Huduma ya Kwanza (First Aid) Maana ya Huduma ya Kwanza: Huduma ya kwanza ni msaada wa haraka unaotolewa kwa mtu anapopatwa na ugonjwa au ajali. Bila kuwepo kwa huduma ya kwanza, mtu huweza kudhurika zaidi au kupoteza maisha. Sababu za Kuzirai: 1. Maumivu makali ya mwili 2. Mshtuko wa moyo kutokana na habari njema au mbaya 3. Kutokwa damu kwa wingi 4. Uchovu uliokithiri 5. Kufanya kazi ngumu bila kupumzika Hatua za Kutoa Huduma ya Kwanza kwa Mtu Aliyezirai: 1. Mazingira Salama: - Mlaze mgonjwa chali mahali palipo na hewa ya kutosha - Ikiwa ni ndani, fungua madirisha na milango ili kuongeza mzunguko wa hewa - Hakikisha mgonjwa yuko mahali penye kivuli au mazingira salama 2. Kulegeza Nguo: - Legeza nguo zake shingoni - Legeza nguo kifuani - Legeza nguo kiunoni Hii husaidia kupunguza msongo na kuwezesha upumuaji mzuri 3. Kuboresha Hali ya Mgonjwa: - Mpepee mgonjwa ili apate hewa ya kutosha - Mnawishe uso kwa maji safi - Mwangalie kwa karibu hali yake ya kupumua 4. Hatua za Ziada: - Tafuta msaada wa dharura - Mpeleke hospitalini kwa uchunguzi zaidi - Endelea kumhudumia hadi msaada utakapofika Tahadhari Muhimu: - Usimzunguke mgonjwa kwa ukaribu sana kwani anahitaji hewa nyingi - Usisubiri muda mrefu kumtafutia msaada wa kitabibu - Usimhamishie sehemu yenye joto jingi - Hakikisha unampa nafasi ya kupumua vizuri Huduma ya kwanza ni msaada wa haraka unaotolewa kwa mtu anapopatwa na ugonjwa au ajali. Darasa la tatu ulijifunza namna ya kutoa huduma ya kwanza kwa mtu aliyeumwa na mdudu. Katika sura hii utajifunza namna ya kutoa huduma ya kwanza kwa mtu aliyezirai. Soma habari ifuatayo, kisha fanya zoezi la 1. Amani, Johari na Jumanne ni marafi ki. Marafi ki hawa wanaishi katika kijiji cha Maendeleo. Siku moja, Amani alikuwa nje akicheza na wenzake. Mama yake alimwita Amani na kumtuma akachote maji kisimani. Amani alichukua ndoo na kuelekea kisimani. Rafi ki zake Amani, nao waliamua kuongozana naye kuelekea kisimani. Wakiwa njiani, Amani akamwona nyoka mkubwa mweusi amekatisha njiani. Amani alishituka, akaanguka chini na kuzirai. Rafi ki zake walishituka na kuanza kumwita Amani! Amani! Lakini Amani hakuweza kuamka. Johari na Jumanne walimsogeza pembeni wakamlaza chali chini ya mti palipokuwa na kivuli. SAYANSI STD 4 (05/07/2021).indd 112 8/5/21 4:00 PM FOR ONLINE USE ONLY DO NOT DUPLICATE FOR ONLINE USE ONLY 113 Kielelezo namba 1: Huduma ya kwanza kwa mtu aliyezirai Walianza kumpepea kwani alikuwa akitokwa na jasho mwili mzima na kupumua kwa tabu. Johari alikimbia kwenda kutoa taarifa kwa mama yake Amani. Mama yake alipofi ka walimchukua na kumpeleka hospitalini. Daktari aliwaambia "Amani anaendelea vizuri ila alikuwa amepata mshtuko uliomsababishia kuzirai." Daktari aliwaelezea sababu za mtu kuzirai. Aliwaambia, "Mtu huweza kuzirai kwa