Fedha ya Tanzania Katika sura hii, utajifunza jinsi ya kutumia matendo ya kujumlisha, kutoa, na kuzidisha fedha ya Tanzania. Pia utajifunza jinsi ya kufumbua mafumbo yanayohusiana na manunuzi na mauzo ya vitu. 1. Kujumlisha Fedha Kujumlisha fedha kunafanana na kujumlisha namba. Kujumlisha huanza na mamoja, makumi, mamia, maelfu, na makumi elfu. Mifano: Sh. 71400 + Sh. 24500 = Sh. 95900 Sh. 19850 + Sh. 45350 = Sh. 65200 Sh. 11650 + Sh. 78450 = Sh. 90100 Zoezi la 1: Jibu maswali haya. Sh. 25300 + Sh. 60200 = Sh. 52670 + Sh. 17380 = Sh. 36800 + Sh. 44000 = Sh. 11500 + Sh. 80150 = Sh. 66000 + Sh. 3500 = 2. Kutoa Fedha Kutoa fedha kunafanyika kama kutoa namba. Mifano: Sh. 48000 - Sh. 5550 = Sh. 42450 Sh. 90900 - Sh. 75300 = Sh. 15600 Sh. 90800 - Sh. 36950 = Sh. 53850 Zoezi la 2: Jibu maswali haya. Sh. 1700 - Sh. 1200 = Sh. 9250 - Sh. 2100 = Sh. 92450 - Sh. 38510 = Sh. 93500 - Sh. 40650 = Sh. 74000 - Sh. 35600 = 3. Kuzidisha Fedha Tunazidisha fedha kwa namba kama ifuatavyo. Mifano: Sh. 750 × 4 = Sh. 3000 Sh. 650 × 7 = Sh. 4550 Zoezi la 3: Jibu maswali haya. Sh. 950 × 7 = Sh. 75 × 13 = Sh. 560 × 12 = Sh. 105 × 80 = Sh. 200 × 25 = 4. Mafumbo ya Kujumlisha Fedha Mfano: Mapunda alitumia shilingi 45000 kwa mwezi kununua maziwa na shilingi 52500 kwa usafiri. Jumla alitumia kiasi gani cha fedha? Njia: Maziwa: Sh. 45000 Usafiri: + Sh. 52500 Jumla: Sh. 97500 Zoezi la 4: Jibu maswali haya. Jeni alipata hasara ya shilingi 2500 baada ya kuuza bidhaa kwa shilingi 87500. Je, bidhaa hiyo ilikuwa imenunuliwa kwa kiasi gani? Muuza mboga alipata noti za shilingi 5000, 2000, 1000, na sarafu ya shilingi 200 baada ya mauzo. Tafuta jumla ya fedha alizopata. Mwanafunzi alinunua kitabu cha shilingi 5500 na daftari za shilingi 2600. Je, alitumia kiasi gani cha fedha katika manunuzi yake? Bupe alinunua mchele kwa shilingi 38000. Baada ya kuuza alipata faida ya shilingi 6000. Je, aliuza mchele kwa shilingi ngapi? Juma alinunua unga wa mahindi kwa shilingi 9500 na njegere kwa shillingi 14750. Je, jumla alitumia shilingi ngapi?