|
Matumizi ya Nishati katika Kuhifadhi na Kuandaa Chakula |
|
Jokofu |
|
Jokofu ni kifaa kinachotumika kuhifadhi vyakula katika hali ya ubaridi ili visiharibike. Linatumia nishati kama umeme au mafuta ya taa. Lina sehemu mbili kuu: |
|
|
|
Friza β Hugandisha vyakula na hutumika kuhifadhi nyama, samaki, maziwa, njegere, na vyakula vinavyoweza kuota kwenye ubaridi wa kawaida. |
|
Friji β Hifadhi ya vyakula visivyogandishwa kama wali, mboga zilizopikwa, na vinywaji. Mlango wa jokofu hutumika kuhifadhi chupa na dawa, lakini si maziwa yanayoharibika haraka. |
|
Matumizi Bora ya Jokofu |
|
Epuka kuweka vyakula vya moto β Huongeza joto na kusababisha vijidudu kuzaliana. |
|
Usizime na kuwasha mara kwa mara β Inapunguza ufanisi na huongeza matumizi ya umeme. |
|
Safi sha mara mbili kwa mwezi β Tumia maji na sabuni, na usitumie vitu vyenye ncha kali. |
|
Panga vyakula kwa usahihi β Vihifadhi kwenye vyombo vyenye mfuniko, na epuka kuhifadhi chakula kikavu kama unga na vitunguu ndani ya jokofu. |
|
Funga mlango kwa usahihi β Hii huzuia hewa baridi isitoke na kuhakikisha ufanisi wake. |
|
Umuhimu wa Jokofu |
|
Huhifadhi vyakula kwa muda mrefu. |
|
Hutumika hospitalini na maduka ya dawa kuhifadhi dawa zinazohitaji ubaridi. |
|
Husaidia biashara za vinywaji baridi, hasa maeneo yenye joto kali. |
|
Majiko ya Kupikia |
|
Majiko hutofautiana kulingana na aina ya nishati yanayotumia, kama vile: |
|
|
|
Mkaa na kuni β Yanatumika sana lakini yanaharibu mazingira. |
|
Mafuta ya taa β Yapekezwa kwa aina mbili: yanayotumia utambi na yasiyotumia utambi. |
|
Gesi na umeme β Ni rafiki kwa mazingira na yanapunguza uharibifu wa misitu. |