sababu ya maumivu makali ya mwili." Hali kadhalika, kupata mshituko wa moyo kutokana na habari njema au mbaya. Pia, kutokwa damu kwa wingi, uchovu uliokithiri na kufanya kazi ngumu bila kupumzika husababisha mtu kuzirai. Daktari alisisitiza kuwa, kumsaidia mtu aliyezirai inakupasa ufuate hatua zifuatazo: mlaze chali mahali palipo na hewa ya kutosha. Legeza nguo zake shingoni, kifuani na kiunoni ili kumpa ahueni. SAYANSI STD 4 (05/07/2021).indd 113 8/5/21 4:00 PM FOR ONLINE USE ONLY DO NOT DUPLICATE FOR ONLINE USE ONLY 114 Ikiwa mtu huyo yupo ndani, fungua madirisha na milango. Ikiwa hewa haitoshi, mpepee ili apate hewa nyingi ya kutosha. Pia, unaweza kumnawisha mgonjwa uso kwa maji safi kisha mpeleke hospitalini. Baada ya maelezo hayo walimshukuru daktari kwa elimu aliyowapatia. Zoezi la 1 1. Huduma aliyopatiwa Amani kabla ya kwenda hospitali inaitwaje? 2. Kwa nini Amani alipomwona nyoka alidondoka? 3. Mama Amani alimkuta mwanae katika hali gani? 4. Ni vyanzo vipi alivyotaja daktari vinavyosababisha mtu kuzirai? 5. Eleza namna ya kumsaidia mtu aliyezirai. Kazi ya Kufanya: Kutoa huduma ya kwanza kwa mtu aliyezirai Fanya igizodhima na wenzako la namna ya kutoa huduma ya kwanza kwa mtu aliyezirai kwa kuzingatia hatua zake. SAYANSI STD 4 (05/07/2021).indd 114 8/5/21 4:00 PM FOR ONLINE USE ONLY DO NOT DUPLICATE FOR ONLINE USE ONLY 115 Zoezi la 2 Andika NDIYO kwa sentensi sahihi na HAPANA kwa sentensi isiyo sahihi. 1. Ukimwona mtu yeyote anapumua harakaharaka ujue anakaribia kuzirai. __________________ 2. Tusiwe na tabia za kuwashitua wenzetu maana wanaweza kuzirai. ______________ 3. Mtu ambaye si mwoga hawezi kupatwa na tatizo la kuzirai. ______________ 4. Kuna sababu moja tu inayoweza kumsababishia mtu kuzirai. ________________ 5. Mtu aliyezirai anaweza kupatwa na tatizo la kushindwa kupumua. _______________ 6. Kutokwa na damu nyingi huweza kusababisha kuzirai. __________________ 7. Tunashauriwa kumzunguka mtu aliyezirai ili apate hewa ya kutosha. ____________________ 8. Tunashauriwa kumfunika kwa blanketi mtu aliyezirai ili asipate baridi. ________________ 9. Kufungua milango na madirisha huweza kumsaidia mtu aliyezirai akiwa ndani. _________________ SAYANSI STD 4 (05/07/2021).indd 115 8/5/21 4:00 PM FOR ONLINE USE ONLY DO NOT DUPLICATE FOR ONLINE USE ONLY 116 Zoezi la 3 1. Eleza maana ya huduma ya kwanza. 2. Kwa nini unashauriwa kumpepea mtu aliyezirai? 3. Eleza umuhimu wa kutoa huduma ya kwanza kwa mtu aliyezirai. 4. Eleza sababu nyingine zinazoweza kusababisha mtu kuzirai. 5. Unapochelewa kumpatia huduma ya kwanza mtu aliyezirai anaweza kupata madhara gani? Msamiati Blanketi nguo nzito iliyotengenezwa kwa sufu au pamba inayotumiwa kujikinga dhidi ya baridi Fahamu kuwa na uelewa wa jambo fulani Zirai hali ya mtu kupoteza fahamu