwa kukiuka makubaliano ya mkataba na mteja wake.Kwa kosa hilo, Simba inatakiwa kulipa faini ya kiasi hicho cha fedha ndani ya siku 30 kuanzia tarehe ya kupokea barua hiyo ya Fifa iliyoandikwa Mei 3, mwaka huu na kufika nchini Mei 6, mwaka huu.Katika barua hiyo ambayo TFF ina nakala yake, Simba imepewa amri ya kuhakikisha inalipa na isipotekeleza agizo hilo mara moja itakatwa pointi tatu katika mechi zake za Ligi Kuu Tanzania Bara.Fifa imekwenda mbali zaidi ikisema ikiwa klabu hiyo haitalipa katika muda uliopangwa yaani siku 30 kutoka sasa, itaishusha Simba daraja kutoka Ligi Kuu Tanzania Bara hadi Ligi Daraja la Kwanza au zaidi.Kwa upande wake, TFF imeagizwa kuhakikisha uamuzi huo unasimamiwa vema utekelezwaji wa maagizo hayo vinginevyo itachukuliwa hatua stahiki, ikiwamo kuiondoa Tanzania katika mashindano ya kimataifa.
5michezo
Ramadhan Hassan BUNGE limeelezwa kuwa Wizara ya Kilimo ipo katika hatua za mwisho kuwasilisha bungeni mapendekezo ya mabadiliko ya Sheria ya Maendeleo ya Ushirika yatakayoendana na mahitaji ya sasa. Kauli hiyo ilitolewa bungeni jana na Naibu Waziri wa Kilimo, Hussein Bashe wakati akijibu swali la Mbunge wa Mbinga Mjini, Martini Msuha (CCM) ambaye alitaka kujua kuwa Serikali ina mpango gani wa kurekebisha Sheria ya Vyama vya Ushirika ili kuondoa mapungufu yaliyopo. Akijibu swali hilo, Bashe alisema mabadiliko hayo yatahusisha mfumo na muundo wa uongozi ili kuendana na mahitaji ya teknolojia na kuleta ushindani wa kibiashara. “Tunaelewa kuwa ushirika ni dhana ya hiari, lakini Serikali ni msimamizi mkuu wa vyama vya ushirika pale ambapo viongozi wake au vyama vyenyewe havitekelezi malengo yaliyokusudiwa na ushirika. “Tunakiri vyama vinakabiliwa na changamoto za kiutendaji, usimamizi, viongozi kutokuwa waadilifu na mapungufu ya kimfumo ya uendeshaji wa vyama vya ushirika hapa nchini,” alisema Bashe. Aidha, Bashe alisema vipo baadhi ya vyama vya ushirika ambavyo vinafanya vizuri. “Mfano, Chama cha Ushirika cha Chai Mkonge, Mafinga na Chama Kikuu cha Ushirika Kahama (KACU), ushirika ndicho chombo cha kuwaletea wananchi maendeleo ya kiuchumi kwa kuwaunganisha wakulima ili kuwa na nguvu ya pamoja katika kutoa huduma za ugani, upatikanaji wa pembejeo na kutafuta masoko ya mazao,” alisema Bashe. Hata hivyo, alisema Ilani ya Uchaguzi ya CCM mwaka 2015 – 2020 (Ibara ya 22 (g)(iv) na 86 (a), inaelekeza kuifanyia mapitio sera ya vyama vya ushirika na kusimamia utekelezaji wa Sheria ya Vyama vya Ushirika na upatikanaji wa takwimu zitakazosaidia kuandaa mipango. “Nyingine ni kuleta mageuzi katika sekta ya ushirika na kuimarisha uchumi wa taifa na kuviimarisha vyama vya ushirika kuwa na uwezo wa kutafuta masoko ya mazao ya wakulima ya ndani na nje kwa kuweka mfumo madhubuti wa ukusanyaji, uchambuzi na uenezaji wa taarifa za masoko na kutoa elimu juu ya uongezaji thamani na biashara,” alisema Bashe.
3kitaifa
AWAMU ya pili ya ujenzi wa reli ya kisasa kwa kiwango cha kimataifa kwa kipande cha Morogoro - Makutupora, imeanza kwa kasi huku nguvu ikielekezwa katika sehemu korofi , hasa zenye athari za mara kwa mara nyakati za mvua katika baadhi ya maeneo ya mikoa ya Morogoro na Dodoma.Mkoani Morogoro, maeneo korofi yapo zaidi wilayani Kilosa katika Mto Mkondoa unaoathiri miundombinu, makazi na hata mashamba ya watu, wakati kwa upande wa Dodoma, athari za mara kwa mara katika eneo la Gulwe, wilayani Mpwapwa.Umbali kati ya maeneo hayo `sugu’ mawili ni takribani kilometa 83. Akizungumza wakati wa ukaguzi wa awamu ya pili ya mradi huo jana, Meneja wa Mradi wa reli ya kisasa ya SGR kwa kipande cha Morogoro-Makutupora, Faustine Kataraia alisema kutokana na jiografia ya maeneo hayo, maeneo yenye milima yatachongwa, mengine kutengenezwa mahandaki ili kuruhusu reli kupita ndani ya milima kwa umbali wa takribani kilometa moja.“Kama hapa Kilosa, athari za Mto Mkondoa zinafahamika na mara nyingi ziliharibu miundombinu ya reli kiasi cha kufanya nyakati za mvua safari ziahirishwe mara kwa mara. “Sasa, kwa mradi huu mpya na wa kimataifa wa reli ya kisasa ya SGR, athari za mafuriko zitabaki kuwa historia kwani reli zitapitishwa mbali na Mto Mkondoa ambao ni moja ya sehemu korofi sana, ni eneo kama la kilometa 83 kati ya Kilosa na Gulwe, wilayani Mpwapwa.“Hivyo njia ya reli itahamia milimani na hii inamaanisha kwamba tutakuwa na madaraja makubwa, ya kawaida, makalavati, lakini pia tutakuwa na tunnels (mahandaki) kama nne. Hizi tunnels zitakazokuwepo zitakuwa na urefu wa jumla ya kilometa 2.7, lakini refu zaidi litakuwa na takribani meta zaidi ya 800 hadi 900, yaani karibu kilometa moja, hii itatobolewa chini ya mlima na kuibukia katika daraja la juu linalopita katika mto Mkondoa kwa umbali wa kilometa moja na kuingia tena katika mlima mwingine,” alisema.Mhandisi huyo mkongwe alisema tayari kazi za kuchoronga milima hiyo na usanifu mwingine zinaendelea. Kazi nyingine zinazoendelea katika mradi huo uliofikia asilimia 4.5 tangu ukabidhiwe kwa mkandarasi, kampuni ya Yapi Merkezi ya Uturuki Februari mwaka huu, ni pamoja na kusafisha eneo la ujenzi, kukata udongo usiohitajika na kujaza vifusi, uthamini wa maeneo yatakayopisha mradi na kadhalika.Aidha, mkandarasi ambaye pia anafanya kazi hiyo katika kipande cha Dar es Salaam- Morogoro kilichokamilika kwa zaidi ya asilimia 36, ikiwa ni pamoja na kutandaza mataruma na reli, anaendelea kuongeza vifaa vya kazi na wafanyakazi katika mradi wa awamu ya pili unaotarajiwa kukamilika ndani ya miezi 36 kuanzia Februari mwaka huu.Mitambo ya kusaga mawe kwa ajili ya kokoto imeshafungwa katika eneo la Kimambila, wilayani Mvomero na ina uwezo wa kuzalisha tani 300 za kokoto kwa saa. Dhamira ya mkandarasi ya kufanya kazi usiku na mchana ili zipatikane tani 6,000 kila siku. “Pia kwa sababu reli yetu itatumia umeme, unafanyika ujenzi wa njia maalumu ya umeme kwa ajili ya mradi.Upande wa Morogoro – Makutupora kutakuwa na vituo saba vya kupozea umeme utakaopozwa kutoka Kilovoti 220 hadi kilovoti 25,” alisema Kataraia. Kati ya Morogoro na Makutupora kunatarajiwa kuwa na stesheni za Mkata, Kilosa, Kidete, Igandu, Dodoma Mjini, Bahi na Makutupora. Awamu ya pili ya mradi itakuwa na jumla ya kilometa 336 za njia kuu na kilometa 86 za njia ya kupishania treni, jumla yote ni kilometa 422.Hizi zikiunganishwa na jumla kilometa 300 za awamu ya kwanza kati ya Dar es Salaam na Morogoro, awamu hizi mbili zitakuwa na jumla ya kilometa 722. Mradi huo uliogawanywa katika vipande vitano, hadi kukamilika unatarajiwa kuwa wa kilometa 1,219 kutoka Dar es Salaam hadi Mwanza. kipande cha kwanza ni kutoka Dar es Salaam hadi Morogoro kitakachogharimu Sh trilioni 2.7.“Kipande kingine ni kutoka Morogoro hadi Makutupora chenye urefu wa kilometa 422 ambacho kitagharimu Sh trilioni 4.4, Makutupora hadi Tabora kilometa 376.5, Tabora hadi Isaka kilometa 162.5 na Isaka hadi Mwanza kilometa 311.25,” anafafanua Mkurugenzi Mkuu wa TRC, Masanja Kadogosa na kwamba awamu ya kwanza ya mradi huo wa reli kutoka Dar es Salaam hadi Makutupora unagharimu Sh trilioni 7.1.Akiweka jiwe la msingi la ujenzi wa mradi huo Aprili mwaka huu, Rais Magufuli alisema ili nchi yoyote iweze kujitegemea, ina wajibu wa kumiliki vitu muhimu kama reli, bandari, nishati, barabara, mawasiliano na vingine. Aliongeza kuwa, ujenzi wa reli ya kisasa utaongeza tija na ufanisi katika usafiri wa reli nchini kwani utarahisisha usafirishaji wa mizigo na abiria.Mathalani, safari kati ya Dar es Salaam na Mwanza inayotumia saa 36 kwa usafiri wa reli ya kawaida, sasa itapungua mara nne na kufikia saa 7 hadi 9 tu. Dar es Salaam na Morogoro safari yake itakuwa chini ya saa 1:30 wakati kwenda Dodoma hazitazidi saa 3. Kwa upande wa biashara, inatarajiwa kuimarisha biashara kati ya Tanzania na nchi jirani za Burundi, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC), Rwanda, Uganda, Zambia na kadhalika ambazo hazina bahari, hivyo kutegemea kusafirisha mizigo kupitia bandari ya Dar es Salaam.Treni za mizigo zinatarajiwa kubeba tani milioni 17 kwa mwaka. Hii, si tu itapunguza uharibifu wa barabara kutokana na malori ya mizigo, lakini itaongeza pia kasi ya biashara nchini na nchi za jirani pia. Reli ya kisasa ya Tanzania itakuwa na kasi ya kilometa 160 kwa saa, hivyo kuifanya kuwa ya aina yake kwa reli za masafa marefu barani Afrika.Ni ya mizigo na abiria na ina urefu wa kilomita zaidi ya 722 pamoja na njia za kupishania kutoka Dar es Salaam –Morogoro mpaka Dodoma ukitoa njia za kupishania ni zaidi ya kilomita 500 kutoka Dar es Salaam – Dodoma huku ikiwa ni ya mizigo na abiria”. Katika nchi tisa zenye miradi ya SGR barani Afrika, Afrika Kusini, Morocco na Tunisia wamejenga reli ambazo ni fupi zenye urefu wa kilomita 80 mpaka 100 zina kasi kubwa ambayo ni kilomita 200 kwa saa zikiwa treni maalumu kwa abiria tu.
3kitaifa
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Isack Kamwelwe, ametoa miezi mitatu kwa Wakala wa Ufundi na Umeme (TEMESA) kutopeleka magari ya Serikali kwenye karakana binafsi kwani Wakala unajitosheleza kwa kuwa na wataalamu na vifaa vya kutosha.Kamwelwe, amesisitiza kwa Wakala huo kuhakikisha unatengeneza magari kwa bei nafuu na muda na mfupi ili kupunguza malalamiko kutoka kwa wateja wao.Waziri Kamwelwe ametoa agizo hilo jijini Dar es Salaam katika kikao kazi na uongozi pamoja na wafanyakazi wa Wakala huo ambapo pamoja na mambo mengine alikagua vitendea kazi vya kisasa vilivyofungwa katika karakana ya MT. Depot iliyopo jijini hapo."Ninyi ni taasisi ya Serikali fanyeni vitu viwe nafuu na mtengeneze kwa viwango ili watu wafurahie huduma zenu", amesisitiza Waziri Kamwelwe.Aidha, ametoa wito kwa Wakala huo kutoa ushauri wa magari ya Serikali kwa umahiri na weledi na kutokubali kutengeneza magari ya Serikali endapo gari hilo litaonekana gharama yake ni sawa na kununua gari nyingine. Waziri Kamwelwe ameupongeza Wakala huo kwa kupunguza gharama za kutengeneza taa za barabarani ambazo zinatumia mfumo wa dakika."Wakala umetumia kiasi cha shilingi milioni 150 katika kitengeneza taa hizo badala ya milioni 250 na tayari zimeanza kufungwa katika mikoa mbalimbali ikiwemo mkoa wa Morogoro" amesema Waziri Kamwelwe.katika bajeti ya Serikali ya mwaka wa fedha 2019/20 Waziri Kamwelwe amefafanua kuwa Serikali imetenga kiasi cha Shilingi milioni 800 kwa ajili ya kununua boti za uokoaji kwa ajili ya kutoa huduma kwa wananchi kwa urahisi katika visiwa vya Ukerewe (Ilugwa, Nafuba na Gana).Awali akitoa taarifa ya utendaji kazi wa TEMESA kwa Waziri huyo, Mtendaji Mkuu wa TEMESA, Japhet Masele, amemueleza kuwa Wakala umejipanga kipindi cha mwaka wa fedha 2019/20 kuanzisha karakana katika ngazi za Wilaya ikiwemo Wilaya ya Kahama, Simanjiro, Same, na Chato lengo likiwa ni kupeleka huduma karibu na wateja hasa kwa walio mbali na karakana za mikoa.Ameendelea kueleza kuwa hadi sasa Wakala umeshafanya uwekezaji wa shilingi bilioni 66 kwa ajili ya kununua vivuko 18 na hivyo kufanya kufikia jumla ya vivuko 31 na boti ndogo tano hapa nchini.Kuhusu kukamilisha ujenzi wa vivuko nchini Masele amesema kuwa tayari wakala umekamilisha ujenzi wa kivuko kipya cha MV Mwanza kinachotoa huduma eneo la kigongo-Busisi, ujenzi wa miundombinu katika kivuko cha Lindi Kitunda na inaendelea kukamilisha ujenzi wa Kivuko cha Kayenze- Bezi kitakachotoa huduma kati ya Kayenze na kisiwa cha Bezi mkoani Mwanza.Wakala wa Ufundi na Umeme (TEMESA) ulianzishwa chini ya sheria ya Wakala Na.30 ya mwaka 1997 ikiwa na majukumu ya kufanya matengenezo ya magari na mitambo ya Serikali, matengenezo ya usimikaji wa mifumo ya umeme, uendeshaji wa vivuko vya Serikali, utoaji huduma za ukodishaji wa mitambo ya Serikali, kufanya usanifu na usimamizi wa usimikaji wa mifumo ya uhandisi wa mitambo, umeme na elektroniki.
3kitaifa
Na KULWA MZEE-DODOMA BUNGE limepitisha Muswada wa Sheria ya Fedha kwa mwaka 2017, ambapo pamoja na mambo mengine umeweka adhabu ya kulipa faini ya Sh 200,000 hadi Sh 1,000,000 au kifungo cha mwaka mmoja hadi miwili jela, kwa kosa la kutupa taka ovyo. Kabla ya muswada huo, faini ya kosa hilo ilikuwa Sh  50,000 na kifungo kisichozidi miezi 12. Katika hatua nyingine Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Bajeti, Hawa Ghasia, amepinga Serikali kuongeza ushuru kwenye vinywaji baridi, huku kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni, ikipinga faini za magari barabarani kufanywa sehemu ya mapato ya Serikali. Akiwasilisha maoni ya kamati hiyo bungeni jana baada ya Waziri wa Fedha na Mipango, Dk. Philip Mpango, kusoma Muswada wa Sheria ya Fedha wa mwaka 2017, Ghasia alisema kamati yake inaitaka Serikali iangalie upya tozo 14 zilizobakia katika shule binafsi ili nazo ziondolewe kwa lengo la kupunguza gharama uendeshaji kwa shule hizo. Wakati Ghasia akisema hayo, Naibu Waziri Kivuli wa Wizara ya Fedha, David Silinde, alisema Serikali inatakiwa kuacha tabia ya kugeuza makosa ya barabarani kuwa sehemu ya chanzo cha mapato yake. Badala yake, alitaka elimu itolewe kwa watumiaji wa vyombo vya moto barabarani ili kupunguza idadi ya makosa hayo. “Kuna taarifa zisizo rasmi, kuwa maofisa usalama barabarani wamekuwa wakipangiwa idadi ya magari wanayotakiwa kuyakamata kwa ajili ya kukusanya fedha. “Kutokana na taarifa hizo, askari wa usalama barabarani wamekuwa kero kwa watu kwa sababu wamekuwa wakiwabambikia makosa waendesha vifaa vya moto na kuwafanya waone ni kero kutumia vyombo hivyo,” alisema Silinde. Katika hatua nyingine, Silinde alisema Serikali ya CCM imekuwa ya kibaguzi na inaonyesha nia mbaya kwa vyama vya upinzani ingawa vimesajiliwa kisheria. Naye Waziri Mpango, alisema Muswada wa Fedha wa mwaka 2017, umelenga kuzifanyia marekebisho sheria 15 zinazohusu masuala ya fedha, kodi, ushuru, tozo na mawasiliano. “Marekebisho hayo, yatafanyika kwa lengo la kuweka, kurekebisha, kupunguza au kufuta viwango vya kodi, ushuru, ada na tozo mbalimbali na kuboresha ukusanyaji wa kodi. “Sheria zilizofanyiwa marekebisho ni Sheria ya Benki Kuu, sura ya 197 ambapo tunataka kuweka sharti la ulazima kwa taasisi za Serikali kufungua akaunti na kuhifadhi mapato na fedha zake Benki Kuu. “Nyingine ni Sheria ya Posta na Mawasiliano ya Kielektroniki, sura ya 306 ambapo tunalenga kupanua wigo wa mauzo ya hisa za asilimia 25 zitakazouzwa na kampuni ya mawasiliano kwenye soko la hisa kwa kutoa fursa kwa Watanzania, au taasisi yoyote ya kitanzania. “Fursa hiyo pia itawahusu Watanzania wanaoishi nje ya nchi, kampuni zinazomilikiwa kwa pamoja baina ya Watanzania na raia wa nje, raia na kampuni ama taasisi za nchi wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki au raia na makampuni kutoka nchi nyingine. “Kuondoa sharti la kuuza hisa katika soko la hisa kwa kampuni ndogo za mawasiliano zenye leseni na kubaki na kampuni kubwa zenye leseni ya mtandao au huduma. “Lengo jingine ni kuwezesha mamlaka ya masoko ya dhamana baada ya kushauriana na waziri mwenye dhamana na masuala ya masoko ya dhamana, kutoa maelekezo ya namna kampuni iliyoundwa kufikia mauzo ya hisa asilimia 25 itakavyoweza kufikia mauzo ya kiwango husika kwa kadri hali ya soko itakavyoruhusu,” alisema Dk. Mpango. Akizungumzia marekebisho ya Sheria ya Ushuru wa Bidhaa, sura ya 147, alisema kwa kuzingatia mkakati wa Taifa wa kukuza uchumi wa viwanda, kiwango cha ushuru kwa baadhi ya bidhaa zinazozalishwa nchini kimepunguzwa au kubakia ilivyo sasa. Naye Mbunge wa Nzega Mjini, Hussein Bashe (CCM), alitaka Serikali iweke nguvu zaidi ya kukusanya kodi kwenye michezo ya kubahatisha na kuipeleka kwenye mazingira. Aliendekeza pia tozo hiyo iongezwe kutoka asilimia sita hadi 12 kwa mapato yatokanayo na michezo hiyo na pia Serikali iongeze tozo hiyo kwenye leseni katika michezo hiyo. Kwa upande wake, Mbunge wa Babati Mjini, Pauline Gekul (Chadema), aliiomba Serikali iondoe Sh 40 kwenye mafuta ya taa kwani kiasi hicho kitaongeza mzigo kwa Watanzania wengi wasio na nishati ya umeme. Mbunge huyo pia aliitaka Serikali kututumia suala hilo kama njia ya udhibiti na kutaka mfumo ya wa uchakachuaji wa mafuta uimarishwe.
3kitaifa
Asha Kigundula -Dar es salaam LICHA viongozi wa klabu zenye wachezaji wa kimataifa kutaka Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), kupunguza masharti ya wachezaji wa kigeni waliotimkia makwao  kwa ajili  ya mapumziko, Rais wa TFF, Wallece Karia, amesisitiza mchezaji aliyesafiri nje ya Tanzania atakaa karantini siku 14 atakaporejea nchini. Ili kukabiliana na tishio la virusi vya ebola, TFF imeagiza mchezaji yoyote wa kigeni anayecheza soka hapa nchini aliyesafiri nje ya Tanzania, kufikia sehemu maalum ya uangalizi kwa muda wa wiki mbili atakaporejea nchini. Hatua hiyo ni wazi itawakuta baadhi ya wachezaji wa klabu za Simba, Yanga na Azam, ambao walitimkia makwao  baada ya Ligi Kuu Tanzania Bara kusimama. Ligi Kuu, Ligi Daraja la Kwanza na Ligi Daraja la Pili zimesimama, baada ya Serikali kupiga marufuku kwa siku 30 shughuli zenye mikusanyiko ikiwemo michezo, ikiwa ni tahadhari ya kuepuka kusambaa kwa virusi vinavyosababisha ugonjwa wa corona, ambao umeuwa maelfu ya watu duniani, tangu uliporipuka kwa mara ya kwanza nchini China. Hatua hiyo imezilazimisha klabu za soka nchini kuwapa mapumziko wachezaji wao kwa kipindi cha siku 30. Jana Rais John Magufuli akihutubia Taifa, alisema idadi ya watu waliobainika kuambukizwa  corona hapa nchini imefikia 12. Akizungumzia na MTANZANIA  jana, Karia alise alisisitiza  wachezaji wa kgeni waliosafiri katika mataifa yao kufikia sehemu maalum  ambako watafanyiwa uchunguzi wa afya ili kubaini kama wana maambukizi ya corona kabla ya kuungana na wenzao. Alisema ameshangaa kusikia kuna baadhi ya makocha na wachezaji wamesafiri katika nchi zao, wakati  hakuna aliyepewa ruhusa ya kutoka nje ya Tanzania. Karia alisema hata Rais Magufuli akizungumza na Watanzania alisisitiza hakuna ruhusa ya mtu kusafiri nje ya Tanzania. Alisema kuna baadhi ya mashabiki wanajisahau kuwa, endapo wachezaji hao wakirudi na maambukizi itakayoendelea kuathirika ni Tanzania, ikiwa pamoja na ligi kwa ujumla, hivyo kuchukua hatua kwa upande wao ni sehemu ya kuzuia kuenea kwa virusi vya ugonjwa huo. “Hakuna ambaye amepewa ruhusa ya kutoka nje ya nchi kwani sio likizo bali ni sitisho la muda kwa ajili ya kujikinga na maambukizi ya Virusi ya corona, hivyo kwa kocha au mchezaji ambaye ameatoka nje ya nchi hataruhusiwa kujiunga na wenzake mpaka akae sehemu maalum kwa wiki mbili na atajilipia kila kitu,” alisema Karia. Yanga kupitia kwa Mhamasishaji wao, Antonio Nugaz, alisema wao ni miongoni wa timu yenye wachezaji waliosafiri nje ya Tanzania ambao waliondoka baada ya kutangazwa kusimama kwa ligi kwa kipindi cha siku 30. Wachezaji wa Yanga waliotimkia katika mataifa yao ni Haruna Niyonzima(Rwanda) na David Molinga wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo(DRC) pamoja na kocha wao Luc Eymael, wakati kwa Simba ni Meddie Kagere(Rwanda), Clatous Chama(Zambia), Sharaf Shiboub(Sudan) na Luis  Miquissone, Msumbiji. Wachezaji saba wa Azam nao wametimkia makwao akiwemi  Razak Abalora(Ghana), Nicolas Wadada(Uganda),  Bruce Kagwa(Zimbabwe), Mohamed Yakubu(Ghana), Danny Amola, Donald Ngoma(Zimbabwe) na Never Tigere, Ivory Coast. Kocha Mkuu wa timu hiyo Mromania Aristica Cioaba na msaidizi wake Vivian Bahati, pia wamesafiri nje ya Tanzania.. Ofisa Habari wa Azam,  Zakaria Thabit Zaka Zakazi, alisema  kwa upande wao waliwapa ruhusa wachezaji wao wote baada ya Serikali kupitia kwa Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa,  TFF  na Bodi ya Ligi kutangaza, kusimama kwa mashindano kwa siku 30. “Tuliwapa nafasi maana hata mechi za kirafiki hakuna, ndiyo maana tuliwaruhusu tutafanya mawasiliano  hivyo watarudi kwa muda ili waweze kukaa karantini kama utaratibu uliyopangwa,”alisema Zaka za Kazi.
4afya
SERIKALI ya Awamu ya Tano chini ya Rais John Magufuli ilipofunga mlango wa ufisadi na kusisitiza kila Mtanzania kulipa kodi, huenda ulikuwa kama utamaduni wa kigeni kwa walio wengi tena usiotekelezeka.Hata hivyo, miaka minne ya uongozi wake, inaelezwa kuwa kodi zimezaa matunda kwenye elimu bila malipo, uboreshwaji huduma za afya, ununuzi wa ndege, ujenzi wa barabara, reli, madaraja na bwawa kubwa la kufua umeme la Julius Nyerere katika mto Rufiji lenye uwezo wa kuzalisha megawati 2,115 na mambo mengine.Mambo haya yote yanatajwa kuwa yanatokana na usimamizi bora wa kodi ambazo ndizo zinazowezesha miradi hiyo yote. Hata hivyo, gazeti hili limebaini uwepo wa mbinu mpya ya ukwepaji kodi inayoendelea huku baadhi ya wafanyabiashara wasiokuwa waaminifu wakibuni mbinu mbadala dhidi ya zile zilizobainika na kudhibitiwa.Uchunguzi wa makala haya imebaini kuwa, wafanyabiashara hao licha ya kuhujumu mapato halali ya serikali, pia wamekuwa ni chanzo cha kuwadhulumu wananchi ambao wamekuwa wakinunua bidhaa mbalimbali kutoka kwao.Kwa takribani miezi mitatu ya uchunguzi, imebainika utoaji ‘ofa’ kama staili mpya ya kukwepa kodi kwa baadhi ya wafanyabiashara jijini Dar es Salaam.Ilibainika udanganyifu huo unafanywa zaidi na wafanyabiashara wenye maduka ya vifaa vya ujenzi huku wakiwa na mazoea ya kusema kwa wateja; ‘Ukinunua tutakupa ofa mpaka mlangoni’ kumaanisha mzigo unaonunua utafikishwa kokote uendapo bila ya kuwepo gharama za ziada za kuusafirisha.“Kiukweli kuna mbinu mbalimbali za kukwepa kodi, lakini kwa sasa ili tuwe salama tunaweka ‘ofa’ kama njia ya kumvuta mteja kisha faida yetu inaongezeka kwa kukwepa kodi.  Kwa staili hii Serikali inakosa mapato, lakini pia wateja watakapotaka kurudisha kile walichonunua iwapo kina upungufu watashindwa kwa sababu hatutakubali kupokea risiti ambazo zinaonesha pungufu ya bei halisi ya kile walichonunua,” anasema mfanyabiashara mmoja anayekataa jina lisiandikwe gazetini katika eneo la Mbezi Mwisho, wilayani Ubungo, Dar es Salaam.Licha ya kubainika kwa mbinu hiyo mpya, mwaka jana gazeti hili lilifanya uchunguzi na kubaini mbinu mbalimbali zilizotumiwa na wafanyabiashara hao kama vile; kusingizia ubovu wa mashine za EFD, kujikosesha kwa makusudi katika kuandika risiti, kuwabambikizia wateja wasiokuwa makini risiti zilikwishanunulia mizigo au huduma nyingine, lakini pia wafanyabiashara na wateja walipunguziana bei kwa mashauriano, ikiwa ni mbinu inayoiumiza serikali moja kwa moja.Tangu, Serikali ya Awamu ya Tano iingie madarakani, TRA imebainisha kuwepo kwa ongezeko la mapato licha ya kuwepo kwa ukwepaji kodi.Ripoti ya TRA iliyowasilishwa Novemba mwaka huu, inaonesha kuwa, katika kipindi cha miaka minne ya TRA imeongeza mapato yake na kufikia Sh trilioni 58.3 kutoka Sh trilioni 34.97 kabla Serikali ya Awamu ya Tano haijaingia madarakani (sawa na ongezeko la Sh trilioni 23.4).Aidha kulingana na ripoti hiyo, kwa miaka minne ya hivi karibuni walipa kodi wameongeza kutoka milioni 2.2 mwaka 2015/16 hadi kufikia milioni 3.0 mwezi Oktoba 2019, pia TRA imekusanya wastani wa Sh trilioni 1.3 kila mwezi ikilinganishwa na wastani wa Sh bilioni 850 kabla ya awamu ya tano. Kama hiyo haitoshi kuanzia Julai hadi Oktoba, katika mwaka wa fedha 2019/20 , wastani wa makusanyo umepanda hadi kufikia Sh trilioni 1.45 kwa mwezi.Akizungumzia ripoti hiyo, Naibu Kamishina Mkuu wa TRA, Msafiri Mbibo anasema licha ya kuwepo kwa wastani mzuri wa ongezeko la kodi, bado kuna changamoto ukwepaji kodi wa makusudi, biashara za magendo kutokana na kuwapo kwa ukanda mrefu wa pwani, mipaka mingi na rushwa.Pia alibainisha kuwa, changamoto nyingine ni utunzaji dhaifu wa kumbukumbu na baadhi ya wafanyabiashara wenye nia mbaya kutokutumia EFD.APOTEZA AJIRA KISA OFAMolel (si jina halisi) ni fundi mwashi aliyefanya ujenzi wa nyumba mbalimbali eneo la Tegeta, mkoani Dar es Salaam, anaeleza kuwa alipoteza kibarua chake cha ujenzi wa nyumba ya kuishi familia baada ya kushindwa kutoa risiti ya kile alichonunua kwa kuwa alirubuniwa kwa staili ya kupewa ofa ya usafiri hivyo akakubali kupewa risiti ya EFD isiyo sahihi.Anasema, “Nina uzoefu wa miaka tisa wa kujenga nyumba, nimefanya kazi hii kwa uaminifu na nimekuwa nikipewa fedha na wenye nyumba nikanunue baadhi ya vifaa vya ujenzi, lakini ilinikuta kwa mmoja ambaye alikuwa akisisitiza risiti kwenye kila manunuzi …”“…nakumbuka, huyo tajiri aliyenituma aliniagiza nije na risiti na mara nyingi tunapoenda kule kununua kama mafundi huwa tunapewa kamisheni huku taarifa za risiti zikibaki vilevile, lakini kilichotokea sikupewa risiti licha ya kuwa mwenye duka alifikisha mzigo kwenye eneo la ujenzi,” anaeleza.Fundi huyo anasema kuwa ni jambo la kawaida pale fundi anapopeleka mteja kwenye duka. “Huwa tunapata kamisheni kwa kuleta mteja, na tukifika pale huwa tunapewa ofa, ikiwemo ya usafiri na kutokana na wengine kutaka faida kubwa, huwa wanatuuliza kama tunaowafanyia kazi za ujenzi watahitaji risiti…”“…kama hawatahitaji huwa hawatuandikii, na hata kama ikihitajika huwa kuna zile za kughushi ambazo hazisomeki kwenye mifumo ya TRA,” anasema na kuongeza kuwa, ofa zinazotolewa kwa wateja hasa katika usafirishaji wa mizigo huambatanishwa na risiti feki au zisizokuwa na usahihi kwenye muda, kiwango cha fedha kilichotolewa.WASTAAFU NAO MTEGONIOfisa Ardhi mstaafu (ana miaka 64) alikumbana na mkasa mmoja maeneo ya Mbagala, wilayani Temeke alipokuwa akiendelea na ujenzi wa nyumba yake ambapo alikuwa na utaratibu wa kwenda kununua vifaa mbalimbali vya ujenzi mwenyewe na kuvipeleka kwenye eneo lake la ujenzi.Anasema, “Mimi nina gari linaloweza kubeba mizigo (Toyota pick-up), nilipokuwa nikinunua mizigo waliniambia wanipe ofa ya usafiri, lakini nilikataa kwa kuwa nina gari na badala yake niliomba ofa iwe kwenye punguzo la bei ya bidhaa. Cha kushangaza wauzaji walikuwa wakigoma na kudai kuwa bei ya bidhaa haipungui ila usafiri unaweza kuwa bure.“Sikuambulia ofa yoyote, na nikaamua kubeba mizigo yangu, lakini kwa kuwa nilikosa umakini wakati wa kuchukua risiti nilikuta wamenipa risiti ambayo haipo sawa (iliyokuwa imetolewa siku mbili zilizopita), na niliposimamishwa na maofisa, ilibainika kuwa risiti ile ina kasoro na mimi sikusita kuwapeleka kwa aliyeniuzia bidhaa na hakika walimchukulia hatua …”“…lakini nilianza kuona usumbufu huo ni mkubwa. Nilipoenda kuagiza mzigo sehemu nyingine bila ya kwenda na gari langu nilinunua na kutaka ofa ya usafiri, lakini kila walipokuwa wakiniletea mizigo walinipa visingizio vya risiti huku wakati mwingine wakidai imepotea, mara wanipe iliyoandikwa siku moja kabla ya manunuzi… Hii ilinikera na nilipouliza kwa dereva wa gari hilo alinieleza kuwa, mabosi wake wanafanya hivyo,” anaeleza mstaafu huyo.ITAENDELEA KESHO…
1uchumi
Patricia Kimeleta-DAR ES SALAAM RAIS Dk. John Magufuli anatarajia kuwa mwenyeji na mwenyekiti wa mkutano wa 39 wa wakuu wa nchi na Serikali wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika SADC unaotarajia kufanyika Agost 17 na 18, mwaka huu jijini Dar es Salaam Rais Magufuli ambaye kwa sasa ni Makamu Mwenyekiti wa Jumuiya hiyo alishika nafasi ya uenyekiti wa SADC Agost mwaka jana, katika mkutano uliofanyika Windhoek nchini Namibia nafasi ambayo ni ya mzunguko akiichukua kutoka kwa Rais wa nchi hiyo Dk. Hage Geingob na atahudumu kwa muda wa mwaka mmoja kuanzia Agosti 2019 hadi Agosti 2020. Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana, Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki,  Profesa Palamagamba Kabudi, alisema kwa sasa maandalizi ya mkutano huo yanaendelea kufanyika. “Maandalizi ya maonesho na maadhimisho haya ya wiki ya viwanda yanaratibiwa na Wizara za Viwanda na Biashara pamoja na Wizara ya Mambo ya Nje, ni adhimu na muhimu sana, nawaomba wafanyabiashara na wadau wote wajitokeze katika kushiriki maonesho haya ambayo yataleta tija ya masoko na viwanda kwenye nchi yetu,” alisema Profesa Kabudi. Alisema hadi sasa tayari wajumbe sita kutoka katika Sekretarieti ya SADC wamewasili nchini kwa ajili ya maandalizi ya awali ya mikutano na maadhimisho hayo. Akizungumzia maandalizi Naibu Katibu Mtendaji wa Sekretariat hiyo, Balozi Joseph Nourrice alisema lengo ni kuhakikisha wanafanikisha azma yao hiyo. “Sisi Sekretarieti tumekuja kufanya maandalizi ya mikutano hii kuanzia ngazi ya maofisa, mawaziri, makatibu wakuu na wakuu wa nchi na Serikali zao, tuna hakika tutafanikisha jambo hili,” alisema Balozi Nouricce Mwenyekiti wa sasa wa SADC Rais Dk. Magufuli atashirikiana na Sekretariat ya SADC katika kusimamia utekelezaji wa shughuli zote za kikanda pamoja na kuratibu na kusimamia mikutano mbalimbali ya kisekta kwenye nchi hizo. Kwa mara ya mwisho mkutano wa SADC ulifanyika Tanzania mwaka 2013 ukiwa chini ya uenyekiti wa aliyekuwa Rais wa Awamu ya Tatu, Benjamini Mkapa ambapo kwa sasa ina nchi 16 wanachama zikiwepo za Tanzania, Angola, Botswana, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, Jamhuri ya Visiwa vya Comoro, Falme ya Eswatini, Falme ya Lesotho, Namibia, Shelisheli, Afrika Kusini, Malawi, Msumbiji, Mauritius,  Zambia, Zimbabwe na Madagascar.
3kitaifa
JESHI la Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam limepiga marufuku magari ya serikali na yanayobeba wagonjwa, kutumia barabara ya mabasi yaendayo kasi, isipokuwa pale inapotokea dharura maalumu, hususani linapokuwa limebeba mgonjwa.Hatua hiyo imekuja baada ya jeshi hilo kuwashikilia waendesha bodaboda 20 kwa tuhuma za kulishambulia basi la mwendokasi, lenye namba T 155 DGW na kusababisha uharibifu mkubwa wa basi hilo.Tukio la kushambuliwa kwa basi hilo ni la saa 2.15 usiku Desemba 8 mwaka huu katika eneo la Manzese Tip Top wilayani Ubungo. Lilitokea baada ya pikipiki yenye namba za usajili MC 964 BYN kupita katika barabara ya mwendokasi na kugonga basi la mwendokasi.Ajali hiyo ilisababisha vifo vya watu watatu. Alisema pikipiki hiyo ilikuwa imebeba abiria wawili (mshikaki) ambao walifariki papo hapo. Dereva wa bodaboda hiyo alifariki muda mchache wakati akipatiwa matibabu hospitalini, baada ya kujeruhiwa vibaya.Baada ya tukio hilo, baadhi ya madereva wa bodaboda waliokuwa wamesimama kando ya barabara hiyo, walianza kumshambulia dereva, abiria na basi kwa mawe na kusababisha uharibifu wa gari hilo.“Kimsingi matukio haya yanatokana na matumizi mabaya ya barabara ya mwendokasi, nitoe rai kwa magari yote yasiyohusika na barabara hiyo kuacha kuitumia, vinginevyo wahusika watachukuliwa hatua za kisheria ikiwemo kukamatwa na kufikishwa mahakamani,” alisema Mambosasa. Alisema kwa magari ya wagonjwa, yatatumia barabara hiyo, pale tu endapo yanakuwa yamebeba wagonjwa.Aliyataka kuacha kupiga ving’ora, kwa kuwa tayari yanakuwa yapo katika barabara maalumu. Lakini pia yanatakiwa kuacha kutumia barabara hiyo, pale yanapokuwa hayajabeba wagonjwa. Aidha alisema ili kutoa fundisho kwa watu wanaofanya makosa kwa makusudi kwa kutegemea kulipa faini, kwa sasa hawatapokea faini hizo, badala yake watawakamata na kuwafikisha mbele ya vyombo vya sheria.
