content-pipeline / data /texts /namba za kirumi g4.txt
AK1239's picture
Prepare for Hugging Face Spaces deployment
91e999e
SURA: NAMBA ZA KIRUMI
Utangulizi
Namba za Kirumi ni mfumo wa namba unaotumia herufi za alfabeti kuwakilisha namba. Katika sura hii, utajifunza kutambua, kusoma, na kuandika namba za Kirumi kutoka I hadi L (1 hadi 50).
1. Namba za Kirumi kuanzia I hadi X
Namba za Kirumi za 1 hadi 10 ni kama ifuatavyo:
1 - I (Moja)
2 - II (Mbili)
3 - III (Tatu)
4 - IV (Nne)
5 - V (Tano)
6 - VI (Sita)
7 - VII (Saba)
8 - VIII (Nane)
9 - IX (Tisa)
10 - X (Kumi)
Kanuni za Kuandika Namba za Kirumi
Namba I inaweza kurudiwa mara tatu tu: I, II, III.
Ikiwa namba ndogo ipo kushoto ya kubwa, huondolewa thamani yake (IV = 5 - 1 = 4).
Ikiwa namba ndogo ipo kulia ya kubwa, huongezwa thamani yake (VI = 5 + 1 = 6).
Zoezi la 1
Panga namba IX, VI, X, IV, VII, V, VIII kwa mpangilio wa kutoka ndogo hadi kubwa.
Badili namba hizi za Kirumi kuwa za Kiarabu: VII, IV, VI, V, VIII, IX.
Badili namba hizi za Kiarabu kuwa za Kirumi: 3, 6, 7, 1, 8, 4, 10, 9, 5.
2. Namba za Kirumi kuanzia XI hadi XX
Namba za Kirumi za 11 hadi 20 ni kama ifuatavyo:
11 - XI (Kumi na moja)
12 - XII (Kumi na mbili)
13 - XIII (Kumi na tatu)
14 - XIV (Kumi na nne)
15 - XV (Kumi na tano)
16 - XVI (Kumi na sita)
17 - XVII (Kumi na saba)
18 - XVIII (Kumi na nane)
19 - XIX (Kumi na tisa)
20 - XX (Ishirini)
Zoezi la 2
Namba ipi ina thamani kubwa zaidi kati ya XI, XII, XIII, XV, XVI, XVII, XVIII, XIV, XIX?
Andika namba hizi za Kirumi kwa maneno: XIV, XVI, XX, XI, XV, XIX.
Badili namba hizi za Kiarabu kuwa za Kirumi: 19, 17, 13, 16, 20, 14, 12, 18, 11, 15.
3. Namba za Kirumi kuanzia XXI hadi XXXIII
Namba za Kirumi za 21 hadi 33 ni kama ifuatavyo:
21 - XXI
22 - XXII
23 - XXIII
24 - XXIV
25 - XXV
26 - XXVI
27 - XXVII
28 - XXVIII
29 - XXIX
30 - XXX
31 - XXXI
32 - XXXII
33 - XXXIII
Zoezi la 3
Andika namba hizi kwa Kirumi: 29, 26, 32, 23.
Andika namba hizi kwa Kiarabu: XXII, XXXI, XXVIII, XXV.
Jaza namba zinazokosekana katika mfululizo huu:
XXI, ____, XXIII, ____, ____, XXVI.
XXIV, ____, XXVI, ____, ____, XXIX.
4. Namba za Kirumi kuanzia XXXIV hadi L
Namba za Kirumi za 34 hadi 50 ni kama ifuatavyo:
34 - XXXIV
35 - XXXV
36 - XXXVI
37 - XXXVII
38 - XXXVIII
39 - XXXIX
40 - XL
41 - XLI
42 - XLII
43 - XLIII
44 - XLIV
45 - XLV
46 - XLVI
47 - XLVII
48 - XLVIII
49 - XLIX
50 - L
Zoezi la 4
Andika namba hizi kwa Kirumi: 35, 39, 40.
Andika namba hizi kwa Kiarabu: XXXIV, XLVII, XLII.
Jaza namba zinazokosekana katika mfululizo huu:
XXXV, ____, XXXVII, ____, XXXIX.
XL, ____, XLII, ____, XLIV.