Takwimu Darasa la tatu ulijifunza kutumia takwimu kuwasilisha taarifa mbalimbali. Katika sura hii utajifunza jinsi ya kukusanya, kurekodi na kuwasilisha taarifa kwa kutumia picha na grafu kwa mihimili. Zoezi la 1: Marudio Angalia picha katika jedwali lifuatalo linaloonesha mauzo ya samaki katika soko la Mwananchi kisha jibu maswali. Siku Idadi ya samaki waliouzwa Jumatatu Jumanne Jumatano Alhamisi Ijumaa Jumamosi Jumapili Hisabati DRS 4 Final 30/JULY/2021.indd 174 30/07/2021 11:39 FOR ONLINE USE ONLY DO NOT DUPLICATE FOR ONLINE USE ONLY 175 1. Jumatatu waliuzwa samaki wangapi? 2. Jumamosi waliuzwa samaki wangapi? 3. Jumla waliuzwa samaki wangapi kwa wiki? 4. Tafuta tofauti ya idadi ya samaki waliouzwa siku ya Jumatatu na Jumapili. 5. Ni siku gani waliuzwa samaki wachache zaidi? 6. Ni siku gani waliuzwa samaki wengi zaidi? 7. Ni siku zipi waliuzwa idadi sawa ya samaki? 8. Andika idadi ya samaki waliouzwa siku ya: (a) Alhamisi (b) Jumatano (c) Ijumaa Hisabati DRS 4 Final 30/JULY/2021.indd 175 30/07/2021 11:39 FOR ONLINE USE ONLY DO NOT DUPLICATE FOR ONLINE USE ONLY 176 Kukusanya na kurekodi taarifa Taarifa mbalimbali zilizokusanywa na kurekodiwa huitwa data. Data zinaweza kutafsiriwa kwa kutumia picha au grafu za mihimili. Kuwasilisha takwimu kwa picha Picha hutumika kuwakilisha taarifa zilizokusanywa na kurekodiwa. Picha moja inaweza kutumika kuwakilisha idadi fulani ya vitu kulingana na taarifa husika. Picha yoyote inaweza kutumika kuwakilisha idadi ya vitu. Mfano Mwaka 2014 wanakijiji wa Kalenga walivuna mahindi, maharage, viazi na mtama kama inavyoonesha katika jedwali. Chora picha za magunia kuwakilisha takwimu hizo. Kipimio: Picha ya gunia 1 inawakilisha magunia 1000. Mazao Idadi ya magunia Mahindi 25000 Maharage 14000 Viazi 30000 Mtama 8000 Hisabati DRS 4 Final 30/JULY/2021.indd 176 30/07/2021 11:39 FOR ONLINE USE ONLY DO NOT DUPLICATE FOR ONLINE USE ONLY 177 Jibu Takwimu kwa picha Mazao Idadi ya magunia kwa kipimio Idadi kwa picha Mahindi 25 Maharage 14 Viazi 30 Mtama 8 Hisabati DRS 4 Final 30/JULY/2021.indd 177 30/07/2021 11:39 FOR ONLINE USE ONLY DO NOT DUPLICATE FOR ONLINE USE ONLY 178 Zoezi la 2 Jaza nafasi zilizoachwa wazi katika jedwali lifuatalo, namba 1 imefanyika kama mfano. Idadi Idadi kwa picha Kipimio 1. Miti 15000 Picha ya mti 1 inawakilisha miti 1000 2. Mayai 11000 Picha ya yai 1 inawakilisha mayai 1000 3. Boksi 200 Picha ya boksi 1 inawakilisha boksi 100 4. Magunia ya karanga 40000 Picha ya gunia 1 inawakilisha magunia 10000 5. Machungwa 80000 Picha ya chungwa 1 inawakilisha machungwa 10000 6. Chupa 50 za maji Picha ya chupa 1 inawakilisha chupa 10 Hisabati DRS 4 Final 30/JULY/2021.indd 178 30/07/2021 11:39 FOR ONLINE USE ONLY DO NOT DUPLICATE FOR ONLINE USE ONLY 179 Kutumia picha kupata idadi ya vitu Mfano Maria alikusanya mayai kama inavyoonesha katika jedwali. Kipimio: Picha ya yai 1 inawakilisha mayai 50. Siku Idadi ya mayai Jumatatu Jumanne Jumatano Alhamisi Ijumaa Jumamosi Jumapili Maswali (a) Ni siku gani Maria alikusanya mayai mengi zaidi? (b) Mayai mangapi yalikusanywa siku ya Jumanne? (c) Mayai mangapi