content-pipeline / data /texts /kujumlisha namba g4.txt
AK1239's picture
Prepare for Hugging Face Spaces deployment
91e999e
Kujumlisha Namba
Katika sura hii, utajifunza kujumlisha namba zenye tarakimu hadi tano.
Zoezi la 1: Marudio
Jibu maswali yafuatayo:
9327 + 432 =
8195 + 1502 =
5362 + 235 =
845 + 5101 =
9735 + 235 =
Maswali ya Maisha Halisi
Maria alinunua vifaranga 2464 na baadaye akanunua vingine 5758. Ana jumla ya vifaranga wangapi?
Juma alivuna maembe 4395 na maparachichi 226. Jumla ya matunda aliyovuna ni ngapi?
Kujumlisha Namba Bila Kubadili
Katika kujumlisha, anza na mamoja, kisha makumi, mamia, maelfu, na makumi elfu.
Mfano 1: Kujumlisha kwa Ulalo
Jumlisha:
68942 + 30051
Njia:
6 8 9 4 2
+ 3 0 0 5 1
---------------
9 8 9 9 3
Hatua za Jumlisho:
Mamoja: 2 + 1 = 3
Makumi: 4 + 5 = 9
Mamia: 9 + 0 = 9
Maelfu: 8 + 0 = 8
Makumi elfu: 6 + 3 = 9
Mfano 2: Kujumlisha kwa Wima
Jumlisha:
45248
+ 20231
--------
65479
Hatua za Jumlisho:
Mamoja: 8 + 1 = 9
Makumi: 4 + 3 = 7
Mamia: 2 + 2 = 4
Maelfu: 5 + 0 = 5
Makumi elfu: 4 + 2 = 6
Zoezi la 2
Jumlisha namba zifuatazo:
54351 + 12045 =
63124 + 35743 =
34570 + 55018 =
80021 + 17734 =
Kujumlisha Namba kwa Kubadili
Ikiwa jumlisho linazidi 9 katika nafasi fulani, ongeza tarakimu iliyobebwa kwenye nafasi inayofuata.
Mfano 1: Kujumlisha kwa Ulalo
Jumlisha:
58271 + 32989
Njia:
5 8 2 7 1
+ 3 2 9 8 9
---------------
9 1 2 6 0
Hatua za Jumlisho:
Mamoja: 1 + 9 = 10 (weka 0, beba 1)
Makumi: 1 + 7 + 8 = 16 (weka 6, beba 1)
Mamia: 1 + 2 + 9 = 12 (weka 2, beba 1)
Maelfu: 1 + 8 + 2 = 11 (weka 1, beba 1)
Makumi elfu: 1 + 5 + 3 = 9
Mfano 2: Kujumlisha kwa Wima
13827
+ 15685
--------
29512
Hatua za Jumlisho:
Mamoja: 7 + 5 = 12 (weka 2, beba 1)
Makumi: 1 + 2 + 8 = 11 (weka 1, beba 1)
Mamia: 1 + 8 + 6 = 15 (weka 5, beba 1)
Maelfu: 1 + 3 + 5 = 9
Makumi elfu: 1 + 1 = 2