3kitaifa
MANCHESTER, ENGLAND BASI la klabu ya Manchester United lilishambuliwa kwa mawe lilipokuwa linaelekea katika Uwanja wa Upton Park ambao unamilikiwa na wapinzani wao, West Ham. Mashabiki wa West Ham walikuwa wanalisubiri basi hilo wakati linaelekea uwanjani hapo kwa ajili ya mchezo wa Ligi Kuu nchini England katika mchezo ambao ulimalizika kwa United kupokea kichapo cha mabao 3-2 na kuifanya klabu hiyo ishuke ‘top four’. Shambulizi hilo lilisababisha mchezo huo baina ya Manchester United na West Ham kucheleweshwa kwa zaidi ya dakika 45. Mchezo huo ulikuwa umeratibiwa kuanza saa tatu na dakika 45 usiku, lakini ukaanza saa nne na nusu, hivyo kuwafanya Man United waupoteze. Hata hivyo, madirisha ya basi hilo yalivunjwa na mashabiki hao ambao walikuwa wanarusha mawe na chupa za bia ila askari walipambana na ghasia hizo kwa ajili ya kuwalinda na kuwasindikiza wachezaji hadi uwanjani. “Ilikuwa tukio la kushtua sana, haikufurahisha kabisa kushambuliwa na mashabiki wa timu pinzani hadi gari letu linaharibiwa,” alisema nahodha wa Manchester United, Wayne Rooney. Hata hivyo, kocha wa Man United, Van Gaal, aliweka wazi kwamba timu yake ilipoteza mchezo huo kutokana na wasiwasi za mashabiki ambao walionekana uwanjani hapo wakiwa na hasira. Mchezo huo ulikuwa wa mwisho kwa West Ham kuutumia uwanja huo kwa michezo yao ya nyumbani kwa kuwa inatarajia kuhamia makao yao mapya ya Olympic Stadium. West Ham imekuwa ikiutumia uwanja wa Upton Park kwa miaka 112 sasa.
5michezo
['Real Madrid wana imani watafanikiwa kumsajili kiugo wa kati Mfaransa Paul Pogba kutoka Manchester United msimu ujao. (ESPN)', 'Bayern Munich wameanza mazungumzo na Manchester City kuhusu usajiliwa wa winga wao wa miaka 23 Mjerumani Leroy Sane, amabaye thamani yake inakadiriwa kuwa £90m. (Mirror)', 'Romelu Lukaku, 26, amesafiri nyumbani Ubelgiji siku ya Ijumaa kufanya mazungumzo na ajenti wake huku Inter Milan wakikaribia kufikia mkataba wa £70m kumnunua kuingo huyo wa safu ya ushambulizi kutoka Manchester United. (Daily Mail)', 'Mmiliki wa Newcastle Mike Ashley amesema chamsingi ni maishani ni "pesa kwanza kisha klabu baadae" kwa maneja wake wa zamani Rafael Benitez, na kuongeza kuwa "ni vigumu" kuendelea kumng\'ang\'ania raia huyo wa Uhispania. (Mail)', 'Atletico Madrid wanataka kumsajili kiungo wa kati wa Colombia James Rodriguez, 28, kutoka kwa mahasimu wao Real Madrid. (Independent)', 'Mshambuliaji wa Ureno Rafael Leao, 20, anajiandaa kuondoka Lille kwenda AC Milan kwa mkataba wa euro milioni 35 - utakaojumuisha 20% ya makataa ya kumuuza. (RMC Sport)', 'Bournemouth wanapania kuipiku Brighton katika usajili wa £15m wa kiungo wa kati wa Huddersfield Philip Billing, 23. (Sun)', 'Swansea City wanakabiliwa na hatari ya kumkosa mchezaji wa safu ya kati wa Chelsea mwenye umri wa miaka 22-Kasey Palmer. (Wales Online)', 'Panathinaikos wanatafakari uwezekano wa kumnunua kiungo wa kati wa Ivory Coast anayechezea Celtic Kouassi Eboue, 21. (Daily Record)', 'Bekiwa Real Madrid wa miaka 22 Mhispania Jesus Vallejo anafanyiwa vipimo vya kimatibabu Wolves kabla ya kuhamia klabu hiyo kwa mkopo. (Talksport)', 'Meneja wa Liverpool Jurgen Klopp amepuuzilia mbali madai kuwa wanamlenga mshambuliaji wa Real Madrid Gareth Bale, 30, na kusisitiza kuwa kipaumbele chake kwa sasa ni kuimarisha kikosi kilichopo badala ya kununua wachezaji wapya. (Independent)', 'Manchester United huenda ikalazimika kulipa Leicester City £80m kumnunua mlinzi wake Harry Maguire baada ya Eric Bailly kuumia goti katika mechi ya kirafiki dhidi ya Tottenham. (Mirror)', 'Mshambuliaji wa Lyon Mfaransa Moussa Dembele , 23, atakuwa katika urodha ya kujiunga na Manchester United klabu hiyo ikiamua kumuuza nyota wa kimataifa wa Ubelgiji Romelu Lukaku, 26. (Sky Sports)', 'Mshambuliaji wa Juventus Cristiano Ronaldo, 34, hana uwezo wa kumshawishi Neymar kujiunga na miamba wa Italia- kwa sababu nyota huyo wa Brazil wa miaka 27-ameamua kujiunga na Barcelona. (Star)', 'Borussia Dortmund wanafanya mazungumzo ya kumsajili mshambulizi wa Barcelona Malcom kwa euro milioni 42 (£37.5m). (Goal)']
5michezo
MWANDISHI WETU-MWANZA Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA), imesema kuwa inakabiliana na changamoto ya uwepo wa bandari bubu zaidi ya 300 katika Ziwa Victoria. Imesema kuwa kwa sasa wanapambana kwa mujibu wa sheria ili ziweze kuondoka kwa kuzirasimisha ili ziweze kutambulika jambo ambalo litasaidia kuleta ufanisi katika ukusanyaji wa mapato ya Serikali huku akitenga zaidi ya Sh bilioni 16 kwa ajili ya kuboresha na kujenga bandari zilizopo katika ziwa hilo. Bandari hiyo kwa sasa imeanza kuhudumia kwa kusafirisha mizigo katika nchini za Uganda, Sudani Kusini na Rwanda. Kauli hiyo imetolewa leo na Meneja wa Bandari za Ziwa Victoria, Morris Machindiuza, alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari kuhusu shughuli za bandari zilizopo ndani ya ziwa hilo. Amesema pamoja na hilo TPA imepewa jukumu ya kuendeleza bandari na kuendesha, kutangaza huduma za bandari kwa kushirikiana na sekra binafsi katika uendeshaji wa bandari. “Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania katika Ziwa Victoria imejipanga na tayari ilikishaanza  kuhudumia shehena mbalimbali kama vile za Shirika la Chakula Duania (WFP), mashudu, viwanywaji baridi pamoja na kusafirisha vifaa vya ujenzi kwa ajili ya nchi za Uganda na Sudani Kusini. “Katika mwambao wa Ziwa Victoria TPA inamiliki na kusimamia bandari kubwa za Mwanza Kaskazini na Kusini, Nansio, Kemondo Bay, Bukoba na Musoma pia kuna bandari zingine ndogo za mwambao zaidi ya 15 ambazo zote tunazihudumia kwa kuwa chini ya usimamizi wetu,” amesema Machindiuza Pamoja na hilo amesema kuwa TPA inaendesha Bandari Kavu ya Isaka ambayo inamilikiwa na Shirika la Reli Tanzania ambapo kuwa ghala kubwa lenye uwezo wa kuhifadhi shehena ya tani 3,000, yadi ya makasha na yadi ya Rwanda yenye eneo la ekari 17.05. Meneja huyo wa Bandari za Ziwa Victoria, amesema kuwa kwa sasa wapo mbioni kuanzisha Bandari Kavu nyingine ya Fela wilayani Misungwi mkoani Mwanza ambapo hadi sasa tayari wamelipa fidia kwa nyumba 14 na mpango wa matumizi ya ardhi unaandaliwa katika eneo eno hilo. Amesema kwa kipindi cha mwaka 2014/15 hali ya utendaji kwa Bandari za Ziwa Victoria ulidorora kwa muda kutokana na kushuka kwa hali ya utendaji wa Reli ya Kati na kupungua kwa idadi ya meli zinazofanya kazi katika Ziwa Victoria. “kwa miaka mitano iliyopita 2014/2015-2018/2019 shehena inayohudumiwa katika Bandari ya Mwanza imekuwa ikipanda kwa wastani wa asilimia 0.5  kwa kutoka tani 129,767 mwaka 2014/15 hadi tani 157,808 mwaka 2018/19. “katika kipindi cha miezi minne ya kwanza mwaka 2019/20 Julai hadi Novemba Bandari ya Ziwa Victoria imeweza kuhudumia tano 76,168.44 ikiwa ni asilimia 99.14 ya lengo la kuhudumia tani 76,833,” amesema Machindiuza Akizungumza hali ya mapato amesema imepanda kutoka Sh milioni 600 hadi kufikia Sh bilioni 1.4 jambo ambalo ni la kutia moyo katika uendeshaji wa shughuli za bandari. “Kwa sasa Serikali ya Awamu ya Tano mkakati mkubwa ni kukusanya mapato ya ndani, nasi TPA kama wadaui taasisi muhimu tunalizingatia hilo kwa kuhakikisha tunatafuta wafanyabishara ambao ilin waweze kutumia bandari zetu,” amesema Machindiuza
3kitaifa
SHIRIKA la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF) limeanza kuhakiki malipo kwa ajiri ya wanachama wake, waliokuwa wakifanya kazi zisizo za weledi kwenye sekta mbalimbali kabla ya kuachishwa kazi.Hatua hiyo imekuja baada ya agizo la Rais John Magufuli alilolitoa, alipokutana na viongozi wa vyama vya wafanyakazi Desemba 28 mwaka jana Ikulu, Dar es Salaam, la kutaka wafanyakazi wa aina hiyo kupewa fao lao la kuachishwa kazi.Akizungumza na waandishi wa habari jana, Meneja Kiongozi wa Matekelezo wa NSSF, Cosmas Sasi alibainisha kuwa malipo yatalipwa mara tu baada ya mfanyakazi husika kuhakikiwa.Sasi alisema uhakiki huo utachukua siku 30, tangu mfanyakazi kuwasilisha ombi lake na kuwa kwa maombi yatakayotiliwa shaka, yatafanyiwa uchunguzi kwa muda wa mwezi mmoja.Alisema NSSF imejipanga vyema kutekeleza uhakiki huo kwa wakati na muda mwafaka ili kila mwenye haki apewe haki yake kwa wakati, huku akiwataka wenye kustahili kulipwa fao hilo kutosita kuwasilisha maombi kwenye ofisi za NSSF zilizopo kila mkoa.“Tumejipanga kuwalipa kwa wakati hawa wafanyakazi wote waliokuwa kwenye ajira ya muda na ambao labla ajira imesitishwa au mradi kuisha, hawa watapewa mafao yao yote,” alisema. Alifafanua kuwa kila mhusika akishapewa fedha zake zote, alizokuwa amechangia NSSF, ataongewezewa na asilimia nyingine ya fedha kama nyongeza, ambazo hakuwa tayari kuziweka wazi kuwa ni ngapi.Alisema kwa wafanyakazi wanaofanya kazi za kitaaluma na walikuwa wakichangia zaidi ya miezi 18, wakisitishiwa ajira zao, watalipwa asilimia 33.3 ya mshahara waliokuwa wakilipwa kwa miezi sita kabla ya kupata ajira nyingine.Alibainisha kuwa kwa wale waliokuwa wakichangia chini ya miezi 18, watalipwa asilimia asilimia 50. Kwa upande wake, Meneja Kiongozi Uhusiano na Elimu kwa Umma, Lulu Mengele akizungumzia kuhusu malipo ya pensheni kwa wastaafu wanaonufaika na mfuko huo, alibainisha kuwa wastaafu ambapo hawatakuwa wamehakikiwa hadi kufikia mwishoni mwa mwezi huu, malipo yao yatasitishwa.“Wastaafu ambao hadi sasa hawajahakikiwa wanaombwa kuwasilisha nakala stahiki kwenye ofisi za NSSF kwenye mikoa wanayotokea ili uhakiki ufanyike wakati,” alisema Mengele. “Kwa kuwa tunazo ofisi 65 Tanzania Bara ni dhahiri kuwa hakuna sababu za wastaafu hao kushindwa kwenda kuhakikiwa wajitokeze kwa wingi wakahakikiwe ili waje kunufaika na mapato na pia hata wale waliokuwa wakifanya kazi za muda mfupi na wamesitishiwa au kufukuzwa kazi au mradi kuisha, nao walete vielelezo wahakikiwe tayari kwa malipo stahiki,” aliongeza.Katika kikao cha Rais Magufuli na viongozi wa vyama vya wafanyakazi, aliagiza wastaafu kulipwa mafao yao kwa kufuata vikokotoo vya awali kwa muda wa miaka mitano ya mpito kuanzia sasa, tofauti na mapendekezo yaliyokuwa yametolewa chini ya Kanuni za Mamlaka ya Usimamizi wa Mifuko ya Hifadhi ya Jamii (SSRA).SSRA ilipendekeza kikokotoo cha asilimia 25 kwa wastaafu kwa mkupuo, kisha kuendelea kulipwa asilimia 75 kila mwezi hadi kufa kwao. Rais Magufuli alipinga hatua hiyo na kuagiza kuwa kuanzia sasa Mfuko wa Hifadhi ya Jamii kwa Watumishi wa Umma (PSSSF) na wa sekta binafsi NSSF, iliyoanza kufanya kazi mwaka jana, ianze kulipa wastaafu kwa kutumia kikokotoo cha zamani kwa mujibu wa mifuko waliyokuwemo kabla haijaunganishwa.
3kitaifa
RAIS Yoweri Museveni akiwa na wajukuu zake, ameitumia Desemba 26 ambayo ni mapumziko, kuchunga ng’ombe wake katika shamba lake lililopo Rwakitura, wilayani Kiruhura.Aidha, kiongozi huyo aliyezaliwa mwaka 1944, aliwaambia wajukuu zake hao kuwa wajijengee utaratibu wa kukusanyika pamoja na familia zao katika kipindi cha sikukuu za mwisho wa mwaka ili kutathmini matukio ya mwaka mzima.Museveni alisema kupitia mikusanyiko hiyo pia wataweza kujipanga namna bora ya kuanza mwaka unaofuata na namna ya kutimiza malengo waliyojiwekea kwa kila mwaka ili kuwa na maisha bora.Katika ukurasa wake wa Twitter, Rais Museveni aliandika haya: “Tukiwa katika shamba la ufugaji la Rwakitura na wajukuu zangu katika urithi tulioachiwa. Tutakuwa tukitumia sikukuu kama hizi kufundisha vizazi vya sasa kuhusu utamaduni wetu, tunachunga pamoja, nawasihi wazazi kuungana na watoto wenu katika kipindi hiki.”Katika salamu zake za Krismasi na Mwaka Mpya, Rais Museveni aliwapongeza wananchi wa Uganda kwa kusherehekea kwa amani na utulivu.
3kitaifa
MBUNGE wa Ubungo, Saed Kubenea (Chadema) amesema upande wa upinzani mpaka sasa hautambui uamuzi wa kumng’oa Meya wa Jiji la Dar es Salaam, Isaya Mwita. Kwamba wamejipanga kuhakikisha vikao na shughuli za jiji, havifanyiki bila uwepo wa meya huyo.Aidha, alisema Mkurugenzi wa Jiji hilo, Sipora Liana alicheza mchezo mchafu katika kikao cha kupiga kura za kumuondoa meya huyo, kwa kuandika jina la diwani asiyekuwepo na kutumia vibaya cheo chake.Kwa upande wake, Liana alimtaka mbunge huyo na vyama vya upinzani, kumpeleka Taasisi ya Kupambana na Kuzuia Rushwa (Takukuru), kama wanadhani alicheza mchezo huo mchafu. Akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam jana, Kubenea alisema hawatambui hatua hiyo ya kuondolewa madarakani meya, kwa kuwa tuhuma zinazomkabili, siyo za kweli na pia mchakato wa kumuondoa, ulikuwa batili, kwa kuwa haukidhi akidi ya baraza hilo.“Kikao kinatakiwa ili kikidhi akidi kiwe na wajumbe 17, hilo lilifanikiwa kwani walikwenda wajumbe 18 ambao 16 walikuwa ni CCM na wawili upinzani,” alisema Kubenea.Alieleza kuwa tatizo lilikuja kwenye kupiga kura, ambapo kwa mujibu wa Kanuni, inatakiwa kura za ‘ndiyo’ zifikie akidi ya wajumbe 17, lakini waliopiga kura za ‘ndiyo’ ni 16 na mbili za ‘Hapana’.“Ndio maana baadaye tukaona mkurugenzi ameandika jina la diwani, ambaye si tu hayuko kwenye kikao, hata hapa Dar es Salaam hayupo,” alisema.Aidha, alisema tuhuma tano alizotuhumiwa Mwita, zote si za kweli, kwani nyingine zinamgusa zaidi mkurugenzi na si Mwita. Miongoni mwa tuhuma anazokabiliwa nazo Mwita ni matumizi mabaya ya mali za ofisi (gari), kushindwa kufanya matumizi ya fedha za hisa za UDA, kuwaingiza mameya wa manispaa zote za Dar es Salaam kwenye kamati ya fedha ya jiji na kushindwa kuzuia vurugu, zinazotokea kwenye mikutano.Kuhusu matumizi mabaya ya gari, alisema haiwezekani meya ashitakiwe kwa uzembe wa dereva, ambaye ndiye aliyepita kwenye njia ya mwendokasi na kumgonga bodaboda.Badala yake, alimtupia lawama mkurugenzi kuhusika na kosa hilo, kwa kuwa yeye ndiye mwajiri. Kuhusu ya matumizi ya fedha za hisa za UDA, Kubenea alisema fedha hizo mpaka sasa hazipo, zimeshapelekwa kwenye ujenzi wa kituo cha mabasi cha Mbezi, baada ya Baraza hilo la Jiji, kugomea miradi zaidi ya minne, aliyoiita kuwa haina tija. Alisema katika tuhuma ya kutotuliza vurugu kwenye kikao, suala hilo aliyelalamikia tuhuma hiyo, hana uadilifu wa kuzungumzia suala hilo, kwani yeye ndio chanzo cha vurugu, zilizowahi kutokea kwenye kikao hicho.“Hili naliweka wazi, huyu Chaurembo ndio chanzo cha vurugu kwanza, hana ‘moral authority’ ya kuzungumzia maadili na akibisha hawezi kunifanya kitu. Akinigusa, tutanuka wote,” alisema Kubenea.Alisisitiza kuwa msimamo wa upinzani ni kwamba bado Mwita ni Meya wa Dar ea Salaam na kamwe hawatakubali shughuli zozote za jiji katika miezi sita iliyobaki, zifanyike bila uwepo wake.Alisema ili suala hilo lipatiwe ufumbuzi, jiji lianzishe mchakato mpya wa kumtuhumu Mwita, ikiwemo kufuata kanuni za Halmashauri ya Jiji katika kumuondoa madarakani. Aidha, alisema endapo mchakato huo, utashindikana Jiji na wizara husika, ziishauri mamlaka kuu (Rais) alivunje jiji hilo.“Kama yote hayo yatashindikana, basi watambue kuwa jiji halitatawalika bila Meya Mwita. Hatutakubali, hata ngumi tutapigana,” alisisitiza.Naye, Mkurugenzi wa Jiji, Liana alisema tuhuma zote dhidi yake, ziwasilishwe Takukuru, ikiwemo suala la kughushi jina la diwani. Pia, Liana alisema kuhusu suala la kutokubaliana na uamuzi wa kuondolewa madarakani Meya, wakate rufaa kwa Waziri wa Tamisemi. Mwita ameshapewa barua ya kumtaka akabidhi ofisi ndani ya siku 14, baada ya kung’olewa madarakani wiki iliyopita.
3kitaifa
Wakati Watanzania wanajiandaa kwa mabadiliko ya matumizi ya mifuko mbadala ya plastiki, wadau wakiwemo wazalishaji wa malighafi zinazotumika katika utengenezaji wa mifuko mbadala, wameipongeza serikali kwa hatua ilizochukua.Pia, wameelezea mipango yao itakayosaidia kutekeleza mpango wa mabadiliko hayo.Kauli za wadau hao zimekuja wiki chache, baada ya serikali kutoa uamuzi wake wa kupiga marufuku ya mifuko ya plastiki, ikiwa ni mikakati endelevu ya kukabiliana na kasi ya uharibifu wa mazingira na kuvilinda viumbe hai vya majini.Tafiti za kimataifa zinataja kuwa itakapofika mwaka 2050, kutakuwa na mifuko mingi ya plastiki baharini kuliko samaki.Wamesema hatua ya serikali ya kudhibiti matumizi ya mifuko hiyo, imekuja wakati muafaka kwa kuwa pamoja na mambo mengine itasaidia kuokoa mazingira nchini, ikizingatiwa kuwa baadhi ya nchi za Afrika ya Mashariki zikiwemo Kenya, Rwanda na Uganda, tayari zilikwishakomesha matumizi ya mifuko hiyo.Mbali na mataifa hayo, Zanzibar pia ilishaachana na matumizi ya mifuko hiyo na hivyo kufanya mkakati huo uliochukuliwa na Tanzania Bara hivi sasa kuwa kama hatua yake muhimu ya kulitekeleza kwa vitendo agizo hilo.Wakizungumza na gazeti hili, baadhi ya wazalishaji wa malighafi hususani karatasi zinazotumika katika kutengenezea mifuko hiyo na bidhaa nyingine, akiwemo Kaimu Meneja Mkuu wa kiwanda cha Mufindi Paper Mills (MPM), Gregory Chogo walisema hakuna hofu yoyote ya uhaba wa mifuko mbadala wakati huu ambao Taifa limeamua kupiga hatua nyingine.Alisema kinachotakiwa kufanyika hivi sasa ni kwa watengenezaji wa mifuko hiyo na wapya waliopo katika mikakati ya uzalishaji wa mifuko hiyo, kuzingatia hatua mbalimbali zitakazofanikisha azma yao, ikiwa ni pamoja kupata malighafi sahihi za uzalishaji wa mifuko hiyo zitakazoendana na viwango.Alisema wakati huu ambapo mifuko mbadala inakwenda kuanza kutumika, kuna kila dalili za soko kujaa mifuko tofauti ikiwemo iliyozalishwa kwa kutumia karatasi zisizo na ubora na hivyo kutia dosari mkakati huo wa serikali.“Kuna kila dalili soko la mifuko hiyo kuja kuvamia na mifuko iliyotokana na malighafi kutoka katika madampo na hata mifuko iliyotokana na ubebaji wa saruji, kitu ambacho ni hatari kiafya, kikubwa tunapoenda kutekeleza hatua hii muhimu ni jukumu la kila mtanzania kuzingatia usalama na matumizi ya karatasi sahihi,” alisema Chogo.Alisema hakuna sababu ya wazalishaji wa mifuko hiyo kutumia karatasi zisizo na viwango, kwa kuwa kuna uzalishaji wa kutosha wa karatasi hizo huku akibainisha changamoto iliyokuwepo hapa nchini kuwa ni ukosefu wa soko wa karatasi hizo hatua inayowafanya kuzipeleka nje ya nchi.Alisema soko la karatasi hizo kwa hapa nchini ni asilimia 25 pekee huku kiasi cha asilimia 75 kilisafirishwa katika nchi za Rwanda, Burundi, Uganda, Kenya na Zanzibar huku akibainisha kuwa uwezo wa kiwanda hicho kuzalisha karatasi hizo ni tani 4,500 kwa mwezi na kudai kuwa kiwango hicho kinaweza kuongezeka kulingana na mahitaji yaliyopo ya soko la karatasi hizo.“Hatupendi kusafirisha karatasi hizi kwenda nje ya nchi, isipokuwa tunafanya hivyo kutokana na kutokuwepo kwa soko la uhakika la hapa nchini, tunaamini kupigwa marufuku kwa mifuko hiyo kutaongeza soko la karatasi zetu,” aliongeza Chogo.Akizungumzia suala hilo wakati wa mkutano wa wadau mbalimbali kujadili fursa za mifuko mbadala, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais, Mazingira, January Makamba alisema kwa sasa Taifa linajielekeza katika uzalishaji wa mifuko mbadala, ikiwa ni utekelezaji wa agizo lililowahi kutolewa huko nyuma.Alisema awali matumizi ya mifuko hiyo ya plastiki lilikuwa lifanyike mwaka 2016, kabla ya wamiliki wa viwanda kuomba kusogezwa kwa muda wa agizo hilo hadi Desemba 31, mwaka 2017, jambo utekelezaji wake haukufanyika hadi wakati huu ambao Serikali imeamua kuzuia rasmi mifuko hiyo ifikapo Mei 31, ikiwa ni miezi 18 tangu ombi hilo lilipotolewa.Alisema mifuko iliyopigwa marufuku kupitia agizo hilo la Serikali ni ile inayotumika kwa ajili ya kubebea bidhaa na siyo ile inayohusisha vifungashio zikiwemo korosho, maziwa na bidhaa nyingine za kilimo na viwandani.Amesema kwa sasa ambapo Serikali inajiandaa kutekeleza agizo hilo, wanasheria wake wapo katika maandalizi ya sheria na kanuni mbalimbali kwa ajili ya kusimamia suala hilo ambalo utekelezaji wake unatarajiwa kuanza rasmi ifikapo Juni Mosi.“Kimsingi adhabu hizo wazalishaji wote, wasambazaji na wauzaji wa mifuko hiyo ikihusisha faini, vifungo vya jela au vyote kwa pamoja kulingana na kile kitakachokuwa kimetajwa katika kanuni hizo,” ameongeza Makamba.Alisema katika utekelezaji wa sheria ya kudhibiti mifuko hiyo, Serikali itashirikiana na vyombo vyote ikiwemo TBS, TFDA, Jeshi la Polisi, Mamlaka ya Bandari, viwanja vya ndege kupambana na uingizaji na usafishaji wa mifuko hiyo.Akinukuliwa na gazeti moja la kila siku nchini, Meneja wa kiwanda cha Dar es Salaam Oceanic Development (DOD) kinachofanya biashara ya bidhaa za plastiki Abdallah Issa, mbali na kudai kuupokea mpango hulo alisema agizo hilo kwao maana yake ni kujiandaa kupata hasara.“Hivi ninavyozungumza tuna mwezi mmoja kama na nusu hivi wa kumaliza malighafi tuliyonayo na bidhaa zetu, inawezekana vipi katika kipindi hiki kifupi,” anasema Abdallah.Anasema kwamba anatambua kilio cha bidhaa za plastiki na kukiri majirani Kenya, Rwanda na Zanzibar wameshachukua hatua, lakini alisema suala la maandalizi na watu kupewa muda wa kutosha lilipaswa kufanyika.Anaongeza kuwa huko nyuma yaliwahi kufanyika mazungumzo kuhusu mifuko ya plastiki yaliyohusisha wadau mbalimbali, lakini suluhisho halikufikiwa na kwamba linapokuwa wakati huu ina maana wazalishaji wa mifuko hiyo wajaindae kuja na njia mbadala
3kitaifa
.Waziri Mkuu Kassim Majaliwa ameuagiza Ubalozi wa Tanzania nchini Russia kuratibu mipango ya Wafanyabiashara wa nchi hiyo wanaokusudia kuwekeza nchini kwa kuwaunganisha na Taasisi na Wizara husika.Waziri Mkuu Majaliwa ametoa agizo hilo baada ya kugundua uwepo wa Wafanyabiashara wengi wa Russia wanaokusudia kuja Tanzania kwa ajili ya kuangalia maeneo ya uwekezaji pamoja na kutafuta Wafanyabiashara wa Kitanzania watakaoungana nao katika uwekezaji wanaokusudia kuufanya. “Tayari miadi imekwishawekwa ya kuwakaribisha Wawekezaji wa Russia kuja Tanzania kwa ushawishi wa kwangu mwenyewe pamoja na ushawishi wa Wafanyabiashara wa Tanzania, hivyo nisingependa Wafanyabiashara hao wasumbuliwe au kukatishwa tamaa katika kutimiza nia yao hiyo”, amesisitiza Waziri Mkuu Majaliwa.Ameongeza kuwa, mkutano baina ya Wakuu wa nchi na Serikali kutoka Mataifa ya Afrika na Russia  uliomalizika katika mji wa Sochi, ulilenga kujenga uhusiano mzuri zaidi katika nyanja mbalimbali hususani za kiuchumi.Kwa mujibu wa Waziri Mkuu Majaliwa, Russia imeutumia mkutano huo kueleza bayana maeneo ambayo wako tayari kushirikiana na Afrika katika kuwekeza kwa faida ya pande zote mbili.Ameyataja maeneo hayo kuwa ni pamoja na uuzaji wa zana za kilimo, uwekezaji katika sekta za mafuta, gesi na madini na ujenzi wa miundombinu hasa reli.Leo Waziri Mkuu Majaliwa anaondoka nchini Russia na kuelekea nchini Azerbaijan ambako pia atamwakilisha Rais John Magufuli katika mkutano wa siku Mbili wa nchi zisizofungamana na upande wowote.
1uchumi
MANCHESTER, ENGLAND KOCHA wa Manchester City, Pep Guardiola, ameanza kujisalimisha mapema kutokana na ushindani wa Ligi Kuu nchini England huku akisema hawezi kuwa bingwa kila msimu. Kocha huyo amesema hata kwenye mchezo wa gofu na tenisi mabingwa huwa wanapoteza, hivyo hata yeye kwenye soka kuna msimu anaweza kukutana na ushindani wa hali ya juu na akashindwa kufanya vizuri. Nafasi ya Manchester City kutetea ubingwa msimu huu ni ndoto kutokana na ushindani uliopo, timu hiyo kwa sasa inashika nafasi ya kwenye msimamo wa Ligi baada ya kucheza michezo 13 na kujikusanyia pointi 28, wakati huo Leicester City wakiwa na pointi 29 nafasi ya pili huku Liverpool wakiwa vinara kwa pointi 37. Manchester City imeachwa pointi tisa na wapinzani hao Liverpool, hivyo Guardiola anaamini anaweza hasifanye vizuri msimu huu, ilo ni jambo la kawaida kwenye michezo ya aina yoyote. “Presha kubwa iliopo kwa sasa kwenye timu yetu ni kuhofia kushindwa kutetea ubingwa, lakini hili ni jambo la kawaida kwenye mchezo wa aina yoyote, siku zote ushindani unakuwa mkubwa na tunapambana ili kuhakikisha tunatimiza lengo letu. “Bingwa wa mchezo wa gofu hawezi kushinda kila wakati, hata mabingwa wa tenisi pia wanapoteza, hivyo hata mimi ninaweza kupoteza kwa kuwa michezo ndiyo ilivyo, ila tunapambana kuhakikisha tunatetea ubingwa, bado tuna nafasi kwa kuwa ligi bado ipo nyuma, lakini wapinzani wetu na wao wanapigania nafasi ya ubingwa,” alisema Guardiola. Mabingwa hao watetezi wamekuwa na wakati mgumu msimu huu kutokana na baadhi ya wachezaji wake kuwa majeruhi tangu mwanzo wa msimu, lakini kuna taarifa kutoka ndani ya klabu hiyo kuwa baadhi ya wachezaji wake wameanza kufanya mazoezi mepesi kwa ajili ya kutaka kurudi viwanjani.
5michezo
Mara baada ya kutua, Samatta ambaye pia ni mfungaji bora wa michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika kutokana na mabao yake saba, alisema wachezaji wa Tanzania wanaweza kuizamisha Algeria na pia kupata mafanikio binafsi, kikubwa ni kuweka juhudi, malengo na kujua wanataka nini.Akizungumza baada ya kuwasili Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA), Dar es Salaam ambako Samatta alipokelewa na familia yao ikiongozwa na baba yake mzazi Ally Samatta na mashabiki wa soka, alisema kujituma kunaweza kukufikisha mbali zaidi hasa pale unapokuwa na nia ya dhati na mafanikio katika soka.Samatta alijikuta akishindwa kujizuia kuonesha furaha baada ya kukutana na familia yake ikiwa inamsubiri uwanja wa ndege kwa ajili ya kumpongeza kwa mafanikio yake pamoja na kusalimiana naye kabla ya kuchukuliwa na uongozi wa Shirikisho la Soka nchini (TFF) ili kuingia kambini.Akizungumzia pambano dhidi ya Algeria, alisema na wanafahamu Algeria ni timu bora na ngumu barani Afrika, lakini watashirikiana na wachezaji wengine wa Stars kuhakikisha ushindi unapatikana.Samatta na Thomas Ulimwengu walitua jana baada ya kukwama kwa simu moja Nairobi, Kenya ambako ndege iliyokuwa iwalete nchini ilizuiliwa kuruka kutokana na hali ya hewa kuwa mbaya.
5michezo
NAIROBI, KENYA RAIS Uhuru Kenyatta alijibu maswali ya mashabiki katika ukurasa wake wa Facebook juzi asubuhi, ambapo pamoja na mambo mengine alitetea rekodi ya serikali yake akisema haijaachwa nyuma na Tanzania linapokuja suala la usafiri wa umma. Ikiwa ni siku moja kabla ya mdahalo wa urais, ambao awali timu yake iliashiria kutohudhuria kabla ya baadaye jana kufuta ratiba ya kampeni katika eneo la Samburu, Rais Kenyatta siku hiyo alichagua kuzungumza na mashabiki, tukio lililotangazwa moja kwa moja na vituo vya KBC na K24 TV. Mkuu huyo wa taifa alijibu maswali yaliyotumwa kabla na ambayo yeye na timu yake walichagua ya kujibu. Maswali hayo yaliangazia masuala ya uchumi, rushwa na chaguzi zijazo na maendeleo ya miundo mbinu. Kenyatta aliwataka mashabiki wake milioni tatu wa Facebook pamoja na wafuasi kuombea amani uchaguzi mkuu ujao huku akiwasihi wampe nafasi nyingine ya kuongoza Kenya kwa kipindi cha miaka mitano ijayo. Akifahamu kuwa asilimia 51 ya wapiga kura milioni 19.6 ni vijana wa miaka kati ya 18 na 35, Rais Kenyatta alitengeneza majibu yake yaliyowalenga vijana akieleza kwanini serikali yake ndiyo jibu la matatizo yao. Alitolea mfano wa miradi ya reli ya kiwango cha Standard Gauge (SGR), barabara, umeme kuwa itatengeneza mamilioni ya ajira kwa ajili yao. “Tuna mpango wa kujenga mtandao mwepesi wa reli kwa ajili ya usafiri wa umma jijini Nairobi, kuipanua SGR hadi Naivasha, Narok, kisha Kisumu,” alisema, akijibu swali la mtumiaji mmoja wa Facebook aliyekosoa Kenya kuachwa nyuma na Tanzania linapokuja suala usafiri wa umma. “Na wala hatujaachwa nyuma, bali tuko katika ratiba,” alisema. Kuhusu Ufisadi, Rais Kenyatta alitetea rekodi yake akisema dhamira ya serikali yake kupambana na rushwa  iko wazi. “Serikali yangu ni ya kwanza kuanzisha mpango unaohusisha mashirika mbalimbali kushughulika na ufisadi. Na kutokana na hilo nimepoteza marafiki wa karibu, mawaziri.” Ushirika wa upinzani National Super Alliance (Nasa) ukiongozwa na mpinzani mkuu wa Kenyatta, Raila Odinga wameufanya ufisadi kuwa ajenda kuu ya kampeni yao.
2kimataifa
MWANAMUZIKI na mfanyabiashara mkubwa, Jay-Z (pichani) kupitia kampuni yake ya usimamizi wa masuala ya michezo, Roc Nation Sports amefunguliwa mashtaka mahakamani na bondia Daniel Franco akidai kampuni hiyo ilimlazimisha kupigana mara tatu ndani ya siku 79.Franco amedai alipigana mapambano hayo kwa siku hizo, ikiwa ni kinyume na sheria akiwa chini ya kampuni hiyo na kumsababishia madhara makubwa ya ubongo wake mpaka sasa.Bondia huyo ambaye aliingia mkataba na Roc Nation mwaka 2015 alianza kupata matatizo hayo mwaka 2017 alipohitaji kuahirishwa kwa pambano lililo mbele yake kwa kuwa alikuwa akiumwa mafua makali na hakupata muda wa kutosha wa kujifua juu ya pambano hilo.Ameeleza kwamba Roc Nation walikataa ombi lake hilo na wakamhitaji aingie ulingoni ambapo alipoteza vibaya kwa kupigwa katika raundi ya tatu tu, baada ya hapo Roc Nation walipanga pambano jingine ndani ya siku 50 na hawakumpa muda wa kupona majeraha yake.Baada ya pambano hilo, siku 29 baadaye wakampangia pambano jingine bila ya kuangalia maendeleo ya afya yake, kitu alicholalamika kingeweza kugharimu uhai wake kwa kuwa tayari alihisi hayupo sawa ndani ya kichwa chake na alihisi kuvuja kwa damu kabla ya pambano hilo la tatu.
