MFUMO WA MMENG'ENYO WA CHAKULA Utangulizi Mfumo wa mmeng'enyo wa chakula ni muhimu kwa mwili wa binadamu. Mmeng'enyo wa chakula huanzia mdomoni kuelekea tumboni na kuishia kwenye utumbo mwembamba. Chakula ambacho hakijameng'enywa huishia kwenye utumbo mpana. Sehemu Kuu za Mfumo wa Mmeng'enyo: - Kinywa - Koromeo - Umio - Tumbo - Utumbo mwembamba - Utumbo mpana - Ini - Kongosho - Kifuko nyongo KASORO KATIKA MFUMO WA MMENG'ENYO WA CHAKULA 1. Kuvimbiwa Sababu: - Kula chakula kingi kupita kiasi - Chakula kutomeng'enywa vizuri tumboni Dalili: - Kuumwa tumbo - Kuhisi tumbo kujaa gesi - Kupiga mbweu - Gesi yenye harufu kali Njia za Kuzuia: - Kula chakula kiasi - Kunywa maji ya kutosha - Kula matunda na mboga za majani kwa wingi 2. Kiungulia Sababu: - Kula chakula kingi kupita kiasi - Vyakula vya kukaanga na vyenye mafuta mengi - Vyakula vyenye asidi nyingi - Kula muda mfupi kabla ya kulala - Vinywaji kama juisi ya machungwa na nyanya Dalili: - Maumivu ya kuungua kifuani - Kucheua sana - Kuhisi uchachu mdomoni Njia za Kuzuia: - Kula chakula taratibu - Kula kidogokidogo mara kwa mara - Epuka vyakula vinavyosababisha kiungulia - Pumzika saa 2-3 kabla ya kulala - Epuka mazoezi au kazi nzito mara baada ya kula 3. Vidonda vya Tumbo Sababu: - Vyakula vingi vyenye asidi - Mawazo mengi - Bakteria - Kukaa na njaa kwa muda mrefu Dalili: - Maumivu makali tumboni - Kutapika damu - Haja kubwa iliyochanganyika na damu Njia za Kuzuia: - Kula kwa wakati - Punguza vyakula vyenye asidi nyingi - Acha kuvuta sigara na kunywa pombe - Punguza mawazo na wasiwasi TABIA SAHIHI ZA ULAJI WA CHAKULA - Kula mlo kamili - Kula nafaka zisizokobolewa - Kunywa maji ya kutosha (nusu saa kabla au baada ya kula) - Kula kwa wakati maalum - Kula matunda na mboga za majani