yalikusanywa kwa wiki? Hisabati DRS 4 Final 30/JULY/2021.indd 179 30/07/2021 11:39 FOR ONLINE USE ONLY DO NOT DUPLICATE FOR ONLINE USE ONLY 180 Jibu (a) Maria alikusanya mayai mengi zaidi siku ya Ijumaa (b) Mayai aliyokusanya siku ya Jumanne ni: Njia Kipimio: Picha ya yai 1 inawakilisha mayai 50 Mayai aliyokusanya ni sawa na; 9 x 50 = 450 Kwa hiyo, siku ya jumanne alikusanya mayai 450. (c)Mayai aliyokusanya kwa wiki ni: Njia Kipimio: Picha ya yai 1 inawakilisha mayai 50 Mayai aliyokusanya kwa wiki sawa na 51 x 50 = 2550 kwa hiyo, alikusanya mayai 2550 kwa wiki. Hisabati DRS 4 Final 30/JULY/2021.indd 180 30/07/2021 11:39 FOR ONLINE USE ONLY DO NOT DUPLICATE FOR ONLINE USE ONLY 181 Zoezi la 3 1. Tumia takwimu kwa picha kujibu maswali yafuatayo: Maumbo ya pembetatu katika jedwali yanawakilisha idadi ya mauzo ya nafaka kwa mwezi katika duka la Amani. Jibu maswali yanayofuata. Mwezi Mauzo katika kilogramu Juni Julai Agosti Septemba Oktoba Maswali Kipimio: Pembetatu moja inawakilisha kilogramu 1000 (a) Ni mwezi upi aliuza nafaka chache zaidi? (b) Kilogramu ngapi ziliuzwa mwezi Agosti? (c) Tafuta tofauti ya mauzo ya nafaka kwa miezi ya Oktoba na Septemba. Hisabati DRS 4 Final 30/JULY/2021.indd 181 30/07/2021 11:39 FOR ONLINE USE ONLY DO NOT DUPLICATE FOR ONLINE USE ONLY 182 2. Tumia jedwali lifuatalo kuchora takwimu kwa picha kuonesha idadi ya wanafunzi kwa kila shule: Kipimio: Picha ya mwanafunzi 1 inawakilisha wanafunzi 100. Shule ya Msingi Idadi ya wanafunzi Umoja 800 Minazini 1200 Mwenge 900 Kilimani 1000 Juhudi 600 Kuwasilisha data kwa kutumia grafu kwa mihimili Grafu kwa mihimili hutumika kuwasilisha taarifa zilizokusanywa na kurekodiwa. Grafu kwa mihimili huundwa na mihimili iliyosimama sambamba yenye urefu unaotegemea idadi ya data. Kila mhimili unawakilisha idadi ya vitu kulingana na data husika. Katika kuchora grafu kwa mihimili zingatia yafuatayo: (a) Kila mhimili unawakilisha data husika kwa kutumia kipimio. (b) Upana wa mihimili ni sawa kwa kila mhimili. (c) Nafasi iliyo sawa huachwa kati ya mhimili na mhimili kwenye mstari wa ulalo. Hisabati DRS 4 Final 30/JULY/2021.indd 182 30/07/2021 11:39 FOR ONLINE USE ONLY DO NOT DUPLICATE FOR ONLINE USE ONLY 183 (d) Urefu wa mhimili hutegemea idadi ya data kwenye mstari wa wima. (e) Grafu kwa mihimili inakuwa na kichwa cha habari. Mfano wa 1 Grafu kwa mihimili inayoonesha idadi ya wanafunzi wa darasa la I-IV katika Shule ya Msingi Mwenge. Kipimio: sm 1 inawakilisha idadi ya wanafunzi 20 kwa wima sm 1 inawakilisha upana wa mhimili 1 kwa ulalo Darasa Idadi ya wanafunzi 0 I II III IV 20 40 60 80 Grafu kwa mihimili kuonesha idadi ya wanafunzi wa Darasa la I-IV Hisabati DRS 4 Final 30/JULY/2021.indd 183 30/07/2021 11:39 FOR ONLINE USE ONLY DO NOT DUPLICATE FOR ONLINE USE ONLY 184 Maswali 1. Mstari wa wima unaonesha nini? 2. Mstari wa ulalo unaonesha nini? 3. Darasa la I lina wanafunzi wangapi? 4. Darasa lipi lina idadi kubwa ya wanafunzi? Idadi hiyo ni ngapi? 5. Madarasa yapi yana idadi sawa ya wanafunzi? Idadi hiyo ya wanafunzi ni ngapi? Jibu 1. Mstari wa wima unaonesha idadi ya wanafunzi 2. Mstari wa ulalo unaonesha madarasa 3. Darasa la I lina idadi ya wanafunzi 20. 