5michezo
Na Waandishi Wetu – Dar es Salaam MKE wa mwanasiasa mkongwe nchini, Peras Kingunge Ngombale Mwiru, amefariki dunia jana katika Hospitali ya Taifa Muhimbili, huku hali ya afya ya mumewe ikiwa si nzuri. Akizungumza na MTANZANIA Dar es Salaam jana, mtoto mkubwa wa Kingunge, Kinje, ambaye muda mwingi alikuwa akilia, alikiri mama yake kufariki dunia, huku baba yake akilazwa chumba cha wagonjwa mahututi (ICU) katika hospitali hiyo. Kingunge (88) amelazwa Muhimbili karibu wiki mbili sasa baada ya kung’atwa na mbwa sehemu mbalimbali za mwili wake. “Mama amefariki hata baba (mzee Ngombale) hajui juu ya jambo hili kwa sababu naye ni mgonjwa ndiyo kwanza ametolewa theatre (chumba cha upasuaji) anaumwa… aling’atwa na mbwa nyumbani tutamueleza atakapoamka,” alisema. Kinje alisema kuwa mama yake alianza kupatiwa matibabu hospitalini hapo kutokana na tatizo la kupooza mwili tangu mwishoni mwa mwaka jana. “Mama alianza kupooza tangu mwaka jana, tukamhamishia Muhimbili kwa ajili ya matibabu zaidi, lakini Mungu amempenda zaidi,” alisema Kinje. Alipoulizwa baba yake amefanyiwa upasuaji wa nini, Kinje alishindwa kuzungumza kutokana na muda mwingi kulia. Naye Ofisa Uhusiano wa Muhimbili, John Steven, alithibitisha kifo cha Peras na kusema kuwa alilazwa hospitalini hapo tangu Oktoba 3, mwaka jana. “Kweli mama Kingunge amefariki mchana wa leo (jana), wakati akiendelea kupatiwa matatibu hapa,” alisema. AFYA YA KINGUNGE Mmoja wa wana familia hiyo, Toni Kingunge, aliiambia MTANZANIA kuwa hadi jana machana, Kingunge alikuwa amelazwa ICU, akisubiri kufanyiwa upasuaji. “Mzee amelazwa ICU kutokana na matatizo yanayomkabili, si kwamba ana hali mbaya, lakini madaktari wamempumzisha huko kwa ajili ya uangalizi… ana matatizo kwa sababu alishambuliwa na mbwa akiwa nyumbani kwake,” alisema Toni. Alisema Kingunge alishambuliwa na mbwa karibu wiki mbili na nusu zilizopita nyumbani kwake Victoria, Dar es Salaam nyakati za asubuhi alipokuwa akitoka kwa ajili ya kufanya mazoezi. “Baba alishambuliwa na mbwa karibu maeneo manane tofauti mwilini mwake, sasa hali hiyo imemletea matatizo ambayo jopo la madaktari wanahangika kumtibu, licha ya kupata tiba ya awali ya kuzuia wadudu au sumu hatarishi. “Hawa mbwa kwa kawaida hufungiwa ndani ya banda pale nyumbani, siku hiyo inaonekana mzee wakati anatoka walikuwa hawajafungiwa, wakaanza kumshambulia ovyo, tukajitahidi tukamwahisha hospitali kupata tiba za awali,”alisema Toni. Alisema hadi jana, Kingunge alikuwa na tatizo jingine la kuvimba miguu jambo ambalo hawajajua limesababishwa na nini. “Mzee anajitambua mpaka muda huu, lakini ana tatizo la kuvimba miguu na vile vidonda alivyong’atwa na mbwa vinaendelea vizuri, tunaamini akiwa ICU atapata matibabu zaidi… mie niko nyumbani kwa ajili ya maandalizi ya msiba wa mama, nitakupa mawasiliano ya Kinje ambayo yuko na mzee Muhimbili akueleze zaidi,” alisema Toni. Kuhusu msiba wa mama yao, alisema taratibu nyingine zinaendelea kufanyika na ratiba kamili itatolewa wakati wowote.
3kitaifa
MAKAMISHNA na Warajisi Wasaidizi wa Mikoa wameshauriwa kuhamasisha Vyama vya Akiba na Mikopo (Saccos) na Ushirika vianze kuwekeza katika miradi mikubwa itakayovipa maendeleo zaidi na wanachama kwa ujumla.Saccos na Vyama vya Ushirika vinaweza kujenga majumba ya kupangisha, kujenga vitega uchumi vikubwa, kujenga njia za usafiri na kuwekeza katika miradi mingine mingi. Akizungumza katika Kikao Kazi cha Makamishna na Warajisi Wasaidizi wa Mikoa jijini hapa, Mwenyekiti wa Tume ya Maendeleo ya Ushirika Nchini, Dk Titus Kamani alivitaka vyama hivyo kufanya uwekezaji katika miradi.Alisema vyama vya ushirika na Saccos nchini, zinatakiwa kuwekeza kwenye miradi mikubwa kama zinataka kushiriki katika mkakati wa serikali ya awamu ya tano ya kuingia katika uchumi wa kati na maendeleo ya viwanda.Pia aliwataka wale wote wanaodaiwa madeni au waliojimilikisha mali za vyama vya ushirika ngazi za juu hadi chini kuzirudisha mali hizo. Alisema warajisi ndio wasimamizi wa rasilimali za ushirika za maeneo yao, hivyo wawaagize waliopora mali hizo kuzirejesha kwa ngazi zote.Alisema wadaiwa waliokopa au kujimilikisha maghala, majengo, miundombinu mbalimbali, mashamba na raslimali nyingine za ushirika na Saccos wote wanatakiwa kurudisha mali hizo.Aliagiza wakopaji hao wasipoteze fedha zao kwenda mahakamani kwani wanapoteza bure fedha zao, hakuna njia nyingine zaidi ya kulipa. Alisema vyama vya ushirika na Saccos zinatakiwa kuunganisha nguvu kukuza mitaji na kujiingiza katika uwekezaji badala ya kufanya shughuli ndogo zinazoleta maendeleo kidogo.Alisema warajisi wa mikoa na maafisa ushirika wa wilaya na ngazi za chini, wanatakiwa kufanya kazi wakishirikiana na wakuu wa mikoa, wilaya na maofisa tawala, wakurugenzi na walezi wa vyama hivyo katika ngazi zote.Alitaka wahakikishe wakulima, wafugaji na wavuvi na taasisi wanaanzisha shughuli zao kwa ushirika, kwani una nguvu na sauti kubwa zaidi kama walivyofanya wakulima wa korosho.Alisema watu wanatakiwa kuuamini ushirika na Saccos kwani ni benki za nyumbani, kutokana na urahisi wake wa kutoa mikopo yenye riba ndogo, hivyo wananchi wajiunge na ushirika na waumini ni mkombozi wa wananchi wengi. Katibu wa Tume ya Maendeleo ya Ushirika nchini, Tito Haule aliwataka Warajisi Wasaidizi kufanya kazi hiyo kwa weredi na kuhakikisha ushirika katika maeneo yao unakuwa imara.Aliwataka viongozi hao kujipima uongozi wao kwa kufanya mambo ya maendeleo ikiwemo la kukusanya fedha za Mfuko wa Usimamizi wa Mrajisi ambao ni muhimu kwa maendeleo yake. Haule alisema katika kujipima wanatakiwa kuunda bodi na taasisi nyingine kwa umakini na siyo kisiasa ili kupata uongozi bora zaidi. Aliwataka warajisi hao kukusanya mapato kutokana vyama vya ushirika kwani baadhi ya mikoa haijafanya vizuri katika makusanyo.
3kitaifa
Na NORA DAMIAN-DAR ES SALAAM MAPATO ya Halmashauri ya Manispaa ya Ilala yameshuka hadi kufikia kukusanya chini ya asilimia 50, kwa mwezi. Sababu zilizotajwa kuchangia hali hiyo ni kunyang’anywa na Serikali kuu jukumu la kukusanya kodi ya majengo na  kufungwa kwa baadhi ya biashara. Nyingine ni upungufu wa watumishi na marekebisho ya sheria za leseni za biashara, ambapo utaratibu wa sasa wa kupata leseni ni lazima mtu awe na Namba ya Utambulisho wa Mlipakodi (TIN). Hayo yaliainishwa jana wakati wa kikao cha Baraza la Madiwani wa Halmashauri hiyo ambacho pia kilijadili taarifa za Kamati ya Kudumu ya Fedha na Utawala na Kamati ya Uchumi na Huduma za Jamii. Taarifa ya fedha inayoanzia Oktoba hadi Desemba mwaka jana, inaonesha katika kipindi hicho halmashauri hiyo ilijiwekea lengo la kukusanya Sh bilioni 16.3 kwa hesabu za robo mwaka kuanzia Oktoba hadi Desemba mwaka jana, lakini ilikusanya Sh bilioni 12.8. Akiwasilisha taarifa hiyo, Mwenyekiti wa Kamati ya Fedha, Greyson Celestine, alisema hali ya mzunguko wa fedha ni ngumu, biashara nyingi zimefungwa, wamenyang’anywa kodi za majengo na hata maofisa biashara waliopo hawatoshelezi. Kwa mujibu wa mwenyekiti huyo, hadi sasa maofisa biashara waliopo katika halmashauri hiyo ni 24 wakati mahitaji ni 39. Akizungumza na MTANZANIA jana baada ya kikao hicho, Celestine alisema licha ya ripoti hiyo ya robo mwaka hata katika robo nyingine za mwaka hali ya ukusanyaji mapato haikuwa nzuri. Alisema kwa mwaka wa fedha 2016/2017 walijiwekea lengo la kukusanya Sh bilioni 83 na kwamba katika kodi ya majengo pekee walitegemea kukusanya Sh bilioni 20, lakini fedha hizo zimekosekana kutokana na Serikali kuu kuchukua chanzo hicho. “Siwezi kukupa taarifa zinazoonyesha mpaka sasa tumekusanya shilingi ngapi lakini kwa kifupi hali si nzuri, tumekuwa tunakusanya chini ya asilimia 50 na kuna wakati tunakusanya hadi asilimia 35. “Maduka mengi yamefungwa kama pale Aroma na Segerea yako maduka nayafahamu yamefungwa kutokana na kufilisiwa na benki, watu walikopa wakashindwa kupeleka marejesho,” alisema Celestine”alisema. Naye Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri hiyo, Msongela Palela, alikiri baadhi ya biashara kufungwa na kwamba wako wafanyabiashara waliotoa taarifa na wengine wameamua kukimbia. “Si siri hali ya uchumi imekuwa ngumu, wakati wa kupanga bajeti ya mwaka 2016/2017 kuna baadhi vya vyanzo vya mapato vilipitishwa lakini vimeondolewa na kusababisha halmashauri kushindwa kufikia lengo. Pale kwangu (ofisini) kuna mabango ya milioni 200 yameshushwa kwa sababu wahusika wameshindwa kuyalipia. “Makubaliano yalifikiwa tuendelee kupokea ada za leseni za biashara na kuwapa watu risiti lakini tusitoe leseni, suala hili lilifika ngazi ya kitaifa tukatuhumiwa kutofuata utaratibu wa TIN na kuisababishia Serikali hasara hivyo tukaamua kusitisha,” alisema Palela. Baadhi ya tozo zilizopitishwa katika bajeti kisha kuondolewa kutokana na changamoto mbalimbali ni pamoja na ada za machinjio na nyingine zilizoko kwenye masoko. Pia alisema kutokana na changamoto ya uhaba wa watumishi wamelazimika kuchukua maofisa ustawi wa jamii 10 ili wasaidie katika ukusanyaji wa mapato. “Ajira zilisimamishwa kwa maelekezo ya serikali na sisi tumekwama tunashindwa kuendelea mbele, tuliamua kutafuta watumishi kutoka halmashauri nyingine lakini hili nalo limegonga mwamba haturuhusiwi kuhamisha watumishi,” alisema. Mkurugenzi huyo alisema wameamua kutumia vikosi kazi ambavyo vinahamasisha wananchi na kupita kila kata kukusanya mapato hivyo kuwapunguzia mzigo wa kuja halmashauri. Naye Mkuu wa Idara ya Maendeleo ya Jamii, Ustawi wa Jamii na Vijana, Fransisca Makoye, alisema changamoto ya makusanyo ya mapato imewaathiri hasa katika kutoa mikopo ya vikundi vya wanawake na vijana. Sheria imeelekeza kila halmashauri kutenga asilimia 10 ya mapato ya ndani kwa ajili ya kukopesha vijana na wanawake ambapo kwa Dar es Salaam fedha hizo zimekuwa zikipitia katika Benki ya DCB. “Kiasi kilichopangwa kupelekwa kinapungua na katika robo ya mwaka iliyopita tulipeleka Sh milioni 450 lakini bado mahitaji ni mengi, mweka hazina anajitahidi kupeleka fedha kadiri inavyopatikana,” alisema Makoye. MADIWANI Diwani wa Kata ya Ukonga, Jumaa Mwaipopo (Chadema), alisema hali ya biashara katika kata yake imekuwa ngumu na hadi sasa maduka 220 yamefungwa. “Wakati tunaokwenda nao si mzuri, maduka mengi yanafungwa hivyo ni lazima tuwe na mikakati mingine. Hayati Gadafi (Rais wa zamani wa Libya), baada ya kuona mafuta yanapungua aliamua kuanzisha kilimo cha matunda, sisi tunaweza kutafuta eka 400 ama 500 halafu tukaanzisha kilimo cha mtama,” alisema Mwaipopo. Naye Diwani wa Kata ya Kitunda, Nice Gisunte (Chadema), alisema “Tunaandaa makisio lakini hatufikii lengo, napata shaka kama wataalmu wetu wanafanya kazi sawasawa,” alisema. Diwani wa Kata ya Kipawa, Kenedy Simion (Chadema), alipendekeza kuwapo na utaratibu wa kupata mapato kutokana na biashara ya pikipiki maarufu kama bodaboda. Hata hivyo Mbunge wa Segerea, Bonnah Kaluwa (CCM), alipinga hoja hiyo na kudai kuwa biashara hiyo imekuwa suluhisho kubwa la ajira kwa maelfu ya vijana nchini. “Bodaboda ni watu wetu na ajira hakuna, wanafanya kazi katika mazingira magumu Trafic (Askari wa Usalama Barabarani), Sumatra (Mamlaka ya Usafiri wa Nchi Kavu na Majini) na askari wa jiji wanachukua fedha zao. Na sisi tukiweka utaratibu tutakuwa hatujawatendea haki…ni watu wetu tunawahitaji mwaka 2020,” alisema Kaluwa. Naye Mbunge wa Ukonga, Mwita Waitara (Chadema), alipendekeza ifanyike tathimini kuonesha miradi iliyokwama na kupendekeza vyanzo vipya vya mapato. Hata hivyo Mkurugenzi wa Manispaa ya Ilala, Palela, alisema wana mpango wa kuwaingiza bodaboda na wamachinga na kuwa vyanzo vya mapato ya halmashauri hiyo.
3kitaifa
WAZALISHAJI wa mkaa endelevu unaozalishwa kwa vumbi la mbao na takataka za miti, wameiomba serikali itoe ruzuku na kupunguza baadhi ya kodi ili bidhaa hiyo ihimili ushindani dhidi ya mkaa wa asili na kuni. Waliotoa ombi hilo jana kwa Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk Hamis Kigwangalla katika kikao kilichoikutanisha wizara yake na wadau wa sekta ya misitu wa Mkoa wa Iringa mjini Iringa. Mkurugenzi wa Kampuni ya Mena Wood Briquetting Ltd, Anyezwisye Mahenge ambaye pia ni kiongozi wa wazalishaji hao, alisema mkaa endelevu ni nishati mbadala na rafiki wa mazingira.“Mkaa huu unaokoa ukataji ovyo wa miti kwa matumizi ya mkaa na kuni na matokeo yake hulinda mazingira,” alisema Dk Kigwangalla.Mahenge alimwambia Dk Kigwangalla kwamba kodi (ikiwemo Kodi ya Ongezeko la Thamani - VAT) zinazotozwa kwa wazalishaji wa mkaa huo na ukosefu wa masoko zinadhoofisha viwanda vyao.Akitoa takwimu, Mahenge alisema viwanda vinne kati ya 12 vya mkaa huo vimeshafungwa kwa sababu ya kushindwa kumudu gharama za uendeshaji.“Tunaishauri serikali itoe ruzuku ili viwanda hivi vyenye mchango mkubwa katika uhifadhi wa mazingira, visife lakini bidhaa hiyo izalishwe kwa wingi kumudu soko la ndani,” alisema.Dk Kigwangalla aliahidi kuzichukua changamoto hiyo na kuzifanyia kazi na idara nyingine za serikali ili kuinusuru sekta hiyo ya viwanda vya mkaa mbadala.
3kitaifa
Kijana huyu anafanya shughuli za ulimaji mboga baada ya kupatiwa mashine ya kuvuta maji kwa ajili ya umwagiliaji pamoja na jembe la plau miezi mitatu iliopita. Zana hizo alizipata kupitia mradi wa kampuni ya simu ya Airtel, Airtel Fursa Tunakuwezesha.Akielezea furaha yake baada ya kukabidhiwa chombo cha usafirishaji mazao kutoka kampuni ya simu ya mkononi ya Airtel, alisema sasa kila kitu kitaenda vyema.Akikabidhi pikipiki kwa ajili ya usafirishaji mazao kwa Innocent, baada ya kumtembelea shambani kwake mwishoni mwa wiki hii na kuona maendeleo yake ya shughuli zake za ulimaji, meneja masoko wa kampuni ya Airtel kanda ya Ziwa, Emmanuel Raphael amewataka vijana kuiga mfano unaonyeshwa na Innocent.Aliongeza kwa kusema: “Vijana inabidi waachane na dhamira ya kutaka kukaa tu vijiweni na kusubiri watafutiwe ajira. Ni juhudi zao wao wenyewe ndio zitakazoweza kuwakomboa na kupata maendeleo kama alivyoweza kufanikiwa Innocent.“Kufuatia kushikwa kwake mkono na Airtel, Innocent ameweza kubadilisha maisha yake na familia yake. Hivyo nawahimiza vijana wasikate tamaa na kujitokeza kwa wingi kwa kuchangamkia fursa hii na nyingine nyingi zinazowazunguka.”
1uchumi
Simba Jumatatu iliibuka na ushindi wa bao 2-1 dhidi ya Kagera Sugar katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara uliofanyika kwenye uwanja wa CCM Kambarage mjini Shinyanga.Alisema lengo lao ni kuhakikisha wanashinda mechi zao zote zilizobaki ili kumaliza katika nafasi ya pili na kuweza kupata nafasi ya kuwakilisha nchi katika Kombe la Shirikisho la Afrika.Kopunovic alisema ushindi huo wa Shinyanga ulitokana na wachezaji wake kujitoa kwa kupambana na wapinzani wao na kupata matokeo hayo, ambayo yalikuwa muhimu kwao.“Nimefurahi kuona wachezaji wangu wakicheza kwa kiwango cha juu na kupata ushindi nadhani imetokana na kila mmoja wetu kutambua umuhimu wa ushindi katika mchezo ule naamini tutaendelea kucheza kwenye ubora ule ule katika mechi zetu zijazo,” alisema Kopunovic.Kopunovic alisema mikakati yao ni kuhakikisha Simba inamaliza msimu katika nafasi ya pili na hilo litawezekana endapo tu watashinda mechi zao tano zilizobaki kabla ya kumalizika kwa msimu huu.“Najua ligi imezidi kuwa ngumu kutokana na kila timu kutaka kujiweka sehemu salama kwa kutimiza malengo yake, lengo letu ni kumaliza msimu nafasi mbili za juu na hili linawezekana kutokana na kasi na kiwango tunachokionyesha hivi sasa,” alisema Kopunovic.Aidha, Mserbia huyo alisema kama kocha hana matumaini ya kupata ubingwa msimu huu kutokana na kasi ya wapinzani wao, Yanga wanaoongoza ligi hiyo pamoja na Azam inayoshika nafasi ya pili, lakini hawawezi kukata tamaa watajitahidi kuhakikisha wanashinda mechi zao ili kutimiza kile walichojipangia mwishoni mwa msimu.“Kama kocha sina matarajio ya ubingwa msimu huu ingawa ikitokea nitafurahi, lengo langu kubwa ni angalau kumaliza nafasi ya pili ili tuweze kupata nafasi ya kushiriki michuano ya kimataifa mwakani, kwa sababu nitakuwa na timu kwa muda mrefu na hata masuala ya usajili nitasimamia mimi,” alisema Kopunovic.Baada ya kuifunga Jumatatu iliyopita Simba imeendelea kushika nafasi ya tatu kwenye msimamo wa ligi ya Vodacom ikiwa na pointi 35 tofauti ikiwa ni pointi moja na Azam inayoshika nafasi ya pili ikiwa na pointi 36 na tano kwa vinara Yanga wenye pointi 40 na timu hizo mbili leo zinacheza mechi zao za viporo.
5michezo
  Msimu wa soka sasa umerejea rasmi! Wiki iliyopita, Ligi Kuu ya England ilianza kutimua vumbi na wikiendi hii pia tutashuhudia nyasi zikiwaka moto kunako Ligi Kuu ya Uhispania ‘La Liga’ na ile ya Ujerumani ‘Bundesliga’ msimu wa 2019/2020. Mechi hizo pia zinatoa fura ya kupiga mkwanja kwakutabiri matokeo ya michezo kadha wa kadha. Opera News itakuwa ikikuletea michezo mitatu ya kutabiri kila wikiendi. Sasa wikiendi hii tunaanza na michezo hii. Arsenal VS Burnley(Jumamosi) Arsenal almaarufu Washika Bunduki walishinda mchezo wao wa ufunguzi ambao walikuwa ugenini kwa bao 1-0 dhidi ya Newcastle. Jambo la kuvutia zaidi, kocha Unai Emery hakuwa na nyota wake Mesut Ozil pamoja na beki wake wa kushoto Sead Kolasinac wakati huo huo akimpumzisha mshambuliaji wake hatari Alexandre Lacazette. Kwa upande wao, Burnley wakiwa nyumbani waliwaadhibu Southampton magoli 3-0 na kuwa mbele ya Arsenal kwenye msimamo wa ligi. Hata hivyo hawajawahi kuwafunga Arsenal ndaniya mechi 5 za mwisho walizokutana. Alama za kutabiri: Arsenal wamepewa @1.36 za kushinda Everton-Watford(Jumamosi) Mechi iliyopita walitoka sare ya bila kufungana dhidi ya Leicester City na watakuwa wakihitaji ushindi ili kuwafurahisha mashabiki wao katika uwanja wa nyumbani wikiendi hii. Everton maarufu ‘The Toffees’ wana timu nzuri kiasi na msimu uliopita walipata matokeo ya kuridhisha mbele ya baadhi ya wababe, Arsenal walipigwa 3-0 huku United wakichakazwa 4-0! Wakati huo huo, Watford walishuhudia wakipokea kipigo kizito nyumbani msimu uliopita mbele ya Brighton ambao wameshuka daraja cha mabao 3-0. Alama za kutabiri: Everton wamepewa @1.73 za kushinda Manchester City-Tottenham Hotspurs(Jumamosi) Mabingwa hao watetezi wamethibitisha kwamba bado wana kiu ya ubingwa kwa kuwafunga West Ham mabao 5-0 katika dimba lao la nyumbani la London Stadium. Raheem Sterling alipiga hat-trick katika mchezo huo ambao vijana wa Pep Guardiola walitawala vilivyo. Tottenham waliibuka na ushindi wa mabao 3-1 dhidi ya wageni Aston Villa waliopanda daraja msimu huu. Historia inawabana Spurs kwani hawajawahi kupata matokeo ya ushindi Etihad mbele ya Pep Guardiola. Alama za kutabiri: Manchester City wamepewa @1.36 za kushinda
5michezo
Aveline Kitomary -Dar es salaam IDADI ya majeruhi wa ajali ya lori la mafuta iliyotokea mkoani Morogoro waliofariki dunia, imefikia 95. Wakati idadi ikiongezeka, majeruhi Rusuje Mollel (38), ambaye alikuwa akipatiwa matibabu hospitali ya mkoa huo, jana amehamishiwa Hospitali ya Taifa Muhimbili kwa matibabu zaidi. Mollel, anakuwa majeruhi wa 47 waliopokewa hospitalini hapo. Akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam jana, Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano ya Umma Muhimbili, Aminiel Aligaesha, alisema majeruhi waliobaki ni 20 na wote wamelazwa chumba cha uangalizi maalumu (ICU). Aligaesha alisema majeruhia Rajab Ally (32), alifariki dunia usiku wa kuamkia jana na kufanya idadi ya majeruhi waliofariki wakipatiwa matibabu hospitalini hapo kufikia 27. “Jana mchana tulimpokea majeruhi mmoja ambaye alikuwa akipatiwa matibabu Morogoro, baada ya kuzidiwa ameletwa Muhimbili ili apate matibabu zaidi. “Lakini usiku wa kuamkia leo (jana), majeruhi mmoja amefariki dunia na kufanya idadi yao kufikia 27 waliofariki dunia, wamebaki 20 na wote wako ICU,” alisema. WATU WAZIDI KUTOA DAMU Aligaesha alisema kuanzia Agosti 11, hadi jana, wamefanikiwa kupata chupa 700 za damu ambazo zimetokana na juhudi za watu na makundi mbalimbali waliojitokeza kutoa msaada. “Mwitikio wa watu kujitokeza kuchangia damu ni mkubwa na tangu Agosti 11, mwaka huu, mpaka sasa tumepata uniti 700, natoa wito kwa makundi, taasisi na watu binafsi waendelee kuchangia damu kwani inatumika hata kwa wagonjwa wengine,” alieleza  Aligaesha. Jana, zaidi ya watu 50 kutoka Chama cha Wafanyakazi wa Malori Tanzania (Chawamata), walitoa damu kwa matumizi ya majeruhi hao. Akizungumza wakati wa uchangiaji damu, Katibu Mkuu wa Chawamata, Greysona Michael, alisema wao kama madereva wameamua kutoa damu kutokana na kuguswa na tukio lililotokea, hivyo wameamua kuwasaidia majeruhi hao. “Tumekuja na wanachama wetu zaidi ya 50 kuchangia damu kwa majeruhi wa ajali, suala hili limetugusa sisi kama madereva. Aliyepata ajali ni mwanachama wetu, tunafanya mpango wa kumsaidia,” alisema Michael. Alisema wanaendelea kupitisha michango katika chama chao ili kuweza kutoa misaada mingine ya vifaa vitakavyoweza kuwasaidia majeruhi hao. “Hatutaishia tu kutoa damu, wiki ijayo tuna mpango wa kuwasilisha  msaada wa vifaa kwa majeruhi hawa ili kuwatia moyo na kuwafariji. Tunajiona kama sehemu muhimu kwa msaada kwao,” alisema Michael.
4afya
DOHA, QATAR   NYOTA wa mchezo wa tenisi raia wa nchini Serbia, Novak Djokovic, ameanza mwaka vizuri kwa kutwaa taji la Qatar Open dhidi ya bingwa namba moja kwa ubora duniani, Andy Murry. Fainali hiyo ilikuwa ya kwanza kwa nyota hao kukutana kwa mwaka 2017, lakini Djokovic ambaye anashika nafasi ya pili kwa ubora duniani kwa upande wa wanaume, ameweza kumtembezea kichapo bingwa namba moja Murray. Djokovic alionesha uwezo wake huku akishinda kwa seti 6-3, 5-7, 6-4 na alionekana kutumia nguvu nyingi sana katika mchezo huo ambao walitumia saa mbili na dakika 54. Wataalamu wanadai kuwa katika mchezo huo wa juzi, Djokovic alionesha kiwango cha hali ya juu dhidi ya mpinzani wake tofauti walivyokutana katika michuano ya Barclays ATP World Tour, jijini London kwenye uwanja wa 02 Arena. “Huu ulikuwa ni mchezo mgumu kwangu na ndio maana nimeupoteza, lakini naweza kusema kwamba ni jambo la kujivunia kuuanza mwaka, nimekutana na mpinzani ambaye ana uwezo mkubwa hivyo nimejivunza mengi kutoka kwake,” alisema Murray. Kwa upande wa Djokovic, alisema haikuwa rahisi kupambana na bingwa namba moja, lakini anashukuru ameweza kuonesha moto wake na kuuanza mwaka vizuri. “Nilikuwa na wakati mgumu kucheza na mpinzani mwenye uwezo mkubwa, nilifanya vizuri seti ya kwanza na yeye alifanya hivyo kwa seti ya pili, nakumbuka miezi mitatu ya mwisho mwaka jana sikucheza kama nilivyocheza sasa, hivyo kushinda dhidi ya bingwa ni kama ndoto,” alisema Djokovic. Hata hivyo, Djokovic aliongeza kwa kusema kwamba, ameanza mwaka vizuri hivyo anaamini ataendelea kufanya hivyo hadi mwisho wa mwaka huu.
5michezo
Stars inacheza na Congo ikiwa na kumbukumbu ya kipigo cha mabao 4-1 ilichopata toka kwa Algeria wiki iliyopita katika mechi nyingine ya kirafiki ya kimataifa.Akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam jana, Kocha msaidizi wa Taifa Stars, Hemed Morocco alisema wamejiandaa vema kwa mchezo huo baada ya kupoteza dhidi ya Algeria pamoja na kwamba ana majeruhi wawili."Tumejiandaa vizuri kwani ninajua Congo ni timu nzuri na sisi tunahitaji ushindi baada ya kupoteza mchezo uliopita. Kikosi changu kina majeruhi Aishi Manula ambaye anasumbuliwa na kifundo cha mguu na Abdulaziz Makame," alisema Morocco.Nahodha msaidizi wa Stars, Himid Mao alisema wao wamejiandaa kuhakikisha wanawapa raha mashabiki kwani makosa yaliyojitokeza katika mchezo uliopita wameyafanyia kazi.Kwa upande wa Kocha wa DR Congo, Ibenge Florent alisema anaamini mchezo utakuwa mgumu kwani Taifa Stars itakuwa inapambana kuhakikisha inashinda mbele ya mashabiki wake huku akimtaja Simon Msuva na Mbwana Samatta kama wachezaji wanaowahofia."Tanzania ni jirani zetu pia ni ndugu zetu ndiyo maana tumekubali kucheza nao. Mchezo utakuwa mgumu kwani Taifa Stars haitakubali kufungwa kirahisi mbele ya mashabiki wake na wachezaji Samatta na Msuva tunajua wakipata nafasi wanaweza kufunga bao," alisema Ibenge.Mchezo huo unatarajiwa kuanza saa 10:00 jioni na viingilio ni Sh 5000 VIP A na B huku maeneo mengine ikiwa ni Sh 1000.
5michezo
NA MWANDISHI WETU MABINGWA wa Kombe la Kagame, timu ya Azam imeshtushwa na taarifa za uongozi wa Yanga kumfungia kazi mshambuliaji wake tegemeo, Kipre Tchetche, ili kumsajili kwenye dirisha dogo la usajili linalofunguliwa Jumapili hii. Uongozi wa Azam jana umesema kuwa mshambuliaji huyo bado yupo kwenye mipango ya muda mrefu ya benchi la ufundi la timu hiyo chini ya Kocha Mkuu Stewart Hall na ataendelea kuwepo sana ndani ya timu hiyo. Tchetche amekuwa mwiba mkali kwa timu pinzani, mpaka sasa akiwa ameshafunga jumla ya mabao sita kwenye mechi tisa walizocheza za Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara (VPL) msimu huu. Moja ya mabao hayo ni lile alilotupia walipocheza na Yanga Oktoba 17, mwaka huu kwenye sare ya 1-1, akiisawazishia timu yake alipoingia kipindi cha pili kuchukua nafasi ya Allan Wanga. Mtendaji Mkuu wa timu ya Azam FC, Saad Kawemba, aliliambia MTANZANIA jana kuwa mpaka sasa wamezipata taarifa hizo kupitia magazeti tu na hakuna barua yoyote iliyofika kwao kutoka Yanga ikionyesha kuwa wanamuhitaji Kipre Tchetche. “Hakuna barua yoyote tuliyopokea kutoka Yanga kama inavyodaiwa, Kipre Tchetche bado ni mchezaji wetu, ana furaha kuwa hapa, ana mkataba mrefu Azam FC na bado ataendelea kuwa hapa. “Imekuwa ni kawaida sana kutokea hali hii kila usajili unapofunguliwa, hivi sasa wachezaji wetu wapo mapumzikoni na hatutaki wasumbuliwe,” alisema. Mpaka sasa ligi ikiwa imesimama, Azam FC ndiyo vinara wakiwa na pointi 25 kwenye msimamo, wakifuatiwa na Yanga iliyojikusanyia pointi 23, Mtibwa Sugar 22 na Simba 21.RE
5michezo
Mabao hayo ya jana yalifungwa na Samatta na mchezaji wa Ivory Coast, Roger Assale. Ushindi huo umeifanya Mazembe kutwaa taji hilo kwa ushindi wa jumla ya mabao 4-1 baada ya timu hiyo ya Congo kushinda 2-1 katika mchezo wa awali uliofanyika Algiers Jumamosi ya wiki iliyopita.Samatta ndiye alikuwa wa kwanza kufunga bao katika dakika ya 75, na kuiweka TP Mazembe mbele baada ya kufunga kwa penalti baada ya mchezaji mmoja wa timu hiyo kuchezewa vibaya katika eneo la hatari.Hilo lilikuwa bao la saba la Samatta katika kampeni hizo za kutwaa ubingwa wa Afrika wakiwa sawa na Bakry 'Al Medina' Babiker wa Al Merreikh ya Sudan. Assale alihakikishia ushindi TP Mazembe kwa bao alilofunga katika dakika za mwisho baada ya juhudi kubwa iliyofanywa na Samatta.Mazembe, ambayo inafundishwa na kocha Mfaransa Patrice Carteron,ilitwaa taji hilo kwa mara ya kwanza mwaka 2010, baada ya kuichakaza Esperance ya Tunisia kwa jumla ya mabao 6-1. Mazembe sasa itaiwakilisha Afrika katika mashindano ya Kombe la Dunia kwa klabu yatakayofanyika baadae mwaka huu nchini Japan.Wakati wa kukabidhiwa medali, Samatta na Mtanzania mwingine Thomas Ulimwengu walikuwa wamejifunika bendera ya Tanzania kuonesha uzalendo wao kwa nchi yao. Kwa ushindi huo, TP Mazembe mbali na kutwaa taji hilo la Afrika, pia iliondoka na kitita cha dola za Marekani 1,500,000 huku mshindi wa pili alipata dola 1,000,000 huku timu mbili zilizotolewa katika nusu fainali kila moja iliondoka na dola 700,000.Timu ya tatu katika Kundi kila moja ilipewa kiasi cha dola za Marekani 500,000 huku timu ya nne katika kila Kundi ilipata dola 400,000 kila moja.
5michezo
KAMPUNI ya Ndege Tanzania (ATCL) imesema safari za ndege zake kwenda Harare nchini Zimbabwe na Lusaka nchini Zambia zimepata mwitikio mzuri kutoka kwa wateja tangu zianze wiki mbili zilizopita.Safari hizo za Harare na Lusaka zilianza Februari 22, mwaka huu na zinazihusisha ndege mbili mpya aina ya Airbus A220-300. Ndege hizo zimepewa jina la Ngorongoro na Dodoma.Akifafanua kuhusu safari hizo, Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano wa ATCL, Josephat Kagirwa alisema safari hizo zinafanyika mara tatu kwa wiki katika siku za Jumanne, Ijumaa na Jumapili.Kagirwa alisema japo mpaka sasa ni muda mfupi tangu safari hizo za Harare na Lusaka zianze, lakini mwitikio wa wateja uko vizuri na wanatarajia utakuwa mkubwa zaidi kwa siku za hivi karibuni.“Ndege zetu mbili za Airbus A220- 300 ndiyo zinazofanya safari hizo nchini Zimbabwe na Lusaka kwa kupokezana zamu, na zinachukua masaa mawili kusafiri kutoka Dar es Salaam hadi Harare na huchukua dakika 40 kusafiri kutoka Harare kwenda Lusaka na muda wa kupumzika katika kila kiwanja ni dakika 30,” alisema Kagirwa.Ndege hizo mpya za Airbus A220- 300 zina uwezo wa kubeba abiria 132 kila moja.Kuanza kwa safari hizo nchini Zimbabwe na Zambia ni sehemu mwendelezo wa jitihada za ATCL kujitanua kibiashara ndani na nje ya nchi. Agosti mwaka jana, ATCL ilianza safari za kwenda Entebbe nchini Uganda na Bujumbura nchini Burundi.Ndege zinazofanya safari hizo ni Bombardier Dash 8 Q400 zenye uwezo wa kubeba jumla ya abiria 76 kila moja. Kama ilivyo kwa Airbus A220-300, Kagirwa alisema wakati huo kuwa safari za Entebbe na Bujumbura nazo zinafanyika mara tatu kwa wiki.Amesema safari za kutoka Dar es Salaam kupitia Kilimanjaro kwenda Entebbe zinafanyika siku za Jumanne, Ijumaa na Jumapili, wakati safari za kutoka Dar es Salaam kupitia Kigoma kwenda Bujumbura ni siku za Jumatatu, Jumatano na Jumapili.Alisema ATCL imeweka bei nafuu kwa wateja wao wanaosafiri na ndge hizo kwenda Entebbe, Bujumbura, Harare na Lusaka.
