Matumizi ya Nishati katika Kuhifadhi na Kuandaa Chakula Jokofu Jokofu ni kifaa kinachotumika kuhifadhi vyakula katika hali ya ubaridi ili visiharibike. Linatumia nishati kama umeme au mafuta ya taa. Lina sehemu mbili kuu: Friza – Hugandisha vyakula na hutumika kuhifadhi nyama, samaki, maziwa, njegere, na vyakula vinavyoweza kuota kwenye ubaridi wa kawaida. Friji – Hifadhi ya vyakula visivyogandishwa kama wali, mboga zilizopikwa, na vinywaji. Mlango wa jokofu hutumika kuhifadhi chupa na dawa, lakini si maziwa yanayoharibika haraka. Matumizi Bora ya Jokofu Epuka kuweka vyakula vya moto – Huongeza joto na kusababisha vijidudu kuzaliana. Usizime na kuwasha mara kwa mara – Inapunguza ufanisi na huongeza matumizi ya umeme. Safi sha mara mbili kwa mwezi – Tumia maji na sabuni, na usitumie vitu vyenye ncha kali. Panga vyakula kwa usahihi – Vihifadhi kwenye vyombo vyenye mfuniko, na epuka kuhifadhi chakula kikavu kama unga na vitunguu ndani ya jokofu. Funga mlango kwa usahihi – Hii huzuia hewa baridi isitoke na kuhakikisha ufanisi wake. Umuhimu wa Jokofu Huhifadhi vyakula kwa muda mrefu. Hutumika hospitalini na maduka ya dawa kuhifadhi dawa zinazohitaji ubaridi. Husaidia biashara za vinywaji baridi, hasa maeneo yenye joto kali. Majiko ya Kupikia Majiko hutofautiana kulingana na aina ya nishati yanayotumia, kama vile: Mkaa na kuni – Yanatumika sana lakini yanaharibu mazingira. Mafuta ya taa – Yapekezwa kwa aina mbili: yanayotumia utambi na yasiyotumia utambi. Gesi na umeme – Ni rafiki kwa mazingira na yanapunguza uharibifu wa misitu.