4. Darasa la III lina idadi kubwa ya wanafunzi ambayo ni 80. 5. Darasa la II na la IV yana idadi sawa ya wanafunzi ambayo ni 40. Shughuli ya kufanya Kusanya na panga vitabu kama ifuatavyo: Jina la kitabu Idadi ya vitabu Hisabati 18 Kiswahili 14 English 10 Maarifa ya Jamii 20 Hisabati DRS 4 Final 30/JULY/2021.indd 184 30/07/2021 11:39 FOR ONLINE USE ONLY DO NOT DUPLICATE FOR ONLINE USE ONLY 185 Maswali 1. Mpangilio wa vitabu vipi ni mrefu zaidi 2. Mpangilio wa vitabu vipi ni mfupi? 3. Chora grafu kwa mihimili kuonesha mpangilio wa vitabu hivyo Mfano wa 2 Angalia mahudhurio ya wanafunzi wa darasa la nne katika Shule ya Msingi Mashujaa kisha jibu maswali yanayofuata. Siku Jumatatu Jumanne Jumatano Alhamisi Ijumaa Idadi ya wanafunzi 90 120 70 60 110 Kipimio: sm 1 inawakilisha wanafunzi 20 kwa wima sm 1 inawakilisha upana wa mhimili 1 kwa ulalo Maswali (a) chora grafu kwa mihimili kuonesha taarifa hiyo (b) mhimili wa siku gani ni mrefu zaidi? (c) mhimili wa siku gani ni mfupi zaidi? Hisabati DRS 4 Final 30/JULY/2021.indd 185 30/07/2021 11:39 FOR ONLINE USE ONLY DO NOT DUPLICATE FOR ONLINE USE ONLY 186 Jibu (a) (b) Mhimili wa siku ya Jumanne ni mrefu zaidi. (c) Mhimili wa siku ya Alhamisi ni mfupi zaidi. 0 Jumatatu Jumanne Jumatano Alhamisi Ijumaa Siku Idadi ya wanafunzi 20 40 60 80 100 120 Grafu kwa mihimili kuonesha mahudhurio ya wanafunzi wa darasa la nne Hisabati DRS 4 Final 30/JULY/2021.indd 186 30/07/2021 11:39 FOR ONLINE USE ONLY DO NOT DUPLICATE FOR ONLINE USE ONLY 187 Zoezi la 4 1. Maimuna alivuna mahindi kwa miaka minne kama inavyonekana kwenye jedwali: Mwaka Idadi ya magunia ya mahindi 2012 2013 2014 2015 Kipimio: sm 1 inawakilisha magunia 2 kwa wima sm 1 inawakilisha upana wa mhimili 1 kwa ulalo Maswali (a) Chora grafu kwa mihimili kuwakilisha takwimu hizo. (b) Taja mwaka wenye mhimili mrefu zaidi. (c) Nini tofauti kati ya mhimili wa mwaka 2012 na 2015. Hisabati DRS 4 Final 30/JULY/2021.indd 187 30/07/2021 11:39 FOR ONLINE USE ONLY DO NOT DUPLICATE FOR ONLINE USE ONLY 188 2. Chora grafu kwa mihimili inayoonesha matokeo ya jaribio la somo la Hisabati kwa wanafunzi 6 wa darasa la IV kisha jibu maswali . Wanafunzi Alama Bakari 85 Amani 60 Neema 90 Shukuru 40 Ashura 80 Bahati 60 Kipimio: sm 1 inawakilisha alama 10 kwa wima sm 1 inawakilisha upana wa mhimili 1 kwa ulalo Maswali (a) Mhimili gani ni mrefu zaidi? (b) Tafuta tofauti kati ya mhimili mfupi zaidi na mrefu zaidi. (c) Taja majina ya wanafunzi wenye mihimili inayolingana kwa urefu. Hisabati DRS 4 Final 30/JULY/2021.indd 188 30/07/2021 11:39 FOR ONLINE USE ONLY DO NOT DUPLICATE FOR ONLINE USE ONLY 189 3. Angalia grafu kwa mihimili inayoonesha mvua zilizonyesha katika mwezi Januari, Februari, Machi na Aprili kisha jibu maswali. Grafu kwa mihimili kuonesha kiwango cha mvua Kipimio: sm 1 inawakilisha mm 20 za mvua kwa wima sm 1 inawakilisha upana wa mhimili 1 kwa ulalo Maswali (a) Mwezi gani mvua ilinyesha nyingi zaidi? (b) Miezi ipi ilikuwa na kiwango sawa cha mvua? (c) Mwezi Machi mvua ilinyesha kwa kiwango gani?