1uchumi
Ma AVELINE KITOMARY MAMLAKA ya Maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali, imekuwa na nafasi kubwa katika vipimo vya utambuzi na udhibiti wa kemikali. Wakati wa kuanzishwa kwake lengo kuu lilikuwa ni kufanya utafiti wa magonjwa ya ukanda wa joto (tropical disease) mwaka 1895 na magonjwa yaliyolengwa kwa wakati huo yalikuwa ni malaria na kifua kikuu. Baada ya uhuru, maabara hiyo ilikuwa ni idara ndani ya Wizara ya Afya lakini kwa sasa ni mamlaka inayojitegemea kutokana kuundwa rasmi kisheria kupitia Sheria ya Mamlaka ya Maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali Na.8 ya mwaka 2016. Maabara hiyo ina jukumu la kufanya uchunguzi wa kitaalamu au kisayansi wa sampuli mbalimbali zinazotokana na makosa ya jinai, usalama na ubora wa bidhaa, masuala ya kijamii na usalama wa afya kazini. Licha ya majukumu hayo, inasimamia utekelezaji wa sheria za udhibiti wa kemikali viwandani na majumbani na kudhibiti matumizi ya vinasaba vya binadamu na kutoa ushahidi wa kitaalamu mahakamani kwenye mashauri yote yanayohusisha uchunguzi wa kimaabara. Majukumu mengine ni kutoa ushauri wa kitaalamu na mchango katika tiba kwa kushirikiana na hospitali mbalimbali ndani ya nchi ikiwamo huduma za upandikizaji wa figo na utambuzi wa jinsia tawala kwa watoto waliozaliwa na jinsia mbili. Uimarishaji wa sekta ya afya unaofanywa na serikali ya awamu ya tano umeweza kufanya huduma za uchunguzi wa sampuli, uchunguzi wa ubora wa bidhaa na uchunguzi wa uchafuzi wa mazingira. Mafanikio ya maabara hiyo yanaendelea kuonekana hasa katika Kanda ya Ziwa ambapo maabara sasa imekuwa na uwezo mkubwa wa kupima sampuli za aina mbalimbali ikiwamo ile ya mazingira. Kanda ya Ziwa inajumuisha mikoa Mwanza, Mara, Simiyu, Shinyanga, Geita, Kagera na Kigoma. Akizungumza wakati wa Kampeni ya ‘Tumeboresha sekta ya Afya’ inay- oendeshwa na Maofisa habari wa Wizara ya Afya na Taasisi zilizoko chini ya wizara hiyo, Meneja wa Mamlaka hiyo Kanda ya Ziwa, Boniventure Masambu, anasema maabara hiyo ilizinduliwa Januari mwaka 2005 ili kusogeza huduma karibu na wananchi pamoja na kuongeza ufanisi katika utoaji huduma. “Huduma tunazotoa ni uchunguzi wa sampuli za makosa ya jinai kama ubakaji, sumu, mauaji na dawa za kulevya. Nyingine ni uchunguzi wa ubora wa bidhaa, uchunguzi wa uchafuzi wa mazingira unaolenga kulinda afya na mazingira na kutoa ushahidi wa kitaalamu mahakamani. “Huduma zingine ni usimamizi na udhibiti wa kemikali, hapa tunafanya uk- aguzi wa maeneo yenye kemikali, usajili wa maeneo yenye kemikali, usimamizi na udhibiti wa kemikali katika mipaka iliyoko kanda ya ziwa, kutoa vibali vya kusafirisha, kuingiza na kuuza nje ya nchi kemikali,” anaeleza. Mamlaka upande wa Kanda ya Ziwa pia inafanya tafiti mbalimbali ili kuweza kuendana na teknolojia ya sasa. Uwekezaji wa miundombinu wezeshi ya uchunguzi wa sampuli umefanya uchunguzi wa maabara kuongezeka kutoka sampuli 1,085 mwaka 2015 hadi kufikia sampuli 7,193 mwaka 2019. Masambu anasema ununuzi wa miambo umechangia kuboreshwa kwa huduma zinazotolewa hivyo kupunguza muda wa kuchungaza sampuli kwa kusaidia sampuli nyingi kuchunguzwa hapo badala ya kupelekwa makao makuu. “Muda wa kufanya uchunguzi wa sampuli zinazoletwa maabara umepungua kutoka siku 30 mwaka 2015 hadi siku 10 mwaka 2019 kwa sampuli ambazo hazihitaji kupelekwa kwenye maabara zingine kwa uchunguzi. “Katika kipindi cha kuanzia mwaka 2017 hadi sasa sampuli zote huchunguzwa sumu katika maabara hii. Vifaa vya kisasa vya GC vimewezesha sampuli hii kufanyika hapa na kupunguza muda wa kuchunguza na kutoa majibu,” anabainisha. Anasema uchunguzi wa dawa za aina zote za kulevya unafanyika katika kanda hiyo hatua ambayo imerahisisha kuharakisha kesi mahakamani. “Ofisi ya kanda imekuwa ikishiriki katika vikao vya kusukuma mashauri mahakamani na maabara ya kanda imesaidia kuharakisha mashauri yalioyopo mahakamani, vikao hivi vimekuwa vikifanyika kila baada ya miezi mitatu. “Kanda imeshiriki katika vikao vyote vya mahakama kuu, Mahakama ya Mkoa wa Mwanza na wilaya zake, pamoja na kushiriki vikao vya kuharakisha kesi huku wataalamu wa kanda wakiwa wamehudhuria jumla ya mashauri 436 kwaajili ya kutoa ushahidi ambao ni wasatani wa mashauri 188 kwa mwaka,” anafafanua Masambu. SAMPULI ZA UCHAFUZI MAZINGIRA Masambu anasema katika kipindi cha miaka minne serikali ilinunua mitambo ya AAS na DR 5000 iliyowezesha uchunguzi wa sampuli za uchafuzi wa mazingira. Kwa mujibu wa Masambu, matokeo ya tafiti za mazingira zinazofanywa yanatumiwa na serikali katika kuchukua hutua za kisheria. “Jumla ya plant nane, elusion plant nne za uchenjuaji wa dhahabu na maeneo ya kilimo ya Serengeti yaliyosababisha uchafuzi wa mazingra katika Kanda ya Ziwa, sampuli zake zilifanyiwa uchunguzi na maabara hii. “Sampuli za uchafuzi wa mazingira za migodi midogo na mikubwa iliyoko Kanda ya Ziwa zilifanyika katika maabara hii, itakumbukwa katika kipindi hicho kulikuwa na mgogoro mkubwa wa uchafuzi wa mazingira wa Kampuni ya Mgodi ya Acacia North Mara. “Maabara hii ilihusika katika hatua zote za uchunguzi wa jumla ya sampuli 210 ambazo zilichukuliwa katika vipindi tofauti na majibu yake ndio yalitumiaka katika uamuzi wa serikali,” anasema. SAMPULI ZA KEMIKALI Sheria ya udhibiti na usimamizi wa kemikali za viwanda na majumbani namba 3 ya mwaka 2003 inaitaka mamlaka kusimamia uzalishaji, utunzaji, usafirishaji, utumiaji na utupaji wa kemikali ili kulinda afya ya wananchi na mazingira. Kutokana na matakwa ya kisheria, kanda hiyo imekuwa ikifanya ukaguzi, uelimishaji na utoaji vibali ikiwa ni njia ya kudhibiti na kusimamia matumizi ya kemikali nchini. Masambu anasema kanda hiyo ina wakaguzi katika mipaka mitano ya Kanda ya Ziwa ili kuhakikisha ukaguzi wakati wa uingizwaji wa kemikali. “Ukaguzi wa ndani wa maeneo yenye kemikali umeongezeka kutoka maeneo 151 mwaka 2015 hadi kufikia 213 mwaka 2019. “Kanda imeendelea kutoa vibali vya kuingiza na kutoa kemikali nchini kupitia mipaka ya Kanda ya Ziwa, vibali vilivyotolewa vimeongezeka kutoka 1,350 hadi 2,246; kutokana na ongezeko hilo, wadau wengi waliokuwa wanapitisha kemikali bila vibali sasa wanafuata sheria na kuzuia kemikali hatarishi. Anasema usajili wa maeneo yenye kemikali umesaidia kutambua maeneo yanayotunza kemikali na kujua matumizi yake katika maeneo hayo. “Hii husaidia kuzuia matumizi yasiyofaa ya kemikali hasa yanayoendana na uharibifu, katika zoezi hilo maeneo yaliyosajiliwa yameongezeka kutoka 72 mwaka 2015 hadi maeneo 213 mwaka 2019,” anaeleza Masambu. Anasema mafanikio mengine yaliyopatikana ni utoaji elimu juu ya faida ya matumizi salama ya kemikali na kusababisha ongezeko la wachenjuaji na wauzaji. “Watumiaji wa kemikali katika uchenjuaji wameongezeka kutoka 183 mwaka 2015 hadi 592 mwaka 2019 ongezeko hilo limeongeza wauzaji wa kemikali kutoka 15 mwaka 2015 hadi kufikia 92 mwaka 2019. “Kuongezeka kwa wauzaji kumeongeza wasafirishaji kutoka 0 hadi 14 mwaka 2019,” anabainisha. Anasema hatua zote zimekuwa na mafanikio makubwa katika kanda kutokana na kazi iliyofanywa na serikali.
4afya
NAHODHA wa timu ya soka ya taifa, Taifa Stars, Mbwana Samata amesema watapambana na Algeria na Senegal kwa lengo la kujiinua kisoka.Samata ameyasema hayo siku chache baada ya droo ya fainali za michuano ya Kombe la Mataifa Afrika ‘Afcon’ kupangwa na Tanzania kuwekwa kundi C pamoja na Algeria, Senegal na Kenya. Fainali hizo zitafanyika Misri kuanzia Juni 21 mpaka Julai 19 mwaka huu.Akizungumzia droo hiyo, Samata alisema Senegal na Algeria ni timu ngumu katika kundi lao lakini watapambana ili washinde waweze kuinua soka la nchi.“Algeria na Senegal wamepiga hatua katika soka miaka mingi, hivyo ni lazima tuwaheshimu lakini ni lazima tupambane kuonesha tunakwenda walipo na tuna uchu wa kufika huko,” alisema Samata.Pia Samata amesema wanaiheshimu Kenya kwa sababu ni majirani ila hawajaipita Tanzania.“Tunawaheshimu Kenya ni majirani zetu wako vizuri katika maendeleo ya soka, lakini hawajafika mbali sana kuipita Tanzania,” amesema.Aidha amesema Kundi C ni gumu, kwani linawakutanisha na timu kubwa za Afrika zilizowapita katika viwango kwa kiasi kikubwa, hivyo ni vyema kukawa na maandalizi madhubuti ili kushindana na kujaribu kupenya katika hatua ya mtoano na Tanzania inatakiwa kujiwekea malengo ya kushiriki kila fainali za AFCON kuanzia sasa.Taifa Stars ilifuzu baada ya kumaliza nafasi ya pili kwenye Kundi L kwa pointi nane, nyuma ya Uganda walioongoza kwa pointi 13 na kuiacha Lesotho iliyomaliza na pointi sita na Cape Verde pointi tano.
5michezo
Airtel imejishindia tuzo hizo katika kipengele cha matumizi bora ya huduma za kimtandao kufikia wateja wake pamoja na kutoa huduma bora zinazokidhi mahitaji ya wateja katika sekta ya mawasiliano na kushinda kampuni nyingine zilizokuwa zikichuana nazo katika kinyang’anyiro cha tuzo hizo.Wakizungumza wakati wa kukabidhi tuzo hizo , mwandaaji wake, Kishore Bollakpalli alisema: “Airtel imepata tuzo hizi kutokana na kufanya vizuri zaidi katika kuwasiliana na wateja wake, kupitia mitandao mbalimbali ya kijamii na hivyo kuwafikia wateja wake nchini nzima kwa urahisi zaidi.Lakini kwa upande wa tuzo ya Brand excellence, Airtel imeonesha kwa vitendo dhamira yao ya kutoa huduma bora kwa wateja wake huku ikitoa bidhaa na huduma za kibunifu ili kukidhi mahitaji ya wateja wake na kuboresha maisha yao.”Akipokea tuzo hizo Mkurugenzi Mkuu wa Airtel, Sunil Colaso alisema:” Tunayofuraha kupokea tuzo hizi za Tanzania Leadership Award na tunaamini huu ni ushuhuda kamili unaoonesha kwa vitendo dhamira yetu ya kutoa huduma zinazokidhi mahitaji ya wateja wetu zikiwemo huduma za intaneti, huduma za kifedha kupitia simu za mkononi na kuchochea kukua na upatikanaji wa huduma za kifedha nchini”.
1uchumi
KAMA ndio mara yako ya kwanza kusoma makala hii, huu ni muendelezo wa makala ya Ufukwe wa Matema, ambapo mwandishi aliutembelea na kujionea mambo mbalimbali ya kuvutia na kustaajabisha. Ufukwe huu umezungukwa na miamba, lakini pia watu waishio maeneo jirani hufanya shughuli zao za hapa na pale ikiwamo kufua na kuanika mazao ya nafaka. Kujua zaidi yaliyopo na yanayojili katika Ufukwe wa Matema endelea kusoma makala hii kila alhamisi na Ijumaa. Miamba ya Mto Mwalalo Mwanamazingira yeyote au mtu mwenye udadisi anayetembelea bonde la Mto Mwalalo kutoka mwanzo hadi kwenye maporomoko ya Mwalalo hatakosa kuvutiwa na aina mbalimbali za miamba na mawe yaliyo katika bonde hilo. Picha nilizochukua za mawe na miamba hiyo zilipelekwa kwa majiolojia waandamizi, waliobobea katika fani hii muhimu, na wenye uzoefu wa miaka mingi katika kazi, na kuwaomba maelezo kuhusu miamba ya Mto Mwalalo. Maelezo yafuatayo yametolewa na Ndugu Asa Mwaipopo na Dr. Dalaly Kafumu: “Bonde la Mto Mwalalo, Matema lina mpangilio wa mawe wa upekee fulani na unavutia. Kijiolojia, miamba hii inaonesha kuwa na sura (lithology) kubwa mbili, lakini zote zikiwa na chembechembe ndogo ndogo. Moja ni aina ya “granite” ambayo ni aina maarufu ya mawe yanayopatikana upande wa Ziwa Victoria, hasa Mwanza na ya pili ni “delorite’’ mawe ambayo ni matokeo ya volkano iliyotokea baadaye na ambayo majivu yake yenye joto kali (lava) yalijipenyeza (cross cutting veins) kwenye miamba iliyotangulia. Miamba ya Mto Mwalalo inaonesha matukio ya kijiolojia; kuanzia mwagiko la kivolkano la awali na baadaye tetemeko au mmeguko wa ardhi uliochangia kuwapo kwa nyufa ambazo zilijazwa na lava ya volkano iliyotokea miaka mingi baadaye, na lava ilipopoa ikatengeneza mkondo mithili ya mishipa (veins) katika miamba ya awali. Miamba inayopatikana Mto Mwalalo (granite na dolerite) huwa haina vyanzo vya madini yenye thamani (precious metals) au madini mengine ambayo kiasili hupatikana kwa wingi na kirahisi ardhini. Hata hivyo, kama mwamba una chembechembe ndogo ndogo na ni mkubwa na hauna nyufa nyingi, unaweza kutumika katika uchimbaji wa mawe ya kuchonga (dimensional stones). Mawe hayo (cut and polished stones, slabs) hutumika katika ujenzi. Miamba ya Mto Mwalalo inaweza kuwa na sifa za kuwa mgodi wa mawe ya kuchonga (dimensional stone) kama ni miamba mikubwa, endelevu na isiyokuwa na nyufa nyingi. Ili mgodi uwezekane, unahitajika utafiti wa kjiolojia na uchorongaji ili kujiridhisha na uwezekano huo. Aidha, kwa kuwa miamba hii ipo katika bonde la mto, tathmini ya athari kwa mazingira itahitajika. Pamoja na yaliyotangulia, eneo hili inabidi lifanyiwe uchunguzi wa kijiolojia, wanafunzi wa jiolojia, jiografia, mazingira na wengine wahamasishwe kutembelea eneo hilo na litangazwe kuvutia watalii.   Lyulilo Lyulilo ni kitongoji cha Kijiji cha Ikombe, kilichopo ghuba ndogo inayoashiria mwisho wa Ziwa Nyasa unapoambaa mashariki kutoka kusini kwenda kaskazini. Ghuba hiyo imekaa kimkakati. Ufukwe wake ni mchanganyiko wa mchanga na mawe madogo. Ufukwe uko kwenye kina kirefu kiasi kwamba meli kubwa kama vile MV Songea inayosafirisha abiria na mizigo hutia nanga mita 200 hivi kutoka sokoni Lyulilo.   Lyulilo ni soko maarufu kwa samaki wa Ziwa Nyasa na kwa vyungu na bidhaa mbalimbali zinazotengenezwa kwa udongo wa mfinyanzi. Mitumbwi na boti hutia nanga Lyulilo zikisafirisha vyungu kutoka Ikombe na bidhaa kwenda Ikombe. Umaarufu wa Lyulilo unatokana na kuwa soko la vyungu vya asili vinavyotokana na udongo wa mfinyanzi. Si rahisi hasa kwa vijana wetu waliokulia mjini kufahamu umuhimu wa vyungu hivi. Kwani vijana wa zamani tunakumbuka jinsi mama zetu, shaangazi zetu na bibi wazaa mama au baba jinsi walivyotumia vyungu hivi kupikia na jinsi chakula kilichotoka humo kilivyokuwa na ladha na utamu wa aina yake. Lakini pi tunakumbuka jinsi ambavyo vyungu hivi vilitumika kama jokovu. Kwa kuweka chungu kilichojaa maji juu ya mafiga matatu na kuweka mchanga chini ya chungu na kunyunyizia maji mchanga huo, maji yaliwea kupoa na kuwa ya baridi kana kwamba yametoka kwenye jokofu. Mnada wa vyungu hufanyika jumamosi. Hata hivyo, mauzo ya samaki, vyungu, mchele, ndizi na bidhaa nyingine hufanyika kila siku. Halmashauri ya Wilaya ya Kyela imejenga soko la samaki kwa matarajio ya ongezeko la biashara. Soko hilo lenye majokofu ya kutunzia samaki halitumiki. Kwani umeme haujafika Lyulilo.   Ikombe Moja ya vivutio vikubwa kwa wageni na watalii wanaofika Matema ni kitongoji cha Ikombe kilicho katika Kijiji cha Ikombe katika kata ya Matema. Kitongoji cha Ikombe kiko kando kando ya Ziwa Nyasa kwenye mitelemko ya Milima ya Livingstone. Ni kitongoji cha mwisho kusini mwa Matema kinachopakana na Wilaya ya Ludewa, Mkoa wa Njombe. Ikombe ni peninsula au rasi ndogo inayoingia Ziwa Nyasa. Haifikiki kwa urahisi kwa nchi kavu. Kwani miteremko ya milima Livingstone ni mikali. Barabara inajengwa, yanahitajika madaraja kukamilisha ujenzi huo. Baadhi ya watalii hupenda kutembea kwenda Ikombe. Njia rahisi kwa sasa kufika Ikombe ni kutumia boti, safari inayochukua dakika 20. Wenyeji hutumia ngalawa kwa usafiri na kupeleka bidhaa mbalimbali Ikombe. Ras ya Ikombe ina mvuto wa kipekee. Ufukwe wake ni wa mawe madogo na kawaida. Ufukwe umejaa ngalawa. Ikombe ni kijiji cha wavuvi, usafiri wa kwenda sehemu nyingne za Kata ni wa kutumia ngalawa. Madhari ya kitongoji inapendeza kutokana na miti mingi ya asili na iliyopandwa inayoipa Ikombe tabianchi ya kipekee. Hapa ndipo vyungu vya asili hutengenezwa na huvushwa kwa mitumbwi kupelekwa Lyulilo kuuzwa. Udongo mfinyanzi unaopatikana Ikombe ndio unaofaa kutengeneza vyungu. Ikombe pana zahanati na shule ya msingi.   Huduma za kijamii Baada ya kuugua kwa muda mrefu na kutibiwa India na hapa nchini kati ya mwaka 2011 na 2013 kila ninapoulizwa kipaumbele cha maendeleo kiwe nini, hasa pale ambapo rasilimali ni kidogo, huwa najibu afya na elimu. Kabla ya hapo jibu langu lilikuwa elimu na elimu tu. Kwa upande wa Matema, suala la afya linaweza kugawanywa katika sehemu mbili; elimu ya usafi wa mazingira na tiba. Maeneo ya mwambao wa maziwa na bahari barani Afrika bado yana changamoto kubwa inayohusu usafi wa mazingira, maneno ya kistaarabu yanayomaanisha uwepo au la wa vyoo. Jamii nyingi, vijijini na mijini katika mwambao wa maziwa na bahari hutumia bahari na maziwa kama vyoo vya kudumu. Nilipotembelea Pangani nikiwa Waziri wa Nchi mwenye dhamana ya Mazingira, nilikumbana na changamoto mbili. Kwanza, mji huo wa kihistoria ulikuwa unaharibiwa na mawimbi ya bahari yaliyokuwa yakimeza ufukwe pole pole na kuharibu nyumba na miundombinu kwa sababu ya kiwango kikubwa cha mabadiliko ya tabianchi. Changamoto ya pili ilikuwa ni uhaba wa vyoo. Jamii ilikuwa ikienda ufukweni mwa bahari ili kujisaidia, ilitupa taabu ya kukagua uharibifu wa pwani ya Pangani, ilitubidi kukagua eneo lote kwa kutembea ufukweni na kila mara kuruka kinyesi. Nilipata changamoto ya aina hiyo Mikindani, Lindi. Ukikaa katika hoteli nzuri ya kitalii na ukiwa makini unaweza kugundua kuwa makazi mengi ya Mikindani hayana vyoo, wakazi wa eneo hilo hutumia Bahari ya Hindi kama eneo la kutimiza wito asilia. Pangani na Mikindani ni miji midogo. Kuna wakati nilienda Accra, Ghana kuhudhuria mkutano wa kimataifa kuhusu madhara ya mabadiliko ya tabianchi. Kama ilivyo kawaida yangu, alfajiri huwa natoka hotelini ili kufanya mazoezi ya matembezi. Umbali kidogo kutoka hoteli ya kitalii niliyokaa kuna ufukwe wenye mchanga na mawe. Nililoliona na lililonishangaza ni kwamba jamii kutoka kitongoji cha jirani walishuka ufukweni kila asubuhi kwa kile nilichodhani wanaenda kuoga au kuogelea. Haikuwa hivyo, walikuwa wamekaa tu. Nilipouliza nini kilikuwa kinaendelea, wahudumu pale hotelini wakaniambia kuwa wale wote niliowaona walikuwa wameenda baharini kujisaidia. Itaendelea kesho…
4afya
Wadau wa soka wametoa maoni yao baada ya Yanga kupoteza mchezo wao dhidi ya Ruvu Shooting kwa bao 1-0 katika Uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam. Akizungumza baada ya mchezo huo, mtangazaji wa Clouds FM na mshabiki mkubwa wa Yanga, Antonio Nugaz ambaye alikuwa muhamasishaji katika tukio la kilele cha Wiki ya Mwananchi amesema hajashtushwa na kipigo hicho na kuongeza kuwa Yanga ilikuwa lazima afungwe katika mchezo huo ili wajiweke katika nafasi nuri ya kutwaa ubingwa. Yanga ili awe bingwa ilikuwa lazima mechi ya leo (jana) afungwe. Unadhani Yanga ataufungwa mechi tano mfululizo kama ule muunganiko umekuwa tayari? Yanga amefungwa kwa sababu ya distance (umbali). Amesema wachezaji walitumia nguvu nyingi kwenye mchezo wa Ligi ya Mabingwa dhidi ya Towship Rollers na kufanikiwa kuibuka na ushindi wa bao 1-0, hivyo mchezo wa leo ilikuwa lazima wafungwe kutokana na uchovu. "Ili ya iwe bingwa, ilibidi ipoteze mchezo wa leo". A post shared by SHAFFIH KAJUNA DAUDA (@shaffihdauda_) on Aug 28, 2019 at 11:22am PDT Amesema kwa sababu nafasi ya kimataifa huja mara moja kwa msimu ilikuwa lazima watumie nguvu, laki mchezo wa ligi inawezekana kupoteza mchezo mmoja na kufanya vizuri nyingine. Kwa upande wake, Abbas Tarimba ambaye ni Mkurugenzi wa Utawala na Utekelezaji wa SportPesa Tanzania, ambaye pia ni Mwanachama hai wa Yanga amesema ilikuwa siku yao Ruvu Shooting na walistahili kushinda na kudai kuwa kulikua na mapungufu machache kwa upande wa Yanga ila anaamini kocha atafanyia kazi. Mdau wa Yanga Abas Tarimba amekiri kwamba, kikosi cha Ruvu Shooting kilistahili kupata matokeo ya ushindi kutokana na kilivyocheza dhidi ya Yanga. Tarimba anaamini kuwa, Yanga ikikutana na Zesco United kwenye mechi ya CAF Champions League haitacheza kama ilivyocheza mechi ya ligi dhidi ya Ruvu Shooting. A post shared by SHAFFIH KAJUNA DAUDA (@shaffihdauda_) on Aug 28, 2019 at 2:08pm PDT “Yanga ni wazuri, si wabaya hata kidogo, walikuwa na matatizo kidogo katika mchezo huu. Na katika mchezo dhidi ya Zesco watakuwa ni timu nyingine kabisa,” amesema Tarimba. Ally Mayay, ambaye ni mchezaji na nahodha wa zamani wa Yanga amemlenga moja kwa moja mshambulizi mpya wa timu hiyo David Molinga na kusema kuwa, ana sifa za kuwa mshambuliaji huku akibainisha baadhi ya mapungufu aliyoyaona kwa mchezaji huyo. “Molinga ana vigezo vya kuwa mshambuliaji lakini bado ukiangalia mikimbio yake, kuna vitu nafikiri mwalimu anatakiwa avifanyie kazi kwe yeye na viungo ambao wanatarajia kumpa pasi,” Mayay amesema. Mashabiki wa soka wa Bongo ni kama hawana imani na mshambuliaji mpya wa Yanga David Molinga, katika mechi chache alizocheza amekuwa akikosolewa sana na mashabiki. Mchezaji wa zamani wa Yanga Ally Mayay Tembele anasema, Molinga ana sifa za kuwa mshambuliaji huku akibainisha baadhi ya mapungufu aliyoyaona kwa mchezaji huyo. A post shared by SHAFFIH KAJUNA DAUDA (@shaffihdauda_) on Aug 28, 2019 at 2:37pm PDT  
5michezo
SERIKALI kisiwa cha Songosongo imetakiwa kushirikisha wananchi katika kuibua na kubuni miradi ya kimkakati ambayo itakujwa endelevu katika kusaidia, kuanzisha na kupanua wigo wa vyanzo vipya vya mapato katika kisiwa hicho. Kisiwa hicho kipo katika wilaya ya Kilwa na maarufu sana kwa uchimbaji wa gesi na uvuvi wa samaki wakiwemo pweza.Akizungumza katika ufunguzi wa jukwaa la pili kla wadau wa sekta ya uzinduaji wa gesi asilia na mafuta kata ya Songosongo, Diwani wa kata hiyo Said Mwinyi alisema kitendo cha kisiwa hicho kuendelea kutegemea mrabaha wa asilimia 20 kutoka wilaya hautoi sura ya mbele ya kisiwa hicho wakati gesi itakapokuwa imekoma.Alisema pamoja na Mtandao wa Mashirika yasiyo ya kiserikali mkoa wa Lindi (LANGO) kuwezesha uwapo wa majukwaa hayo ambayo yamesaidia kutoa elimu wakati umefika kwa wananchi na serikali kuibua miradi mipya ili kisiwa kuwa na uhakika wa kipato cha mtu mmoja na jamii.Lango limeendesha majukwaa hayo kwa ufadhili wa Shirika la Open Society Initiatives For Eastern Africa (OSIEA) na moja ya mafanikio ni kuwezesha wananchi wa Songosongo kupata haki yao ya mrabaha kutoka halmashauri ya wilaya ya Kilwa, mrabaha ambao wamesema unawasaidia kurekebisha hali ya mapato na matumizi ya serikali kisiwani hapo.Majukwaa hayo ambayo yanakuwa eneo huru la kuulizana maswali kati ya wananchi na taasisi zinaozohusika na sekta ya uziduaji kisiwani Songosongo,yamelenga kuimarisha ushiriki wa wananchi, uwazi na uwajibikaji katika usimamizi wa mapato ya tozo ya huduma katika sekta ya uziduaji wa gesi asilia na mafuta.Diwani Mwinyi alisema mradi huo wa mwaka mmoja sasa umewezesha wananchi kuelewa masuala mbalimbali kuhusu sekta ya uziduaji na namna ambavyo sekta hiyo inachangia maendeleo na kuona tozo ya huduma ya kutoka halmashauri ya Kilwa inayosababishwa na gawio la asilimia 20 linavyofanyakazi katika kisiwa hicho.Alisema mafunzo yaliyotolewa na LANGO na kuwezeshwa kuundwa kwa majukwaa yamewezesha wananchi kuona na kuibua fursa mbalimbali zinazoambatana na sekta ya uziduaji gesi asilia na mafuta .Aidha kwa sasa wananchi wanaweza kuhoji fedha zao na kuona namna bora ya kuweza kuwekeza kwa manufaa ya vizazi vijavyo. Katika jukwaa hilo Ofisa Mtendaji wa kijiji cha Songosongo Hamza Hamza alisema kutokana na mafundisho na msaada wa LANGO, wameweza kubaini na kufuatilia halmashauri ya Kilwa ya tozo ya huduma kwa kijiji hicho yenye thamani ya sh milioni 254.Alisema halmashauri ya wilaya ya Kilwa ambayo ‘ilijikopesha’ fedha hizo za kuanzia mwaka 2014 hadi 2018 kwa sasa imelipa kwa mikupuo miwili jumla ya Sh milioni 116 na kubakiza Sh milioni 138. Aidha Ofisa mtendaji huyo alisema kwamba Sh 29,800,000 kati ya fedha hizo, zimetumika kulipa posho ya walimu wanne wa kujitolea, posho kwa walinzi na kuchangia fedha za kambi ya darasa la saba na kidato cha nne mwaka huu.
3kitaifa
Na JOSEPH SHALUWA HIVI karibuni mwanamuziki mahiri Bongo ambaye alikuwa akiimba muziki wa Taarab akiwa na Bendi ya Jahazi Modern Taarab, Mzee Yusuf aliachana na muziki huo na kutangaza kumgeukia Muumba. Kwa uamuzi huo, alisema hataimba kabisa muziki wa Taarab na akawataka mashabiki wake kuacha kumwita kwa jina lake maarufu la Mfalme, akisema Mfalme ni mmoja tu na siyo yeye. Msanii huyo aliyekuwa tishio kwenye muziki huo kwa sasa ameanza kuimba Kaswida na hivyo kufuta kabisa ndoto za waliokuwa wakifikiri huenda angerejea jahazini. Tukio la Mzee Yusuf likiwa halijapoa, msanii mwingine aliyeanza kuja juu hivi karibuni kwenye muziki wa Bongo Fleva, Khadija Maige ‘Khadija Nito’ akitokea Jumba la Vipaji Tanzania (THT) ametangaza kuokoka na kuachana na Bongo Fleva. Pamoja na kuokoka pia amebadili jina lake ambapo kwa sasa anajulikana kama Natasha Maige Lisimo na tayari ameachia kibao chake cha kwanza kiitwacho Ufunguo akimshirikisha Bahati Bukuku. Natasha (Khadija) amebadilika kila kitu, kuanzia mavazi na hata namna anavyoimba. Kabla ya kuokoka nyimbo zilizoanza kumpa umaarufu ni pamoja na Si Ulisema, Sina Maringo na Nifanye Nini. Sasa cheki listi ya waliotangulia kuachana na muziki wa kidunia na kugeukia dini.     CHIDUMULE Mwanamuziki wa muda mrefu Cosmas Chidumule kwa muda mrefu sasa ameokoka. Baada ya kuokoka tu aliachia wimbo wa Yesu ni Bwana ambao mpaka sasa bado unatamba. Mbali na wimbo huo wa Injili, anao mwingine uitwao Hosiana ambao ameshirikiana na mwimbaji mwingine aitwaye Mwansasu – nao unafanya vizuri kama ilivyo Yesu ni Bwana. Amepitia bendi nyingi na ameimba vibao mbalimbali maarufu kikiwemo kile cha Neema kilichovuma miaka ya nyuma huku kikiendelea kukubalika mpaka sasa.   K BASIL Anaitwa Basil Kashumba ‘K Basil’ ambaye ni msanii mkongwe kwenye muziki wa kizazi kipya. Alikuwepo enzi akina Bob Rudala, Bizman, Mr. Paul, Stara Thomas na wengineo wakitamba kwenye Bongo Fleva. Kibao chake maarufu hadi anaacha muziki miaka kadhaa iliyopita kilikuwa ni Riziki. Basil ni msomi wa Chuo Kikuu akiwa na Shahada ya Kwanza ya Jiografia na Mazingira. K Bazil ameokoka muda mrefu na ameshatoa albamu moja ya Injili iitwayo Yesu Ananipenda ikiwa na nyimbo kama Namjua, Wakati na Bahati, Wewe ni Baba, Rudisha, Utukuzwe, Moyo, Tunasonga Mbele, Mama na Asante Yesu. Mpaka sasa ni miongoni wa watumishi wa Kanisa la Ufufuo na Uzima lililopo Ubungo jijini Dar es Salaam, chini ya Askofu Josephat Gwajima.   RENEE LAMIRA Juhudi zake kwenye muziki ni kubwa kwani kupitia muziki wake alishawahi kutia maguu mpaka kwenye Tuzo za Kora. Wimbo wake maarufu uliompa mafanikio hayo ni Ngoma ya Kwetu wenye mahadhi ya asili na kitamaduni. Mbali na Ngoma ya Kwetu ambayo ndiyo jina la albamu pekee aliyopata kutoa, Lamira alitamba pia na nyimbo kama Fitina na Ondoka. Msanii huyu kwa miaka mingi sasa ameamua kuachana na muziki na kumrudia Mungu. Hadi anaamua kuokoka wakati huo alikuwa akisali katika Kanisa la Living Water chini ya Mtume Onesmo Ndegi.   STARA THOMAS Mwanadada mwenye sauti tamu, Stara Thomas naye alitangaza kuokoka zaidi ya miaka mitano iliyopita na kugeukia muziki wa Injili. Ana nyimbo nyingi nzuri alizopata kuimba zikiwemo Mimi na Wewe, Sogea Karibu na Nipigie alioshirikishwa na msanii AT. Akiwa ameokoka ametoa nyimbo kadhaa ukiwemo Nani Mshamba na Uwezeshwaji Mwanamke ambao aliutoa maalumu kwa siku ya mama.   Q JAY Kijana huyu mwenye sauti tamu alikuwa ndani ya Kundi la Wakali Kwanza akiwa na wasanii wenzake, Makamua na Joseline. Q Jay yeye aliamua kujitenga na wenzake na kuokoka kisha kuanza kuimba muziki wa Injili ingawa hatambi kwenye muziki huo. Akiwa na Wakali Kwanza alipata kutamba na Sifai, Nimebaki Lonely, Natamani na Kitu Gani.   DOKII Dokii ambaye jina lake halisi ni Ummy Wenceslaus naye alipata kutangaza kuokoka na kuimba muziki wa Injili. Awali Dokii alikuwa msanii wa filamu lakini baadaye akaingia kwenye muziki wa Bongo Fleva. Kati ya nyimbo zake za Gospo ambazo hata hivyo hazijapata umaarufu mkubwa ni Nani wa Kumwabudu. Mbali na Gospo, Dokii anaimba nyimbo za kawaida (lakini siyo za kidunia) ambapo alipata kuimba wimbo maalum wa kumkaribisha aliyekuwa Rais wa Marekani Barack Obama ‘Obama Welcome Tanzania’ wakati wa ujio wake nchini Julai, 2013 chini ya utawala wa Rais Jakaya Kikwete. Hivi karibuni aliimba wimbo wa Uhuru Kenyatta ambao ulikuwa ukisifia utendaji kazi wa Rais huyo wa Kenya ambaye ameshinda kuongoza mhula mwingine katika Uchaguzi Mkuu uliofanyika Agosti 8, mwaka huu. Kwa sasa pamoja na mambo mengine, anatangaza kwenye kituo cha Redio E FM cha jijini Dar es Salaam.
0burudani
Hayo yalisemwa na Ofisa Mtendaji wa Programu ya UNCDF ya LFI, mwenye makazi yake Dar es Salaam Peter Malika na Ofisa Mtendaji wa Taasisi ya sekta Binafsi (TPSF), Godfrey Simbeye wakati wakifungua warsha ya siku 1 ya wajasiriamali kuhusu mitaji ya ndani kwa maendeleo.Simbeye alisema kwa kushirikiana na taasisi hiyo ya Umoja wa Mataifa wamelenga kuondoa dhana ya kukosekana kwa mitaji kwa ajili ya uanzishaji wa ujasiriamali mdogo na wa kati.Alisema katika tafiti zao nyingi wafanyabiashara wadogo na wa kati wamekuwa wakilalamikia mitaji na wengine mitaji yao ikianguka katika kipindi kifupi na hivyo wakaona vyema kuendesha warsha hiyo.Simbeye alisema katika warsha hiyo watapata uzoefu na namna ya kupata mitaji ya kuanzishia biashara na pia namna ya kuimarisha biashara zao. Alisema kazi kubwa inayofanywa na TPSF ni kuhakikisha kwamba wadau na wanachama wanatambua fursa zilizopo za mitaji ili kusaidia kuendeleza nchi, kwa kuwa hakuna taifa linaloweza kusonga mbele kiuchumi kwa kujivuna bila kuwa na wajasiriamali wadogo na wa kati wenye mafanikio.Naye Peter Malika katika ufunguzi wa warsha hiyo alisema kwamba kimsingi tatizo la mitaji halipo kama wajasiriamali hao watatumia ushauri wao wa kiufundi katika kuandika miradi na utafutaji wa mitaji.Alisema taasisi hiyo ya Umoja wa Mataifa ina uwezo wa kusaidia wajasiriamali wadogo na wa kati kuanzisha na kusimamia biashara zao kutokana na uzoefu ilionao ya namna ya kukusanya mitaji na pia wao wenyewe kupitia mfuko unaochangiwa na taasisi mbalimbali.Malika alisema UNCDF imewalenga wajasiriamali kwa kuangalia fursa zilizopo na namna ya kupata mitaji huku ikitoa ushauri wa kiufundi katika miradi hiyo kuanzia mwanzo hadi utekelezaji wake.Alisema kupitia LFI anaamini kwamba wajasiriamali wa Tanzania watakuwa na nafasi ya kutumia mitaji ya ndani kutoka katika mabenki na taasisi nyingine za kifedha, kama Hifadhi ili kujenga miradi ya maendeleo na ustawi wa jamii.Malika alisema UNCDF inaamini kwamba kwa kutumia vyanzo vya ndani kutafanya taasisi za kifedha kuacha kununua hati fungani za Hazina na kuwekeza katika maendeleo ya miradi mbalimbali yenye lengo la kuhudumia wananchi au kuthamanisha bidhaa.Alisema UNCDF inaendesha programu zenye lengo la kuleta mabadiliko chanya kwa jamii, usalama wa chakula na ajira. Aidha katika warsha hiyo washiriki wake ambao ni kutoka maeneo mbalimbali ya Tanzania wanaojishughulisha na biashara na ujasirimali wadogo na wa kati, walielezwa shughuli mbalimbali zilizodhaminiwa na taasisi hiyo.Tangu mpango wa LFI ulipoanza nchini Tanzania mwaka 2012 imesaidia miradi 30 ya kiuchumi kuanzia mwanzo wake hadi kusimama kwake.
