# Vipimo vya Metriki Katika sura hii, utajifunza kubadili vipimo vya metriki vya urefu, uzani, na ujazo, pamoja na kutatua mafumbo yanayohusu vipimo hivyo. ## 1. Kubadili Vipimo vya Urefu Kipimo cha msingi cha urefu ni meta (m). Vipimo vingine ni: * 1 sentimeta (sm) = 10 milimeta (mm) * 1 meta (m) = 100 sentimeta (sm) = 1000 milimeta (mm) * 1 kilometa (km) = 1000 meta (m) ### Kubadili Kipimo Kikubwa Kuwa Kidogo **Mfano**: Badili m 3 kuwa sm \[1m = 100sm\] \[3m = 3 × 100 = 300sm\] **Mfano**: Badili km 5 m 250 kuwa m \[5km = 5 × 1000 = 5000m\] \[5000m + 250m = 5250m\] ### Zoezi **Badili km kuwa m** * km 17 * km 85 * km 36 * km 19 * km 35 m 20 **Badili m kuwa sm** * m 13 * m 2 * m 9 * m 2100 * m 990 **Badili sm kuwa mm** * sm 5 * sm 30 * sm 12 * sm 8 * sm 102 ## 2. Kubadili Kipimo Kidogo Kuwa Kikubwa **Mfano**: Badili sm 500 kuwa m \[500sm ÷ 100 = 5m\] **Mfano**: Badili m 4500 kuwa km \[4500m ÷ 1000 = 4km\, 500m\] ### Zoezi **Badili m kuwa km** * m 9000 * m 15000 * m 6000 * m 1750 **Badili sm kuwa m** * sm 2000 * sm 150 * sm 600 * sm 1550 **Badili mm kuwa sm** * mm 40 * mm 100 * mm 250 * mm 245 ## 3. Kupima Urefu Urefu wa vitu hupimwa kwa kutumia rula au futikamba. ### Shughuli Pima na rekodi urefu wa vitu vifuatavyo kwa sm na mm: * Ubao * Darasa * Dirisha * Mlango ### Zoezi Chagua kipimo sahihi kati ya sm, m, km kwa kupima: * Urefu wa dawati * Umbali kutoka shule hadi sokoni * Urefu wa mlingoti wa bendera * Umbali kutoka nyumbani hadi shuleni * Urefu wa kalamu ## 4. Mafumbo ya Vipimo vya Urefu **Mfano**: Urefu wa kiwanja cha mpira ni m 100, badili kuwa sm \[100m × 100 = 10000sm\] **Mfano**: Fausta alitembea km 8 m 700, Tasha alitembea m 6928. Fausta: \[8km × 1000 + 700 = 8700m\] Tasha: \[6928m\] Fausta alitembea zaidi kwa m 1772. ### Zoezi Badili m 6 sm 75 kuwa sm