1uchumi
CHRISTIAN BWAYA TULISHAWAHI kujadali nafasi ya dada wa kazi katika malezi. Tuliona kuwa pamoja na unafuu wa huduma zao, wamekuwa wakikabiliana na uhusiano hafifu na waajiri wao.  Kwa kuwa huduma za malezi kupitia wadada hawa zinaweza zisikwepeke, ni muhimu kujadili namna gani tunaweza kupunguza uwezekano wa kumfanya msichana wa kazi akose ari na hamasa ya kufanya kazi yake kwa bidii. Makala haya yanajadili mapendekezo ya namna ya kuboresha uhusiano na wadada wanaosaidia kazi na kulea watoto majumbani. Fahamu historia yake Ipo haja ya kujitahidi kufahamu msichana ametoka familia gani, aliishi vipi na familia yake, misimamo yake, imani, angalau mambo ya msingi. Ili hayo yawezekane, ni vizuri kumpata kupitia watu wanaomfahamu vizuri. Unapokuwa na fursa ya kumfahamu binti unayeishi naye vizuri, unaweza kufanya uamuzi sahihi mapema ikiwa unaweza kukaa naye ama la. Mwelimishe majukumu Mitafuruku mingi kati ya waajiri na hawa mabinti wakati mwingine inachangiwa na kutokufahamika kwa majukumu yake ipasavyo. Waajiri wengi huwa na matarajio makubwa kwa akina dada na hivyo hawawasaidii kujua wanachopaswa kukifanya. Ni vyema mara baada ya kukubaliana naye kuwa anaishi na familia yako kwa lengo la kumwangalia mtoto, uhakikishe anajua utaratibu kamili wa kazi. Ukifanya hivyo unapunguza uwezekano wa makosa yanayotokana na kutokujua jambo sahihi la kufanya. Kujenga uhusiano mzuri Mfanye binti wa kazi awe sehemu ya familia yako. Mfanye ajisikie kupendwa kama mwanafamilia mwingine. Unapofanya hivyo, unamfanya achangamke moyo na hivyo kuwa na hamasa ya kujituma. Kwa mfano, unaweza kumtambulisha kwa wageni kama sehemu ya familia yako na unaweza kufikiria kumweka kwenye picha rasmi za familia unazoning’iniza ukutani. Sambamba na hilo, epuka uhusiano usio wa kimaadili na wasichana hawa. Unapofanya hivyo, unajenga mazingira ya kudharaulika. Ukidharaulika, ni rahisi mwanao kuwa mhanga. Mpe huduma anazostahili Hakuna mfanyakazi ambaye hatamani kupata marupurupu. Hata wewe unahitaji mkubwa wako wa kazi akuangalie kimaslahi, na atambue kazi nzuri unayomfanyia. Vivyo hivyo, nawe fikiria kumpa msichana wako wa kazi huduma zinazomvutia. Mtengenezee mazingira bora ya kazi. Kwa mfano, unaweza kufikiria kumtengenezea utaratibu wa kujiendeleza kitaaluma. Pia unaweza kuhakikisha unatambua kazi anazozifanya kila siku jioni unaporudi nyumbani. Kwa kufanya hivyo unamjengea ari ya kazi. Onesha mfano mzuri Huwezi kutarajia binti wa kazi aishi vizuri na watoto, wakati wewe mwenyewe huoneshi kuwajali. Onesha kwa vitendo namna unavyotarajia mtoto ahudumiwe. Binti atajifunza kwa vitendo. Kadhalika, kuwa mfano kwa kufanya kazi za ndani kama unavyotarajia afanye yeye. Pika, tenga chakula mezani, fua nguo inapobidi ili kuonesha kuwa unaishi matarajio yako. Unapofanya hivyo, binti atakuheshimu. Tumia muda wa kutosha na mtoto Mtu anayetumia muda mrefu na mwanao ndiye mwenye nafasi zaidi ya kuwekeza. Kwa sababu binti ndiye anayekaa na mwanao kwa muda mrefu, upo uwezekano wa mwanao kufundishwa mambo usiyoyatarajia. Ni vizuri kuhakikisha unafuatilia maendeleo ya kitabia ya mwanao mara unaporudi nyumbani. Jitahidi kuzungumza na mwanao kubaini ikiwa yapo yasiyofaa aliyojifunza. Unapoyabaini, weka mbadala wake mapema. Pamoja na kuchukua hatua hizi, hatusemi kuwa mambo yatakuwa sawia. Zinaweza kuwapo changamoto, lakini si kama ambavyo hautajenga utamaduni wa kuwafatilia watoto. Christian Bwaya ni Mhadhiri wa Saikolojia, Chuo Kikuu cha Kikatoliki Mwenge (MWECAU). Twitter: @bwaya, Simu: 0754 870 815.
4afya
NA KULWA MZEE, DAR ES SALAAM  Muiguizaji wa filamu ‘Bongo Movie’ ambae pia aliwahi kuwa Miss Tanzania mwaka 2006, Wema Sepetu amefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu akituhumiwa kuchapisha video ya ngono kupitia mtandaoni wake wa Instagram. Wema amesomewa mashtaka yake leo Novemba Mosi na wakili wa Serikali, Mwanaamina Kombakono mbele ya Hakimu Mkazi Maira Kasonde. Mwanaamina anadai mshtakiwa amefanya kosa la kusambaza picha hizo Oktoba 15 mwaka huu katika sehemu tofauti tofauti Dar es Salaam. Hata hivyo mshtakiwa huyo amekanà mashtaka huku  upande wa mashtaka ukidai upelelezi wake haujakamilika hivyo kesi imehairishwa  na itatajwa Novemba20 mwaka huu. Akitoa masharti ya dhamana Hakimu Kasonde amemtaka Wema Sepetu kutoweka video zinazohusiana na ngono wala maneno yoyote yenye mwelekeo huo katika mtandaoni wake wa kijamii wa Instagram. Pia Wema ametakiwa kuwa na mdhamini mmoja wa kusaini dhamana ya maandishi ya Sh milioni 10. Kabla ya kupewa dhamana hiyo wakili Kombakono aliiomba mahakama kumpatia masharti magumu ya dhamana ili iwe fundisho kwa wengine kwa sababu anawafuasi wengi wanaomuangalia wakiwemo watoto. Wakili Ruben Simwanza anayemtetea Wema ameomba mteja wake apewe dhamana ya masharti nafuu kwa kuwa ni haki yake. Mahakama imekubali kumpa dhamana kwa masharti yaliyotajwa.
0burudani
Sepetu aliyewahi kutwaa taji la ulimbwende wa Tanzania mwaka 2006 (Miss Tanzania 2006), alisema baada ya kukabidhiwa fomu hiyo na Katibu wa UWT Wilaya ya Ikungi, Yagi Kiaratu, kuwa atakuwa msaada mkubwa kwa wasanii nchini na atahakikisha anakomesha wizi wa kazi zao.Alisema iwapo atafanikiwa kuwa mbunge atatumia vyema nafasi hiyo kutetea kazi za wasanii na kuongeza kuwa mtu akiwa kiongozi ana nafasi nzuri zaidi ya kushughulikia masuala kama hayo kuliko mtu wa kawaida.Aidha, alisema kutokana na ukweli kwamba amekuwa akifanya kazi za wasanii kupitia tasnia hiyo kwa muda mrefu, atahakikisha anakuza na kuinua vipaji vya wasanii vijana katika Mkoa wa Singida.“Lakini pia nitakuwa sauti ya akina mama wa mkoa huu wa Singida. Nitakaa nao kusikia kero na mahitaji yao kisha kuangalia vipaumbele vyao na kuwasaidia kadri ya uwezo wangu,” alisema.Kwa upande wake, Sitti ni miongoni mwa makada wanane waliochukua fomu hadi jana za kuomba kuteuliwa kugombea ubunge kundi la Umoja wa Vijana UVCCM Mkoa wa Morogoro.Hata hivyo, baada ya kukabidhiwa taji la Redd’s Miss Tanzania 2014 Oktoba 11, mwaka jana, Kampuni ya Lino International Agency ililazimika kumvua taji mrembo huyo kutokana na kushutumiwa kwa kosa la kudanganya umri katika mashindano hayo na taji hilo lilikabidhiwa kwa mshindi wa pili, Lilian Kamazima.Sitti ambaye ni mtoto wa Mbunge wa Temeke, Abbas Mtemvu, ni Mjumbe wa Mkutano Mkuu wa Vijana Kata ya Kilakala katika Manispaa ya Morogoro, alichukua fomu juzi na katika kinyang’anyiro hicho yumo nduguye Lulu.Kaimu Katibu wa UVCCM Mkoa wa Morogoro, Ignas Kinyowa aliwataja wengine waliochukua fomu ni Harriet Sutta ambaye ni Mwenyekiti wa UVCCM Mkoa, Sophia Kizigo ambaye ni Mjumbe wa NEC Taifa, Bupe Makibi ambaye ni Mjumbe wa Baraza Kuu la Vijana Wilaya ya Morogoro, Amina Nyamgini, Bertha Bisanda na Salha Kibowa.Kwa mujibu wa Kinyowa, wagombea wanaohitajika kuomba ubunge kupitia UVCCM ni pamoja na kuwa na umri wa miaka 21 hadi 30 na kuwa kadi ya Umoja wa Wanawake (UWT) pamoja na CCM.
5michezo
Na JONAS MUSHI -DAR ES SALAAM WAZIRI wa Nchi Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Angellah Kairuki, amesema Serikali kupitia Chuo Cha Utumishi wa Umma (TPSC) itaendelea kuwajengea uwezo watumishi wa umma ili waendane na kasi ya mabadiliko, changamoto na mahitaji ya sasa katika utumishi wa umma. Akiwasilisha taarifa ya chuo hicho kwa Kamati ya Kudumu ya Bunge, Utawala na Serikali za Mitaa Dar es Salaam jana, Waziri Kairuki alisema mafunzo hayo ni muhimu kwa watumishi. Aliongeza kuwa Serikali inakamilisha mchakato wa maandalizi ya mafunzo ya lazima kwa watumishi wa umma nchini. Katika kuongeza ufanisi na tija, chuo hicho kimejenga, kuhuisha na kusimika mifumo mbalimbali ya kusimamia utekelezaji wa majukumu. “Baadhi ya mifumo hiyo ni mpango mkakati wa mwaka 2016-2021, utekelezaji kikamilifu wa mkataba wa huduma kwa mteja na kuanzishwa kwa dawati la malalamiko na kamati za uadilifu. Aidha Kairuki aliyataja majukumu mengine kuwa ni kuendelea kusimika mifumo ya tehama, miundombinu ya mtandao (LASN), mtandao wa Serikali (Govnet), mfumo wa simu za Serikali (Voip) na mfumo wa barua pepe za Serikali (GSM). Waziri Kairuki aliiambia kamati hiyo kuwa katika kuendeleza weledi wa watumishi wa umma kwenye utunzaji wa kumbukumbu na uhazili, chuo kinatarajia kuanzisha shahada ya kwanza kwenye maeneo hayo mawili. Naye Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge, Utawala na Serikali za Mitaa, Jasson Rweikiza, alikipongeza chuo hicho kwa jitihada zake za kuwaendeleza watumishi wa umma na kutoa ushauri kwa Serikali ili ifungue tawi la chuo hicho jijini Mwanza kuwahudumia wakazi wa Kanda ya Ziwa.
3kitaifa
NAIROBI, KENYA MSANII wa muziki nchini Kenya, Charles Njagua ‘Jaguar’ amemshambulia mkali wa mastari CMB Prezzo kwa kitendo cha utovu wa nidhamu alichokionesha mwishoni mwa wiki iliyopita kwenye runinga ya taifa nchini humo ya KTN. Katika kipindi cha ‘Friday Briefing’ ambacho msanii anayealikwa hupewa nafasi ya kusoma taarifa ya habari, lakini katika mahojiano na mtangazaji wa kipinid hicho, Betty Klalo, Prezzo alionekana kukosa nidhamu ambapo alianza kwa kumsifia mtangazaji huyo ambaye ni mke wa mtu, huku akidai kwamba ni mzuri na mume wake ana bahati ya kuwa na yeye. Ghafla Prezzo alionekana akimkumbatia mrembo huyo na kumfanya akose kujiamini katika kipindi hicho ambacho kikionekana ‘Live’. Kutokana na hali hiyo Jaguar aliamua kumshambulia msanii huyo kwa njia ya mtandao wa kijamii wa Instagram na kudai kwamba ‘Prezzo anatakiwa kupelekwa kwenye kituo maalumu cha kuwasaidia watu ambao wana matatizo ya akili’. Mbali na Jaguar, wadau mbalimbali wamemshambulia msanii huyo kwa kitendo cha kukosa nidhamu huku akiwa anahojiwa.
0burudani
Yanga iliibuka na ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya mtani wake Simba katika mechi ya raundi ya pili ya Ligi Kuu bara iliyochezwa kwenye uwanja wa Taifa juzi.Mabao ya Yanga katika mechi hiyo yaliyovuta hisia za mashabiki wengi yalifungwa na Donald Ngoma na Amisi Tambwe katika kila kipindi.Ushindi huo umeirejesha Yanga kileleni mwa msimamo wa Ligi Kuu ikiwa na pointi 46 huku Azam na Simba zikifuatia zikiwa na pointi 45 kila moja.Pluijm alisema baada ya mechi hiyo kwamba ushindi huo haumaanishi kuwa tayari wamechukua ubingwa na kwamba kazi ngumu iko mbele yao mpaka kutetea ubingwa wao.“Angalia bado tuna mechi nyingi za kucheza na nyingi ugenini, tunaenda mechi baada ya mechi, tunafurahi kuifunga Simba lakini bado tuna kazi kubwa,” alisema.Alisema kila timu inataka kuonesha uwezo wake dhidi ya Yanga na hilo linafanya kila mechi wanayocheza kuwa kama fainali. Aidha kuhusu ushindi dhidi ya Simba, Pluijm alisema walishinda kwa sababu walifanya maandalizi mazuri ya kuwaandaa wachezaji kisaikolojia na kimchezo.“Tulijiandaa vizuri, tuliwaandaa wachezaji kimashindano na kisaikolojia na hilo limesaidia kwa kiasi kikubwa kwani kila mchezaji alionekana kujiamini na kuonesha juhudi,” alisema.Pluijm alikipongeza kikosi chake kwa kuonesha mchezo mzuri kama alivyokielekeza akisema kuwa amefurahishwa na matokeo.Pia, aliisifu safu yake ya ulinzi kwa kutendea haki mchezo huo na kufanikiwa kuwazuia wapinzani kushindwa kupenya.Safu ya ulinzi iliongozwa na Vicent Bossou, Mbuyu Twite na Pato Ngonyani tofauti na mchezo wa raundi ya kwanza ambapo iliongozwa na wakongwe Kelvin Yondani na Nadir Haroub ‘Canavaro’.Kocha huyo wa Yanga hakusita kuwazungumzia wapinzani wao Simba kuwa walicheza vizuri pia.
5michezo
KITENDAWILI juu ya mauaji yaliyotokea Kijiji cha Kazikazi, Kata ya Kitaraka, Tarafa ya Itigi wilayani Manyoni, kimeteguliwa jana baada ya Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Singida, Sweetbert Njewike kusema chanzo cha mauaji hayo ni Isaack Petro kutuhumiwa kuharibu mali ya mwanakijiji mwenzake, Rose Andrew.Kamanda Njewike alieleza kuwa Februari mosi mwaka huu, Petro ambaye sasa ni marehemu, alidaiwa kuharibu mali mbalimbali yakiwemo mabanda katika shamba analolima Rose, ambaye alitoa taarifa kwa uongozi kwa kijiji.Amesema kutokana na eneo hilo la Tanganyika Packers kumilikiwa na Halmashauri ya Mji wa Itigi, uongozi wa halmashauri hiyo akiwamo Mkurugenzi Mtendaji (DED), Pius Luhende, ulienda kwenye shamba analolima Rose ili kuona na kujiridhisha juu ya uharibifu huo.“Baada ya kuona uharibifu huo na kumkosa mtuhumiwa, walilazimika kwenda kwenye kanisa moja jirani ambapo waliambiwa mtuhumiwa alikuwa ameenda kwa ajili ya ibada na kwa bahati walimkuta,” amesema Kamanda Njewike.Alieleza kuwa mara walipofika kanisani humo na kuanza taratibu za kumtia nguvuni mtuhumiwa, kulitokea vurugu iliyosababisha DED Luhende kukimbilia nje huku akifunga mlango ili kuhakikisha mtuhumiwa hatoroki.Hata hivyo, inadaiwa kuwa katika heka heka za kumtia nguvuni, risasi moja ilimpata mtuhumiwa kisogoni na hivyo kukimbizwa hospitalini kwa matibabu.“Bahati mbaya, mtuhumiwa alifariki dunia kutokana na jeraha lililompata,” alisema Kamanda Njewike.Kutokana na sakata hilo, alisema Jeshi la Polisi linawashikilia watu saba kwa ajili ya mahojiano ya kina kisha watafikishwa mahakamani wote watakaobainika kuhusika na kitendo hicho.Amewataja wanaoshikiliwa ni DED wa Halmashauri ya Itigi, Luhende, Silvanus Lungwisha (Ofisa Kilimo na Mifugo), Eric Paul (Mwanasheria wa halmashauri) na Eliutha Augustino (Ofisa Tarafa Itigi).Watuhumiwa wengine ni Yusuph John (Ofisa Mtendaji wa Kijiji cha Kazikazi), Rodney Elias (Askari Wanyamapori) na Makoye Steven ambaye ni Askari wa Wanyamapori Hifadhi ya
3kitaifa
NA MWANDISHI WETU TIMU ya  mpira wa kikapu ya Toronto Raptors imejiweka katika nafasi nzuri ya kuibuka mabingwa wa Ligi Kuu ya Marekani maarufu kama NBA, baada yajana kuibuka na ushindi wa vikapu 105-92 dhidi ya Golden State Warriors.  Kwa ushindi huo, Raptors inaongoza kwa ushindi wa michezo mitatu dhidi ya mmoja wa Worriors, hivyo inahitaji kupataushindi moja tu katika michezo mitatu iliyosalia kati ya timu hizo ili kutwaa ubingwa. Katika mchezo wa jana, Kawhi Leonard aliwaongoza wachezaji wa Raptors  baada ya kufunga vikapu 36,  huku Serge Ibaka akitokea bench na kufunga vikapu 20. Wachezaji Pascal Siakam na Kyle Lowry, pia walitoa mchango mkubwa uliosaidia kufanikisha ushindi huo. Mchezo namba tano kati ya timu hizo utachezwa kesho Alfajiri, Scotiabank Arena, Canada. Raptors itakuwa ikipata sapoti kubwa ya  kushangiliwa na shabiki wao mkubwa mwanamuziki wa Rap, Drake. Raptors haijawai kushinda ubingwa wa NBA, hivyo itakua imeandika historia mpya kama itafanikiwa kushinda ubingwa wa ligi hiyo itakapocheza nyumbani kwao.
5michezo
['Barcelona inasubiri pembeni kumuajiri kocha wao wa zamani Pep Guardiola iwapo ataamua kuiaga miamba ya ligi ya Premia Manchester City mwisho wa msimu huu.. (Sunday Express)', 'Mkufunzi wa Leicester City Brendan Rodgers ni miongoni mwa wanaopigiwa upatu kumrithi Guardiola iwapo raia huyo wa Uhispania atandoka katika klabu hiyo ya Uingereza(Sun on Sunday)', 'Mshambuliaji wa klabu ya Red Bull Salzburg, mwenye umri wa miaka 19 na raia wa Norway Erling Haaland ameweka wazi kwamba Man United ndio klabu anayolenga kuhamia iwapo ataondoka katika klabu yake mwezi Januari.. (Star on Sunday)', 'Makocha wanaopigiwa upatu kumrithi Unai Emery katika uwanja wa Emirates wanazuiwa na hali ya klabu hiyo kutotaka kununua wachezaji wapya katika dirisha la uhamisho.. (Express)', 'Manchester City imeajiandaa kushindana na Manchester United, Liverpool na Chelsea katika kumsajili upya winga wa Uingereza mwenye kwa thamani ya £90m Jadon Sancho, 19. (Sun on Sunday)', 'Mkufunzi wa West Ham Manuel Pellegrini anakaribia kupigwa kalamu licha ya timu yake kupata ushindi siku ya Jumamaosi huku kocha wa zamani David Moyes akitarajiwa kujaza pengo lake. (Star on Sunday)', 'Chelsea imeweka dau la 30m euros (£25m) kwa klabu yoyote inayotaka kumnunua beki wa kushoto wa Uhispania Marcos Alonso, 28. (Calciomercato)', 'Manchester United inafikiria kumnunua mshambuliaji wa Napoli na Ubelgiji Dries Mertens, 32. (Tuttomercato)', 'Klabu hiyo ya Old Trafford pia inafikiria uwezekano wa kumnunua mshambuliaji wa Inter Milan raia wa Argentina Lautaro Martinez, 22, na kiungo wa kati wa Paris St-Germain Leandro Paredes, 25. (Mirror)', "Kiungo wa kati wa Chelsea N'Golo Kante, 28, anataka kuondoka katika klabu hiyo lakini atapuuzilia mbali ushauri wa mchezaji mwenza wa Ufaransa Ousmane Dembele, 22, kuelekea Juventus au Real Madrid badala ya Barcelona. (Eldesmarque)", 'Mchezaji wa zamani wa Chelsea Eden Hazard, 28, ameapa kurudi klabu yake ya zamani mkataba wake Real Madrid utakapokamilika . (Sun on Sunday)', 'Mkufunzi wa Tottenham Jose Mourinho anasema kwamba hatofichua maelezo ya mazungumzo yake na kiungo wa kati wa Tottenham Christian Eriksen kuhusu hatma ya mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 27. (Sunday Mirror)']
5michezo
Na MWANDISHI WETU-DAR ES SALAAM BARAZA la Taifa la Biashara (TNBC) limesema kuwa katika kutekeleza mpango kazi wake nusu ya mwaka wa fedha wa 2019/2020 na kuchangia vikubwa mapinduzi ya kiuchumi Tanzania, linatarajia kutumia Sh 1,104,590,000. Katika taarifa iliyotolewa Dar es Salaam kuhusu shughuli za baraza kwa kipindi cha mwaka wa fedha 2019/20, baraza hilo licha kutoa mchanganuo wa mkiasi cha fedha utakaochangwa na wadau, lakini limesema litapokea mgawo wa Serikali, mgawo wa mradi wa LISC na mgawo kutoka wadau wengine. Taarifa hiyo ilieleza kwamba TNBC inatazamiwa kuchangia vikubwa katika mapinduzi ya kiuchumi Tanzania. Pamoja na mambo mengine, baraza linatarajia kushirikiana na Tamisemi kuhakikisha mabaraza ya mikoa na wilaya yanakutana kama ilivyoainishwa kwenye mwongozo. “Itafanyika jitihada ya kuimarisha baraza na kuwa kitovu cha taarifa zinazohusu maboresho ya mazingira ya biashara nchini na kuendelea kushirikiana na wadau mbalimbali katika kufanya tafiti zitakazochochea majadiliano yenye tija kati ya sekta ya umma na sekta binafsi. “Katika hili, baraza linatarajia kufanya majadiliano katika maeneo kama ushiriki wa mwanamke katika uwekezaji na biashara, ikiwemo changamoto zake, changamoto zinazokabili biashara ndogo ndogo na za kati na fursa zilizopo,” ilieleza taarifa hiyo. Baraza pia litaendelea kuimarisha ushirikiano uliopo kati ya sekta binafsi na sekta ya umma katika kuchochea mapinduzi ya kiuchumi nchini. “Serikali ya Awamu ya Tano chini ya Mheshimiwa Rais John Magufuli, imewekeza kwa kiasi kukubwa katika sekta ya usafirishaji. “Hivyo basi ni muhimu kwa baraza kuonyesha fursa mbalimbali zilizopo kwenye sekta ya usafirishaji na jinsi Watanzania wanavyoweza kujikomboa kiuchumi kupitia kwenye mnyororo wa thamani wa sekta ya usafirishaji,” ilisema taarifa hiyo.
3kitaifa
TASNIA ya mitindo imebeba maisha ya watu ndani yake, kuna watu wanaipa heshima kubwa sekta hiyo kwa sababu imewapa maisha, imewapa umaarufu unaofanya waishi vyema hapa duniani. Haijalishi nafasi waliyonayo sasa hivi waliitafuta vipi ila hata siku moja huwezi kuona wanaichezea kazi hiyo. Kuichezea tasnia ya mitindo siyo lazima uwadharau waasisi wake, hata kitendo cha kutafuta umaarufu kwa kigezo cha mitindo kwa kujifanya modo ambaye unakiuka misingi, tamaduni na taratibu za tasnia hiyo unakuwa unaidharau tasnia na kuwakosea mamodo wenye heshima zao. Licha ya kuwa mchekeshaji ambaye muda mwingi huendekeza utani, Idris Sultan moja katika ya posti zake kwenye mitandao ya kijamii wiki hii aliandika ujumbe mujarabu sana ambao umenigusa na kuwagusa watu wote wanaohusika na tasnia ya mitindo nchini kufuatia kuibuka kwa watu wengi wanaotumia kivuli cha mitindo kupitisha uhuni wao. Mshindi huyo wa shindano la Big Brother mwaka 2014, aliwashukia wanamitindo wachanga wakike ambao wamekuwa wakiitumia mitandao ya kijamii vibaya kwa kuweka picha za utupu wakitumia kigezo uamitindo. Idris aliiendelea kutoa somo kwa mamodo chipukizi ambao wanapiga picha zinazoacha sehemu kubwa za miili yao kwa kuwauliza lengo lao ni nini haswa mpaka kuingia studio au kwenye fukwe na kupiga picha hizo chafu zinazopakaza matope tasnia ya mitindo, Kufanya hivyo ni kutangaza brandi gani? Je ni kutangaza mataulo, vumbi au majani, kampuni gani kubwa itawekeza fedha zake kwa mtu ambaye tayari heshima yake kwenye jamii imeshuka? Hakuna. Hapo ndipo niliposhawishika kuandika andiko hili ambalo ni kama nyundo ya kugongelea msumari wa Idris kwa mamodo chipukizi ambao kiukweli wanaivunjia heshima tasnia ya mitindo kwani kiuhalisia modo si kuacha mwili wazi. Kwa maana hiyo endapo modo chipukizi atatumia njia hiyo kujipatia umaarufu anakuwa anaivunjia heshima tasnia hiyo hali kadharika anakuwa anawakosea wanamitindo wanaoishi kupitia kazi hiyo, wote wanaonekana wahuni ilhali si kweli. Mbona wanamitindo kama Flaviana Matata, Herieth Paul, Niler, Lorraine Pascale, Millen Magese, Maggie Vampire, Dax, Lota, Calisah na wengine wengi hawafanyi hiyo michezo, iweje wewe utumie kivuli cha mitindo katika kukamilisha adhma yako mbaya. Ni lazima suala hili la watu kuichafua tasnia ya mitindo kwa kuleta michongo ambayo si ya kimitindo tuikemee kwa nguvu zote, tunahitaji wanamitindo ambao tutawatambua kwa kazi zao nzuri na siyo kwa matukio ya kuweka picha za utupu kwenye mitandao ya kijamii.
0burudani
Serengeti imefuzu fainali za michuano hiyo zitakazofanyika Gabon mwezi ujao na jana ilikwenda Morocco kwa kambi ya maandalizi kabla ya kwenda Gabon.Mama Samia aliwaalika wachezaji hao nyumbani kwake juzi kwa chakula cha jioni na ndipo alipowapa neno hilo akikumbushia matokeo ya sare ya mabao 2-2 katika mechi ya kirafiki dhidi ya Ghana iliyochezwa mwanzoni mwa wiki hii kwenye Uwanja wa Taifa ambapo Serengeti ililazimika kusawazisha mabao hayo katika dakika 10 za mwisho.“Matokeo ya mechi dhidi ya Ghana yalikuwa mazuri lakini yalinipa hofu kidogo kwa sababu kilichotokea ilikuwa ni miujiza kwani ndani ya dakika 10 mlirudisha mabao mawili, sio kitu rahisi, kwa kawaida maajabu huwa hayana kanuni kwa hiyo naomba msicheze kwa maajabu, chezeni ndani ya dakika 90 mapate ushindi,” alisema.Alisema akiwauliza walitumia fomula gani kusawazisha mabao hayo katika mechi ile hawawezi kueleza kwani ni uwezo wa Mungu aliyetaka yatokee yaliyotokea na kwamba kama si Ghana kupoteza muda kwa kujiangusha hovyo uwanjani hapo, hali iliyofanya mwamuzi kuongeza dakika 10 pengine timu hiyo ingefungwa 2-0.Pia alitoa mwito kwa viongozi na benchi la ufundi kuishi na kuwalea wachezaji hao kama marafiki lakini kuwarekebisha kwa kuwachapa pale wanapokosea na utukutu unapozidi kwani huruma hailei mwana.“Vijana wanahitaji matunzo mema, hamasa, upendo, mshikamano na kupendana wao kwa wao kupendwa na walimu na viongozi ndivyo wanaweza kufanya vizuri hivyo tunawakabidhi hii timu, mnakwenda nje ya nchi mtakaa kwa muda mrefu, hatupendi kusikia lolote baya limetokea kwa hawa vijana,” alisema Samia.
5michezo
Hayo yalibainishwa na Ofisa Mtendaji Mkuu wa CMSA, Nasanda Massama, wakati akizungumza kwenye uzinduzi wa kampuni ya Soko la Bidhaa (TMX), iliyozinduliwa na Rais Jakaya Kikwete Dar es Salaam, hivi karibuni.Alisema kwa upande wa kampuni za ndani masoko hayo ya mitaji mchango wake umeongezeka kutoka asilimia sita, mwaka 2005 hadi asilimia 24, mwaka huu.“Hali hii inatokana na ukweli kuwa kumekuwa na ongezeko kubwa la kampuni zilizoorodheshwa katika masoko ya mitaji. Kwa sasa kuna kampuni 25 kutoka kampuni sita zilizoorodheshwa wakati wa kuanzishwa kwa masoko haya,” alisisitiza Massanda.Kwa upande wake, Rais Kikwete alipongeza jitihada zinazoendelea kufanyika nchini kwa ajili ya kuboresha masoko ya mitaji, hisa na bidhaa, hali ambayo alisisitiza itasaidia kukuza uchumi wa Tanzania na kutimiza lengo la kuwa moja ya nchi zenye uchumi wa kati.Hata hivyo, alisema pamoja na kwamba Serikali inajitahidi kukuza uchumi huo wa nchi kupitia kilimo, kutokana na Tanzania kuwa na idadi kubwa ya wakulima, bado kuna haja ya kushirikisha hadi sekta binafsi kwa ajili ya kutafuta jawabu la uhaba wa maghala ya kuhifadhia chakula.“Nafurahi kuona namaliza muda wangu kama kiongozi wa Tanzania, lakini jitihada nilizofanya zikianza kuonekana. Sasa mageuzi ya kilimo ndio yanaanza kupitia soko la bidhaa TMX, kilimo chetu kitaimarika, lakini bila kupata jawabu la maghala ya kuhifadhia mazao, ukuaji wa kilimo utakua mgumu,” alisisitiza Rais Kikwete.Aidha alisema sera ya kilimo kwanza inafanya vizuri, ingawa bado suala la stakabadhi ghalani limekuwa likipigwa vita, kwani wakulima wengi wamekuwa wakizalisha mazao mengi kiasi cha mengine kukosa maghala ya kuhifadhia.“Uwezo wa Wakala wa Taifa wa Hifadhi ya Chakula (NFRA) ni tani 150,000 tu, lakini mazao yamekuwa mengi sana na wakulima wanafikiri kuwa NFRA ndio mnunuzi pekee wa mazao yao. Natumaini kupitia soko la bidhaa TMX, soko la mazao haya litaimarika.
1uchumi
Klabu ya simba imemteua Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Mkonda kuwa kuwa mshauri mkuu katika bodi ya wakurugenzi. Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam ambaye pia ni Mwanasimba mwenzetu, Paul Makonda ameteuliwa kuwa Mshauri Mkuu wa Bodi ya Wakurugenzi. Karibu sana RC Makonda. #NguvuMoja A post shared by Simba Sports Club (@simbasctanzania) on Jan 17, 2020 at 9:21am PST Makonda mabaye pia ni shabiki wa Timu hiyo yenye maskani yake Msimbazi jijini Dar es Salaam amekaribishwa na wapenzi wa timu hiyo pamoja na Mkurugenzi wa bodi Mohammed Dewji. Katika mitandao ya kijamii Dewji ambaye pia ni muwekezaji katika klabu hiyo amemkaribisha akisema anaamini watafanya kazi vizuri na kuijenga simba kuwa bora zaidi. Nafurahi sana kumkaribisha RC wetu, Mnyama mwenzangu PAUL MAKONDA kwenye Bodi ya Wakurugenzi ya Simba akiwa kama Mshauri Mkuu (Senior Advisor). Karibu kaka. Pamoja tutajenga Simba bora zaidi! Hongera kwa uteuzi 🙏🏽 pic.twitter.com/lfKbaEZA9K — Mohammed Dewji MO (@moodewji) January 17, 2020
5michezo
WAZIRI Mkuu, Kassim Majaliwa ametoa mapendekezo matano, yatakayosaidia kuwa na matumizi endelevu ya rasilimali ya maji kwenye Bonde la Mto Nile ili kuziwezesha nchi wanachama kupata maendeleo kupitia rasilimali adimu ya maji.Miongoni mwa mapendekezo aliyoyatoa ni kuzitaka nchi wanachama, kuimarisha ushirikiano kwa kuwa bila kuwa na ushirikiano madhubuti, hawataweza kusimamia matumizi endelevu wa maji na pia hawataweza kushughulikia changamoto zinazokabili bonde hilo.Alisema kwa sasa bonde hilo linakabiliwa na changamoto mbalimbali, ikiwemo kupungua kwa mtiririko wa maji kwenda Ziwa Victoria, ambalo ni moja ya vyanzo muhimu vya mto Nile na hiyo imetokana na uharibifu wa mazingira na mabadiliko ya tabia nchi.Alisema Bara la Afrika ni miongoni mwa maeneo yanayokabiliwa na matatizo makubwa ya maji duniani, ambapo takwimu zinaonyesha kwamba takribani nchi 14 hivi sasa zinakabiliwa na uhaba au upungufu wa maji.Majaliwa aliyasema hayo jana jijini Dar es Salaam, wakati akifungua mkutano wa 21 wa Baraza la Mawaziri la Nchi za Bonde la Mto Nile zilizopo Ukanda wa Maziwa Makuu (NELCOM), ambao umehudhuriwa na wawakilishi wa nchi hizo na wadau wa maendeleo.Katika mapendekezo yake, pia alizitaka nchi hizo kuongeza utashi wa kisiasa katika kutekeleza miradi ya pamoja, kwa kuwa kumekuwepo na ucheleweshaji usiokuwa wa lazima katika utekelezaji wa miradi.Alitoa mfano majadiliano ya mradi wa Rusumo, yaliyoanza mwaka 1970, lakini utekelezaji wake ulianza mwaka 2015.Pia aliwataka kuimarisha taasisi na kutoa rai kwa nchi wanachama, ambao hawajafanya hivyo kuridhia mkataba kuanzisha Kamisheni ya Bonde la Mto Nile na kuwataka ulipaji wa michango kwa wakati ili kuziwezesha taasisi hizo, kutekeleza majukumu yake hususan miradi ya maendeleo.Mapema, Waziri wa Maji ambae pia ni Mwenyekiti wa NELCOM, Profesa Makame Mbarawa alisema mkataba wa kuanzisha rasmi ushirikiano wa nchi za Bonde la Mto Nile(NBI), ulisainiwa jijini Dar es Salaam Februari 22, 1999, lakini hadi sasa mambo mengi yameshindwa kutekelezwa.Waziri wa Nishati, Dk Medard Kalemani alisema wizara yao ni mdau mkuu kwenye mkutano huo muhimu na kwamba Tanzania ni nchi ambayo ni wanufaika wakubwa na kuomba mkutano huo kuendelea kuweka mikakati ambayo itasaidia kupatikana kwa nishati ya umeme ili kuhakikisha kunakuwa na umeme wa bei nafuu.Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano waa Afrika Mashariki, Balozi Augustine Mahiga alisema mto Nile ndio mto mrefu duniani na Ziwa Victoria ni miongoni mwa maziwa makubwa ambako ndiko chanzo cha mto huo na kuzitaka nchi wanachama kutatua changamoto zao kwa mazungumzo.
3kitaifa
Na Upendo Mosha, Moshi  Mkuu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), Dk. Fredrick Shoo, amesema wale wote wanaojaribu kupotosha ukweli wa waraka wa maskofu kwa kuupaka matope ni wajinga. Askofu Shoo ametoa kauli hiyo leo katika Usharika wa Moshi Mjini Dayosisi ya kaskazini, mkoani Kilimanjaro wakati akitoa salamu za Pasaka katika ibada maalumu ya kusherekea sikukuu hiyo. Amesema kumekuwa na baadhi ya watu wakiwamo wanasiasa ambao wamekuwa wakitumia nguvu nyingi kupotosha waraka  wa maaskofu hao na kulipaka kanisa matope kwa malengo yao binafsi jambo ambalo halipendezi na kwamba watu hao ni wajinga. “Wapo wanaotumia nguvu nyingi kutaka kupotosha ujumbe wa waraka wa maaskofu na wamekuwa wakilipaka kanisa matope ili waweze kurejea katika waraka ule, watu hawa naweza kuwaita ni wajinga lakini pamoja na hilo nataka wakayatafakari na kama wanaona kuna hatua za kuchukua wachukue. “Kanisa limekuwa linapata kejeli za aina mbalimbali kutoka kwa watu hao na kuwatuhumu kuwa maskofu walifikia maamuzi ya kuandika waraka huo kutokana na sababu za kimaslahi kwa maana ya sadaka makanisani kupungua jambo ambalo si la kweli. “Kanisa linasitikika sana, tunaposema jambo la kweli na jambo linalohusu maisha ya Watanzania wote, halafu kunatokea watu chache ambao naweza kuwaita wajinga wanakebehi na kusema eti kwa sababu sadaka zimepungua kanisani sisi sadaka hazijapungua kwani wakristo wanajitoa sana na hatujapungukiwa na kitu ila tunasema yale tunayoyaamini,” amesema. Askofu Shoo amesema anafahamu kuwa kupitia waraka ule maaskofu wa kanisa hilo watabatizwa majina ya aina mbalimbali na kwamba hizo ni jitihada za kujaribu kuuzima ukweli ulipo katika wataka huo na wao hawajali kuhusu hilo bali watasimamia ukweli zaidi. “Najua tutaitwa majina mengi maaskofu na hizo ni jitihada za upotoshaji wa ule ukweli ulipo katika waraka na tukumbuke hili si jambo la hivi hivi tu…. kwani kwa wakati mmoja mabaraza ya  maaskofu wa makinsa makubwa mawili nchini kukaa na kutoa waraka ambao una ujumbe ulioshabihiana si kitu cha kawaida mimi nasema kuna kitu Mungu anataka kutuambia kupitia ujumbe ule tutafakari hili kama taifa,” amesema.
3kitaifa
PENDO FUNDISHA-MBEYA WASICHANA wenye umri wa miaka 15 hadi 24 nchini, wanatajwa kuathiriwa zaidi na maambukizo mapya ya Virusi Vya Ukimwi (VVU) na matatizo ya afya ya uzazi. Hayo yalielezwa jana na Mkurugenzi Mtendaji Tume ya Kudhibiti UKIMWI Tanzania (TACAIDS), Dr. Leonard Maboko, wakati akizungumza na vyombo vya habari Mkoa wa Mbeya na kueleza lengo la uzinduzi wa programu ya usikilizaji wa vipindi vya redio kwa vijana itakayojulikana kwa jina la ‘Ongea’. Alisema, utafiti wa viashiria vya ukimwi wa mwaka 2016/17, unaonyesha watu 72,000 wenye umri wa miaka 15 na kuendelea hupata maambukizo mapya ya VVU kila mwaka nchini. Alisema, changamoto kubwa ipo kwenye kundi la vijana wenye umri kati ya miaka 15-24 ambao huchangia kwa asilimia 40 ya maambukizo mapya kati ya maambukizo 72,000 kitaifa kwa mwaka. Aidha, Maboko alisema miongoni mwa kundi hilo la vijana  changamoto kubwa ipo kwa wasichana ambao huchangia asilimia 80 ya maambukizo mapya ya VVU. “Changamoto nyingine kwa wasichana ni kuhusu afya ya uzazi kwani asilimia 27 ya wasichana wamepata ujauzito au wameshapata mtoto katika umri wa miaka 15-19 huku ndoa za utotoni asilimia 31 ya wanawake wenye umri wa miaka 20-24 waliolewa kabla ya kufikia umri wa miaka 18,”alisema. Akielezea upande wa elimu, Mkurugenzi huyo alisema asilimia 80ya wasichana humaliza shule ya msingi lakini asilimia 68 hujiunga na masomo ya sekondari na kati ya hao asilimia 38.7 ndio hufanikiwa kumaliza masomo yao. Tume ya kudhibiti Ukimwi Tanzania, imeshirikiana na Shirika la Kimataifa la Kuhudumia Watoto(UNICEF) na wadau wengine, kuzindua program hiyo ili kuelimisha vijana hususani wa umri wa miaka 15-19 walio ndani na nje ya shule kuhusu kujikinga na VVU na magonjwa mengine .
3kitaifa
Na JANETH MUSHI -ARUSHA WAZAZI wa watoto Maureen David (6) na Ikram Salim (3), waliotekwa na kukutwa wakiwa wamefariki katika shimo la maji taka eneo la Uzunguni, Mtaa wa Olkerian Kata ya Olasiti, wameeleza kile walichokishuhudia kwenye miili ya watoto wao wakati ilipokuwa ikifanyiwa uchunguzi na madaktari. Maureen ambaye alikuwa ni mwanafunzi wa darasa la kwanza katika Shule ya Msingi ya Lucky Vincent aliyetekwa Agosti 21 huku Ikram akitekwa Agosti 25 na Septemba 5 miili yao kukutwa kwenye eneo hilo.   Akizungumza na MTANZANIA jana, baba Maureen, David Njau, alisema juzi jioni alikuwa hospitali ya Mkoa wa Arusha ya Mount Meru, akishuhudia uchunguzi wa mwili wa mwanaye uliofanywa na madaktari kutoka Hospitali ya Rufaa ya KCMC. Alisema wakati wa uchunguzi hakuweza kuchunguza sana ila aliona majeraha sehemu za kichwani,sikioni pamoja na kwenye mguu wa mwanaye. “Siwezi kulizungumzia sana, mimi baada ya kutambua mwili, hayo mengine sikuchunguza sana. Ameumizwa sehemu ya sikioni ilionekana damu imegandia ndani, sehemu ya mguuni ilikuwa na jereha, hatambuliki sana kwani alikuwa ameharibika, hayo mengine sikuyachunguza nilishindwa nikatoka nje,”alisema Njau. Salim Kassim ambaye ni babu wa Ikram, alisema licha ya mwili wa mtoto kuharibika sana, ulionekana kuwa na viungo vyote na kusema hawakufuatilia matokeo ya uchunguzi zaidi wa madakatari. “Nilikuwepo wakati wanamfanyia uchunguzi ila sikuuliza wataalamu zaidi walichokigundua kwani tulikuwa tunataka tu mwili tuuzike,”alisema Kassim. Ikram alizikwa jana majira ya saa 4 asubuhi katika eneo la Makaburi ya Msikiti wa Olasiti baada ya kufanyiwa ibada nyumbani kwao. Mwili wa Maureen, unatarajia kuzikwa leo katika  makaburi ya JR-Majengo saa 7 mchana, baada ya ibada inayotarajiwa kufanyika nyumbani kwako Olkierian, Kata ya Olasiti. Kauli za daktari, Polisi Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Mkoa wa Arusha ya Mount Meru, Dk. Jackline Urio, alisema miili ya watoto hao ilifanyiwa uchunguzi na wataalamu kutoka hospitali ya KCMC, juzi usiku.   Dk.Urio alisema wataalamu waliofanya uchunguzi huo  walishirikiana na Polisi na maji ya uchunguzi huo yapo polisi.   Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha, Charles Mkumbo, alisema. “Huwezi kupewa majibu wa uchunguzi, tangu lini majibu wanapewa waandishi? Hiyo ni shughuli ya kiupelelezi utapewaje? Hiyo ni kumbukumbu ya kesi, hiyo ndiyo kesi yenyewe utapewaje majibu sasa?” alihoji.
3kitaifa
  Na MWANDISHI WETU  -DAR ES SALAAM RAIS Dk. John Magufuli, ameagiza kuvunjwa kwa sehemu ya jengo la Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) na jengo la Wizara ya Maji yaliyopo eneo la hifadhi ya barabara ili kupisha ujenzi wa miundombinu ya daraja la Ubungo. Rais Dk. Magufuli, alitoa agizo hilo Dar es Salaam jana baada ya kukagua ujenzi wa daraja la juu Tazara na ujenzi wa daraja la ghorofa tatu la Ubungo kwa nyakati tofauti. Alimuagiza Meneja wa Wakala wa Barabara Tanzania (TANROADS) Mkoa wa Dar es Salaam, Mhandisi Ndyamukama Julius, kuvunja sehemu ya majengo hayo ili kupisha ujenzi wa miundombinu ya daraja hilo. Alisema sheria ya hifadhi ya barabara katika eneo hilo ni mita 90 kila upande kutoka katikati ya barabara hivyo haina budi kuzingatiwa hata na Serikali yenyewe. “Ninataka ikiwezekana leo au kesho jengo la TANESCO liwekwe X, wapeni notisi baadaye mje mkate mnapohitaji, kwa sababu sheria ni msumeno Serikali ikifanya kosa inasulubiwa, raia akijenga kwenye hifadhi ya barabara naye anachukuliwa hatua,” alisema Rais Dk. Magufuli. Alisema Sheria ya Hifadhi ya Barabara ilikuwapo tangu mwaka 1932 na kwamba ilifanyiwa marekebisho mwaka 1964, 1966 na mwaka 1967. “Lazima sheria iheshimiwe ili kuharakisha ujenzi wa daraja unafanyika bila vikwazo, sheria ni msumeno haina budi kuzingatiwa hata na Serikali yenyewe,” alisisitiza Rais DK.  Magufuli. Pia aliiagiza TANROADS kutangaza zabuni ya ujenzi wa barabara yenye urefu wa kilomita 16 kutoka eneo linapoishia daraja hilo katika eneo la Ubungo kuelekea Chalinze ili itanuliwe kwa lengo la kurahisisha usafiri katika Jiji la Dar es salaam. Rais Dk. Magufuli, aliwataka makandarasi wanaojenga madaraja ya Tazara na Ubungo kuharakisha ujenzi kwa kufanya kazi usiku na mchana ili yaweze kumalizika kwa wakati ama kabla ya muda huo kwa lengo la kurahisisha maendeleo ya kibiashara katika jiji. ”Dar es salaam ni jiji la kibiashara hivyo hakuna budi miundombinu yake ya usafiri iweze kurahisisha usafirishaji wa bidhaa mbalimbali kutoka ndani ya jiji na nje ya jiji,” alisema. Naye Mhandisi wa Masuala ya Usalama wa Ujenzi, Richard Baruani, alisema ujenzi wa daraja la Tazara umefikia asilimia 64 na  linatarajiwa kukamilika Oktoba, mwakani. Kuhusu daraja la ghorofa tatu la Ubungo, alisema ujenzi wake unatarajiwa kuanza rasmi mwezi ujao.  
3kitaifa
MORONI, COMORO MAHAKAMA Kuu  Comoro imewatangaza wagombea 13 watakaoshiriki Uchaguzi wa Rais   mwezi ujao  ikiwazuia wapinzani wakuu wa Rais Azali Assoumani. Wagombea 19 walijiandikisha kwa ajili ya uchaguzi huo uliopangwa kufanyika Machi 24 na kati ya waliopitishwa, ni Rais Azali pekee anayewakilisha chama cha siasa. Wengine wote wanashiriki kama wagombea binafsi katika uchaguzi huo, ambao unatarajia kumrudisha madarakani Azali aliyechaguliwa kwa mara ya kwanza mwaka 2016. Wapinzani wake wakuu walikuwa Makamu Rais wa zamani, Mohamed Ali Soilih na Ibrahim Mohamed Soule, ambao juhudi zao za kuwania wadhifa huo zilitupiliwa mbali na mahakama iliyojaa washirika wa Azali. Mpango wa kupokezana madaraka miongoni mwa visiwa vitatu vya taifa hilo ulisaidia kuzuia hali ya kutoridhika iliyotawala kwa miaka kadhaa pamoja na mapinduzi ya mara kwa mara mwishoni mwa miaka ya 1990. Uchaguzi utafanyika kwa mujibu wa  vifungu vya Katiba vilivyorekebishwa kwa utashi wa Rais Azali katika kura ya maoni iliyofanyika Julai 2018. Mageuzi hayo yanamwezesha rais kushika madaraka kwa mihula miwili ya miaka mitano kila mmoja badala ya muhula mmoja. Iwapo Azali atashinda, atachukuliwa kuwa ndiyo anaanza muhula wake wa kwanza, jambo ambalo litamruhusu kuwania muhula wa pili mwaka 2024. Soilihi alisema amezuiwa kugombea kwa tuhuma kuwa alificha umiliki wa kampuni yenye thamani ya mabilioni ambayo amekana kuifahamu. “Wagombea wote wa upinzani ambao wangetoa changamoto kwa Azali wamezuiwa,” alisema, na kupinga kile alichokiita ucheleweshaji wa uchaguzi. Soule alisema alizuiwa kwa sababu hati yake ilisainiwa na Naibu Katibu Mkuu badala ya Katibu Mkuu, Ahmed el-Barwane, ambaye alikuwa gerezani kwa miezi kadhaa kwa madai ya kumshambulia mwanajeshi. Upinzani umeparaganyika baada ya viongozi wake kadhaa kukamatwa. Mahakama ya Usalama imetoa hukumu kadhaa za vifungo jela kwa wanasiasa mashuhuri waliopinga kura ya maoni inayomruhusu Azali kurefusha muhula wake madarakani. Ikiwa awamu ya pili itahitajika kwa kukosa mshindi wa moja kwa moja, itafanyika Aprili 21. Katiba mpya imebakisha mzunguko wa urais miongoni mwa visiwa vitatu vya Grande Comore, Anjouane na Moheli, lakini kipindi kimeongezwa kutoka miaka mitano hadi 10. Kisiwa cha Azali cha Grande Comore, hivi sasa ndiyo kinashikilia fursa hiyo. Azali mwenyewe alianza kutwaa madaraka kwa njia ya mapinduzi dhidi ya kaimu rais mwaka 1999 na alirudishwa madarakani hadi 2006 katika uchaguzi wa vyama vingi. Hii leo  wakosoaji wa Azali wanachukulia kwamba amechukua mwelekeo wa udikteta, akiwa na uwezekano wa kubaki madarakani hadi 2029.
2kimataifa
WAANDISHI wa Habari wakongwe nchini waliowahi kufanya kazi na Marehemu William Lobulu (68) katika Shirika la Habari Tanzania (Shihata) katika miaka ya nyuma, wamemwelezea marehemu alikuwa mwandishi makini na mwenye kufaa katika idara yoyote katika chumba cha habari.Lobulu aliyeacha mke na watoto watatu na mjukuu mmoja alifariki dunia saa 12 asubuhi ya Oktoba 6 mwaka huu nyumbani kwake Sanawari wilayani Arumeru mkoani Arusha kwa maradhi ya Asthma {Pumu} na anatarajiwa kuzikwa kesho nyumbani kwake katika makaburi ya familia.Mwandishi mkongwe, Josephat Qorro amesema walipokuwa wakifanya kazi Shihata marehemu alikuwa mtu mkimya, mcheshi, makini na mwenye kuchapa kazi saa zote na alikuwa akifiti katika idara zote katika shirika hilo.Qorro alisema kifo chake kimemshitua na kueleza kuwa marehemu Lobulu alikuwa mwandishi mkongwe mwenye kujua wajibu wake alipokuwa kazini na baada ya kustaafu aliamua kuanzisha gazeti lake la Arusha Time Jijini Arusha lililokuwa na sifa kubwa sana kutoka na uhodari wake wa kujuwa kuandika na kuhariri habari.Alisema alikuwa akimfahamu vizuri marehemu Lobulu pamoja na mke wake Elizabert Malialle kwani wote walikuwa wafanyakazi wa Shihata miaka hiyo kabla ya kuona na kufunga ndoa na kupata watoto.Mwandishi mkongwe aliyewahi kufanya kazi Shirika la Magazeti ya Serikali (TSN), Danford Mpumilwa akimzungumzia marehemu Lobulu alisema kuwa alikuwa rafiki yake wa karibu sana toka walivyokuwa kidatu cha tano katika shule ya sekondari ya Mkwawa Mkoani Iringa wakati yeye akiwa kidatu cha nne katika shule hiyo.Mpumilwa baada ya kumaliza elimu ya sekondari na marehemu, alikwenda chuo kikuu cha UDSM mwaka 1973 na yeye alimfuata mwaka 1974 na baada ya kuhitimu chuo, marehemu aliajiri Shihata na katika nyakati za masomo na walikuwa wakishirikiana katika masomo hivyo walikuwa wakijuana vilivyo kwa undani zaidi.
3kitaifa
Na CHRISTIAN BWAYA HEMEDI anavuta zaidi ya pakiti moja ya sigara kwa siku. Ingawa mara kadhaa, amejaribu kuacha tabia hii asiyoipenda, bado hajafanikiwa. Nia ya kuacha sigara anayo lakini kuacha ameshindwa. Unaweza kufikiri Hemedi yuko tofauti na sisi wengine. Lakini ukweli ni kwamba nasi, kwa namna tofauti, tunakabiliwa na mitihani mikubwa ya kitabia, pengine kuliko huo alionao Hemedi.  Kuna mambo fulani kwenye maisha yetu tunatamani kuyaacha lakini hatuwezi. Inawezekana ni matumizi mabaya ya fedha; kuongea kupita kiasi; hasira ya kulipuka; kusengenya na tabia nyingine tusizosipenda. Kwa upande mwingine, tunaweza kutamani kujenga tabia mpya lakini tunashindwa. Nawafahamu watu wengi ambao kila mwaka mpya unapoanza wanajipanga kufikia malengo makubwa. Wanautazama mwaka mpya kwa mtazamo tofauti na wanatamani kuwa watu tofauti na walivyokuwa kwa mwaka uliomalizika. Wengine wanajiapiza kuanza kusoma vitabu; wengine kufanya mazoezi ya mwili; wengine kuanza kuweka akiba ya fedha; wengine kuamka mapema na kuwahi kazini; wengine kuwahi nyumbani na kutulia na watoto. Lakini siku chache baada ya kusherehekea mwaka mpya, tabia zile zile za zamani zinarejea. Wanarudi kulekule wasikokutaka. Mwaka huu rafiki yangu mmoja aliniambia anataka kupunguza uzito wa mwili. Hakupenda kuwa na kitambi. Juzi nilimwuliza amefikia wapi na lengo lake la kuanza kufanya mazoezi ya kukimbilia kila alfajiri mwaka huu. ‘Wiki ya kwanza nilienda vizuri. Nilijitahidi kuamka asubuhi na kukimbia. Baadae nilishindwa kuendelea kwa sababu ya maumivu ya viungo. Nilipopumzika, ndio mpaka leo.’ Alikuwa na orodha ndefu ya visingizio. Hayuko peke yake. Ukiwa mkweli wa nafsi yako, kuna vitu ungependa kuvifanya lakini huwezi kwa sababu tu umeshindwa kujenga tabia (mazoea) mapya. Kwa kawaida, kila malengo tunayoyaweka yanaenda sambamba na mazoea mapya. Huwezi, kwa mfano, kufikia lengo la kusoma angalau kitabu kimoja kwa wiki, kama huwezi kutunza muda wako. Ukishashindwa kutunza muda wako, lengo lako haliwezi kutimia. Kwa hiyo swali tunalohitaji kulijibu kwa uhakika ni kwamba, kwanini mara nyingi tunataka kujenga tabia mpya na hatuwezi? Kwanini tunashindwa kuacha tabia fulani fulani tusizozipenda? Shida ipo wapi? Kuna watu wanaofikiri sababu kubwa ni kukosa utashi –nia ya dhati ya kujenga au kuacha tabia fulani. Kwamba bila kumaanisha kuacha tabia fulani huwezi kuiacha hata kama huipendi. Hata hivyo, tunafahamu watu wengi, mfano wao, Hemedi niliyesimulia kisa chake hapo awali, wanaotaka kwa dhati kuacha tabia fulani lakini hawawezi. Watu hawa, nia ya dhati wanayo, madhara ya tabia zao wanayajua, lakini kuchukua hatua ya kuacha inakuwa vigumu. Wengine wanasema nia bila kuwa na uelewa wa madhara ya tabia husika ni vigumu kubadilika. Wanaoshikilia mtazamo kama huu wanafikiri kutangaza madhara ya tabia fulani ndio njia sahihi zaidi ya kuwashawishi watu kubadilika. Wanafikiri kinachohamasisha mabadiliko ni uelewa wa madhara. Niliwahi kuzungumza na mhamasishaji mmoja wa kampeni dhidi ya Ukimwi/VVU. Alikuwa akiwaelimisha wananchi kuhusu umuhimu wa kuwa mwaminifu na kufanya ngono salama ikiwa lazima. Kimsingi alionesha uelewa wa hali ya juu kuhusu hatari ya kuwa na wapenzi wengi na kufanya ngono zembe. Lakini nilipomfahamu baadae, nilibaini si tu alikuwa na foleni ndefu ya wapenzi, lakini alikuwa amezaa na wanawake kadhaa tofauti. Maana yake ni kwamba, pamoja na kuelewa hatari ya ngono isiyo salama, bwana huyu, alikuwa akifanya ngono isiyo salama. Kwahiyo, unaweza kuona kuwa uelewa pekee hautoshi kuacha tabia usiyoipenda kama ambavyo dhamira ya dhati nayo haitoshi. Hata katika kujenga tabia mpya, nia na uelewa pekee hautoshi. Tunafahamu kwa mfano, ni muhimu kuacha vyakula fulani fulani ili kulinda afya zetu. Tunafahamu umuhimu wa kufanya mazoezi ya mwili ili kujenga afya bora. Tunaweza kutaja faida za kutenga muda kwa ajili ya kusoma vitabu. Kwa nini, basi, hatuwezi kusimamia kile tunachotamani kukianza? Hili ndilo swali nitakaloanza nalo kwenye makala inayofuata panapo majaaliwa. ITAENDELEA
4afya
GAZA, PALESTINA         |        KUNDI la Hamas limetangaza kusitisha mapigano na Israel katika Ukanda wa Gaza, baada ya siku kadhaa za machafuko ambayo yalisababisha vifo vya mwanajeshi mmoja wa Israel na Wapalestina wanne. Msemaji wa Hamas, Fawzi Barhoum, amethibitisha uamuzi wa kundi hilo kupitia mtandao wa Twitter kuwa makubaliano na Israel yamefikiwa kwa msaada wa Serikali ya Misri na Umoja wa Mataifa. Kwa upande wake, Msemaji wa Jeshi la Ulinzi la Israel, Jonathan Conriczs, amesema hangeweza kuyajadili masuala ya kisiasa, lakini amethibitisha kuwa, Israel kwa sasa haifanyi mashambulizi yoyote katika ukanda wa Gaza. Conriczs amesema jeshi la nchi hiyo tangu juzi lilishambulia maeneo 60, yakiwamo makao makuu matatu ya wapiganaji wa Hamas. Awali Jeshi la Israel lilisema kuwa, mashambulizi yake ya angani yalilenga kujibu shambulizi la ufyatuaji risasi dhidi ya wanajeshi wake waliotumwa kusini mwa mpaka wa Gaza, ambako waandamanaji wa Kipalestina walikusanyika kwenye uzio. Wizara ya Afya ya Palestina imekiri kupokea miili ya Wapalestina wanne waliouawa na wanajeshi wa Israel kufuatia mapambano hayo. Kundi la Hamas, ambalo linadhibiti Ukanda wa Gaza, limesema watu watatu kati ya waliouawa walikuwa wanachama wao. Mjumbe wa Umoja wa Mataifa katika Mashariki ya Kati, Nickolay Mladenov, aliziomba pande zinazohusika kujizuia na kuwa watulivu. Vyombo vya habari vya Israel viliripoti kuwa, Misri ilitoa onyo la mwisho kwa Hamas kutoka kwa Israel, likisema kuwa, kama mashambulizi hayatasimama ifikapo wikiendi hii, itafanya mashambulizi mapya ya kijeshi katika ukanda wa pwani. Hamas na Israel walipigana vita vilivyodumu siku 50 katika mwaka wa 2014. Kwa jumla, Wapalestina 2,250 waliuawa au wakafariki baadaye kutokana na majeraha, wakati Waisrael 74 waliuawa katika mgogoro huo.
2kimataifa
SERIKALI imetangaza Juni Mosi, 2019 kuwa ni mwisho wa matumizi yote ya mifuko ya plastiki na hivyo, wananchi wanapaswa kuanza kutumia mifuko mbadala kubebea bidhaa.Kutokana na zuio hilo, wananchi hawataruhusiwa kufanya uzalishaji, uingizaji, usafirishaji nje ya nchi, usambazaji, uuzaji wala kufanya matumizi ya mifuko hiyo kwa namna yoyote. Watu wengi wamekuwa wakijiuliza mifuko gani watumie kubebea bidhaa baada ya hatua hiyo ya serikali ya kupiga marufuku mifuko ya plastiki maarufu kama mifuko ya rambo.Serikali kupitia Ofisi ya Makamu wa Rais, inawatoa hofu wananchi na kusema kuwa ipo mifuko mbadala wa ile ya plastiki ambayo inaweza kutumika kubebea bidhaa. Mifuko inayotajwa kuwa mbadala ni ile ya karatasi, nguo, vikapu na gunia ambayo ni rafiki kwa mazingira kwani inapoisha muda wake, huoza katika mazingira tofauti na ile ya plastiki iliyokatazwa.Pamoja na hayo, pia mifuko mbadala haina madhara kwa afya ya binadamu na mazingira kwani pindi imalizapo matumizi, huweza kuharibika kwa urahisi na kwa haraka inapochomwa. Unaweza kujiuliza wakati mifuko ya plastiki inazuiwa, je uhakika wa upatikanaji wa mifuko mbadala utakuwaje? Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira), January Makamba anawahakikishia wananchi upatikanaji wake utakuwa wa uhakika.Waziri Makamba anasema wapo wawekezaji ambao tayari wameonesha nia ya kuzalisha mifuko mbadala ya karatasi na kuwa hapa nchini zipo malighafi za kutosha. Uwezo na utayari wa uzalishaji wa mifuko mbadala ni wa kuridhisha na kuwa, vipo viwanda 25 vya karatasi hapa nchini sambamba na viwanda vinavyozalisha mifuko mbadala ya karatasi, ukili na nguo.Viwanda hivyo vinatarajiwa kuongeza kiwango cha uzalishaji katika muda mfupi kuanzia sasa hivyo, ku- saidia wananchi kupata nyenzo za kubebea bidhaa zao. Lipo kundi lingine la wawekezaji na wamiliki wa viwanda waliokuwa wanasubiri tamko la Serikali ili waweze kuwekeza mara moja katika uzalishaji wa mifuko mbadala.Kundi la tatu ni lile la viwanda ambavyo vinazalisha kwa ajili ya soko la nje zaidi ikiwemo kiwanda cha Mufindi Paper Mills (MPM) cha Iringa ambacho huzalisha malighafi za karatasi katika nchi za Kenya, Uganda, Rwanda na Zambia. Sambamba na hilo tayari wamiliki wa viwanda hivyo wameihakikishia Serikali kuzalisha kwa wingi malighafi za kutosheleza watengenezaji wa ndani wa mifuko ya karatasi.Serikali kupitia Ofisi ya Makamu wa Rais, imeendesha kikao cha wadau mbalimbali kujadili fursa za uwekezaji wa uzalishaji wa mbadala wa mifuko ya plastiki. Wakati huo huo, imeandaa mpango kazi wa utekelezaji wa katazo hilo kwa kutoa elimu kwa umma ili kuhakikisha wananchi wote wanapata taarifa sahihi na kwa wakati. “Wananchi wanahimizwa kuwekeza ili kuongeza kasi katika uzalishaji wa mifuko mbadala ili kwenda sambamba na dhamira ya Serikali ya Awamu ya Tano ya kujenga uchumi wa viwanda na wakati huo huo, kutoa huduma bora kwa wananchi,” ananukuliwa Waziri Makamba.Aidha, Serikali inatoa wito kwa wadau wote wakiwemo wawekezaji katika viwanda nchini kuzingatia umuhimu wa uchumi wa mbadala wa mifuko ya plastiki. Serikali inatoa mwito kwa wenye nia ya kuwekeza katika uzalishaji wa mifuko mbadala wa plastiki, wawasiliane na Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC), Baraza la Taifa la Usimamizi na Hifadhi ya Mazingira (NEMC), Shirika la Viwango Tanzania (TBS), Shirika la Maendeleo la Viwanda Vidogo (SIDO) na Taasisi za Fedha.Hatua hiyo itawezesha ajira nyingi zaidi na kukuza kipato kwa wananchi wa kawaida hasa wanawake katika kutengeneza mifuko mbadala ikiwemo kusuka vikapu ambako kunahitaji teknolojia rahisi na nguvu kazi. Katika kuhakikisha shehena ya mifuko ya plastiki inamalizika, utaratibu maalumu unafanywa kwa kila wilaya kutenga eneo maalumu la kuikusanyia na wananchi kutangaziwa maeneo hayo.
3kitaifa
NAIBU Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Dk Angeline Mabula amepiga marufuku wananchi wanaoshitakiana katika mabaraza ya ardhi, kutoa fedha kwa ajili ya kugharamia usafiri wa kwenda eneo lenye mgogoro.Alisema hayo wakati wa akizindua Baraza la Ardhi na Nyumba la Wilaya ya Ulanga mkoani Morogoro mwishoni mwa wiki.Dk Mabula alisema kutoa pesa ya kugharamia usafiri kwa mmoja wa wanaoshitakiana katika Mabaraza ya Ardhi kwenda eneo la tukio, kunaweza kuleta ushawishi kwa wajumbe wake, hasa kwa yule aliyetoa kiasi kikubwa cha pesa.Alisema ni lazima wakati wa kwenda eneo lenye mgogoro kwa wanaoshitakiana katika Mabaraza ya Ardhi, Mkurugenzi wa Halmashauri husika aratibu zoezi hilo huku ratiba nzima ikiwasilishwa kwa Mkuu wa Wilaya katika kipindi cha mwezi mmoja.‘’Jamaa anatoa shilingi laki mbili anayelalamika, hana kitu, unategemea hapo haki itatendekaje, ni marufuku kabisa na taratibu zote za kwenda barazani zipitie kwa DC na ratiba ijulikane mapema,’’ amesema Dk Mabula.Akizindua Baraza la Ardhi na Nyumba katika wilaya ya Ulanga, Naibu Waziri huyo alisema serikali imezindua baraza hilo ili kupeleka huduma karibu na kurahisisha usikilizaji kesi za ardhi kwa wananchi, ambao baadhi ya maeneo wamekuwa wakisafiri umbali mrefu kupata huduma hiyo.Amebainisha kuwa sasa wananchi wa Ulanga, watapata haki kwa wakati na kwa umbali mdogo.Amewaasa wananchi wa wilaya ya Ulanga, kulitumia vyema Baraza la Ardhi na Nyumba lililozinduliwa na wafuate taratibu zote za utatuzi wa migogoro ya ardhi na kuachana na migogoro ya kifamilia, kwa kutumia Mabaraza ya Vijiji na Kata kushughulikia migogoro hiyo.Msajili wa Mabaraza ya Ardhi na Nyumba nchini, Stela Tulo alisema uzinduzi wa Baraza la Ardhi katika Wilaya ya Ulanga, limejibu kiu ya muda mrefu ya wananchi wa wilaya hiyo kupata huduma karibu, ambapo huko nyuma walisafiri umbali mrefu hadi Kilombero kupata huduma.Kwa mujibu wa Stela, kuzinduliwa kwa Baraza la Ulanga sasa kunaufanya mkoa wa Morogoro kuwa na Mabaraza ya Ardhi na Nyumba Manne.Kwamba baraza hilo sasa linaongeza idadi ya mabaraza yanayofanya kazi nchini kufikia 54 kati ya 97 yaliyoidhinishwa
3kitaifa
Pambano hilo la raundi 12 litapigwa kwenye uwanja wa Kinesi Dar es Salaam ambapo Pazi atakuwa anautetea mkanda alioutwaa Februari baada ya kumchapa Mmalawi, Felix Mwamaso.Akizungumza na gazeti hili jana Pazi alisema anaendelea na mazoezi kwenye ‘Gym’ na tayari ameshamchunguza mpinzani wake na kujua ana jeraha hivyo, mapema atamaliza mchezo huo.“Najua Mwekyembe ni bondia mkongwe ila hanitishi zaidi nimejipanga kumkabili na nina uhakika wa asilimia 95 nitatetea mkanda wa Afrika Mashariki,” alisema.Alisema muhimu ni mashabiki wa mchezo huo kujitokeza na kuwaunga mkono kushuhudia bondia bora akimmaliza mpinzani wake mapema. Bondia huyo alisema anahitaji kushinda ili kuendelea kutengeneza rekodi bora na kuvutia mialiko mingi ya nje.Pazi anashika nafasi ya kwanza Tanzania kutokana na viwango vya ubora vya Boxrec huku akishika nafasi ya 140 duniani kati ya mabondia 1,351 kwa uzito wa Supermiddle Weight na mpinzani wake, Mwakyembe anashika nafasi ya pili Tanzania katika uzito wa Light Heavyweight na nafasi ya 263 duniani kati ya mabondia 1,105.Mbali na hao, wengine watakaopanda jukwaa moja ni Mfaume Mfaume atakayechuana dhidi ya Habibu Pengo ‘Bad Face’, mkongwe Mada Maugo akipambana dhidi ya Kanda Kabongo na Francis Miyeyusho dhidi ya mpinzani atakayetajwa baadaye.
5michezo
WATU wengi kwa kadiri ya uwezo wao hupenda kula mayai karibu kila siku, wakiamini ni mazuri kiafya hasa kile kiini cha kati. Ni kwa vile kwa miaka mingi wamehakikishiwa na wataalamu wa afya juu ya manufaa ya mayai mwilini. Wengi wanaofahamu umuhimu huo wa yai hupendelea kula angalau yai moja kila siku wakati wa kifungua kinywa na tafiti za nyuma zimeshauri hivyo. Miongoni mwa faida zinazoelezwa ni kwamba protini zilizoko ndani ya mayai hukufanya kutohisi njaa mapema. Ina maana kuwa ukila mayai unaweza kukaa muda marefu zaidi bila kula ikilinganishwa na mikate au vyakula vingine vya ngano. Kadhalika, inaelezwa kwamba ulaji wa mayai husaidia kupunguza uzito wa mwili. Baadhi ya tafiti zinasema watu wanaokula mayai wamefanikiwa kupunguza uzito wa miili yao kwa kiasi kikubwa ikilinganishwa na wasiokula. Kadhalika inaelezwa ukilinganisha na vyakula vingine vya protini kama vile nyama, mayai ni bei rahisi zaidi. Hivyo basi, mayai yanaweza kupatikana na kuandaliwa kwa urahisi wakati wa kifungua kinywa kuliko vyakula vingine. Lakini pia licha ya kwamba kuwa mayai yana kiwango fulani cha lehemu (cholesterol). Lakini utafiti uliofanyika huko nyuma ulibaini lehemu iliyoko katika mayai inapoliwa haina athari kwenye kiwango cha lehemu kwenye damu. Hivyo hakuna haja ya kuhofia juu ya magonjwa ya moyo yatokanayo na lehemu. Hali kadhalika tafiti za nyuma zilieleza kirutubisho kinachoitwa ‘Choline’ kinachopatikana kwenye mayai ni muhimu katika ukuaji na maendeleo ya ubongo. Pia kinahusishwa katika kuongeza uwezo wa ubongo wa kutunza kumbukumbu. Pia inaelezwa kuwa kemikali za leutin na zeaxanthin zinazopatikana kwenye mayai zinaaminika kulinda macho dhidi ya madhara ya mionzi mibaya. Pia inaaminika kuwa zinazuia kutokea kwa tatizo la mtoto wa jicho uzeeni. Lakini wataalamu wamekuwa na shaka kuhusu uhakika wa hayo baada ya kubaini kuwapo kwa visababishi vya maradhi ya moyo pamoja na vifo vya mapema katika yai iwapo yataliwa kwa wingi. Hivyo, kwa miaka kadhaa wataalamu wa afya wamekuwa wakiumiza kichwa iwapo ulaji wa mayai ni mzuri au mbaya kwa afya ya mwanadamu. Na hivyo, tafiti zimefanyika ukiwamo huu mkubwa uliofanyika hivi karibuni, ambao umehitimisha kwamba jibu la swali hilo linategemeana na kiwango cha mayai unayokula kwa wiki. Kwa mujibu wa utafiti mpya uliochapishwa kwenye jarida la Jumuiya ya Tiba Marekani (JAMA), kula mayai mawili tu kwa siku kunaweza kusababisha maradhi ya moyo na hata kifo cha mapema. Hilo linatokana na kiwango kikubwa cha lehemu kinachopatikana kwenye kiini cha yai, matokeo ambayo kama tulivyoona yanahitilafiana na tafiti za nyuma. Kwa mujibu wa Idara ya Kilimo ya Marekani yai kubwa moja lina hadi miligramu 300 za lehemu, kikiwa ni zaidi ya nusu ya kiwango cha lehemu, ambacho Shirika la Afya Duniani (WHO) linashauri mtu ale kwa siku miligramu 185. Utafiti wa JAMA ulichakata taarifa kutoka katika majaribio sita yaliyohusisha zaidi ya watu 30,000 katika kipindi cha miaka 17. Watafiti wamefikia hitimisho kuwa kula miligramu zaidi ya 300 za lehemu kwa siku kunaongeza hatari ya kupata maradhi ya moyo kwa asilimia 17 na vifo vya mapema kwa asilimia 18. Uwiano huo wa hatari huongezeka zaidi kwenye ulaji wa mayai na wanasayansi wamebaini kuwa kula mayai matatu au manne kwa siku kunaongeza hatari ya kupata maradhi ya moyo kwa asilimia sita na vifo vya mapema kwa asilimia nane. Kwa mujibu wa utafiti huo, madhara hayo ya mayai hayaathiriwi na umri, nguvu ya mwili, matumizi ya tumbaku na historia ya kuwa na shinikizo la damu. “Utafiti wetu umebaini kuwa endapo watu wawili watafuata aina moja ya mlo na tofauti pekee ikawa ni ulaji wa mayai, basi yule ambaye mwenye kula mayai mengi ana uwezekano mkubwa wa kupata magonjwa ya moyo kuliko yule asiyekula,” anasema Norrina Allen, Profesa Mshiriki wa Dawa za Kinga katika Chuo Kikuu cha Northwestern ambaye pia ameshiriki kuandika utafiti huo. Utafiti mpya unatofautiana na kazi za tafiti za awali, ambazo zilibaini kuwa hakuna uhusiano kati ya ulaji wa yai na uwezekano mkubwa wa kupata maradhi ya moyo. Lakini, Allen anasema kwamba kulikuwa na sampuli tofauti chache na zilikuwa na muda mfupi wa kufuatilia walaji wa mayai. Hata hivyo, watafiti wanakiri kuwa huenda kuna makosa katika uchunguzi wao. Data kuhusu ulaji wa yai zilikusanywa kwa njia ya maswali, ambapo ilibidi walioulizwa kukumbuka chakula chao katika kipindi cha miezi na miaka kadhaa. Watafiti wengine pia wanasema kuwa matokeo hayo ni ya kuchunguzwa zaidi na ingawa walieleza uhusiano kati ya ulaji wa yai na kuongezeka kwa hatari ya ugonjwa wa moyo na kifo cha mapema, hawawezi kuthibitisha sababu ya hali hiyo. “Umuhimu wa utafiti huu ni kwamba uliwakilisha jamii tofauti za watu wa Marekani na chakula kinacholiwa na Wamarekani wa kawaida,” anasema Tom Sanders, Profesa wa Masuala ya Lishe katika Taasisi ya King’s College mjini London. “Ukomo wake unategemea kipimo cha ulaji wa lishe moja,” alisema. Mwandishi mwenza wa utafiti huo, Allen anapendekeza kutokula mayai zaidi ya matatu kwa wiki. Pia anatoa ushauri kwa wanaopenda kula mayai, kula hasa sehemu nyeupe ya yai. “Siwaambii watu wayaondoe kabisa mayai kwenye mlo wao, bali ninapendekeza tu kwamba watu wayale kwa kiasi,” anasema. Kwa mujibu wa utafiti wa mwaka 2015 wa Tume ya Kimataifa ya Mayai (IEC), nchi zinazoongoza duniani kupenda kula mayai kwa kuzingatia kiwango cha mayai yaliyoliwa kwa mwaka ni: Mexico wastani wa mtu kula mayai ni 352 kwa mwaka, Malaysia 342, Japan 329, Urusi 285, Argentina 256, China 254.8, Marekani 252, Denmark 245. “Wastani wa kiwango cha cholesterol kinacholiwa na Wamarekani kinaweza kufikia karibu mayai 600, hiki kikiwa ni kiwango cha wastani wa juu kuliko kile kinacholiwa nchini Uingereza, ambacho ni miligramu 225 kwa siku,” Tom Sanders anaeleza. Katika takwimu za hivi karibuni kutoka IEC, kuanzia mwaka 2015, inaonyesha kuwa Marekani ni nchi ya tano kwa ulaji zaidi wa mayai duniani – huku kila mtu akila mayai 252 kwa mwaka. Lakini nchi hiyo ina matatizo ya moyo ambayo husababisha asilimia 20 ya vifo. Japan, ambako ulaji wa mayai unafikia kiwango cha mayai 328 kwa mtu, ilirekodi asilimia 11 pekee ya vifo. “Ulaji wa mayai walau matatu hadi manne kwa wiki ni sawa,” Wanasema wataalamu nchini Uingereza.
4afya
MIAMI, MAREKANI KLABU ya Manchester City imejaa hofu juu ya mshambuliaji wake mpya Riyad Mahrez, kuwa anaweza kuukosa mchezo wa Ngao ya Jamii ambao utapigwa Jumapili ijayo dhidi ya wapinzani wao Chelsea. Mchezo huo ni dalili ya kufunguliwa kwa pazia la Ligi Kuu nchini England, lakini Mahrez anaweza kuukosa kutokana na kupata majeruhi jana alfajili kwenye mchezo wao dhidi ya Bayern Munich. Mchezaji huyo ambaye amejiunga na Manchester City katika kipindi hiki cha majira ya joto akitokea Leicester City kwa uhamisho wa kitita cha pauni milioni 60, aliisaidia timu hiyo kuibuka na ushindi wa mabao 3-2, lakini alipata tatizo la enka. “Sijui atakuwa nje kwa muda gani, najua amepata tatizo la enka, lakini tutaona labda hakupata tatizo kubwa sana, kitu ambacho kinanipa wakati mgumu ni kuona mchezaji anaumia, huku wachezaji wengine wakiwa bado wapo kwenye mapumziko baada ya michuano ya Kombe la Dunia nchini Urusi. “Siwezi kuwalaumu wachezaji ambao bado hawajawasili, lakini ninafurahia kile walichokifanya kwenye michuano hiyo ya Kombe la Dunia. Mahrez anaweza kuukosa mchezo wa Ngao ya Jamii dhidi ya Chelsea, lakini ninaamini tuna kikosi kipana kuweza kuziba nafasi hiyo,” alisema Guardiola. Hata hivyo kocha huyo alieleza sababu ya kumuacha benchi mshambuliaji wake wa pembeni Leroy Sane baada ya kucheza katika mchezo wa kwanza dhidi ya Liverpool. “Sane bado hayupo sawa kiakili, hivyo anatakiwa kufanya mazoezi taratibu ili kuweza kurudi katika ubora wake, lakini wala hana majeruhi yoyote kama watu wanavyodhani,” aliongeza
5michezo
NA GLORY MLAY MKALI wa muziki wa Bongo Fleva aliyewahi kunyakua tuzo 5 za Kili, Abas Kinzasa ‘20 Percent’, anatarajiwa kuibuka upya na wimbo wa ‘Mbaya hana Sababu’. Wimbo huo kwa sasa anaendelea kukamilisha video yake anayoamini itakamilika kabla ya mwishoni mwa mwezi huu. Hata hivyo, licha ya ukimya wake, 20 Percent anadai kwamba muziki wake si wa kushindana na msanii mwingine yeyote, ndiyo maana mwenendo wake katika muziki huo ni wa taratibu. “Mimi sishindani na mtu katika muziki wangu, nafanya muziki wangu ninavyojisikia, moyo ukitaka naingia studio natoa, lakini nyimbo zangu zote nina hakika zitazoa mashabiki kwa kuwa ujumbe wangu ni wa kueleweka na upo tofauti na wasanii wengine,’’ alijinadi. Msanii huyo aliongeza kwamba, wimbo wake mwingine wa ‘Mapenzi Sina’ alioukamilisha ‘audio’ yake pia anataraji kuufanyia video yake hivi karibuni. “Mimi sijapotea, ninarudi na nyimbo hizo na nimeshatoa huo wimbo wa ‘Mapenzi Sina’ ambao nao nakamilisha video yake, lakini kwa sasa sina studio maalumu, narekodi studio yoyote inayoweza kufanya muziki wa aina yangu,’’ alieleza 20 Percent.
0burudani
Kocha wa zamani wa Yanga, Mzambia, George Lwandamina amefunguka kuwa anakuja Tanzania kwa kazi moja tu ya kuhakikisha anaifunga timu hiyo katika mchezo wa hatua ya kwanza ya Ligi ya Mabigwa Afrika. Lwandamina ambaye kwa sasa amerejea kwenye timu yake ya zamani, Zesco United, baada ya kuachana na Yanga msimu uliopita kabla ya kutua Mwinyi Zahera raia wa DR Congo. Mzambia huyo anatarajia kukutana na timu yake hiyo ya zamani katika mchezo wa hatua ya kwanza ya Ligi ya Mabingwa Afrika utakaopigwa kati ya Septemba 13-15, mwaka huu kwenye Uwanja wa Taifa Dar kabla ya mchezo wa marudiano utakaopigwa Septemba 27, mwaka huu nchini Zambia. Lwandamina anakutana na Yanga kwenye hatua hiyo baada ya kuwaondoa Green Mamba huku Yanga ikiwaondoa mabingwa wa Ligi Kuu ya Botswana, Township Rollers. Lwandamina alisema kuwa anakuja nchini kwa kazi moja tu ya kuhakikisha anaifunga Yanga katika mchezo wa hatua ya kwanza kabla ya mchezo wa marudiano utakaonfanyika kwao Zambia. “Unajua timu yeyote kwenye michuano hii inahitaji ushindi ili iweze kusonga mbele na ndivyo ilivyo kwetu, ninakuja Tanzania kwa mara nyingine lakini kwa sasa ninakuja kwa ajili ya kazi moja tu ya kuhakikisha ninaifunga Yanga. “Yanga ni timu nzuri na kwa sasa ina wachezaji wengi wageni ambao sikuwahi kuwafundisha, pia huwezi kuwalinganisha wachezaji hao wapya na wachezaji ambao walikuwepo wakati niko Yanga kwa sababu wana tofauti kubwa, lakini kama nilivyosema awali kwamba waambie Watanzania, Lwandamina anakuja kuifunga Yanga,” alisema Lwandamina.
5michezo
WAJAWAZITO wanaojifungulia nyumbani ni changamoto kubwa mkoani Rukwa huku wengi wao wakihusishwa na matumizi yasiyokubalika ya dawa za miti shamba kupunguza maumivu ya uchungu au kuongeza.Hata hivyo, mbali na chamgamoto hizo, imebainika kuwa baadhi ya vijiji wanavyoishi havina zahanati huku umbali wa kufuata huduma kwenye vituo vya afya ukiwa kikwazo, hivyo wengi hukata tamaa na kuamua kujifungulia nyumbani. Hayo yalibainishwa hivi karibuni na Mganga Mkuu wa Mkoa wa Rukwa, Dk Boniface Kasululu wakati akiwasilisha taarifa ya huduma ya afya na hali ya vifo vya wajawazito vinavyotokana na uzazi na vifo vya watoto wachanga kwenye kikao cha wadau. Dk Kasululu alisema asilimia 99 ya wanaojifungulia nyumbani hufanya hivyo kwa kuamini ushirikina iwapo wataenda hospitalini.Uchunguzi uliofanywa na gazeti hili kwa muda sasa umebaini baadhi ya wajawazito wanaojifungulia nyumbani wanatumia dawa za miti shamba kupunguza maumivu ya uchungu au kuongeza uchungu wa uzazi kabla ya kujifungua. Lakini pia hawa wanaojifungulia katika hospitali za umma kwa siri wanatumia dawa hizo ambapo baadhi wanatumia kwa kuweka kwenye uji au chai kwa siri bila madaktari kujua.Akizungumzia hilo, Dk Emanuel Mtika ambaye mara kadhaa amekuwa pia Kaimu Mganga Mkuu wa mkoani humo, alikiri kuwa baadhi ya wajawazito hutumia dawa za miti shamba kupunguza maumivu ya uchungu kabla ya kujifungua na kwamba jambo hilo bado ni changamoto kubwa mkoani humo. Ili kukabiliana na changamoto hiyo utawala wa hospitali hiyo umepiga marufuku ndugu wa wajawazito waliolazwa hopitalini hapa wakisubiri kujifungua wasiwaletee chai kutoka nyumbani.Alizitaja athari za kiafya zinazosababishwa na matumizi ya dawa hizo za miti shamba kwamba ni pamoja na kuharibika kwa mimba, kupasuka kwa mfuko wa uzazi na kutokwa kwa damu nyingi pia vifo. Aliwaasa wajawazito wote kuhakikisha wanajifungulia kwenye vituo vya afya kwa kuwa wana uwezo wa kugundua tatizo la mjamzito na kulitibu badala ya kusubiria kujifungulia nyumbani ambako hakuna mtaalamu wa tiba aliyesomea. Hata hivyo, mkoa wa Rukwa bado unakabiliwa na uhaba wa zanahati ambapo vijiji 139 hazina zanahati.
3kitaifa
WIZARA ya Fedha na Mipango imetoa orodha ya kwanza ya wadaiwa sugu wafanyabiashara 15 walionufaika na Mpango wa Kusaidia Uingizwaji wa Bidhaa nchini (CIS) na FACF, wafanyabiashara Mohamed Dewji na Yusuf Manji ni kati ya wadaiwa hao.Kwa mujibu wa taarifa kwa vyombo vya habari iliyotolewa jana na wizara hiyo, imewataka wadaiwa hao kulipa madeni yao haraka iwezekanavyo kabla hatua za kisheria kuchukuliwa. Watu wengine mashuhuri waliopo kwenye orodha hiyo ni pamoja na mwanasiasa aliyekuwa Waziri kwenye utawala uliopita, Stephen Wassira kupitia kampuni yake ya Siza Cold Storage Co. Ltd pia mwanasiasa Hashim Rungwe kupitia kampuni yake ya Bahari Motor Co. Ltd.Ikizungumzia madeni hayo, taarifa hiyo ilifafanua kuwa yanatokana na mkopo wa masharti nafuu kwa Taasisi, Kampuni, Viwanda na Wafanyabiashara ambapo wakopaji walitakiwa kulipa deni husika bila ya kutozwa riba katika kipindi cha miezi 18 tangu muda waliopewa mikopo hiyo.Ilinukuu kifungu cha sheria cha CIS ya mwaka 2008 (1)(b), inayosema kuwa mkopaji akichelewa kulipa katika kipindi cha miezi 18 tangu kupatiwa mkopo, atapaswa kulipa riba ya asilimia sawa na kiwango kinachotozwa na Benki Kuu ya Tanzania (BoT) inapoikopesha serikali katika kipindi husika. Ilielezea kuwa zaidi ya kampuni 980 zimekopeshwa chini ya utaratibu huo ambapo tangazo hilo lililotolewa jana lilikuwa ni la mara ya mwisho kwa kuwa imeshatangaza mara kwa mara na wadaiwa wameshindwa kuitikia mwito.Ilisema matangazo yalitolewa mnamo Desemba 30 mwaka 2015 na Aprili 4 mwaka jana, lakini hakuna jitihada za ulipaji wa madeni hayo zilizofanyika. Ilielezea kuwa wadaiwa ambao majina yao yametajwa jana kwa hiyo mara ya mwisho wakishindwa kujitokeza na kulipa hatua za kisheria zitachukuliwa. Kwa upande wa mfanyabiashara Mohamed Dewji anadaiwa kupitia kampuni zake za 21st Century Textiles na Afritex Ltd huku Manji akidaiwa kupitia kampuni zake za Farm Equipment Tanzania Ltd, Quality Group Ltd, Dunhill Motors Ltd, Quality Seed Ltd, Quality Garage Ltd.
3kitaifa
MAKAMU wa Rais, Samia Suluhu Hassan amesema Tanzania imetaifi sha mali zenye thamani ya zaidi ya Sh bilioni 93.16 sawa na Dola za Marekani milioni 41 zilizotokana na uhalifu.Mali zilizotaifishwa ni madini, nyumba, magari, fedha za upatu, mbao na maliasili kwa kipindi cha mwaka 2013 hadi 2019 zilizotokana na uhalifu wa kupangwa, utakatishaji fedha, kughushi na wanyamapori.Akifungua Maadhimisho ya Miaka 10 ya Umoja wa Taasisi zinazokabiliana na Uhalifu kwa nchi za kusini mwa Jangwa la Sahara (ARINSA), jana jijini Dar es Salaam, Samia alisema miongoni mwa mali walizotaifisha ni madini yenye thamani ya Sh bilioni 32.Samia alisema mafanikio yaliyopatikana yametokana na marekebisho makubwa katika sheria za nchi, ikiwemo Sheria ya Utakatishaji wa Mali zinazotokana na Uhalifu na Sheria ya Kuzuia Utakatishaji wa Fedha Haramu ili kuhakikisha zinakuwa na ufanisi unaotakiwa katika kupambana na mbinu mpya za kihalifu hasa unaovuka mipaka.Alieleza kuwa pamoja na kuwepo wapelelezi na waendesha mashitaka wachache waliopata mafunzo kupitia umoja huo, wamechangia kutaifishwa kwa mali hizo. Alisema hatua ya kutaifisha mali imerudisha heshima kwa kuhakikisha kuwa maliasili za Tanzania zinawanufaisha Watanzania na ni matokeo ya ARINSA inayohakikisha malengo yanafikiwa.“Niwahakikishie tutaendelea kuunga mkono kwa dhati juhudi za nchi wanachama wa umoja huu katika kufikia malengo yake ili kuhakikisha kuwa nchi za ukanda huu zinakuwa salama kwa maendeleo ya kiuchumi na kijamii kwa wananchi wake,” alisema Samia.Aliongeza kuwa umoja huo umetanua wigo wa ushirikiano katika masuala ya upelelezi na kurahisisha upatikanaji wa taarifa muhimu za kiupelelezi zinazosaidia kuharakisha kukamilika kwa maombi ya ushahidi nje ya nchi na upatikanaji wa mali zinazohusiana na uhalifu. Samia alisema makosa mengi ya kupangwa na mbinu za utendekaji wake wa kisasa kutokana na kukua kwa sayansi na teknolojia hususani Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (Tehama).Pia alisema kupitia programu za wapelelezi na waendesha mashitaka wameweza kujengewa uwezo kwenye makosa ya kifedha, wanyamapori na misitu na ufadhili wa ugaidi, ikiwa ni pamoja na kufuatilia mali walizozipata wahalifu au kuzitumia kutenda uhalifu ili kuzitaifisha. “Nimeambiwa kuwa mkaa nao unachangia uhalifu kwani wapo baadhi ya watu wanauza mkaa nje ya nchi na kufadhili uhalifu.Kama msimamizi wa mazingira, tutahakikisha kuwa miti haikatwi kwa mkaa,” alifafanua. Alisema nchi wanachama zimefaidika kupitia programu za mafunzo kwa kurekebisha sheria mbalimbali zilizokuwepo au kutunga sheria mpya ili kurahisisha utaifishaji na urejeshaji wa mali zinazohusiana na uhalifu na kuhakikisha nchi zinaendelea kuwa salama.Aidha, alizitaka nchi wanachama kuhakikisha kuwa kila mali inayotaifishwa kwenye nchi yao, asilimia kidogo ya fedha inayopatikana inaingia kwenye Ofisi ya Mwendesha Mashitaka na kupelekwa ARINSA ili iweze kujitegemea na kuendeleza nchi mbalimbali za Afrika.Kwa upande wake, Rais wa ARINSA, Biswalo Mganga alisema kuwa kuanzia mwaka 2013 hadi 2019 umoja huo umeweza kutaifisha mali zenye thamani ya Dola za Marekani bilioni 1.406. Mganga ambaye ni Mkurugenzi wa Mashitaka nchini (DPP), alisema mwaka huu pekee mali zilizotaifishwa ni Dola za Maarekani milioni 700 na kwamba mali zinazoshikiliwa zinathamani ya dola za Marekani 594.23 na maombi ya kutaifisha mali ni 142.Alisema changamoto wanazokabiliana nazo ni kupoteza thamani ya mali zinazokamatwa na kukaa muda mrefu kwenye vituo vya polisi na baadhi zinaharibiwa na wahalifu wenyewe. Naye, Waziri wa Katiba na Sheria, Balozi Dk Augustine Mahiga alisema ushirikiano wa kiuchumi, kisiasa na kijamii hauwezi kutimia endapo hakuna amani kwa watu na mali zao kwenye nchi wanachama. Aliwataka wawakilishi kutoka nchi 16 za ARINSA kutembelea vivutio mbalimbali vilivyopo nchini ili kujifunza na kufurahia uwepo wao hapa nchini.
3kitaifa
KATIKA kuboresha huduma za maji, Benki ya Dunia (WB) imeipa Halmashauri ya Wilaya ya Kibaha Sh milioni 77 ikiwa ni malipo ya miradi ya ufanisi.Hayo yalisemwa na Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Kibaha, Rebman Ganshonga wakati wa kikao cha baraza la Madiwani kupitia taarifa za Kata. Alisema kuwa kwenye bajeti iliyopita Halmashauri ilipokea Sh milioni 33 ikiwa sehemu ya mradi wa malipo ya ufanisi katika miradi ya maji na kuongeza kuwa fedha hizo zimelenga katika kufungua vituo vipya vya kutoa huduma ya maji katika Kata ya Dutumi, Kikongo na katika kata nyingine za halmashauri ya wilaya ya Kibaha vijijini.“Tumefanya vizuri katika miradi ya malipo kwa ufanisi ndiyo sababu ya kuongezewa fedha ambazo zitasaidi uboreshaji huduma za maji,”alisema Ganshonga. Alisema licha ya baadhi ya changamoto za huduma za maji, halmashauri imejipanga kuhakikisha wananchi wanapata maji safi na salama.Diwani wa Kata ya Dutumi, Mkali Kanusu alisema Kata yake imepokea Sh milioni 13 kwa ya malipo ya ufanisi na kwamba wamezitumia fedha hizo katika uboreshaji miundombinu ya maji. Kanusu alisema wamekuwa wakipata changamoto kubwa ya maji ikifika katika msimu wa kiangazi kutokana na kupungua kwa kina cha maji katika chanzo wanachokitegemea kwenye Mto Ruvu.Alisema wanaipongeza Benki ya Dunia kwa kuwapatia fedha hizo kwani itawasaidia kukabili changamoto ya maji. “Lengo ni kuhakikisha maji yanapatikana kwa uhakika na wananchi wanaondokana na adha hiyo,”alisema Kanusu.
3kitaifa
Na RAMADHAN HASSAN-DODOMA MWENYEKITI wa Tume ya Uchaguzi (NEC), Jaji Mstaafu, Semistocles Kaijage, amewataka wasimamizi wa uchaguzi kuhakikisha wanazingatia maadili na kuepuka dosari ambazo zinaweza kuathiri Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 28, huku akisema wapiga kura walio kwenye daftari ni milioni 29. Akifungua kikao kazi cha wasimamizi wa uchaguzi jijini Dodoma juzi, aliwataka kuzingatia sheria, maadili ya uchaguzi na maelekezo ya tume na watakaokiuka watakuwa wametenda kosa la jina kwa mujibu wa kifungu 98 cha Sheria ya Uchaguzi. Pia alisema pamoja na wajibu wao wa kusimamia uchaguzi, wanatakiwa kujua jiografia, mazingia na maeneo wanayosimamia na wana wajibu wa kusimamia watendaji wa uchaguzi waliopo chini yao ili watekeleze majukumu yao kwa weledi na umakini. “Wasimamizi wa uchaguzi hii ni nafasi ya kubadilishana na kupeana uzoefu wa utekelezaji shughuli za uchaguzi ili kuhakikisha tunaepusha dosari ambazo zinaweza kujitokeza na kuathiri shughuli za uchaguzi,” alisema Kaijage. Kaijage alisema tume ilianza kujiandaa kwa uchaguzi huo siku nyingi kwa kufanya shughuli nyingi zikiwemo za kukamilisha uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapigakura ambao umefanyika mara mbili. Awamu ya kwanza ilifanyika Julai 18, 2019 hadi Februari 23, 2020 na awamu ya pili Aprili 17 hadi Mei 04, 2020. “Awamu ya pili ya uboreshaji ilifanyika pamoja na uwekezaji wazi wa daftari la awamu ya kwanza katika vituo 37,814 vilivyotumika katika uboreshaji awamu ya kwanza,” alisema. Kaijage alisema uwekaji wazi wa daftari awamu ya pili ulifanyika Juni 17-20, mwaka huu ambapo daftari la wapigakura lilibandikwa katika vituo vyote vilivyotumika wakati wa uandikishaji awamu ya kwanza. Kaijage alisema katika uboreshaji wa daftari hilo awamu zote mbili, waliandikisha wapigakura wapya 7,326,552 sawa na asilimia 31.63 ya wapigakura 23,161,440 walioandikishwa mwaka 2015. Aidha, wapiga kura 3,548,846 walioboreshewa taarifa zao na wapigakura 30,487 waliondolewa kwenye daftari kwa kukosa sifa na hivyo daftari lina wapigakura takaribani milioni 29. Kaijange aliwataka wasimamizi hao kuwa makini na matumizi ya fedha zinazotumwa kwao kwa kuzingatia sheria za fedha za umma, ya manunuzi ya umma, ya uchaguzi na maelekezo yanayotolewa na tume wakati wa matumizi ya fedha hizo ambazo awamu ya kwanza zimeshatumwa. Alisema katika uchaguzi wa mwaka huu, hakuna marekebisho ya sheria za uchaguzi, lakini tume imefanya marekebisho kanuni za uchaguzi wa rais na wabunge na kanuni za uchaguzi wa serikali za mtaa zote za mwaka huu na maboresho ya maelekezo kwa ajili ya wadau na watendaji yamekamilika. Kaijage alisema tume kwa kushirikiana na Serikali na vyama vya siasa iliandaa maadili ya Uchaguzi Mkuu wa mwaka huu ambayo yalisainiwa Mei 27, 2020 yameainisha mambo yanayotakiwa kuzingatiwa na tume, vyama na serikali. Hivyo wasimamizi wa uchaguzi ambao watakuwa wenyeviti wa kamati za maadili katika majimbo wanayosimamia, wayasome na kuyaelewa vizuri ili kuyasimamia vizuri. Kaijage alisema kanuni zilizorekebishwa zinaelekeza uteuzi wa wagombea, upigaji kura na mchakato mzima wa uchaguzi na hivyo watendaji wa tume wanatakiwa wakato wote kuwepo katika maeneo ya kazi, kwani uzoefu unaonesha  wamekuwa wakikiuka maadili kwa kutokaa vitutoni na hivyo kusababisha malalamiko. Tume imeshanunua baadhi ya vifaa vya uchaguzi pamoja na kuchapisha fomu, sheria za uchaguzi, kanuni na maelekezo na baadhi vimeshaanza kupokelewa bohari kuu ya tume, hivyo vikisambazwa kwao wasimamizi mnatakiwa kuvipokea, kuvihifadhi katika hali ya usalama. Tayari tume imeshatoa vibali 97 kwa ajili ya watazamajini wa uchaguzi mkuu wa ndani na tayari imewasilisha mwaliko kwa wizara ya mambo ya nje na ushirikiano wa Afrika mashariki kuruhusu watazamaji wa kimataifa kuja nchini kuangalia uchaguzi huo. Pia Tume imetoa vibali kwa asali 245 Tanzania Bara na asasi saba za kiraia Zanzibar kwa ajili ya kutoa elimu kwa wapigakura wakati wa uchaguzi, hivyo wasimamizi wanatakiwa kuhakikisha elimu inayotolewa katika maeneo yao inazingatia mwongozo wa utoaji elimu uliotolewa na tume. Pia aliwataka wasimamizi hao kuhakikisha mawakala wa vyama wanaruhusiwa kuwepo vituoni, kwani kitendo hicho kioongeza uwazi lakini watakuwa na vitambulisho vinavyotambulisha. Alisema kwa mujibu wa sheria ya uchaguzi mawakala wa vyama vya siasa wataruhusiwa kuwepo vituoni jambo ambalo linasahdia kudhihirisha uwazi katika uchaguzi huo, ni wajibu wao kuhakikisha wanakuwa na vitambulisho na wakati wakiangalia utekelezwaji wa sheria, kanuni na taratibu za uchaguzi. Katika kufanikisha uchaguzi huo tume imeteua watendaji wake wakiwemo waratibu 28,  wasimamizi wa uchaguzi 194, wasimamizi wasaidizi wa majimbo 742 na wasimamizi wasaizidi katika kata 7,912.
3kitaifa
BRAZIL, nchi inayoshika nafasi ya nne kwa uzalishaji wa pamba duniani, imedhamiria kusaidia kuliinua zao hilo Ukanda wa Afrika Mashariki ili liweze kuwa na tija kwa wakulima wake.Kwa kuanzia, imeelekeza nguvu katika nchi za Tanzania, Kenya na Burundi ambako imewekeza fedha na teknolojia katika `Mradi wa Pamba Victoria’ na nchi ya Brazil kwa zaidi ya dola za Marekani milioni 9 (Sh bilioni 21 za Kitanzania).“Tupo hapa kuitumia teknolojia inayotumika Brazil katika uzalishaji wa pamba, lakini sasa katika ardhi na mazingira ya Tanzania na Afrika Mashariki,” alisema Balozi wa Brazil nchini Tanzania, Antonio Cesar wakati wa mkutano wa kutathimini mafanikio na changamoto katika sekta ya pamba. Balozi Cesar alisema mradi huo ulizinduliwa mwaka 2016 na kuanza rasmi mwaka 2017.Katika kikao hicho cha tathmini, Naibu Waziri wa Kilimo, Innocent Bashungwa alikuwepo na kusisitiza kuwa, Tanzania licha ya kuwa moja ya nchi zinazozalisha pamba kwa wingi barani Afrika, ina uhaba wa viwanda vya kusindika zao hilo, jambo linalochangia kuyumbisha soko la wakulima. Alisema pamba inalimwa katika mikoa 17 na wilaya 56, lakini uzalishaji si mzuri sana kutokana na kukosekana zana na mbinu za kisasa za kilimo hicho.Aidha, kupitia mpango huo ulioletwa na Wabrazili, alisema lengo ni kuzalisha mara tatu zaidi ya sasa kwa kila hekta, kwani Tanzania hekta moja huzalisha kilo 300 ikilinganishwa na kilo 4,200 zinazovunwa Brazil kwa kila hekta. Kaimu Mkurugenzi wa Bodi ya Pamba Tanzania, alisema Brazil imeanzisha mradi huo katika Afrika Mashariki baada ya nchi hizo kulalamika katika Shirika la Biashara Duniani (WTO) kuwa nchi za Marekani Kusini zimekuwa zikiweka vikwazo vya kibiashara nchi nyingine zinazolima zao hilo. Naye mtafiti kutoka Taasisi ya Utafiti wa Kilimo Tanzania (TARI), Everina Lukonge, alisema wadau kadhaa wa Tanzania wameshapelekwa Brazil kujifunza zaidi juu ya kilimo cha kisasa cha pamba, lengo likiwa kukuza uzalishaji nchini.
3kitaifa
MABINGWA wa Ligi Kuu nchini, Simba wanatarajiwa kucheza mechi maalumu ya kirafi ki dhidi ya Sevilla ya Hispania Mei 23 mwaka huu.Awali waandaaji wa mechi hiyo kampuni ya SportPesa walikuwa kwenye kigugumizi cha nani acheze na Sevilla kati ya Simba na Yanga lakini jana Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) kupitia kwa katibu wake mkuu, Kidao Wilfred walikata mzizi wa fitina na kuitangaza Simba kupata nafasi hiyo kwa vigezo walivyoweka. Kidao aliwaambia waandishi wa habari kuwa timu iliyofanya vizuri kwenye michuano ya SportPesa iliyofanyika nchini ndiyo itakayopata nafasi hiyo na hivyo wameiteua Simba kwa vile ilifika nusu fainali.“Timu ya Tanzania ambayo ilifanya vizuri katika mashindano ya Sportpesa yaliyopita ni Simba na ilifika nusu fainali hivyo ni rasmi sasa Simba itacheza na Sevilla ni jambo la kujivunia,” alisema Kidao. Awali Sportpesa ikishirikiana na serikali ilipeleka ombi kwa bodi ya ligi ya Tanzania kuomba nafasi ya kuandaa mechi ya Simba na Yanga ili mshindi wa mchezo huo acheze na Sevilla lakini ilishindika na ndipo ilipokabidhi jukumu hilo kwa TFF.Pia klabu hizo zimegomea kuunda timu ya kombaini ambayo itacheza na Sevilla baada ya nafasi ya kuandaa mechi kukosekana. Mbali na kuishia nusu fainali kwenye michuano ya SportPesa iliyoshirikisha pia timu kutoka Kenya, Simba pia imekuwa na msimu mzuri kwenye michuano ya kimataifa baada ya kucheza robo fainali ya Ligi ya Mabingwa na kung’olewa na TP Mazembe ya Congo DR. Msemaji wa Simba, Haji Manara alisema jana ni heshima kubwa kwao kucheza dhidi ya Sevilla iliyowahi kuwa bingwa wa Europa kwa misimu mitatu mfululizo.
5michezo
RAIS John Magufuli, anatarajiwa kuwa mgeni rasmi kwenye tamasha la Mwezi wa Urithi litakalozinduliwa kitaifa katika Uwanja wa Jamhuri jijini Dodoma Septemba 15, mwaka huu. Akizungumza na waandishi wa habari Dodoma jana, Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Japhet Hasunga alisema lengo la tamasha hilo ni kuenzi, kudumisha, kuburudisha na kujifunza masuala muhimu yanayohusu urithi wa mtanzania hususani utamaduni, historia, malikale na maliasili.Aidha, alisema kwa kutambua hazina kubwa ya malikale na utamaduni wa makabila zaidi ya 128 yaliyopo nchini, tamasha hilo litaongeza wigo wa mazao ya utalii kwa kukuza utalii wa utamaduni wa malikale hatua itakayongeza ushindani wa Tanzania kama kituo bora cha utalii kwenye masoko mbalimbali duniani. Alisema kuwa Urithi Festival itasadia kukuza utalii wa ndani kwa kuongeza muda wa watalii wa kimataifa kukaa nchini kwa vile tamasha hilo lifanyika katika kipindi ambacho watalii wengi wanatembelea Tanzania.Naibu Waziri huyo alisema kutokana na watalii kuongeza muda wa kukaa nchini kutaleta faida kwa wananchi na uchumi wa nchi kwa ujumla Aidha, Naibu Waziri huyo alitaja mikoa sita pamoja na tarehe ambayo tamasha hilo litafanyika ikiwemo Dodoma litakalofanyika kuanzia Septemba 15 hadi mwaka huu. Maeneo mengine ni Zanzibar litafanyika Septemba 23 hadi 29, Dar es Salaam na Mwanza tamasha hilo litafanyika Septemba 29 hadi Oktoba 6 na Arusha litafanyika kuanzia Oktoba 8 hadi 13, mwaka huu.Alisema tamasha hilo litakuwa na shughuli mbalimbali kama vile sherehe za uzinduzi na kilele, kuenzi lugha adhimu ya Kiswahili na kutoa tuzo kwa wasanii na wadau wa Urithi. Alifafanua kuwa tamasha hilo litapambwa na shamrashamra za carnival ya mirindimo ya urithi, burudani za ngoma za asili, muziki na kwaya pamoja na sanaa na maonesho ya bidhaa ya wadau. Katika hatua nyingine, Naibu Waziri huyo alisema kuwa tamasha hilo litahusisha makongamano ya wataalamu, usiku wa urithi, ziara ya kutembelea vivutio vya utalii pamoja na kunadi urithi katika mitandao ya kijamii na vyombo vya habari kupitia kaulimbiu ya Mvalishe, Misosi ya Kwetu na Michongo ya Urithi. Tamasha la Urithi litakuwa linafanyika kila mwezi Septemba ya kila mwaka kuanzia mwaka huu.
3kitaifa
Mahakama Kuu nchini Kenya imemruhusu mgombea urais kupitia chama cha Thirdway Alliance, Ekuru Aukot, aliyekuwa ameshiriki uchaguzi mkuu tarehe 8 Agosti ashirikishwe kwenye uchaguzi mkuu mpya utakaofanyika tarehe 26 Oktoba. Hapo awali, Tume ya Taifa ya Uchaguzi ya Kenya (IEBC) ilitangaza kuwa ni wagombea wawili pekee ambao ni Rais Uhuru Kenyatta wa chama cha Jubilee na Raila Odinga wa Muungano wa National Super Alliance (NASA) wangewania kwenye uchaguzi huo. Hata hivyo, Raila Odinga alijiondoa kwenye uchaguzi huo siku ya Jumanne. Kwa upande wake, Dkt Aukot amesema amefurahia uamuzi huo na kwamba sasa watakuwa kwenye uchaguzi kwani Mwenyekiti wa IEBC, Wafula Chebukati alijaribu kuwafungia nje. Ameongeza kuwa chama chake bado kina mambo ambayo kilitaka yashughulikiwe na tume hiyo ya uchaguzi tangu mwezi Agosti na bado hayajashughulikiwa. Lakini pia amesema chama chake kitatoa maelezo ya kina kuhusu msimamo wao ndani siku mbili baada ya mashauriano zaidi. Maafisa wakuu wa IEBC walikutana jana kutafakari kuhusu hatua za kuchukua baada ya hatua ya Odinga japo mpaka sasa bado hawajatoa tamko. Pamoja na mambo mengine, kujumuishwa kwa mgombea huyo kuna maana kwamba IEBC haiwezi kumtangaza Uhuru Kenyatta kuwa mshindi wa moja kwa moja hata baada ya kujiondoa kwa Raila Odinga.
2kimataifa
BENKI ya Maendeleo ya Afrika (AfDB) imeridhia kutoa Euro milioni 235 sawa na shilingi za Kenya bilioni 27.4 kwa ajili ya kugharamia ujenzi wa bwawa la umeme la Thwake lililopo katika mto wa Thwake kusini mwa Kenya.Mradi huo ambao ni mkubwa nchini Kenya kugharamiwa na benki hiyo, unajumuisha pia mradi wa kusambaza maji katika Kaunti ya Makueni na katika maeneo yanayozunguka mradi huo, ikiwa ni pamoja na Mji wa Teknolojia wa Konza. Fedha hizo zinajumuisha Euro milioni 192.5 zilizotolewa na Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB) na Euro milioni 43 kutoka katika Mfuko wa Afrika Ikue Pamoja (AGTF).Kukamilika kwa bwawa hilo lenye urefu wa mita 80.5 kutawezesha kuhifadhiwa kwa maji kiasi cha mililita za ujazo milioni 681 yatayotumika kwa ajili ya uzalishaji wa umeme pamoja na kilimo cha umwagiliaji.Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na serikali ya Kenya, kiasi cha maji mililita za ujazo milioni 22 itatumika kwa ajili ya kilimo cha umwagiliaji wakati milimita za ujazo milioni 34 itatumika kwa ajili ya matumizi ya nyumbani.Bwawa hilo ambalo linajengwa kwa awamu tatu, linatarajiwa kukamilika kwa awamu ya mwisho Desemba 2022. Awamu ya kwanza itakuwa ni kukamilisha ujenzi wa kiwanda kitakachokuwa na jukumu la kuchuja maji mililita za ujazo 34,600 ya kutumiwa na wananchi wapatao 674,700.Awamu hiyo hiyo ya kwanza itashuhudia pia uchujaji wa maji kiasi cha mililita 117,200 kwa ajili ya wananchi wapatao 640,000 katika mji wa teknolojia wa Konza. Awamu ya pili itakuwa ni ujenzi wa kiwanda cha uzalishaji wa umeme kwa kutumia maji yaliyotengwa kwa ajili ya kazi hiyo.
3kitaifa
KOCHA Emmanuel Amunike ameita kikosi cha Taifa Stars kwa ajili ya mchezo wa mwisho dhidi ya timu ya taifa ya Uganda, The Cranes na hakumjumuisha hata mchezaji mmoja wa Mtibwa Sugar.Mchezo huo wa kundi L utapigwa kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam Machi 24 ni muhimu kwa Taifa Stars kufuzu kwa fainali za Mataifa ya Afrika ambapo mara ya mwisho kufuzu kwa fainali hizo ni miaka 38 iliyopita.Kwa mara ya kwanza, Mtibwa Sugar imeshindwa kutoa mchezaji hata mmoja kwenye kikosi cha Taifa Stars lakini kocha wa timu hiyo, Zubery Katwila alisema hayo ni maamuzi yake na yeye hawezi kumuingilia.“Siwezi kumchambua kocha mwenzangu kwanini hajamuita hata mchezaji mmoja kwenye kikosi changu, hilo nawaachia wachambuzi.“Kama kocha, ni wazi Amunike ana vigezo vyake juu ya wachezaji wa aina gani awaite kwenye kikosi chake na ambao anaamini watampa matokeo mazuri na kama mtanzania niko nyuma yake kuona timu yetu ya taifa inapata matokeo mazuri,” amesema Katwila ambaye amewahi kuichezea Taifa Stars.Tangu nyota huyo wa zamani wa kimataifa wa Nigeria atangaze kikosi chake kitakachoivaa timu ya taifa ya Uganda Machi 24, kumekuwa na maoni mbalimbali kutoka kwa mashabiki na wachambuzi juu ya uteuzi wake.Wengi wamekuwa wakitaja majina ya wachezaji kama vile Salim Ayee, Ibrahim Ajibu, Mohamedi Hussein’Tshabalala’, Paul Godfrey na Abdallah Shaibu ‘Ninja’ kuwa walistahili kuitwa kwenye kikosi hicho.
5michezo
Na KOKU DAVID -DAR ES SALAAM MAMLAKA ya Mapato Tanzania (TRA) imefanikiwa kukusanya Sh bilioni 42.8 zilizotokana na makusanyo ya ushuru wa bidhaa kupitia mfumo wa stempu za kodi za kielektroniki. Akizungumza Dar es Salaam jana, Kamishna Mkuu wa TRA, Charles Kichere alisema makusanyo hayo yametokana na ushuru wa bidhaa uliokusanywa katika kipindi cha mwezi Machi 2019. Kichere alisema makusanyo hayo ni sawa na ongezeko la Sh bilioni 3.5 ambazo ukuaji wake ni asilimia 9 ukilinganisha na kipindi kama hicho ambacho kabla ya matumizi ya mfumo wa stempu za kodi za kielektroniki walikusanya Sh bilioni 39.3. Alisema mfumo huo ambao kwa awamu ya kwanza ulianza kutumika Januari 15, mwaka huu ulihusisha bidhaa za sigara, pombe kali, mvinyo, bia na aina zote za vileo. “Katika awamu ya pili itakayoanza mwezi Mei itahusisha bidhaa za vinywaji baridi, maji, juisi pamoja na CD/DVD na kwamba hadi sasa tumeshafunga mitambo 44 katika viwanda 23 vya bidhaa za awamu ya kwanza. “Pia tumefunga mitambo hiyo katika viwanda vyote vya sigara nchini ambavyo vipo vinne, viwanda vyote saba nchini vya bia, viwanda vya mvinyo na pombe kali ambavyo vipo 12 ikiwa ni pamoja na viwanda vidogo saba ambavyo vinatumia mfumo huu kwa kubandika stempu hizo kwa mikono chini ya uangalizi wa TRA kutokana na uchanga wa teknolojia ya mitambo yao ya uzalishaji,” alisema. Kichere alisema katika ufungwaji wa mfumo huo kwa viwanda vya bidhaa za awamu ya pili wameshafunga mitambo 45 katika viwanda 19 vya vinywaji baridi. Alisema matumizi ya mfumo huo wa stempu za kodi za kielektroniki yamekuwa na faida na kwamba yamewezesha kuongeza mapato kutokana na ushuru wa bidhaa, kuondoa malalamiko ya kutokutendewa haki katika makadirio ya kodi, Serikali kutambua mapema ushuru wa bidhaa utakaolipwa. Aidha, alisema faida nyingine ni kuzibwa kwa mianya ya uingizaji nchini wa bidhaa kiholela ambazo hazijalipiwa ushuru stahiki na zisizokuwa na viwango vinavyokubalika, kuongeza uhiyari wa kulipa kodi, kuwezesha ufuatiliaji wa bidhaa pamoja na kulinda afya ya mlaji kwa kumwezesha mtumiaji au msambazaji kutambua bidhaa yenye stempu halali na isiyo halali. Kichere alisema matumizi ya stempu za kodi za karatasi yalikuwa na changamoto ambazo zilisababisha upotevu wa mapato ya Serikali, uwezekano mdogo wa kutambua stempu za kughushi, kuibuka kwa wadanganyifu waliotumia udhaifu wa mfumo wa stempu za karatasi kwa kuiibia Serikali kwa kughushi stempu. Aliongeza kuwa kwa matumizi ya stempu za kodi za karatasi haikuwa rahisi kutambua uhalali wa bidhaa iliyokuwa sokoni kuwa imetengenezwa na mzalishaji halali wa bidhaa hiyo. “Matumizi ya stempu za kodi za kielektroniki yalianzishwa mwaka 2018 na Serikali kupitia mamlaka ya mapato kwa bidhaa zinazostahili kutozwa ushuru wa bidhaa ili ziweze kutozwa kwa mujibu wa kifungu namba 124 cha sheria ya ushuru wa bidhaa sura ya 147 inayoainisha aina za bidhaa zinazotozwa ushuru huo kwa mujibu wa jedwali namba 4 la sheria hii,” alisema Kichere.
3kitaifa
WASHINGTON, MAREKANI WAZIRI wa Mambo ya Nje wa Marekani, Mike Pompeo anasema makubaliano muhimu na Iran ya nyuklia yalitokana na uongo, baada ya Israel kudai kwamba ina ushahidi kuhusu mpango wa siri wa nyuklia wa Iran. Amesema inadhihirisha makubaliano hayo ya Iran na mataifa sita yenye nguvu duniani mwaka 2015, yalitokana na uongo na si nia njema. Rais Trump ameashiria kwa muda mrefu azma yake ya kujitoa katika makubaliano hayo na anatarajiwa kutoa uamuzi katika wiki chache zijazo. Mapema wiki hii, Waziri Mkuu wa Israeli Benjamin Netanyahu aliishutumu Iran kwa kuendeleza mpango wa kuunda zana za nyuklia kupitia mradi uliopewa jina ‘Project Amad’. Amesema nchi hiyo imeendelea kujifunza kuhusu kuunda silaha za nyuklia baada ya awali mradi huo kusitishwa mwaka 2003. Hilo lilifuata ufichuzi wa mwaka 2002 wa kundi la upinzani linaloishi uhamishoni lililosema Iran inaunda maeneo ya siri ya urutubishaji nyuklia kinyume na makubaliano ya nyuklia ambayo Iran ilitia saini kuyatii. Netanyahu aliwasilisha kile alichokitaja kuwa ushahidi wa maelfu ya nyaraka za siri za nyuklia zilizoonyesha kuwa Iran ilidanganya kuhusu azma yake ya kuunda zana za nyuklia kabla ya makubaliano hayo muhimu yalioidhinishwa mwaka 2015. Lakini Iran imekuwa ikikana kuunda zana za nyuklia, na ilikubali miaka mitatu iliyopita kusitisha mpango wake wa kuunda nishati ya nyuklia ili iondolewe vikwazo. “Nyaraka zilizopatikana na Israel kutoka ndani ya Iran zinaonyesha pasi na shaka kuwa utawala wa Iran ulikuwa hausemi ukweli,” Pompeo alisema katika taarifa yake. “Tumekagua nyaraka tulizoziona ni za kweli, “alisema akiongeza: “Iran ilificha mpango mkubwa wa nyuklia dhidi ya dunia na Shirika la Kimataifa la Nishati ya Atomiki (IAEA) – mpaka leo.” Pompeo pia alionya kwamba Marekani sasa “inakagua ufichuzi huo wa nyaraka za siri wa Iran una maana gani kwa siku zijazo”. Trump, ambaye alizungumza wazi kuhusu upinzani wake wa makubalian hayo na Iran yaliyofikiwa wakati wa utawala wa Rais Barack Obama, amesema ametizama sehemu ya aliyowasilisha Netanyahu, akisema hali hiyo haikubaliki. Amesema atafanya uamuzi kuhusu iwapo aendelee kushikilia makubaliano hayo siku au kabla ya Mei 12.
2kimataifa
Na Mwandishi wetu-Lusaka KATIBU Mkuu wa Jumuiya ya Maendeleo ya Nchi za Kusini mwa Afrika (SADC), Dk Stagomena Tax, amesema Tanzania imepewa nafasi ya kuwa mwenyekiti wa jumuiya hiyo kutokana na kutimiza vigezo vinavyohitajika na ambavyo ni uwepo wa demokrasia na utawala bora. Kwa mujibu wa taarifa kwa umma iliyotolewa na Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Tax alisema hayo baada ya kumalizika mkutano wa 21 wa kamati ya mawaziri kuhusu asasi ya siasa, ulinzi na usalama ya SADC  kinachofanyika Lusaka Zambia. Taarifa hiyo ilisema Dk Tax, alizitaka nchi wanachama wa jumuiya hiyo kuendelea kukuza demokrasia na utawala bora kwa kuwa ndio nguzo muhimu za jumuiya hiyo. “Licha ya uchanga wa demokrasia katika ukanda huu, nchi zimeendelea kupiga hatua katika kuboresha demokrasia na utawala bora na Tanzania ni mojawapo ya nchi zinazozingatia uwepo wa demokrasia na utawala bora miongoni mwa nchi wanachama,” taarifa ilimnukuu Dk Tax. Ilisema pia mkutano huo umeridhishwa na ukuaji wa demokrasia na utawala bora miongoni mwa nchi wanachama kutokana na chaguzi zilizofanyika kwa haki, uhuru na amani katika nchi takribani sita ikiwemo Afrika ya Kusini, Eswatini, Malawi, Madagascar na Congo DRC. Naye Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Prof. Palamagamba Kabudi, alisema kumalizika kwa chaguzi katika nchi sita wanachama wa jumuiya hiyo, kunaidhihirishia dunia namna ambavyo Ukanda wa Kusini mwa Afrika ukiyasimamia mambo yake yenyewe bila ya kuingiliwa na mataifa mengine una uwezo wa kuimarisha taasisi zake za demokrasia, utawala bora na haki jambo ambalo Tanzania. Alisema mkutano huo pia umejadili maombi ya Burundi kujiunga na jumuiya hiyo ambayo yamekuwepo kwa takribani miaka mitatu sasa, na kutanabaisha kuwa Burundi imetekeleza kwa kiwango cha asilimia sabini masharti iliyotakiwa kuyatimiza ili kupata ridhaa ya kuwa mwanachama wa SADC . Alisema asilimia 30 yaliyosalia, Tanzania kwa kushirikiana na sekretarieti ya SADC  na nchi nyingine wanachama zitaendelea kuisaidia Burundi ili iweze kuwa mwanachama jambo litakaloisaidia Burundi kuimarika kisiasa na kidemokrasia na kushiriki katika maendeleo ya Bara la Afrika.
3kitaifa
Na MOHAMED HAMAD,KITETO DIWANI wa Kata ya Ndirigishi mkoani Manyara, Chitu Daima (CCM), anashikiliwa na Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) kwa tuhuma za kudai na kupokea rushwa ya Sh 500,000. Tukio hilo limetokea kijijini hapo baada ya wananchi kumtuhumu Chitu kupokea rushwa ndipo wakaamua kutega mtego na kufanikiwa kumnasa akipokea kutoka kwa mmoja wao. Kwa mujibu wa Ainoti Sepewa mmoja wa wafugaji aliyedaiwa fedha hiyo ili aweze kupatiwa maeneo ya kulisha mifugo yao, alisema awali walimpa zaidi ya Sh milioni moja bila mafanikio ya kupata maeneo kwa ajili ya shughuli za ufugaji. “Baada ya kuchoshwa na hali hii, nililazimika kwenda PCCB kuomba msaada zaidi, ndipo akataka nimpe laki tano nikamwahidi kuwa naenda mnadani kuuza ng’ombe na kufanikiwa kupewa fedha na PCCB na kumkamatisha,” alisema Sepewa. Alisema awali wananchi kwa pamoja walikubaliana kumega sehemu ya Hifadhi ya Emboley Murtangos ili wagawane wakulima na wafugaji, badala yake eneo hilo limegawiwa wakulima peke yao na kusababisha manung’uniko makubwa. Kwa upande wake mwananchi mwingine, Mathew Isaya, alitaja baadhi ya madhara waliyopata kutokana na rushwa hizo kuwa ni pamoja na kutopatikana haki na kusababisha uhusiano mbaya kati ya wakulima na wafugaji kupigana. Naye Kadege Mario wa Kitongoji cha Kuti, Kijiji cha Ndirigishi, alisema mara ya kwanza walimpa Sh 500,000, Sh 300,000 na siku nyingine walimpa Sh 400,000 na mbuzi mmoja akisema maisha yao ni duni. Kwa upande wake, Kamanda wa Takukuru Wilaya ya Kiteto, Jastine Maingu, amekiri kutokea kwa tukio hilo akisema hawezi kuzungumza chochote kwa kuwa wako katika hatua ya awali pamoja na kufanya mahojiano juu ya tukio hilo na hadi sasa mtuhumiwa anashikiliwa.
3kitaifa
WAZIRI wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Profesa Palamagamba Kabudi amesema Serikali ya Awamu ya Tano itaendelea kutengeneza fursa nyingi za ajira ili kuwezesha wahitimu wengi wa vyuo vikuu nchini na waliosoma nje kupata ajira na kutumia utaalamu walioupata kujenga taifa lao.Aliyasema hayo wakati akizungumza kwenye mahafali ya kwanza kwa wanafunzi waliosoma nje ya nchi kupitia Kampuni ya Global Education Link yaliyofanyika Mlimani City Dar es Salaam.Waziri Kabudi alisema serikali inaendelea kushirikiana na wadau wa sekta binafsi kuweka mazingira mazuri yatakayoongeza fursa nyingi za ajira kwa vijana wanaomaliza vyuo vya nje na ndani ya nchi.Aliwapongeza wahitimu hao kwa kwenda kusoma nje ya nchi na kurudi na ujuzi watakaoutumia kujenga taifa lao kwenye sekta mbalimbali kama ujenzi wa miundombinu na katika sekta nyingine zilizopo.“Serikali inaendelea kutekeleza awamu ya pili ya Mpango wa Maendeleo kwa ufanisi mkubwa. Inataka kujenga uchumi wa kati utakaoongeza nafasi nyingi za ajira kwa vijana wetu,” amesema Profesa Kabudi.Alisema serikali imejipanga kuendelea pia kudhibiti mianya ya ufisadi ili fedha zinazopatikana zielekezwe kwenye miradi ya maendeleo na kupunguza umasikini kwa Watanzania wa mijini na vijijini.Aliipongeza Global Link Education kwa namna ambavyo imeweza kuwapeleka zaidi ya wanafunzi 5,600 kwenda kusoma vyuo vikuu nje ya nchi na kufuatilia maendeleo yao mpaka walipohitimu masomo yao.Mkurugenzi Mkuu wa Global Link Education, Abdulmalik Mollel alisema mahafali hayo ni ya kwanza kufanyika nchini na mwaka huu pekee kampuni hiyo inatarajia kupeleka wanafunzi 1,000 kusoma nje.Alisema mamia ya wanafunzi waliopelekwa nje kusoma wengine wamepata bahati ya kuwa wakurugenzi wa kampuni na wengine wamejiajiri na wengine wameajiriwa kwenye taasisi mbalimbali hapa nchini.Alisema baadhi ya wahitimu hao bado wanatafuta fursa hivyo aliwaomba wawekezaji nchini kuhakikisha wanawapa kipaumbele vijana hao kwenye nafasi za ajira badala ya kuajiri wataalamu kutoka nje.“Tuna vijana wenye ujuzi wa kutosha kwenye taaluma mbalimbali, Mheshimiwa Waziri nakuomba hili ulibebe utusaidie zinapotokea nafasi za ajira vijana wetu wapate nafasi kwani ujuzi wa kutosha wanao.“Hawa vijana wamesoma kwao wanajua tamaduni zao wanajua kila kitu kuhusu nchi zao. Huu ni muda muafaka wawekezaji wanaokuja watoe kipaumbele kwa vijana hawa wapate ajira,” amesema Mollel.
3kitaifa
Derick Milton, Geita Mkoa wa Geita umefanikiwa kuwafanyia tohara wanaume 115,000 sawa na asilimia 95, kati ya wanaume 119,000ambao walilengwa kufanyiwa katika kipindi cha Oktoba mwaka jana hadi Septemba mwaka huu. Hayo yamesemwa na Mganga Mkuu wa Mkoa huo, Dk. Japhet Simeo, wakati akifungua mafunzo kwa waandishi wa habari kutoka mikoa ya Mwanza, Simiyu, Shinyanga, Kagera na Geita kuhusu kuandika habari za tohara yaliyoandaliwa na Shirika la IntraHealth. Dk. Simeo amesema kufanya tohara kwa wanaume na watoto wadogo, ni moja ya kampeni inayoendeshwa na serikali mkoani humo kwa kushirikiana na IntraHealth lengo likiwa kupunguza maambukizi ya virusi vya Ukimwi. “Takwimu za maambukizi ya Ukimwi zimekuwa zikipanda kutoka asilimia 4.5 mwaka 2016/17 hadi kufikia asilimia tano mwaka huu. “Bado mkoa watu wanaoishi navirusi vya ukimwi wanaendelea kutoweka na hawajulikani walipo kutokana na wengi wao kuhama hama kutokana na shughuli za uchimbaji madini, uvuvi na kilimo. “Mpango wetu mpya kwa sasa ni kufanya tohara kwa watoto wadogo, kuendelea kutoa elimu kwa wananchi juu ya umuhimu wa tohara kwa wanaume, lakini pia tunaviomba vyombo vya habari, kutusaidia kutoa elimu kwa wananchi kufanya tohara hasa wanaume, ” amesema Dk. Simeo. Kwa upande wake Mshauri wa huduma za tohara kutoka IntraHealth mkoa, Dk. Peter Sewa, amesema mwanaume ambaye hajafanyiwa tohara yuko kwenye hatari zaidi ya kupata maambukizi ya Virusi Vya Ukimwi kuliko mtu aliyepata tohara ambaye uwezo wa kutopata maambukizi ni asilimia 60.
4afya
Na RAMADHAN HASSAN-DODOMA WATU saba wamefariki dunia mkoani Dodoma kwa kuugua ugonjwa wa Kipindupindu, huku 329 wakiugua ugonjwa huo. Akizungumza na waandishi wa habari juzi mjini hapa, Mganga Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Dk. James Kiologwe alisema takwimu hizo ni kuanzia Oktoba 20, mwaka huu  ambapo kwa Wilaya ya Mpwapwa wamefariki watu watatu huku 208 wakiugua. Dk. Kiologwe alisema katika Wilaya ya Kongwa walifariki wagonjwa wawili huku 18 wakiugua ugonjwa huo, Chamwino 18 wakiugua na wanane kufariki dunia. “Hizi ni takwimu za Oktoba ugonjwa wa Kipindupindu umetokea wilayani Kilosa kule ni mpakani na Mpwapwa na kulikuwa na bonde ambalo wananchi walikuwa wakijishughulisha na kilimo hivyo walikuwa wakishirikiana katika shughuli za  kijamii ndio maana ugonjwa huo ukaingia Mpwapwa,”alisema. Alisema kutokana na hali hiyo Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Jordan Rugimbana alikuja na kampeni ya tokomeza Kipindupindu ambayo ilisaidia kwa kiasi kikubwa kupunguza idadi ya wagonjwa kutokana na kutoa elimu kwa wananchi. Dk. Kiologwe alisema mpaka sasa wagonjwa waliopo ni nane tu katika Mkoa wa Dodoma kutokana na kampeni hiyo iliyoanzishwa na mkuu wa mkoa. Mganga Mkuu huyo alitoa wito kwa wananchi wa mkoa huo kufuata taratibu za usafi katika kipindi hichi cha Sikukuu kwani ugonjwa huo kwa kiasi kikubwa husababishwa na uchafu.
3kitaifa
Na FARAJA MASINDE -DAR ES SALAAM BAADA ya kupata dhamana ya Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu juzi, mfanyabiashara maarufu nchini, Yusuf Manji, amelazwa tena kwenye Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI) iliyoko katika Hospitali ya Taifa Muhimbili. Kwa mujibu wa taarifa zilizothibitishwa na Ofisa Uhusiano wa Taasisi hiyo jana, Anna Nkinda, Manji alifikishwa hospitalini hapo juzi jioni ikiwa ni muda mfupi baada ya kupata dhamana dhidi ya kesi ya kutumia dawa za kulevya aina ya heroin inayomkabili. “Ni kweli Manji yupo hapa, aliletwa jana jioni (juzi) kwa matibabu ambapo hadi leo (jana) ninavyoongea na wewe bado yupo hapa amelazwa anaendelea na matibabu kama kawaida,” alisema Anna. Hii ni mara ya pili kwa Manji ambaye pia ni Diwani wa Kata ya Mbagala Kuu, kulazwa kwenye taasisi hiyo. Mara ya kwanza ilikuwa ni Februari 12, mwaka huu alipolazwa hapo akitokea katika Kituo Kikuu cha Polisi Dar es Salaam, alipokuwa ameshikiliwa tangu Februari tisa akifanyiwa mahojiano. Mfanyabiashara huyo alifika mwenyewe kwenye kituo hicho cha polisi kutokana na wito uliotolewa na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda, aliyetaja majina 65 ya watu aliodai wanajihusisha na biashara ya dawa za kulevya. Mbali na Manji, baadhi ya watu wengine waliotajwa na Makonda na kutakiwa kufika kituoni hapo ni Mchungaji wa Kanisa la Ufufuo na Uzima, Josephat Gwajima, Mbunge wa zamani wa Kinondoni, Idd Azzan ambao tayari wamehojiwa polisi huku Mbunge wa Hai, Freeman Mbowe, akiwa bado hajahojiwa licha ya kutajwa kwenye orodha hiyo. Juzi Alhamisi, Manji alifikishwa kwenye Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, ambapo shauri lake lilisikilizwa na Hakimu Mfawidhi wa Mahakama hiyo, Cyprian Mkeha. Karani wa mahakama hiyo, Sarah Mulokozi, alimsomea mshtakiwa shtaka lake ambapo alidai kuwa kati ya Februari 6 na 9, mwaka huu eneo la Upanga Sea View jijini Dar es Salaam, Manji alitumia dawa za kulevya aina ya heroin. Mtuhumiwa huyo alikana shtaka hilo na Mkurugenzi wa Mashtaka Msaidizi (ADPP), Osward Tibabyekomya, alidai kuwa upelelezi wa kesi hiyo bado haujakamilika na kuiomba Mahakama kupanga tarehe nyingine ya kutajwa. Upande wa mawakili wa utetezi ambao ni Alex Mgongolwa na Hudson Ndusyepo, waliiomba Mahakama kumpa mshtakiwa dhamana  kwa sababu ya mashtaka yanayomkabili yanadhaminika. Hakimu Mkeha alisema mshtakiwa atakuwa nje kwa dhamana kwa kutakiwa kusaini hati ya dhamana ya Sh milioni 10 pamoja na mdhamini mmoja wa kuaminika ambapo Katibu Mkuu wa Klabu ya Yanga, Charles Mkwasa, alimdhamini Manji, ambaye aliachiwa kwa dhamana hadi Machi 16. Mara baada ya kupata dhamana, Manji aliondoka mahakamani hapo saa 9:40 akiwa kwenye gari yenye namba T670 BBX aina ya Hummer.  
3kitaifa
MAKAMU wa Pili wa Rais wa Zanzibar, Balozi Seif Ali Iddi amesifu juhudi zinazofanywa na Rais John Magufuli katika kuhakikisha taifa linakuwa na uchumi wa kati likitegemea viwanda.Kauli hiyo ameitoa kwenye maadhimisho ya sherehe za miaka 55 za mapinduzi zilizofanyika mjini hapa hivi karibuni.Alisema kazi kubwa anayoifanya Rais Magufuli inawapa nguvu kubwa watanzania kuhakikisha kwamba wanashiriki katika kuimarisha uchumi.Alisema kwa kasi ya Rais Magufuli katika kuiweka Tanzania ya viwanda kumefanya pia mapinduzi kuwa na nguvu kubwa ya kutimiza malengo yake katika sekta zote za elimu, afya, kilimo na hata utalii.Balozi Seif akihutubia kumkaribisha Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi na Rais wa Zanzibar, Dk Ali Mohamed Shein alisema mapinduzi yameleta neema kubwa kwa wazanzibari na hasa Muungano ambao ndani yake wazazibari wapata nafasi ya kufanya mambo kwa amani na kujenga jamii.Alisema kutokana na utendaji kazi wa serikali uliotukuka umesababisha uchumi wa Zanzibar kukua na kuanza kuachana na utaratibu wa utegemezi.Kwa sasa uchumi ukiwa unapaa kwa asilimia 7.5 huku matarajio ya serikali ya kukusanya Sh bilioni 100 hadi ifikapo mwaka 2020 yameanza kuonekana baada ya hivi karibuni kukusanya zaidi ya Sh bilioni 807 kwa mwaka.Waziri wa Fedha na Mipango, Dk Khalid Salum Mohamed amesema hali ilivyo ni ishara nzuri ya kufikia malengo ya ilani ya CCM inayoelekeza ukusanyaji wa kiasi hicho na mapato katika kipindi hiki.Mapato ya Serikali ya Zanzibar yanatokana na makusanyo ya Mamlaka ya Mapato nchini (TRA) na Bodi ya Mapato Zanzibar (ZBR).Mwaka 2018 Zanzibar imekusanya Sh bilioni 807 ikiwa ni ishara njema ya kufikiwa kwa malengo.
3kitaifa
Msanii wa muziki na uigizaji Bongo Gigy Money, ameonekana kumkingia kifua Menina Tz kwa kusema picha na video zilizovuja mitandaoni, kuna mtu alifanya makusudi na anamuhisi Mwijaku kwa sababu aliwaona wakiwa wote katika mapozi ya mahaba mkoani Tanga. Gigy Money ameeleza hayo kupitia EATV & EA Radio Digital, baada ya kupost video fupi kupitia ‘Insta Live’ ya mtandao wa kijamii wa Instagram, akionekana akiwaponda watu wanaoshadadia tukio hilo la kuvuja kwa picha na video hizo. “Kama nisingekuwa mimi hakuna staa yeyote angeongelea suala la Menina, mbona hawakuongea za Amber Rutty au Nandy hata msamaha aliomba, hakuna mtu anayeweza kupost vile kwa sababu anatafuta kiki, wasipende kumshambulia mtu maana hii mitandao inaweza ikampa mtu msongo wa mawazo au kumpotezea mtu maisha” amesema Gigy Money. Aidha Gigy ameongeza kuwa, “Hii ni kweli naongea hapa mbele ya kamera nilishawahi kuwaona Mwijaku na Menina Tanga, wakiwa katika gari hata zile video na picha zimevujishwa sidhani kama ni yeye, hawezi kufanya kitu kama kile, hata kutoka kwao kazi maana kuna dini sana, ameacha muziki kwa ajili ya familia yake“. Gigy Money ameendelea kusema, hata alivyosikia Mwijaku amevujisha zile video, alijisikia vibaya kwa sababu aliwaona wakiwa katika mahaba mazito na kama watu wanasema Mwijaku amesambaza video basi ni kweli.
0burudani
Na BRIGHITER MASAKI. MREMBO aliyewahi kushiriki shindano la Miss Tanzania mwaka 2014 na kushinda kisha kupokwa taji hilo, Sitti Mtemvu (Sitti), ameibuka na kuweka wazi kwamba alikuwa kimya muda mrefu kwa kuwa alirudi masomoni nchini Marekani kwa ajili ya kusaka cheti. Sitti alisema wakati Rais Magufuli alivyoagiza wasio na vyeti wachunguzwe, aliamua kurudi chuoni nchini Marekani kwa ajili ya masomo na kupata vyeti kwa ajili ya kumsaidia kuendesha harakati alizokuwa amezianzisha baada ya kupokwa taji la Miss Tanzania kwa madai ya kudanganya umri mwaka 2014. Sitti, ambaye alifanikiwa kushinda taji hilo kisha ushindi wake kutenguliwa na kupewa aliyekuwa mshindi wa pili, Lilian Kamazima, ameliambia MTANZANIA kuwa, kimya chake cha muda mrefu kitafikia kikomo hivi karibuni, atakapoendeleza harakati zake, ikiwamo uandishi wa kitabu chake cha Chozi la Sitti ni Kampuni yake. “Kimya changu kwa muda mrefu ni kutokana na kurudi masomoni Marekani kisha kupata vyeti, lakini kwa sasa nimeshamaliza na mambo mbalimbali yataendelea, ikiwamo uzinduzi wa taasisi yangu ya Sitti,” alisema Sitti.
0burudani
Na Kulwa Mzee -DAR ES SALAAM WAFANYABIASHARA wawili walioingiza magari matatu ya kifahari kwa kuyaficha katika kontena wakidai limebeba nguo za mtumba, wametiwa hatiani na watafilisiwa magari yote na kutakiwa kulipa fidia ya jumla ya Sh milioni 100. Hukumu hiyo ilitolewa jana na Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, Dar es Salaam mbele ya Hakimu Mkazi Mfawidhi, Cyprian Mkeha baada ya washtakiwa kukiri makosa mawili yaliyokuwa yakiwakabili. Washtakiwa  Sultani Ibrahimu (36) raia wa Uganda na Ramadhani Hamis (48) maarufu Ukwaju, wanadaiwa kutumia nyaraka za uongo Januari 18, mwaka huu Makao Makuu ya Bandari, Dar es Salaam, kwamba walibeba mitumba katika kontena wakati walibeba magari ya kifahari matatu na shtaka la pili kusababisha hasara ya zaidi ya Sh milioni 190. Akitoa hukumu, Hakimu Mkeha alisema: “Nimezingatia hoja zilizowasilishwa na pande zote mbili, mahakama inaamuru magari yafilisiwe, lakini si kwa matakwa ya washtakiwa, bali sheria inatamka hivyo.” Alisema thamani ya magari hayo ni kubwa, Sh 287,779,536 ambayo ni kubwa kuliko hasara inayodaiwa kusababishwa. “Kutokana na hoja hizo, kwa kosa la kwanza kila mshtakiwa anatakiwa kulipa faini ya Dola za Marekani 10,000 akishindwa atakwenda jela miaka mitatu na kosa la pili kila mshtakiwa anatakiwa kulipa faini ya Sh milioni tano, akishindwa atakwenda jela miaka mitatu,” alisema. Awali baada ya kukiri makosa hayo, washtakiwa walisomewa maelezo ya awali kwamba kati ya Desemba mosi 2016 na Machi 2017, pamoja na watu wengine wanaoishi Uingereza, walikubaliana kuingiza magari Tanzania. Inadaiwa Oktoba 13, 2016 kupitia nyaraka ya kuingizia mizigo bandarini namba 5709947971, washtakiwa na wenzao walioko Ulaya walisafirisha kontena namba MRKU 3049836 ambalo lilibeba magari matatu ya kifahari aina ya Range Rover Evoc yenye chesesi namba Salva, 2AE9DH766530, Range Rover Sports yenye chesesi namba Salga 2JE6A1596651 nyeusi na gari la tatu aina ya Audio Q3 yenye chesesi namba WAUZZZ844 DRO28763 ya rangi ya kijivu. Inadaiwa katika Makao Makuu ya Bandari, Dar es Salaam walitoa tamko la uongo kwamba kontena hilo lina mitumba ya nguo, viatu na magodoro kwa lengo la kukwepa kodi huku wakijua kwamba thamani ya mali waliyotamka ni ndogo ukilinganisha na magari waliyobeba. Kutokana na tamko hilo la uongo, walisababisha maofisa forodha wa Mamlaka ya Mapto kukadiria kodi ya chini ya Sh 31,548424 badala ya kodi sahihi waliyopaswa kulipa Sh 190,923,267.76 . Wakili wa Serikali Mkuu, Mutalemwa Kishenyi, alipotakiwa kusema lolote kuhusu washtakiwa kabla ya mahakama kutoa adhabu, alisema ni wakosaji wa mara ya kwanza, aliiomba mahakama ikitoa adhabu katika kosa la pili itoe amri ya faini, fidia na magari yataifishwe.
3kitaifa
Na KADAMA MALUNDE-SHINYANGA MKUU wa Wilaya ya Shinyanga mkoani hapa, Josephine Matiro, ametembelea ghala la kuhifadhia chakula Kanda ya Shinyanga,  huku akiwataka wananchi kupuuza taarifa za uhaba wa chakula nchini. Mkuu huyo wa wilaya alitembelea ghala hilo jana huku akiwa na wajumbe wa Kamati ya Ulinzi na Usalama ya wilaya hiyo kwa lengo la kujionea hali halisi ya akiba ya chakula na kusema kipo cha kutosha. “Itakapofikia hatua kuwa kuna ulazima wa chakula cha msaada kwa kaya ambazo hazina kabisa zimezidiwa kwa kukosa chakula, ifahamike kuwa tunacho chakula cha kutosha kimehifadhiwa vizuri kwenye ghala letu hili,” alisema Matiro. Akizungumzia hali ya chakula katika ghala hilo, Wakala wa Taifa wa Hifadhi ya Chakula (NFRA) Kanda ya Shinyanga, Mary Shangali, alisema hadi sasa kanda hiyo inayounda mikoa minane ina jumla ya tani 9,146.916 na wanatarajia kupokea chakula tani 10,000 kutoka Mpanda mkoani Katavi. “Katika Kanda ya Shinyanga yapo maghala manne yaliyohifadhi chakula ambapo ghala la Bukene lililopo mkoani Tabora kuna tani 2,898.994, ghala la Shinyanga tani 6,050.969, ghala la Kasulu lililopo mkoani Kigoma  tani 196.629 hivyo kuna jumla ya tani 9,146.916,” alisema Shangali. Alisema Juni mwaka jana Jeshi la Magereza walikuwa na tani 4,035 na walichukua tani 1,105 hivyo kubakiwa na tani 2,000 ambazo bado hawajachukua hadi sasa katika mgawo wao. Shangali alisema kanda hiyo inajumuisha mikoa ya Mwanza, Simiyu, Mara, Tabora, Kigoma, Geita, Kagera na Shinyanga. Kwa upande wake Ofisa Ugavi kutoka Hifadhi ya Kanda ya Shinyanga, Bitteme Mgabo alisema wamekuwa wakitoa chakula kwa maombi kutoka Ofisi ya Waziri Mkuu kitengo cha Maafa.
3kitaifa
RAIS wa Rwanda, P aul Kagame ameushangaza ulimwengu baada ya kuwaachia huru wafungwa 2,140 wal ioomba msamaha, ikiwa ni pamoja na wanasiasa maarufu nchini humo.H atua hiyo imepongezwa na wanasiasa walioachiwa huru na imeleta furaha kubwa katika taifa hilo la Afrika Mashariki, kwa kuonesha mwelekeo mpya wa kisiasa na kidemokrasia. Miongoni mwa wafungwa walioachiwa huru ni Victoire Ingabire, ambaye ni Mwenyekiti wa chama cha upinzani cha Force Democratiqu e Unies du Rwanda (FDI). Ingabire alihukumiwa miaka 15 jela tangu mwaka 2 0 10 . Mwingine ni mwanamuziki, Kizito Mihigo ambae alikuwa amehukumiwa kifungo cha miaka 10 jela.Ingabire aliyefungwa mwaka 20 10 , alikutwa na hatia ya kufanya uchochezi kwa wananchi ili kuiasi serikali na kuunda makundi ya silaha ili kuivuruga nchi na kupuuza mauaji ya kimbari ya 19 9 4 dhidi ya watutsi. Aahidi kumsaidia Kagame kuijenga Rwanda Baada ya kuachiwa huru, Ingabire alimshukuru Rais Kagame na kusema kuanzia sasa ndio mwanzo wa uhuru wa kisiasa na demokrasia ya kweli nchini Rwanda. Alisema kutokana na nia nzuri ya rais ya kujenga nchi, yuko tayari kumuunga mkono katika kuiletea maendeleo Rwanda.“Nina furaha kwa hatua iliyochukuliwa na rais, sasa nitarejea kuendelea na maisha kama kawaida na kusaidia maendeleo ya nchi,” alisema Ingabire. “Nimekuwa nikifuatilia nikiwa gerezani hali ya mambo inavyoendelea nchini, kuna mafanikio mengi yaliyofikiwa, na ninadhani tunaweza kupiga hatua zaidi tukishirikiana pamoja kwa sababu kuna mengi ya kufanya.H ii ndiyo njia nzuri ya kujenga nchi yetu kwa kuheshimu mawazo ya wale tunaohisi ni wapinzani, nampongeza rais ambaye ameamua kunipa msamaha na kutoka nje ya gereza,” aliongeza Ingabire. Tangu wakati huo, kumekuwa na shinikizo la kumtaka Rais Kagame kumwachia huru. H atua ya serikali kumwachia huru, inatajwa kuwa hatua muhimu kuchukuliwa na utawala wa Rais P aul Kagame, ambaye anaongoza taifa hilo la Afrika Mashariki kwa muhula wa tatu sasa.Kwa upande wake, Februari 2 0 15 mwanamuziki Kizito Mihigo alihukumiwa miaka 10 gerezani baada ya kukiri kuhusika na uhalifu, ikiwa ni pamoja na njama ya kumuua Rais P aul Kagame na viongozi wengine wa nchi. Mwanasiasa mwingine aliyeachiwa huru mwishoni mwa wiki ni aliyekuwa Makamu Mwenyekiti wa FDI, ambaye naye pia alimshukuru Rais Kagame kutokana na hatua ya kijasiri na ya kizalendo.Alisema pamoja na kwamba hatua hiyo imechochewa na shinikizo linaloendelea kimataifa hasa wakati huu ambapo Waziri wa Mambo ya Nje wa Rwanda, Louise Mushikiwabo akiwania nafasi ya kuwa katibu mkuu wa shirika la nchi zinazozungumza Kifaransa. Katibu Mkuu katika serikali ya Rwanda anayehusika na mambo ya nje, Olivier Nduhungirehe alisema hatua hiyo imekuja kutokana na ombi la wahusika wenyewe, kumuandikia rais mara kadhaa wakimuomba msamaha ; na sio vinginevyo.
3kitaifa